Friday, February 17, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA 15




WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com






SEHEMU YA KUMI NA TANO!!
Alikuwa akiendesha maisha hayo hapo kijiji akijifanya  ni mdogo wa babu yake mzaa mama, alikuwa yupo katika kuonekano wa kizee kabisa ambapo ingekuwa ngumu kabisa kwa mtu yeyote ambaye anamfahamu kuweza kumtambua. Huko kijini alikuwa akiishi kwa amani zaidi kuliko hata huko mjini ambapo kulikuwa na kila aina ya raha, alipaona ni mahali sahihi kwake kuweza kutulia kwa siku hizo akiwa huko hadi pale hali itakapokuwa shwari.






_______________TIRIRIKA NAYO

  Moyo wa kumsaidia yule ambaye hana hatia aliyekuwa amekumbwa na kadhia, tayari ulikuwa umeshamjia. Alipofikiria maadui waliokuwa wakimngojea, aliona tatizo ataenda kuongezea. Moyo wa subira ulimjia hakika ndiyo alichokuwa akikitakia, Jama Wa Majama aliacha bao kujichezea.

 Akili yake ya kiusalama ilikuwa imeshaamka tayari na alikuwa akicheza hilo bao huku kichwani mwake kukiwa na ukinzano mzito sanaa, mawazo yake yalijigawa sehemu mbili na alikuwa akivutwa katika kila upande wa mawazo hayo. Upande mmoja ulikuwa ukitaka aelekea huko na upande mwingine ulikuwa ukitakia naye abaki hapo. Hakika ulikuwa ni ukinzano mzito sana ndani ya kichwa chake uliokuwa umetokea, upande mmoja ulikuwa ukimsihi asiondoke ndani ya kijiji na aendeleea kubaki hapohapo huku upande mwigine ulikuwa ukimsihi aondoke hapo kijiji kwani kulikuwa na yule ambaye alikuwa akiteseka sana ilihali yeye mkombozi alikuwepo.  Aliendelea kucheza bao huku ule ukinzano wa mawazo yake  ukiwa na mzigo mzito uliokuwa umekielemea kichwa chake, mzigo huo ulimfanya hadi muda huo aliokuwa akicheza bao ajisahau kabisa kuwa alikuwa yupo ndani ya mchezo huo. Ilikuwa ni zamu yake kucheza bao kwani mwenzake aliyekuwa akicheza naye alikuwa keshalala tayari.

"Mwenehu ukafikira mbali" Mzee aliyekuwa akicheza naye alimuambia na kupelekea Jama Wa Majama ndiyo arudi kwenye mchezo huo aliokuwa akiutumia kupoteza muda ndani ya kijiji hiko akiwa na wazee, alitoa tabasamu na kisha aliendelea kucheza kama kawaida.


****


 Kesi tayari ilikuwa imeshafungulia hadi kufikia muda huu wa alasiri, Mheshimiwa Kabinuki aliondolewa ndani ya kituo cha polisi alichokuwa amewekwa  kwani hakuwa ndani ya umiliki wa Polisi hadi muda huo kutokana na kuwa tayari amefunguliwa kesi. Alikuwa yupo ndani ya umiliki wa jeshi la magereza kwani alikuwa tayari ni mhasbusu hadi inafikia wakati huo.  Safari ya kuelekea gerezani ilianza ndani ya muda mfupi, aliwekwa  ndani ya gari ya jeshi la polisi ambayo ilikuwa ni ya kawaida tena aliwekwa kwenye sehemu ya nyuma ya gari hiyo ambako kuikuwa kumewekwa kiti. Mbele na nyuma ya gari hiyo kulikuwa kuna magari mawili ya jeshi la polisi ambayo yalikuwa yapo kwa ajili ya kuhakikisha usalama wake na pia kuhakikisha hawezi kukimbia. Msafara huo ulitokea Kituo cha polisi Oysterbay na ulitumia dakika kumi na tano tu ukawa umefika eneo la Tabata kwenye gereza la Segerea, hapo alishushwa na kuingizwa ndani ya gereza  wote. Alifuata taratibu zote za hapo gerezani na kisha moja kwa moja alipatiwa vazi lake, alitupwa kwenye chumba cha Mahabusu  huku hadhi yake ikiwa imeangaliwa na akawekwa kwenye chumba cha Mahabusu aliokuwa akiendana nao.

 likuwa ni siku ambayo hakuwa akiamini kabisa kuwa ndyo alikuwa amekuwa kumbe dhalili sana, kujitolea kote kule siku hiyo alikuwa haamini kabisa kama ndiyo alikuwa akiishia nyuma ya nondo. Hakika pamoja  na kuwa mtu mzima alijikuta akidondosha chozi akiwa humo gerezani kwa yaliyomkuta, heshima yote aliyokuwa nayo matokeo yake alikuwa akiishia namna hiyo. Mheshimiwa Kabinuki alijua kabisa kuwa alikuwa amepata ajali ya kisiasa, hakuona mkombozi wake kwa vidhibiti vilivyokuwa vimeshikwa kwenye mali yake. Aliona kabisa kuwa alikuwa akienda kupatiwa hukumu ndefu sana kwani ilikuwa ikija kumkuta, vifo vya mamia na mamelfu ya wakazi wa jijini vilivyokuwa vimetokea alikuwa amegeuziwa mpira yeye hakuona kabisa uwepo mtetezi wake hasa kwa vidhibiti vilivyokuwa vimekutwa. Jambo jingine ambalo lilikuwa likimfanya ajute zaidi ilikuwa ni kauli ambayo aliitoa mfanyakazi wa shamba lake, huyo ndiye aliyemuweka pabaya zaidi na yeye hakutarajia kabisa kama angekuja kuongea uzushi kama huo aliouongea kwa jeshi la polisi. Mfanyakazi huyo ndiye aliyeenda kutoa taarifa juu ya uwepo wa vitu hivyo huko shambani kabla hata kibali cha kumkamata hakijawekwa sahihi na Rais Zuber.


  Jinsi alivyokuwa akimtambua Rais Zuber ni mtu asiyependa masihara kabisa kwenye masuala yanayohusu nchi, aliona kabisa hicho ndiyo kiama chake kwani hata hao waliokuwa wakiendesha shughuli za kimahakama walikuwa wakimuhofia sana. Hofu ya watu hao iliwafanya watende haki kabisa kwenye shughli zote za kimahakama jambo ambalo mwanzo Mheshimiwa Kabinuki aliliona ilikuwa ni jambo zuri sana, muda huo aliliona ni jambo ambalo halikuwa likifaa kabisa kutokana  na kuwa ni jambo ambalo lilikuwa likienda kumkumba yeye mwenyewe. Maisha ambayo hakuwahi kuwaza kama atakuja kuishi ndiyo ndani ya siku moja tu alikuwa ameyaanza kuyaishi akiwa hana mtetezi kabisa.



****


    USIKU WA SIKU HIYO
  Norbert na Khemiri walikutana jirani kabisa na geti la bandari ambalo muda huo lilikuwa limefungwa na halitumiki kwa matumizi ya kawaida,muda huo Norbert alikuwa amevaa kofia kama ilivyo kawaida kuzidi kuvuruga utambulisho wake kwa watu hao kwani walikuwa wakimfahamu vyema jinsi alivyo katika mambo kama hayo. Khemiri  mwenyewe alikuwa akimjua kama ni  mwandishi ambaye alikuwa akifuatili sana watu waliokuwa wakifuata nyendo zake lakini kwa hapo hakuwa amemjua kutokana na muonekano mpya aliokuwa nao. Mwendo wake ulishindwa kabisa kuonesha kuwa huyo ndiye alikuwa yule Norbert hatari, alikuwa akitembea mwendo wa majigambo sana na muda huo alikuwa ameshika mkongojo wa dhahabu mkononi mwake kuonesha ni mtu ambaye alikuwa ana damu iliyokuwa imechafuka kwa pesa.

  Alipokutana naye walipeana salamu na kisha wote wawili waliingia ndani ya geti hilo la bandari baada ya kufunguliwa, ndani walikuta kukiwa na taa zilizokuwa zikiwaka na vijana waliokuwa wameshika silaha wakiwa wamejipanga katika sehemu tofauti. Kawaida ya Jasusi ilikuwa ni kutotuliza macho yake katika sehemu moja hasa kwenye maeneo kama hayo, hivyohivyo Jasusi huyu hakuwa ametuliza macho sehemu moja bali alikuwa akitembea huku akiyazungusha kwa kasi ya ajabu katika kila pande. Shingo yake haikugeuka kabisa katika muda huo aliokuwa akizungusha macho yake, Khemiri hakuwa amejua juu ya  kutaliiwa kwa mazingira ya hapo na Norbert yeye alimuona kama alikuwa akitembea kuelekea huko walipotakiwa kufika ndani ya muda huo. Walitembea kwa mwendo mrefu sana kutokana na eneo hiolo kuwa kubwa sana, walienda hadi kwenye sehemu maalum ya kuifadhia mizigo ndani ya bandari ambapo Khemiri alichukua muda huo kumfafanulia juu ya kila kitu.

"Hii ghala ni maalum kwa mizigo ambayo imeshakaguliwa na kulipiwa kodi kila kitu ikisubiri kusafarishwa tu na mmiliki" Khemiri alimuambia  na kisha akatazama katika uso wa Norbert ambaye alikuwa ameshusha kofia, alipohakikisha alikuwa yupo pamoja naye baada ya Norbert kumpa ishara aliendelea.

"Pindi mzigo wako uatakaposhuka tu jua utaingizwa ndani ya ghala hii na siku hiyo wahusika wote watakaohusika na kuushuhsa mzigo huu jua wamepangwa na Mheshimiwa" Aliendelea kumueleza na muda huo walitoka wakawa wanaelekea kule ambako kulikuwa  sehemu ambayo meli inaegeshwa kwenda kupata maelekezo mengine, walifka hadi eneo hilo ambako kulikuwa na meli ambayo ilikuwa imeegeshwa baada ya kumaliza kupakua mizigo yake. Hapo alipewa na maelekezo muhimu kabisa ambayo alitakiwa kupewa, baada ya hapo walikuwa wakirudi kule ambako walikuwa walipokuwa awali.

 Muda huo waliokuwa wakirudi ndiyo ilijidhihidrisha katika vitu visivyo na staha ndani ya dunia hii si wanadamu pekee hata viumbe visvyo na uhai pia huwa havina staha, kofia ambayo alikuwa ameivaa kichwani Norert ambayo ilikuwa  imeegeshwa ilimletea kadhia nyingne ambayo hakutegema kama ingeweza kutokea. Kadhia hiyo ilikuwa imesababishwa na kile ambacho hakikuwa na staha kabisa, kitu hakikuwa kingine bali ulikuwa ni upepo wa eneo la hapo baharini. Upepo huo uliokuwa ukivuma kutoka nchi kavu kuelekea baharini uliikumba kofia yake kwa ghafla sana kupelekea kuanguka,  ilipoanguka kofia hiyo ndipo Khemiri alipoweza kubaini kuwa alikuwa akitazamana  na mwandishi wa habari  hatari. Hapo alijua kabisa kuwa alikuwa amekuja kupelelezwa na mwandishi huyo na hakukuwa na jingine, macho yalitoka pima huku akimtazama Norbert ambaye alikuwa ametulia tu kama alikuwa hajali kitu hicho kilichokuwa kimetokea.

"Wewe!" Alipaza sauti kwa nguvu sana na kisha akapeleka mkono kiunoni mwake na  kutaka kutoa bastola, mkono huo haukufika kabisa kwani ulipigwa teka la nguvu sana hadi akapatwa na maumivu. Norbert alipotaka kumfuata amuongeze kipigo kinggine milio ya risasi ilianza kurindima kulenga huko alipokuwa yupo, kiuwepesi zaidi aliamua kujibiringisha kutoka hilo eneo na kisha akaingia eneo lenye makontena mengi. Kundi la vijana wale waliokuwa wakilinda nalo lilikuwa katika eneo hilo mara moja, walielekea kwenye upande ule ambao alikuwa ameelekea muda huo akiwa na silaha zao.  Eneo ambalo  alikuwa amepitia ambalo lilikuwa na mkontena matupu hawakuweza kabisa kumkuta na wanatembea hadi mwisho wa eneo hilo bado hakuwepo, walijigawa makundi katika kumsaka mtu huyo ambaye alikuwa amempiga bosi wao teke ambalo lilimletea maumivu mkononi.


    Vijana hawa hawakujua kabisa kuwa huyo mtu waliokuwa wakimtafuta alikuwa ni ninja na pia komandoo mwenye mafunzo ya hali ya juu sana, walipoyatazama makontena hayo yalivyokuwa na kimo kirefu kwenda kutokana jinsi yalivyojipanga. Hawakuamini kabisa kuwa huyo mtu ambaye walikuwa wanamtafuta alikuwa amepanda kuelekea juu, lakini ukweli utabaki kuwa uleule kuwa alikuwa amepanda kuelekea juu ingawa wao walipuuzia. Uwezo wa kupanda vitu wa Norbert kama ni mnyama ungeweza kumfananisha na nyani kiuwezo huo, kwani muda huo waliokuwa wakimtafuta yeye huko chini hakuwepo. Kasi ya jabu ilikuwa haielezeki kwani alikuwa ameshafika kabisa juu ya makontena na muda huo alikuwa amejilaza kifudifudi akiwa ametulia. Alikaa kwenye eneo hilo kwa sekunde kadhaa na kisha kwa kasi ya ajabu alinyanyuka na akaruka kutoka kontena alilokuwa amekaa hadi jingine, alito kishindo mabcho kilisikiwa na wale walinzi wakaanza kulekea huko alipo. Yeye hakutaka hata kusimama alikuja na kasi nyingine kabisa na aliruka hadi kontena jingine. Hakutaka napo kukaa kwani aliona alikuwa akijichimbia kaburi zaidi ikiwa ataendelea kuwepo hapo, napo kwa kasi ya jabu alirukia kontena jingine ambalo ndiyo lilikuwa upande wa mwisho jirani kabisa na bahari. walinzi waliokuwa wakimfukuza walikuwa wakifuata vishindo hivyo walikuwa wameshachelwa tayari kwani alijiachia kutoka huko juu na kuingia moja kwa moja kwenye maji. Kutokana na eneo la bandari kuwa na kina kirefu sana ilikuwa rahisi kwake kuweza kutoroka hapo, alianza kupiga mbizi akiwa yupo huko ndani ya maji kuelekea upande ambao kulikuwa na soko la feri. Alikuwa tayari ameshapata kitu ambacho kitakuwa ni mwangaza kwake ingawa mambo tayari yalikuwa yameshaharibika, aliwaacha wale waliokuwa wakitaka kummaliza wakiwa amebaki mdomo wazi kutokana na jinsi alivyokuwa amewatoroka.


 Alikuja kwenye kutokea soko le feri katika eneo ambalo kulikuwa na Mashua mengi yaliyokuwa yakitumiwa na wavuvi, alitoka akiwa amelowana kuanzia nguo hadi viatu hadi wavuzi waliokuwa wapo eneo hilo wakamshngaa. Hilo yeye hakujali alitembea hadi barabarani na kisha akaanza kushiriki matembezi ya hisani kwa kuchelea kuwa akichukua teksi au pikipiki angeibua maswali mengi sana kwa dereva, alikata mitaa ya kata ya magogoni na hatimaye alikuja kutokea kwenye ofisi yake ambayo ilikuwa ipo katikati ya jiji. Norbert alipoingia ndani ya ofisi hiyo ambayo ilikuwa imejikamilisha kila kitu jambo la kwanza kulifikiri ilikuwa ni kubadili nguo zake, alibadili nguo hizo kwa haraka sana na kisha akahamisha vitendea kazi vyote kwenye nguo mpya alizozivaa. Baada ya hapo ndipo alipotoka kwenye ofisi hiyo akatumia pikipiki yake ya kazi ambayo alikuwa ameiegesha kuondoka ndani ya eneo hilo na kuelekea kwenye makao yake kwa muda akiwa yupo kazini.


****


 Muda mfupi baadaye Khemiri alikuwa yupo mbele ya Askofu Valdermar, alikuwa ameshampa taarifa zote juu ya kufika eneo la bandarini akiwa na mtu ambaye alikuwa akijua ni  Mteja kumbe alikuwa ni Norbert. Jambo hilo lilimshtua sana Askofu akaona kuwa kazi yao ilikuwa imeingiwa na hatari kubwa sana kwa kuwepo mtu huyo ambaye ameanza kuwanyima usingizi, tuhuma walikuwa wamempatia mwingine walitegemea kuwa huyo angeweza kukaa chini na kutulia akijua kazi imeisha kumbe bado alikuwa yupo kazini. Wote walichanganywa wakachnganyika na taarifa hiyo, muda huo wote walikuwa wapo kwenye sebule wakiwemo kina Josephine. Spider naye alikuwepo akiwa na ogo sehemu ya mkono pamoja na mguuni kutokana kile ambacho kilikuwa kimemkumba mapema sana ndani ya siku hiyo.

"Yaani huyu mtu mmoja anatutesa sana sisi jamani" Akosfu aliongea

"Shaw huyu mwandishi ni hatari sana na sisi tupo pabaya hadi muda huu, inabidi auawe mara moja" Khemiri alionga akiwa hajui kabisa uhalisia wa Norbert, kauli hiyo ilimfanya Askofu aanze kucheka kutokana na muongeaji alivyokuwa akiichukulia kirahisi sana.

"Hivi unafikiri kumuua huyo ni kazi rahisi sana Khemiri, hebu mtazame Spider nafikiri unamtambua kuwa ni mpiganaji hodari lakini kateguliwa mguu na mkono. Yote kazi ya huyo unayesema tumuue" Askofu alimuambia na kupelekea Khemiri abaki kinywa wazi kwani hakutarajia kabisa kuwa mtu huyo angekuwa hatari namna hiyo.

"Ooooh! No" Alijikuta akitamka akiwa haamini

"Khemiri napenda ujue hatushindani na binadamu wa kawaida pale, yule ndiye N001 halisi kabisa wa EASA nafikiri ushasikia habari zake" Aliambiwa.

"Tumekwisha basi ni huyo maana sifa zake nishawahi kusikia, mwanzo nilijua ni hadithi tu kumbe yupo halisi" Khemiri alismea kwa kukata tamaa

"Hakuna kukata tamaa mapema yote hiyo, cha msingi nikumuwekewa mtego, ana udhaifu wa wanawake yule nafikiri tutamuingiza mtegoni tu. Kwanza kalipa huyu hebu angalia akaunti yetu" Josephine aliuiza na kupelekea Khemiri awashe tarakilishi yake kwa haraka sana na kisha alifungua akunti ya benki kwa njia ya mtandao, alichokiona alijikuta akipiga kelele kama mwendawazimu hakuamini kabisa kama angeweza kukuta kitu kama hicho.

   Wote wlibaki wakimshangaa sana wakiwa hawajaelewa alikuwa anapiga kelele kwa sababu gani, Khemiri hakutaka kuongea chochote yeye alimpa Tarakilishi Askofu ambaye naye aliingiwa na ubaridi wa ghafla kwenye moyo wake akiwa haamini kabisa kwa alichokiona. Askofu naye aliweka kiganja cha mkono usoni mwake na kisha akampatia Tarakilishi Scorpio ambaye alikuwa yupo pembeni yake, naye alitoa macho pima kama alikuwa ameingiwa na umeme wenye hitilfu kwenye mwili wake. Alimsogezea Josephine ambaye alishtuka sana akiwa haamini kwani walikuwa amehangaika sana, alimpatia Spider ambaye alijikuta akiinamisha uso wake na huku Tarakilishi hiyo akiiweka pembeni.

"Aaaargh! Norbert hii ni too much sasa, naingia mwenyewe kazini haiwezekani tuhangaike kote aje kufagia akaunti yote" Akosfu Valdermar aliongea




ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment