Monday, February 20, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA KUMI NA NANE



WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com



SEHEMU YA KUMI NA NANE!!
Muda aliokuwa akiendesha gari alipokuwa yupo kwenye barabara ya Mandela alitoa simu yake na kupiga mahali na kisha alizungumza kwa lughz ya kikabila na akakata, walipofika jirani na eneo la Tabata relini aliweka gari kando na watu watatu waliingia kwenye gari hiyo. Wawili kati yao walikaa nyuma katika kile upande na kumuweka Jama kati na mmoja alipanda mbele.





________TIRIRIKA NAYO

  Haikufika mbali ile gari ikiwa inakaribia eneo lenye njia ya kwenda Tabata, vioo voyte vilipandishwa na kiyoyozi ndani ya gari kikachukua nafsi yake. Muda huo Jama alikuwa ameshatambua kabisa kuwa alikuwa amepanda gari moja na wajanja wa maji waliokuwa wanajua  yeye ni mshamba, alitulia kimya kama alikuwa ni mjinga vile kwa kitu ambacho kilikuwa kipo vichwani mwa hao watu. Huo ulikuwa ni mpango wa Dereva Teksi kama ilivyo madereva wengine ambao walikuwa wakishiriki vitendo vya uhalifu maeneo ya vituo vikuu vya mabasi. Madereva hawa ndiyo waliokuwa wakichangia kuibiwa kwa wale waliokuwa wakitafua riziki kihalali kabisa, walikuwa wameshawafanya abiria wajenge picha ya ujambazi kila akiona magari yao eneo hilo la  kituo kikuu hasa majira ya usiku. Huyu aliamua kuwaleta wenzake katika majira hayo ya mchana akijua huyo aliyekuwa amembeba alikuwa ni mshamba wa jiji, hawakujua kuwa walikuwa wamembeba mtu ambaye ni hatari sana kwenye anga za kutumia silaha na hata kupigana ana kwa ana.

  Kutokana na Jama kumtajia kuwa alikuwa akielekea kuwa alikuwa akielekea Kajiungeni, aliamua kuingia njia iendayo Tabata baada ya kufika kwenye njia hiyo na kisha akaongeza mwendo. Muda huohuo wale Watu waliokuwa wamekaa nyuma mmojawapo alitoa bastola lakini kabla hata haijafika kichwani mwa Jama ambapo alitaka kumuwekea alipigwa karate mkono wake silaha ikaanguka chini ya kiti. Alipotazama kule ambako ilikuwa imeanguka silaha hiyo alipigwa ngumi nzito ya shingo hadi akaenda kujigongwa kwenye eneo ambalo lipo pembeni ya kioo. Wa pembeni yake naye alitaka kumkaba alidakwa mkono wake ukavunjwa , muda huohuo mtu wa mbele alileta panga kwa kasi ya ajabu sana akitaka kumchoma lakini halikufika lengo kwani Jama tayari alijosogeza pembeni kwa ustadi mkubwa kisha akaubana kwa miguu mkono wake uliokuwa umeshikilia panga. Kilichofuata hapo ilikuwa ni kuizungusha miguu yake kidogo akaugosha mkono huo hadi panga likamponyoka na kisha akampiga teka jingine la nguvu sana lilipelekea arudi huko mbele kwa kasi sana hadi akaenda kujigonga kwenye eneo lenye makabati madogo ya kuweka nyaraka muhimu. Yule aliyekuwa amejeruhiwa mkono huko nyuma alijaribu tena kurusha ngumi lakini kutokana na ushupavu wa macho aliokuwa nao Jama Wa Majama aliikwepa hiyo ngumi ikapita, alipopita na ngumi alikuwa amesogeza kichw chake jirani kabisa na adui ambapo alipigwa kiwiko cha sehemu ya kisogoni hadi akazira papo hapo. Mwingine kule nyuma alijaribu kuinama chini aweze kuifikia silaha yake lakini kabla hata hajaigusa alipigwa goti la kichwa  lililoachiwa na Jama ambalo lilienda kumpigiza kwenye mlango wa gari hilo, akiwa hata hajakaa sawa alipewa ngumi ya kichwa ambayo ilikuwa ni nzito sana ambayo ilimfanya aende kujipigiza kwa mara ya pili. Aliumia sana huyo Jambazi kutokana na ngumi nzito aliyokuwa amepigwa kwani hakutarajia kabisa mtu ambaye walikuwa wakimdhania ni Mzee angeweza kutoa ngumi nzito namna hiyo akiwa anaendelea kuuguliwa maumivu yule aliyekuwa kiti cha mbele alijiweka sawa baada ya maumivu kumuisha na kisha akajaribu kuleta konde kwa mkono mwingine ambao haukuwa umevuunjika. Konde hilo lilikosa lengo kutokana na yeye kuvaa koti la kuteleza ambalo lilikuwa likitoa tahadhari kwa Jama kila akirusha ngumi kwa mlio wake, alikuta Mlengwa alikuwa ameshahama kando na kabla hajakaa sawa alipewa ngumi aina ya uppercut(hii ngumi ambayo hupigwa kwa kuchimbua kidevuni). Hapo alirudi hukohuko alipotoka na akawa ametoa nafasi nzuri sana kwa adui yake waliyemuona mchovu kuingiza mguu chini ya kiti na kutoka akiwa na akiwa na silaha ambayo alikuwa ameibana kwa  vidole vya miguu, alimuongezea pigo jingine yule Jambazi wa nyuma kisha akaichukua silaha hiyo kwa mikono yake na akaanza kutabasamu.

"Mmmekuwa mkiwafanya abiria wa kituoni  kuwa mitaji wa shughuli zenu haramu siyo sasa leo mtakuwa mfano" Aliongea huku akiwa ameikamta ile bastola mkononi mwake, alipomaliza kuongea aliunyanyua mkono huo uliokuwa na bastola na kuutuliza kwenye kichwa cha Jambazi mwengine ambaye alikuwa amekaa nyuma kusababaisha kumuharibu fahamu zake zote kutokana na ugumu wa kitako hicho. Baada ya hapo alinyoosha bastola mbele  na kisha akatulia kama alikuwa hajavamiwa, yule Jambazi aliyekuwa amekaa mbele ujanja ulimuisha kwani aliyekuwa na silaha ya moto alikuwa ni mmoja pekee na ndiyo huyo alikuwa ameshalazwa usingizi.



****


  Tarakilishi zote nne kwa muda huo zilikuwa zipo ndani ya nyumba ya EASA kwenye ofisi maalum, nenosiri lote kwa ujumla lilikuwa limeshapatikana na limeungwa kutokana namba za Tarakilishi hizo zilivyo. Lilikuwa ni neno ambalo halikuwa na maana kabisa kwa jinsi lilivyokuwa limeandikwa ingawa aliambiwa kuwa lilikuwa na maana kubwa sana kwa jinsi lilivyokuwa limeandikwa kimafumbo. BARA JANGWA NA USTARABU LIWE NA MAHAJAJI ALEKUWA UMRA UA HIJA, ndiyo lilikuwa ni neno ambalo halikuwa limeandikwa kisarufi zaidi na pia halikuwa na maana ilinyooka mbele ya Norbert. Utaalamu  wote wa kuchambua maneno ambayo yalikuwa yana mafumbo kwenye neno hilo alijikuta akishindwa kwani lilikuwa limefumbika zaidi kwa jinsi lilivyokuwa limeandikwa, aliona kabisa kulikuwa kuna umuhimu wa kuweza kumtaufuta Jama ambaye muda huo hakuwa anajua alikuwa amejichimbia wapi kutokana na kupoteza kwenye mazingira ya kawaida. Hapo aliamua tu kuzivunga tarkilishi hizo na kisha akawa anajifikiria jinsi wa kuweza kumpata Jama Wa Majama kwani ndiyo alikuwa ni msaada mkubwa sana, ilikuwa ni muda ambao akiwa anajifikiria hili alijikuta pia akiikumbuka familia yake aliyokuwa ameiacha nyumbani hasa mtoto wake ambaye alikuwa amemdanganya na kumtoroka. Aliona kuwa kazi ndiyo mchawi wa kila kitu lakini hakuwa na jinsi kabisa kwani alikuwa ameshayavulia maji na ilimbidi ayaoge tu,  wingi wa mawazo ndiyo ulifanya wazo hio kuchipuka tena ambalo alilifanya  moyo wake uingiwe na hisia nyingine kabisa. Hisia hizo hakutaka kabisa kuviweka kichwani mwake yeye aliamua kuziondoa na kisha akawa anafikiri zaidi kuhusu kazi, aliamua kuingia tena kazini kwani hakuwa na muda wa kupumzika kabisa kutokana na siku ambazo alikuwa amepewa za kumaliza kazi hiyo na kisha wahusika waliokuwa wamesabaisha mauaji ya wenzake waliyokuwa wapo nchini Kenya kuweza kubainika na  kuweza kutiwa nguvuni.


****


  Upande wa kina Askofu hali ilikuwa mbaya kwani hadi kufikia muda huo aliwakuwa wamshabaini kuwa mwenzao mmoja alikuwa ameuawa, ilikuwa ni pigo jingine kwao kwani huyo alikuwa ni mmoja kati ya vijana tegemezi sana kwenye kazi hiyo hivyo alikuwa akihitajika sana. Kitendo cha Askofu kutoka ndani ya siku hiyo akimuacha huyo hapo ndani kutokana na kuuguza majeraha yake ya kuteguliwa, aliona alikuwa amefanya uzembe mkubwa sana kwani ndiyo alikuwa tayari ameuawa kwa kuvunjwa shingo. Akili yake kwa haraka sana alijua kuwa aliyekuwa amefanya tukio hilo alikuwa ni Norbert moja kwa moja ila hakujua kabisa alikuwa kafika vipi ndani ya nyumba hiyo aliyokuwa ameamua kukaa katika eneo hilo lililokuwa limejificha sana. Uhatari wake ulizidi kabisa tofauti na alivyokuwa kiufikiria hapo awali, hii ilimfanya awe na tahadhari zaidi kwani alikuwa ameshatambua kuwa alikuwa akipambana na mtu ambaye alikuwa ni wa ajabu sana kwa jinsi alivyokuwa akiingia eneo lolote na kufanya tukio na kisha kutokomoea bila hata kujulikana kama alikuwa ameingia. Vijana wake tegemezi had muda huo walikuwa wamebaki wawili tu na mwingine alikuwa yupo ndani ya kituo cha polisi kwani alikuwa amekamatwa vilevile kwa kuingia kwenye mtego wa huyo mtu ambaye alikuwa akiwapa homa kila kukicha. Hakika alichanganyikiwa sana kwani hakutarajia kabisa kuwa ndani ya nchi hii kutakuwa na watu hatari zaidi, alikuwa amejenga dharau kabisa mbele ya watu weusi waliokuwa  wapo nchi hii na sasa aliamini kuwa lisemwalo lipo. Kwani aliweza kuona uhatari aliokuwa amefanyiwa, muda huo alikuwa ameagiza kijana mwingine aende kushughulika na kupoteza ushahidi na sasa yanatoke mengine ya kutokea ambayo ambayo hakutarajia kama yatatokea, alikuwa ametoka kufanya mpango wa kuichezea arafu serikali pasipo kutambua kuwa na yeye alikuwa amefanyiwa mpango wa kuchezewa rafu. Sasa alikuwa akiumia kwa kitu hicho alichokuwa akifanyiwa pasipo kujali kuwa kulikuwa na wengine nao walikuwa wanaumia kwa kuharibiwa kazi na mipango yake kama alivyofanyiwa, ama kweli mkuki kwa Nguruwe tu kwa binadamu mchungu. Kuumia aumie yeye wala hakujali kuwa kulikuwa a wengine ambao walikuwa wakiumia kama yeye kwa mambo aliyokuwa akiyafanya, alizoea kuona sherehe sana kwa wengine kuumia lakini sasa alikuwa ameumia yeye na anaona huo ni msiba mkubwa sana zaidi hata ya kifo cha mkuu wa nchi. Hakika alijiona alikuwa amewaweza wengine kumbe na yeye alikuwa amewezwa vilevile kwa jambo hilo alilokuwa amefanyiwa na mjanja kiakili zaidi yake, upinzani aliozea kuukuta kwa vyombo vya usalama vya magharibi anaukuta ukiwa upo ndani ya vyombo vya usalama vya ndani ya Afrika tena kwenye ukanda wa Afrika ya mashariki. Hakika alidharau sana udogo wa sindano bila ya kutambua udogo huo ilikuwa ikifanya mambo makubwa, udogo wa kudharauliwa ilikuwa ikishona koti zito kabisa hilo alikuwa amesahau na sasa ilikua imemdhihirishia kuwa ilikuwa na uwezo kuliko kawaida.


****

 
  Muda huo Askofu alikuwa ametoka kusuka mpango na Josepine wa kuzidi kuwaumiza wengine waliokuwa wapo kazini kama yeye, alikuwa ametoka kusuka mpango wa kwenda kumuangamiza mwenzao aliyekuwa yupo kwenye mikono ya polisi kituo cha Oysterbay baada ya kukamatwa nyumbani kwa Kaboneka alipotumwa. Alikuwa amefeli kwenye kazi yake kwa namna ambayo yeye aliita ni namna ya kijinga sana sasa alitakiwa kuangamizwa mara moja akiwa yupo kwenye mikono ya polisi kutokana na uzembe huo aliokuwa ameufanya. Aliposuka mpango huo na Josephine na kisha kaondoka alimuacha Mwanamke huyo aliyekuwa amempa kazi hiyo akiwa yupo katika maandalizi ya kwenda kuitekeleza kazi hiyo.


 Josephine alitoka ilipo ofisi yake akiwa na muonekano mwingine kabisa, alikuwa ameweka nywele kwenye mtindo mpya kabisa na usoni alikuwa na miwani ambayo ilimfanya aonekane kama mwanamke ambaye alikuwa mtafutaji na wala siyo golikipa. Aliingia kwenye gari nyingine ambayo ilikuwa ni ya gharama sana akiwa anaelekea huko kituoni kwani ilikuwa imepigwa simu hapo na aliongea na huyo mwanzao aliyekuwa amekamatwa hapo kituni, alikuwa akija hapo akiwa na muonekano wa wakili aliyekuwa akija kumtetea hyo kijana.

  Muonekano wake pamoja na kitambulisho cha kufoji alichokuwa amekibebea haukupingwa kabisa na maaskari wa kituo pindi alipofika na kujitambulisha na kisha kutaka kuonana na Mteja wake. Alipewa nafasi hiyo ya kuongea na Mteja wake kabla hata hajaaza kuhojiwa,alipoipata nafasi hiyo ndiyo aliona ilikuwa ni nafasi pekee ya kuweza kutumiza adhma hiyo wakiwa wapo wawili tu.

"Kwanini unakuwa mzembe hivyo?" Alimuuizaa pindi alipoachiwa nafasi ya kuongea naye

"Si uzembe ila ndani ya nyumba ile kulikuwa na yule mwandishi wa  habari"

"Nani Norbert?"

"Huyo huyo alikuwa amekaa nyuma ya mlango katika muda ambao mimi nilikuwa nikiingia ndani ya nyumba hiyo ndiyo maana akaniwahi"

"Sasa wewe kweli ulikuwa unaingia ndani ya nyumba ya mtu ambaye humjui vizuri na wala hupajui palivyo kama kondoo vile"

"Nilikuwa tayari nimeshautuliza ulinzi wa nyumba uliokuwa upo chini ya mlinzi mmoja hivyo sikuwa na wasiwasi kabisaa"


"Kwahiyo ndiyo ukadhania kuwa mlinzi ndani ya nyumba hiyo yupo mmoja tu?"

"Ndiyo"

"Damn! Umefanya kosa kubwa sana ila hatuna budi kukusadia kwani kiongozi amesema utolewe mara moja" Josephine alimueleza kwa sauti ya chini sana na kisha akamtazama yule kijana ambaye alikuw akimsikiliza kwa umakini, alipopewa ishara ya kukubali kutolewa huko aliamua kupanga hila yake. Alimuambia, "Unahojiwa ukiwa upo mbele yangu kama wakili wake hivyo usiwe na hofu kil kitu nilikuwa nimekipanga kama kilivyo".

  Hapo walipeana mikono wote kwa pamoja na kisha wakaeleka kwenye chumba cha mahojiano kwani walikuwa wameomba kuongea muda mfupi tu, huko walikuta maafisa ambao walikuwa wakiwasubiri ambapo mahojiano yalianza mara moja. Kutokana na kuwepo kwa Josephine wakijua kuwa alikuwa ni wakili wake mahojiano hayo yalifanyika kwa taratibu na kistarabu sana, maaskari walikuwa wakihofia kuwekwa hatiani na Wakili kwani ilikuwa ikitambulika kabisa walikuwa hawatakiwi kuwapiga watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi. Laiti wangenyanyua mkono na kumpiga basi walikuwa wakizidi kumuweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kujiteteta huko Mahakamani hata kama angekubali  kuwa alikuwa akihusika kwenye tuhuma hiyo aliyokuwa amekamatwa nayo


 Walihofia huyo waliyekuwa wanamuona ni wakili angeweza hata kuwageuzia kibao Mahakamani akawaambia kuwa walitumia nguvu kumlazimisha na Mteja wake alikiri kutokana na hofu aliyokuwa nayo baada ya kutumika nguvu nyingi katika kumfanya akiri. Hizo zilikuwa ni mojawapo wa hila ambazo walikuwa wakizitumia mawakili katika kumtetea Mteja wake hivyo waliogopa kabisa zisije kutumika kwao kwani zingeweza kuwaweka pabaya kwa kuvunja sheria na pia kuhariu ushahidi muhimu sana kwenye kesi pindi itakapofunguliwa.


  Mahojiano yalipomalizika Mtuhumiwa alirudishwa kwenye chumba cha selo alichokuwa amehifadhiwa na kisha jalada lilifunguliwa ili asiweze kukaa ndani ya kituo hicho, ulikuwa ukisubiriwa muda mzuri wakuweza kumpeleka rumande tu wakti akiwa anaendelea na kesi yake. Muda huo Josephine aliondoka kwenye eneo hilo la kituo cha polisi kwani kazi yake iliyomleta hapo ilikuwa imeshakamilika na hakuwa na la ziada. Alikuwa amewaachia kisanga maasakari wenyewe kwa kijana huyo, jambo ambalo halikuwa limejulikana na maofisa hao wa jeshi la polisi ilikuwa ni kwamba Josephine alikuwa amemuwekeawsumu ambayo ilikuwa ikiingia ndani ya ngozi yule mwenzake. Pale waliposhikana mikono baada ya kuongea kwa pamoja ndiyo alimtilia sumu hiyo  na kisha yeye mwenyewe aliingiza mkono ndani ya mkoba wake na kugusa dawa ya maji ambayo ilikuwa ni kinga kisha akaelekea kwenye mahojiano hayo.


  Ulipofika muda wa kumpeleka rumande ndiyo kuliibuka kwa kizaazaa kwa Maasakri hao wakaona kuwa walikuwa na  balaa lililokuwa likiwangojea, walipoenda kumtoa yule Kijana kule selo walikuwa akiwa amelala  na mwili ake ukiwa umebadilika rangi kabisa na kuwa mweusi. Wote kwa pamoja walishtuka sana na walienda kutoa taarifa kwa wakubwa zao ambao nao walipatwa na mshtuko sana, waliona walikua na hatari kubwa ya kujibu kesi nyingine kwani yule waliyekuwa wanamdhania ni wakili alikuwa akioneakana kabisa alikuwa yupo makini sana na kazi yake. Hawakutaka kabisa kuugusa mwili wake na walichoamua ni kuita Askari aliyekuwa na taaluma ya udaktari waweze kumuangalia, baada ya robo saa  alifika Askari huyo akiwa na nguo za kiraia ambako kutokana na ukubwa wake kicheo baadhi ya maaskari walimpa heshima yake na kisha aliingia ndani ya chumba hicho cha selo. Alipouona tu huo mwili alijikuta akiweka mkono kidevuni mwake na akaanza kukuna kidevu chake kilichokuwa hakina ndevu kutokana na kuzinyoa mara kwa mara, alipoacha kukuna aligeuza macho na kumtazama Askari ambaye alikuwa akikaribiana naye kicheo.

"Rangi hii ya ngozi ni dalili tosha ya kuwa aliuawa kwa sumu, sasa inabidi tuchunguze ili kuhakikisha hilo" Aliongea huku akivaa mipira ya mikono.

ITAENDELEA!!



UKIHITAJI RIWAYA HII KUANZIA ILIPO HADI MWISHO, BEI NI  SHILINGI 2400. WASILIANA NASI KWA NJIA YA UJUMBE MFUPI WA  MANENO(SMS) KWENDA NAMBA +255762219759 AU WHATSAPP +255713776843

No comments:

Post a Comment