Sunday, November 29, 2015

KOSA SEHEMU YA KUMI NA MBILI

RIWAYA: KOSA


MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



 ILIPOISHIA

Tuliendelea na zoezi letu kwa mara ya pili huku nikivua shati langu na Sarina akivua nguo yake ya juu, tulijikuta tukibaki na nguo za ndani pekee na joto lilikuwa kali sana. Kupunguza joto ilinidi niende nikawashe feni la hapo ukumbini, upande ulipo feni ilibidi nimpe mgongo wakati naenda kuliwasha kwani swichi y
a kuliwasha feni  ilikuwa upande huo, nilipopiga hatua mbili kwenda kwenye swichi Sarina aliona kitu kilichomfanya anifuate akiniambia nisimame kwanza. Aliponifikia alinishika katika ya mgongo huku akiniuliza, " Avez-vous déjà tricoter?(umewahi kushonwa?)", nilikataa akaniuliza juu ya alama ndogo ya mshono iliyopo mgongoni mwangu ambayo nilikuwa siijui.



ENDELEA NA MKASA WENYE KUSISIMUA NA KUELIMISHA


SEHEMU YA KUMI NA MBILI!!

Ukweli ni kwamba sikuwahi kushonwa mgongoni hata siku moja kwani sikuwahi kuumia hadi nikashonwa na wala sikuwahi kufanyiwa upasuaji wowote hadi nishonwe mgongoni, Sarina alikuwa akinishika sehemu ambayo alisema kuna mshono na hapo nikahisi kuna alama ipo mgongoni mwangu. Sikuijua hiyo alama niliwahi kupatwa na nini hadi nikawa hivyo, Sarina aliendelea kuishika ile alama kwa namna ya kupapasa huku akinibusu shingoni kwangu hadi nikaanza kujihisi nina hali tofauti kabisa katika mwili wangu kutokana na msisimko uliokuwa ninaupata. Nilipowasha feni la hapo sebuleni ilikuwa ni mwanzo wa jambo lililowaka katika miili yetu lililohitajiwa kuzimwa na kwa kupata kile ambacho hatukuwa nacho katika miili yetu, ilikuwa ni mambo ambayo hayawezi kuelezeka kwa maandishi kwa kila hatua kwa mtu mwenye maadili timamu ya rika zote za umri ni safari ya ajabu isiyotakiwa kusimuliwa kwa mwingine ili kuepuka vichochezi na ushawishi kwa wengine kutaka kusafiri kama hii. Niliweza kusafiri kwa saa na dakika kadhaa katika safari hii isiyokuwa na karaha kwa wahitaji wake hadi nilipofikia kituo kikuu cha mwisho cha safari hii, Sarina alikuwa naye yupo pamoja nami katika kwa kila hatua na hata nilipotua mzigo mwisho wa safari hii naye alitua mzigo vilevile. Tulipomaliza wote tulienda bafuni tukajisafisha kisha Sarina aliingia jikoni kuandaa chakula cha jioni na mimi nikakaa sebuleni nikawa naangalia runinga kama kawaida yangu, niliwasha nikaangalia chaneli za Tanzania kujua kinachojiri nikawa nimeshasahau kabisa suala la Sarina kuuona mshono mgongoni kwangu. Nikiwa naangalia televisheni simu yangu iliita kwa mara nyingine huku jina la mpigaji likionekana ni lile la mtu anayenipa kazi nisizozipenda kila kukicha, niliipokea simu kisha nikaiweka sikioni nikatulia kimya bila kuongea chochote.
"sasa muda wa kazi umewadia inabidi ujiandae mwenzako anakusubiri katika kibanda cha simu kilichopo jirani na hoteli ya Hilton, inabidi umchukue uende nae atakapokuelekeza. Pia hongera kwa kumtafuna Sarina" Aliniambia kisha akakata simu, nilibaki nikiwa nina hasira hasa kutokana na mambo anayonifanyia huyu mtu akionesha kuniona kila ninachofanya. Kwa mara nyingine nilianza kuyafikiria mambo ambayo ninafanyiwa na huyu ambaye anaonekana ananiona kwa  kila hatua yangu, nilifikiria matukio yote hadi pale Sarina aliponiambia kuhusu alama ya mshono iliyopo mgongoni kwangu. Nilijaribu kukumbuka filamu mbalimbali za kipelelezi nilizowahi kuziangalia na nyingine za mapigano ambapo zilinikumbusha juu ya uwepo wa kifaa kidogo mithili ya  punje ya ngano ambacho mtu akiwekewa mwilini mwake hujulikana alipo na kipi akifanyacho. Awali nilipokuwa nikiziangalia filamu hizo tangu nikiwa mdogo nilikuwa nahisi ni uongo wa wazungu  lakini hapo nikaanza kuziamini moja kwa moja na nikabaki nikiwa nina shauku ya kukitoa hicho kitu nahisi ndicho kilichopo mwilini mwangu.
  Sarina alipomaliza kupika nilimueleza juu ya  kila kitu nilichoambiwa na mtu aliyenipigia simu na nikachukua wasaa huo kumueleza kuwa inabidi nimuage ili niweze kwenda kuifanya kazi hiyo. Ilikuwa ni jambo gumu kulikubali kwa Sarina kwani alihofia usalama wangu katika sehemu ninayoelekea, nilimbembeleza akatulia na kukubaliana na uamuzi wangu na nilimpa ahadi kwamba ningerejea tu nitakapomaliza kazi hiyo kutokana na uwepo wa Ilham kwake ambaye kutunzwa kwake ni dhamana yangu. Pia uwepo wa mapenzi yangu kwake nj jambo jingine lililonifanya nimpe ahadi  , nilitakiwa niuvae ujasiri ambao niliuvaa wa kutengana na huyu mwanamke niliyempenda kuliko kitu chochote kwa wakati huo. Ilham alipoamka naye nilimuaga ingawa sikumuambia naenda kufanya nini kwa muda huo, baada ya kumaliza kula chakula cha usiku niliondoka rasmi nikiwa nina vitu vyangu vya muhimu. Nilitumia gari yangu ambayo nilipewa na Jasmin baada ya kumburudisha kwa usiku mzima, gari ambayo ni gari yenye kasi zaidi duniani pia ni gari ghali sana niliamua kuitumia usiku huo na hata kwa safari zangu zinazofuatia. Nilipotoka nyumbani kwa Sarina nilikuwa nina kitita cha pesa ambacho nilipatiwa na Sarina kwa ajili ya matumizi ya dharura njiani, niliendesha gari kwa mwendo mkali ambao ulinifikisha katika hoteli ya Hilton kwa muda wa dakika takribani tano  tu. Nilisogea hadi kwenye kibanda cha simu kilichopo jirani na hoteli hiyo ambapo nilimkuta mwanamke mrefu na mwembamba aliyevaa sweta lenye kofia pamoja na suruali  akiwa amesimama, kofia ya sweta alilolivaa ilikuwa imefunika sehemu kubwa ya uso wake  kiasi cha kutoweza kumtambua. Nilisogeza gari karibu na kibanda hicho cha simu kisha nikapiga honi mara moja na kupelekea yule mwanamke aje kwenye mlango wa mbele ulio pembeni ya dereva kwa upande wa kushoto. Niliruhusu mlango ufunguliwe naye akafungua kisha akakaingia ndani ya gari akaketi.
"lets go (twende)" Aliniambia kwa kingereza tena kwa sauti ninayoijua kabisa ingawa uso wake sikuwa nauona kabisa, ili niuone uso wake vizuri ilinibidi nimvue kofia aliyoivaa kichwani na hapo ndipo moyo wangu ulipiga kwa nguvu hadi nikahisi ulikuwa unataka kupasuka kwani sikutegemea kumuona mwanamke huyu niliyemuona  muda huo.
"Nurulayt!" Nilijikuta nikutamka kwa mshangao baada ya kuiona sura ya Nurulayt kwa mara ya kwanza tangu miaka kumi ipite katika siku ambayo Huwaida alipoteza maisha, Nurulayt  aliposikia natamka jina lake alinitazama vizuri usoni mwangu kwani mara ya kwanza hakuwa ameniangalia usoni.
"Abdul! Ni wewe kweli?!" Nurulayt alijikuta akiniuliza kwa huku akinishika mashavuni mwake kwa viganja vya mikono yake, niliitikia kwa kichwa nikikubali kama ndiyo mimi huku mapigo yangu ya moyo yakinienda mbio. Nurulayt alikuwa kashaanza kutiririkwa na machozi ya furaha kwa kuniona mimi kwa mara nyingine kwani nilipomtazama nilimuona akinitazama huku akiwa na tabasamu lenye kuashiria kurudi kwa matumaini yaliyopotea kwa muda mrefu.
"vipi unaishi huku siku hizi" Nurulayt aliniuliza akiwa anahema kwa nguvu kwa mshtuko uliotokana na kuiona sura yangu mahala hapo.
"hapana Nuru ni matatizo ndiyo yamesababisha niwe huku, vipi wewe unaishi huku?" Nilimueleza kisha nikamuuliza swali, Nurulayt aliposikia swali langu alijiinamia kwa muda wa sekunde kadhaa kisha akainua kichwa akanitazama macho yakiwa yana na machozi.
"Abdul sijui hata nianze kukueleza vipi?" Nurulayt aliongea kisha akaanzs kulia kwa sauti ya chini iliyoambatana na kwikwi.
"usilie Nuru we nieleze" Nilimuambia huku nikimuinua kichwa, aliponyanyua kichwa chaks nilimfuta machozi yaliyoanza kumtiririka mashavuni mwake.
"kwanza tuondoke hapa haraka sana" Nurulayt aliniambia huku akijifuta michirizi ya machozi iliyoanza kumtoka mashavuni mwake, nilimkubalia Nurulayt kisha nikaweka gia ili nirudishe gari nyuma niondoke lakini nilishtuliwa na kioo cha gari langu ambacho ni cha guza kikigongwa. Nilipoangalia nje niliwaona walinzi wanne wa hoteli ya Hilton wakiwa wameongozana na wanaume watatu ambao wawili kati yao walikuwa na sare za jeshi la polisi la nchini Namibia na mmoja alikuwa amevaa kiraia. Kengele ya hatari ililia katika kichwa changu nikajua moja kwa moja tukio nililolifanya hapo hotelini limekuwa kesi na watakuwa wamelikariri gari langu, nilipomuangalia Nurulayt naye alinisihi nisifungue na uoga ulionekana dhahiri kwenye macho yake. Wale walinzi wa hoteli waligonga kioo cha gari kwa fujo kisha mmoja wao akataka kuufungua mlango lakini nilikuwa nimeshaibana, nilipotazama nyuma niliona kuna magari mawaili ya polisi yamekaa yamekaa sambamba yakiacha uwazi ambao ungeweza  kupita gari dogo linaloendeshwa na dereva mzoefu. Nilipowaangalia wale walinzi wa hoteli niliwaona walikuwa wanajadiliana jambo na wala maaskari kisha mmoja wa walinzi akawa anaishika bunduki yske vizuri akija kwenye kioo kwa mwendo wa kukazana. Nilipoona hivyo nilijua nini kinafuata hivyo nilimtazama Nurulayt nikamuambia, "funga mkanda". Nurulayt alifunga mkanda kwa haraka kisha akatulia, yule mlinzi alipokaribia kioo akalenga kioo kwa kitako cha bunduki aliyoishika ili avunje kioo awezs vifunga mlango afunguo mlango, mimi nilipoona hivyo nilikanyaga mwendo wa gari kwa nguvu na gari ikaanza kurudi nyuma kwa kasi ya ajabu hadi pale magari yalipoacha upenyo nikimuacha yule mlinzi akiwa ameanguka chini. Nililipitisha gari kwenye upenyo ule kisha nikalizungusha mithili ya pia kugeukia upande niliotoka, nilipohakikisha gari lipo sawa barabarani nilibadilisha gia nikitoa gia ya kurudi nyuma na nikanyaga mwendo kwa nguvu kuelekea upande wa kusini nikiwaacha wale maaskari wapo mdomo wazi jinsi nilipita kwenye uwazi ulioachwa na magari yao bila hata kuchubua gari. Nikiwa barabarani nilikuwa nikibadilisha gia kila muda na kuifanya gari ikimbie kwa kasi hadi nikawa naingiwa na hofu kwani sikuwahi kuendesha gari yenye mwendo mkali kama hii bugatti niliyopewa na Jasmin, nilipoaangalia nyuma nilikuwa siwaoni hata hao maaskari Niliona taa ndogo ya rangi bluu ikiwa inawaka yenye kama antena ya redio ndogo.
"Shit! wamenibandikia GPS  hawa" Nilisema huku nikikanyaga breki kwa nguvu halafu nikashuka nikaenda hadi nyuma, niliiong'oa ile antena nikaitupa halafu nikarudi ndani ya gari nikaendelea kuendelea kuendesha gari tena safari hii Nurulayt akawa ananielekeza pa kwenda. Baada ya kuhakikisha tumewapotea polisi  kabisa tulielekea nje kidogo ya jiji la Widhoek katika kitongoji ambacho sikukijua jina na hata leo hii pia silijui, Nurulayt aliniongoza hadi kwenye nyumba yenye uzio mrefu pamoja na geti lililochakaa , alishuka hapo akafungua geti nikaingiza gari ndani kisha akafunga. Nilishuka kwenye gari nikaingia ndani nikimfuata yeye aliyetangulia kuingia katika nyumba iliyopo ndani ya uzio huo, nilikaribishwa katika nyumba isiyo na samani za kutosha zaidi ya viti vichache, makochi na meza.
"Abdul karibu sana hapa ndipo ninapoishi" Nurulayt alinikaribisha kwa mara ya pili akiwa amekaa kwenye kochi la watu watatu sebuleni hapo.
"asante Nuru, kumbe umejijenga hivi ukiwa huku ugenini hongera" Nilimwambia huku nikikaa jirani naye kisha nikamwambia, "enhee nipe mkasa mzima uliokufanya uwe huku".
"Ni miaka mitano sasa imepita tangu nilipompoteza mwanangu na nikapopigiwa simu nije nchi hii nikitakiwa nifanye mambo ya kihalifu kwa miaka sita ndiyo nimpate mwanangu, sasa hata ulivyoniona pale nilikuwa nikikusubiri ingawa sikujua kama ni wewe ili twende Zimbabwe tukaibe kilo 500 ya almasi" Nurulayt alieleza sababu ya yeye kuwa katika nchi hii.
"inamaana upo huku kwa ajili ya kumkomboa mwanao?" Nilimuuliza
"si mwanangu  peke yangu bali ni mwanetu, Abdul kumbuka mara ya mwisho nilikuambia nimebeba ujauzito wako. Sasa huyu aliyetekwa ndiye mtoto wetu" Nurulayt aliongea
Maneno yake hayo yalinifanya nijifukirie kwa umakini kisha nikamuuliza, "unamjua aliyemteka?"
Nurulayt alitikisa kichwa kukataa kama hamjui kisha akawa ananitazama usoni akiashiria anatala kunisikiliza nitakavyosema juu ya hilo.
"inaonekana tunasumbuliwa na mtu mmoja ambaye sijui lengo lake ni nini?" Niliongea huku nikimtazama usoni.
"tena anaonekana anajua kila hatua yetu na nyendo zetu" Nurulayt naye akadakia.
"ni kweli usemayo kwani  nimejigundua nina hardware baada ya kuona mshono ambao siujui" Nilmwambia Nurulayt kisha nikamsimulia kilichonikuta nikificha habari za Sarina na Ilham na nikamalizia hadi pale tulipoonana. Baada ya kumsimulia kisa hicho nilimuomba anisaidie kukitoa kifaa nilichohisi kipo mwilini mwangu naye akakubali bila ya kuweka walakini wowote. Nurulayt aliniamuru nimfuate nilipomuambia hivyo nami nikatii, tulienda kwenye chumba kimojawapo katika nyumba hiyo chenye mandhari ya wodi ya hospitali ambayo yalinishangaza sana katika nyumba hiyo.
"usishamgae sana Abdul kwa mtu kama ninayefanya kazi  haramu kama uhalifu lazima niwe na sehemu ya kujitibia majeraha madogo madogo ninayoweza kujitibu, lala hapo unioneshe hiyo alama ya mshono" Aliongea huku akinionesha sehemu ya kulala nami nikatii nikatii nikavua shati nikalala kifudifudi pale aliponioneaha. Nurulayt alichukua kifaa kilicho na umbo la mkasi uliochongoka kwa mbele akanitoboa pembeni ya mshono kisha akaingiza mkasi huo ndani ya ngozi yangu, nilikuwa nasikia maumivu kwa kitendo alichonifanyia lakini sikuwa na jinsi ilnibidi nivumilie tu. Nurulayt alitoa vitu mfano wa mbegu ya ngano vikiwa viwili mwilini mwangu, aliviweka kwenye mkebe wa hospitali wa chuma kisha akanionesha.
"hizi ni hardware mbili tofauti ambazo uliwekewa katika mwili wako, moja hutumika kuonesha mahali ulipo na nyingine imenasa mfumo wako wote wa neva za fahamu na kila chochote unachokifanya waliokufunga hivi vitu wanajua" Nurulayt aliongea huku akinifunga jeraha lililotokea baada ya yeye kupitisha mkasi mgongoni.
"asante sana, nafikiri ni muda wa kazi sasa tuliyopangiwa" Niliongea huku nikivaa shati baada ya Nurulayt kumaliza kunitoa vifaa vilivyokuwa vipo mwilini mwangu.
"inabidi tuondoke hapa kuelekea huko tunapoelekea kwa ajili ya kumkomboa Ilham namuhitaji mwanangu tu" Nurulayt kwa kutaja jina la Ilham ambaye ana jina sawa na binti tuliyepewa mimi na Sarina, niliishia kushtuka tu lakini sikutaka kujiwekea uhakika asilimia mia kuwa yule ndiyo mwanangu na hata ningemuambia Nurulayt kuwa ninaye yupo kwa mpenzi wangu asingeweza kuniamini kwani mwanzo nilimficha nilipomsimulia juu ya masaibu yaliyonikuta. Hivyo niliamua kukaa kimya tu bila kumuambia jambo lolote juu ya Sarina na Ilham, Nurulayt aliniongoza hadi chumba kingine ambacho ukutani mwake kulikuwa kuna mageti ya kutokea nje. Ndani ya chumba hicho kulikuwa kuna gari aina ya diffender yenye  rangi nyeusi isiyo na sehemu ya kuwekea mizigo, pia kulikuwa kuna silaha za kila aina za kupambana humo ndani ambazo nyingine nilikuwa sizijui.
"Abdul kutumia bunduki si unajua?" Nurulayt aliniuliza huku akiniangalia usoni.
"najua sana" Nilimjibu huku nikikumbuka kuwa nilipomaliza kidato cha sita  nilipitia jeshi kama sheria ya Tanzania ilivyo kwa wahitimu, mafunzo ya kulenga shabaha bado yalikuwa yapo kichwani hivyo niliona ndiyo wakati muafaka wa kuyatumia katika kuokoa kila kilicho changu hadi mwanangu ambaye bado hakuwa huru kwa wazazi wake. Napenda nilishukuru jeshi la kujenga taifa kwa kunipa mafunzo haya ya kivita na hata ya kutumia silaha kwani mwanzo sikuyaona umuhimu wake niliyaona ni mateso niliyokuwa nayapitia tu ingawa nilizingatia mafunzo yote, faida ya mafunzo haya ndiyo niliiona katika siku hiyo ambayp ilihitajika nikomboe kila kilicho changu.
"kurutuu! Shonaa tuliaa nyungu juu" Maneno ya maafande wakati nipo katika mafunzo ya kijeshi yalinirudia kichwani yalikuwa yanahusu kusimamia ngumi chini ukiwa umeambatanisha mikono yote, mazoezi haya ndiyo cha mimi kuweza kuhimili silaha ya aina yoyote na hata Nurulayt aliponiambia suala la silaha wala sikuwa na wasiwasi nalo.
"mmh! Umejifunzia wapi?" Nurulayt aliniuliza baada ya kumkubalia kuwa najua kutumia bunduki.
"depo miezi mitatu silaha nimeweza kushika, na bastola nimejifunza mwenyewe kwani nilikuwa nimenunua kwa ajili ya ulinzi nilipokuwa Dar" Nilimjibu Nurulayt huku nikitabasamu naye akatabasamu.
"poa chukua silaha kiasi chako uingize kwenye gari hiyo katikati ya viti vya nyuma  vuta kapeti ya gari kuna sehemu ipo na mlango, funguo uziweke humo" Nurulayt aliniambia huku akienda sehemu yenye silaha.
Nilienda sehemu yenye silaha nikachagua bastola za aina mbili pamoja na maboksi kadhaa ya risasi, kwa bunduki kubwa nilichukua bunduki aina ya UZI ya nchini Israel ambayo imeundwa na mwanajeshi wa kiyahudi anayeitwa Uziel Gal mwaka 1948. Bunduki hii ni moja  kati ya bunduki hatari duniani yenye uwezo kupiga risasi mfululizo kama ilivyo AK47, MP5 na nyinginezo, nilibeba risasi za kutosha na viwambo vya kuzuia sauti nikaenda kuviweka pale nilipoelekezwa.
"vipi visu hubebi?" Nurulayt aliniulixa huku anipatia visu sita vikubwa, nilivipokea visu hivyo bila ya kusema chochote nikaviweka kwenye gari kisha nikamtazama kama anaweza kuniambia la ziada.
"panda tuondoke" Nurulayt aliniambia nami nikazunguka mbele kwenye mlango wa pembeni ya dereva nikapanda.

*jingine hilooo

No comments:

Post a Comment