Friday, February 3, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA PILI



WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com




SEHEMU YA PILI!!
Utulivu humuingia akipokea simu  kutokana na kupokea simu ambazo huwa na taarifa tofauti kwa kipindi tofauti cha muda hivyo umakini ulikuwa unahitajika sana zaidi hata ya atembeavyo eneno lenye vumbi kulinda macho yake yasiathiriwe, alitulia kabisa na sikio lake moja ndiyo likawa linafanya kazi zaidi kuliko jingine katika kusikiliza taarifa hiyo.

"Jambooo" Aliitikia baada ya kusikia salamu ya kiaskari kutoka upande wa pili wa simu .

"Unasemaa!" Aliongea kwa mshangao mkubwa baada ya kupokea taarifa  kutoka kwa mwanausalama aliyempigia simu.






_____________TIRIRIKA NAYO

    Uwezo mkubwa na upana wa njia za mawasiliano ilisababisha habari mbili tofauti zilizotokea kwenye sehemu tofauti kusambaa kwa kasi sana mithili ya moto wa kifuu hadi zikafika sehemu mbalimbali za nchi hii, polisi nao ambao waliokuwa hawana uaminifu katika kazi yao walivujisha tarifa hii mapema sana kwa watu  wao wa karibu na kupelekea taarifa hii isambae kwa muda mfupi kwa kila mtu. Taarifa hiyo ndiyo ilikuwa imefika kwa IGP Mbwambo ndani ya muda ambao watu wa kawaida tayari ilikuwa imshawafikia, ilikuwa ni taarifa yenye kushtusha sana hasa kwa kuzingatia  watu hao waliouawa ni watu walikuwa ni wazito sana ndani ya serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Watu waliokuwa na jina kubwa na wenye vyeo vikubwa katika sehemu tofauti ndani ya serikali, watu ambao mmoja alikuwa na vyeo viwili lakini hakuweza kujifahamu kabisa kimoja zaidi ya kukifahamu kile kinachojulikana na hadhira ya watanzania. Watu ambao walikuwa wakijulikana kutokana na kazi zao pamoja na mchango wao kwa watanzania ndiyo hao taarifa ilikuwa ipo mezani kwake. Hakika ilimchanganya kwa kutokea kwa vifo hivyo ndani ya muda ambao hakutarajia kabisa, kufa kwa mlipuko katika sehemu mbili tofauti ni jambo ambalo halikuwa la kawaida kabisa. Vifo vyao vyote watu hao vilikuwa vinalingana kabisa na ilimpelekea kabisa kuvihusisha kuviona ni vifo vilivyosababishwa na watu wa aina moja kutokana na jinsi vilivyotokea.

    Mmoja alimtambua kabisa kuwa alikuwa anasubiria masaa mahcache tu aweze kuanza hatua ya awali ya kuanika cha ndani ambacho haakikupaswa kuanikwa nje kwa wahusika, mmoja alimtambua alikuwa ni mkuu wa shirika kubwa la kiserikali nchini . Alipofikiria nyadhifa zao hao watu hakuwa kabisa na hisia kuwa walikuwa wameuawa kwa sababu moja. Vuguvugu la kifo cha mmoja ambaye ni Mheshimiwa alihisi ni kutokana na kile ambacho alikuwa akienda kukizungumza leo, vuguvugu la pili hakuweza kabisa kuhusisha na kifo hicho kutokana na mtu huyo wa pili aliyeuawa ndani ya jiji la Dar es salaam kuwa hahusiki kabisa na sababu hiyo ya kifo hicho cha kwanza. Suala hilo lilimfanya akune kichwa hasa kutokana na hali hiyo iliyotokea na mwishowe aliamua, akiwa katika fikra hizo simu yake ya mezani iliita kwa mara nyingine jambo ambalo lilimfanbya asitishe fikra zote alizokuwa akiziwaza na macho yote akayaelekeza kwenye mkonga huo wa simu. Hakutaka hata kusubiri kwa sekunde kadhaa  baada ya kuyaekeza macho hayo kulipo mkonga wa simu, haraka sana aliunyanyua mkonga huo na kuuweka sikioni mwake alipobaini kuwa simu hiyo ilikuwa ikitoka ndani ya jengo hilo tena kwa mtu ambaye alikuwa ni mkubwa wake kikazi.

"Ndiyo mheshimiwa.....nimezipata muda si mrefu nilikuwa nikizifikiria sana taarifa hizo muda huu....ndiyo mheshimiwa nitaagiza vijana sasa hivi waweze kufanya kazi....sawa nitakutaarifu" IGP Mbwambo aliongea na simu hiyo na alirudisha mkonga mahala pake baada ya simu hiyo kukatwa.

  Baada ya kuuweka mkonga huo mahala pake alichukua simu yake ya mkononi kisha akagusa juu ya kioo akiwa ni mwenye kutafuta kitu ndani yake, hatimaye aliacha kugusa simu hiyo na aliipeleka moja kwa moja sikioni akionekana alikuwa akipiga simu kwa mtu mwingine. Baada ya simu hiyo kugusa tu shavu lake alitulia kimya sana mithili ya maji yanavyotulia mtungini, sikio lake moja hilo ambalo simu ilikuwa imeligusa lilikuwa limeweka umakini mkubwa sana kuliko sikio la pili jambo ambalo huwa ni kawaida sana anapokuwa anaongea na mtu muhimu sana akiwepo kikazi.

"Jeph njoo ofisini kwangu haraka sana uje na Mutonga" Baada ya hapo alikata simu na kisha akaiweka mezani akiwa ni mwenye kusubiria jambo liweze kutimia.




****


                      DODOMA
    Muda huo tayari kamihsna wa polisi wa Dodoma John Faustin alikuwa tayari  ameshatoa taarifa ya kila kilichotokea mkoani humo, Kamishna John alithibitisha kabisa kutokea kwa tukio hilo mkoani kwake na akatoa ahadi ya kushughulikiwa jambo hilo kwa haraka sana na jeshi la polisi ambalo lipo chini yake mkoani Dodoma. Baada ya kutoa ahadi hiyo mbele  ya wanahabari aliondoka kwa haraka sana kwenda eneo la tukio kuangalia kile kilichokuwa kikiendelea, alitumia muda mfupi tu akawa amefika eneo la tukio ambapo alikuta vijana wake wakiwa wanaendelea na kazi na umakini wao uliongezeka baada ya yeye kuwasili.

    Alipokea heshima kutoka kwa maaskari tofauti ambao walikuwa wapo chini yake, baada ya hapo aliuliza juu ya kile kilichokuwa kikiendelea hapo. Kamishna John aliridhishwa sana na ufanyaji kazi wa vijana wake ambao walikuwa wameshafanya utafiki wa kila kitu, muda huo alikuwa yupo  Mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi(ASP) ambaye ndiye aliongoza uchunguzi huo wote wa tukio hilo lilitokea.

"Afande haya mabaki ya bomu hili lililolipuka hapa hatujafikiwa kuyaona kabisa, ingawa kwa mlipuko mzito uliotokea inaonesha kabisa hilo lilikuwa ni bomu" ASP alieleza.

"Sawa, je   gari hii ilivyoingia hapa hakushuka kabisa Mheshimiwa Bai?" Kamishna John aliuliza

"Hakushuka kabisa Afande kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hili, gari lake lilipofika parking lilitulia tu hakukuwa na dalili ya kushuka mtu kabisa hadi muda ambao mulipuko unatokea"

"Ok uchunguzi ufanyike mara moja mimi ninarudi ofisini naomba matokeo hata ya vipimo vya daktari juu mwili wake uliokutwa ndani ya gari  yanifikie mwenyewe pindi yatakapokamilika"

  Baada ya hapo Kamishna John alipanda gari lake alilokuja na kisha akaondoka ndani ya eneo hilo, askari waliopo chini yake waaliokuwa wamebakia katika eneo hilo waliendelea kuchakarika na wajibu wao uliowafanya wawepo ndani ya hapo.



****



   Muda huo upande wa ofisini kwa IGP Mbwambo baada ya kusubiri kwa kipindi cha muda wa dakika kadhaa vijana wawili waliokuwa wamevaa nguo za kiraia waliingia humo ofisini, vijana hao walipofika mbele ya IGP Mbwambo kila mmoja alitoa heshima kwa kubana mikono kisha akakamaa. IGP Mmbwambo aliwaruhusu wote kwa pamoja waketi kwenye viti viwili vilivyokuwa vipo mkabala na meza iliyokuwa ipo mbele yake. Vijana hao ambao walikuwa na miili ya wastani na mmoja alikuwa amevaa maavazi ya kileo sana na mwingine alikuwa amevaa suti, walikaa kwenye viti hivyo na kila mmoja akawa ameyaelekeza macho kwa IGP Mbwambo ambaye alikuwa amekaa akiwa anawasubiria kwa hamu kubwa waweze kuketi kwenye viti vyao.

"Jeph" IGP Mbwambo aliita huku akimtazama yule kijana aliyevaa mavazi ya kileo.

"Mkuu" Jeph aliitika


"Mutonga" IGP Mbwambo alimuita na yule kijana wake aliyekuwa amevaa suti nadhifu sana.

"Taarifa za matukio mawili tofauti yaliyotokea nafikiri mnazo, matukio ambayo yamepelekea kifo cha Mheshumiwa Bai na mkurugenzi mkuu wa NSSF. Jambo nililowaitia hapa ni kuhusu suala hilo" IGP Mbwambo aliongea na kisha akaweka kituo na kuwatazama vijana wake mmoja baada ya mwingine kama walikuwa wakimsikiliza. Baadaya hapo aliendelea, "Mheshimiwa huko tayari ameshacharuka na anahitaji kwa kina uchunguzi juu ya suala hili uanze, hii imenifanya niwaite nyinyi hapa".

"Jeph wewe kuanzia muda huu unatakiwa uondoke kwenda Dodoma kuhakikisha suala hilo wahusika wanapatikana, wewe Mutonga utabaki hapahapa jijini Dar es salaam uhakikishe wahusika hawa wanapatikana haraka iwezekanavyo. Hii ni amri kutoka kwa Mheshimiwa na uharaka wa kazi hii umesababisha nisiwape kazi hii polisi wa kawaida, ndiyo maana nikaiweka chini yenu CID nina uhakika mtaikamilisha ndani ya siku chache tu" IGP Mbwambo aliendelea kuwaeleza.

"Ndiyo afande" Wote kwa pamoja waliitikia

"Sasa basi taratibu zote zipo tayari nafikiri muende ofisini kwa Mheshimiwa ana jambo jingine la kuwaeleza" IGP Mbwambo alihitimisha maelezo hayo ambapo vijana hao wa kitengo cha siri cha jeshi la polisi walinyanyuka, wote kwa pamoja walikakamaa kiheshima na kisha wakapeana mikono na IGP Mbwambo halafu wakaondoka ndani ya ofisi yake.



   CID ambalo  neno linalotokana na neno la kingereza ambalo kirefu chake ni 'Criminal investigation department, hii ni idara ya siri ya jeshi la polisi ambayo hujihusisha na utafiti wa mkosa makubwa ya kiuhalifu. Idara hii maofisa huwa hawavai sare kabisa na wana muonekano wa tofauti kabisa na Askari wa kawaida, Maaskari wa ndani ya idara hii wengi wao huwa ni mapolisi wa kawaida wanaovaa  sare kwa muda miaka miwili ndiyo huhamishwa kwenda idra hii baada ya kupata mafunzo zaidi tofauti na Askari wa kawaida ndani ya jeshi la polisi. Hawa ndiyo wanaouhusika upelelezi mzito ndani ya jeshi la polisi, pia ni mojawapo kati ya sehemu tatu muhimu sana ndani ya nchi hii wakiwemo na Usalama wa taifa, Millitary Intelligence na wao. Uharaka wa kazi hiyo ndiyo ulimfanya IGP Mbwambo aweze kuwatumia kwani hao watu walikuwa hawajulikani kabisa kwa raia wa kawaida, pia walikuwa ni wepesi sana katika kufanya kazi zisizoeleweka kabisa.


***

     OFISI YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI
    Baada ya Japhet na Mutonga kutoka ndani ya ofisi ya IGP Mbwambo, moja kwa moja walielekea kwenye ofisi ya waziri wa mambo ya ndani ya jengo hilohilo, huko walikutana na waziri akiwa amekaa mkao wa kuwangoja wao tu waweze kufika kwenye eneo hilo aweze kuwapatia maelezo ambayo yaliwafanya awaite  hapo. Jeph na Mutongta walipoingia tu ndani ya ofisi hiyo kila mmoja alitoa heshima kwa waziri kwa kukakamaa kiheshima. Wote kwa pamoja waliruhusiwa kuketi kwenye viti vilivyopo mkabala  na kisha wakatulia kimya.

"Vizuri kwa kuwahi kufika vijana wangu, kila kitu nafikiri mshaelezwa na Mbwambo kilichobakia sasa ni mimi kuwapa maelezo muhimmu tu. Jeph wewe kwanza shika tiketi ya ndege nimeamua kukupatia ili uwahi kufika Dodoma na kazi hii uianze mara moja" Waziri aliongea huku akimpatia tikiti hiyo ambayo tayari ilikuwa imeshafika ofisini kwake.

"Asante  Mheshimiwa" Jeph alishukuru

"Mutonga wewe hutoki ndani ya jiji hili ila unaweza kuwa msaada kwa mwenzako hivyo uwe tayari kwa lolote, wewe pokea hii hapa" Waziri aliongea huku akimpatia Mutomnga mkoba wenye vifaa muhimu vya kufanyia kazi.

"asante Mheshimiwa" Mutonga alishukuru.

"Nimeamua kuwapatia kila kitu cha muhimu na cha ziada katika kazi hii nikiwa kama askari mstaafu hivyo natambua sana ugumu wa kzai hiyo mnayoenda kuifanya, sasa basi nahitaji kazi hii imalizike haraka iwezekanvyo kutokana na uwepo wenu ndani ya miji ambayo matukio yalitokea. Vijana wangu nawaamini sana ndiyo maana mkateuliwa kwani hamkuwahi kuharibu kazi tangu muhamishiwe CID, natumaini kazi hii mbele yenu vijana wa kazi itakuwa imekwisha kabisa. Niwatakie kazi njema" Waziri alihitimisha na wote walinyanyuka kwenye viti vyao wakatoa heshima, walipeana mikono na Waziri na kisha kila mmoja akageuka nyuma na kutoka ndani ya ofisi hiyo.


****


   Taarifa ya kifo hicho cha waziri ilifanya kikao cha bunge ambacho kilikuwa kikingojewa kwa hamu sana ndani ya siku hiyo kuweza kughairishwa, watu waliokuwa wakisubiiri kwa hamu sana kikao hicho walijikuta wakiingiwa na simanzi baada ya kupokea taarifa ya kifo cha Mheshimiwa aliyekuwa anakuja kuianza kazi yako nzito ambayo alipewa muda iweze kukamilika. Hiyo ndiyo ilikuwa habari kubwa kwa baadhi ya vituo vya redio na telvisheni ndani ya siku hiyo watanzania walimuona Mheshimiwa kama mtu shujaa kabisa aliyekuwa akijaribu kulitetea taifa lake, walilaani sana waliokuwa wamesababisha kifo chake ambacho hadi inafikia majira hayo ilikuwa ikiaminika alikuwa ameuawa kwa kutumia bomu la kutegwa.     Mamia ya makundi ya watanzania walikuwa wamejikusanya  wakiwa wanaongea suala hilo huku kila mmoj akiwa na hisia zake juu ya kulieleza suala hilo, ilikuwa ni huzuni sana na hata watanzania waliohojiwa na vyombo mbalimbali vya habari ambavyo viliwatembelea katika mitaa wanayoishi kusikiliza maoni yao walionesha hisia zao jinsi walivyohuzunishwa na suala hilo lililomkumba Mheshimiwa. Nyumbani kwa Mheshmiwa ambako alikuwa ametoka siku iliyopita tu kuja jijini Dodoma kulitawaliwa na vilio vya wanafilimia hao ndani ya jiji la Dar es salaam, hadi jioni ya siku hiyo unafika tayari watu walikuwa wameshaanza kuja hapo nyumbani kwake kuwafariji wanafamilia wake kutokana na kipindi hicho kigumu.



****

   Giza la siku hiyo lilipoingia tu na jioni ikafukuzwa mbali na usiku uliokuwa ukitaka kuchukua zamu yake kwa haraka sana, Mutonga tayari alikuwa yupo ndani ya uzio wa nyumba ya Mkurugenzi mkuu wa shirika la mfuko wa hifadhi ya jamii Bwana Mabina. Muda huo utepe ulikuwa umezungushiwa ndani ya nyumba hiyo lakini kutokana na cheo chake na pia idara yake anayofanyia kazi alipita bila kizuizi chochote langoni mwa uzio huo ambapo kulikuwa na Askari aliyekuwa akilinda humo asiingie mtu wa kawaida ndani. Akili yote ya kikazi iliamka pindi tu alipoingia ndani ya lango hilo, macho yake ya umakini yalikuwa yakiangaza kila pande ya nyumba hiyo kama afanyavyo mgeni akiwa anaingia ugenini. Alipitiliza moja kwa moja  hadi kwenye baraza la nyumba hiyo ambayo hadi muda huo ilikuwa ikionekana kama gofu kutokana na kuungua sana, barazani hapo Mutonga alitaka kuingia ndani ya nyumba hiyo lakini akasita na kisha akaanza kutembea kuzunguka nyuma ya nyumba hiyo huku akiwa makini kutazama mandhari ya hapo nyumbani ilivyo. Alitembea kuizunguka nyumba akiwa ni mwenye kutazama kila upande na hatimaye alirejea pale barazani, alipiga hatua kusogelea eneo la nyumba hiyo ambayo lilikuwa halina mlango kutokanana mlango wa nyumba hiyo kuvunjwa na mlipuko uliotokea. Macho yake yote yalikuwa yapo kwenye eneo hilo la mlango alipolifikia kwa muda wa sekunde kadhaa, aliporidhika kulitazama eneo hilo alitoa mipira ya mikononi mfukoni mwake ambayo aliivaa mikononi kisha akashika sehemu zenye mabaki ya mbao ambayo yalikuwa yamegeuka mkaa kabia baada ya kuungua.

  Mutonga alipiga hatua kuingia ndani ya nyumba  baada ya kumaliza kuyaangalia mabaki yaliyokuwa yapo mlangoni, alitokea kwenye sebule pana ya nyumba  ambayo kimuonekano ilikuwa ni sebule moja ya kifahari lakini kwa muda huo ilikuwa  ni kama gofu huku vitu vya ndani ya nyumba hiyo viliyokuwa vimejengwa kwa malighafi ngumu vikiwa vimebakia na vingine visivyoungua vikiwa vina rangi nyeusi kutokana na kupitiwa  na mlipuko. Mutonga alitembea ndani ya eneo la sbule hadi kwenye kila kingo yake  akiwa anaitazama kwa umakini sana, aliridhika kulitazama eneo lote pindi macho yake yaliyokuwa yapo makini sana ndani ya eneo kufuata kufuata  yake aliyoishika mkononi alielekea ulipo mlango wa jikoni. Mlango wa sehemu maakuli  ulimvutia sana kuutazama na akajikuta kabisa akivutika kuusogelea pia ingawa kimuonekano ulikuwa hauvutii kabisa kwa jinsi ulivyoungua, alijikuta akipiga hatua kuelekea eneo hilo la jikoni ambapo kulikuwa kumemvutia sana.

*CID KAZINI
*KUCHUNGUZA KIFO CHA KIZITO


ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment