Thursday, February 16, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA KUMI NA NNE



WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com





SEHEMU YA KUMI NA NNE!!
Norbert alipoona hivyo  kuwa muonekano wa mwanamke huyo ulikuwa ni kama yupo akiendelea na shughuli zingine, ili kumshtua ilimbidi aachie mguno wa nguvu. Alipotoa mguno huo alihisi kunyemelewa, alisogea kando  kwa haraka sana baada ya kuhisi kitu kikija kwa nyuma yake.







_________TIRIRIKA NAYO

  Kusogea huko pembeni hakukuwa kutupu bali kuliendanana yeye kujizungusha nyuzi tisini na kuudaka mkono uliokuwa na bastola ambao ulikuwa ukitaka kumuwekea kisogoni. Aliuzunguhsa mkono huo kwa kasi sana na kupelekea yule ambaye alikuwa yupo nyuma atoke mguno wa maumivu kwani alimuumiza sana, bastola ambayo ilikuwa ipo mkononi ilimuanguka kutokana kuumizwa vilivyo mkono. Norbert hakutaka kumlazia damu kabisa alichokifanya ni kumvuta mbele kwa nguvu sana, naye alienda mbele na kisha alinyanyuliwa kwa mtindo wa judo na kutulizwa sakafuni ambapo aliangukia mgongo.  Akiwa yupo hapo chini Norbert aliushika mguu wake na kuuvuta nyuma na kupelekea yule mtu ambaye muda huo alikuwa amevaa sweta lenye kofia kujifyatua na kisha akapeleka teke, Norbert alilikwepa teka hilo na kisha akautegua mguu wake na kumuacha akiwa na maumivu . Alipomaliza hapo aliiokota bastola yake na kisha akaketi kwenye kiti akimtazama mtu huyo ambaye alikuwa ameegemea sehemu ya kabati humo ndani kofia ikiwa imemvuka, alimuona Spider kwa macho yake mawili ndiyo alikuwa akitaka kumvamia hapo. Hapo alijua kabisa alikuwa amewekewa mtego na watu hao, kwa kuiona sura hiyo.

"Ukimtaja Norbert jua limebeba maana ya mastermind, hivyo usitegmee kabisa kumshika kijinga namna hiyo. Ujanja huo uliokuwa unaufanya ni level ya chekechea kabisa kwenye ujanja wangu Spider" Norbert alimuambia huku akijenga tabasamu lake  ambalo ilikuwa ni kawaida sana akiwa tayari amemshinda adui yake katika kupambana.

"Kipindi nasogea kwenye mlango huo wa tinted sikutaka nijiaminishe kijinga namna hiyo kuwa hii ni ofisi salama wakati najua mabosi wake ni maadui zangu, nimejifanya najiangalia kwenye kioo cha tinted kama vile naenda kupiga passport size lakini haikuwa lengo kujiangalia bali ilikuwa nikihadae ili nivae miwani hii ukiona kuwa nilikuwa nikitaka kupendeza zaidi. Miwani hii ndugu hata kwenye tinted naona ndani ndiyo nikakuona na hiyo basola yako ila sikuijua sura yako" Norbert alimuambia kwa mara ya pili na kisha alisimama na kwenda hadi mezani, alichukua kitabu cha risiti na kisha akamtupia hapo alipokuwa amekaa pamoja na kalamu.

"Haya andika risiti mwenyewe" Alimuamrisha, Spider hakuwa na ujanja zaidi ya kuandika risiti stahiki kwa Norbert ambaye alizama mfukoni na kisha akachomoa burungutu la hela ambalo alimrushia. Baada ya hapo alitoa kibeba risasi chote na kisha akachukua risasi zote na akamrushia  bastola tupu, muda huo Spider alikuwa akiunguliwa maumivu ya kuteuliwa hadi ngozi ikawa nyekundu.

"Sishindwi kukuua kabisa ila sitaki hao wafanyakazi wa kawaida ambao wengine wananifahamu wajue mimi ni mhalifu wataniweka pabaya" Alimuambia huku akichukua risiti yake na alitoka ndani ya ofisi hiyo akiwa na risiti, alienda hadi alipokuwa yupo Cellina na alimuaga na kisha alipanda pikipiki yake na kuondoka kwenye eneo hilo akiwa amemuachia maumivu makubwa sana Mzungu aliyekuwa akijaribu kupima uwezo wake.



****



  MUDA MCHACHE BAADAYE
  Ulikuwa ni muda ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu sana kwa Norbert na Khemiri wakutane kwani ulikuwa ndiyo muda muafaka, ilikuwa ni majira ya saa tano asubuhi ambapo kutokana na suala ambalo Norbert alikuwa amelitunga ilibidi wakutane kwenye chumba cha hoteli kwa ajili ya maongezi hayo. Norbert siku hiyo alikuwa amevaa muundo wa nguo zilezile ambazo alikuwa  amezivaa siku mbili zilizopita aliokuwa yupo ofisini kwa Khemiri, ndani ya chumba hicho cha kukutana hakikuwa chumba kulala kama ilivyotazamiwa bali ilikuwa ni chumba cha mkutano ambacho kilikuwa kikitumiwa watu wazito sana waliokuwa na mambo nyeti sana ya kuyazngumza. Khemiei siku hiyo alikuwa yupo ndani ya vazi la kanzu kwani ilikuwa  ni siku ya ibada na akitoka hapo alikuwa akielekea msikitini moja, alikuwa amepitia eneo hilo kwa ajili ya miadi hiyo ambayo walikuwa wamewekeana.

"Ndiyo Mr Mashishanga nipe details za mzigo wako ili tujue namna ya kuuuvusha pale" Aliongea Khemiri.

"Mimi ni wakala wa waasi kutoka Kongo na walikuwa wamepungukiwa na risasi, hivyo mzigo huo wote uliokuwa upo kwenye matenki ya mafuta ya Semi trela ni risasi tupu ila nisafirishiwe na magari yako ili kuepuka kukaguliwa. Kenye ulinzi ni mkali sana ila hapa kutokana na uwepo wenu natumai hichi kitu kitakuwa kirahisi sana" Norbert alijieleza

"Huo mzigo ni another issue Goverment ipo makini sana,  nitajiweka pabaya sana"

"Nitakupa kiasi chochote ilimradi mzigo huo uweze kuvuka bandari ile tu maana ndiyo kikwazo kikubwa sana kwetu"

"Ni hatari sana tuseme wewe una bei gani huo mzigo uweze kupita hapo kwani nishakipata tayari, nikusikilize"

"Nikusikilize wewe maana wewe ndiyo mwenye gharama inabidi utaje  halafu nitakuambiwa kama inawezekana aua haiwezekani"

"Kwanza hizo tenki zipo ngapi nijue gharama halisi ya mzigo huo"

"Zipo tenki ishirini"

"Dola elfu kumi kwa kila tenki hapo ni gharama za kila kitu"

"No Mr Khemiri hapo umeanzia mbali ndugu"


"Mashishanga hii ni too dangerous kabisa akijua Rais tumekwisha  wote na inabidi agents wetu wapate kidogo kwenye kila kitengo unachopitia ili usikaguliwe ndugu"

"I know butu hiyo si business ndugu bali ni kufukuza mteja"

"Ok Dol Elfu nane kwa kila tenki zinasafirishwa hadi huko DRC"

"Ok no problem nahitaji namba zenu za beki nikadeposit then nawaletea pay in slip, mzigo unaingia kesho usiku hivyo mazingira nahitaji kwenda kuyaona usiku wa leo nina imani tutakuwa wote. Niyaone then niwape information waendane na mchoro wetu"

"Exactly nitakuwepo hapo, namba hizi hapa ni Barclays " Khemiri aliomgea huku akimpatia karatasi ambayo Norbet aliiangalia na kisha akaiweka mfukoni.


"Ok tutakutana bandarini"

"Hamna shida Mr Mashishanga wacha niwahi masjid muda bwana huu"

"Ok hamna tabu"
 Huo ndiyo uliokuwa mwisho wa makubaliano baina ya Norbert na Khemiri, wote walitoka kwa pamoja ndani ya chumba hicho na kila mmoja alielekea njia yake. Norbert alizidi kuachia tabasamu la ushindi hasa baada ya kuzidi kuwaksribia mafisadi wa nchi hii, alijiapiza kufanya kitu ambacho kingewafanya walie na kusaga meno. Hakika alikuwa na uchungu sana wa kuona kuwa nchi yake iliyokuwa na utajiri mkubwa sana watu wake wakiishi kwenye mazingira magumu, maneno ya Khemiri kuwa yupo kiongozi mkubwa nyuma ya tukio hili aliyekuwa akisababisha kila kitu kiende  hivyo ilimuuma na alijiapiza kufanya kile ambacho kitawafanya wote hao walie na kusaga meno na pia kujuta kwa kuweza kufanya naye makubaliano wakati si mmoja wa wanyonyaji.


****


        ADHUHURI
   Muda ambao Norbert alikuwa yupo hotelini hakujua kabisa kuwa upande mwngine muwa mtu aliyekuwa ameshika tarakilishi ya mwanausalama mwingine aliyeuawa na Tarakilishi hiyo ilikuwa ipo mikononi mwa Askofu Valermar hadi muda huo, tarakilihi hiyo ilikuwa ni ngumu sana kuliko tarakioishi ambayo walikuwa wameipata hapo awali. Hii ilikuwa imefungwa katika sehemu mbalimbali jambo ambalo ilimuwia vigumu sana katika kufikia nenosiri jingine walilokuwa wanalitaka, hapo walijikuta wakihangaika hadi wakachoka na wakajikuta wakihitaji mtu mwingine ambaye angeweza kuifungua Tarakilishi. Hapo iliwabidi wamsake Mtundu wa tarakilishi ambaye angeweza kuwasaidia katika kuifungua hiyo tarakilishi, muda huo vijana waliokuwa wapo chini ya Askofu huyo waliingia kazini kumtafuta huyo aliyekuwa akihitajika huku wakimuacha yeye mwenyewe akiwa anahangika nayo Tarakilishi huenda atapata bahati ya kuweza kuifungua. Alifika hadi eneo ambalo lilikuwa na faili lenye nenosiri lakini alishindwa kabisa kulifungua kutokana na mfumo wa tarakilishi huo ulivyo, alihangaika sana na mwisho alichoka akaifunga tarakilishi hiyo akisubiri huyo mtaalamu wa tarakilishi aliyetafutwa aweze kufika atatue kitendawili kilichokuwa kikiwasumbua wao kwenye vichwa vyao.


   Robo saa baadaye wale  vijana waliweza kurudi wakiwa wameongozana na kijana mwenye asili ya kihindi hadi ndani, kijana huyo alielezwa kila kitu juu ya tatizo ambalo lilikuwa likiwatatiza. Aliwatajia kiasi cha pesa ambcho angepata angetatua tatizo hilo, hilo halikuwa tatizo kabisa wao walimpatia kiasi hicho cha pesa na kisha wakamsogezea tarakilishi hiyo aweze kucheza na ngoma ambayo alikuwa na ujuzi nao. Kijana huyu waliyekuwa wamemtafuta hakika alikuwa ni mtundu wa tarakilishi kuliko kawaida kwani ndani ya dakika mbili tu tayari alikuwa ameweza kufungua faili husika lililokuwa likihitajika. Ilikuwa ni furaha sana kwa Askofu Valdermar kwa kuweza kufunguliwa faili hilo na kisha walimruhusu kijana huyo aondoke kwenye eneo hilo kwani kazi yake ilikuwa imeshaisha tayari.

"Jamani haya maneno tuanyoyakuta humu ndani siyaelewi" Askofu Valdermar aliongea kuwaambia vijana wake

"ALEKUWA ALEKUWA UMRA AU HIJA " Aliongea mmoja wa vijana wake wadogo kabisa ukiachana na wale kina Spider

"Umeona sasa, yaani tunahangaika kote halafu neno ni hili tu la kwanza ni BARA JANGWA kwenye laptop ya kwanza mara hii ya nne iwe hivyo. Yaani haieleweki" Alilalamika

"Madam walioandika haya maneno si watu waliokuwa na ukichaa bali walikuwa na akili timamu. Inabidi tutafute hiyo ya mwisho tujue ina maana gani" Mmoja wa vijna wale alishauri.

"Sasa huyu wa mwisho haijulikani kabisa yupo wapi, alipotea katika mazingira ya ajabu sana. Huyu ni Jama na ule mtego ulipamta mke wake tu sijui yeye yupo wapi" Aliongea akionekana kuchoshwa.

"Madam inabidi kuanzia sasa ni tutrap all commnication ndani ya TISS tu huku tukiendesha msako" Alishauriwa

"Wazi zuri hilo na ni kazi yenu hii kuanzia hivi sasa naamini mtaweza tu" Aliwaambia

"Hilo ondoa shaka kabisa linawezekana, tunaanza kazi leo hii kila siku ni kufuatilia hayo mawasiliano yao" Baada ya hapo wote waliruhusiwa kuianza hiyo kazi mpya kutafuta huyo mwenye  kujua nenosiri na tafsiri yake iliwaweze kuwanusuru wakubwa zao,




****


  Utata wa maneno yaliyokuwa yapo Tarakilishi zile za wanausalama haukuwa ukiwasumbua maadui wa Tanzania tu, bali ulikuwa ulikuwa ukiwasumbua hata wanayoitetea. Ndani ya nyumba ya EASA Norbeet alikuwa yupo na Moses ambaye ndiye mkurugenzi wa TISS. Aliamua kumuita hapo kutokana na utata ambao ulikuwa umemkumba hata yeye kwani maneno hayo hakuwa ameyaelewa kabisa, suala hilo pia lilikuwa ni tata kwake yeye mwenye kiongozi wa hao vijana waliokusanya ripoti hiyo kwani yeye hakuwa amehusika kabisa na uchunguzi huo. Wale wote waliokuwa wamehusika na uchunguzi huo walikuwa tayari wameshatangulia mbele ya haki na alikuwa amebaki mmoja tu ambaye alikuwa hajulikani ni wapi alipo hadi muda huo. Bosi wake mwenyewe hakuwa akijua ni wapi alipo kutokana na Mtu huyo kutotaka kabisa kujiweka wazi hata kwa Bosi kwakuwa hakuwa akiamini mtu kwa suala kama hilo.

"Jama wa Majama ndiyo mtu pekee ambaye anaweza kutatua kitendawili hiki lakini hajulikani ni wapi alipo" Moses aliongea

"Hii nayo ni ishu sana, inaoekana kaijua hali si nzuri kabisa kwenye ngazi  za uongozi ndiyo maana hataki kutaja ni wapi alipo" Norbert naye aliongea muda huuo tarakilihi zote mbili zilikuwa zipo mezani.

"Halafu kibaya zaidi Mheshimiwa aliniambia niteua timu ianze kazi ya utafiti na ikusanye ripoti ya madudu yote yalipo kwenye wizara ya fedha na wizara ya uchukuzi, jamaa wamemaliza ripoti wakaiweka kwenye laptop moja tu halafu nyingine zikawekwa maneno ambayo yakiunganishwa na kuchambuliwa basi ndiyo yanafungua hiyo laptop. Ripoti nyingine ikapelekwa kwa Mheshimiwa Bai huku hii nyingine ikabaki kwa tahadhari ikiwa ile itapotea"


"Sasa inaonekana hadi kwenye idara yako kuna nyoka"

"Hili nahisi Jama kalijua ndiyo maana hataki kabisa kuniambia ni wapi alipo. Uwepo wa msaliti nahisi upo kila mahali si humuo tu, haiwezekani na IGP atume CID wawili na wawindwe na wauawe ndani ya siku moja hii inamaanisha walikuwa wamejulikana wameshaingia kazini sasa nani nikatoa hiyo taarifa wakati waliitwa tu na kisha wakachukua jukumu waondoka. Jibu ni msaliti"

"Hata hiyo ripoti ya kwenye laptop zote zile nayo ni msaliti pia"

"Hilo halipingiki yaani, kuna watu wachache wanaotaka kufelisha utawala wa mheshimiwa na ndiyo wanafanya haya. Mmoja ndiyo huyo kakamatwa na mkanda uliomrekodi akiongea kuhusu kuwangamiza wanausalama umepatikana"

"Huyo kwa sasa simuhukumu kama ni msaliti hadi pale hiyo ripoti itakapo kuja"

"Ok tusubiri tuone miujiza itakayomtetea, yaani laiti ile ripoti ningeisoma kabla haijafika huko basi isingekuwa tabu hivi ila kwa masharti ya Mheshimiwa kuwa niwache na uhuru kwenye kazi ndiyo haya"

"Ndiyo ishatokea tena na isitoshe tunapambana na adui mkubwa tusiyemjua ilihali yeye anatujua"

"Hiyo ni vita mbaya sana lakini katu hatuwezi kuweka silaha chini tunaianza taratibu, wewe leo usiku ukienda bandarini usisahau kamera na sound recorder tuweze kuwanasa tena chukua Kamera ambayo ni  waterproof kwa tahadhari"

"Hilo lipo akilini tayari na nikitoka hapa ni kuanza uchunguzi wa kujua wapi alipo Jama na hiyo laptop"




****


   ALASIRI
  Habari ya kuuawa kwa mtu mwingine aliyekuwa ameshikilia moja ya tarakilishi zenye siri, ilimfikia mzee aliyekuwa yupo kijiji cha Kibewani. Muda huo alikuwa yupo akiwa anacheza bao na wazee wengine wa kijiji hicho katika majira hayo. Alipoisikia habari hiyo ndipo alipata uhakika kabisa kuwa Tarakilishi zote hazikuwa mikononi mwa watunzaji ispokuwa tarakilishi yake pekee, aliendelea kucheza bao huku akili ikiwa inawaza kwingine kabisa. Akili yake ilikuwa ipo ndani ya jiji la maraha na lenye kila aina ujanja, alipoipata na taarifa ya pili juu ya tuhuma ambazo zilikuwa zikimkabii Mheshimiwa Kabinuki aliona kabisa kuwa tayari mpira ulikuwa umegeuzwa kwa mwingine kabisa ambaye alikuwa hahusiki na lolote. Moyoni hakuvilaumu kabisa vyombo vya dola wala maamuzi ya Rais Zuber ya kutoa kibali cha kukamatwa kwa waziri huyo, aliumia sana moyoni kwa kukamatwa kwa waziri mzalendo ndani ya nchi akituhumiwa kwa tuhuma ambayo haikuwa inamuhusu kabisa lakini hakuona kabisa kuwa huo ulikuwa ni muda muafaka kwa yeye kwenda kumkomboa katika balaa hilo kwani alijua wazi alikuwa akitafutwa na wabaya wake kwa udi na uvumba.

"Kabinuki anahitaji mwamvuli wa kumkinga na mvua kwani manyunyu ndiyo haya yameanza kumuangukia, mvua ikiwa kubwa zaidi sitakuwa na jinsi zaidi ya kwenda na mwamvuli" Aljisemea huku mkononi akiwa na kete kadhaa  akicheza bao, alikuwa amezungukwa na  baadhi ya wazee ambao alikuwa wakitazama mchezo huo.

  Huyu Mzee hakuwa mwingine bali alikuwa ni Jama wa Majama ambaye anatafutwa kwa pande tofauti kutokana na kile alichokuwa nacho, alikuwa amejificha kwenye kijiji hiko ikiwa ni siku kadhaa tu tangu mke wake afe kwa bomu la barua lilokuwa likimlenga yeye. Alikuwa akiendesha maisha hayo hapo kijiji akijifanya  ni mdogo wa babu yake mzaa mama, alikuwa yupo katika kuonekano wa kizee kabisa ambapo ingekuwa ngumu kabisa kwa mtu yeyote ambaye anamfahamu kuweza kumtambua. Huko kijini alikuwa akiishi kwa amani zaidi kuliko hata huko mjini ambapo kulikuwa na kila aina ya raha, alipaona ni mahali sahihi kwake kuweza kutulia kwa siku hizo akiwa huko hadi pale hali itakapokuwa shwari.


ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment