Saturday, November 28, 2015

KOSA SEHEMU YA KUMI NA MOJA

 KOSA


MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE



 ILIPOISHIA
Sauti ya yule mtu iliniambia, nilikuwa nikimsikiliza kwa umakini huku nikiuendea ule mzigo hadi nikaufikia bila hata kumuangalia Sarina aliyekuwa ananitazama kwa umakini.
"fungua mzigo sasa usiutazame tu" niliambiwa na mimi nikatii nikaufungua mzigo huo ambao uliniacha nikiwa nimepigwa na bumbuwazi kwa kile nilichokiona, hata Sarina naye alipigwa na bumbuwazi kwa alichokiona ndani ya boksi hilo.
"vizuri kwa kuufungua mzigo huo, sasa kama unataka ujute maishani mwako kidharau hicho ulichokikuta humo ndani na kama hupendi kujuta basi ukitunze nilichokukabidhi kwani si mali yangu ila kipo chini ya uangalizi wangu" Sauti ya kwenye simu ilinisisitiza kisha simu ikakatwa.



ENDELEA NA MKASA HUU WENYE KUSISIMUA NA KUELIMISHA


SEHEMU YA KUMI NA MOJA!!
Macho yangu yote niliyaelekeza ndani ya boksi hilo kwa kutazama kile nilichokiona ndani yake, sikutegemea kabisa kama nitaletewa  mzigo mwingine wakati tayari nina gunia zito la mchanga katika kichwa changu ambalo linaonekana kunizidia uzito. Mtu huyu anayenipa tabu zote hizi nilimuona kama amepanga kuniongezea uzito akijua tayari nimeelemewa ili nianguke, ndani ya boksi hilo kulikuwa kuna mtoto wa kike wa kisomali apataye miaka kumi au tisa  kama ungekadiria umri wake. Alionekana ni binti mrembo na mwenye kuvutia ikiwa utamtazama machoni, alikuwa na nywele ndefu sana zenye rangi nyeusi sana. Sura ya mtoto huyu niliifananisha kama niliwahi kuiona mahali lakini sikuwa nakumbuka ni wapi niliiona, nilibaki nikimshangaa huku moyoni nikichoka kabisa kutokana na kuhisi nimeelemewa na mzigo mwingine wa kumtunza huyu binti mdogo na mrembo ambaye nilihisi hakuwa na hatia yoyote mpaka aletwe mbele yangu mimi aje kuteseka akikosa matunzo ya wazazi wake. Binti mdogo mwenye kila sifa ya kuitwa mzuri hata akiwa mkubwa basi angekuwa ni tishio kwa urembo wake ambao unaonekana mapema tu akiwa na umri huo, akiwa ndani ya boksi alikuwa yupo ndani ya usingizi mzito sana kwani nilimtingisha hakuonekana kuamka kabisa. Alivyolala ndani ya boksi hilo ni wazi alikuwa anaumia na hata angeamka angejihisi maumivu kwa jinsi alivyojikunja, nilimtoa kwenye boksi na nikamlaza kwenye kochi ili aweze kulala vizuri kutokana na kujikuta nikiingiwa na huruma ya ghafla kila nikimuangalia jinsi alivyolala hapo kwenye boksi. Sarina alibaki kapigwa na butwaa baada ya kumuona mtoto huyo na hata nilipokuwa ninayafanya yote hayo yeye alibaki akishangaa kama mtu aliyepumbazika, alikuja kutoka kwenye kupumbazika huko baada ya kusikia kilio changu cha chinichini kilichoanza kunipata baada ya kupewa mzigo mwingine. Sarina alipoona kilio changu kinazidi alinisogelea halafu akaniambia, " Abdul huil nie jy is 'n man, 'n bepaling van die
hart(Abdul usilie wewe ni mwanaume, kuwa mkakamavu)".
" Sarina seer het ons net gelaat word, wat nie die
man wat ek mkisea weet wat?(Sarina inauma we acha tu, sijui huyu mtu nimemkosea nini?) Niliongea huku nikibubujikwa na machozi na macho yangu yote nikiwa nimeyaelekeza alipo msichana mdogo niliyemtoa kwenye boksi, hakustahili kuletwa kwa mtu mwenye matatizo kama mimi tena asiye na mbele wala nyuma huku ugenini kwenye nchi yawatu.
" nou was sy sy skuld Wat my bring ng, nie sal jy
ly sonder enige skuld( sasa huyu binti kosa lake ni lipi mpaka niletewe mimi, huoni kama atateseka bila ya kuwa na hatia" Niliendelea kulalamika huku machozi yakiwa yananitoka bila hata kuonesha dalili yoyote ya kuonesha kikomo chake kinakaribia, Sarina alizidi kunitazama na huzuni hasa nilipozidi kulia mtoto wa kiume kwa kumuhurumia msichana niliyetewa.
" Sarina het niks om te dra, sy deel van die slaap
en doen sy deel te kos. U is my hulp, nou sy
was om te sien of dit is 'n las en sal ly( Sarina sina cha kuvaa, sina sehemu ya kulala na wala sina sehemu ya kupata chakula, Wewe ndiyo msaada kwangu, sasa huyu binti huoni kama ni mzigo na atateseka)" Niliendelea kuongea huku machozi yakinitoka kila nikimtazama msichana niliyeletewa, Sarina alipoona ninazidi kulia alinikumbatia bila kusema chochote na alipoacha kunikumbatia alinibusu kwenye paji la uso halafu akaenda hadi pale alipolazwa yule binti halafu akaketi jirani naye. Alimnyanyua yule binti kichwa chake akakiweka kwenye mapaja yake kisha akaanza kuzichezea nywele za binti huyo, nilibaki nikimtazama huku kilio changu nikiwa nimekisitisha nikimtazama yeye tu.
" Abdul as ek is nuttig vir jou, dan is dit nuttig om
te sy dogter sal wees, ek toevallig baie lief en ek
kan nie laat dit om te ly wanneer ek kan steun te
gee(Abdul ikiwa mimi ni msaada kwako basi huyu binti nitakuwa msaada kwake, nimetokea kumpenda sana na siwezi nikamuacha ateseke wakati uwezo wa kumsaidia ninao)" Sarina aliongea huku akimtazama yule binti kwa huruma sana, maneno hayo yalinifanya nimuone Sarina ni mwanamke wa kipekee sana kwani si jambo rahisi kwa mwanamke mwingine wa kawaida na wenye mioyo ya aina hiyo duniani laiti tungewahesabu  na kuwaweka katika asilimia basi wangekuwa ni asilimia mbili kati ya asilimia mia moja. Sarina ni mwanamke wa kipekee sana kwa uamuzi huo aliouchukua, nilijikuta nikienda kukaa karibu naye katika lile kochi halafu nikachukua miguu ya yule binti nikaipakata kwenye mapaja yangu kama Sarina alivyokipakata kichwa chake. Sarina aliniangalia nilipofanya hivyo halafu akatabasamu bila hata kuniambia jambo lolote, na mimi nilitabasamu kisha nikamvuta Sarina nikambusu mdomoni halafu nikamuambia " Sarina is lief vir jou en ek ophou om jou lief te
hê, is jy beslis unieke vrou (Sarina nakupenda sana na sitoacha kukupenda, hakika wewe ni mwanamke wa kipekee)". Maneno hayo yalimfanya Sarina atabasamu kisha akaniegemea begani huku mkoni wake ukiwa umeshika shingo yangu, tukiwa tupo namna hiyo msichana tuliyetewa alianza kupiga chafya mara mbili huku akifikicha macho yake. Wote wawili tulishtuka na tukawa tunamtazama huyu binti kwa mshangao wa kutaka kutaka kumuona akifungua macho yake, binti alipopiga chafya mara ya tatu alifumbua macho taratibu na akashtuka baada ya kutuona sisi ambao ni wageni kwake.
"nyinyi wakina nani? Hapa ni wapi?"   Binti huyu aliongea kiswahili fasaha huku akirudi nyuma kwa wasiwasi kabisa na hapo ndipo nikatambua kuwa anaongea kiswahil, Sarina alishangaa sana kwani lugha hiyo hakuwa anaitambua kabisa.
"hapa ni sehemu salama" Nilimwambia kwa kiswahili ili kumtuliza nikimuacha Sarina akiwa haelewi chochote.
"mmenihamisha kwingine sio, sitaki namtaka mama yangu" Binti huyu alianza kulia huku akigaragara lakini niliwahi kumtuliza kisha nikampa maneno mazuri yaliyomfanya awe na sisi, alipotulia kabisa tulimketisha katikati yetu mimi na Sarina.
"mtoto unaitwa nani?" Nilimuuliza kwa upole.
"Ilham" Alijibu
"sikiliza mtoto mzuri nipo tayari kukusaidia, umuone mama yako. Lakini kwanza tuambie ulikuwa wapi kama unakumbuka na ikiwezekana utueleze yaliyokukuta kwa ufupi" Nilimwambia huku nikimshika kichwani nikimtazama kwa macho ya huruma sana. Nilipomuuliza hivyo alijibu, "nilikuwa nikitoka shule tu nikajikuta nimekamatwa nikawekewa kitambaa mdomoni, nililala nilipokuja kuamka nikajikuta nipo nisipopajua".
"polee Ilham, unakumbuka ilikuwa lini?"  Nilimuuliza huku nikimshika bega tena safari hii nilipiga magoti mbele yake. Ilham nilipomuuliza hivyo alinitajia tarehe, mwezi na hadi  siku aliyokamatwa pamoja na mwaka, nilibaki nikiwa nimepigwa na butwaa baada ya kubaini kwamba siku aliyokamatwa Ilham  ni miaka mitano iliyopita hivyo amefungiwa kwa miaka mitano hadi inafika siku hiyo tunamkuta ndani ya boksi. Nilimfasiria Sarina yote aliyokuwa akiyaongea Ilham ambayo pia yalimshangaza hata yeye, Ilham mwenyewe alionekana kutoelewa muda aliokaa ndani.
"kwenu ni wapi na unaishi na nani?" Nilimuuliza
"Kwetu ni Mwanza naishi na mama" Ilham alijibu
"Pole sana mtoto mzuri baba yako yupo wapi?" Nilimuuliza, swali hilo llionekana lilikuwa ni gumu kwa Ilham na akashindwa kulijibu akabaki akiwa ameinamisha uso wake chini.
"Mtoto mzuri utakaa na sisi hadi tutakapokupeleka kwa mama umesikiaeh! Mimi naitwa anko Abdul na huyo hapo ni anti Sarina" Nilimwambia maneno yaliyoambatana na utambulisho mimi na Sarina, Ilham alionesha kuyakubali hayo maneno halafu akamtazama Sarina akiwa anatabasamu pana usoni mwake. Ilham alimkumbatia Sarina huku akitabasamu na Sarina naye akampokea.
" Algehele as 'n ma en kind(Mnapendeza kama mama na mtoto)" Nilimwambia Sarina huku nikitabasamu na yeye akatabasamu alipisikia maneno hayo ambayo hayakueleweka kwa Ilham.
"Anko umesemaje mbona sijakuelewa?" Ilham aliniuliza baada ya kusikia naongea kiafrikaas nikiwa hapo
"katoto hapa sio Tanzania, hivyo hatuongei kiswahili hiki ni kiafrikaas" Nilimwambia Ilham maneno yaliyomshangaza sana kwani mwanzo hatukumuambia alipo ni nchi gani. Ilham alizidi kushangaa  sana na ikabidi nimueleze ukweli juu ya eneo ambalo tupo na nchi yake, pia nikamueleza juu ya Sarina kutojua kiswahili.
"Anko basi mimi hata kifaransa naongea au anti Sarina naye hawezi" Ilham alianza kuchangamka hapohapo hadi akanifanya na mimi nifurahi.
"unaweza kweli kifaransa? Ngoja nikujaribu" Nilimwambia kimasihara huku nikionesha tabasamu ambalo lilimfanya na yeye atabasamu, Sarina alikuwa akituangalia huku akitabasamu baada ya kumuona Ilham ana furaha.
"ndiyo naweza tumefundishwa shuleni toka Nursery" Ilham aliendelea kuweka uchangamfu wake wa kitoto.
" Ce est là?(hapa ni wapi?)" Nilimuuliza kwa lugha ya kifaransa ili nimpime kama anajua kifaransa au hajui kwani na mimi nilikisoma kifaransa nilipokuwa shule ya sekondari pia katika biashara nilikuwa nakitumia kuzungumza na wafanyabiashara  wa kifaransa.
" Maintenant que vous me avez dit vous-même ici,
ce est la Namibie, pourquoi me demandez-vous
à nouveau?(umeniambia mwenyewe hapa ni Namibia, kwanini unaniuliza tena?)" Ilham aliniambia kwa kifaransa fasaha kabisa hadi nikawa namshangaa na kicheko ndicho kilichofuata kwangu na kwa Sarina.
" Je me demande pourquoi je demande même
quand il se dit
(hata mimi nashangaa kwanini anakuuliza wakati amekuambia mwenyewe)" Sarina naye aliongea kifaransa kwa mara ya kwanza tangu nifahamiane nae, sikuwa na natambua kama Sarina anajua kifaransa na hapo ndipo nilipobaki nikimshangaa.
" vous vous demandez pourquoi Abdul, je parle
français? Les gens parlent plusieurs langues
Namibie de six(unashangaa nini Abdul, Mimi kuongea kifaransa? Namibia watu wanaongea lugha zaidi ya sita)" Maneno hayo ya Sarina kwa lugha ya kifaransa ndiyo yalinishangaza sana kwani sikutambua kama raia wa nchi hii wanajua lugha zaidi ya moja.
Maongezi baina yetu yaliendelea ndani ya muda mrefu na furaha ikiwa imetawala maongezi yetu hasa baada ya kuongezeka kwa Ilham katika nyumba hii, Ilhama alikuwa ni binti mchangamfu sana kutokana na kutawaliwa na akili za kitoto. Muda wa mchana ulipowadia ilinibidi nimwambie Sarina kuhusu suala kupeleka pesa kule kwenye sanduku la posta nililopewa namba zake, Sarina alinishauri nizitume zote kwa njia ya posta katika ofisi ya posta ya mjini Widhoek kwenda kwenye sanduku la posta la ghuba ya Walvis. Wazo lake hilo nililiafiki na muda huo huo wote tukaingia kwenye gari kuelekea zilipo ofisi za posta pembezoni mwa barabara ya uhuru (Independence avenue) katika jiji hilo, niliamua kuwa makini sana kwani nilikuwa nina wasiwasi wa kutafutwa kutokana na tukio nililolifanya katika hoteli ya Widhoek siku iliyopita. Njiani Sarina alininunulia kofia ambayo ilinisaidia kuficha sehemu kubwa ya uso wangu, yeye alivaa kawaida sana kutokana na shungi alilolivaa siku iliyopita isingekuwa rahisi kumtambua. Ilham hatukuwa na wasiwasi naye wala hakuwa ana wasiwasi wa chochote, yeye alivaa kawaida tu, baada ya dakika kadhaa tulifanikiwa kufika zilipo ofisi hizo na taratibu zote za kutuma pesa kwenda sanduku la posta la ghuba ya Walvis ikafanywa. Tulifanikiwa kutuma pesa hizo kisha tukaondoka mahala  hapo salama kabisa bila hata kusumbuliwa na hofu ya nafsi ya kuwaona askari waliopo katika ofisi hizo za posta, usukani nilimuachia Sarina safari mimi nikapumzika. Sarina aliendesha gari siku hiyo akipita sehemu mbalimbali ambazo zina maduka ambazo alinifahamisha kama ni maduka aliyoachiwa na baba yake na ndiyo yanayomfanya awepo mjini, tulimaliza kutembelea maduka hayo yote na tukarudi nyumbani muda wa mchana  tukiwa tumefurahia kuzunguka sehemu mbalimbali tukiwa pamoja. Siku hiyo tulishinda nyumbani baada ya kurudi  safari hiyo hadi jioni inaingia tukiongea mambo mbalimbali, kuna muda Ilham alilala na ukawa uhuru kwetu katika kuongea zaidi. Muda Sarina alinisimulia historia ya Maisha  yake kwa ufupi na mimi nikamsimulia yangu pia huku nikiruka kisa changu na Faiz. Kukikwepa kwangu kicho hakukudumu kwani Sarina alitaka nimsimulie historia yangu katika mapenzi baada ya yeye kuanza kunisimulia yake, kwakweli ilinikuwa ni jambo gumu sana kumuelezea juu ya jambo nililolofanya huko nyuma ambalo sitaki linirudie kichwani mwangu. Ilikuwa ni jambo gumu sana kumueleza kisa hicho nikihofia kuvurugika kwa upendo wake kwangu ulioanza kuchipua siku hiyo hiyo, machozi yalianza  kunitoka nilipofikiria kisa hicho ambacho ndiyo chanzo cha mimi kujiingiza katika unywaji wa pombe pamoja na ununuaji wa machangudoa hadi najikuta nchini hapa kwa mara ya mwisho. Hofu ya kumpoteza niliona inanijia waziwazi na jambo hilo sikuhitaji litokee, ningeamua kukaa kimya ningeonekana simkweli hivyo jambo pekee nililoliona wakati huo ni kueleza ukweli kwani dunia haina siri hata siku moja na ukitaka siri fanya jambo la peke yako vinginevyo ukifanya na mtu mwingine jua hiyo siri itajulikana hata kama huyo mtu awe bubu. " est dans l'histoire, ni l'histoire m'a rappelé que je
aimerais que quelqu'un, je si je aimais je
ai trouvé que je ai fait une grosse erreur(ni katika historia nisiyopenda kuikumbusha wala kuihadithia, nilipendwa nisipopendwa nikajikuta nimefanya kosa kubwa" Nilijikakamua nikamueleza kwa ufupi nikitumia lugha ya kifaransa ninayoielewa zaidi kuliko kiafrikaas, Sarina alinitazama kwa umakini sana aliposikia maneno hayo na alikuwa akiniangalia kwa macho yanayohitaji niendelee kumsimulia. Nilishusha pumzi kisha nikaanza kuongea ukweli mtupu kuhusu mambo yaliyotokea nyuma hadi pale Huwaida alipouawa, nilimuelezea kila kitu sikutaka kumficha na machozi muda huo yalikuwa yameshika hatamu katika macho yangu. Nilimaliza kwa kumsimulia kuhusu Nurulayt kuwa na ujauzito kisha nikamtazama yeye nimuone alipokeaje historia yangu, Sarina alionekana kuwa na sura masikitiko sana nilipomaliza kumsimulia haya.
" . Abdul.......Abdul a fait une très grosse erreur
que vous devez être pardonné et offensé, devrait
être libre de trouver le pardon dans votre cœur
pour votre ami(Abdul.....Abdul umefanya kosa kubwa sana ambalo unahitaji usamehewe na uliyemkosea, inabidi uwe huru moyoni mwako kwa kupata msamaha wa rafiki yako)" Sarina aliongea kwa masikitiko huku akinitazama usoni kwa huruma. Sarina aliongea suala la ukweli kabisa kwamba nilikuwa nahitaji msamaha wa Faiz ili niwe na amani ya moyo, lakini ningeanzia wapi wakati sindano ya sumu aliyochomwa Faiz ilikuwa inamuua siku moja inafuata ya tangu Huwaida afariki. Nilimueleza juu ya kutowezekana kwa suala hilo huku nikimsihi asinichukie kutokana na kosa hilo nililotenda kipindi cha nyuma, nilimueleza kwa jinsi ninavyompenda sikuwa tayari kutengana naye.
" Abdul avait fait il ya dix ans ne existait pas, ici
parler à mon copain que je aime Abdul(Abdul aliyefanya jambo hilo miaka kumi iliyopita hayupo, hapa naongea na Abdul mpenzi wangu ninayempenda sana) Sarina aliongea huku akinitazama usoni akiwa na tabasamu pana halafu akanisogeza mdomo wangu karibu na wake tukabadilishana kimininika kisichotoa kiu wala kujaza tumbo. Zoezi hilo lilitupendeza sana na tukajikuta tukiendelea nalo, tulipokuja kuacha kila mmoja alikuwa snatabasamu. Tuliendelea na zoezi letu kwa mara ya pili huku nikivua shati langu na Sarina akivua nguo yake ya juu, tulijikuta tukibaki na nguo za ndani pekee na joto lilikuwa kali sana. Kupunguza joto ilinidi niende nikawashe feni la hapo ukumbini, upande ulipo feni ilibidi nimpe mgongo wakati naenda kuliwasha kwani swichi ya kuliwasha feni  ilikuwa upande huo, nilipopiga hatua mbili kwenda kwenye swichi Sarina aliona kitu kilichomfanya anifuate akiniambia nisimame kwanza. Aliponifikia alinishika katika ya mgongo huku akiniuliza, " Avez-vous déjà tricoter?(umewahi kushonwa?)", nilikataa akaniuliza juu ya alama ndogo ya mshono iliyopo mgongoni mwangu ambayo nilikuwa siijui.

*Moto unazidi kukolea


No comments:

Post a Comment