Tuesday, November 24, 2015

KOSA SEHEMU YA SABA




 KOSA


MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE





 ILIPOISHIA


" wat is die probleem?(nini tatizo?)" Sauti ya Sarina ilinirudisha ndani ya chumba hicho na nikakumbuka uwepo wake kwa muda huo, niliinamisha uso wangu chini hata baada ya kusikia swali lake . Sarina aliamua kunishika kidevu kisha akaniinua juu uso wangu na nikawa natazamana naye, hapo ndipo nikatambua kama Sarina ametoka kwenye kochi alipokuwa ameketi na sasa yupo mbele yangu.
" Vertel my wat is die probleem?(niambie nini tatizo)" Sarina aliniuliza huku akinishika shavuni kwa mikono yake milaini hadi nikajihisi nimesisimka mpaka kwenye nywele zangu, niliinamisha kichwa changu chini nikihofia kuonekana naongea alinacha kama nilivyoonekana na Jonas kwa mara ya kwanza nilipomueleza matatizo yaliyonikuta. Nikiwa nimeinamisha kichwa changu hivyo mkono laini wa Sarina ulichezea nywele zangu za singa ambazo sikuwa nikizitunza, mwili wote ulinisisimka kwa jinsi alivyokuwa anazichezea nywele zangu.
"Sarina  is 'n lang storie te vertel, maar ek het besef ek
het ernstige probleme(Sarina ni hadithi ndefu nikikusimulia ila tambua nina matatizo makubwa)" Nilimuambia Sarina huku nikiangalia juu ya dari kinyonge sana kutokana na matatizo niliyonayo, macho yangu juu ya dari yalivutika ni kitu nilichokiona na nikabaki nikikihakikisha kwa umakini.
"Haa!  Dit dwaas(Haa! Pumbavu huyu)" Nilisema kwa hasira huku nikisimama nikiangalia juu ya dari nikiwa nimekunja sura.





ENDELEA NA MKASA HUU WENYE KUSISIMUA NA KUELIMISHA

SEHEMU YA SABA!!
Maneno yangu yalimshtua hata Sarina na  ikambidi aangalie juu nilipoangalia mimi ili aweze kuona kilichonifanya nipayuke kwa hasira, kamera ndogo sana ya CCTV (Closed Circuit Television)  ilikuwa imefumgwa kwa ustadi mkubwa jirani ns taa ya kisasa ya kuning'inia iliyopo humo chumbani. Ufungwaji wa kamera kama hii katika chumba cha hoteli ni kinyume na utaratibu wa sheria za hoteli yoyote ili kuwapa uhuru wateja wao, siku zote kamera za hotelini huwa zinafungwa kwenye ukumbi mwembamba unaotenganisha vyumba vya hoteli na si vyumbani. Sasa hapo ndipo nikaona kuwa nafuatiliwa na mtu ananifanya mimi mtumwa wake kwani kunipa kazi yake haramu, pia nilikumbuka kwa mara ya kwanza nilipoingia humo ndani nilijitupa kitandani na nikapigiwa simu na huyu mtu akitaka nikafanye kazi na si kustarehe. Hapo ndipo nilipopata uhakika kuwa natazamwa na huyu nikiwa humo ndani, mawazo yangu hayo niliyawekea uhakika lakini niliuondoa  uhakika huo na jambo la kuwa nafuatiliwa kila hatua yangu hata nje ya hoteli ndiyo lilinijia kutokana matukio kadhaa yaliyonikuta nikiwa nchini Namibia. Kwanza tukio la mimi kuletewa barua kule kijijini kwenye ghuba ya Walvis na tukio la kupigiwa simu pale kwenye kituo cha basi niliposhuka nikitakiwa nitoke kwenye nguzo ya taa, mawazo hayo yalipita kwenye kichwa changu kwa dakika moja tu na dakika iliyofuata nikaweka meza ndogo jirani na eneo ilipo kamera hiyo kisha nikapanda  nikaivuta na nikaitoa hapo nikabaini uwepo wa waya mwembamba ambao ulionekana unaelekea kushoto kwangu ukiashiria muwekaji wa hii kamera hayupo mbali na eneo hili. Sarina muda wote alikuwa ananitazama tu bila hata kutambua kipi ninachokifanya, wasiwasi mwingi ulikuwa usoni mwake kwa kila kitendo ninachokifanya hakuelewa zaidi ya kuitazama kamera hiyo. Kamera hii ilionekana kuwekwa na mtu ambaye hayupo mbali na eneo hili na akili yangu ikaniambia niangalie chumba cha kushoto kwangu na si vinginevyo.
" is wat(kuna nini)" Sarina aliuliza akiwa na sura ya wasiwasi sana kutokana na mambo niliyokuwa nayafanya muda huo.
" iemand geplaas sommige kameras hierin, en wag
vir my hier( kuna mtu kaweka kamera humu ndani, nisubiri hapa") Nilimwambia Sarina ambaye mwili wake ulikuwa hautulii, Sarina alikubali kwa kutikisa kichwa na mimi nikatoka nje  kuelekea kwenye chumba kilichopo kushoto mwa chumba changu kwa haraka sana. Nilipofika kwenye chumba hicho mlango ulifunguliwa na akaonekana kijana mmoja  mwenye asili ya kihindi akiwa na haraka sana na aliponiona mimi alionekana kushtuka sana, kitendo cha yeye kuonesha wasiwasi kilinipa asilimia mia kwamba kuna kitu anakijua kinachonihusu ingawa sikutambua ni kitu gani. Sikutaka hata kumpa nafasi ya kufikiria jambo jingins lolote baada ya hapo kwa kuhofia kuzidiwa ujanja naye, nilimpiga teke la tumbo lililomrudisha ndani ya chumba kisha na mimi nikaingia ndani kwa haraka bila hata kuangalia usalama. Huko nilikutana na vijana wawili wenye ngozi nyeusi wakiwa wamekaa kwenye vioo vya tarakilishi zaidi ya moja vikiwa vinaonesha mandhari ya chumba changu kwa kila upande ikionesha kwamba kamera ipo zaidi ya moja mule chumbani. Wale vijana waliokaa kwenye vioo vya tarakilishi waliponiona waliniwahi kwa mapigo mbalimbali ambayo hayanikia kabisa, nilipambana nao kwa nguvu zote hadi nikawanyamazisha kwa muda kisha nikamgeukia yule mhindi ambaye alikuwa kaanguka chini akitoa miguno ya maumivu kutokana na teke zito nililompiga tumboni. Niliukamata ukosi wa nguo yake aliyovaa kisha nikamuinua huku nikimtazama kwa hasira, hasira za mambo ninayofanyiwa zilianza kunipanda kichwani na nikajikuta nimemuachia ngumi mfululizo kisha nikamvuta hadi dirishani. Nilifungua dirisha kisha nikamtoa nje  nikamuinamiaha kichwa chini akiwa anatazama eneo la maegesho.
"who sent you(nani kakutuma)?" Nilimuuliza nikiwa sijali makelele aliyoanza kupiga muda huo.
"I don't know him (simjui yeye) simjui kabisa nakuapia" Mhindi huyu aliongea kingereza huku akichanganya kiswahili kutokana na uoga na hapo ndipo nikabaini anajua kiswahili.
"utatumwaje na mtu usiyemjua?" Nilimuuliza huku nikitishia kumuachia ghorofani aanguke.
"napokea emails na simu za ketu lakini simjui zaidi ya kuitambua sauti yake" Mhindi huyu alijibu huku akionesha kwamba ni muoga wa kifo na si mtu mwenye roho, Nilimrudisha juu kisha nikampiga pigo moja la kisogoni akazirai. Nilitoka humo chumbani kwa haraka na nikarejea chumbani kwangu nilipomuacha Sarina, nilipoingia tu nilichukua mkoba wa pesa na vitu vya muhimu kisha nikamshika mkono Sarina nikaondoka naye nje bila hata kusema lolote. Tulishuka hadi mapokezi kisha tukaingia kwenye gari yangu na tukaondoka eneo hilo upesi sana, Sarina alibaki ametulia tu akiwa na wasiwasi mwingi sana. Niliondoa gari kwa kasi sana nikiwa sina uelekeo maalum wa kuelekea kwa dakika takribani kumi na tano hadi nikawa nimeuacha mji mbali kidogo na sasa nikawa nipo katika sehemu tulivu yenye miti mingi pamoja na nyumba chache.
"is jy reg(upo sawa)" Nilimuuliza Sarina huku nikiegesha gari pembeni ya barabara.
"ja , Wat gaan aan?(ndiyo kuna nini kinaendelea)" Sarina aliniuliza huku akiwa na wasiwasi mwingi sana hata akawa anaelekea kuniogopa kwa mambo ninayofanya, niliamua kumsimulia kila kitu kuhusu mimi nikiwa naficha baadhi ya mambo kama vile kutembea na wanawake wawili ambao ni matajiri pamoja na suala langu la kuchukua machangudoa nilikuwa jijini Dar es salaam. Maelezo yangu yalimfanya Sarina ashushe pumzu halafu akanipa pole kwa yaliyonisibu na akaniambia
" dit het gelyk asof niemand is verontreg en nou is
hy het teruggeslaan, is daar iemand wat jy
aanstoot?(inaonekana kuna mtu umemkosea na sasa analipa kisasi, je kuna mtu umemkosea?)". Swali la Sarina lilinifanya nijifikirie sana ili kukumbuka sehemu nilipomkosea mtu lakini mwisho wake sikukumbuka kama nilimkosea mtu kiasi cha huyo mtu kuamua kunifanyia hivi. Ukweli mwanadamu ana kawaida ya kusahau kila kitu na hata kama akifanya jambo baya huweza kusahau kabisa, ndivyo na mimi nikawa nimesahau kama niliwahi kumfanyia ubaya huyu mtu anayenipigia simu kila kitu.
" Nee, ek het nie aanstoot iemand te bereik hierdie
stadium voer(hapana, sijamkosea mtu mpaka afikie hatua ya kunifanyia hivi)" Nilimjibu Sarina huku nikionekana kuchanganyikiwa kabisa na hata gari lenyewe nisingeweza kuendesha.
" maw ek het nêrens om te gaan in hierdie stad (yaani hapa sina hata pa kwenda)"  Niliongea kwa unyonge huku mikono nikiwa nimeweka kichwani nikiwa nimeuegemea usukani wa gari, Sarina alikuwa akifanya kazi ya kunifariji huku mikono yake ikiwa inatalii kichwani mwangu hasa kwenye nywele. Nilipoinua uso wangu juu nilimuomba Sarina aendeshe gari kama anaweza, alikubali na mimi nikamuachia usukani akawa ananiongoza kwa kutumia uelekeo nisioujua. Sarina alipita njia mbalimbali za mkato na mwishowe akawa ametokea sehemu nyingine ya mji wa Widhoek ambayo nilikuwa siijui, tulikatisha mitaa kadhaa na hatimaye tukaingia sehemu yenye nyumba nyingi zinazofanana zenye hadhi ya kutumiwa na watu wenye maisha ya kawaida zikiwa na namba kwa kila nyumba. Sarina aliingiza gari kwenye uzio wa nyumba mojawapo na hapo ukawa ndiyo mwisho wa safari yetu, alishuka kwenye gari na mimi nikashuka sambamba naye. Tuliingia ndani ya nyumba hiyo yenye muonekano wa kawaida wenye kuvutia, Sarina alinikaribisha katika nyumba hiyo huku akinifahamisha kuwa ndiyo nyumba yake katika mji huo. Alinieleza kuwa ndiyo sehemu ambayo anaishi na ndiyo sehemu aliyokuwa anakaa siku zote katika mji huo, nilipata faraja angalau kidogo kwa kupata sehemu ya kujihifadhi kutokana na tukio langu la kuchafua usalama kule hotelini. Nilijua fika tukio langu la kumpiga teke yule mhindi pale mlangoni litakuwa limeonekana na kamera ya ulinzi iliyopo kwenye ukumbi mwembamba unaotenganisha vyumba pale hotelini, niltamani sana Sarina anikaribishe hapo kwake walau nikae kwa muda kabla hajaniambia nitakuwa niikiishi pale na hata aliponiambia nitakuwa nikiishi pale nilishukuru moyoni. Ukarimu alinionesha Sarina kwa kunipa hifadhi ulinifanya nimshukuru mungu kwasababu yeye ndiyo chanzo cha kukutana na mwanamke mkarimu na mwenye moyo wa kipekee mpaka anafikia kunipa hifadhi mtu kama mimi niliyejuana naye siku mbili zilizopita katika basi dogo litokalo Walvis kuja huku Widhoek, ingekuwa mwanamke mwingine asingejaribu kufanya hivyo hasa kwa mambo niliyokuwa nayafanya pale hotelini. Ukweli alinifanya nimuone ni mwanamke wa  kipekee sana  hapo nikamlinganisha na Huwaida kwa mara ya pili nikaona kuwa Huwaida halingani naye hata kama wote wangekuwa ni vito vya thamani basi Sarina sngekuwa yupo juu zaidi,  nilianza kukumbuka jinsi nilivyomuona Huwaida kwa  mara ya kwanza na jinsi nilivyohangaika naye ili kuupata moyo wake lakini nikaukosa.
  
     Nakumbuka siku ya kwanza kumuona Huwaida ilikuwa ni siku ya kwanza ya mimi kukanyaga miguu yangu katika chuo kikuu cha Dar es salaam kama mwanafunzi wa mwaka wa kwanza hapo chuoni, kwenye zoezi la usajiri wa wanafunzi tulikaa mstari mmoja na yeye alikaa nyuma yangu. Nikiwa kwenye foleni hapo ujumbe mfupi wa maneno wa mtandao wa whatsapp uliingia kwenye simu yangu na ikanilazimu niufungue na niusome. Nakumbuka vizuri siku hiyo nilivaa kama hadhi ya familia ninayotoka ilivyo, uturi niliojipulizia uliashiria natoka kwenye familia ya gharama, miwani ya giza niliyovaa ilinifanya nizidi kuonekana nimependeza kutokana na kupangilia rangi za nguo nilizozivaa. Ujumbe mfupi ulioingia kwenye simu yangu ulinifanya nianze kuujibu palepale huku nikisahau kama mstsri inaenda, nikiwa naandika kwenye simu yangu aina ya Ipad mini nilihisi kuguswa na mkono wenye joto ambalo lilileta athari kidogo kwenye bega langu ambapo uligusa. Sikuhitaji stashahada au shahada ya aina yoyote katika kuutambua mkono ulionigusa ulikuwa wa jinsia gani, nilitambua wazi kama nimeguswa na mkono wa msichana na kama ningemuita mwanamke basi ningejiona namzeesha mapema. Niligeuka nyuma kumuangalia huyo mwanamke aliyenigusa na hapo moyo wangu nikahisi kama umetaka kupasuka kwa sura niliyoiona iliyonifanya niduwae sana, nilimuona msichana mrembo mrefu mwenye juba la rangi  nyeusi lililomkaa vyema mwilini mwake. Binti huyu alibeba kipochi kipochi kidogo pamoja na bahasha  ndogo mkononi, asili ya binti huyu ilikuwa haitofautiani na mimi kwani wote tulikuwa wasomali ila yeye alionekana kuwa na weupe kwa mbali uliomfanya azidi kuonekana mrembo na kunifanya nizidi kumshangaa hadi nikavua miwani ya giza niliyokuwa nimeivaa.
"kaka foleni inatembea" Aliniambia huku akionesha tabasamu hafifu usoni mwake, mimi nilishtuka kisha nikaangalia mbele nikakuta foleni imesogea na sasa ipo mbali kidogo na mbele yangu kulikuwa na uwazi mkubwa kutokana baada ya mimi kusimama nikijibu ujumbe mfupi wa maneno mtandao wa Whatsapp.
"oooh! Sorry" Niliongea kwa mtindo wa aina yake kama mmrekani au mtanzania aliyekaa  Marekani kwa muda mrefu, hapo ndipo ukawa mwanzo wetu wa kuongea hadi tunamaliza kufanya usajiri na pia nilikuja kubaini wote tunasoma kozi moja hivyo nikaona ukaribu wa zaidi ndiyo unafuatia. Siku hiyo kwa mara ya kwanza macho yangu yalitamani na moyo wangu ukahitaji kuwa kuwa na huyu binti ambaye aliniambia anaitwa Huwaida ingawa sikuwa na ujasiri wa kumwambia kwa muda huo. Maisha mapya ya chuo niliyaanza kwa kukaa katika hosteli za chuo hicho  na huko ndipo nikapata marafiki wapya kutoka sehemu mbalimbali, chumba nilichopangiwa nilipata rafiki anayesoma shahada ya uhandishi wa  tarakilishi (Bachelor in computer engineering)  ambaye alionekana ni mjanja wa mji kuliko mimi mtoto wa kitajiri niliyekulia jijini Tanga. Faiz Faiim ndiyo jina lake huyu rafiki yangu mpya katika hosteli hii, siku ya kwanza tu kukaa katika hosteli hiyo tulitokea kuwa marafiki wakubwa kutokana na kuelewana sana kwa muda mfupi. Faiz alitokea kuwa mtu mchangamfu na mwenye kujali urafiki wangu na mimi pia nilikuwa najali urafiki wake kwangu, tulipendana kama ndugu ingawa mwenzangu alikuwa ana weusi wa kiafrika kabisa. Masomo yalipoanza kila mtu alikuwa anachukua masomo tofauti na mwenzake na muda mzuri wa kuonana ikawa ni baada ya muda wa masomo, kipindi chote hicho sikuwahi kumueleza kuhusu suala la mimi kumpenda Huwaida na wala yeye hakuwahi kunionesha mpenzi wake zaidi ya kuniambia tu kuna shemeji yangu kwake anasoma hapo chuoni kozi tofauti na yeye. Kila nilipomuambia anioneshe alinijibu muda bado na muda wa kufanya hivyo ukifika atanionesha, nakumbuka siku moja ilikuwa ni jumapili tulivu nikiwa nimepumzika chumbani  nikiwa nimechoka sana. Siku hiyo Faiz aliingia chumbani akiwa na furaha sana tofauti na siku zingine, alinikuta nikiwa nimelala kifua wazi kitandani usingizi ukiwa unaninyemelea.
"Oyaaa! Amkaa babu" Faiz alinitikisa huku akiongea kwa sauti ambayo kwangu niliiona kero kutokana na usingizi nilionao.
"aaaaah! Faiz unajua jana nimechelewa kulala na leo nimewahi kuamka hebu wacha nipumzike babu" Nilimwambia Faiz huku nikijigeuza kuangalia ukutani nikimpa mgongo Faiz.
"Mwana acha uzee hebu amka saa nane mchana hii usingizi wa nini?" Faiz aliniambia huku akinigeuza kwa namna iliyonikera sana.
"Faiz acha kunizingua babu mbonji limenikaba hadi kwenye macho" Nilimwambia Faiz kwa sauti yenye kuonesha wazi kukereka na suala hilo.
"Abdul unataka kuniangusha ndugu yako wa hiyari, shemeji yako amesema anataka akuone na akujue  sasa ukilala hapo si unaniwekea usiku ndugu au unataka bishosti anione mimi mduwanzi babu" Faiz aliongea na kusababisha nikurupuke kutoka kitandani huku nikisema, "usiniambie man".
"ndiyo hivyo man, sasa wewe upo tayari mwanao wa ukweli nioneksne mduwanzi mbele ya usingizi wangu" Faiz aliniambia huku akikaa kitandani kwake.
"hapana man, ngoja nikalitoe hili mbonji bafuni kisha tumuibukie" Nilimwambia Faiz huku nikiinuka kuelekea nje nikiwa na uchovu. Nilienda moja kwa moja bafuni nikaoga kisha nikarudi chumbani nikamkuta Faiz akiwa kashavaa nguo ambazo nilimnunulia kama rafiki yangu, nilivaa na mimi nikawa naonekana nimependeza kama alivyopendeza yeye.
"hapo vipi unanionaje?" Nilimuuliza Faiz huku nikikaa kama mwanamitindo wa kiume.
"hapo upo poa kabisa yaani kama unaenda kunipora tunda vile" Faiz aliongea huku akitia masihara.
"wacha zako wewe au hujioni ulivyotupia zaidi yangu man" Nilimwambia Faiz huku nikicheka kutokana na masihara.
"hamna kama hicho Abdul we upo juu hata usipotupia kivile tena utakuja kupata kisu kikali zaidi ya hicho ninachoenda kukuonesha leo" Faiz aliniambia huku akielekea mlangoni.
"wacha zako wewe hebu tujikatae nikamuone shem wangu wa ukwee" Nilimwambia huku nikimfuata Faiz ambaye tayari alikuwa ameshatoka nje. Tulifunga mlango wa chumba chetu kisha tukachukua teksi nje ya hosteli zetu, Faiz alimwambia dereva mahali pa kwenda naye akatutajia bei ambayo niliikubali bila tatizo na safari ikaanza kwenda kumuona shemeji yangu kwa rafiki yangu. Safari yetu ilifika maeneo ya  Kunduchi kwenye ufukwe mwanana wa bahari ya hindi pamoja  eneo la kupumzika watu, Faiz alimuamrisha dereva asimame naye akatii kisha tukampa pesa zake. Faiz alipiga simu kisha akaongea na mpenzi wake akimuuliza yupo wapi, alipokata simu aliniambia "twende".

*mambo yanazidi kunoga



No comments:

Post a Comment