Sunday, February 12, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA KUMI




WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com




SEHEMU YA KUMI!!
Hakika walifanya kazi ya ziada nao lakini katu hawakuthubutu kuyatelekeza magari yao hata kulipotokea milipuko hiyo, waliendelea  na kazi ya kuzima moto na pia kuokoa baadhi waliokuwa wamejeruhiwa wakishirikiana na vikosi vya uokoaji ambao nao walikuwa wamejitoa mhanga wasikimbie kazi yao ili tu waokoe maisha ya majeruhi ambao walihitajika kupata msaada waweze kuendelea kuvuta pumzi ndani ya dunia hii.




___________TIRIRIKA NAYO


****

  Muda ambao wafanyakazi wote wanaruhusiwa kwenda makwao kwa hofu ya kukumbwa na tukio la kigaidi wakiwa hapo maofisini, Norbert alikuwa yupo kwenye ofisi ambazo alikuwa akifanyia kazi Moses hapa nchini.Ilikuwa ni ndani ya maabara ya umoja wa mataifa kwenye chumba cha ofisi ya Moses ambako walikuwa wapo wawil tu, ndani ya muda huo  kila mmoja  alikuwa tayari ameshampa  taarifa aliyokuwa akikifahamu yeye kwa upande wake. Walibadilishana mawazo na wote hawakuona kabisa kiini kilichokuwa kikiwapa mwangaza juu ya suala hilo, wala hawakuona dalili zozote za utegwaji wa mambomu mazito kwenye suala hilo. Wote waliona kuwa hilo suala lilikuwa na zaidi ya jambo nyuma yake.


   Muda mfupi baadaye wakiwa wamekaa hapo ofisni simu ya Norbert ambaye alikuwa kifahamika kama mwandishi wa habari kwa waandishi wa habari nchii, iliingia ujumbe mfupi wa maneno ambao alipoufungua tu alibaki akiguna na kisha aliinua uso wake kumtazama Moses. Ilikuwa ni habari juu ya kushuhudiwa kwa mtu akiwa amekumbwa na mlipuko kwenye hadhara kwa mara ya kwanza, jambo hilo lilimfanya Norbert aguna kwani alikuwa ameshapta uhakika wa jambo walilokuwa wakilitafuta kwa jinsi walivyoshuhudia ujumbe huuo mfupi wa maneno ambao uliingia kwenuye simu yake.

"Vipi kuna mpya?" Moses alimuuliza alipoona mguno umemtoka.

"Hii ni zaidi ya mpya na sasa ndiyo napata jibu ya chanzo hata cha kulipuka ile ya nyumba ya mwanausalama kule Kiwalani, hapa nimetumiwa na mwandishi wa habari mwenzangu yeye anasema ameshuhudia mtu akifungua bahasha nyeupe kwenye kituo cha daladala na alikumbwa na mlipuko akafia hapohapo" Norbert aliongea

"Ooooh! Damna hawa watu wanasambaza Mail bomb, inabidi tahadhari itolewe mapema kabisa la si hivyo jiji litaisha hili"

"Yap ni mail bomb hizi na katika msambazaji mmoja tayari nilikuwa nimemuweka chini ya ulinzi nilimpompekua nilimkuta akiwa na bahasaha ndani yake. Nilipoifungua bahasha hiyo nilikutana na ujumbe na bahasha nyingine yenye stempu ya mwanamke kisu akiwa ameonesha mgongo na kisha ina mhuri pamoja na neno lililosomeaka 'wito wa kuzimu', aise nilipotaka kuifungua hiyo bahasha ya ndani nilimuona yule jamaa akicheka kumbe alikuwa akijua nilikuwa nafungua kaburi. Sasa inabidi kuwasaka tu hao wanaopelekea bahasha hizo mikoani kabla hata hawajaleta maafa zaidi naamini tutapata na kingine tulichokuwa tukikihitaji ndani ya muda muafaka"


"Muda huohuo tujishughulishe na kumtafuta Jama Wa Majama nafikiri Tanzania itabaki huru kabisa ikiwa atakuwepo"

"Kwani huyu jama katekwa au kayeyuka kujihami"

"Kayeyuka kujihami ana maadui wengi sana wanaomuwinda kwani yeye ndiye pekee aliyebaki katika watu wale waliofanya utafiti baada ya kubaini kulikuwa madudu makubwa kwenye wizara zaidi ya mbili"

"Aise basi poa ila muonye shem asije akapokea mzigo kama huo tu si unajua ana kichanga itakuwa msala sana kwako"

"Hilo usihofu sana, nitafannya sasa hivi"


  Mail bomb au Letter bomb au kwa kugha ya kiswahili bomu kwa njia ya barua, ni  bomu ambalo hutumiwa mtu kwa njia ya barua. Hili bomu ambalo hutengenezwa kwa njia ya barua likiwa nalengo la kuua au kujeruhi mpokeaji wake. Bomu hili hutengenezwa kwa asilimia 75 za unga aluminium na silimia 25 za unga wa madini ya chuma, vitu hivi huwekwa kwenye kitu ambacho ni kigumu sana kupitisha joto na hewa na kisha hufungwa kwa nje na kuwekwa bahasha ya kawaida tu. Barua hii kamamtumiaji akiipata na kuifungua bila ya kujua basi  maisha yake huwa yanakatikia hapo kwani ndiyo namna ambavyo inalipuka , hii ilikuwa ni tishio sana katika miaka ya nyuma katika bara la Amerika na Ulaya ambako vikundi mbalimbali vya uhalifu vilikuwa vikiua raia kwa namna hiyo pasipo wenyewe kutambua. Mtindo huo hakuwa kusikika sana ndani ya ukanda huu wa Afrika ya mshariki na muda huo ilikuwa ni mara ya kwanza kusikika katika ukanda huu, ulikuwa tayari umemaliza mawaziri wawili pamoja na wanausalama wa vitengo tofauti pasipo wao kujua kuwa ilikuwa ni bomu la njia ya barua. Maaskari wa jeshi la polisi walihisi kuwa hiyo ilikuwa ni ni tukio la ugaidi wa kujilipua kwa mhanga lilivyoanza kukumba jiji la Dar es salaam

 Kuingia ujumbe maneno ambao ulikuwa na taarifa juu ya kushuhudiwa mtu akifa kwa mlipuko kwenye kituo cha daldala baadaya kufungua bahasha hiyo,  Norbert ndipo alipotambua kuwa maadui wa nchi hii walikuwa wakitumia mabomu hayo kuweza kuwapoteza lengo na kulikuwa na zaidi ya kitu walichokuwa wakikifanya. Aliona hiyo ilikuwa ni njia mojawapo pia ya kuvichnganya vyombo vya usalama visiweze kufanya kazi yake kwa ufasaha kabisa. Yeye mwenyewe alikuwa amesalimika kabisa kutoka kwenye kifo kama hicho haswa baada ya kutaka kufungua  sehemu ya ndani ambayo ilikuwa ipo kwenye mfumo wa bahasha ambao ilikuwa imetuna kidogo, hapo ndipo alijua kuwa sehemu hiyo ya ndani ilikuwa ni maarufu kwa jina la isolation ambayo laiti kama ingeonekana nje tu basi angekuwa ni maiti yeye na wote waliokuwa ndani ya nyumba ile kule Kiwalani.


 Bahasha ya ndani ilikuwa imewekwa mihuri ikiwa stempu ambazo hazikuwahi kuonekana kwenye ofisi za posta, stempu hizo Norbert alibaini kabisa kuwa zilikuwa na lengo la kuzidi kumshawishi mpokeaji afungue  bahasha hiyo hasa kwa kuweka mhuri ambao  ulikuwa ni kama utani vile kwani hakukuwa na mhuri kama huo. Pia aliweza kubaini kuwa  bahasha ile yenye muhuri ilikuwa imesambazwa kwa kufichwa ndani ya bahasha nyingine kwani ingeleta kabisa wasiwasi kwa wasambazaji wa kawaida na hata isingemfikia mlengwa ikiwa tu itaonekana jinsi ilivvyo kwa ndani. Hakika kulikuwa na watu wenye akili zaidi waliokuwa wakicheza na akili zao ndani ya kipindi cha muda mfupi kabla hajaweza kubaini.

"Kazi hii ishafika mikononi mwangu  jana tu ikitoka kwa CE wacha niingie kazini, waambie waliokuwa wapo kazini kwenye kazi hii wawe off sipendi kuingiliwa kazi labda nikihitaji mtu. Nina siku tisa hadi sasa za kuikamilisha kazi hii sasa  ndani ya siku siku hizi sipendi kazi yangu iharibiwe na yeyote yule nafikiri uanielewa" Norbert alisema

"Hilo halina shaka nafikiri ni kuwaambia vijana wangu pamoja na millitary intelligence waliokuwa wapo kazini wawe off ikiwa wewe umeingia kwenye kazi hiyo" Moses alisema

"Kabisa"

"Oki kila heri najua unaenda kucheza makida na rafiki kifo"

"hakika ni makida kweli jana yenyewe nimecheza naye Bugurni Chama, ningechelewa kucheza basi ningekuwa ni marehemu kwa jinsi Altezza ile ilivyobamiza kwa nguvu pikipiki niliyokuwa nimeipanda"


"Kuwa mwangalifu tu usije ukanilizia shem wangu Norene, pia ukijogoo huo uwe makini"

"Hata kuli huhitaji liwazo katika muda wa kazi hivyo na mimi nitajitaji pia sitaki uzito uzidi si unajua kazi yenyewe sifa wepesi"

"Haya ndugu kila la heri tu kwenye kazi yako hiyo"


   Muda huohuo Norbert aliondoka ofisini hapo kwa Moses akimuacha akiendelea na kazi nyingine, yeye alikuwa hajaondoka kabisa ingawa wafanyakazi wa maabara hiyo pia walikuwa wameondoka majumbani kwao. Hakuwa na uoga kuhusu milipuko iyo iliyokuwa ikitokea, aliendelea na kazi zake kwani alikuwa ni tegemezi sana ndani ya maabara hiyo hivyo hakutaka alemae kwa kitu kidgo kama hicho. Ujasiri wake wa kimafunzo ndiyo ulimuongoza kubaki hapo na si kitu kingine kile, hakufunzwa uoga kabisa hivyo kuondoka kisa suala hilo kuhofia kupoteza maisha haikuwa ndani ya ubongo wake kabisa.


****


  ROBO SAA BAADAYE

 Simu ya kuondolewa kwa vijana wa kijeshi wa kitengo maalum waliokuwa wakifuatilia matukio hayo, ilikuwa tayari imeshafika kwenye meza ya Jenerali Marwa. Alikuwa ameipata simu hiyo muda mfupi kutoka kwa Moses akiwa anamuambia juu ya uwepo wa jasusi hatari kazini, alitakiwa aondoe vijana hao kwenye kazi hiyo wasije wakaharibu kazi ya jasusi wa kuaminika aliyekuwa ameingia kazini


  Jenerali Marwa alipoipata simu hiyo moja kwa moj aliamua kumuita Mnadhimu mkuu wa ndani ya ofisi yake, haikuchukua muda L.J Belinda aliwasili ndani ya ofisi hiyo akiwa ametimia kimavazi kama ilivyokuwa kawaida. Alikuwa na kofia yenye rangi ya damu mzee pamoja na gwanda la kiofisi ambalo lilikuwa lipo kwenye muundo wa sketi na shari, ilikuwa ni nadra sana kuvalia gwanda hilo lakini kutokana na ni sehemu ya vazi la ofisini L.J Belinda alilivaa lakini hakuwa mpenzi wa kuvaa sketi kabisa akiwa yupo eneo la kazi. Alipoingia ofisini kwa mkuu wake kwakuwa alikuwa kamili kimavazi alitoa saluti ya heshima kabisa na si ile kiukakamavu ikiwa hayupo kamili kimavazi


"Keti kwenye kiti Belinda" Jenerali Marwa alimpa amri akitikisa kichwa kwa ishara kukubalia pale alipopewa saluti hiyo.

"Ndiyo Afande"  L.J Belinda aliitikia


"kuna suala jipya limeingi hapa mezani kwangu kutoka TISS ambao walikuwa wapo kwenye kazi moja na vijana niliokuwa nimewaweka chini ya amri yako" Jenrali Marwa aliongea na kisha akaweka kituo halafu akaendelea, "sasa basi inahitajika uwaambie hao vijana waachane kabisa na kazi hiyo kwani N001 ameshaingia kazini na ana siku tisa tu za kuimaliza hiyo kazi hivyo hataki kabisa kingiliwa kazi yake"

"Ndiyo mkuu nimekuelewa"

"OK fanya hivyo sasa hivi ongea na section kamanda wa section iliyoingia kazini"

"Afande"

"sina la ziada ni hilo tu" Jenrali Marwa alihitimisha na muda huo huo L.J Belinda alisimama kwenye kiti, alitoa saluti na kisha akageuka nyumana kutoka humo ofisni kwa mkuu wake.



****

  Hadi kuingiz ndani ya siku hii ya pili Norbert alikuwa ameshafinikisha kwa kiasi kikubwa cha kumteka  Cellina kwa siku  ambayo alikuwa amewasiliana naye tangu achukue namba yake kule kwenye ofisi yao alipoleta gari lililokuwa likihitajika kupigwa rangi. Muda huo majira ya jioni walikuwa wapo ndani ya hoteli moja wakiwa wapo pamoja, Cellina alionesha ni jinsi gani alikuwa amevutika na Norbert katika siku hiyo tu  hasa akiwa na muonekano wake wa kipesa. Binti huyu hakuwa tofauti kabisa na mabinti wengine wale  waliokuwa wakimpenda mtu mwenye uwezo wa juu kiuchumi ingawa alikuwa akijiweza kabisa kiuchumi, yeye mwenyewe ndani ya siku hizo alijikuta akivutika kabisa hasa akiuangalia utanashati na uzuri wa sura aliokuwa nao mwanume huyo mkware aliyemuita mahala hapo. Hakika alivutika kwa kila kitu alichokuwa nacho huyo kidume cha jogoo ambaye alikuwa akipenda kufuata kila mtetea utakaopita mbele yake, hakujua kabisa kijogoo huyo alikuwa akimfuata yeye na pia ameonesha dalili za kuvutika naye akiwa na lengo la kupata kile ambacho alikuwa hakijui kabisa kutoka kwake.

  Muda huo alikuwa ameshapewa maneno ya sumu ya kuchoombeza na akawa amelainika kimsimamo zaidi hata ya alivyolainisha usiku uliopita alipopigiwa simu  naye. Usiku ulipita alikuwa akijivuta sana kuweza kukubali ombi hilo lakini ndani ya siku hiyo mpya hakuwa na namna zaidi ya kukubali tu kwani moyo wake ulikuwa ushalainika kwa kila kitu.

"Ila Norbert kuna kitu nataka nikuulize" Cellina aliongea

"Ok kuwa huru bibie uliza tu" Norbert alimtoa hofu

"Hivi niko peke yangu kweli na huo uhandsome wako"

"Hilo swali mazingira ya eneo hli nafikiri yanakujibu kabisa"

"Kivipi?"

"Hapo ulipokaa kwenye meza hii nikiondoka mimi utabaki na nani?"

"Nitabaki peke yangu"

"Ok ndiyo ulivyo wewe kwenye vyumba vya tufaa jekundu lilipo kifuani mwangu"

"Mhh! Nawe una maneno"

"Huwa moyo wangu kama automatic doors za Ghorofa ambazo zikisogelwa kwa karibu hufunguka zenyewe, ndiyo na mimi nikipata kinipacho upendezo wa moyo basi maneno hujitoka automatically"

"Mh!" Aliguna huku akitabasamu kisha akatupa jicho kando baada ya kuona jicho la Norbert halikuwa na dalili ya kushuka lilipokuwa likimtazama usoni.

"ni sauti yenye kuburudisha kila unapoitoa, hata huko kuguna ni burudani tosha ndani ya moyo wangu"

"Mh1 Hay sina usemi mie"

    Jioni iiibadilikana hatimaye ikawa usiku wakiwa bado wapo hapo mezani, waliendelea kula na kunywa ambapo Cellin aliagiza vinywaji vyenye kilevi kwa kiasi kikubwa sana katika muda wote ambao walikuwa wapo hapo mezani, Norbert alikuwa akitumia kilevi lakini hakuacha kuwa pembeni na kinywaji kilichokuwa kikondoa kilevi kwakuwa alikuwa yupo kazini. Aliona hatari ya kujiachia na kutmia kilevi kwa kiasi kikubwa ilikuwa ni kuharibu kazi na hata kuweza kuropoka yale yaliyokuwa yakihusiana na kazi. Taratibu kinywaji kilianza kumchangamsha Cellina na akajikuta, alisogeza kiti jirani kabisa na Norbert na hata ile haya ya kike aliyokuwa nayo hapo awali ilimtoka kabisa. Ilikuwa ni mwendo wa kujiachia kwa kumkumbatia Norbert kimahaba  zaidi katika eneo hilo la hoteli ambalo kila mtu alikuwa akiendelea na mambo yake, hakujali kabisa eneo alilokuwepo ni la wazi yeye alianza kumpa mabusu motomoto Norbert huku akiongea akionekana ni mwenye furaha kupitiliza. Norbert naye alijua kuongea naye kwa kumuambia maneno ambayo yalikua yakifurahisha zaidi na kumfanya azidi kuwa na furahs kupitiliza.

  Haikuchukua hata muda mrefu Cellina alihitaji kwenda kupumzika baada ya kilevi kuwa kimezidi, alikuwa akionesha dalili za kusinzia na akimuegemea Norbert huku akimbusu kila mara, Ilikuwa ni hatua ambaye ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu sana na kijogo huyu huyu ambaye alikuwa akiwinda mtetea huyo kwasababu maalum sasa mtetea huyo aliyekuwa yu mbioni alikuwa ameshafikia  hatua ya kumdonoa kichwani ili aweze kupata burudiko. Hakutaka kabisa kupoteza muda tena ikiwa tayari ameshaingia ndani ya anga zake, alichokifanya ni kunyanyuka naye na kisha akaelekea hadi sehemu ya ndani hoteli hiyo kwenye eneo la mapokezi. Alipofika hapo Cellina alikuwa bado amemugemea huku mkono wa Norbet ukiwa umezunguka kiunoni mwake, alichukua  chumba na kufanya malipo papo hapo na kisha akaongozana na Mhudmu wa hapo hotelini kwenda kuwaonesha chumba chao. Ilikuwa ni ghorofa ya juu kabisa ya hoteli hiyo ambapo walipelekwa hadi kwenye chumba chao ambapo  Mhudumu alifungua mlango wa chumba hicho kisha akawakabidhi funguo ya mlango huo na akaondoka akiwaacha wawili, Kijogoo alimaarufu kama kidume mpando alijisokomeza ndani ya mlango wa chumba hicho baada ya mlango tu kufunguliwa akiwa ameshikilia kiuno cha mrembo wake alimyemuwekea windo akanasa. Mlango wa chumba chao kufungwa ndiyo hatua iliyofuata baada ya wao kuingia tu ndani yake, kilichofuata hapo ilikuwa ni kukumbatiana kiuhuru zaidi na mwenye jinsia mbondeko alikuwa ni mwenye papara kabisa na alikuwa akilazimisha kulana ndimi akionekana ni mwenye kuhitaji sana suala hilo.

  Hakujua kabisa kuwa huyo aliyekuwa naye alikuwa yupo hapo kwasababu maalum, yeye alichokuwa akiwaza ni penzi tu kutokana na kuchangamshwa sana na kilevi alichokuwa akikitumia. Hitaji ya kutengeneza nishati katika mwili nalo lilimfanya kijogoo aweze, yalikuwa ni majibizano ya kimapasho ya miili.

"Mamba na windo meno ndiyo huongea" Norbert alijisemea moyoni.



*JOGOO PORI NAYE





ITAENDELEA!!


No comments:

Post a Comment