Thursday, February 2, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA KWANZA




WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com






                  ******MWANZO********


   Akiwa ameketi ofisini kwake aliendelea kufanya kazi iliyokuwa ikimuhusu sana na ilitakiwa kufanywa ndani ya siku hiyo, kazi hiyo ilikuwa ni muhimu sana kuwasilishwa bungeni kwa siku
iliyokuwa ikifuatia kutokana na unyeti wake. Ilikuwa  ni kazi ambayo ripoti yake muhimu ndiyo ilikuwa imefika mezani kwake kwa siku hiyo ,  aliingojea sana kwa hamu  hiyo ili aweze kukamilisha maelezo mengine kwa ajili ya kuwasilisha wajibu huo. Ilikuwa katika muda ambao hakua akitaka kabisa kuonanana mtu yeyote ili aweze kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi, ndiyo maana alimpa agizo  Katibu Mukhtasi wake la kutoruhusu mtu aje kuonana naye kwa muda huo aliokuwa hapo ofisini.

  Haikuwa kawaida kabisa kwa yeye kufanya hivyo lakini kutokana na unyeti wa suala hilo ilimbidi afanye hivyo, ripoti hiyo ambayo alikuwa akiiandikia kazi yake ilikuwa  ikihitajika sana kwa udi na uvumba. Ilikuwa ni kaba koo kwa baaahi ya watu lakini pia ilikuwa ni ilikuwa yenye manufaa kwa hadhira ya watu waliyokuwa wakiiongojea kwa hamu sana iweze kukamilika. Hakuna mwenye nia nzuri aliyekuwa hakiitaka ripoti hiyo isifike kwa watu ijulikane, hofu yakupoteza kibarua pamoja na kuonekana ni mzembe ndiyo ilimfanya ajifungie humo ofisini kwake akiwa anaiandaa ripoti hiyo iweze kuwafikia walengwa wake. Tarakilishi ya mapakato aliyokuwa akiitumia kwa siku zote ilikuwa ipo mezani na faili lililokuwa limesheheni makaratasi yaliyochapishwa lilikuwa lipo wazi huku kalamu ya wino ikiwa ipo katikati ya faili hiyo.

   Aliendelea kufanya kazi yake kwa ufasaha sana lakini ufasaha huo uliyokuwa upo kwenye kazi yake uliondolewa mara moja baada ya karaha kuingia, karaha ambayo ilimpunguza ufanisi ambao ingembidi aweze kutulia vizuri aweze kuurudie ndiyo ilivamia ndani ya eneo hilo. Karaha hiyo ilivamia kwa kuita kwa mlio wa simu yake ya mkononi ambayo ilikuwa ipo jirani kabisa na Tarakilishi yake ya mpakato humo ofisini kwake., aliitazama simu yake hiyo akakuta namba ni ngeni kabisa ikiwa ina jina tu kuashiria kuwa aliyekuwa akipiga namba hiyo alikuwa akitumia mtindo wa kuweka namba binafsi(private number). Alipoiona namba hiyo aliacha kufanya kazi na kisha akaichukua simu hiyo akaitazama kwenye kioo chake aliitazama namba hiyo binafsi kwa muda wa sekunde kadhaa kama aliyekuwa akijifikiria kitu na hatimaye aliamua kuipokea na kisha akaweka spika ya nje huku akiendelea kufanya kazi zake.

"Ndiyo nani mwenzangu" Aliongea

"Heshima yako mheshimiwa" Sauti ya mtu aliyempigia tena ikionekana ni ya mwanamke ilisikika

"Ndiyo nakusikiliza" Mheshimiwa aliongea huku akiendelea kufsnya kazi zake.

"Kama jina langu ulivyoliona Mheshimiwa mimi ni Malikia wa kuzimu, nimetumwa kukuambia uache hicho uanchokifanya la si hivyo utatumiwa wito wa kuzimu"

"Hivi wewe umekosa kazi ya kufanya mpaka uchukue muda wako mwingi kuweza kuiweka namba yako hivyo na kisha unipigie simu halafu uongee huo utumbo wako"

"Nimekuambia tu Mheshimiwa achana na hicho unachokifanya, kuwa  mtoto wa kike haimaanishi onyo langu haliwezi kukufikia. Sauti hii nyororo ninayokuonya nayo jua ikifika siku utatamani hata irudie tena kukuambia nilichokuambia lakini haitawezekana"

"Malaya mkubwa wewe"
Mheshimiwa aliongea kwa hasira sana na kisha akaikata simu hapohapo, aliisogeza mbali na eneo alilokuwepo  na kisha akajariu tena kutulia aweze kukamilisha kazi hiyo aliyokuwa akiifanya. Alijaribu kuuweka ule umakini aliokuwa ameuweka hapo awali lakini ilishindikana kabisa kuwepo, hapo alijikuta akifunika Tarakilishi ya mapakato liyokuwa akiitumia. Umakini wote ulivurugika na hata hamu ya kuendelea na maandalizi ya kazi haikuwepo kabisa, moyoni alilaani kupigiwa simu na mwanamke ambaye ndiyo alikuwa amemchanganya kabisa kwa maneno hayo aliyomwambia.


****

 MASAKI
DAR ES SALAAAM
   Muda huohuo nyumbani kwa mtu muhimu sana kwa kampuni moja ya kiserikali na pia mtu muhimu katika idara nyeti, mtu wa kuleta barua alifika mara moja ndani ya nyumba hiyo akiwa na barua muhimu sana kwa mwenye nyumba hiyo ambaye alikuwa yupo mapumzikoni baada ya kumaliza kazi nzito ambayo ilihitajika muda mrefu sana kuiandaa. Mtu huyo wa barua alimpatia mmoja wa wanfamilia ya mwenye nyumba hiyo na kisha akaondoka bila ya kuaga, mwanafamilia huyo naye hakutaka kabisa kushughulika na kuichunguza hiyo barua yeye aliichukua na moja kwa moja aliiwasilisha kwa mwenyewe ambaye alikuwa yupo  sebuleni akiwa amekaa. Baada ya kumpatia mzigo wake aliingia ndani moja kwa moja akiwa ameshafikisha ujumbe stahiki kwa mhusika, mwenye nyumba hiyo ambaye alikuwa ndiyo kwanza anaianza likizo yake aliichukua barua hiyo na kisha akaitazama kwenye sehemu ya nje ya bahasha.

 Alikutana na jina lake ndiyo lipo juu ya bahsha  ikimaamnisha yeye ndiye alikuwa mlengwa wake, baada ya kuliona jina hilo aliiachana bahasha  kuweza kuona kilichomo ndani yake. Alikutana na bahasha nyingine nyeupe kabisa ikiwa na stempu yenye picha ya mwanamke akiwa anaonekana mgongo ambao haukuwa umefunikwa na kitu chochote kile, alipoiona picha  ya stempu alijikuta akishangaa sana kwani haikuwahi kuonekana stempu ya namna hiyo kwenye barua ya aina yeyote ile na wala haipo kwenye maduka yanayouza stempu.  Alijikuta akiitazama picha hiyo ya stempu kwa sekunde kadhaa akiwa ameingiwa na shaka na kisha akapeleka macho yake katika upande mwingine wa bahasha hiyo, napo alikutana na na mhuri wenye rangi nyekundu ambao ulikuwa una nembo ya moto katikati. Juu ya nembo katika sehemu ya juu ya mhuri huo alikutana na maneno yaliyokuwa yakisomeka kwa ufasaha kabisa, maneno hayo ndiyo yalimfanya hata azidi kuwa na shaka sana na barua hiyo ilipotoka.

 'KUZIMU' ndiyo neno ambalo lilikuwa lipo juu ya nembo hiyo sehemu ya mhuri, kuona neno hilo alijikuta kwa haraka akijaribu kuminya bahasha aone ndani ya kulikuwa kuna nini kwani haikuwa kawaida kabisa kuwahi kupokea barua ya namna hiyo. Alipoiminya bahasha hiyo alijikuta akiguna.  Baada ya kubaini kitu alichokihisi kwa viganja vyake vya mikono alivyokuwa ameiminya bahasha hiyo kidogo tu, alikata shauri na kuamua kuifungua bahasha  akiwa anataka kujua kile alichokuwa ametumiwa na kipo ndani ya bahasha hiyo.



****


   Kazi ilivurugwa ikavurugika kwake Mheshimiwa na akajikuta hata akiwa hana hamu ya kufanya kazi tena zaidi ya kuwa na hamu ya kwenda kupumzika hotelini alipokuwa amefikia, alifunga vitu vyake vya muhimu kabisa na kisha akatoka nje ya ofisi yake akiwa amechanganyikiwa. Aliufunga mlango wa ofisi yake pia na kisha akaelekea moja kwa moja hadi kwa Katibu Mukhtasi wake ambaye alikuwa akiendelea na kazi kama kawaida.

"Ninatoka sasa hivi nitaurdi kesho mchana nikitoka kwenye bungeni" Alimuambia

"Sawa mheshimiwa ila kuna barua yako imeletwa sasa hivi na mtu wa posta" Katibu Muhktasi alimuambia

"Ok nipe nitaenda kuisoma hotelini akili ikiwa sawa" Alimuambia Katibu Mukhtasi wake ambaye alifungua mtoto wa meza yake akatoa bahasha nyeupe ambayo ilikuwa na mstari mwekundu kwa juu akampatia Mheshimiwa, alipoipokea barua hiyo aliitazama sehemu ya juu akakuta kukiwa hata hamna stempu ya barua. Hilo suala hakujiuliza kabisa yeye aliichukua barua hiyo akafungua koti lake la suti akaiweka kwenye mfuko wa ndani wa koti hilo na kisha akauweka vizrui mkoba wake wa begani akawahi kutoka nje


    Kituo chake cha kwanza baada ya kutoka nje ya jengo la ofisi yake ilikuwa ni ndani ya gari lake la kifahari ambalo lilikua limeegeshwa kwenye eneo maalum ndani ya ofisi hiyo, aliingia ndani ya gri hiyo na kisha akauweka mkoba wake wa begani ambao ulikuwa una tarakilishi yake katika kiti cha nyuma. Baada ya hapo alitoa funguo za gari yake na kisha akaliwasha na kuliondoa ndani ya eneo hilo akiwa ana haraka ya kuweza kufika hotelini alipokuwa akiishi aweze kupumzisha kichwa chake kutokana na kuvurugwa kabisa na mwanamke aliyekuwa amempigia simu. Aliwasha taa ya pembeni ya upande wa kushoto alipofika barabarani kutokea kwenye maegesho, na taratibu akaliingiza barabarani na kuelekea huko hotelini alipokuwa akiishi.



****


 Muda ambao  Mheshimiwa alikuwa akitoka ndani ya ofisi yake ni muda ambao ndani ya nyumba ya mtu yule muhimu sana katika shirika la serikali na pia idara nyeti kulitokea jambo la kustajaabisha sana, Mlinzi aliyekuwa yupo getini katika nyumba hiyo ndiyo aliweza kulishuhudia jambo kwa macho yake mawili kipindi linatokea. Yeye mwenyewe alipatwa na mshtuko mkubwa sana hadi akarushwa mita kadhaa kutoka kwenye eneo hilo alilokuwa amekaa. Ulikuwa ni mlipuko mzito sana ambao ulitokea katika sehemu ya chini ya nyumba hiyo ya ghorofa na ukaenda kuathiri hadi sehemu ya juu, mlipuko huo uliambatana na kurushwa kwa vioo vya nyumba hiyo kwa umbali mrefu baada ya madirisha kupasuka kwa nguvu sana. Mlipouko huo ulimrusha mlinzi hadi akaenda kujibamiza kwenye uzio wa ukuta wa nyumba hiyo, mlipuko huo uliathiti kabisa hata matairi ya magari ambayo yalikuwa ymeegeshwa jirani kabisa na nyumba hiyo. Mlipuko huo ulipotokea hata hakusikika kelele ya aina yeyote ndani ya nyumba hiyo ambao mabosi wa mlinzi huo walikuwepo, mlipuko huo ndiyo chanzo cha mkinzi huyo kuweza kushuhudia hali nyingine kabisa ambayo hakuwahi kuishudia katika kipindi chote cha maisha yake akiwa ni kama mlinzi katika sehemu tofauti hadi akafikia kuwa mlinzi wa ndani ya nyumba hiyo.

   Baada ya kujibamiza ukutani kutokana na mshtuko uliotokana na mlipuko huo, alitulia papo hapo akiwa na maumivu sana hasa katika eneo la mgongoni ambalo alikuwa amegonga ukutani. Hakuwa hata na nguvu ya kunyayuka kutokana jinsi alivyokuwa ameumia . Alibaki akiwa ni mwenye kufumba macho kwa maumivu  hapo chini alipokuwa ameanguka baada ya kujigonga ukutani. Alishindwa hata kuhema kawaida kwa jinsi alivyoumia hata sauti zilizopo jirani na eneo hilo alikuwa akisikia kwa tabu sana kama vile alikuwa ana masikio mabovu. Macho yake yalikuwa yenye kuona kwa tabu sana haswa kutokana jinsi alivyojigonga hapo ukutani katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku mgongo ukiwa ndiyo ulioathirika zaidi, hadi ving'ora vya gari la zimamoto vinasikika vikiingia ndani ya nyumba hiyo  alikuwa akivisikia kwa mbali sana kama vile vilikuwa vipo mita nyingi zaidi kutoka pale alipokuwepo. Yote hayo ilitokana na kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na mlipuko  huo ambao umesababisha ajigonge sehemu mbalimbali za mwili wake, kuchanganywa na maumivu hayo ya eneo hilo alilojigonga ndiyo kulifanya hadi awe katika hali hiyo. Alikuwa ni mwenye kuhisi na kuona kile kilichokuwa kikiendelea karibu yake lakini hakuwa mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote kile,hadi wanakuja watu wa huduma ya kwanza wanambeba katika eneo hilo na kumuweka kwenye kitanda cha wagonjwa yeye hakuwa na uwezo wowote wa kuwapinga au kuwaruhusu wamnyanyue.


****

    Muda huo  kwa upande mwingine kabisa gari ya kifahari aina Toyota landcruiser V8 ilionekana ikiingia kwenye hoteli moja maarufu sana, gari hilo liliingia hadi sehemu ya maegesho na kisha likasimama kwenye eneo hilo. Haikupita muda gari hilo lilizimwa, kuzimwa kwa gari hilo hakukuonesha kuwa kulikuwa na dalili yeyote ile ya mtu kushuka ndani yake. Ilipita dakika takribani tano haikuonekana dalili ya mtu yeyote kushuka ndani yake, bado hakukuwa na binadamua yeyote aliyekuwa akijali juu ya kutoshuka kwa mtu aliyekuwa yupo ndani ya gari hilo. Mazingira tu yaliyokuwa yakilishangaa hilo gari kama ilivyo msomoji unavyoshangaa jinsi ya kukaa  kwa muda mrefu mtu aliyekuwemo ndani ya gari hilo bila kushuka, vilivyokuwa na hamu ya kuona mtumiaji wa gari hilo kushuka kama ilivyo kawaida yake akizima gari hilo bado viliendelea kuangalia pale kwenye gari hilo kumuona akishuka. Wanadamu waliokuwa wapo na mambo yao wala hawakushughulika kabisa katika kumtazama huyo mwenye gari kungojea ashuke,  kimya ndani ya gari hilo kiliendelea kutawala kama ilivyokuwa limezimwa gari hilo baada tu ya kufika kwenye eneo la maegesho la magari hapo hotelini.

 Muda mfupi baadaye wale waliokuwa wapo karibu na eneo hilo waliweza kushuhudia gari hiyo likivunjika  vioo kukiambata na mlipuko mkubwa sana, gari hiyo lilirushwa juu kabisa lilipolipuka na kisha alikatua chini likabiringita na kwenda kuyazonga magari mengine yaliyokuwa yapo jirani nalo. Mayowe ya watu yalisikika baada ya kutokea mlipuko huo na kisha kila asiyekuwa na ustahimilivu aliamua kukimbia kabisa kwani waliingiwa na uoga mkubwa sana. Watu waliokuwa wapo ndani ya hoteli hiyo ya hadhi ya nyota tano hawakubaki hata mmoja kila mmoja alikimbia kutokana na hofu ya nafsi yake, hakuna aliyekuwa hapendi kuendelea kuishi duniani hivyo kusikia pamoja na kushuhudia huo mlipuko waliona ni ishara tosha ya kutaka kuporwa uhai wao ikiwa tu watabakia ndani ya eneo hilo. Ili kuyanusuru maisha yao iliwabidi wakimbie kabisa tena wakina mama ndiyo walikimbia huku wakipiga kelele kabisa.

    Muda mfupi baadaye eneo hilo lilikuwa ni kimya kabisa kutokana na kutokuwa na watu huku gari lililolipuka likiwa linateketea, ilichukua karibu robo saa badaye ndiyo maaskari wa kawaida pamoja wale wa kikosi cha zimamoto wakawa wamewasili katika eneo hilo. Utepe maalum wa kuzuia watu wasiingie katika eneo hilo wakati uchunguzi ukiwa unendelea ndiyo ulizungushiwa ,askari wa jeshi la polisi kwa pamoja walianza kazi mara moja katika kulifanyia uchunguzi suala hilo na pamoja kutoa kile kilichokuwa kikistshiki kutolwa ndani ya eneo hlo la tukio.



****

 MAKAO MKUU YA WIZARA YA MAMBO  YA NDANI
   MAKAO MAKUU JESHI LA POLISI
        DAR ES SALAAM
       TANZANIA


    Ndani ya ofisi ya mkuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania IGP Jumanne Mbwambo ambaye ndiyo alikuwa ana muda mfupi tu tangu apandishwe cheo na Mheshimiwa Rais, aliingia ofisini baada ya mkuu wa jeshi la polisi IGP Rashid Chulanga kumaliza muda wake.Muda huo IGP Mbwambo akiwa yupo ofisini kwake simu ya mezani iliita kwa mfululizo jambo ambalo lilimpelekea aipokee kwa haraka sana kwani mara nyingi sana simu  huwa ni za muhimu sana, simu hiyo alikuwa akipigiwa kwa ajili ya kazi za kiofisi tu na inabidi aipokee kwani inakuwa na umuhimu wa kila jambo. IGP Mbwambo aliichukua simu hiyo na kuipokea kwa haraka sana na kuiweka sikioni mwake, alitulia kusikiliza mpigaji wa simu hiyo alikuwa akisemaje. Utulivu humuingia akipokea simu  kutokana na kupokea simu ambazo huwa na taarifa tofauti kwa kipindi tofauti cha muda hivyo umakini ulikuwa unahitajika sana zaidi hata ya atembeavyo eneno lenye vumbi kulinda macho yake yasiathiriwe, alitulia kabisa na sikio lake moja ndiyo likawa linafanya kazi zaidi kuliko jingine katika kusikiliza taarifa hiyo.

"Jambooo" Aliitikia baada ya kusikia salamu ya kiaskari kutoka upande wa pili wa simu .

"Unasemaa!" Aliongea kwa mshangao mkubwa baada ya kupokea taarifa  kutoka kwa mwanausalama aliyempigia simu.


ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment