WITO WA KUZIMU
NA: HASSAN O MAMBOSASA
MAHALI:TANZANIA
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
+255762 219759
BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com
SEHEMU YA TANO!!
"Naona wewe kijogoo umekuja leo, mke wako umemkosa" Msichana huyo alimuambia
"Kwa akaliaye kiti hicho siku zote ni mke wangu sasa sijamkosa huyo hapo nimemkuta" Norbert aliongea na yeye
"Loh! Lione hivi ukijogoo utaacha lini wewe?"
"Simba akiacha kung'ata na mimi ndiyo nitaacha"
________________TIRIRIKA NAYO
"Na huyo mkeo ana kazi nakuambia"
"Si useme tu wewe ndiyo una kazi sana kuwa na mume kama mimi maana nimekuambia kuwa anayekalia hicho kiti hapo ni me wangu"
"Ha! Ha! Babu wee hapo umenikosa, kwanza ingia huko mkuu anakusubiria kwa hamu sana"
"Doh! Na Mzee wenu huyu nakuambia bora astaafu akapumzike maana ananishtukiza kila kukicha"
"Ndiyo raha ya kuwa Secret service hiyo, acha uionje. Ingia anakusubiri kwa hamu sana"
Norbert alipoambiwa maneno hayo alisogea kwenye mlango uliokuwa upo pembeni ya mlango wa chumba cha Katibu Mukhtasi, aliufungua mlango huo akaingia ndani ambapo alikutana na CE kama kawaida yake akiwa yupo anamsubiria kwa hamu kubwa. CE alipomuona Norbert yeye aliangalia saa yake ya mkononi na kisha akamtazama usoni, Norbert alitoa heshima hapohapo kwa mkuu wake huyo wa kazi na kisha akasogelea kiti kilichokuwa kipo hapo mbele yake akakikalia.
CE alimtazam Norbert kwa mara ya pili na kisha akaitazama saa yake ya mkononi halafu akasema, " dakika tatu zaidi umechelewa kisa kuongea na mke wako mwingine hapo mlangoni, N001 wanawake ni sumu mbaya sana kwenye kazi zako".
Maneno hayo yalipita tu bila ya kujibiwa na Norbert kwani alikuwa akiuona ni wimbo aliokuwa akiiimbiwa kila siku na mkuu wake huyo tangu aanze kazi hiyo, alifikia hata kuhamishwa makzi na kupelekwa uswahilini akitegemewa angeweza kuacha hiyo lakini hakuiacha. Maneno hayo yalikuwa ni maneno ambayo alikwisha yazoea kutoka kwa Mkuu wake, hakuyajibu hata siku moja alimuacha alalamike na kisha atakaponyamza aweze kumuambia kile kilichokuwa kimemfanya amuite hapo kwani kuitwa kwake namna hiyo kwa ghafla sana huwa kulikuwa na jambo ambalo lilikuwa limeambatana na wito huo.
"NOO1 je unajua kilichomkuta Bai,mke wa Jama,maCID wawili wa kuaminika na pia vijana wa usalama wa taifa waliokuwa na kazi maalum ya kuandaa ripoti ya kamati ya Bai?" CE aliullza
"Ndiyo nafahamu kutokanaa na wigo mpana wa vyombo vya habari" Norbert alijibu
"Sasa basi suala hilo linawigo mpana tofauti unavyofikiria na pia na sisi limetukumba, Open service wa shirika letu wa nchini Kenya walishirikiana sana na vijana hawa wa TISS katika kuandaa ripoti kwani kuna kitu ambacho kilikuwa kinahusiana sana na nchi hiyo katika ripoti yaoo. Nao katika muda tofauti wameuawa kwa bomu na haijulikani mtu anayeawaua ana mkono mpana kiasi gani" CE aliongea na kisha akamtazama Norbeet kama kweli alikuwa yupo pamoja naye, alipoona yupo pamoja naye alifungua faili lililokuwa lipo hapo mezni mwake na kisha akapitisha macho juu ya faili hilo.
"Huu ni utafiti wa mwanzo kabisa ndani uliofanywa na Open service, sasa kila kitu ndani ya tukio hilo unahitajika wewe ndiyo ukimalize ukiwa ni Secret service pekee uliyebaki bila kazi. Nimeamua kuvunja mapumziko yako kwa ajili ya hili kwani N002,N003,N004,N005,N006 wa daraja moja na wewe wote wana kazi nje ya nchi hii hivyo uliyebaki ni wewe tu. Hatuwezi kuona taifa linaanza kukumbwa na tishio la kigaidi wakati wewe upo ukiwa umejipumzisha tu, N001 nahitaji uingie kazini mara moja vifaa vingine utavichukua hapo kwa mke wako wa pili sina la ziada. Nakupa siku kumi tu kuanzia leo hilo suala liwe tayari " CE alihitmisha na kisha akamkabidhi faili hilo Norbert ambaye alilipokea kisha akasimama wima na akaatoa heshima, aligeuka nyuma na kisha akaanza kupiga hatua taratibu kutoka ndani ya ofisi hiyo.
"Norbert" CE alimuita kwa jina lake halisi pale alipotaka kushika kitasa cha mlango baada ya kuufikia, Norbert aligeuka nyuma alipoitwa jina lake hilo kwani haikuwa jambo la kawaida kabisa kuitwa hivyo.
"Umekua sasa hivi,fanya uwezavyo umuoe Norene uachane na ukapera maisha yanaenda haya. Unaweza ukaenda" CE alimuambia na Norbert alitoka humo ndani baada ya kumpa tabasamu hafifu akionesha alikuwa ameuridhia ushauri wake alioutoa kwake.
Norbert alitoka hadi nje ya ofisi iyo akaelekea hadi kwenye ofisi ya Katibu Mukhtasi wa CE, alimkuta akiwa anaendelea na kazi akiwa hajutambua ujio wake mahala hapo. Baada ya kuona hivyo alinyata hadi karibu yake na kisha akamgusa maeneo ya fumbatio na kupelekea Msichana huyo aruke sana na kisha akageuza macho na kumtazama.
"Nor bwana ushaanza mambo yako nina kazi mwenzio" Alilalamika kwa kitendo hicho alichofanyiwa.
"Oooh! Hata mimi nilikuwa na kazi na ndiyo hii naianza hapa" Norbert alijibu kimafumbo na kupelekea Msichana huyo asimuelewe hata kidogo.
"Sasa kazi yako ndiyo utake kuniharibia yangu"
"Kazi yangu naifanya kwako tu yaani na ndiyo hivi nimeanza"
"Looh! Lione ndiyo unachowaza hiko tu, hebu twende nikakupe vitu vyako"
"Poa usisahau na kile nilichokuwa nakitaka hapa nikaanza kukigusa"
"Muone jogoo pori wewe" Msichan huyo aliongea baada ya kuomuona Norbert alizidi kuongelea mambo ya gwaride lisilo rasmi tu badala ya kuzugumzia vitendea kazi atakavyovitumia kwa ajili ya kazi hiyo.
"Tena tangulia mbele kabisa maana nakujua wewe" Msichana huyo alimuambia huku akisimama ampishe Norbert apite mbele lakini hakupita badala yake na yeye alisimama tu bila kwenda mbele.
"Mimi chuma sharti niwe nyuma ya sumaku jua nikiwa mbele nitavutwa kuelekea nyuma tu, sasa chagua hapo nikae mbele au nyuma maana utachelewa kuja kumalizia kazi yako tu" Norbert aliongea na kupelekea Msichana huyo akose ubishi na kuamua kufuata njia ambayo angekuwa yupo mbele ya Norbert. Safari yao iliishia kwenda sehemu nyingine kabisa ambayo ilikuwa na vifaa vingi vya kijasusi, yule Misichna alimuongoza hadi sehemu ambapo kulikuwa na kitu kilichokuwa kimefunikwa kwa kitambaa kigumu sana. Alienda hadi mbele ya kitambaa hicho na kisha akageuka nyuma kumtazama Norbeet akiwa na tabasamu, taratibu alikifungua kitambaa hiko na Pikipiki ya kisasa ambayo ilikua vikolombwezo vingi sana zaidi ya pikipiki ya kawaida ndiyo ilionekana ambapo Norbert aliachia tabasamu alipoiona tu.
"Duh! Ndiyo maana hii kazi inahitaji haraka nyingi kukamilika" Norbert aliongea
"Ndiyo hivyo kazi kwako" Msichana huyo aliongea
"Kumbe kanipa hii ndege ya ardhini ndiyo maana nataka kazi hii ikalimike upesi"
"Hilo unalo babu wee, pocket za ndani ya hii pikipiki zina kila kitendea kazi chako. Nafikiri sina la ziada tena kufikia hapa"
"La ziada lipo bibie umemaliza ya kwako bado ya kwangu tu"
Norbert aliongea huku akianza kumsogelea huyo Msichana, na yeye pia tayari alikwishatambua kuwa Norbert alikuwa akitaka kitu gani alitulia na kubaki akimtazama tu. Norbert alipomfikia karibu zaidi aliupeleka mkono wake ukashika kiuno cha huyo Katibu. Msichana huyo alitoa muhemo wa hisia baada ya mkono wa Kidume cha mbegu kutua kiunoni hapo, alishindwa kabisa kumtazama Kidume ambaye alikuwa akimtazama sana kwa macho yasiyo na aibu hata kidogo kama ilivyo kawaida yake akiwa na anatazamana na uso wa msichana yeyote . Norbert alianza kuufanya mkono wake ufanye matembezi yasiyo rasmi kwenye mwili wake na kupelekea atoe miguno, alijiachia zaidi kwa kujisogeza mbele na akajikuta akiegemea kifua cha Norbert ambaye hakufanya makosa kabisa. Yeye aliamua kusogeza papi za midomo yake zikakutana na papi za midomo ya Msichana huyo, taratibu walianza kubadilishana shurubati ya midomoni kwa huku yule Msichana akionekana ni mwenye kuishiwa nguvu kabisa kutokana na kitendo hicho alichokuwa akifanyiwa na hata alipoachiwa papi za midomo yake bado alijikuta kisogeza zaidi kichwa cha chake kwa Mhamasishaji wake akiashiria kuwa alikuwa akitaka kitu hicho kiendelee. Norbert hakutaka kufanya ajizi kabisa yeye alitaka kuleta midomo yake kwa mara ya pili lakini alisita ghafla na kisha akarudi nyuma hatua moja kwa kasi sana, muda huo mlio wa kufunguka kwa mlango ulisikika na kisha akaonekana Mfanyakazi mwenzao wa shirika hilo akiingia humo ndani akiwa amebeba vifaa vipya vya kijasusi kwa ajili ya kuvihifadhi humo kwani hiyo ndiyo ilikuwa ghala kuu.
"Fuguo yako hii hapa, code number ya hiyo pikipiki ni jina la mkuu wako wa kazi tu" Msichana huyo aliongea kuzuga huku akimpatia funguo hiyo Norbert kwani ilibaki kidogo tu waweze kufumwa humo ndani wakiwa wapo ndani ya ulimwengu mwingine, Norbert alizipokea funguo hizo huku akimtazama Mfanykzi huyo Mwenzao anayehusika na humo ndani ya chumba cha kuhifadhia vitu. Alikuwa akitamani sana Mfanyakzi huyo atoke lakini hakutoka kabisa yeye ndiyo kwanza alienda kwenye kiti chake cha kazi baada ya kuweza vitu hivyo, hapo Norbert hakuwa na ujanja tena wa kuendelea na kile ambacho alikuwa amekianza na ilimbidi aoke humo ndani kwa kutumia Pikipiki hiyo aliyokuwa amekabidhiwa. Msichana huyo aliamua kutoka humo ndani akimuacha Norbert akieiendea hiyo pikipiki na kuikwea na kisha akaichomeka ufunguo, aliiweka namba za siri kwenye Pikipiki hiyo na kisha akaiwasha.
Lango jingine kabisa lililokuwa lipo humo ndani ya ghala ya zana muhimu ulifunguiwana Mtu yule aliyekuwa akihusika na humo ndani, Norbert kwa taratubu kabisa aliiondoa Pikipiki hiyo humo ndani akimuacha Mhusika wa hapo akimpungia mkono baada ya yeye kumpungia mkono na kisha aliufunga mlango wa hapo ndani baada ya N001 kuweza kuondoka kabisa.
****
BAGAMOYO
Ni ndani ya eneo ambalo lipo mita kadhaa tu kutoka ilipo stendi kuu ya magari ya jijini Bagamoyo, mtaa wa pili kutoka anapoishi mtunzi mahiri wa riwaya Ibrahim Marijani Gama. Ndani ya mtaa huo kwenye nyumba ambayo ilikuwa na uzio wa ukuta pamoja na lango lililonakshiwa vizuri, ilionekana gari aina ya Mazda yenye muundo wa Altezza ikiwasili neneo la jirani ya lango hilo. Gari hilo liliegeshwa mbele ya lango kuu la kuingila ndani ya nyumba hiyo, mlango wa gari hilo ulifunguliwa na akashuka Msichana mwenye umbo la kirembo sana akiwa amevalia suruali nyeusi iliyokuwa imemkaa mwilini, juu alikuwa amevaa blauzi nyeupe ambayo ilikuwa nyepesi sana kiasi cha kufanyia brazia aliyokuwa ameivaa ndani yke kuweza kuonekana. Mguuni alikuwa amevaa kiatu kirefu sana ambacho kilimfanya azidi kupendeza sana. Msichana huyo aliposhuka tu aliweka miwani ya giza yenye urembo wa kike kwenye macho yake na kisha akaanza kupiga hatua kuelekea kwenye lango la nyumba hiyo mkoba wake ukiwa upo kwapani mkanda wake ukiwa unaning'inia begani.
Alifika hadi mbele ya lango la Nyuma iliyopo mbele yake ambapo alibonyeza kengele ya mlangoni, haukupita muda mrefu mlango huo ulifunguliwa na Mwanamke wa makamo alionekana akiwa mlangoni ambaye alimkaribihsa hapo nyumbani kutokana na huyo Misichana kuwa mgeni mbele ya macho yake.
"Za saa hizi dada yangu?" Msichana huyo alimsabahi Mwanamke huyo aliyemkuta hapo mlangoni.
"Safi tu mdogo wangu, nikusaidie nini?" Mwanamke huyo alijibu na kisha akamuuliza juu ya shida iliyokuwa imempeleka hapo nyumbani kwake.
"Kuna dada mmoja anaitwa Sakina anaishi ndani ya nyumb hii sijui nimemkuta?"
"Haswaa umemkuta mdogo wangu ndiyo mimi hapa Sakinabinti wa Majaliwa"
"Dada yangu nimetoka Mlandizi nimeelekezwa nije hapa kwako nina shida sana na wewe"
"Mlandizi kwa mdogo wangu karibu sana ndani" Mwanamke huyo alimkaribihsa na kisha akasogea hapo mlangoni kumpisha Msichana huyo mrembo aingie ndani ya nyumba hiyo, Msichana huyo bila ya hofu ya ndani ya nyumba hiyo ngeni ambayo hakuwahi hata mara moja kuingia alipita. Ukimya wa ndani ya nyuma hiyo wala haukumtia hofu hata kidogo yeye aliona ni kawaida na aliingia ndani na kisha akasimama akimsubiri mwenyeji aje kumuongoza njia.
Mwanamke uyp mwenyeji hapo ndani ya nyumba hiyo alitembea akakaa mbele yake ambako alimuongoza hadi wanaingia ndani ya nyumba hiyo, alipelekwa hadi kwenye sebule ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa ni kubwa sana na ilikuwa imetawaliwa na ukimya sana. Alikaribishwa kwenye kochi mojawapo la kisasa la ndani ya sebule hiyo na kisha mwenyeji wake akatoka hadi kwenye sebule maalum ya kulia chakula, baada ya muda alirejea akiwa na kinywaji mkononi mwake ambacho alimuwekea mgeni wake mezani na kisha akaketi pembeni yake.
"Nisamehe sana mdogo wangu kinywaji kilichobaki ndiyo hicho tu, hivyo karibu hivyohivyo" Mwanamke huyo aliongea huku akifungua kinywaji hicho.
"Dada yangu usijali tu yaani mgeni hachagui ukaribisho wa kupewa" Msichan ahuyo aliongea kumtoa hofu sana
"Ndiyo mdogo wangu niambie"
"Dada yangu nimekuja hapa kwako nikiw nimefuata maelekezo yote niliyopewa, na kikubwa nilikuwa na shida kubwa san"
"Nakusikiliza mdogo wangu niambie"
"Shida yangu kuu ni ile laptop ya marehemu iliyokuwa ipo kwenye kabati chumbani kwako tu na si kingine" Kauli hiyo ilifanya yule mwanamke ashtuke sana kwani muongeaji alikuwa amebadilika ghafla na alikuwa amevaa sura isiyo na mzaha hata kidogo
"Kwani wewe ni nani?"
"Haina haja ya kunijua mimi ni nani timiza nilichokuambia" Msichana huyo aliongea huku akitoa miwani ya giza aliyokuwa ameivaa na kupelekea macho yake ya kirembo yaliyokuwa yamejaa ukali kuonekana kwa Mwanamke. Pamoja na hayo mwanamke huyo hakuwa na hofu hata kidogo hasa akiutazama muonekano wa Mgeni wake ambao ulikuwa ni wa kidhaifu sana.
"Sikiliza kama umetumwa nenda kawaambie hao waliokutuma wamegonga mwamba, mimi ndiyo Sakina Bint wa Majaliwa ukisikia mwingine jua ni wa kuchongsha. Kama kakutuma huyo mke mkubwa wa marehemu hapa imeshindikana tena na utoke huna hata hadhi ya kukinywa hicho kinywaji nilichokukribisha"
"Nafikiri hutambui unaongea na nani Sakina, sasa naongea kwa mra ya mwisho leta laptop ya marehemu sasa hivi"
"Sileti tuone uta nifanya nini" Kauli hiyo alipoiotoa Sakina alijikuta kipigwa teke la pembeni la ghfla sana ambalo lilimtoa kutoka hapo kwenye kochi hadi akangukia upande wa pembeni chini kwenye sakafu ya nyumba hiyo. Mwenyewe alibaki akiwa ameshangazwa kwa jinsi Msichan huyo alivyokuwa na nguvu za miguu hadi kufikia kiasi cha kuweza kumrusha hivyo mtu mwenye mwili kama yeye, alipoanguka chini alikuwa ameumia haswa hata kunyanyuka ilikuwa tabu tu ingawa alikuwa anaweza. Aliishia kujigeuza tu akawa amelala chali huku akifumba macho kwa maumivu, hali hiyo haikusaidia kabisa katika kumfanya Msichana huyo aweze kumuachia kutokana na majibu ya jeuri aliyokuwa amemjibu. Yeye alimuongezea teke la tumboni na kumfanya azidi kuwa na maumivu zaidi, uso wa msichana huyo ulikuwa tayari umeshabadilika na ukiwa umevaa sura isiyo ya kibinadamu kabisa kwa jinsi alivyomuadhibu.
"Haya nyanyuka mwenyewe tena ukiguna maumivu tu kwa sekunde chache wakati nakupa amri hii nakuongeza tena, uongoze njia unipelke ilipo lapatop hiyo"
Hakuwa na ujanja tena wa kuweza kuipinga amri hiyo kutokana na mapigo hayo mawili ya nguvu aliyokuwa amepewa ndani ya dakika zisizozidi mbili tu, mwenyewe aliongoza njia na kumpeleka huko kulipokuwa na kitu hicho alichokuwa akikitafuta Mgeni wake.
*N001 KAZINI
*BI SAKINA KAVAMIWA
ITAENDEKEA!!
No comments:
Post a Comment