Monday, November 30, 2015

DHAHAMA SEHEMU YA KUMI NA TATU




TEMBELEA: www.facebook.com/riwayamaridhawa 



 DHAHAMA


MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



SEHEMU YA KUMI NA TATU!!
"Faridaaa!" Shafii aliita jina la mke wake  kwa nguvu huku akijaribu kuinuka kitandani
"Shafii hebu tulia kwanza utasababisha  matatizo mengine tu" Mzee Buruhan alimuambia huku akimzuia asifanye fujo.
"Mama Zayina, Zayina mpo wapi?" Shafii alipiga kelele zaidi na ikabidi daktari aitwe mara moja ili kumtuliza, Mzee Buruhan na Mzee Mahmuf walimshikilia  Shafii hadi daktari alipokuja akamchoma sindano ya usingizi ndiyo ikawa ahueni.
Baada ya Shafii kulala mzee Buruhan na mzee Mahmud  walitoka pamoja na mke wa Hamis wakaenda kuka kwenye madawati ya kusubiria wagonjwa, baada ya muda mke wa Hamis aliondoka kwenda kufuata chakula kwa ajili ya mgonjwa akawaacha wazee hao peke yako.
"Kama nilivyokuambia mzee mwenzangu kuhusu huyu mwanao, awe mkweli ujue tatizo alilonalo ndiyo nitakubali kumsaidia" Mzee Mahmud aliongea.


****


"Mzee mwenzangu tatizo kila kukicha una misemo ambayo imejaa vitendawili vitupu hebu niweke wazi walau kidogo nipate fununu ya jambo linalomsumbua mwanangu" Mzee Buruhan alimlalamikia rafiki yake kutokana na kauli zake zilizo jaa mafumbo.
"mzee mwenzangu hiyo kinyume na utaratibu wa taaluma yangu siwezi kusema hata kama nalitambua tatizo hili, huwa sina tabia ya kukuficha kitu ila kwa hili wacha nikuambie ukweli tu nitakuwa nimekiuka masharti ya utalaamu wangu wa uganga ikiwa nitalisema suala hili pasipo muhusika mwenyewe kufungua kinywa chake na kuliongelea. Utanisamehe kwa hilo" Mzee Mahmud aliongea huku akimshika bega mzee Buruhan ambaye alionekana kuwa njia panda kutokana na matatizo yaliyomkumba mwanae
"mzee mwenzangu hakuna hata njia nyingine ya kunisaidia niweze pata fununu kidogo ya hili suala?" Mzee Buruhan aliuliza huku akiwa ameinamisha uso wake chini akionekana amekata tamaa kabisa ya suala hilo.
"Siku zote mwanamke atakaye mtoto lazima akubali kuvua nguo ya ndani ili alichokificha kionekane na hawezi kupata mtoto ikiwa atakataa kuivua hiyo nguo. Ndiyo hivyo hivyo mwanao akubali alilolificha moyoni mwake lifumbuke la si hivyo hataweza kupata msaada katika hilo, cha kukusaidia akiamka muambie umebaki peke yako ukitaka usipoteze vyote awe muwazi kwangu na kwako. Naenda msalani mara moja mzee mwenzangu" Mzee Mahmud aliongea kisha akajiinua kivivu  kwenye dawati la kusubiri wagonjwa akawa anaelekea chooni, mzee Buruhan alimtazama tu akiwa anatamani sana ajue jambo lililopo ndani ya kichwa chake lakini hakuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Mzee Mahmud  aliipopotea katika upeo wa macho yake aliinua kichwa juu akiweka ishara ya kuomba dua halafu akatikisa kichwa kuonesha anasikitishwa, hakuwa na jambo jingine alilomuomba Mungu zaidi ya kumshtakia tu  juu ya balaa lililomkuta mwanae na kumfanya awe na matatizo tu katika mwaka huo ambapo miaka mingine yote aliishi kwa amani na furaha pamoja na familia yake lakini sasa furaha hiyo imetoweka  katika maisha yake. Laiti angelijua kwamba alikuwa anashtaki mtuhumiwa kuwa ameonewa wala asingelifanya hivyo lakini kwakuwa hakujaliwa uwezo wa kulibaini kwani alikuwa ni mwanadamu wa kawaida tu, hakutambua kama jereha la mwanae ni  la kujitakia hivyo halihitaji pole hata kidogo.
   
Mzee Mahmud alipofika kwenye mlango wa msalani baada ya kuondoka pale kwenye dawati alihisi hali isiyokuwa ya kawaida katika mwili wake lakini aliipuzia na kuingia humo msalani, alipoingia ndani alipitiliza sehemu za kujisaidia haja ndogo akawa anaelekea sehemu maalum ya yenye vyoo ndani ambayo hutumiwa na wale wanaohitaji kumaliza haja zao kwa siri tu. Alipofika hilo eneo  alifuata mlango wa moja wa vyoo akashika kitasa ili aufungue lakini alisita baada ya  kusikia upepo mzito ukivuma kwa ghafla ambao ulitaka hata kuupeperusha msuli aliojifunga kiunoni lakini aliuzuia, upepo huo ulipotulia Mzee Mahmud alionekana kukerwa nao kwa kitendo cha kutaka kumuadhiri ambapo aligeuka nyuma akionekana kuwa na hasira za waziwazi juui ya tukio hilo.
"Adabu gani hizo ewe mwanajini wataka kuniadhiri kwa hizo nguvu zako ulizojaliwa?" Mzee Buruhan alilalamika baada ya kumuona yule aliyetaka kumuadhiri kwa kutaka kuupeperusha msuli aliojifunga kiunoni alikuwa yupo mbele yake baada ya kugeuka nyuma, alikutana uso kwa uso na Zalabain akiwa amefumbata mikono kifuani mwake.
"Samahani mzee wangu kwa hilo" Zalabain aliomba radhi.
"sema una shida gani" Mzee Buruhan aliongea huku akiuweka msuli aliojifunga kiunoni vizuri.
"nimekuja kukuambia tu mimi ndiye ninayemtesa Shafii na huwezi kuharibu kazi yangu kwa kujaribu kumsaidia" Zalabain aliongea kwa msisitizo.
"Ndiyo nimeshakutambua tangu unajitokeza pia sipo kwa ajili ya kumsaidia dhalim kama yule bali nipo kwa ajili ya kumsaidia Buruhan ili asiondokewe na nguzo zake zote, kiufupi ni hivi nazuia usimuue yule mziwanda wake asiye na hatia" Mzee Mahmud alimuambia huku akijiamini halafu akameza mate kidogo kisha akaendelea, "Shafii ni haki yake kwa alichokifanya ila Ally hana hatia yoyote na usimuingize katika orodha hiyo, pia ningependa mumponyeshe sikio lske na taya lake ambayo mumjeruhi kutokana na kujaribu kuleta kile kitakachoyafanya majini ya marehemu Hamis yafanye kazi. Ukumbuke pia  yeye anachukia ulilofanyiwa ila mali yako anayoimiliki Shafii ndiyo inamfanya ashindwe kufanya jambo lolote, usihukumu yule asiye na hatia kama ni ufalme utapewa pasipo yeye kupoteza uhai wake".
"unasema nini wewe?" Zalabain alimuuliza Mzee Mahmud
"kama ulivyosikia ewe mwana wa jini, ukumbuke mimi nilikataa kutengeneza uchawi kama uliomtapisha mama yako jana kwasababu najua siyo haki kufanya hivyo, pia niligoma kufanya dawa ya kumuua baba yako ili mama yako awe chini ya mwingine kwasababu najua haikuwa haki. Pia utambue nakuambia usimuue Ally kwasababu najua utakuwa hutendi haki ewe mwanajini kamuuulize ibin Zultash atakueleza, mwisho kabisa nakuambia hivi upotee sasa hivi kuna mtu anaingia humu msalani sasa hivi asije akaniona naongea peke yangu kama kichaa wakati nina akili  zangu timamu" Mzee Buruhan aliongea kisha akageuka nyuma akaingia chooni bila kujali kama Zalabain ameondoka au yupo, baada ya kumaliza haja zake  alitoka hakumkuta Zalabain na akarudi kule alipokuwa yupo awali. Alimkuta mzee Buruhan yupo na Ally wakiongea na iilonekana Ally alikuwa kapona kabisa tatizo la kuvunjika taya na sikio kwani hakuwa mwenye kuweza kuzungumza wala kusikia, lakini hapo alikuwa akizungumza na kusikia vizuri kabisa.
Mzee Mahmud alimuonesha ishara ya kumsalimia Ally kama ilivyokuwa akifanyiwa kwa kutoweza kusikia vizuri lakini.
"Mzee mwenzangu anaongea huyu na kusikia sasa hivi usimsabahi kama vile unamsabahi bubu" Mzee Buruhan alimuambia rafiki yake.
"Yapaswa  tumshukuru Mungu basi mzee wangu maana huu muujiza tosha" Mzee Mahmud aliongea akionekana kufurahishwa na suala hilo.
"Alhamdililah" Ally na baba yake waliitikia kwa pamoja.
Mzee Mahmud alibaki kutabasamu tu kila alipomuangalia Ally kwa kufurahishwa na usikivu alionao Zalabain baada ya kufanya kile alichomuambia, tabasamu lake lilifanya Mzee Buruhan na Ally nao watabasamu  wakijua kafurahishwa na hali ya Ally kutengemaa.
"Ally hebu sogea karibu" Mzee Mahmud alimuambia Ally  huku akimtazama kwa umakini, Ally alimsogelea Mzee Mahmud pasipo kujua ni kipi alichokuwa anataka kufanyiwa kwani alimzoea sana mzee Mahmud na alimchukulia kama baba yake tu. Alipomsogelea Mzee Mahmud aliambiwa achuchumae mbele yake naye akatii amri kama alivyoambiwa, mzee Mahmud alimshika kichwani na akamtamka maneno yasiyoeleweka na kusababisha Ally ashtuke halafu aangalie mazingira ya hapo yalivyo halafu akaenda kukaa kwenye dawati pembeni ya baba yake alipokaa awali.
"Baba hivi hapa tupo kwa ajili gani?" Ally aliuliza tu baada ya kukaa pembeni ya baba yake akionekana kutotambua yupo hapo kwa ajili gani.
"Kha! We Ally maswali gani hayo hutambui kama tupo hapa kumuangalia kaka yako kalazwa tangu jana" Mzee Buruhan alimuambia Ally akionekana kutoelewa kitu alichofanyiwa na  mzee Mahmud hadi akasahau  yupo pale kwa lengo gani wakati alipoingia tu aliulizia hali ya kaka yake.
"Khaa! Kumbe tupo hapa kwa ajili ya kumuangalia firauni huyo, sina muda huo muache afe  maana huyo ni zaidi ya shetani" Ally aliongea maneno ambayo yalizidi kumshangaza sana Mzee Buruhan na akajikuta  akimtazama  mzee Mahmud akionekana kutoelewa kafanya nini, Ally alinyanyuka ili aondoke lakini mzee Mahmud alimuita akamuomba aketi akakaa chini.
"Ally tambua undugu ni kovu na halifutiki usifanye hivyo, najua unaumia kwa kile alichokifanya kaka yako lakini kumbuka ndugu ni ndugu tu" Mzee Mahmud aliongea kwa ustarabu wa hali ya juu akitegemea ataeleweka na Ally lakini haikuwa hivyo.
"Baba zangu mngejua alichokifanya huyo firauni mnayekuja kumuangalua wala msingethubutu kukaa hapa, na sijui hata ni kwasababu gani nilikuwa nikimpenda kwa kipindi chote hicho nahisi aliniroga yule maana miale ya mkufu wake sielewi hata imemifanyaje wakati nilikuwa nikimchukia" Ally aliongea  huku akionesha kumchukia  kaka yake.
"Ally unaongea nini wewe?" Mzee Buruhan aliuliza akionekana kushangaza na maneno anayoyaongea mwanae.
"Mzee mwenzangu kama nilivyokuambia hili tatizo linajulikana ila huyu hatakiwi kulisema na akilisema atakuwa kiziwi kama mwanzo muache huyo Shafii aeleze kila kitu. Unajua..." Mzee Mahmud aliongea maneno yaliyomfanya Mzee Mahmud atulie kimya na alishindwa kumalizia kauli yake baada ya mke wa Hamis kurudi akiwa amebeba chombo cha chakula kwenye mfuko wake.
"Vipi mgonjwa jamani tayari ameshaamka?" Mke wa Hamis aliongea baada tu ya kuwasili na alimuonesha Ally tabasamu kisha akampa mkono akampa mkono ili amsalimie akijua kuwa Ally hawezi kuongea.
Ally hakuupokea mkono wa Mke wa Hamis zaidi ya kusonya kwa nguvu kisha akanyanyuka akasema, "shetani jike mkubwa wewe".
Ally alinyanyuka kwenye dawati la kusubiri wagonjwa akaelekea mahali akimuacha wazee wake na mke wa Hamis wakimshangaa sana, mke wa Hamis alipotaka kumfuata nje Mzee Buruhan alimshika akamzuia.
"Salma mama naomba unisikilize kwa umakini, achana na Ally kwa sasa kaa hapo usubiri muda wa kumuona mgoniwa akizinduka tukamuone" Mzew Buruhan alimuambia Salma mke wa Hamis.
"Lakini Ally kapatwa na nini wazee wangu kwani alikuwa hawezi kuongea na kusikia ila sasa hivi anaongea na kusikia  ila amekuwa kama akili haziko sawa hadi ananisonya mimi" Salma aliongea huku akishangazwa na hali ya Ally yule aliyekuwa anamsikiliza na kumtii na kumuheshimu ameamua kuonesha dharau.
"Hebu mama kuwa muelewa achana na habari za Ally sasa hivi, tufikirie kuhusu mgonjwa tu" Mzee Mahmud aliongea kwa msisitizo huku  akionekana kutopendezwa na maneno ya Salma.
"Sawa baba zangu nimewaelewa" Salma alijibu kwa shingo upande ili tu asiwaudhi  wazee ambao anawaheshimu.


****

 Wakati Ally akifunguliwa na kuanza kumuoneshea dharau upande wa himaya ya Majichungu Zalabain ndiyo alikuwa amerejea muda huo na aliamua kupitia chumbani walipo mama yake na dada yake ili awaone kutokana na upendo alionao kwao, alibisha hodi kwa adabu ingawa alitambua hata akiingia muda huo asingewakuta wakiwa bila stara. Alipokaribishwa aliingia kwa adabu  na akaenda hadi walipokuwa wamekaa kitandani na akawasalimia, halafu naye  akaketi kitandani jirani yao.
"Mwanangu kila nikikutazama namuona baba yako kwa jinsi wote mlivyokuwa na sura zilizofanana, haya niambie unatoka wapi?" Bi Farida aliongea kisha akamuuliza Zalabain.
"Nilikuwa Tanga kwenye  hospitali ya SBN nilienda kuongea na mzee Mahmud" Zalabain alimuambia mama yake.
"Mh! Huyo mzee huko hospitalini anafanya nini?" Bi Farida aliuliza.
"Amekuja kumuangalia mumeo amelazwa" Zalabain alimuambia mama yake.
"Jamadin sina mume kama huyo mimi tena sitaki kumsikia ukimtaja, mume aliyetakiwa kunioa mimi ni Faimu tu na sijui ilitokea nini mpaka nikamkana na nikamsababishia matatizo makubwa sana akahama kijijini akiwaacha jamaa zake. Nampenda Faimu na natamani nimuone hata leo ili nimuombe msamaha maana yeye ndiyo kila kitu kwangu" Bibi Farida aliongea na  mwishowe akalia kutokana na kujutia aliyoyafanya ya hapa zamani, Zalabain ilimbidi amkumbatie mama yake ambembeleze kutokana na upendo alionao kwake.
"Samahani mama kwa kukupa taarifa smbayo hutaki kuisikia,  sipendi uhuzunike nakupenda sana" Zalabain alimuambia mama yake baada ya kunyamaza.
"Nakupenda pia mwanangu" Bi Farida alisema huku akitabasamu kwa mbali, waliendelea kuongea maongezi mengine kwa furaha wakiachana na suala ambalo lilionekana kutomfurahisha kabisa Bi Farida.


****


 Baada ya masaa mawili Shafii aliamka kutoka usingizini akiwa yupo vizuri kiafya kuliko awali, hali yake iliendelea kutengemaa na ilipofika muda wa alasiri aliruhusiwa na daktari na alirudi nyumbani akiwa ameongozana ns wote waliokuja  kumuona hospitali kasoro Ally tu ambaye hakurudi tangu aondoke pale hospitali. Shafii alipelekwa moja kwa moja chumbani kwake na akaachwa apumzike na kisha wazee wake wakakaa sebuleni hadi ilipoingia jioni ndiyo mzee Buruhan na mzee Mahmud waliingia chumbani kwa Shafii wakamkuta akiwa ameamka ameegemea mito kitandani kwake,  Shafii alipoona ujio wa wazee wale alihisi kuna jambo ila alikaa kimya ili apate uhakika wa wasiwasi wake.
"Shafii" Mzee Buruhan alimuita
"Naam Baba" Shafii aliitikia
"unajua kama wewe ndiyo nguzo kuu kati ya nguzo zangu nne zilizobakia?" Mzee Buruhan alimuuliza
"nafahamu hilo baba" Shafii alijibu.
"Hussein hatunaye, Hamid hatunaye, Hassan ni mdogo kwako, Falzal ni mdogo kwako na Ally pia ni mdogo kwako. Wewe pekee ndiyo mkubwa ndiyo kiongozi wao ingawa wote wana maisha yao na hata wanajisomesha wakitaka kujiendeleza kielimu. Nadhani unatambua hilo" Mzee Buruhan alisema.
"Ndiyo baba natambua hilo" Shafii alijibu.
"Sasa basi inapotokea tatizo lenye kuhitaji kuelezewa ili lisizidi zaidi inabidi lielezewe mwanangu ikiwa utakaa kimya haitasaidia chochote" Mzee Buruhan aliongea.
"Baba sijakuelewa unachomaanisha" Shafii aliongea.
"Shafii najua unatambua suala la upotevu wa mke wako na hata mwanao linalokufanya uwe na matatizo kila kukicha, sasa mwanangu ukilificha itakusaidia nini ikiwa unalifahamu chanzo chake. Kumbuka mficha maradhi kifo humuumbua mwanangu, mwanangu ni bora uitoe aibu mbele ya daktari ili utibiwe kuliko kuficha tatizo halafu ufe na ugonjwa. Ongea chanzo cha  haya ni nini?" Mzee Buruhan alimsihi mwanae.
"Baba kusema ukweli sijui wala sitambui suala hili linasababishwa na nini?" Shafii alikataa.
"Shafii vuta kumbukumbu zako vizuri umefanya nini mpaka yote haya yatokee au hutaki  familia yako uione tena ikiwa na upendo" Mzee Buruhan alizidi kumsihi.
"Baba napenda sana familia niione tena ikiwa ina upendo lakini sikukumbuki chochote kilichosababisha haya ninayofanyiwa"  Shafii alikana kabisa juu ya suala hilo.
"Jirani na mashine ya kusaga unga kule Mpirani miaka ishirini na moja iliyopita unakumbuka kilitokea nini pale kwenye  nyumba yako uliyokuwa unaishi  baada ya wewe kuhama tena ilikuwa majira ya saa sita usiku?" Mzee Mahmud aliongea kwa mara ya kwanza na kumfanya Shafii ashtuke kwa jambo alilotajiwa, lilikuwa ni jambo ambalo alishalisahau kabisa katika ubongo wake na sasa alikumbushwa na mzee huyu ambaye ni mganga mtaalam.
"Shafiii unakumbuka nini hiyo siku" Mzee Buruhan naye aliunganisha maelezo ya rafiki yake ingawa hakuyaelewa kabisa, maneno ya mzee  Mahmud  yalimfanya anyamaze ghafla huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini.
"Shafii si nakuuliza" Mzes Buruhan aliongea huku akimtikisa bega baada ya kuona yupo kimya, Shafii alikurupuka baada ya  kutikiswa bega kama alikuwa yupo  katika usingizi mzito.
"Ha..hapana  si....sikumbuki chochote" Shafii aliongea kwa kubabaika baada ya kuhisi moja ya jambo baya alilolifanya linakaribia kugundulika.
"Una uhakika?" Mzee Mahmud aliuliza.
"ndiyo baba zangu nina uhakika wa kile ninachokiongea" Shafii alijikaza akajibu kwa kujiamini.
"mzee mwenzangu sisi twende tukanywe kahawa si unaona muda huu na kiubaridi cha kipupwe kimeanza, Shafii kama hujui juu  ya hilo basi inakupasa utambue kuwa maisha ya mkeo  na binti yako yapo kwenye kinywa chako kueleza unachojua na ukikaa kimya jua kinachofuata ni kama kilichowapata wadogo zako ia utambue umebaki peke yako" Mzee  Mahmud huku akiwa tayari amesimama na Mzee Buruhan naye akasimama, wote kwa pamoja walianza kutembea kuelekea ulipo  mlango ili waondoke lakini sauti ya Shafii ikiwaita iliwafanya wasimame na kugeuka wakamtazama.
"Nipo tayari kuwaambia kilichotokea wazee wangu naomba mnisaidie" Shafii aliongea baada ya kuona maji yamemfika shingoni na maneno ya mzee Mahmud ndiyo kabisa yalimfanya akubali. Mzee Mahmud alimtazama Shafii kwa tabasamu hafifu halafu akamuambia, "kesho muda kama huu pale ulipokuwa unaishi kule mpirani ndiyo kutakupa ahueni ya  tatizo lakokwa familia yako"
Mzee Mahmud aliposema maneno hayo alitoka humo ndani bila hata kumuangalia Shafii kwa mara nyingine, Mzee Buruhan naye alifuata akiwa nyuma yake.


****


Maneno ya Ally baada tu ya kupewa mkono na Salma yalimfanya Salma karibia siku nzima akiwa anajifikiria kwani Ally alikuwa amepatwa na nini mpaka awe vile, ilipofika jioni aliamua kutoka na kwenda kumtafuta Ally bila ya kumueleza mtu ili aongee naye tu kwani Ally alikuwa ni mmoja kati ya wanaume aliokuwa anawapenda na kipindi cha nyuma alipokuwa msichana alishajaribu kujivika ujasiri na kumueleza Ally yaliyo moyoni mwake lakini aliishia kukataliwa baada ya Ally kuwa anamuheshimu sana Hamis ambaye alikuwa na mahusiano na Salma kabla hajamuoa. Baada ya mpango ambao ndiyo chanzo cha balaa lote lililowakumba watoto wa  mzee Buruhan, Ally alifungwa akili na akawa anasikiliza wote waliofanya mpango ule bila hata kuwapinga na alifungwa akili baada ya kuujua mpango huo akawa  amekasirishwa nao. Baada ya kufungwa akili ndipo Salma alipompata Ally kutokana na yeye pia ni mmoja kati ya watu walioshiriki huo mpango, alimtumia Ally vyovyote atakavyo baada ya Ally kutopinga kauli yake. Sasa akili ya Ally ilipofunguliwa na Mzee Mahmud na Salma kujibiwa vile alijikuta roho ikimuuma akijua Ally amepatwa na tatizo hivyo  aliamua kumtafuta.  Hakukujua kama Ally wa leo siyo wa jana alichokuwa anakijali yeye ni penzi lake  haramu alilolianzisha kwa Ally hata alipokuwa yupo ndani ya ndoa.
Tamaa za kutamani kingine wakati akiwa tayari ana kingine mkononi ndiyo zilimfanya Salma afanye jambo hilo ambalo lilipelekea afiche siri nzito sana ambayo laiti ingaligundulika mapema basi angekuwa ameleta matatizo makubwa sana kwa Hamis na Ally.
Juhudi za Salma kumtafuta Ally ziliendelea kwa usiku huo akiwa yupo ndani ya gari yake na hatimaye alimkuta akiwa amekaa kwenye matairi yaliyochimbiwa katika uwanja wa mpira  uliopo mkabala na shule ya sekondari ya Usagara, Salma alimfuata hadi hapo akaegesha gari pembeni kisha akashuka akaenda kumkumbatia Ally akitegemea atapokelewa lakini alijikuta akisukumwa hadi akaanguka chini akaumia.
"Kaa mbali na mimi malaya wewe!" Ally alimuambia kwa ukali.
"Lakini Ally mpenzi wangu nimefanyaje?" Salma aliuliza kwa masikitiko makubwa huku akionekana kuumia baada ya kusukumwa.
"Unajifanya hujui siyo tena usiniite mpenzi wako kuanzia hivi sasa, we wa kunifanya mimi mtumwa wa ngono hadi umesababisha nisioe wakati natakiwa kuwa na familia sasa hivi" Ally alifoka.
"Ally nakupenda ndiyo maana nimefanya hivyo hadi nikazaa na wewe" Salma akaongea huku akilia.
"Weee tena ishia hapo hapo" Ally alimkaripia huku akimuongeza teke la mguu Salma.
"Ally nikatae ila ukae ukijua Hamida siyo mtoto wa mume wangu bali ni damu yako, ndiyo maana hata alipozaliwa kaka yako alikutania umefanana naye miguu ila ukweli ile ni damu yako kabisa" Salma aliongea huku akilia, Ally alipuuza maneno ya Salma akaondoka eneo akimuacha akilia ingawa kuna jambo lilikuwa likiisumbua akili baada ya kusikia maneno hayo.




ITAENDELEA!1

No comments:

Post a Comment