Saturday, November 21, 2015

KOSA SEHEMU YA NNE




                 
        KOSA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



 ILIPOISHIA


"haya haraka sana fungeni hiyo diary nimewaambia" Ilisikika sauti  ya mwanamke kutoka mlangoni ikiwapa amri Hassan na Hussein.

"mama! Umerudi?!"" Wote kwa pamoja waliacha kusoma diary kisha wakamkimbilia mama yao halafu wakamkumbatia huku wakisema, "shikamoo mama".
"marahaba wanangu, wazima nyinyi?" Mams aliitikia salamu halafu akawajulia hali.
"sisi wazima mama, za safari?" Hassan alimuuliza mama yake.
"salama tu, wanangu mnasahau hadi kula hebu twendeni kwanza mkale, saa mbili hii " Mama yao aliwaambia, Hassan na Hussein walishtuka kusikia kuwa muda wa kula umefika tayari. Usomaji wa shajara uliwafanya hata wasitambue kama umeenda kiasi hicho, wote kwa pamoja walitazamana kwa mshangao.
"hivi hiyo diary kawapa nani? Baba yenu?" Mama yao aliwauliza.
"Ndiyo mama" Hussein alijibu.
"haya fungeni mkale mje kuendelea kusoma wanangu wazuri"  Mama yao aliwaambia kisha akatoka chumbani kwao.




ENDELEA NA MKASA HUU WA KUSISIMUA

SEHEMU YA NNE!!
Hassan na Hussein walimfuata mama yao  kuelekea katika ukumbi wa chakula, walimkuta baba yao akiwa tayari yupo mezani akiwa anakula na  chakula. Nao walijumuika naye katika chakula hicho wakiwa kimya kuonesha nidhamu ya kula baada ya kumuona mama yupo mezani, kitendo cha mama yao kuchukia maongezi wakati wa kula ndicho kilichopelekea ndicho kilichopelekea mapacha hawa wakae kimya. Hassan na Hussein walikuwa wakila kwa haraka tofauti na ilivyo kawaida yao, jambo hili liligunduliwa hata na mama yao.
"hey! Hivi nyie mnakimbizwa?!" Mama yao aliuliza kwa jazba kutokana na kushindwa kuvumilia kuwaangalia wakila namna hiyo, Hassan na Hussein walishindwa kujibu swali hilo na wakabaki wameinamisha vichwa vyao.
"si nawauliza nyie, mpo vitani hapa mpaka?! Naona diary ndiyo inawachanganya sio, sasa mkimaliza kula muilete!" Mama yao aliongea kwa ukali akiwa anawatazama  usoni kila mmoja.
"mke wangu wasemehe....na nyinyi hebu kuleni taratibu" Baba yao aliongea.
"hapana Baba Ilham hii sio adabu ya kula yaani hata dini hairuhusu kula namna hii, inabidi niwanyang'anye hiyo diary ili washike akili zao" Mama yao aliongea.
"usifanye hivyo mke wangu, nimewapa kwa lengo maalumu na nitakuambia hilo lengo....haya na nyinyi hebu kuweni na adabu ya kula" Baba yao aliongea kumtuliza mke wake kisha akawageukia Hassan na Hussein akawakaripia. Baada ya hapo mlo ulilika kwa taratibu hapo mezani hadi wanamaliza, hali hiyo kidogo ilimfurahisha Mama yao na akawa ameondoa hasira yake aliyokuwa nayo hapo awali. Baada ya kumaliza kula jambo walilokuwa wanaliwaza vichwani mwao ilikuwa ni kwenda kuendelea kusoma shajara, walinawa mikono yao baada ya kula waliondoka ukumbini hapo kuelekea chumbani. Wahka wa kusoma shajara hiyo ndiyo uliokuwa unawasumbua kwa muda huo walikuwa wanaona wanachelewa kwenda kuisoma shajara hiyo, walipofika chumbani kwao waliifungua shajara kwa pupa hadi walipoishia kisha wakaanza kuisoma.

****

"Maneno yake kwangu hayakusikika ingawa yalikuwa yanasikika na watu waliokuwa pembeni yangu, binti huyu alizidi kuongea akijua nipo naye kutokana na macho yangu kutonasuka katika uso wake kama yamenasa na gundi. Akitabasamu kwangu ilikuwa ni ugonjwa tosha hata mapigo ya moyo yakienda mbio muda wote, binti huyu aliongea sana na hatimaye akaniuliza swali ambalo sikulisikia kutokana na kuwa mbali kimawazo. Kitendo cha kutolijibu swali lake kilisababisha anigundue kama sipo naye, aliniuliza swali hilo tena na nikawa sikumjibu kutokana umbali ambao mawazo yangu yako. Binti huyu alipoona sikumjibu swali lake kwa zaidi ya mara mbili na macho yangu  yakiwa yanamtazama bila kupepesa hata jicho moja, aliamua kunirudisha kwenye gari hilo kimawazo kwa kunifanyia kitu kilichonirudisha ndani ya gari kimawazo kwa kunipiga kibao cha mkono baada ya kushindwa kupepesa macho hata aliponisogezea vidole vyake karibu na macho yangu. Kibao hicho kilinishtua sana na nikawa kama mtu mwenye hofu asikiapo sauti ya kutisha, kushtuka kwangu kulisababisha huyu binti acheke na hata abiria wengine nao wacheke. Abiria waliokaa upande wa nyuma wote walikuwa wananitazama huku wakicheka, nami nikajikuta nikicheka sana baada ya kushtuka vibaya.
"is jy okay(upo sawa)" Binti aliniuliza kwa lugha ya kiafrikaas baada ya kuacha kunicheka.
" ek  okay(nipo sawa)" Nilimjibu huku nikiwa najihisi nimefanya jambo la aibu kwa kuwa mbali kimawazo.
"okay, My naam is Sarina en jou?(sawa, jina langu ni Sarina na wewe?) Aliniuliza swali baada ya kumjibu kama nipo sawa.
"my naam is Abdul...Abdulhafidh" Nilijitambulisha baada ya binti huyu kuhitaji utambulisho wangu, hapo ndipo nilitambua kama anaitwa Sarina na jina lake liliendana na urembo wake alionao kabisa. Hakika alikuwa mzuri kama jina lake lilivyo zuri, nilijikuta nikivutiwa na jina lake sana.
"befok naam, is jy moslem(jina zuri sana, hivi wewe ni muislamu)?" Alilisifia jina langu kisha akaniuliza.
"ja ek moslem(ndiyo mimi ni muislamu) Nilimjibu swali lake, napenda nishukuru tu kwa kupata nafasi ya kuishi katika kijiji ambacho rafiki yangu Jonas alinikaribisha na akanipa hifadhi kama ndugu yake, vinginevyo ningekuwa nababaika sana katika kuongea lugha ya kiafrikaas. Kule ndipo shule yangu ya awali ya kuijua lugha hii na iliyonifanya nisibabaike katika kuongea mbele ya mtoto wa kike, mapigo ya moyo bado yalikuwa yapo juu sana kila muda hasa binti anapozidi kuongea na mimi.
"good ek moslem te(vizuri mimi ni muislamu pia)" Sarina aliniambia kwa uchangamfu sana na kunifanya nisahau sehemu ya matatizo yangu yaliyonikuta kwa kipindi hicho, ninavyoongea hivi unaweza kusema labda nimechanganyikiwa kila nilipoliona tabasamu la Sarina au labda nimelogwa na muonekano wake wake. Hali niliyonayo mimi inaweza hata kumkuta mwanaume yoyote rijali na asiye na mtu kama mimi, napenda niseme Mungu kamjaalia kila kizuri na hata kasoro nilikuwa sizioni na nilimuona alikuwa ni mwanadamu aliyekamilika. Uzuri wake Sarina ulinifanya hata nikufuru kwa kumfananisha na malaika waliotukuka katika ufalme wa Muweza wa kila kitu, maongezi baina yetu yaliendelea yakilenga kufahamiana zaidi kwetu sote. Sarina nilikuja kumuelewa kama ni binti mzaliwa wa mataifa tofauti yaani chotara anayefanya kazi huko Widhoek ninapoelekea, baada ya masaa kadhaa gari ilifika Swakopmund ikaweka kituo cha muda mfupi kisha ikaendelea na safari baada ya muda wake wa kuwa hapo kituoni kuisha. Safari yetu iliendelea kwa amani huku maongezi kati yetu yakizidi kuchukua nafasi zaidi, Sarina mchangamfu, Sarina mrembo na Sarina huyuhuyu mwenye kuvutia ndiye aliyenipa furaha kwa mara ya kwanza tangu napatwa na matatizo. Hadi tunaingia jiji la Widhoek baada ya masaa manne tangu tusafiri, nilianza kuhisi huzuni ikianza kuingia taratibu ndani ya moyo wangu hasa kila nikifikiria kuwa muda mfupi ujao tutatengana gari hiyo itakapofika mwisho wa safari. Tulipofika mwisho wa safari ilitubidi tuagane na kila mmoja ashike njia yake, hapo ndipo ukawa mwisho wa kuongea naye kwa siku hiyo. Moyoni nilijihisi kuumia na nikaona kuwa sitoweza kuonana naye tena ndani ya jiji hili kubwa la nchi hii, niliamua kujikaza kiume nikawa natoka ndani ya kituo cha mabasi cha jiji hilo.
" Verskoon my(samahani)" nilisikia sauri ikitokea nyuma yangu iliyonifsnya nigeuke, nilimkuta kijana kashika kasha dogo lenye rangi nyeusu.
"is jy Abdul?(wewe ni Abdul)?" Kijana huyo aliniuliza.
"ja(ndiyo)" Nilimjibu huku nikiwa nina maswali mengi sana ambayo nilitaka majibu yake, yule kijana alinipatia lile kasha jeusi ambalo nilipolishika nilihisi lina kitu chenye uzito wa wastani ndani yake. Nililipokea lile kasha kisha nikataka kummuliza swali lakini nilijikuta nikijikuta nikisukumwa na kikumbo cha mtu kutoka nyuma yangu hadi nikataka kuanguka, nilipogeuka nilikutana na mtu aliyebeba mabegi mawili makubwa ya kuwekea nguo.
" Jammer!(samahani!)" Yule aliyenipiga kikumbo na mabegi yake aliniomba radhi kwa haraka, nilikubali kumsamehe kisha nikageuka nyuma nilipomuacha yule kijana aliyenipa kasha. Hakika nilikuwa nina maswali mengi sana ambayo yalihitajika kujibiwa na huyo kijana, maswali yangu yaliishia moyoni tu baada ya kutomuona yule kijana mahali nilipomuacha. Nikiwa nafikiria huyu kijana kaondoka muda gani eneo nililomuacha, lile kasha lilianza kutetemeka kisha mlio wa simu ukaanza kusikika ukitoka ndani ya kasha hilo. Nililifungua hilo kasha kwa haraka nikaiona simu ikiita kwa fujo pembeni yake kuna ufunguo wa wenye bango lenye namba 108, niliipokea ile bila hata kufikiria inatoka wapi kutokana na kuchanganywa na matukio yanayonitokea kama vile  kujikuta nchini humo na jinsi kijana aliyenipa kasha alivyoondoka bila hata kumuona.
"Abdul karibu Widhoek jiji kuu la Namibia, sasa ondoka hapo jirani na mlingoti wa taa za kituo cha basi na uelekee kwenye kituo cha taksi na hapo utakuta teksi nyingi katikati kukiwa kuna gari yenye rangi tofauti na teksi hizo. Panda hiyo  gari na utulie kama maji mtungini hadi utakapofika mwisho wa safari yako" Sauti ninayoifahamu ilinipa maelezo ya kitu ambacho ninatakiwa kukifanya, maelezo haya kiukweli yalinishangaza sana kwani anayeongea sauti yake ilikuwa sio ngeni kwangu na alionekana kutambua nilipo. Sikuweza kutambua ananiona vipi lakini akili yangu ilinipa uhakika wa jambo hioo kuwa ninaonekana na mtu anayenichezea mchezo huu, ni kweli nilisimama jirani na nguzo  ya taa kwenye kituo cha mabasi na hata aliniambia nitoke eneo hilo nilijikuta nashtuka. Niliirudisha ile simu kwenye kisha nikaenda hadi kwenye kituo cha teksi nilichoelekezwa na nikaikuta gari niliyotajiwa, niliingia ndani ya gari hiyo bila hata kujifikiria nikakuta pembeni yangu kuna suti nadhifu na viatu. Mbele kulikuwa na dereva akiwa yupo kwenye usukani na mkanda kafunga.
"vua hayo matambara na uvae hiyo suti na viatu vyake" Dereva wa gari hiyo aliniambia kwa kiswahili fasaha bila hata kuniangalia, nilitii kila alichoniambia na nikavaa suti iliyonifanya nionekane kama nilivyokuwa jijini Dar es salaam nikiwa kwenye kazi zangu. Dereva huyu alianza kuendesha kwa mwendo wa taratibu kisha akaongeza wa gari baada ya kuingia barabara kubwa, baada ya dakika kadhaa tulikuwa mbele ya hoteli ambayo nilikuwa nimechukua chumba nilipokuja  kwa mara ya kwanza ndani ya nchi hii kibiashara na chumba hicho nilikuwa nakifanyia malipo ili nikipata safari ya kibiashara nikija tena nchi hii nifikie hapohapo. Hilton hotel ndiyo hoteli niliyochukua chumba na hadi namba ya chumba nikawa naikumbuka, nilishuka baada ya dereva kunitaka nifanye hivyo nikawa nimebaki nikiwa nashangaa huku lile kashaa likiwa mkononi mwangu. Nilijifikiria kwa muda mfupi kisha nikatoa ufunguo nilioukuta ndani ya lile kasha na nikaitazama namba iliyopo kwenye kibango cha ufunguo huo chenye umbo la kadi ya benki, namba 108 niliiangalia kwa mara ya pili na nikajikuta nikiikumbuka kuwa ni namba ya chumba changu katika hoteli iliyopo mbele yangu na funguo ni yangu. Sikujua ile funguo kaitoa kwani mara ya mwisho ilikuwa nyumbani kwangu katika kabati langu na mwanzo nilishindwa kuitambua kwa sababu ya papara ya kulifungua kasha nililopewa baada ya simu kuita.
Kuchanganyikiwa kwa jambo linalonitokea nilianza kukuzoea na hata hapo niliona kawaida, niliondoka kuingia ndani  ya hoteli hiyo huku nikipokea salamu za wafanyakazi kutokana na unadhifu wangu hasa nikiwa katija vazi la suti niliyoikuta ndani ya gari. Nilipita mapokezi katika hoteli hiyo kisha nikaingia kwenye lifti iliyonipeleka hadi ghorofa ya tatu, lifti ilipofika ilijifungua mlango  na nikatoka kuelekea chumbani  kwangu. Niliingia ndani ya chumba changu kwa amani na nikajikuta natabasamu baada ya kuyafikia mazingira niliyoyakumbuka kwa muda mrefu, nilifunga mlango kisha nikajitupa kitandani ili kulilalia godoro laini kwa mara ya kwanza tangu nilipojikuta ndani ya nchi hii. Ulaini wa godoro nilianza kuusikia ukinipa burudani kwenye mgongo wangu ambao ulikuwa umelala kwenye kitanda kikukuu kwa muda wiki kadhaa, niliona raha ya aina yake kwa kulalia aina ya kitanda nilichokuwa nina hamu nacho kwa muda mrefu. Raha hiyo haikudumu kwa muda mrefu kwani ilikatishwa na mlio wa simu ikiita kwa fujo, hapo niliipokea simu kwa haraka.
"naona unastarehe sana ukijisahau una kazi iliyokuleta huku, sasa basi jiandae ukaanze na mwanamke anayeitwa Jasmin muda huu na orodha nyingine ipo kwenye meza ya kioo iliyopo katikati ya masofa" Sauti ile ile iliyonipa amri mwanzo ndiyo iliyotoa maelezo kisha simu ikakatika hapohapo ikiniacha nikiwa sina furaha hasa nilipoifikiria kazi hii ninayoenda kuifanya kwani sikuwa tofauti na malaya anayefanya mapenzi kwa ajili ya pesa. Dola za kimarekani ndiyo zinanifanya niende nikafanye mapenzi na wanawake nisiowajua ili kuzipata katika kipindi hichi cha shida huku ugenini tena nikiwa nachungwa kama vile mfugo. Niliifuata karatasi iliyokuwa kwenye meza ndogo ya kioo nikaitwaa kisha nikaanza kuisoma vizuri, majina yaliyokuwa kwenye ile barua hayakuwa tofauti na haya yaliyokuwa humu.  Jasmin Peterson nyumba namba 14 mtaa wa R.Van der walt, ndiyo nililotakiwa kulianza katika orodha hiyo. Nilipomaliza kulisoma sikuwa na muda wa kupoteza kuanzia hapo na ilinibidi niondoke muda huohuo kuelekea nilipoelekezwa na karatasi ile, nilishuka hadi chini kwa kutumia lifti kisha nikatoka hotelini hapo nikaingia kwenye teksi moja niliyoikuta ipo pembeni ya hoteli hiyo.
"R.Van der walt street house number 14(mtaa wa R.Van der wailt nyumba number 14)" nilimuambia dereva wa teksi  niliyopanda ambaye hakuongea lolote zaidi ya kuitikia kwa kichwa kisha akaweka gia na kuachia breki, gari iliondoka hotelini kwa mwendo wa wastani kuelekea nilipomuelekeza. Baada ya dakika kumi gari ilikuwa imeshafika jirani na nyumba niliyoelekezwa, nilimlipa dereva ujira wake  kisha nikasogea hadi mbele ya geti la nyumba namba kumi na nne ambayo ni ya kifahari sana. Pembeni ya geti kubwa la nyumba hiyo kulikuwa kuna geti dogo la kupitia watu ambalo ndiyo nililolisogelea nikiwa nina wasiwasi sana kutokana na ugeni wa kazi hii niliyopewa, mlango wa geti dogo ulifunguka baada ya mimi kufika karibu na mlinzi mwenye nguo zilizofanana na askari ndiyo alikuwa mbele yangu na begani ana bunduki nzito sana.
"welcome sir(karibu mzee)" Mlinzi huyu alinikaribisha kwa uchangamfu na alionekana kuutambua ujio wangu, wasiwasi uliniingia ndani ya kichwa changu ingawa nilijikaza kisabuni nisijulikane nina hofu yoyote. Niliingia ndani ya uzio wa nyumba hiyo iliyoonekana ina ulinzi mkubwa sana kutokana na uwepo wa walinzi wengine wenye suti  ndani ya jengo la nyumba hiyo, mmojawapo wa walinzi wenye suti aliniongoza hadi ndani ya nyumba hiyo ya kifahari kwenye sebule.
"mam your guest(mama mgeni wako" Yule mlinzi niliyeingia naye alimuambia mwanamke mwenye kigauni kifupi cha kulalia niliyemkuta sebuleni hapo.
"welcome handsome boy(karibu mvulana mzuri) Yule mwanamke ambaye kwa kukadiria angekuwa na miaka takribani arobaini na ushee alinikaribisha kisha akasimama kunifuata, alinikumbatia kisha akanibusu linaloitwa busu la kifaransa  mlinzi wake akiwa pembeni. Aliporidhika kunibusu alimuangalia mlinzi  aliyekuwa kasimama pembeni yake halafu akamkaripia,"you bloody fucking what are you waiting for , get out!".
"ok mam(sawa mama)" Mlinzi aliitikia kwa utiifu kisha akatoka nje akatuacha tukiwa wawili katika sebule hiyo na hakuwa na kufanya zaidi ya kutii amri aliyopewa na bosi iliyo na matusi mazito juu yake. Huyu mwanamke ambaye nilimtambua kama Jasmin alianza mambo yake papo hapo na mimi ikanibidi nitimize wajibu ulionileta hapo kwa mbinu zote ninazozijua, baada ya masaa matatu nilikuwa nimemaliza nusu ya kazi yangu iliyonileta ambayo niliifanya kwa msukumo tu. Kitendo cha kufanya mapenzi na mwanamke nisiyemjua kwangu niliona ni kazi ya kujidhalilisha ingawa tayari nimefanya na sasa ninahitajika nifanye kwa mara nyingine, mtaka cha uvunguni siku zote lazima ainame na huwezi ukachukua cha uvunguni ukiwa umesimama. Pia mtaka waridi sharti avumilie miiba, namaanisha ukitaka jambo lolote zuri kwa njia ya mkato lazima ukubaliane na hali ya kulipata hilo jambo. Binafsi nilikuwa nataka dola milioni moja ili niokoe kampuni yangu kwa muda wa siku kumi hivyo lazima nikubaliane na njia rahisi ya kuipata na masharti yake.


*ABDULHAFIDH ANAANZA KUIKABILI KAZI NA SASA YUPO KAZINI

*JE KAZI HIYO ATAIFANIKISHA?



MUHIMU: UKIITAKA HADI MWISHO IPO KWA BEI NAFUU WASILIANA NA MWANDISHI KWA UJUMBE MFUPI WA MANENO NAMBARI  +255713 776843

No comments:

Post a Comment