Wednesday, November 25, 2015

KOSA SEHEMU YA NANE

(SASA INAPATIKANA KATIKA ORODHA YA VITABU VYA AMAZON/ NOW AVAILABLE INA THE AMAZON'S BOOK LIST)




 KOSA


MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



 ILIPOISHIA


"hapo upo poa kabisa yaani kama unaenda kunipora tunda vile" Faiz aliongea huku akitia masihara.
"wacha zako wewe au hujioni ulivyotupia zaidi yangu man" Nilimwambia Faiz huku nikicheka kutokana na masihara.
"hamna kama hicho Abdul we upo juu hata usipotupia kivile tena utakuja kupata kisu kikali zaidi ya hicho ninachoenda kukuonesha leo" Faiz aliniambia huku akielekea mlangoni.
"wacha zako wewe hebu tujikatae nikamuone shem wangu wa ukwee" Nilimwambia huku nikimfuata Faiz ambaye tayari alikuwa ameshatoka nje. Tulifunga mlango wa chumba chetu kisha tukachukua teksi nje ya hosteli zetu, Faiz alimwambia dereva mahali pa kwenda naye akatutajia bei ambayo niliikubali bila tatizo na safari ikaanza kwenda kumuona shemeji yangu kwa rafiki yangu. Safari yetu ilifika maeneo ya  Kunduchi kwenye ufukwe mwanana wa bahari ya hindi pamoja  eneo la kupumzika watu, Faiz alimuamrisha dereva asimame naye akatii kisha tukampa pesa zake. Faiz alipiga simu kisha akaongea na mpenzi wake akimuuliza yupo wapi, alipokata simu aliniambia "twende".





ENDELEA NA MKASA WENYE KUELIMISHA NA KUFUNDISHA



SEHEMU YA NANE!

Faiz aliniongoza hadi ndani kabisa ya sehemu hiyo ya kupumzika watu pamoja na kujipatia vinywaji, tuliingia kwenye ufukwe wenye ghorofa lililojengwa kwa ubunifu pamoja kuezekwa na paa lenye umbo la kuvutia. Muda wote huo nilikuwa nimebanwa na shauku ya kutaka kumuona shemeji yangu ambaye anapendwa sana na rafiki yangu, Faiz naye alikuwa akimwagia sifa kedekede mpenzi wake kila kukicha ili nipate shauku ya kutaka kumuona. Tulifika sehemu ambayo kulikuwa na wasichana wawili warefu na wenye asili moja wakiwa wamekaa meza moja yenye viti vinne na kusababisha viwili viwe wazi, wasichana hawa wote wawili walikuwa na asili ya kisomali na walionekana ni ndugu kutokana na kuwa na kila dalili ya kufanana ingawa mmoja alivaa kofia na miwani ya jua iliyoufunika uso wake kwa kiasi kikubwa. Walikuwa ni warembo hata kwa kuwatazama wakiwa na mavazi ya kawaida huku nywele zao wakiwa wameziacha zikiwa zinaning'inia vichwani mwao, eneo walilokaa lilikuwa ni sehemu iliyojitenga hivyo Faiz alipokuwa anawasogelea nilijua dhahiri kwamba mmojawapo ndiye atakuwa shemeji yangu.Tulipokaribia msichana mmojawapo aliyevaa miwani alisimama akaenda kumkumbatia Faiz kisha akampa busu la mdomo, alisalimiana na mimi kwa kupeana mkono kisha tukakaribishwa kwenye meza tujumuike nao. Muda huo wote sikuweza kuiona sura ya shemeji yangu ingawa hapo nilitambulishwa kisha nikatambulishwa na msichsna wa pembeni kama binamu yake.
"Abdul umemuona shemeji yako, ndiye huyu" Faiz aliniambia huku akiwa amemshika mgongo shemeji yangu ambaye hakunitajia jina hadi muda huo, huyu msichana niliyetambulishwa kama shemeji naye aliikia mguso wa Faiz na akawa amejilaza kwenye kifua cha Faiz.
"Faiz nimemuona ingawa hujanitambulisha jina hadi muda huu umenitambulisha binamu yake ambaye ni Nurulayt tu" Nilimuambia Abdul kutokana na kitendo chake cha kutonitambulisha jina la mpenzi wake.
"come on Abdul yaani huyu humjui unasoma nae kozi moja chuo, au hii kofia na miwani  aliyovaa ndiyo zinakufanya usimjua nini" Faiz aliongea huku akimvua kofia mpenzi wake na kupelekea niione vizuri sura ya shemeji yangu ambaye tangu mwanzo nilitamani kumuita mpenzi . Wakati naiona sura ya shemeji yangu ambaye ni Huwaida  msichana ninayemhusudu kuliko kitu chochote, nilijikuta nikishindwa hata nikishindwa kumeza mate nikaanza kuhisi kuna kitu kimenikaba kooni, maumivu niliyoyapata moyoni hayaelezeki hata kitabuni zaidi ya kuishia kuyaeleza kidogo. Huwaida huyu aliyeufanya moyo wangu uwe mbioni kila nikimuona, Huwaida huyu aliyefanya nitamani kila siku kumuona, Huwaida huyu niliyekuwa sina amani nisipomuona, Huwaida huyu ninayemuwaza sana ndiyo leo hii namuita shemeji kwa mtu ambaye ni rafiki yangu ambaye anaonekana mtu kwasababu yangu sasa anamiliki msichana ambaye ni kipenzi cha moyo wangu. Maumivu niliyoyapata kwa sekunde tu nilipouona uso wake wa madaha uliopambwa na tabasamu pana likiwa linaachiwa kwa ajili ya rafiki yangu, Huwaida alionekana kutabasamu kwa tabasamu lililoniumiza mtima wangu nilipoiona sura yake baada ya kuvuliwa kofia. Faiz naye alitabasamu kutokana na mshangao niliuonesha kutokana na kumuona Huwaida, Faiz alijua kuwa mshangao ni kutokana na jambo nisilolitarajia kuwa na shemeji  niliyekuwa namfahamu tangu mwanzo.
"Abdul naona umepigwa na bumbuwazi la mwaka" Faiz aliongea huku akicheka na kupelekea na mimi nicheke bila hata kuelewa nilichokuwa nakicheka ni nini na hata nilipomaliza kucheka nilibaki najishangaa mwenyewe kwa kucheka karika jambo ambalo halikuwa likinifurahisha hata kidogo.
"yaani shem kukaa hapa muda wote ulikuwa hujanitambua tu" Huwaida aliongea kwa kuniita jina ambalo lilikuwa ni mwiba mkali wa sumu unaouchoma moyo wangu na kuniachia maumivu makali yasiyovumilika kwa urahisi.
"Huwaida hilo kofia lako umefunika nusu ya uso mzima we  unafikiri atakujua vipi na hiyo miwani uliyoivaa si atakujua jamaa tu" Nurulayt naye aliongea  akithibitisha ugumu wa kumtambua Huwaida akiwa amevaa kofia na miwani ambavyo alivuliwa na Faiz.
"jamanii! Nimebadilika kwa lipi nikiwa navaa hivi?.... Eti Sweetie nimebadilika nini si niko vilevile tu. Si eti eh!" Huwaida aliongea huku akimchezea kidevu Faiz bila hata kutambua anaumiza moyo wangu kwa kila anachokifanya hapo muda huo kwa rafiki yangu Faiz.
"ndiyo mpenzi umebadilika sana ukiwa na mavazi hayo" Faiz aliafiki suala la kubadilika kwa Huwaida akiwa kavaa kofia pamoja na hiyo miwani.
"Mmmh! Sweetie mbona umeweza kunitambua kama nimebadilika si ungeshindwa" Huwaida aliongea kwa kudeka huku akijiacha huru zaidi katika kifua cha Faiz.
"kumbuka chuma siku zote hufuata sumaku hata sumaku iwe na muonekano wa namna gani, sasa ndiyo na mimi nitakufuata wewe hata ubadilike namna gani kwasababu wewe ni sumaku na mimi ni chuma. So usishangae mimi kukutambua kwa muonekano wa leo na sio ule mashungi" Faiz aliongea huku akimtazama Huwaida usoni na akijua anawafurahisha wanaomuona, hakutambua kama alikuwa anamuumiza rafiki yake kipenzi anayempenda sana mpenzi wake hata kabla hajajua kama ni mpenzi wake.
"mmmh! Makubwa haya tena madogo yana nafuu" Nurulayt aliongea baada ya kusikia maneno ya Faiz akimuambia Huwaida.
"bibiie! Makubwa yapi? Umbea tu muone" Huwaida  aliongea huku akimtazama Nurulayt.
"umbea wapi wewe yaani mtoto umepata anayejua kubembeleza na kuchombeza na shem amepata mtu anayejua kubembelezwa na kuchombezwa, eti Abdul nadanganya?" Nurulyt aliongea kwa madaha na kupelekea Faiz na Huwaida wacheke sana.
"hudanganyi kabisaa!" Nlijilazimisha kukubaliana na maneno ya Nurulayt huku macho yangu yote yakiwa yanamtazama Huwaida hadi  akaona aibu.
"Mpenzi huyu ndugu yako huyu ana maneno huyu....na wewe Abdul unampa support kabisa" Faiz aliongea huku akicheka.
"mwenzangu nahisi lao moja hawa" Huwaida naye alidakia huku akicheka akiwa amelalia kifua cha Faiz, nilipokiona kitendo hicho moyoni nilijihisi kuungua ndani kwa ndani tena kwa moto usio wa kawaida. Nilijikuta natamani hata niondoke hapo lakini nilishindwa kutokana na chakula kuwekwa muda huo huo na wahudumu wa eneo hilo, laiti ningenyanyuka na kuondoka ingeweza kuhisiwa kuna jambo limenikera. Ilinibidi nivilie tu kuka hapo kwenye kiti ambacho nilikiona kama kinanitoboa na miiba katika makalio yangu, chakula kililika hadi kikamalizika kwa ustahimilivu na uvumilivu wa kila ninachokiona. Baada ya kumaliza kula nilitamani ninyanyuke niondoke lakini Faiz na Huwaida wakaniwahi kwa kunyanyuka wakiwa wameshikana.
"Oyaa Abdul si tunaingia ndani mara moja" Faiz aliniaga huku akiwa anaelekea mahali vilipo vyumba vya kulala wageni katika hoteli, mikono yake ilizidi kuniumiza tu kila nilipoiona ikiwa ipo kiunoni mwa Huwaida. Mezani nilibaki mimi na Nurulayt  tukiwa tumekaa kimya bila ya kuongea chochote, Nurulayt alikuwa  makini katika kuperuzi simu yake na mimi ndiyo dimbwi la mawazo juu ya nilichokiona leo likaanza kunizamisha taratibu. Nilijikuta nikianza kumchukia Faiz kwa kuwa na msichana ambaye kwangu ni kila kitu na sikutegemea kama mtu ambaye mwenye maisha ya chini atakuja kunizidi hatua kiasi cha  kuliruka bonde la kuwa peke yake na kufika katika ukingo wa pili katika bustani ya maua yenye ua ambalo nililiwekea malengo tangu mwanzo nilipoliona. Urafiki wa dhati uliokuwa kwa Faiz tangu mara ya kwanza tilipopangiwa chumba kimoja hosteli nilihisi ukianza kuyeyuka taratibu mithili ya barafu linavyoyeyuka kwenye joto, kwa mara ya kwanza moyoni mwangu niliazimia kufanya jambo lolote baya kwa Faiz ingawa alikuwa ananiona kama ndugu kwake. Nilichokuwa nafikiria muda huo ni kumpata Huwaida kwa namna yoyote na sijali lolote, yaani nilijiona natafuta shilingi(Huwaida)  katikati ya majani marefu(Faiz) na sikuwa na namna nyingine ya kuipata shilingi hiyo zaidi ya kuyapinda marefu haya tena ikibidi niyakate kabisa ili kuipata shilingi ambayo kwangu ilikuwa ina thamani zaidi ya lulu marjani ya katikati ya bahari kwenye mpaka wa bahari mbili zenye maji yenye joto tofauti. Mawazo yalizidi uzito hata kiasi cha kuizuia baadhi ya milango yangu ya fahamu isiwe katika kufanya kazi inavyostahiki, kiufupi mwili wangu ulikuwepo hapo jirani na Nurulayt lakini mawazo yangu na kila kiungo changu hakikuwepo katika eneo hilo. Nilikuja kurudi katika hali ya kawaida baada ya kutingishwa na Nurulayt na hapo ndipo nikaisikia sauti yake ikiniita kama ananiamsha usingizini, nilishtuka kidogo kisha nikapangusa uso wangu kwa viganja vyangu kama nilikuwa nafuta maji usoni mwangu.
"Abdul una tatizo gani mbona hivyo?" Nurulayt aliniuliza huku akinitazama kwa udadisi mkuu usoni mwangu.
"sina tatizo nipo sawa kabisa" Nilimjibu kwa kumficha tatizo nililokuwa nalo kutokana uzito wa jambo lenyewe.
"upo sawa kivipi mbona nakuita zaidi ya mara nne huitiki mpaka nikutingishe kama umelala usingizini, unawaza nini?" Nurulayt ambaye ndiyo kwanza ninaonana naye kwa mara ya kwanza alizidi kuniuliza kwa udadisi.
"mawazo ni sehemu ya maisha ya binadamu"Nilimwambia huku nikikaa sawa kwenye kiti.
"ok yameisha sasa, Abdul naomba simu yako tafadhali" Nurulayt aliniomba simu yangu kama mtu mwenye shida sana, nilimpatia simu yangu akaandika namba zake kwenye simu akazipiga halafu akazihifadhi.
"je nimefanya vibaya?" Nurulayt aliniuliza.
"hapana hujafanya vibaya" Nilimjibu kisha tukaendelea kuongea mambo mengine tukiwa tunawasubiri Faiz na Huwaida ambao nina uhakika asilimia zote wameenda kula tunda haramu ambalo hata watu wa kwanza kuletwa duniani walilila ingawa walikatazwa na Muumba. Mnamo saa kumi na mbili jioni Faiz na Huwaida walirejea wakiwa na furaha kama walivyoondoka, tuliondoka kurudi hosteli baada ya kuagana na Huwaida pamoja na Nurulayt.
Kuanzia siku hiyo ndiyo siku ambayo chuki na wivu kwa Faiz vilichukua nafasi na mawasiliano baina yangu na Nurulayt yalizidi kuwa makubwa mpaka ikawa haipiti asubuhi bila ya kuwasiliana, nilimchukia Faiz wa kitu ambacho si kosa kwake na nilitamani kumfanya  kitu chochote kibaya ili aweze kuachana n mwanamke ninayompenda. Mapenzi baina yao yalizidi kuwa makubwa na wivu kwangu ukazidi kuwa mkubwa hadi nikaazimia nifanye jambo ili niweze kumpata Huwaida, mawasiliano yangu na Nurulayt nayo yalizidi kuwa makubwa na katika mawasiliano ya siku zote alikuwa akiniambia kuhusu mpango ambao alitaka kufanya na mimi ili alipe kisasi. Nilipouliza kuhusu mpango huo hakunijibu chochote zaidi ya kuniambia niwe na subira, nakumbuka ilikuwa ni jumapili siku ambayo nilikula njama za kundi la watu wakampige Faiz hadi aachane na Huwaida. Njama hiyo ilifanikiwa kwa kumnasa Faiz akiwa yupo njiani akienda kwao kama alivyoniaga, Faiz alitekwa kama ilivyopangwa na akapigwa sana ili amuache Huwaida. Baada ya siku mbili tangu Faiz aniage alikutwa kwenye mtaro wa barabara ya Sam Nujoma akiwa hajitambui na ana majeraha mwili mzima, taarifa za kuokotwa kwake katika mtaro huo zilinifikia nikiwa nipo hosteli nikiwa nimepumzika baada ya kupigiwa simu na Huwaida ambaye alikuwa analia mfululizo. Taarifa hiyo nilivyoipata nilijifanya nimeshtuka sana na nikivaa haraka ili niwahi kutoka kuelekea hospitali ya Lugao alipopelekwa kutokana na hali ya kuwa si ya kuridhisha, nilipofungua mlango wa chumba chetu ili nitoke nilikutana uso kwa uso na Nurulayt akiwa amekasirika akiwa amesimama katikati ya mlango.
"ndiyo unajifanya una haraka siyo!" Nurulayt alinisemesha kwa ukali.
"Nur kuna ninj si unipishe njia niwahi hospitali nikamuangalie Faiz" Nilimuambia Nurulayt huku nikimtoa mlangoni lakini hakutoka mlangoni na badala yake alinisukuma ndani kisha akafunga mlango.
"eti niwahi hospitali nikamuangalie Faiz, wakati unawalipa  hela Danger boys wamteke na wampige ndiyo baadae ukamuone sio" Nurulayt aliongea huku kabana pua kwa dharau akiwa ameshika kiuno mbele yangu.
"we Nur unaongea nini hivi akili zipo timamu kweli?!" Nilijikuta nikianza kujifanya sijaelewa alichoongea Nurulayt ingawa moyoni nilikuwa najiuliza huyu mwanamke kajuaje wakati ule ni mkataba wa siri na kikundi hicho cha wahalifu. Nurulayt alipoona kuwa najifanya sielewi kinachoendelea alitoa bahasha akanipatia huku akinitazama kwa macho makali, bahasha hiyo niliifungua kwa pupa na nikajikuta nimeshtuka kwa nilichokiona ndani yake.
"sema sasa huelewi kipi?"Nurulayt aliuliza huku akinitazama kwa dharau.
Nilibaki nikiwa nimechoka bila hata kufanya kazi nzito yoyote, nilizidi kuhema kwa nguvu bila hata kukimbia umbali wowote. Niliishia kumtazama Nurulayt bila kumuambia neno lolote, kwakweli sikutegemea kama suala kama hili ambalo litagunduliwa na mtu yoyote mpaka kufikia hatua ya kupigwa picha wakati nafanya makubaliano na muwakilshi wa kundi la wahalifu llilompiga Faiz. Nurulayt alipoona nababaika namna hiyo alianza kucheka kisha akazichukua picha zake kisha akaziweka Nurulayt eka kwenye bahasha. Alinitazama kwa uso uliopambwa na tabasamu kisha akaniambia, "kumbe na wewe muoga hivi".
Niliposikia maneno hayo nilibaki namtazama nikiwa sijamuelewa kitu gani anachomaanisha, alinishika mkononi hadi kitandani kwangu halafu akaketi na mimi nikaketi.
"Abdul both we have the same enemy(Abdul wote tuna adui mmoja) Nurulayt aliniambia huku uso wake ukiwa umeondokwa na tabasamu usoni na umakini ukawa umechukua nafasi yake.
"what(nini)?" Niliuliza kwa mshangao sana baada ya kusikia kauli hiyo ya Nurulayt.
"Faiz ni adui yako kwakuwa amemchukua msichana unayempenda na mimi Faiz ni adui yangu kwasababu kamuua kaka yangu huko Afrika ya kusini na akamuibia kiasi kikubwa cha madini" Nurulayt aliongea huku machozi yakimtoka machoni mwake kwa hasira sana halafu akaniegemea begani huku akisema, "Abdul ukae utambue huyo rafiki yako uliyekuwa unamhusudu mwanzo ni jambazi hatari na ana kundi kubwa la magaidi nchini Afrika ya kusini na kwingineko barani Afrika na pia ametajirika kupitia tani mojaya madini ya almasi aliyomuibia kaka yangu baada ya kumuua". Nurulayt alinieleza mambo ambayo hata sijuyaelewa na wala sikuyategemea kama Faiz huyu mtoto wa kimasikini ninayemjua kama atayafanya.
"Huwaida hatambui lolote juu ya hili na ninayetambua ni mimi niliyeenda kumtembelea kaka yangu Sabir aliyeondoka nyumbani Somalia kwenda kutafuta maisha Afrika ya kusini akiwa na mtaji mkubwa sana aliopewa na baba, kaka yangu alipokuwa anauawa nilimshuhudia kila kitu na Faiz ndiye aliyemuua ndani ya nyumba ya kaka yangu na muda huo anafanya hayo mimi nilikuwa nimejificha sehemu katika nyumba ya kaka yangu ili asinione akaniua" Nurulayt alizidi kuniambia maelezo ambayo yaliniacha kinywa wazi, Faiz huyu ninayemjua mimi kusikia ni muuaji na jambazi mkubwa.
"Nuru kwahiyo wewe ulikuwa unaishi Afrika ya kusini?" Nlimuuliza Nurulayt ili nipate maelezo yake kiupana zaidi.
"hapana sikuwa naishi Afrika ya kusini ila nilikuwa naenda kumtembelea kaka tu mara chache na hata hiyo siku aliyouawa nilikuwa nilikuwa nimekuja kumsalimia na ndiyo siku hiyo Faiz  akapiga hodi nikaambiwa nijifiche" Nurulayt alizidi kunieleza huku akiwa na hasira sana.


*Mazito zaidi ya mzani yamezuka.
*nini hatma ya Faiz




No comments:

Post a Comment