Saturday, February 18, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA KUMI NA SITA



WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com




SEHEMU YA KUMI NA SITA!!
Alimsogezea Josephine ambaye alishtuka sana akiwa haamini kwani walikuwa amehangaika sana, alimpatia Spider ambaye alijikuta akiinamisha uso wake na huku Tarakilishi hiyo akiiweka pembeni.

"Aaaargh! Norbert hii ni too much sasa, naingia mwenyewe kazini haiwezekani tuhangaike kote aje kufagia akaunti yote" Akosfu Valdermar aliongea




________________TIRIRIKA NAYO

 Ilkuwa ni suala ambalo lilikuwa likitosha kabisa kumfanya yule mwenye moyo mwepesi kuweza kupoteza fahamu hata kufa kwa mshtuko kwa jinsi lilivyokuwa limetokea, akaunti yao ya benki ambayo walikuwa wakiitumia kwa ajili ya kazi hizo haramu ilikuwa imesafishwa yote. Hakukuwa na hata na senti tano kwenye akunti yao hiyo ambayo walikuwa wameifanyia kazi, ilikuwa na zaidi ya mabilioni lakini yote walikuwa hawayaoni. Waliona kama macho yao yalikuwa yameingia ukungu waisome kwa sasa lakini haikuwa hivyo, jambo walilokuwa wakilishuhudia hapo lilikuwa halisi kabisa. Wote waliumia sana kwani hiyo ndiyo ilikuwa akaunti yao kubwa na sasa ilikuwa imeshasafishwa, wote hawakuwa na kumlaumu juu ya hilo isipokuwa Norbert tu ambaye ametoka kuchukua namba zake tu mchana wa siku hiyo na sasa  ilikuwa imesafishwa. Hiyo waliamini ilikuwa ni mbinu hatari ya waliofuzu kwa kiwango kikubwa katika matumizi ya Tarakilishi ingawa hawakujua kabisa aliyefanya hivyo alitumia njia gani, hakika walipatikana ndani ya siku hiyo na walikuwa wakitakiwa kuanza moja katika biashara hiyo.

"Yaani akaunti ikaribie kufika Trilioni ndiyo asafishe kweli nase hivi sikubali" Aksofu Vldermra aliongea

"Nikimshika nitamkata vipande vipande huyu mshenzi hii ni too  much" Scorpio naye aliongea kwa hasira huku akiuma meno.

"Yaani sijui nitamfanya kwa jinsi nilivyokuwa na hasira kwani bado ana kisasi changu halafu anazidi kutushusha nguo za ndani maana nguo za juu katuvua huyuu" Josephine naye aliongea kwa hasira sana hadi macho yakawa yanalengwa na machozi, muda huohuo Akosfu Valdermar alinyanyuka na kisha akaingia ndani bila ya kusema chochote. Alikaa kwa takribani dakika moja na alirejea akiwa ameshika mkoba wa namba ambao alimpa Khemiri, mkoba huo ulipokelea kwa mikono miwili na mlengwa  huku akiachia tabasamu.

"Huu mzigo unahitajika uutoe ndani humu na kisha uuweke kwenye kasha zile si unaona tumekombewa hapa nahitaji tujiinue tena" Alimuambiana kisha alimtazama usoni kama alikuwa ameelewa, alipoona alikuwa ameelewa alimruhusu kuondoka eneo hilo akimuambia walikuwa na mpango mzito wa kupanga hivyo kazi ilikuwa imeishi hapohapo hakukuwa na jingine jipya. Hapo Mlengwa aliondoka akiwa amebebea mzigo huo muhimu aliokuwa amekabidhiwa na wenzake

   Zilipopita dakika kadhaa tangu aondoke  wote waliokuwa wapo chini ya Akosfu waligeuza macho na kumtazama usoni, wote hawakuwa wameelewa kwanini alikuwa amefanya vile kwa mtu ambaye hakuwa adui yao. Walikuwa wakitambua kabisa kuwa mkoba aliokabidhiwa Khemiri ulikuwa ni aina ya nyingine ya bomu ambalo halina tofauti na bomu la barua, bomu hilo ukifunguliwa mkoba na hewa kuingia ndani hata sekunde mbili haifiki hulipuka haohapo. Sasa alikuwa amemkabidhi Khemiri ambaye alikuwa ni mtu waliyefanya naye kazi nyingi san,waliona alikuwa amekosea sana kumkabidhi huo mzigo lakini hawakutaka kumkosoa ndani ya muda huo kabla hajafafanua.

"Madam kwanini unampa sumu ile jamaa wakati ni mtu wetu mkubwa inamaana hana umuhimu tena?" Josephine aliuliza

"Yule ni Kondomu tu ikishatumiika haina maana" Alijibu kimafumbo zaidi.

"Kondomu ikitumika ni kutupwa kwani haitokuwa na ubora ule wa awali, ndiyo kama huyo kwa sasa hana ubora huo ndiyo maana kafanya uzembe mkubwa sana" Aliwajibu zaidi

"Lakini wakuu hawatatuelewa kwenye suala kama hili Madam hebu fikiria" Spider naye alishauri

"Ikiwa ameonekana na Norbert basi  jua atamtumia  kama daraja ili atufikie sisi,sasa mimi daraja nalivunja ili asifike upande wetu tu maana atakuwa ni hatari sana" Alifafanua

"Hapo sawa tumekupata, umefanya la msingi sana" Josephine aliongea baada ya kuelewa lengo la Askofu kupanga mpango huo wa kumuangamiza Khemiri wakati alikuwa ni mtu wake wa karibu sana.

"Tulikuwa tumepunguza mzigo yeye anatuletea mzigo mwingine, hiyo ndiyo alilostahiki hakuna jingine"



****


  Hakuwa akiwaza kabisa kuwa alikuwa amebeba  kiama chake mwenyewe,  alipotoka tu kule kwenye makao ya washirika wake aliondoa gari haraka sana akiwa analekea nyumbani kwake. Alikuwa akiutupia sana macho ule mzigo aliokuwa ameubebea ambao aliona ulikuwa na uzito mkubwa sana, moyoni alishukuru kabisa kwa suala kama lile ambalo lilikuwa limeharibika kisa yeye wenzake kumuelewa na kulimaliza kwa namna ya kistarabu sana. Hakujua kabisa kuwa hakuwa ameeleweka na alikuwa amebeba adhabu yake ambayo alikuwa akihitaji kupatiwa kutokana  na uzembe aliokuwa ameufanya, kuweza kumuamini Norbert kisa kusikia hela nyingi ilikuwa ni uzembe mkubwa sana ambao hakutakiwa kuufanya. Kushindwa hata kumchunguza huyo adui yake hakujua kabisa kuwa alikuwa akijichimbia kaburi wakati anatoa maelezo hayo, sasa alikuwa amebeba tiketi yake ya kuzimu ndani ya gari hiyo akiwa hajielewi kabisa.

 Nyumbani kwake kulikuwa ni Mbezi katika kwenda huko alipofika mataa ya mwenge alikuta taa zilkuwa nyekundu, hapo ilimbidi asimame aweze kusubiri magari ya upande mwigine yaweze kusimamishwa na taa hizo ndiyo na yeye avuke. Akiwa kasimishwa ndiyo alijikuta akipata  wahka wa kufungua mkoba huo wa namba, kwakuwa namba alikuwa akizijua haikumuwia vigumu kwani mikoba ya umoja wao ilikuwa ikitumia namba za aina moja yote. Aliweka namba hizo na kisha sehemu ya vibanio za kufunga mooba huo zilifyatuka na kumfanya atabasamu, alipovuta kufungua ndipo kilipotokea kizaazaa kwani alijikuta akirushwa juu huku ukiambatana  mlipuko mzito sana.


   Hilo lilikuwa ni tukio la kushtusha sana kwa watu waliokuwa wapo jirani na gari hilo hasa magari ya jirani, wote walikumbwa na athari za mlipuko ikiwemo kuruka kwa vioo na pia moto kufika kwenye mgari yao na kuanza kuunguza. Nao walijikuta wakikimbia wakaacha magari hayo huku waliojeruhiwa wakibaki ndani ya eneo. Mayowe ya watu waliokuwa na uoga yalisikika kwa nguvu sana kwani hazikuwa hata zimepita siku mbili tangu watu waanze kuawa ndani ya jiji sasa lilikuwa likitokea tukio hilo, hakuna ambaye alikuwa hajipendi kuendelea kukaa eneo hilo wote walikimbia kwani waliona kulikuwa kumevamiwa. Waliliacha gari ambalo yeye mwenyewe alikuwepo humo ndani akitekea kwa moto, ilichukua dakika kadhaa Askari wa jeshi la polisi wakawa wamekifa ndani ya eneo hilo wakiambatana na wenzao wa zimamoto. Moto ulihangaikiwa kuzimwa na ulipozimika ndilo walipohangika katika kuutoa mwili uliokuwa upo ndani ndani ya gari hiyo, baada ya hapo walianza kukagua gari hiyo wakiangalia bati la namba za gari hilo kuweza kutambua mmiliki wa gari hilo kupitia namba zake. Walipozipata namba za gari hilo muda huo vyombo vya habari vilikuwa vimeshafika eneo  hilo na walikuwa wakihitaji kwa kina maelezo yao. Walitumia wasaaa huo kuanza kuwaeleza juu ya hali halisi iliyopo hapo hadi kukatokea hayo, pia waliwatajia namba za gari hilo wakiahidi kuwa uchunguzi ulikuwa ukiendelea.



****




  Habari hiyo ilikuwa imefika katika muda ambao Moses alikuwa yupo mke wake Beatrice aliyekuwa akinyonyesha mtoto wao, wote wawili walipigwa na mishangao tofauti kutokana na habari hiyo iliyokuwa ikitangazwa. Mshangao wa Beatrce ulikuwa ni juu ya mfululizo wa matukio hayo ambapo aiingiwa na uoga mkubwa sana kuhusu tukio hilo, aliona ile hatari ambayo ilikuwa ikitajwa kuwa ilikuwa imeisha baada ya Mhusika kukamatwa ilikuwa ikiendelea kama kawaida haikupita muda mrefu kupitia vyombo vya habari mwenye gari hiyo aliweza kufahamika wakiwa bado wapo hapohapo. Moses  mwanzo alikuwa na mshangao wa juu ya mauaji hayo yalikuwa yakilenga kuharibu ushahidi muhimu, lakini alipopata taarifa za namba za mmiliki wa gari hilo alijikuta akihisi suala hilo lilikuwa likilenga kumuharbia kazi Norbert kwani siku zilikuwa zinayoyoma zaidi. Alikuwa akijua kabisa kuwa Norbert alikuwa ameshamjua  kuwa mtu huyo alikuwa ni mmojawappo  kati ya watu waliokuwa wapo ndani ya mtandao wa kifisadi na sasa alikuwa ameuawa, hapo alihisi mbio za Norbert kwa hatua moja zilikuwa zimeanza kugundulika.

"Halafu baby hii kesi nimeletewa ujue" Beatrice alimuambia

"Ksi ipi hiyo my wife" Alimuuliza

"Si hii ya kumtetea Mheshimiwa Kabinuki, yaani wameniwekea dau kubwa nimtetee" Moses aliposikia hivyo aliona kuwa mke wake alikuwa akielekea kuingia katika upande mgumu sana ilihali bado alikuwa akimuhjitaji.

"Mke wangu hivi unataka hela au unataka maisha yako?" Alimuuliza

"Maisha yangu ni muhimu zaidi"

"Basi usiingie kwenye kesi hiyo waachie mawakili wengine"

"Kwanini?"

"Mke wangu nchi hii na serikali yake ina mengi sana angalia utajiweka matatani ni mtandao huo"

"Lakini hii ni taaluma pia"

"Hivi kumtetea mtu ambaye anachukiwa na watanzania ili awe huru utaniweka kundi gani mumeo?" Swali hilo lilimfanya Beatrice anyamaze kabisa kwani alikuwa akitambua kabisa heshima iliyokuwa imechafuka  baada ya mume wake kupakaziwa jambo ilikuwa imerejea, sasa aliona kweli alikuwa akielekea kuichafua heshima hiyo kwa mara nyingine.

"Sawa mume wangu hapo nimekuelewa sitokubali ofa yao"

"That's my wife"

"Kwasababu nakupenda ndiyo maana, halafu Mzee Kabaita alipiga simu wakati ukiwa bado hujarudi alikuwa na shida na wewe"

"Mh! Ngoja nitaenda kumuona siku ya kesho nyumbani kwake"

"Yaani kakuambia ufanye haraka sana kwani ana jambo la muhimu sana"

  Muda huo waliokuwa wakijadili mambo hayo tayri Mzee Kabaita alikuwa ameshajitoa kwenye siasa na alikuwa  akifanya mambo yake mengine kabisa mbali na siasa. Hakuwa na mtoto na alikuwa akiishi na mke wake ambaye ndiyo alikuwa ni faraja kwake, alikuwa akiwasiliana na pia kuongea na Moses juu ya mambo mbalimbali kwani walikuwa wakiheshimiana sana kama mtu na mwanae, ndiyo maana taarifa hiyo Moses hakutaka kuipuuzia kabisa aliona ilikuwa na uzito wake ndiyo maana alitaka kwenda huko moja kwa moja.


****

     
     [6]
  Asubuhi ya siku iliyofuatia zikiwa zimebaki siku sita kwenye kazi ambayo aalikuwa amepewa Norbert, wakili mwingine kabisa alitafutwa kwenda kutetea kesi ya Mheshimiwa Kabinuki baada ya Beatrice kukataa. Ndani ya asubuhi hiyo Mheshimiwa huyu ambaye alikuwa ameshuka thamani yake, alitolewa kwenye gereza la Segerea akiwa yupo chini ya ulinzi mkali sana kwani ilikuwa ni siku ambayo kesi yake ilikuwa ikisikilizwa kwa mara ya kwanza. Nchi nzima ilikuwa ikitambua kabisa kuwa ndiyo ilikuwa ni siku maaluma ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, alipandishwa kwenye gari maalum alilokuwa ameandaliwa kwa usalama wake na msafara ulianza mara moja. Msafara huo wenye ulinzi mkali sana ulipofika eneo la jirani kabisa na Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu walikutana na idadi kubwa ya wanachi wakiwa wamejaa kwenye mahakama hiyo, wananchi wote walikuwa wamebeba mabango yaliyokuwa yakimlaani kabisa Mheshimiwa huyo. Yeye mwenyewe alipoyaona alijikuta akilia kabisa akiona dunia ilikuwa imemuhukumu na hakuwa na hatia yeyote, msafara huo ulipokaribia kuingia kwenye lango la magari la Mahakama hiyo iliyokuwa ipo maeneo ya Upanga, iliwabidi maofisa wa jeshi la polisi wafanye kazi ya ziada ya kurudisha watu nyuma kwani walikuwa wakileta fujo sana huku wakimtukana Mheshimiwa huyo.

  Msafara uliingia ndani kabisa ya mahakama na ulienda kwenye sehemu maalum, hapo Mheshimiwa Kabinuki aliteremshwa  akiwa amewekewa ulinzi mkali sana. aliingizwa kwenye chumba cha kusubiri kwani muda wa kesi yake haukuwa umefika, baada ya nusu saa muda ulikuwa umefika tayari na alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza ndani ya maisha yake kwa tuhuma ambayo haikuwa yake. Chumba cha mahakama chote kilikuwa kimesheheni waandishi wa habari ambao walikuwa wamekuja kuchukua matukio muhimu yaliyokuwa yakihusu kesi, baada ya muda mfupi Hakimu aliyekuwa na jukumu ndani ya kesi hiyo kwa siku hiyo alikuwa akihitajika kuingia ndani ya chumba cha Mahakama.

"Kooorti" Ilitolewa kauli hiyo muda ambao Hakimu alikuwa akiingia ndani ya chumba cha Mahakama, watu wote walisimama na Hakimu aliyekuwa amevaa vazi lake nadhifu alionekana akiingia ndani ya chumba cha Mahakama. Aliketi kwenye kiti chake mbele kabisa na watu wote ndani ya chumba hicho waliketi nao, baada ya hapo utaratibu ulianza mara moja.

  Muendesha Mashtaka alisimama na kuanza kusoma mashtaka   yaliyokuwa yakimkabili Mheshimiwa Kabinuki, kwakuwa mahakama hiyo haikuwa na uwezo kuiendesha kesi hiyo. Mheshimiwa Kabinuki aliamriwa asijibu chochote, kesi hiyo ilitajwa na kisha ikapangiwa tarehe ya kwenda kusikilizwa Mahakama kuu ambayo ilikuwa ina uwezo wa kuendesha kesi hizo. Alirudishwa tena rumande kwani kesi yake kutokana na uzito wake hakuweza kupata dhamana, muda huo kila kitu kilirushwa kwenye vyombo vya habari kuhusu kesi hiyo ambapo kwa wale waliokuwa hawajui utaratibu wa kisheria waliona kama kesi hiyo ilikuwa ikichelewa kutolewa ukumu kwa jinsi walivyokuwa wakimchukia Mheshimiwa Kabinuki.


****

  Muda ambao Mheshimiwa Kabinuki alikuwa akielekea gerezani Norbert alikuwa yupo kwenye tarakilishi yake, alikuwa akisikiliza kile ambacho alikuwa amekitegea mtego katika siku iliyopita pale alipokutana na Khemiri. Yalikuwa ni mazungumzo  kati ya Khemiri na kundi la wahalifu wenzake baada ya yeye kuweza kumtoroka kule bandarini, alikuwa tayari ameshafanya ujanja katika muda ule ambao alikuwa amekutana na Khemiri kabla hata hawajaingia ndani ya Bandari. Kitendo cha Khemiri kupenda kusalimiana na watu kwa kushikana mikono kutokana na kuwa ni Muislamu aliyekuwa akikanyaga msikiti ila hakuacha maovu, alijikuta kiwa amempa nafasi adimu sana Norbert kwani kushikana huko alikuwa akipenda sana kupeana salamu ya kukumbatiana na kwa kugusanisha mabega ambayo mara nyingi husalimiana vijana wa sasa. Pamoja na kukumbatiana huku hakukuwa kupo kwenye sheria za dini yake yeye alipapenda sana kutokana na kuizoea kwenye genge lake , alipomkumbatia namna hiyo Norbert baadaya kushikana naye mikono ndipo alipowekewa kifaa kidogo sana. Kifaa hicho kilikuwa kina uwezo kurekodi eneo ambalo alielekea hadi anatoka na pia kunasa sauti. Sasa Norbert alikuwa ameshafanikiwa kureodi vyote na muda huo alikuwa akiyapitia maongezi hayo yote, aliyaskiliza kwa umakini akiwa amekaa kwenye  kiti ndani ya nyumba ya EASA. Baada maongezi hayo kuisha alisikiliza sauti zilizokuwa zikifuata hadi pale Khemiri alipopanda gari yake na kuondoka ndani ya eneo hilo, njiani alipokuwa akiendesha gari aliweza kusikia jinsi alivyokuwa akiongea na watu mbalimbali ka kutumia simu yake ya mkononi. Sauti ilikuja kukatika baada ya kutokea mlipuko ambako alisikia kishindo na kisha sauti ikakata, alipomaliza kusikiliza alijikuta akitabasamu kama ilivyo kawaida yake na kisha akatazama kwenye kioo cha Tarakilishi akifungua faili jingine. Aliweza kuona nyendo zote ambazo alikuwa amezipitia Khemiri tangu alipotoka bandari  na hadi anafika kwenye nyumba yenye makao yao, eneo hilo alilikariri pamoja na kuchukua kifaa kingine ambacho alikitia faili hilo. Hicho kilikuwa kifaa ambacho kilikuwa kina uwezo kumuongoza hadi ndani ya eneo husika kwa kutumia rekodi iliyokuwa imechukuliwa hapo awali"

"Kazi kwao" Alisema na kisha akakichukua kifaa hicho na kunyanyuka kitini.



ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment