Sunday, November 22, 2015

DHAHAMA SEHEMU YA TANO

 DHAHAMA


MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGIN


SEHRMU YA TANO!!

Baada ya nusu saa za uchapaji kazi alianza kuhisi kubanwa na haja ndogo na ikambidi aende msalani kutokana na kushindwa kuvumilia kukaa katika hali hiyo, alifunga ofisi kisha akaingia katika maliwato ambayo ipo jirani na ofisi yako.  Aliingia moja kwa moja msalani akajisaidia kisha akatoka akiwa anapiga uruzi wa nyimbo anayoipenda akiwa na tabasamu pana usoni mwake, kama ilivyo kawaida yake huwa akitoka maliwatoni lazima aende kwenye kioo kipana chenye masinki yenye koki kadhaa za maji kwa chini yake ili anawe mikono. Alienda kwenye sinki hilo akafungua maji akanawa mikono kisha akanawa uso akiwa anapiga uruzi wa wimbo anaupenda unaoitwa this i promise you ulioimbwa na kundi la wanamuziki wa kimarekani liitwalo N-sync, akiendelea kupiga uruzi  huo ghafla taa za huko kwenye maliwato zikazima na kukawa giza kutokana na madirisha madogo yaliyomo humo kutopitisha mwanga vizuri.

*****

"shit! Yaani hawa Tanesco wanakera sana" Hussein alisema kutokana na umeme kuzimika humo maliwatoni, lawama zake zote alizielekeza kwenye kampuni ya usambazaji umeme nchini kutokana  na kuzimika kwa taa ya humo ndani. Hakuwa ametambua kama alikuwa anawabebesha lawama kwa wasiohusika na tatizo hilo, hakika hakujua kama kuna ugeni uliokuwa umemfikia na dalili yake ndiyo hiyo ya kuzimika kwa taa humo maliwatoni. Akiwa na uso  ulionekana kukerwa kabisa na tatizo hilo  taa ziliwaka tena akajikuta akitukana tusi zito halafu akainama ili anawe uso ingawa alisita baada ya kuhisi hayupo peke yake blali kuna mtu mwingine, aligeuza uso pembeni akamuona kijana mwenye asili ys uchotara wa kiarabu na mbantu akiwa ananawa uso wake tararibu bila hata kushughulika kumuangalia Hussein na wala haikujikana aliingia muda gani hapo.
"wewe umeingia saa ngapi hapa?" Hussein alimuuliza yule kijana, yule kijana aliposikia swali la Hussein aliacha kunawa kisha akajifuta uso wake halafu akamtazama kwa sekunde kadhaa.
"nimeingia muda si mrefu" Yule kijana alijibu kisha akafungua tena koki ya maji akaendelea kunawa, jibu hilo lilimchanganya zaidi Hussein na akajikuta akimshangaa sana yule kijana hadi akaanza kumuogopa kwani mlango haukuwa umefunguliwa kuashiria kama kuna mtu aliingia.
"Kwanza wewe ni nani mpaka uingie kwenye sehemu ambayo staff wa kawaida hawafiki?" Hussein alimuuliza yule kijana.
"mimi ni Zalabain ndiyo maana nimeingia humu na cheo changu ni prince ndiyo maana nipo humu" Yule kijana aliongea huku akitabasamu.
"unasemaje mbona sikuelewi na sikujui?" Hussein aliongea kutokana na kuchanganywa na maelezo ya yule kijana.
"utanielewa na utanijua" Yule kijana  aliongea na hapo ndani taa zikazimika tena na zikawaka, yule kijana sehemu aliyokuwepo awali hakuonekana kabisa na hapo ndipo Hussein alizidi kuingiwa na uoga. Alipoangalia kwenye kioo ambacho kilimuonesha upande wa nyuma yake ndiyo alizidi kuchanganyikiwa kwa alichokiona, alitaka kusoma dua ya kujikinga na viumbe waovu lakini mdomo wake ulikuwa mziti na haukufunguka kabisa kama amelishwa mawe. Alipogeuka ili aone vizuri kwa kudhani labda anaona maruweruwe tu ndipo akajikuta akipokea kofi zito lililompeleka hadi chini, alipoinua uso wake alikutana uso kwa uso na yule mtoto ambaye aliwatokea Hisan na Hamid muda mfupi kabla hawajaiaga dunia.
"Huna akili kweli yaani unataka kusoma dua chooni kisa umeniona mimi, toka lini jina la Muumba likatajwa chooni wewe na hata ungesoma unafikiri angekusaidia wakati muda unaingia chooni hukumkumbuka hata kidogo kwa kumuomba akulinde ukiwa humu" Yule mtoto aliongea huku akisikitika.
"sio mimi nisamehe" Hussein aliongea huku akitetemeka akiwa amekaa kitako kwenye sakafu ya  maliwatoni hapo.
"Heh! Kwanini siyo wewe, inamaana huitwi Hussein Buruhan mtoto wa tano wa mzee Buruhan" Yule mtoto alimuambia Hussein huku akionekana kushangaa kwa jinsi anavyoongea.
"ndiyo mimi Hussein" Hussein alijibu huku akitetemeka kwa uoga.
"basi kama wewe ndiyo Hussein basi ndiyo wewe" Yule Mtoto aliongea kwa hasira kisha akamsogelea Hussein kwa kasi sana na alipomfikia alimkaba kooni hadi akawa hawezi kupumua vizuri, alimnyanyua juu akambamiza kwenye kioo kikubwa kilichokuwa kipo humo ndani juu ya masinki ya kunawia. Hussein alikatwa na vipande vya vioo na akajikuta akipiga kelele za kuomba msaada huku akimtaja mama yake kama ilivyo watu wengi wakiwa katika matatizo, kelele hizo hazikusaidia chochote kwani kipigo kiliendelea kama kawaida na alizidi kumtaja mama yake.
"Watu kama nyinyi ndiyo mungu hawasaidii hata kidogo, yaani unamkumbuka mama yako kwenye shida halafu unamsahau Mungu wako anayekupa pumzi hizo zinazokutia jeuri. Haya nipe upesi" Yule mtoto alimuambia Hussein.
"si.....sina" Hussein aliongea kwa tabu kutokana maumivu ya kipigo alichokipata.
"ohoo! Huna, basi utaenda kuonana na kaka yako Hamid huko roho yake ilipo" Yule mtoto aliongea kisha akajizungusha kama pia hadi kikatokea kimbunga kilichomzoa Hussein akawa yupo katikati, milio ya makofi ndiyo ilifuatia akiwa yupo humo ndani ya kimbunga hicho na makelele ya maumivu yakawa yanasikika. Kimbunga hicho kilipokuja kuisha Hussen alitupwa chini akiwa amevunjika sehemu mbalimbali za mwili wake, Yule mtoto bado alikuwepo na safari hii alikuwa yupo karibu yake zaidi na mkono wake wa kushoto ukiwa umekamata koo la Hussein.
"salamu zao kwa waliotangulia kabla yako" Yule mtoto aliongea kisha akalivuta koromeo la Hussein hadi akalitoa nje kiaha akalivunja akautoa mfupa wake akauweka pembeni, Hussein tayari alikuwa amekwisha maliza mkataba wake wa kuishi duniani hadi muda huo akiwa miongoni waaiokuwepo duniani kimwili.

****


   KITUO CHA POLISI CHUMBAGENI
                  TANGA


Baada ya yule mama kuvamia mwili wa yule mwanaume aliyekutwa  kwenye majani amekufa katika ajali ya gari ya Hamid, yule Inspekta aliamuru yule mama awekwe chini ya ulinzi kwa mahojiano zaidi na alipelekwa kituo cha polisi Chumbageni kusubiri Inspekta arudi ili afanye mahojiano naye. Inspekta yule aliporudi kituoni baada ya kumaliza kusimamia kazi kule barabarani yule mwanamke aliingiza kwenye chumba cha mahojiano, yule inspekta aliingia katika chumba cha mahojiano akiwa na maaskari waliokuwa wadogo kivyeo.
Naitwa Inspekta Ismail Mdoe, kulia kwangu yupo Sajenti Juma Shehoza na kushoto kwangu kuna Staff sajenti Dickson Mushi, sijui mama unaitwa nani?" Yule Inspekta ambaye ndiye Inspekta Mdoe aliongea huku akitoa utambulisho kwa wenzake.
"naitwa Mwanamkuu Jumanne" Yule mwanamke alijibu kwa unyonge.
"Ok Bi Mwanamkuu  una umri gani, unafanya kazi gani na unaishi wapi?" Inspekta Mdoe alimuuliza.
"nina miaka 48 nafanya biashara ndogondogo, ninaishi hapahapa Chumbageni" Bi Mwanamkuu alijibu kwa unyonge, muda huo Sajenti Shehoza alikuwa akiandika  kila kilichokuwa kinafanyika kwenye mahojiano hayo.
"wewe na marehemu mna uhusiano gani?" Inspekta Mdoe aliuliza.
"Marehemu ni mume wangu" Bi Mwanamkuu alijibu.
"ok, unaweza ukatuambia kilichokufanya utamke yale maneno kwenye eneo la ajali?"  Inspekta Mdoe alimuuliza.
"afande chanzo cha kutamka maneno yale ni kutokana na mume wangu kuingilia mambo yasiyomuhusu na hatimaye akauawa" Bi  Mwanamkuu alizidi kuongea na safari machozi yalikuwa yakimtoka.
"una uhakika gani na hayo unayoyasema? Hebu fafanua kauli yako" Staff sajenti Mushi alimuuliza kwa mara ya kwanza.
"muda mfupi kabla mume wangu alikuwa akiendelea na kazi zake za uganga, alipandisha maruhani yake akasema kuna mtu yupo hatarini kuuawa hivyo anahitaji kumsaidia. Akichukua vifaa vyake vya uganga akaenda huko, na sikumuona tena hadi niliona mnambeba" Bi Mwanamkuu aliongea huku akilia, maelezo hayo yaliwafanya maaskari hao waliokuwa wanamuhoji watazamane kwa muda wa sekunde kadhaa.
"Mama usituletee maelezo yasiyokuwa na uthibitisho wowote" Inspekta Mdoe aliongea akionesha kuchanganywa na maelezo aliyoambiwa.
"Afande hii siyo kiwango chenu naomba muiache na huyu mbaya wangu aliyeniulia mume wangu nitamkomesha" Bi Mwanamkuu aliongea kwa hasira kisha akaanza kuangaza pande zote za humo, alianza kunguruma kama simba akiashiria mashetani yamempanda. Maaskari  waliokuwa wanaomuhoji walibaki wakimtazama tu wakionekana kuwa hofu nae, Bi Mwanamkuu aliposimama akionekana ana hasira kimbunga kizito kiliibuka humo ofisini kikamzoa  na kilipotoweka naye alitoweka papo hapo.

****

Mfanyakazi wa kampuni ya Matro anayehusika na usafishaji vyoo  na korido katika ghorofa la kampuni hiyo alianza kufanya kazi kama ilivyokuwa kawaida yake, alianza kufanyakazi katika ghorofa tofauti na mwishowe akamalizia katika ghorofa ya mwisho ambayo ndiyo inapatikana ofisi ya mmiliki wa kampuni hiyo. Kijana huyo anayeitwa Niko alianza kusafisha korido mbalimbali za ghorofa hiyo na hatimaye zamu ya kusafisha maliwato za ghorofa hiyo ya mwisho ikaanza, alianza kwa kusafisha maliwato ndogo na hatimaye akahamia kwenye maliwato kubwa ambayo ipo jirani na ofisi ya mmiliki wa kampuni hiyo. Akiwa na kotoroli chenye vifaa ambacho alikiburuza hadi katika mlango wa maliwato hiyo kisha akaupa mlango mgongo akawa anakiburuza kitoroli ili aingie nacho ndani akiwa ameufungua mlango kwa kuusukuma na mgongo wake. Alifanikiwa kuingiza kitoroli hadi ndani akiwa anaimba kwa kuchangamka akiwa ameungalia mlango na ameipa mgongo sehemu ya ndani ya maliwato hiyo, akichukua fagio lenye nyuzi maalum kwa kufanyia  usafi akaanza kufanya usafi kuanzia mlangoni na sehemu za pembeni ya mlango. Baada ya kumaliza kufanya usafi maeneo hayo ndipo alipogeuka nyuma ili aendelee na usafi akakutana na hali isiyopendeza kutazamwa. aliuona mwili wa bosi wake mkuu ukiwa upo chini na koromeo lipo pembeni ya mwili huo. Niko alijikuta akitoa ukelelewa uoga kisha akakimbia kuelekea mlangoni, aliponyeza kitufe cha kengele ya hatari ya ghorofa kisha akakaa kitako akawa kama mtu asiyejielewa kabisa.

  Mlio wa kengele ya hatari katika jengo lote ulisikika na kupelekea kundi kubwa la wafanyakazi litoke nje ili kuchukua tahadhari kama kuna uwepo wa jambo la hatari,  walinzi wa kampuni wenye silaha wakaanza kupandisha wakiwa na tahadhari kubwa kwani kengele hiyo ilimaanisha jambo la hatari. Walinzi hao walipita kwenye ghorofa mbalimbali kwa tahadhari na hatimaye wakafika ghorofa ya mwisho, walitembea kwa tahadhari katika ghorofa hiyo hadi walipomuona Niko wakamfuata huku wengine wakiwa wanaangalia usalama. Walipomfikia Niko aliishia kuonesha kidole ndani ya maliwato ndipo maaskari hao walipoingia huku wengine wakimuuliza maswali ambayo hakuyajibu zaidi ya kutetemeka. Walinzi walioingia waliwaita wenzao wakajionea kilichotokea humo ndani ya maliwato, simu ilipigwa haraka kituo cha polisi ambapo polisi walifika ndani ya muda mfupi tu wakajionea hali halisi na wakachukua vipimo mbalimbali pamoja na kuuchukua mwili wa Hussein.

****

    Maeneo hayohayo ya Raskazoni kwa upande mwingine kulikuwa kuna mzee wa makamo aliyekuwa akiangalia luninga sebuleni, alikuwa ni mzee wa miaka takribani hamsini na ushee ingawa alionekana kutozeeka sana. Wakati mwili wa Hussein ukiwa umeondolewa kule kazini na ukiwa tayari umeshafikiishwa hospitali ili kuhifadhiwa, mzee huyu aitwae Shafii Buruhan alipigiwa simu na alipoipokea na akasikia  alichokisikia alizidi kuchanganyikiwa  na akabaki akilia kwa sauti kama mtoto mdogo hadi mkewe akaja sebuleni akamuona mume wake akiwa katika hali hiyo.
"Baba Zayina kuna nini?" Mke wake aliimuuliza baada ya kumkuta akiwa analia kama mtoto.
"wadogo zangu Hamid na Hussein mama Zayina" Shafiu alijibu huku akilia kwa kushindwa kustahimili jambo aliloambiwa.
"wamefanyaje tena?" Mke wake aliuliza akionekana kutoelewa.
"hatunao tena duniani, wadogo zangu mimi jamaniii" Shafii alijibu huku akilakamika na mke wake akaanza kumbembeleza huku yeye mwenyewe akilia baada ya kusikia mashemeji zake wamefariki. Shafii alilia sana kama mtoto mdogo kutokana na vifo hivyo, mkewe naye alikuwa ana kazi ya kumbembeleza ingawa hata yeye alikuwa akitokwa na machozi.
"Baba Zayina jikaze wewe ni mwanaume" Mke wake alimwambia huku akimfuta machozi, muda huo mlango wa hapo sebuleni ukafunguliwa na akaingia mwaume alivaa kinadhifu.
"Ally mdogo wangu" Shafii akimuita yule mwanaume kwa jina lake halisi.
"Kaka kuna nini mbona unalia" Allu alimuuliza kaka yake.
"kaka zako  Hamid na Hussein hatunao" Shafii aliongea kwa huzuni huku akitokwa na machozi, Ally aliposikia taarifa hiyo alijikuta akikaa chini kisha machozi yakaanza kumtoka ingawa hakutoa sauti kuashiria analia.
"Ally jikaze twende hospitali tunahitajika" Shafii aliongea akinyanyuka macho yakiwa mekundu kwa kulia, aliingia ndani halafu akarejea akiwa amevaa viatu na miwani ya jua ili kuficha macho yake.
"Farida sisi tunatoka, wewe baki. Ally twende" Shafii alisema huku akimnyanyua, kisha wakaondoka hadi nje.

***-

Taarifa ya kifo cha mmiliki wa kampuni ya Matro tayari zilishawafikia waandidhi wa habari na hadi anafikishwa katika chumba cha kuhifadhi maiti tayari waandishi wa habari walikuwa wamejaa nje ya chumba hicho wakisubiri kupata habari kamili. Hadi gari aina ya Cadillac la milango sita linawasili jirani na mlango wa chumba cha kuhifadhia maiti bado waandishi wa habari walikuwa wamejazana eneo hilo, dereva wa cadillac hilo aliposhuka kwenda kufungua mlango  waandishi  wa habari walikuwa wapo makini kujua anayeshuka katika gari hilo la gharama ni nani. Shafii alipotangulia kushuka kamera mbalimbali za waandishi wa habari zilikuwa zikifanya kazi ya kumpiga picha tu, waandishi wa habari walikimbilia kumuuliza maswali mbalimbali lakini hawakupata ushirikiano.
Shafii aliingia ndani ya sehemu ya kuhifadhia maiti akiwa na Ally na alipita hadi ofisini ndani ya ofisi hiyo ya chumba cha kuhifadhia maiti alimkuta msimamizi wake akiwa amekaa kwenye kiti akipitia mafaili mbalimbali.
"karibu mzee" Msimamizi wa hicho chumba alimkaribisha.
"Asante" Shafii aliitikia huku akivua miwani  ya jua akafuta machozi.
"pole sana mzee wangu kwa masaibu haya" Msimamizi alimpa pole.
"asante sana, nakusikiliza" Shafii alisema.
"Ok nifuateni" Msimamizi aliongea kisha akainuka akaingia ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti, Shafii na Ally nao walimfuata kwa nyuma. Yule msimamizi alielekea sehemu yenye mitoto mingi kama ya meza au kabati akiwa anatafuta namba maalum hadi akazifikia namba za mitoto ya makabati ya jokofu ya kuhifadhia maiti yanayofuatana, alifungua mojawapo kisha akafungua lailoni lenye zipu akamuonesha Shafii ambapo aliuona mwili wa mdogo Hussein ukiwa hauna koo. Shafii aliutazama mwili ule kwa umakini huku machozi yakimtoka kisha akamuamuru yule msimamizi afungue jingine, jingine lilipofunguliwa aliuona mwili wa mdogo wake Hamid ukiwa umeharibika kutokana na ajali aliyoipata.
"hapa kuna mkono wa mtu nasema sikubali" Shafii aliongea kwa hasira.
"ndiyo maana mzee nikakuita uje kujionea mwenyewe ili uwahi kwa babu kule" Msimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti alimuambia.
"ok nashukuru ngoja niende kwa babu yako kabla mambo hayajawa mabaya" Shafii aliongea huku akimpa burunguru la pesa yule msimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti halafu akaondoka huku Ally akiwa anamfuata, walipotoka nje Shafii alimuambia mdogo wake "Ally wewe nenda ukampe taarifa shemeji Hamisi na wengine juu ya vifo hivi, mimi naenda kwa Mtaalamu Sauti ya radi kule Amboni".
Shafii aliingia ndani ya gari na dereva akaondoa gari, Ally alichukua teksi naye akaondoka.


****

Safari ya Shafii iliishia Amboni kwa mganga wake ambaye ndiye babu yake yule msimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti Bombo, gari yake ilisimama kwenye umbali mrefu kutoka pale yalipo makazi ya mganga huyo kwenye pori dogo lililopo karibu sana na mto Zigi. Shafii alishuka akatembea kwa mguu hadi kwenye kibanda cha mganga Sauti ya Radi kisha akabisha hodi huku akivua viatu vyake, alipopewa ukaribisho aliingia ndani akaketi kwenye jamvi kuukuu mbele ya vibuyu vya mganga.
"Karibu Shafii mwana Buruhan" Mganga Sauti ya radi alimkaribisha Shafii kwa mara ya pili, Shafii aliitikia ukaribisho huo  kisha akaeleza kila kitu kwa mganga.
"hakuna kinachoshindikana hapa mbele ya  sauti ya radi nikinguruma natoa miale maadui wanashindwa wenyewe, kuna kiumbe anakuandama na leo ndiyo kiama chake" Mganga  Sauti ya radi aliongea kwa msjigambo kisha akanyanyuka akatoka nje, alirejea akiwa na moto kidogo kwenye chombo kinachotumika kuwekea ubani. Alikiweka kile chombo  mbele ya Shafii kisha akamwaga dawa zake kwenye moto uliomo kwenye chombo hicho, moshi mzito ulitanda humo ndani na mzee Sauti ya radi akawa anaimba nyimbo zisizoeleweka huku akimzunguka Shafii akicheza kama anacheza ngoma ya kikabila. Moshi huo ulipokuja kupungua Mganga akiendelea kucheza alihisi anashikwa kiuno wakati akicheza, moshi ulipoisha alihisi anashikwa makalio kwa kutomaswa. Alipogeula nyuma kumuangalia anayemshika alikutana uso kwa uso na Zalabain akiwa anatabasamu.
"Yaani ungekuwa mwanamke ungefaa kucheza Baikoko kwa jinsi inavyojua kukata kiuno" Zalabain aliongea akiwa bado hajatoa mikono kwenye makalio ya Mganga Sauti ya radi.


*Mganga kashikwa mhh!
*balaa linaendelea



No comments:

Post a Comment