Saturday, February 11, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA TISA

WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com






SEHEMU YA TISA
Norbert alinakili anuani za makazi ya mmiliki huyo akiwa amemuweka kwenye orodha ambaye alitakiwa kuipitia kwa ajili ya kazi yake hiyo iliyokuwa ikimkabili.

"Tandu ana miguu mingi sana na kila mguu hutoa mchango wake katika safari yake,nina imani yote nitaifikia" Aliongea mwenyewe huku akimkazia macho mmiliki wa kampuni hiyo ya usafirishaji.





__________________TIRIRIKA NAYO

 Majira ya usiku magari yote mawili yaliyoondoka eneo la Yombo kule kulipotokea mlipuko, yaliingia ndani ya nyumba moja ya kifahari sana iliyopo maeneo ya Kibada. Josephine pamoja na  Scorpio walishuka na wote waliingia ndani ya nyumba hiyo ambako walipokewa na Mzungu mwingine anayeItwa Spider ambao ni watu wa karibu sana wa Askofu Valdermar. Alikuwa ni yuleyule ambaye alikuwa naye pamoja na Scorpio katika siku ambayo walimuwekeea Norbert bomu  katika msitu wa Serengeti wakijua alikuwa ni mtumishi  wa kiimani aliyekuwa amekataa kwenda kinyume na matakwa yao, sasa wamerejea nchini kwa pamoja wakiwa muonekano tofauti sana na ule wa kiutumishi wa Mungu. Safari hii walikuwa na muonekano wa watu waliokuwa wakijiweza kiuchumi ambao walikuwa wameamua kuja kuishi nchini Tanzania, wote kwa pamoja waliingia  kwa kazi moja maalum na waliingia kwa nyakati mbili tofauti sana kama vile watu wasiojuana  hata kidogo.


  Walikuwa wakitambulika kama wazungu waliokuwa na uraia wa nchi tofauti kabisa na idara ya uamiaji lakini yote ilikuwa ni kuipumbaza serikali  isiwe na shaka juu yako, wazungu hawa walipoonanaa hapo ndani waligoengesha mkono yao kihuni zaidi na kisha Josephine na Spider wakakumbatiana kama ilivyo salamu wakikutana pamoja. Wote waliongoza njia hadi ndani kabisa na nyumba huyo ya kifahari kwenye sebule pana kabisa, hapo walikutana na Askofu Valdermar mwenyewe akiwa ameketi akiwa na mavazi ya kulalia tu.

   Mikononi mwake alikuwa ameshika bilauri ya mvinyo huku akiangalia luninga, Askofu huyu wa kuzimu ali[owaona tu hao vijana wake aliweka kinywaji mezani kisha akasimama. Alienda hadi walipo vijana hao na alianza kupeana salamu na kila mmoja, alianza na Josephine ambaye walipeana mabusu ya kwenye mashavu kisha akasogea hadi Scorpio ambaye alinyooshewa mkono na Askofu huyo. Yeye kunyooshewa mkono huko kulimfanya aushike mkono wa Askofu huyo kuzimu na kisha akaubusu halafu akakumbatiana naye, baada ya hapo kila mmoja alitafuta mahali pa kukaa kwenye sebule hiyo kwani tayari walikuw wamaeshajulikana kuwa walikuwa na zaidi ya jambo la kuongea muda huo.

 "Ujio wenu unaashiria kabisa kuwa kuna jipya lipi hilo" Askofu Valdermar aliuliza

"Madam knbwa zaidi ni kwamba Kelvin amekwenda na maji, hii inaonekana kuna mtu yupo nyuma ya nyayo zetu akitufuatilia" Scorpio alieleza

"Je hakuacha ushahidi wowote huko eneo la tukio wa kuwaweka ninyi hatiani? Waliulizwa

"Aliacha Subaru ile ambayo ina pean code ila tumeiwahi tayari na tumeileta hapa ndani" Josephine alijibu

"Vizuri sana sasa ibadilini namba za usajili pamoja na stika zote" Aliwapa  amri na kisha akawatazama mmoja baada ya mwingine na akauliza, "ni nyinyi mliyeigonga pikipiki Buguruni mchana wa leo?"

"Ndiyo Madam ni sisi" Josephine alijibu


"Kulikuwa na haja gani ya  kumgonga ile pikipiki kinyama namna ile ikiwa dereva mwenyewe ni normal person? Waliulizwa


"Chanzo ilikua si dereva bali abiria aliyekuwa amembeba" Scorpio alijibu.


"Ok nipe habari yote si nusunusu" Alihitaji kupewa habari yote

"Norbert Kaila ndiyo kiumbe aliyekuwa abiria wa ile pikipiki its better to be wanted for his murder rather to let him  (ni bora kuwa tunatfautwa kwa mauaji yake kuliko kumuacha) apumue ndani ya mgongo wa ardhi" Josephine alifafanua kwa maelezo ambayo yalihitaji ufafanuzi zaidi kwa mkuu wao huyo.

"How(kivipi)?" Alihitaji ufafanuzi

"Ni jasusi wa EASA mwenye code N ya kwanza kabisa maarufu kama N001 nafikiri ushasikia habari za huyo mtu" Josephine alifafanua

"Oooh! No! Sasa mmejiweka pabaya zaidi nyinyi, maiti yake haijonekana eneo la ajali zaidi ya kuonekana ya dereva wa pikipiki tu yule" Askofu Valdermar safari hii alisimama wima alipoongea maneno hayo kisha akawatazama vijana wake.

"Hii inaonesha amekwepa mdomo wa kifo na kama alikuwa hajajua uwepo wenu basi ndiyo mmempa ishara ya kuweza kuwafuatilia" Aliwaambia na wote walichoka na taarifa hiyo kwani hawakutegemea kabisa kama angeweza kutoka kwenye ajali ile ndiyo maana hawakuhangaika kabisa kuangalia kama alikumbwa na kadhia ile.

"How come? Amepona vipi pale huyu?" Scorpio aliuliza kwa mshngao sana


"Inaonekana ni mwenye hisia za ajabu na pia uwezo wa juu wa kutumia sense organs zake, sasa wekeni macho ya umakini na kuanzia sasa ni mwendo wa kupoteza ushahidi tu hakuna jingine tumeni wito kwa watu tofauti kabisa maana washajua hawa tupo after ile ripoti" Askofu Valermar aliwaambia

"Ingependeza zaidi na huyu kiumbe tukampoteza ndani ya siku chache tu kwani yeye ndiye aliyeipoteza timu nzima iliyobaki kidogo tuichukue nchi hii" Josephine aliongea na kumfanya Askofu Valdermar amuangalie huku akikumbuka vifo vya vijana wake ambao wengine alikuwa akiwatumia kimapenzi kabisa tofuati na mume wake wa haramu.


"Huyo hakikisheni mnamleta kwangu akiwa yupo hai ni mimi ndiyo nitajua nini cha kufanya, kwa sasa andaeni silaha nataka ziende kwenye masanduku tofauti ya posta usiku huu huu asubuhi yaanze kazi" Aliwapa amri na kisha alinyanyuka hapo sebuleni akiwaacha vijana wake wenyewe.



"Hivi kaponeje yule kiumbe na mzinga ule niliobamiza?" Aliuliza akionekana ni mwenye kuchnganyikiwa kabisa

"Scorpio yule ni mwanaharamu msikie tu, ana akili kama ana dawa vile" Josephine aliongea

"Inaonekana ni kiumbe mwenye uwezo wa hali ya juu sana na kama hawa Africa wapo wachache sana na inabidi wapotezwe kabisa tuzidi kupata madili" Spider naye alichangia

"Kabisa Spider huyu mara ya pili akionekana mbele ya mcho yetu basi ni kumpiga risasi tu hata kwa sniper au kumuua kwa mkono" Scorpio alichangia

"Akili nyingi zinahitajika kuweza kupigana na kiumbe huyu kuliko hasira. Benjamin na Thomas walipotea walipoleta hasira kwa huyu kiumbe, ni mtu mwnye kutumia akili hata akiwa amewekewa silaha na si mwenye kuingiwa na hofu kabisa" Josephine aliongea na kisha akainuka akaenda hadi lilipo jokofu la vinywaji ndani ya nyumba hiyuo, alitoa chupa moja ya mvinyo na akaelekea mezani ambako alichukua bilauri akaumimina mvinyo huo. Baada ya hapo alirejea sebuleni walipo wenzake ambao walikuwa wakiongea mambo yao ya kawaida tu

"Madam atajua jinsi ya kuwatuliza waheshimiwa Laptop tunsyo moja na bado neno la siri sidhani kama lina maana ndani yake" Aloongea alipofika mbele yao ukiwa akiwakaribisha bilauri hiyo ya mvinyo kiishara.


"Nenola humo linasemaje?" Spider aliuliza

"BARA JANGWA  ndiyo nimelikuta kwenye faili lenye neno la siri bado hatujajua jinsi la kulidadavua hili,Laptop aliyoenda kuifuata Kelvin ilikuwa na neno siri jingine na  baadhi ya ushahidi hivyo tatu zilizobakia ambazo ni namba mbili  tatu na nne ndiyo zina ukamilifu wa hili fumbo kwa mujibu wa kibaraka wetu aliyekuwa yupo TISS. Ya mwisho ina vielelezo vingine vyote ila kiumbe mmoja anayeitwa Jama aliyeshiriki utafiti huu bado anapumua na sumu ilimpata mke wake, tujue maneno ya siri yote yakikusanywa mbele yake wakubwa tumewaweka pabaya na sisi ulaji hatuna kabisa jamani" Aliwafafanulia na kuwafanya wote wazame kwenye tafakuri ya kile walichoambiwa.


****

       [9]
     ASUBUHI ILIYOFUATA

  Norbert akiwa yupo katika muonekano wake wa kinadhifu akiwa ni mwenye suti nyeusi pamoja kofia aina ya hat nyeusi ambayo alikuwa akipenda kuitumia kwenye kazi yake, alienda hadi kwenye ofisi za kampuni ya usafirishaji mafuta maarufu sana nchini. Ilikuwa ni kampuni ile ambayo umiliki wa lori lililokuwa mali ya Nourthers brother ulihamia hapo, akiwa ni mwenye mkoba wa namba mweusi alifika hadi eneo la mapokezi kwenye kampuni hiyo ambako alikuta watu wakiwa wanasubiria  kuweza kupata huduma. Yeye pia ilimbidi asubirie kwenye viti maalum vya kusubiria kwa wageni huku akiwa akipigwa na kiyoyozi pamoja kupoteza muda kwa kusoma jarida, ni ndani ya siku ya pili kati ya siku kumi ambazo alikuwa amepewa kuhakikisha hiyo kazi ilikuwa ikikamilika vilivyo.


  Baada ya kusubiri kwa kipindi kifupi cha muda hatimaye aliruhusiwa aingie ndani kwenda kuonana na bosi wa kampuni hiyo, alikuwa  hana miadi kabisa na bosi wa hapo lakini kutokana na muonekano wake ulivyo kama mtu aliyekuwa akitoa harufu ya pesa kila akitembea. Aliruhusiwa kwenda kuonana naye baada ya kuonekana na kamera iliyokuwa ikionesha watu moja kwa moja chumbani kwa bosi huyo, uso wake ulikuwa umefichwa kwa asilimia kubwa na kofia aliyovaa jambo ambalo lilifanya aweze kupoteza utambulisho kama ni Norbert Kaila yule mwandishi wa habari ambaye alikuwa ni nuksi sana akiwa kazini kwa watu wenye mipango michafu.

"Naam Mr Mashishanga karibu sana" Alikaribishiwa na Bosi yuleyule ambaye aliyekuwa ameona picha zake kwenye tovuti za kampuni hiyo

"Thanks a lot Khemiri, nipo kwa ajili ya kuongea biashara maalum so sorry sikutoa apointment mapema. Nina mzigo upo njiani  na meli ukiwa upo kwenye matenki ya mafuta ya semi trela nahiraji opite bandarini bila kukaguliwa na pia kampuni yako yenye kuaminiwa iweze kunisafirishia hadi kwenye headquarters zangu"  Aliongea kuzidi kumvuta mwenyeji wake kwani alikwisha tambua kabisa kuwa mtu huyo alikuwa akishiriki michezo michafu kabisa kwenye serikali.

"Ok Mr Mashishanga ni mzigo wa aina gani na kama ni zaidi ya petroleum nafikiri nahtaji kuongea na wewe out of this office the daya after tomorrow, ujiandae kulipa hela zaidi ya hapo maaa ni dangerous game tunacheza. Kukwepa kodi na kusafirisha mzigo wa aina hiyo uanozungumza maana nishaujua tayari"


"OK hamna tabu kabisa" Norbert alipokubali hivyo simu ya mezani ya kampuni hiyo iliita na kumfanya Khemiri ampe ishara ya kumuomba radhi na kisha akaipokea simu hiyo na kuongea na huyo aliyempigia simu

"Ndiyo Fina.... ngoja nimuone"  Khemiri aliongea na kisha akatazama kwenye kioo kimojawapo kati ya vioo vya Tarakilishi vilivyokuwa vikitazama upande wake halafu akasema,"Ok akitoka huyu mwambie aingie"


   Alikata simu na kisha macho yake yote aliyarudishwa kwa Norbert aliyekuwa akisubiri amalize kuongea na simu hiyo halafu akasema,"Mr Mashishanga nafikiri mzigo wako bado una siku kadhaa  kabla haujafika bandarini sasa basi the day after tomorrow tutaongea then niende nikachukue kibali kwa Mheshimiwa mzigho huo upitishwe bila ya kukaguliwa".

"Ok Mr Khemiri kadi yangu ya mawasilino ni hii hapa nafikiri tutawasilina zaidi"

"Ok pokea na kwangu kabisa nafikiri kila mmoja sasa anaayo mawasiliano na mwenzake kilichobaki na kuingia deal"

"Ok asante have a nice day" Norbert aliongea na kisha akapeana nkono wa kuagana na alitoka humo ofisni, alipofungua mlango aliweza kumshuhudia Spider akinyanyuka upesi kwenye sehemu ya kupumzika wanaosubiri kuonana na Khemiri. Alimpita kama hamjui vile ingawa moyoni mwake alishaanza kuweka shaka kabisa ya juu ya ujio wake mahala hapo haukuwa wa kawaida kabisa, alijua wazi mtu huyo hakuwa mfanyabiashra yeyote zaidi ya kuwa mhlifu na alikuwa yupo hapo kwa ajili ya kazi maalum. Uwepo wa mahusiano baina yake na bosi wa hapo alihisi kabisa, alijipa tahadhari kabisa na bosi huyo hata katika siku ambayo angeonana naye wazungumze kuhusu suala hilo.



****


    ILIPOTIMU SAA NNE ASUBUHI
  Jeshi la polisi lilichangayikiwa kabisa kutokana na kutokea kwa milipuko katika ofisi za serikali na hata ofisi binafsi, watu mbalimbali walikuwa wameuawa ndani ya milipuko hiyo kwa saa kadhaa tu tangu kuingia kwa siku mpya. Jambo hilo lilipofika kwa raia wa kawaida wa ndani ya nchi hii yenye amani waliingiwa na hofu kabisa wakiona kuwa ugaidi ndiyo ulikuwa umeanza kuikumba nchi nzuri ambayo haikuwahi kukumbwa na mlipuko wa ina hii tangu ulipotokea ule mwaka 1998 kwenye ubalozi wa Marekani. Wale ambao ambao walikuwa na hofu kubwa sana ya kupoteza maisha yao wakiwa wapo ofisini walirudi wote majumbani mwao wakiwa salama huku baadhi yao wakiishia njiani baada ya pumzi zao kukatika kabla hata hawajafika kwenye nyumba zao. Milipuko mingine kabisa ilitokea kwenye baadhi ya daladala na pia magari binfasi jambo ambalo lilzidisha hofu kubwa sana kwa wananchi waliokuwa wakitumia vyombo vya moto barabarani, nusu saa  baadaye kwa hofu kulipuliwa kwa ofisi mbalimbali ilibidi kampuni zile za kiserikali na hata binafsi zifunge ofisi zao. Mamia waliokuwa wakirudi makwao kwenye jiji la Dar es salaama walishiriki matembezi yasiyo na hisani kutokana na hofu ya lipuliwa wakiwa ndani ya vyombo vya moto, wengi walihisi kuwa hao waliokuwa wakifanya matukio hayo walikuwa ni mgaidi waliokuwa wakijitoa mhanga na pia walikuwa wakitega mabomu kwenye ofisi mbalimbali.

  Siku hiyo madereva wa daladala pamoja Teksi waliilaani kuliko siku zao zote zilizowahi kutokea ndani ya maisha yao, waliona kabisa kuwa kulikuwa na kasumba ilikuwa imeingia ndani ya jiji la Dar es salaama ambayo ilikuwa imepanga kuhakikisha wanakosa ulaji kwa siku hiyo. Barabara zilizokuwa zikitumika katikati ya jijizote zilikuwa tupu jambo ambalo halikuwahi kutokea hata pale ulipotokea mgomo wa madereva wa mabasi ya usafiri, wale wenye magari binafsi nao waliogopa kabisa kutumia magari yao kwa siku hiyo kutokana na kuhofia huenda magari yao hayo yalikuwa yametegwa bomu hivyo wangekatishiwa maisha yao wakiwa wapo njiani.

  Ilikuwa ni siku ambayo shirika la posta nchini lilikuwa limetumia sana vyombo vya  vyao usafiri kuelekea sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam kusambaza barua, haikuwahi kabisa kutokea suala kama hili  na  siku hiyo ndiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa. Wafanyazi wa shirika hlo walitumia muda mwingi sana kuzunguka ndani ya siku hiyo masaa kadhaa kabla ya kutokea milipuko hiyo kusambaza barua mbalimbali ambazo zilikuwa zimeingia, ilipotokea kasumba ya mlipuko walikuwa tayari wameshasambaza barua nyingi sana hata wenyewe waliruhusiwa kwenda majumbani mwao na barua za siku  hiyo ambazo hazikumalizika kabisa zingekuja kusambazwa siku inayofuata. Siku hiyo hawakuhisi kabisa kuwa wao ndiyo walikuwa wametumika kama nnjia ya kusambaza kasumba hiyo iliyokuwa ikisumbua ndani ya jiji, waliona ni ugaidi na wala hawakutambua kuwa silaha hizo zilizokuwa zikiwangamiza watu wao ndiyo walikuwa wakizisambaza ndani ya siku hiyo.

   Siku ambayo haitokuja kusahaulika ndani ya nchi ya Tanzania kwa jinsi magari ya zimamoto yalivyofanya kazi ya zaida ya kuzima moto katika sehemu mbalimbali zilizokuwa zimetokea milipuko, walikuwa wakihangaika barabarani ambako magari mengi yalilipuka na hata kwenye baadhi ya ofisi ambazo zilikuwa zimepatwa na balaa hilo. Hakika walifanya kazi ya ziada nao lakini katu hawakuthubutu kuyatelekeza magari yao hata kulipotokea milipuko hiyo, waliendelea  na kazi ya kuzima moto na pia kuokoa baadhi waliokuwa wamejeruhiwa wakishirikiana na vikosi vya uokoaji ambao nao walikuwa wamejitoa mhanga wasikimbie kazi yao ili tu waokoe maisha ya majeruhi ambao walihitajika kupata msaada waweze kuendelea kuvuta pumzi ndani ya dunia hii.


ITAENDELEA!!


No comments:

Post a Comment