Monday, February 13, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA KUMI NA MOJA




WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com




SEHEMU YA KUNI NA MOJA!!
  Hakujua kabisa kuwa huyo aliyekuwa naye alikuwa yupo hapo kwasababu maalum, yeye alichokuwa akiwaza ni penzi tu kutokana na kuchangamshwa sana na kilevi alichokuwa akikitumia. Hitaji ya kutengeneza nishati katika mwili nalo lilimfanya kijogoo aweze, yalikuwa ni majibizano ya kimapasho ya miili.

"Mamba na windo meno ndiyo huongea" Norbert alijisemea moyoni.






_______TIRIRIKA NAYO

  Aipomaliza kutoa kauli hiyo kwa haraka sana alishambulia shingo ya binti huyo aliyekuwa yupo kwenye hali ya kilevi, aliishambulia kwa kutumia ulimi na kuzidi kumchanganya kabisa hadi akawa ni mwenye kukishilia kichwa chake na na kuanza kufanya kama anakichana kwa kucha zake ndefu za kike. Binti huyo alizidi kunogewa kabisa na mtindo huo aliokuwa akiufanya  hadi akajikuta akihema akijigeleza zaidi muda huo waliokuwa wamesimama na kupelekea, mambo yalipozidi jambo aliishia kutamka neno Norbert kwa kila muda kwa jinsi alivyokutana na mtu ambaye alikuwa akijua kuutumia ulimi ipasavyo nje ya matumizi yake ambayo yalikuwa yameumbiwa. Ilikuwa ni kitendo hiko tu ambacho kilimfanya hadi ajihisi hakuna na nguvu kabisa mwilini, kilipokuja kusitishwa alijikuta akishikiliwa kichwa chake asiache kufanya zoezi hilo.

  Ilikuwa ni kama makusudi kwani kidume hiki hakikushusha kichwa chake shingoni,  badala yake alibadili mtindo na kuzidi kumfanya ajione kuwa alikuwa akikaribia kukosa burudani kama angeendelea kukazania kilekile. Muda mfupi baadaye Cellina hata hakujielwa alikuwa ametolewa muda gani vizuizi kwani, huo wote ulikuwa utundu wa Mzee wa toto katika kumfanya awe kichaa kabisa kwa mambo aliyokuwa akiyafanya. Alikuja kujihisi akiongezekewa na nyuzijoto mwilini mwake  baada ya kukutana na ngozi kama yake, hapo alijikuta akiwa anakuwa kichaa kabisa  kwa kupagawa na ubunifu adimu aliokuwa akipewa. Ilichukua saa kadhaa akiwa yupo juu ya ubunifu huo huku bado kilevi kikiwa kipo kichwani, alipokuja kuchoshwa zaidi mwili wake alijikuta akipitiwa na usingizi akiwa amelala juu ya kifua cha huyu Mamba asiyeacha windo hata kama angekumbwa na shibe.




                  [8]
  Asubuhi na mapema ndipo Cellina alipokuja kuamka akajikuta akiwa yupo kifuani, alipofumbua macho tu alikutana na macho yaliyokuwa yakimtazama usoni ambapo alijikuta akitabasamu tu mwenyewe. Alijikuta akimbusu kwenye papi zake za mdomo na kisha akampa salamu ya asubuhi hiyo, ilikuwa ni ndani ya siku ya alhamisi ambapo ilikuwa ni siku ya kazi katika subuhi hiyo mapema sana.

"Vipi umeamkaje?" Cellina aliuliza

"Nimemka fiti sana hadi naona uvivu kwenda job" Norbert alijibu na kusababisha Cellina acheke sana

"Huyooo muone vile uamke fit ushindwe kwenda job, si mzima wewe"

"Kweli vile mimi ufit wangu ukizidi nashindwa hata kwenda job yaani sijui kwako wewe hapo"

"Mimi nikiwa fit ndiyo naenda job kabisa"

"Vipi ukitega?"

"Wee kuna mkurugenzi mkuu pale ukitega umekwisha yaani kazi huna"

"Mmmh! Mkurugenzi mkuu huyo wa jinsia gani asiyejua ufiti ukizidi kupitiliza mtu hubidi kupumzika"

"Ni mdada mmoja huyo tunamjua kwa jina la Madam ana msaidizi wake mzungu wakali hao balaa"

"Wakali wana meno ya simba nini wachovu tu"

"Ngoja nikuonesha uwaone tulipiga nao picha ya pamoja ya ofisi wapo kikazi muda wote sura zao" Cellina alipoongea hivyo alijitoa kifuani mwa kidume cha mbegu na kisha akajisogeza kivivu hadi upande ambao aliiona pochi ya makwapani, alitoa simu yake ya kisasa kwenye ile pochi na kisha akafungua baadhi ya mafaili akamuonesha picha ya huyo aliyemtaja bosi wake.


 Norbert alivutika zaidi na picha hiyo na akajikuta akiitazama kwa umakini sana, baada ya hapo aliachia tabasamu lake lililokuwa likificha kila kitu chake ambacho alikuwa hataki kabisa kijulikana na kumbe wa kawaida. Aliitazama picha hiyo kwa mara ya pili ambapo alijionea mwenyewe kuwa watu hao aliokuwa ametajiwa kama wakuu wa Cellina walikuwa ni watu ambao alikuwa akiwafahamu undani wao kabisa, walikuwa ni watu ambao walikuwa  na zaidi ya jambo kwa uwepo wao ndani ya jiji hili. Walikuwa ni watu ambao alijipa akili nyingine ya ghafla ya kuweza kufuatilia miendenendo yao, walikuwa ni viumbe ambao alikutana katika mazingira tofauti kabisa. Walikuwa binadamu wa jozi moja ambao alikuwa akiwindana kila akionana nao. Hapo alibaini kuwa kulikuwa na uhusiano mkubwa sana kati ya watu hao na yule  Kelvin ambaye alikumbana naye kule Yombo.

"Josepine na Scorpio wapo jijini, nahisi hata kutaka kuuawa Buguruni ni kazi ya mokono wao au wametuma kijana wao" Norbert alijisemea ndani ya moyo wake kisha akamtupia jicho kwa tabasamu Cellina

"Umewaona mabosi zangu hao wakali balaa yaani, inabidi tu leo niende job ingawa nimechoka sana kazi yako si ndogo"

"Mmmh! Watu wenyewe wachovu hao wana mikwara mbuzi tu  yaani mimi ningekuwa na mabosi kama hao wala sitishiki ndiyo kwanza ningewaendesha tu"


"Wee unasema tu unafikiri kazi siitaki hasa yule Madam ni katili balaa, kuna mwenzangu huyo alitaka kufukuzwa kazi na yule MZungu ila alirudishwa kihongo tu"

"Hee kihongo kivipi?"

"Kalala na mzungu yule alipoambiwa hivyo kwa sharti la kurudi kazini, hakuna na kazi nyingine kwa taaluma yake itakayomlipa zaidi ya hiyo. Alipofikiria kuwa alikuwa akikaribia kwenda kuingia kwenye gereji bubu mtaani zisizolipa ilimbidi tu atii matakwa kwani hakuwa na wa kumshtakia"

"Kumbe ndiyo tabia zake huyo jamaa anaonekana mpole"

"Yaani acha tu ni mhuni huyo balaa na hafai"

"Haya hapo ujanja kabisa tena muda unaenda tujiandae nikakushushe kazini kwako"

  Wote kwa pamoja waliingia ndani ya bafu la kisasa lilipo humo ndani ya chumba hicho na kusafisha miiili yao, walipotoka tu nje ya chumba hicho walikimnbilia kujiweka sawa  kimavazi kama walivyokuwa wameingia ndani ya hoteli hiyo jana yake. Cellina alijipamba kama kawaida kutokana na kuwa vipodozi kwenye mkoba wake kama ilivo hulka ya baadhi ya wasichana kutembea na vipodozi mkobani. Baada ya hapo wote kwa pamoja walitoka hadi nje ambako aliiingia kwenye gari jingine kabisa alilokuwa amekuja nalo usiku uliopita Norbert, waliondoka kwenye hoteli hiyo huku Cellin akiwa hatambui kama alikuwa amegawa madini adimu sana kwa kidume huyo bila malipo yeyote yale. Hakujua kabisa kile ambacho alikuwa akikiongea mule ndani kilikuwa kina thamani gani kwa huyo aliyetoka kutumia naye kitanda kimoja, kuweza kupagawawishwa ndani ya usiku mmoja tu alijikuta akitoa ambayo yalikuwa hayatakiwi kutolewa kabisa pasipo kutambua kuwa alikuwa akifanya kosa kubwa sana. Aliona alikuwa amepatwa mwanaume ambaye alikuwa mwenye mvuto hata akitoka naye watu watamsifia kuwa ana mwanaume pasipo kutambua kuwa alikuwa akigawa ramani ya vita kwa adui bila kujitambua, muda huo waliokuwa wapo ndani ya gari kuelekea huko ofisini kwake alikuwa akimtazama sana Noebert kama alikuwa anamuona kwa mara ya kwanza. Kila alipokuwa akifikira sana kile ambacho alikuwa amefanyiwa usiku ulipita alikuwa hamalizi kumtazama, ingawa alikuwa na ulevi bado aliweza kuipata burudani iliyokuwa ikitolewa ndani ya kumbi wa mraba ambao walikuwa yeye na mburudihaji wake. Hakuwa akiwaza kabisa kuwa alikuwa ameuza udhaifu wa bosi wake kwa adui wa bosi yake ambaye alikuwa akitaka sana kuuufahamu na pia alikuwa amewaanika mabosi zake kwa mtu ambaye alikuwa ana uhasama nao na kumfanya atambue kuwa watu hao walikuwa wapo ndani ya jiji hilo. Iliwachukua robo sa tu wakawa wamefika eneo la  Buguruni Rozana ambapo ndiyo kilikuwa kituo cha mwisho cha safari ya Cellina, hapo aliagana na Norbert kwa mabusu motomoto na kisha akaelekea kazini kwake.


    Hapo ndipo Norbert alipoondoa gari na kuelekea yalipo makutano ya  barabara ya Chama, aliingia kwenye barabara ya Mandela alipofikia kwenye eneo hilo kuelekea upande ilipo Ubungo. Baada ya robo saa nyingine alikuwa yupo eneo la Ubungo kwenye makutano wa barabara tatu tofauti ambazo ni barabara ya Morogoro,Sam Nujoma na Mandela. Hapo aliingia kwenye barabra ya Morogoro kwenye upande ambao ilikuwa ikitoka nje ya jiji la Dar es salaam, aliendesha kwa muda wa robo saa nyingine kutokana na msongamano wa daladala akawa amefika Mbezi ambapo aliingia kwenye barabara ya vumbi iliyokuwa ikielekea Mbezi Luxury, Muda huo wote alikuwa na akifuata ramani maalum iliyokuwa ipo ndani yz gari yake ambayo ilikuwa ikimuelekeza mahali pa kwenda. Alifanikiwa kufika hadi maeneo hayo ya Mbezi Luxury kisha akaelekea hadi mwisho wa maelekezo yake, safari yake iliishia kwenye lango la nyumba moja ya kisasa zaidi ambako alipiga honi  alipofika hapo. Lango dogo la eneo hilo lilifunguliwa na kisha Mlinzi aliyekuwa amevalia sare  maalum alitokea na alienda kwenye gari lake akagonga kioo, Norbert alishusha kioo cha gari lake na kisha akampa tabsamu huyo Mlinzi.

"Ndiyo mzee" Mlinzi aliongea

"Kaboneka nimemkuta?" Aliuliza

"Kabisa umemkuta nimuambie nani?"

"Muambie Kaila, Norbert Kaila yupo nje hapa anihitaji kuonana naye kikazi zaidi"

"Ok mzee subiri dakika moja" Mlinzi huyo alipoongea hivyo alikimbia akaelekea ndani ya lango hilo, huko alitulia kwa kipindi kifupi cha muda tofauti ilivyokuwa dakika moja aliyokuwa ameizungumza. Hiyo ilikuwa ni kawaida ya waswahili na wenyewe kwa wenyewe walikuwa wamezoeana kwa ahadi zisizo na muda, Norbert aliendelea kusubiri kwa muda mfupi ambako lango kubwa la Magari lilifunguliwa na kisha akaingiza gari ndani moja kwa moja. Alielekezwa eneo maalum la kuegesha gari na kisha akaenda kuegesha kwenye eneo hilo, baada ya hapo alilizima gari na kisha akashuka na kuingia ndani ya nyumba  kwa msaada wa maelekezo ya Mlinzi.


****


   Muda ambao Norbert alikuwa yupo ndani ya  gari akiwa anelekea kwenye makutano ya barabara ya Chama maeneo ya Buguruni, kijana mwingine aliyekuwa yupo chini ya kina SCorpio alikuwa yupo ndani ya gari dogo aina ya Lexus yenye muundo wa altezza mbayo ilikuwa ni tofauti kabisa na ile ambayo walikuwa akiendesha kina Scorpio walipojaribu kumuua adui yao. Mtu huyu naye alikuwa akielekea eneo ambalo alikuwa ameelekea Norbert akiwa na lengo moja tu la kwenda kuchukua kile ambacho alikuwa amekifuata Norbert. Kaboneka alikuwa ni mdogo wa mmoja wa wanausalama ambaye alikuwa  na Tarakilishi ambayo ilikuwa na siri kubwa ndani yake, hivyo yeye alikuwa amegizwa kwenda kuichukua isije ikafikia mahala pabaya. Hakutambua kabisa kuwa huko alipokuwa akienda kulikuwa na mwingne kabisa ambaye alikuwa amemtangulia katika kuhakikisha kuwa alikuwa akiichukua tarakilishi, gari hiyo ilikuwa ipo kwenye barabara ya Nyerere ikiwa inatoka upande ambako Kariakoo ipo kuelekea huko alipokuwa akienda adui yake mkubwa waliyekuwa wakigombania naye kitu kimoja.



  Muda mabo Norbert anawasili ndani ya eneo la nyumba ya Kaboneka, mtu huyo alikuwa yupo kwenye njia ya vumbi iliyokuwa ikielekea huko, alipofika eneo la jirani ya uzio wa nyumba hiyo alisimamisha garii lake na hakutaka kabisa aonekane kama alikuwa ni mtumiaji wa gari hilo kipindi anaingia ndani ya nyumba hiyo.  Baada ya hapo aliruka uzio wa nyumba hiyo akatokea ndani, akiwa na umakini wa hali ya juu alienda hadi eneo ambalo kulikuwa na kibanda cha Mlinzi na kisha akagonga mlango wa kibanda hiko. Mlinzi wa nyumba hiyo ambaye alikuwa hajui chochote alikutana na pigo la kijasusi ambalo hupigwa kama kofi shingoni, pigo hilo lilimpa usngizi wa lazima ambAye yeye hakutarajia kabisa kama angeulala na kisha mtu huyo aliingia ndani ya kibanda hiko akamkalisha kwenye kiti. Baada ya  alimuweka kwenye kiti na kumlaza kiwiliwili chake juu ya meza yake, alimalizia kwa kuitoa bahasha moja nyeupe ambayo aliiweka jirani na meza hiyo kisha akatoka humo ndani na kurudishia mlango. Baada ya hapo alitoka moja kwa moja na akaenda kwenye hadi kwenye baraza la nyumba kubwa ya kisasa ambayo ilikuwa ipo humo ndani, aliingia ndani ya baraza la nyumba hiyo na kisha akausogelea mlango ambao ndiyo ulikuwa ni sehemu itakayomuwezesha kuingia ndani ya nyumba hiyo.


****


  Norbert baada ya kuingia ndani ya  nyumba hiyo alipokea ukaribisho kutoka kwa mtu ambaye alikuwa akija kumuona ndani ya muda huo, alikuwa ni Kaboneka mwenyewe ambaye alikuwa ni mtu mzima wa makamo. Alimkaribisha hadi ilipo sebule ya nyumba yake ya kisasa ambako waliketi naye kwenye kochi hilo, Kaboneka alikuwa ni mtu ambaye alikuwa akifahamu vyema harakati za Norbert akiwa yupo kwenye kazi zake kama mwandishi. Alikuwa ni mwandishi ambaye alikuwa akimuhusudu sana kwani ni yeye ambaye alikuwa amefanikisha kufichuliwa kwa maovu mengi ndani ya serikali kwa kutumia makala zake kwenye jarida ambalo lilikuwa likitoka katika kila baada ya miezi sita au kukiwa na jambo muhimu sana ambalo jamii ilikuwa ikipaswa kulifahamu. Uhodari wake katika kuelezea makala tofauti ulimfanya aingiwe na furaha kabisa kwa kuweza kuonana na mwandishi mwenyewe ambaye inasemekana ni mwenye akili ya hali ya juu kiasi cha kushindwa kuwekwa mikononi na wabaya wake, mtu huyo aliyekuwa akimuhusudu alikuwayupo hapo mbele yakea akiwa amekuja kiofisi kuonana naye hivyo alijikuta kifarijika sana.

  Kabla hata hajaanza kuzungmza naye kitu ambacho kilichokuwa kimeleta ndani ya eneo hilo alichukua simu ya kisasa kabisa na kisha akaomba kupiga naye picha ya pamoja, hilo lilikuwa ni jambo ambalo halikupigwa na Norbert kwani aliona alikuwa ni kiasi gani alikuwa amekubalika na mwenyeji wake. Alikubali kupiga naye pichana kisha akakaa kwenye kochi ili aweze kuongea naye.

"Karibu sana Bwana Kaila ni faraja sana kuweza kunitembelea ndani ya nyumba yangu  nahisi ujio wake una zaidi ya jambo" Kaboneka aliongea

"Hakika Mar Kaboneka ujio wangu wa kiofisi ndani ya nyumba hii una zaidi ya jambo nafikiri  wewe ndiyo mdogo wake Marehemu Lutonja kaboneka" Norbert aliongea

"Hakika ndiyo mimi kabisa"

"Katika utafiti wangu wa uandishi wa jarida ambalo lipo mbioni kutoka ndani ya majuma mawili yajayo,umeonesha kuwa wewe ni mmoja kati ya watu wanaoweza kunisadia niweze kupata kile ambacho kingeweza kuioko nchi hii"

"Ndiyo Kaila"

"Uchunguzi wangu wa awali ambao umetaka kunigharimu maisha yangu umebaini kuwa kuna laptop tano ambazo zilikuwa zimehifadhiwa siri kubwa sana na ya maneno ambayo yalikuwa ni neno siri ya kutambua mahali lilipo faili lenye utafiti mzima uliofanywa ambao ulitakiwa kuwasilishwa bungeni na Mheshimiwa Bai" Norbert alipoeka kituo hapo aliona mwenyeji wake alikuwa akimsikiliza kwa umakini kabisa.

"Moja kati ya hizo laptop ishaingia kwenye mikono yangu na ipo mikononi mwa mwanausalama wa EASA ajulikanae kama N001 ambaye alikuwa akihitaji kwa kazi yake. Moja imechukuliwa na wasiojulikana bado naisaka nipo radhi nife ila ukweli ujulikane  na moja unayo wewe, hivyo ujio wangu ndani ya eneo hili ni kuhusu hiyo Laptop nilikuwa nikihitaji yenyewe au neno muhimu lililopo" Norbert aliendelea kuongea na alipoweka kituo tu mlango wa mbele wa nyumba hiyo uligongwa mara mbili, kugongwa huk nkwa malngo huo kulitoa sauti ya kuwa ulikuwa umegongwa na kitu kigumu. Kiutambuzi kabisa wa kugongwa kwa namna hiyo Norbert aliweza kutambua kuwa aliyegonga mlango huo alikuwa ni mwenye mkono uliokomaa sana, alijua kabisa mgongaji wa mlango huo hakuwa yule Mlinzi bali kulikuwa na mtu wa ziada.

"Aaargh! Yaani huyu mlinzi badala apige simu kunipa taarifa anakuja kugonga mlango" Kaboneka alinyanyuka na akiwa anaenda kufungua mlango

"Mr Kaboneka wait" Norbert alimsimisha kisha akaongea kwa sauti ya chini, "Kama mlinzi alikuwa na utaraibu uliomuwekea nakuomba usifunue mlango na unisikilize mimi kwani huyo anayegonga mlango hakika siyo mlinzi"

*BABA WA AKILI NYINGI NAYE




ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment