Tuesday, January 3, 2017

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA THELATHINI NA TATU









RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________




SEHEMU YA THELATHINI NA TATU!!
                "siku hiyo mke wa Kamishna Wilfred alipoongea maneno hayo alikuwa ni ana cheo cha SP {superintendent police}, ilikuwa ni majira ya usikua ambapo mke wake aliaga kururdi kwao akipakia nguo zake kwenye begi.

    Kutokana na mapenzi mazito aliyonayo kwa mke wake na kuhofia kuvuja kwa adhma yake alijikuta akilegeza msimamo kimaigizo ndipo mke wake akabaki na aliamua kufanya adhma hiyo kisiri na sasa usaliti wa kusema uongo kwa mke wake pia unamtafuna leo hii).




__________
_________________TIRIRIKA NAYO
__________

     Lawama zake ndani ya muda huo  hazikuweza kabisa kubadilisha kile kilichokuwa kimetokea hadi akawa hapo, alizipa lawama tamaa zake lakini tayari alikuwa ameshachelewa hadi muda huo. Akiwa yupo ndani ya majuto hayo sauti ya viatu vya mtu akitembea kwa taratibu vilisikika kwa nje ya chumba hicho ambapo ndiyo kulizidi kumfanya awe na shauku ya kutaka kumjua yule aliyekuwa akija ni nani, alipowatazama kina DCP John na yule kijana wote walikuwa wakitabasamu tu. Viatu hivyo vilivyokuwa vikisikika vilizidi kukairibia eneo hilo na hatimaye aliyekuwa akitembea akaonekana mlangoni hapo Kamishna Wilfred ndiyo alizidi kuchanganyikiwa kabisa baada ya kumuona mtu aliyekuwa amepanga adhma mbaya dhidi yake akiwa ndiyo yupo mateka katika upande aliopo, alimuona Norbert akiwa amevaa suti tu akiwa hana shati na mkononi akiwa amebeba begi dogo kama la kiofisi. Norbert aliingia ndani ya chumba hiko na akamtazama Kamishna Wilfred kisha akaachia tabsamu la dharau, alimgeukia DCP John kisha akamtazama akiwa na tabasamu kwani alishaamini kuwa kazi ile ilikuwa ni mkono wake ndiyo ulikuwa umehusika hadi Kamishna Wilfred akawa yupo chini ya mikono yao
              "Aisee John umeniwahi bwana na pia umenirahisishia kazi kabisa" Norbert aliongea
               "Nilikuambia nitamsaka huyo kamishna aliyewatuma special forces kuja kumvamia Moses na pia kumvamia shemeji yetu Belinda sasa ni huyu hapa" DCP John aliongea
               "kazi imekuwa rahisi sana sasa hivi" Norbert aliongea huku akimtazama  Kamishna Wilfred.
                "Kiupande wangu imekwisha, nimemnasa alipotoka katika nyumba ile aliyoingia ambayo wamo wasaliti wenzake wote" b DCP John aliongea akazidi kumfanya Norbert ashangae kwani hakuwa akijua kuwa kama walikuwa wapo ndani ya nyumba moja muda uliopita kabla hawajatoka nyumbani kwa Wilson.
                  "Duh! Kumbe tulikuwa wote mule ndani....sasa Kamishna utakuja kuujibu umma mwenyewe imekuwa vipi wewe,Thomas, Filbert Ole, Wilson Ole na three star jeneral muwe upande mmoja. Mnamtuhumu Rais Zuber ni msaliti mkitaka kuipindua serikali yote iliyoleta maendeleo kwa muda mfupi tu kwa sababu zenu binafsi tu, ushahidi wote wa ujinga wenu ninao jua nitauachia redioni karibuni tu ili watanzania wote wausikie eti mnataka ushoga uwe rasm hapa Tanzania kisa hela tu. Ngoja usikie mwenyewe sipigi mikwara tu" Norbert aliongea kisha akatia mkono katika begi lake dogo akatoa kifaa mfano wa redio ndogo isiyotumia kanda akakiwasha, alitulia baada ya sekunde kadhaa na kisha redio hiyo ikaanza kutoa sauti ambayo alikuwa ameirekodi sambamba na kupiga picha mbalimbali bila wahusika kujijua.

   Maneno yaliyokuwa yakiongelea siku hiyo ndani ya mkutano walioutisha kina Wilson baada ya kuuawa wenzao ndiyo yalisikika ndani ya kinasa sauti  hiko, Kamishna Wilfred alijua tayari alikuwa hana ujanja kwani Norbert alikuwa ameshikilia makali na angeleta ujanja tu basi angekatwa. Alimtazama Norbert kwa sura iliyojaa huruma sana lakini huruma ile haikusaidia katika kumbadilisha Norbert awe na sura ya huruma, Norbert ndiyo kwanza alizidi kutabasamu kila alipomtazama  Kamishna Wilfred ambaye uso wake ulikuwa umejaa huruma tu kama Ngamia aliyeona kisu kikikaribia kufika kwenye shingo yake afanywe kitoweo.
             "Kamishnaa yaani naangaliwa na mwanamke mrembo akitaka nimuonee huruma kama Josephine lakini sikumuonea huruma ndiyo nikuonee huruma wewe kidume unaejiona mjanja kufuata mkondo wa pesa na visasi visivyo na maana. Umepotea njia hapo jua hii nitahakikisha inafika redioni sasa tuone utafanyaje na ikitoka tu nakuachia huru hapo nje ya geti mchana kweupe ili wananchi wakuuwe si unajua vijana walivyochoma nyumba ya Moses bila kujua hana hatia sasa hasira zao zitawageukia nyinyi" Norbert alimuambia Kamishna Wilfred huku akimtazama kwa dharau kuu, baada ya maneno hayo yenye kuuumiza kwa Kamishna Wilfred Norbert alitoka ndani ya chumba hicho akifuatana na wenzake na wakafunga mlango na taa zikazimwa kiza kizito ndiyo kikafuata kwa mateka wao.



ASUBUHI ILIYOFUATA
     Siku hii ijumaa ilikuwa ni siku nyingine mpya katika siku ambazo muumba alikuwa amewajalia waja wake wengi waweze kuiona siku hiyo kati ya wachache waliokuwa wameikosa kuiona siku hiyo, eneo la Magogoni hali ilikuwa ni ileile kwa wanajeshi wakiwa wameizunguka ikulu tena ndani ya siku hiyo kuongezeka kwa wanajeshi kuliwafanya raia wa kawaida waliokuwa wakishuhudia tukio hilo waamini kabisa kuwa rais wao alikuwa yupo mbioni kuondolewa ndani ya Ikulu na kuingia rais mwingine ambao watu walikuwa hawamtambui hadi muda huo. Waandshi wa habari kutoka mashirika mbalimbali ya habari duniani walikuwa tayari wameshafika na walikuwa wakirusha matangazo hayo ambayo yalikuwa yakishuhudiwa na watu tofauti kutoka mataifa mbalimbali duniani.

    Si Aljazeera,BBC,DWTV, SKY NEWS,CCTV NEWS, wala CNN waliokuwa hawajakosa kufika eneo hilo hadi asubuhi hiyo inawadia tangu wapate habari za wanajeshi kuizunguka ikulu hiyo. Wanahabari hao wa kimataifa walikuwa wamefika hapo na wakihangaika kutafuta habari kutoka kwa wanajeshi hao wakiuliza sababu ya kuizunguka ikulu hiyo, habari hiyo waliikosa na hata walipojaribu kuingia ndani ya ikulu wakamuhoji rais Zuber ambaye alikuwa hajatoka nje ya ikulku kwa siku ya pili sasa walizuiwa na wanajeshi hao waliokuwa wapo makini katika kutimiza amri ambayo walikuwa wamepewa na mkuu wao. Kikundi cha wanahabari hao wa kimataifa na hata wa kitaifa kiliamua kujitosa ndani ya siku hiyo katika kusaka habari, walijitosa na kwenda hadi makao makuu ya jeshi nchini yaliyopo Upanga ambapo kwa siku hiyo walimkuta L.J Ibrahim akiwa yupo ofisini kwa Jenerali akiiacha ofisi yake ikiwa haina mtu. Waandishi hao wa habari waliomba kumuuliza maswali machache juu ya hali hiyo akiwa yeye kama mkuu wa jeshi aliyekuwa amebakia tu katika jeshi la wananchi wa Tanzania, L.J Ibrahim kwa jinsi anavyopenda kusikilizwa na umma wa watanzania na hata duniani aliamua kuongelea kuhusu sakata hilo na akawakaribisha waandishi hao kwenye chumba cha mkutano ili aweze kuyajibu maswali hayo ya waandishi wa habari kutoka sehemu mbalimbali duniani. Waandishi hao ambao alikuwa wamejifunza lugha mbalimbali kutokana na kazi yao kuwa ya kimataifa nao hawakuichezea nafasi hiyo ili vituo vya televisheni wanavyotokea viweze kupata habari, walishusha maswali kwa L.J Ibrahim kwa mfululizo ambayo hayakujibiwa mmoja bali alitoa maelezo ambayo yalikuwa ni majibu tosha ya mswali hayo.
                   "Mmeuliza maswali mengi ambayo yalikuwa yakihitaji majibu kutoka kwangu na sitowaacha bila ya kuwapa majibu ili mtambue kisa chote cha kutoa amri hiyo ya wanajeshi wote kuizunguka Ikulu. Baada ya kuanguka utawala  wa aliyekuwa rais mheshimiwa Filbert Ole nchi hii iliijua kuwa tulikuwa tumepata kiongozi stahiki anayefaa kuwaongoza watanzania kumbe haikuwa hivyo bali tulikuwa tumepata mbaya zaidi ambaye ni zaidi hata ya aliyetangulia. Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania alikifuta chama cha kisiasa kikuu cha upinzani ambacho kilikuwa kikiongozwa na Mzee Ole hasa baada ya kubaini kitu walichokifanya, na sisi tunasema tunamfuta madaraka rais wa nchi hii baada ya kubaini kile alichokuwa akikifanya kuwa ni kinyume na madaraka yake. Hata juma moja halijaisha tangu tumzike Jenerali wetu na komandoo wa kuaminika kati ya makomandoo kumi na mbili ambao kwa sasa kabaki mmoja tu ambaye ndiye msaidizi wangu ajaye ambaye si mwingine bali ni Meja jenerali Belinda. Uchunguzi ulibainika ya kwamba kuwa Professa Moses Gawaza alikuwa ndiyo muuaji mkuu na ndiye aliyetengeza sumu zilizokuwa zimewaua Jenerali Kulika na wanajeshi wengine wa jeshi langu na pia ndiye alihusika na mauaji ya viongozi wa dini akiwemo Askofu Edson na Mufti mkuu wa jiji la D ar es salaam. Isitoshe msaliti huyuhuyu aliyekuwa yupo ndani ya ikulu akakutana na Professa Gawaza kwa siri ilihali  anatambua ni mtuhumiwa na hakumtia hatiani alipokutana huko na mtu huyo, nilipozipata habari kupitia mtu wangu ambaye ni mmoja wasiopenda usaliti wake niliamua kumuambia atoe maelezo kwanini ameonana naye mtu huyo anayejulikana ni mtuhumiwa na hakuchukua hatua yoyote ile. Nilimpa siku saba za kutoa maelezo hayo vinginevyo Ikulu anatoka lakini yeye hakumfanya hivyo na ndiyo maana vijana wangu waliokuwa na uchungu na jenerali wao waliungana nami katika kuhakikisha anatoka Ikulu. Nafikiri maswali yenu yote nimeyajibu je kuna la ziada?"  L.J Ibrahim alitoa maelezo hayo ambayo yalikuwa na majibu ya maswali ya waandishi wa habari na akawa anasubiri kusikiliza hayo mswali ya ziada, mwandishi moja kutoka Tanzania alinyoosha mkono ambao ulikuwa umeonekana dhahiri na L.J Ibrahim ambaye alimruhusu aulize.
            "Kwa mujibu wa sheria za kitanzania hasa jeshini ni kwamba mwanajeshi yoyote mwenye kuanzia nyota huwa hapandishwi cheo chochote na yeyote isipokuwa na Amiri jeshi mkuu ambaye ndiye mheshimiwa rais, hivyo basi hakuna kiongozi yeyote mwenye mamlaka ya kumpandisha cheo mwanajeshi mwenye kamisheni na rais. Sasa General mara ya mwisho kuonekana mbele ya umma katika mazishi ya General Augustin Kulika ulikuwa na cheo cheo cha luteni jenerali au three star general iweje leo hii tukiwa tumekuja tukuone ukiwa na cheo cha four star general yaani Jenerali, je alikupandisha nani ikiwa mwenye mamlaka hayo ni tayari mmemzuia asitoke ndani ya ikulu?" Mwandishi huyo wa habari aliuliza swali hilo.
              "Swali zuri kijana na jibu lake ni kama ifuatavyo, Zuber Ameir kwa sasa si rais na aliyenipandisha cheo hadi sasa nimekuwa jenerali kamili ni huyo ambaye ndiye ataingia pale ikulu mnamo kesho asubuhi baada ya ikulu yote kuisafisha usiku wa leo. Swali jingine" L.J Ibrahim alijiu swali hilo kisha akahitaji swali jingine la ziada, waandishi wote walikuwa wametosheka na maelezo hayo na walikaa kimya baada ya L.J Ibrahim kuhitaji swali jingine aweze kulijibu kutoka kwao. Hapo kikao kiliisha na L.J Ibrahim alinyanyuka kwenye kiti alichokuwa amekaa akafunga kikao kisha akaondoka kwenye chumba hicho cha mkutano akiwa na imani kabisa maneno yale yatakuwa yamejenga athari mpya kabisa kwa Rais Zuber akisikia kuna rais mpya tayari ameandaliwa.

****

   MTAA WA BREACH CANDY INDIA
JIJINI MUMBAI, NCHINI INDIA
    Ndani ya mtaa huuu ambao upo chini ya dola ya Maharashtra katika jiji la Mumbai taarifa hiyo ya habari ya kile kilichokuwa kikitokea Tanzania ilikuwa ikishuhudiwa vizuri, watu waliokuwa na wapo ndani ya hoteli ambayo ilikuwa ipo mita kadhaa tu kutoka yalipo makao makuu ya kampuni ya kundi la Tata ambao wamiliki wa shirika la ndege,kiwanda cha magari, pamoja viwanda vingine vingi vilivyo chini ya Tata. Watu hao walikuwa wapo katika chumba kimoja cha hoteli hiyo ya hadhi ya nyota tano wakiwa wamelaliana kwa mahaba makubwa huku kioo cha televisheni kikiwa kipo mbele yao wakikitazma. Walikuwa ni watu wa jinsia moja ambao walifaa kuwa vichwa wa familia wote lakini mmoja wao yeye ndiye alikuwa ni kama moyo wa familia kwa mwenzake, mwenzake alikuwa ni kichwa wa familia tena kwa ndoa ya uhalali kwa mataifa ya magharibi. Watu hao hawakuwa wengine ila ni Askofu Valdermar(Jack Shaw) na Sheikh Ahmed wakiwa hawana nguo hata moja, wote walikuwa wakimtazama jinsi kibaraka wao L.J Ibrahim alivyokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari hadi anaondoka kwenye chumba cha mkutano cha makao makuu ya jeshi.
               "Haaaaa! Tayari ameshajipa cheo chake kabla muda wakupewa cheo hujafika" Sheikh Ahmed aliongea
                "Na wewe humjui Ibrahim alivyo yaani anapenda sana kuwa mkuu wa majeshi, ila anapendeza akiwa hivyo maana ana mwili wenye mvuto sana yaani" Askofu Vladermar aliongea huku akizishika ndevu za Sheikh Ahmed ambazo zilikuwa zimejaa kwenye kidevu chake, maneno ya kumsifia L.J Ibrahim yalimkera sana Sheikh Ahmed na aliishia kumtazama Askofu Valdedrmar kwa jicho la chuki sana.
                  "Halafu sipendi umsifie mwanaume mwingine ukiwa na mimi Shaw mbona hunielewi"  Sheikh Ahmed alikuja juu muda huohuo mithili ya moto wa makaratasi.
                  "Basi mume wangu nimekuelewa sirudiii tena"  Askofu Valdermar aliongea pasipo kuwa na haya ya kujifanya mwanamke kwa mume mwenzie, aliamua kumbusu Sheikh Ahmed mdomoni baada ya kumuona amekasirika sana.

     Hasira za Shekh Ahmed zilipoa hapohapo na sura yake ya ukali aliyokuwa akimtazama Askofu Valdermar ikarudi kwenye hali ya kawaida, busu hilo alilopigwa lilimfanya anyanyue mkono wake ambao ulikuwa pembeni ukatua hadi kwenye kalio la Askofu Valdermar. Pasipo aibu wala kuihofia hiyo sijda iliyojengeka katika paji lake la uso kwa kusujudu sana, aliliminya kalio hilo la Askofu Valdermar na kusababisha Askofu huyo afumbe macho kwa hisia. Alipoacha kumminya kalio hilo naye alimbusu mdomoni kisha macho akayarudisha kwenye kioo cha luninga ambapo tayari mazingira ya ikulu ya Tanzania yalikuwa yakionekana dhahiri baada ya kikao cha L.J Ibrahim na waaandishi wa habari kuisha.
                "Watu weusi wajinga sana wapo radhi kuuza nchi kwa pesa tu" Sheikh Ahmed aliongea
                "Yaani pale kama bodi ilivyopanga mpenzi tuitumie hiyo tamaa yao tupate pesa zaidi, najua Ole akikaa madarakani ule mgodi wa almasi pamoja gesi na mafuta yatakuwa yapo chini yetu tu" Askofu Valdermar aliongea.
                 "Halafu sisi tunamwaga misaada mingi kwa mashoga ili kuwashawishi watu wawe hivyo, tunajenga asasi nyingi za mashoga" Sheikh Ahmed aliongea
                   "Kabisaa mpenzi" Askofu Valdermar aliitikia huku akimbusu Sheikh Ahmed shavuni, hawakujua kuwa mambo tayari yalikuwa yemevunda huko kutokana na uwepo wa kundi la wanausalama wa EASA pamoja na maaskari waadilifu wa JWTZ.
                    "Watajiona wana maendeleo sana kumbe ndiyo tunawatia ujinga hawa, tupo nyuma ya The new wrold order daima na mzizi wetu ni uleule" Askofu Valdermar aliongea kwa sauti legevu sana.
                      "Viongozi wajinga acha sisi tuwatie ujinga zaidi wakati mwenye akili zaidi akitoka ndani ya jengo lao lile wanaloliiita Ikulu ili tumuweke kibaraka wetu tutakayemtumia daima kwa manufaa yetu wenyewe" Sheikh Ahmed aliongea huku akiuchezea mwili wa Akofu Valdermar aliyekuwa amelala juu ya kfua chake, Askofu Valdermar naye hakuwa nyuma alikuwa na kaziya kuchzea kifua cha bwana wake huyo kilichojaa bustani ya uoto mweusi wa asili wa kutoka bara Arabu.

     Walikuwa wakifurahia sana kitu hicho walichokuwa wakifanyiana lakini raha zao zilikatwa tu muda mfupi, walipokatika raha zao wote waliojikuta wakitazama pembeni kukitazama kile kilichokuwa kimewakata raha zao ambacho kiliwapa msjhangao sana. Ilikuwa ni simu ya mkononi iliyokuwa ipo sentimita kadhaa katika sehhemu ya juu ya mtoto wa kitanda ambao huwekwa taa maaulum ya kuangza humo ndani ikiwa watumiaji wa chumb hawataki kutumia taa kubwa, Askofu Valdermar alipindisha mdomo aliposikia simu hiyo kisha akajinyanyua kifuani mwa Sheikh Ahmed akaenda kuipokea.
                  "Enhee! Sema kuna habari gani mpya huko?....... tumekuona aisee hongera ni hatua kubwa mmefikia....mkimaliza mna dau nono kila mtu.......kazi njema" Askofu Valdermar aliongea alipomaliza  akakata simu akamgeukia Sheikh Ahmed aliyekuwa akimtazama muda wote aliokuwa akiongea na simu, aliweka uso kwa kudhrau kama wafanyavyo wanawake halafu akajisogeza karibu na Sheikh Ahmed akajilaza kifuani kama alivyokuwa amejilaza hapo awali.
                    "Vipi kuna jipya lipi maana nahisi ulikuwa unaongea na Ibrahim huyo?" Sheikh Ahmed aluliza
                      "wala hana jipya anataka kusifiwa tu si kingine si unajua anavyopenda kusifiwa yule aonekane ni bora sana kwa ngozi nyeupe" Askofu Valdermar aliongea kwa sauti ya taratibu sana ,Sheikh Ahmed aliposikia maneno hayo alicheka kisha aksikitika sana.
                      "Ndiyo ujinga wa ngozi nyeusi huu yaani mtu akiwa na ngozi nyeupe halafu ana hela basi wanamuona kama ni Mungu vile, wacha tuwatumie kwa ujinga wao huo" Sheikh Ahmde aliongea huku akiiweka mkono yake kwenye makalio ya Askofu Valdermar ambaye alihema kwa nguvu mithili ya mtu aliyekuwa akijigeuza ubavu wa pili akiwa usingizni, naye hakuwa nyuma katika kufanya huo upuuzi wao ambao ulikuwa ni aibu sana kwao ikiwa watasikika na jamii au kuonwa wakiufanya upuuzi huo. Walikuwa wakiufanya upuuzi huo kwenye hoteli ambazo zenye usimamizi mkali sanma kuogopa kukutwa, nyadhifa zao za kidini katika nchi zao hapo walizitumia tofauti kabisa pasipo kuwa na lepe la hulka ya kibinadamu ya kushindwa kuyafanya hayo.

****

DAR ES SALAAM
     Majira ya saa nne asubuhi kwa saa za Afrika ya mashariki gari ya kijeshi yenye nyota mbili ambayo ilikuwa imeongozana na gari mbili za kijeshi zilizosheheni wanajeshi  wenye nyota tatu kila mmoja ambao walikuwa ni wa kike watupu zilifika jirani na hema ambalo lilikuwa likitumiwa na wanajeshi wa ardhi kama makao yao makuu ya muda. Waandishi wa habari walipoziona gari hizo zikiingia katika eneo hilo walizikimbilia kwa kasi sana huku kila mmoja akiwa ameweka kamera yake aweze kunasa chochote, gari hizo ziliposimama tu kundi la wanajeshi walienda kuweka mstari moja katika eneo ambalo lilkuwa mbele ya waandishi wa habari waliokuwa wakizikimbilia gari hizo ili wasiweze kufika karibu.

    Waandishi wa habari walipofika waliishia mbele ya mstari huo uliokuwa umewekwa na wanajeshi hao na hawakuvuka, walitoa kamera zao wakawa wanapiga picha magari hayo ambayo tayari wanajeshi wanawake waliokuwa wamepanda walishashuka. Maaskari hao wanawake walijipanga mstari mmoja kwa haraka sana kisha moja wao akafungua mlango wa nyuma wa gari lililokuwa na nyote mbili mbele na nyuma, M.J Belinda alionekana akishuka hapo akiwa amesuka mtindo mzuri sana ambao ulionekana dhahiri ingawa alikuwa ameuficha kwa kofia yake ya kijeshi yenye rangi nyekundu.

     Wanajeshi wote waliokuwa wapo eneo hilo walipiga saluti kwa pamoja kusababisha kamera za waandishi wa habari ziwachukue wakiwa katika hali hiyo, M.J Belinda  naye alizipokea saluti zao hao wanajeshi waliopo chini yake. Alikuwa amevaa gwanda la kijeshila jipya kabisa na kiatu kilichokuwa kinang'aa kwa dawa maalum aliyopakwa, umbo lake la kiurembo halikuweza kufichika hata akiwa amevaa gwanda hilo. Usoni alikuwa amevaa miwani nyeusi ya jua ambayo ilimfanya azidi kupendeza, M.J Belinda aliposhuka tu alitazama upande ule waliokuwa wapo waandshi wa habari akiwa amesimama mtindo ambao uliplekea kamera zao zifanye kazi ya  kupiga picha tu. Waandishi wa habari wengine walikuwa wakiweka vipaza sauti vyao mbele wakiuliza maswali ambayo hayakujibiwa na M.J Belinda zaidi ya kuwatzama tu kisha akapiga hatua kuelekea ndani ya hema la kikosi cha ardhi.






*WANATAKA NCHI WASHINDE NA HAWA WANATAKA KUWAANGAMIZA MAADUI WASHINDE NCHI NI GOMBANIA GOLI
*YA,EBAKI MASAA MACHACHE TU NCHI IWEZE KUPINDULIWA, JE UTAWALA WA RAIS MZALENDO UTASALIMIKA?
*M.J BELINDA NDANI YA MAGOGONI KUUNGANA NA VIJANA WAKE

USIKOSE SEHEMU YA THELATHUNI NA NNE KUJUA KILE KITAKACHOTOKEA KATIKA GOMBANIA GOLI



MUHIMU: WALE WENYE  KUHITAJI TOLEO JIPYA LA RIWAYA ZA NORBERT, WASILIANA NASI KWA UJUMBE MFUPI KUPITIA NAMBA 0762 219759 AU WHATSAPP 0713776843

No comments:

Post a Comment