Friday, November 27, 2015

KOSA SEHEMU YA KUMI

RIWAYA: KOSA


MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



 ILIPOISHIA


Huwaida baada ya kufunguliwa alinifuata kwa kasi huku akiniita mwanaharamu, aliponikaribia alinipiga kibao kikali  halafu akaokota chuma kizito akiwa anahema. Alikinyanyua kila chuma akawa ananielekezea usoni ili anipigae nacho, alikinyanyua kisha akakishusha kwa nguvu. Nilibaki nikifumba macho huku nikisubiri hukumu yangu kwa Huwaida kwa kitendo nilichomfanyia, nilijiona sina thamani tena ya kuendelea kuishi ikiwa yeye anaonesha dhahiri ananichukia na hataki hata kuiona sura yangu kuanzi
a muda huo. Nikiwa nasubiri hukumu yangu nilihisi  kama kitu kikitoboa mfuko wa gunia kisha kimiminika kizito kikinirukia usoni, nilipofumbua macho nilijikuta nikiwa sina hata nguvu ya kusimama.




ENDELEA NA MKASA HUU WENYE KUELIMISHA NA KUFUNDISHA


SEHEMU YA KUMI!!
Nilihisi kuangukiwa na mwili wa mwanamke baada ya kusikia mlio wa gunia likitobolewa , mawazo yangu yaliniambia nimeegemewa au nataka kukumbatiwa na Huwaida baada ya Huwaida kujaribu kuniua. Nilimpokea Huwaida nikamuweka kifuani mwangu kisha nikafungua macho  kumtazama Nurulayt ambaye alikuwa nyuma ya Huwaida kwa muda huo, nilipomuona Nurulayt ameshika kile kisu kirefu ambacho mwanzo kilikuwa kisafi lakini sasa hivi kina damu nilishtuka sana na nikamtoa Huwaida kifuani kwangu halafu nikamtazama, nilipoona jeraha kubwa likiwa katika mwili wa Huwaida nilijihisi  nipo ndotoni hivyo nikafikicha macho ili nione jambo lile sio la kweli lakini nilipoweka mikono usoni nikawa nahisi nimegusa kimiminika kibichi ambacho sikua nakitambua kutokana na kutojiona usoni mwangu. Nilipoitoa mikono usoni mwangu niliiangalia na hapo ndipo nikabaini kimiminika kilichonirukia usoni ilikuwa ni damu ya Huwaida, nilipomtazama Huwaida  bado alikuwa mzima na anapumua kwa tabu, macho yake yalikuwa yakinitazama kwa masikitiko hadi machozi yakaanza kunitoka kwa kushindwa kuvumilia kumuona  mwanamke ninayempenda akiwa akiwa katika hali hiyo. Kilio cha kimya kimya ndicho kilifuata huku machozi yakizidi kunitoka nikimuangalia Huwaida anayeonekana kuvuta hewa kwa shida kutokana na jeraha alilonalo kuwa kubwa sana, Huwaida alinyanyua mkono wake wa kulia akashika ukosi wa nguo yangu ya juu niliyovaa kisha akauvuta taratibu huku akinitazama kwa macho yanayolengwa na machozi kutokana na maumivu anayoyasikia muda huo.
"Abdul aaaargh! Abdul nini umefanya? Kama kunipenda mwanamke wa mwenzako hukutakiwa kwani sikuumbwa mzuri peke yangu ndani ya dunia hii ungepata mwanamke  mwingine atakayekuwa mzuri zaidi yangu" Huwaida aliongea huku akinitazama usoni kwa sura yenye masikitiko makubwa ambayo ilinizidisha kulia kama mtoto mdogo vile.
"nisamehe Huwaida sikuwa na namna nyingine ya kufanya na sikuwa naona mwanamke zaidi yako ndani ya dunia hii, urembo wako uliniweka upofu na kukuona wewe ni zaidi wengine wote, hivyo sikuwa na jinsi zaidi ya kuamua kumteka rafiki yangu" Nilimuambia Huwaida huku machozi yakinitiririka machoni kama chemchem ya maji, kila nilipozidi kumtazama Huwaida ndivyo nilivyozidi kulia hasa alipoanza kutoa kikohozi hafifu huku akionesha kuwa anaumia sana.
"umesababisha mpenzi wangu kauawa na umesababisha na mimi nichomwe kisu na binamu yangu, sina chuki na wewe  nimekusamehe kwa moyo mkunjufu lakini napenda utambue kuwa mapenzi ni sawa na mkondo wa maji hayazuiliki kwa namna yoyote kama ulivyotaka kuyazuia mapenzi yangu na Faiz. Hata kama ulimuua kimya kimya ukitarajia itakuwa ni siri jua siri ni ya mtu mmoja ikiwa ya wawili basi hiyo ni ya jamii nzima ndiyo maana mlipomfanyia Faiz hivyo nimegundua na nisingeweza kuwa nawe hata kama umefanya hivyo kwa mapenzi makubwa juu yangu." Huwaida aliongea huku akinitazama usoni machozi yakiwa yanamtoka, alisitisha kuongea kwa muda kisha akahema kwa nguvu halafu akaendelea "najua sitopona na nitamfuata Faiz wangu alipo nikiwa sina kinyongo na wewe mwanaume uliyenipenda, kiufupi nimekusameh..". Huwaida alishindwa kumalizia kauli hiyo baada ya ladha inayoonjwa na kila mtu kuwa imemfikua yeye mwenyewe, ni umauti ndiyo uliomgubika na roho yake ikawa imeachana na mwili kwa muda huo. Nilipoona katulia sikutaka kuamini ka tayari Huwaida ni marehemu  na nilimtikisa huku nikiita jina lake kwa sauti kubwa iliyojaa huzuni lakini jambo hilo halikuweza kubadilika iwe Huwaida yupo hai. Kilio kilinizidi nikawa nalia huku nimeukumbatia mwili wa Huwaida, Nurulayt alipoona imekuwa hivyo alikuja kuninyanyua huku naye akiwa na machozi machoni mwake ambaye kwangu sikuyaona kama ni ya uchungu kwani yeye ndiye aliyemuua Huwaida.
"Nuru kwanini? Kwanini umefanya hivi wakati unajua kama nampenda kuliko hata nafsi yangu na ndiyo maana nilimuacha aniadhibu hata kuniua kama hanipendi ili nisiishi katika dunia hii nikiwa na maumivu" Nilimwambia Nurulayt kwa hasira baada ya kuuachia mwili wa Huwaida pale chini.
"Abdul sikuwa na jinsi zaidi ya kufanya hivi ingawa hata mimi inaniumiza kumuua binamu yangu, yote haya nilikuwa nahofia kuja kulea mtoto asiye na baba. Mimi ni mjamzito Abdul hivyo sikupenda kuja kulea mimba peke yangu au mtoto asimuone baba yake" Nurulayt aliongea huku akilia lakini sikutaka kumuelewa na niliishia kumfukuza humo ndani nikitishia kumuua ikiwa nitaiona sura yake tena, kuhusu mimba ambayo ilikuwa ni yangu sikuijali hata mara moja.



Tangu siku hiyo sikuwahi kumuona Nurulayt tena na wala sikuwahi kumpenda mwanamke yoyote hadi hii nilipokuja kumuona Sarina mwanamke  mrembo aliyemzidi Huwaida kwa kila kitu tena amekuwa msaada kwangu kwa kila kitu hadi kunipa hifadhi katika nyumba yake. Nilipomfananisha na Huwaida ndipo nilipokiri kuwa kuna wazuri zaidi yake katika dunia hii, sikuhitajika nimfanyie vile rafiki yangu kwa ajili ya mwanamke.
' sikuumbwa mzuri peke yangu ndani ya dunia hii ungepata mwanamke  mwingine atakayekuwa mzuri zaidi yangu' Maneno ya Huwaida aliyoniambia miaka kadhaa iliyopita kabla hajakata roho yalinijia kichwani mwangu na kunifanya nitokwe na machozi nikiwa nimekaa sebuleni nyumbani kwa Sarina bila hata kujijua kama Sarina ananitazama.
"Abdul  moenie bekommerd wees nie alles wat sal eindig (Abdul usijali yote yatakwisha)  Sauti ya Sarina ndiyo ilinifanya nikumbuke kama Sarina yupo karibu yangu baada ya kunipa faraja akijua yanayonifanya nidondoshe machozi muda huo ni matatizo yaliyonikumba tangu nafika ndani ya nchi hiyo. Sarina alikuja kukaa karibu yangu huku akinibembeleza kutokana na uso wangu kuwa na huzuni kubwa sana, kuukumbuka mkasa wangu na Huwaida ndiyo jambo lililonifanya nidondoshe chozi muda huo hasa nilipoyakumbuka maneno yake ya  mwisho. Kumbukumbu juu ya Nurulayt nayo ikanirudia kichwani mwangu na kuhusu ule ujauzito alioniambia nikawa nina shauku ya kujua kama alijifungua salama, sikujua ni wapi nitapata majibu ya maswali yangu kwani Nurulayt sikujua alipo hadi muda huo tangu kilipotokea kifo cha Huwaida miaka kadhaa iliyopita nikiwa chuo mwaka wa kwanza.
" Abdul verduur as 'n man wat ek is bereid om te
help as ek kan(vumilia kama mwanaume Abdul nipo tayari kukusaidia kama nitaweza) Sarina aliniambia wakati ananibembeleza kuhusu suala hili.
"dankie Sarina (asante Sarina)" Nilimshukuru kwa kuonesha nia ya kunisaidia katika kipindi hichi  cha matatizo bila hata kunifahamu kiundani, siku hiyo niliamua kupitisha nikiwa nipo nyumbani kwa Sarina hadi usiku nikiwa naangalia televiaheni tu bila ya kuwa na chochote cha kufanya. Usiku wa manane ulipofika ilinibidi nilale sebuleni kutokana na nyumba hiyo kuwa na chumba kimoja cha kulala, sebule, choo na bafu pamoja na jiko, Sarina alilala chumbani kwake kama kawaida na sikuwa tayari kulala naye chumba kimoja. Asubuhi ya siku  iliyofuata niliwahi kuamka  nikajisafisha mwili wangu kisha nikawasha televisheni ili niangalie kama kawaida kwani sikuwa na jambo lolote la kufanya, baada ya nusu saa Sarina naye aliamka akanikuta nikiwa naangalia televisheni.
" Oggend nuus(habari ya asubuhi) Sarina alinisalimia kwa uchangamfu mkubwa akiwa kavaa vazi la kulalia lenye muundo wa suruali na shati laini, nywele zake alikuwa amezibana vizuri na kunipa wasaa mwingine wa kuijua sura yake akiwa ameweka nywele kwa mtindo huo.
" veilige Ek weet nie wat jy (salama sijui wewe)" Niliikia salamu yake na nikamjulia hali yake.
"veilige(salama)" Alinijibu kisha akaingia jikoni kuandaa kifungua kinywa akiniacha nikiangalia televisheni yake iliyounganishwa na king'amuzi cha DSTV, niliangalia chaneli mbalimbali za kimataifa na mwishowe  nikaikuta chaneli ya nyumbani Tanzania ikionesha kipindi cha mambo ya biashara na sasa mtangazaji wa chaneli hii iitwayo  Star tv alikuwa akimhoji mkurugenzi wa kampuni zangu juu ya maendeleo ya kampuni zangu. Mahojiano hayp yalikuwa yakifanyika katika ofisi yangu iliyopo katika makao makuu ya kampuni zangu, tena meneja huyu anayeitwa anayeitwa Khalid Zaid ambaye ni mwenyeji wa Pemba alikuwa akielezea kuhusu ufanisi wa kazi wa kampuni zangu. Nilipoyaona mahojiano hayo nilikuta nikimuita Sarina jikoni ambaye alikuja kwa kasi kuja kuyashuhudia, katika ofisi yangu bado picha kubwa ya kwangu ilikuwa ipo pale pale ikinionesha nikiwa nimevaa suti ya gharama na tabasamu mwanana likiwa limepamba uso wangu. Khalid alipoulizwa juu ya suala la kutoonekana mwenyekiti mtendaji wa makampuni hayo ambaye ni mimi alijibu kuwa nilikuwa nipo nie ya nchi  kimasomo na hata taarifa hiyo ilikuwa inajulikana na wafanyakazi wote wa kampuni zangu na yeye nimemkabidhi ofisi mpaka nitakaporudi. Nilipoyasikia maneno ya Khalid nilibaki ninashangaa sana kwani sikuwahi kumpa taarifa hiyo hata siku moja lakini yeye ametoa taarifa isiyo ya kweli katika chombo cha habari, Sarina yeye alikuwa anaangalia tu kwani hakuwa akielewa chochote kulichokuwa kinaongelewa katika televisheni kutokana na kutojua lugha ya kiswahili. Kipindi hicho alikiangalia nusu kisha akaenda kuendelea kutayarisha kifungua kinywa, alipomaliza ndipo alipokuja kuniuliza yote kuhusiana na kipindi kile kilichokwa kikirushwa. Nilianza kumfafanulia kitu  kimoja baada ya kingine na niliposhindwa msamiati wowote wa kiafrikaans niliamua kutia kingereza hadi akanielewa nilichokuwa namweleza.
" baie jammer Abdul(pole sana Abdul)" Sarina aliniambia kusikiliza maelezo yangu kwa umakini.
"dankie(asante)" Nilitikia huku nikiwa nimeshika tama nikionesha kuhuzunika kwa kila kinachoonekana.
" daar is iets ernstig gaan oor dat jy nie weet( kuna jambo zito hapo linaendelea wewe hulijui)" Sarina alikisia baada ya kujifikiria kwa muda mrefu, maelezo yake kiupande mwingine yalionekana kuniingia sana nikakubaliana ingawa upande mwingine bado nilikuwa njia panda sana. Nikiwa bado najifikiria kengele ya mlango mkubwa wa kuingia ililia kuadhiria kuna mgeni yupo mlangoni, chini ya mlango bahasha ya kaki ilionekana ikipitishwa na mtu aliyepo nie. Hata Sarina alipoenda kufungua mlango alikuta tayari huyo mtu aliyeweka bahasha alikuwa ameshaondoka, Sarina aliichukua bahasha hiyo kisha akanikabidhi bila kusema lolote baada ya kuiona picha yangu ikiwa ipo juu ya bahasha. Niliipokea bahasha hiyo kisha nikaifungua kwa pupa nikitaka kujua ni nini kilichomo ndani yake, niliikuta karatasi iliyoandikwa ujumbe mzito ambao ulitakiwa kufika kwangu. Ujumbe huo uliandikwa hivi:-
'Abdul hongera sana kwa kuwapiga vijana wangu kwa uwezo wa kupigana, sasa basi nataka umalize kazi ya mwisho ya kuokoa mali zako ili uweze kujua chanzo cha  kupewa kazi hizi, najua unazo dola milioni moja taslimu katika mkoba wako huo sasa unahitajika uzipeleke katika sanduku  la posta la Walvis kwa namna yoyote pia nadhani utakuwa umejua kidogo hizo pesa unazoringia zinavyotafutwa na si kupewa kama unavyopewa wewe baada ya mzazi wako kufariki.
Kazi inayofuata unatakiwa ukaibe kilo 500  ya almasi iliyopo mikononi mwa Gorilla boys wanaoishi msitu wa Chirinda Zimbabwe, vijana hao wana ngome nzito sana sasa basi wewe na mwenzako mwingine mtahusika operesheni hii.

Kila heri
   F.A.Z'.
Karatasi hiyo iliishia hapo kimaelezo ikawa imeacha imeniacha njia panda zaidi kwani hiyo mwenzangu sikumjua na hata hao watu wenye almasi hiyo sikujua wanaishi wapi. Nilipomtafsiria Sarina hiyo barua iliyoandikwa kiswahili alibaki akinihurumia hadi machozi yakawa yanamlenga.
" Abdul asseblief nie gaan na die gorilla seuns is
gevaarlike mense(Abdul tafadhali usiende hao Gorilla boys ni watu hatari)" Sarina aliniambia kwa huruma baada ya kumfasiria ile barua niliyotumiwa.
" Sarina ek nodig het om te gaan, my eiendom te
verlos (Sarina nahitajika niende ili kukomboa mali zangu)" Nilimwambia Sarina huku nikimfuta machozi yaliyoanza kumtoka mashavuni mwake, Sarina alianza kutokwa na machozi papo hapo nilipomueleza hivyo.
" Abdul weet die opbrengs is baie moeilik(Abdul najua kurudi huko ni vigumu sana) Sarina aliniambia kutokan na kuhofia maisha yangu katika kazi inayonikabili.
"Sarina daar is niks om te vrees nie, die basis bid
net vir my om veilig terug( Sarina hakuna cha  kuhofia cha msingi niombee tu nirudi salama)" Nilimuambia Sarina muda huu alikuwa analia sana.
" Elkeen het gevoelens oor 'n ander persoon van
die teenoorgestelde geslag seks, ek pokuona vir
die eerste keer sal sekerlik 'n hartaanval.
Nilipoongea met jou vir die eerste keer beslis
myself Ek wou met jou elke uur, Abdul lief jy hoef
nie te mislei( Kila mtu ana hisia juu ya mtu mwenzake wa
jinsia  tofauti, nilipokuona kwa mara ya
kwanza hakika moyo ulipata mshtuko.
Nilipoongea na wewe kwa mara ya kwanza hakika
nafsi yangu ilitamani kuwa na wewe kila saa,
Abdul nakupenda sihitaji kukupoteza)" Sarina aliongea huku akiwa amenipa mgongo kutokana na uzito wa maneno yenyewe, kwa mara ya kwanza maishani maishani  nilijikuta nikitamkiwa na msichana ninayemhusudu maneno kama hayo ambayo yalinikumbusha maneno ambayo yalinitoa machozi.
"hamna kama hicho Abdul we upo juu hata usipotupia kivile tena utakuja kupata kisu kikali zaidi ya hicho ninachoenda kukuonesha leo" Maneno ya Faiza wakati anaenda kunionesha Huwaida ndiyo yalinijia kichwani mwangu na ukweli wa kauli yake ndiyo nikawa naiona imetokea baada ya kumfanyia kitu kibaya.
Nilimsogelea Sarina kisha nikamkumbatia kwa nyuma na nikambusu shingoni, Sarina aliendelea kulia tu akinisihi nisiende huko ninapotaka kwenda.
" As ons mekaar liefhet, sal ek terugkeer (kama tunapendana nitarudi) "  Nilimwambia  Sarina huku nikimshika na nikamgeuza nikawa natazamana naye uso kwa uso, Sarina alishindwa kuniangalia usoni na alinikumbatia kwa hisia kali.  Tukiwa tumekumbatiana vilevile mlango wa mkubwa wa kuingilia ndani ukagongwa kwa nguvu pamoja na kengele kubonyezwa kwa wakati mmoja, wote tulishtuka sana kwa ugongwaji wa mlango wa namna hiyo.
" verberg(jifiche)" Sarina alinimbia haraka nami nilitoka sebuleni hadi jikoni na nikabana  pembeni ya mlango wa jikoni kwa ndani, nikiwa nimebana hapo nilimsikia Sarina akimlaumu mtu aliyegonga kwa ukosefu wa ustarabu ambao aliomuonesha katika ugongaji wake wa mlango. Yule mtu naye aliomba radhi kisha akamuambia Sarina ametumwa alete mzigo hapo akijitambulisha kama mfsnyakazi wa kampuni ya usafirishaji, yule mtu alipoaga na kuondoka nilitoka hadi sebuleni nikamkuta Sarina akimalizia kufunga mlango akiwa amesimama jirani na boksi kubwa.
"Griiiiiiiiiiiiiiiiii!  Griiiiiiiiiiiiiiii!" Nilipotaka kumsemesha Sarina simu yangu iliita na ikanilazimu niipokee  baada ya kuona mtu anayenipigia ni yuleyule wa siku zote.
"nadhani umeuona mzigo niliouleta hapo sasa hivi ambao umepokelewa na Sarina, sasa basi ufungue na utakachokikuta humo ndani usikidharau ukitunze maana ukikidharau utakuja kujuta mwenyewe" Sauti ya yule mtu iliniambia, nilikuwa nikimsikiliza kwa umakini huku nikiuendea ule mzigo hadi nikaufikia bila hata kumuangalia Sarina aliyekuwa ananitazama kwa umakini.
"fungua mzigo sasa usiutazame tu" niliambiwa na mimi nikatii nikaufungua mzigo huo ambao uliniacha nikiwa nimepigwa na bumbuwazi kwa kile nilichokiona, hata Sarina naye alipigwa na bumbuwazi kwa alichokiona ndani ya boksi hilo.
"vizuri kwa kuufungua mzigo huo, sasa kama unataka ujute maishani mwako kidharau hicho ulichokikuta humo ndani na kama hupendi kujuta basi ukitunze nilichokukabidhi kwani si mali yangu ila kipo chini ya uangalizi wangu" Sauti ya kwenye simu ilinisisitiza kisha simu ikakatwa.

*kitu gani hicho tena?


No comments:

Post a Comment