WITO WA KUZIMU
NA: HASSAN O MAMBOSASA
MAHALI:TANZANIA
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
+255762 219759
BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com
SEHEMU YA KUMI NA SABA
Aliweza kuona nyendo zote ambazo alikuwa amezipitia Khemiri tangu alipotoka bandari na hadi anafika kwenye nyumba yenye makao yao, eneo hilo alilikariri pamoja na kuchukua kifaa kingine ambacho alikitia faili hilo. Hicho kilikuwa kifaa ambacho kilikuwa kina uwezo kumuongoza hadi ndani ya eneo husika kwa kutumia rekodi iliyokuwa imechukuliwa hapo awali"
"Kazi kwao" Alisema na kisha akakichukua kifaa hicho na kunyanyuka kitini.
NA: HASSAN O MAMBOSASA
MAHALI:TANZANIA
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
+255762 219759
BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com
SEHEMU YA KUMI NA SABA
Aliweza kuona nyendo zote ambazo alikuwa amezipitia Khemiri tangu alipotoka bandari na hadi anafika kwenye nyumba yenye makao yao, eneo hilo alilikariri pamoja na kuchukua kifaa kingine ambacho alikitia faili hilo. Hicho kilikuwa kifaa ambacho kilikuwa kina uwezo kumuongoza hadi ndani ya eneo husika kwa kutumia rekodi iliyokuwa imechukuliwa hapo awali"
"Kazi kwao" Alisema na kisha akakichukua kifaa hicho na kunyanyuka kitini.
___________TIRIRIKA NAYO
Alitoka hadi nje kwenye maegesho ya vyombo vya moto yaliyokuwa yapo ndani ya nyumba hiyo, hakuwa na chombo kingine cha kuchukua isipokuwa ni pikipiki yake na aliamua kuitia moto kisha akatoka ndani ya nyumba hiyo baada ya geti kufunguliwa. Aliingia barabarani na aliiondoa kwa kasi sana hadi alipofika eneo la Mtoni kwa Aziz Ally akitokea huko Kurasini. Aliingia kwenye barabara ya Kilwa kwa mwendo wa wastani akiwa upande ilipo barabra iliyokuwa ikielekea Mtoni Mtongani, aliongeza mwendo huo baada ya kuufikia Mlima mdogo uliokuwa upo eneo la Mtoni Madafu na kisha aliendela na mwendo huo huo huku akiyapita baadhi ya magari ambayo yalikuwa yapo kwenye mwendo mdogo sana kuliko yeye. Baada ya dakika takribani kumi alikuwa yupo ndani ya eneo la Mbagala rangi tatu lakini napo hakukaa aliendelea mbele, dakika tano baadaye alikuwa ameshafika Kongowe mwisho na aliingia kwenye barabara iliyokuwa ikielekea Kigamboni. Norbert alipoingia kwenye barabara hiyo hasa kwenye eneo la jirani kabisa na kituo cha Daladala kinachotumiwa na daladala ziendazo Kigamboni, alipunguza mwendo kidogo wa pikipiki hiyo kutokana na kuwepo gari nyingi katika eneo hilo zenye ukubwa tofauti ambazo zilikuwa zikitembea kwa mwendo wa taratibu sana. Hali hii iliyokuwa ikisababishwa na daladala zilizokuwa zikichukua abiria njiani ilimkera sana, lakini na hakuwa na kitu cha kufanya kabisa kwani upande mwingine ulikuwa magari mengi ya mchanga pamoja ya mizigo yaliyokuwa yakipita hivyo ulikuwa si salama kwake. Sifa ya barabara hii ni magari kwenda mbio haikujalishi lilikuwa gari la dogo au kubwa, hiyo ilimfanya asubiri kwenye eneo hilo ambapo alipoteza dakika tano hapo hadi pale daladala zilipoanza kusogea.
Baada ya hapo alikuwa kama amefunguliwa kwenye kifungo kwa jinsi alivyovuta mwendo kwenye pikipiki hiyo, alianza kuyapita magari hayo kwa kasi alipofika kwenye eneo ambalo magari yalikuwa yameachana mabalimbali. Pikipiki hiyo ya kisasa nayo ilijua haswa kuzitii amri zake alizokuwa akiipa, kila alipotoa gia hii na kuweka nyingine nayo ilitii na kupelekea awe kwenye mwendo mkali sana. Alikuwa akipunguza mwendo kwenye maeneo ambayo yalikuwa na Matuta tu au kwenye eneo jirani na makazi ya watu na alipotoka maeneo hayo alikuwa akivuta mafuta sana. Utumiaji wa mwendo mkubwa namna hiyo haikumuwia vigumu kabisa kuweza kufika Kibada mapema, alifika eneo hilo na kupitia kile kifaa ambacho hadi muda huo alikuwa amekipachika kwenye pikipiki. Alifika sehemu ambako kulikuwa kuna kona ambayo aliikata kuendana na kifaa hicho kilivyokuwa kikisema, alitembea kwa mwendo mfupi tu na alifika kwenye nyumba ya kifahari sana iliyokuwa ipo miongoni mwa majengo ya kifahari yaliyokuwa yapo mtaa huo. Kifaa kile kilimuonesha kuwa eneo alilokuwa akielekea lilikuwa ni hilo na hapo Norbert ilimbidi apunguze mwendo na kisha akatafuta eneo zuri la kuegesha pikipiki yake. Alienda hadi kwenye eneo ambalo kulikuwa kuna duka moja kubwa ambalo lilikuwa limeambatana na sehemu ya kunywea vinywaji, hapo aliaingiza Pikipiki yake na kisha akiweka eneo la maegesho ya sehemu hiyo. Alimpungia mkono Mlinzi aliyekuwa eneo hilo ambaye naye alimpungia mkono, hapo alishuka kwenye pikipiki yake na kisha akavua kofia mabyo aliipeleka moja kwa moja kwa Mlinzi huyo.
"Kaka mali hii naingia ndani mara moja nikitoka nitapitia" Alimuambia huku akimkabidhi
"Hamna shida kaka" Mlinzi huyo aliongea huku akiipokea kofia hiyo ya pikipiki ya kisasa kabisa ambayo hakuwani kuziona moja kwa moja katika maisha yake zaidi ya kuziona kwenye luninga tu. Baada ya hapo Norbert alizama ndani ya eneo hilo ambako alitokea kwenye eneo lililokuwa na viti vingi sana, hakutaka kukaa kwnye eneo hilo yeye alizinguka hadi uani ambako kulikuwa na vyoo. Huko aliingia ndani ya choo hiko ambacho kilikuwa na sehemu ambayo ina ukumbi mrefu uliokuwa ukielekeda ndani. Kwenye ukumbi huo hakukuwa na paa kwa juu na hiyo ilimuwia kwa urahisi sana kuuruka ukuta wake na kisha akatokea nje, hapo alichnganya mitaa akiwa amekishika kifaa kile mkononi hadi sehemu ya nyuma ya nyumba ambayo alikuwa amekusudia kwenda. Alipofika hapo alikitazama kifaa hiko ambacho kilinesha ramani ya nyumba hiyo, aliuruka ukuta wa nyumba hiyo na akatokea sehemu yenye maua mengi sana. Hapo alitembea kwa uangalifu sana hadi karibia mwanzo wa kibaraza cha nyumba hiyo. Alijibana kwenye eneo moja na kisha macho akayatupa kwenye lango kuu la kuingilia kwenye nyumba hiyo, aliweza eneo ambalo alikuwa akikaa Mlinzi hakuwepo muda huo na hiyo ikampa nafasi nzuri ya kuweza kutawala kazi yake. Akiwa na mwendo wa kukazana aliingia kwenye baraza la nyumba hiyo na kisha akaelekea ulipo mlango mkubwa, taratbiu alinyonga kitasa ambacho kilitoa mlio wa kukubali kufungua mlango huo.
Aliingia ndani ya sebule pana ambapo muziki ulikuwa ukisikika kwa sauti ya chini sana, hapo alimkuta Spider akiwa amelala kwenye kochi akiwa hana habari yeyote kutokana na ujio huo wa kimyakimya. Norbert alipoingia humo ndani aliona bastola ikiwa ipo kwenye stuli ndogo iliyokuwa ipo jirani na Spider, bilauri yenye mvinyo uliokuwa umeshanyweka ilikuwa nayo ipo pembeni ya batola hiyo. Hapo alichokifanya alienda kuichukua bastola hiyo na kisha akachukua rimoti ya deki ya humo ndani ambayo ilikuwa ikicheza santuri, aliongeza sauti ikawa kubwa zaidi ambayo ilimfanya Spider aamke kutoka kwenye usingizi wake. Spider alipoamka tu alimkuta Norbert kiwa amesimama na mkono akiwa ameweka nyuma, akili yake ilimjia ni kuangalia kwenye stuli iliyokuwa ipo mbele yake akijua silaha yake itakuwa ipo palepale. Alikuta silaha yake ikiwa haipo kabisa ndaniya eneo hilo ambako akiingiwa na ubaridi moyoni mwake.
Muda huohuo Norbert alitoa mikono aliyokuwa ameificha nyuma na alimuonesha bastola hiyo kwani alikuwa ameshajua kuwa alikuwa akiitafuta, alitoa tabasamu na kisha akamfuata hadi jirani yake. Norbert hakuona muda wa kuanza kumsemesha mzungu huyo kwani alikuwa yupo kwenye kazi iliyokuwa na uharaka zaidi, alianza kumshushia kipigo huku akiwa ameongeza hiyo sauti ikawa haisikiki nje. Alimpiga hadi akammuumiza na kisha akammaliza kwa kuvunja shingo yake, baada ya hapo alianza kupekua chumba kimoja baada ya kingine kwani kwani ndaniya nyumba kulikuwa hakuna mtu ndani ya siku hiyo. Alifanikiwa kuzipata zile Tarakilishi mbili ambazo alitoka nazo kupitia mlango wa nyuma ambao aliokuwa ameuona, baada ya hapo aliuendea uzio na kisha aliuruka na kutokea mahala hapo. Alirudi hadi kule alipotokea ambako aliruka tena ukuta wa choo na kisha akaingia ndani akiwa na mkoba wake, alitoka humo chooni na alienda hadi kwenye meza kuu ya kuagiza vinywaji na kisha akaketi kwenye kiti kirefu jirani kabisa eneo ambalo alikuwa amekaa binti mmoja mweupe sana na mrembo aliyekuwa amevaa mavazi maaluma ya wafsnyazi wa eneo hilo.
"Karibu" Alikaribishwa
"Nishakaribia" Aliongea huku akiuweka mkoba wake vizuri mabegani
"Nikusadie nini handsome"
"Kile ambacho husaidia wengine wakashindwa kuacha kukiomba tena" Alipomaliza kuongea kauli hiyo aliachia tabsamu lake ambalo ni sumu sana kwa warembo hukua akikaza macho kwenye uso wa msichana huyo
"Una tabasamu zuri haya niambie kitu kipi hicho?"
"Kilichotukuka kuliko voyote kilichokufanya uonekane lulu"
"Halafu we mkaka hayo mambo yako"
"yana nini?"
"Tuache tu, haya nakusikiliza"
"Nilichokuwa nikikihitaji kile kilichokufanya uonekane lulu, upendeze na uzidi kutamaniwa, ni hicho hapo juu kwenye shelf kilichopewa jina la bia kwani kukiuza kwake ndiyo kumekupa pato ukajipatia vya kujikwatua ukazidi kuonekana lulu" Aliongea kimakusudi maneno ambayo yalikuwa ni nje ya mada ambayo ilikuwa imejengeka kichwani kwa mrembo huyo, maneno hayo yalimfanya mrembo huyo acheke kwani alikuwa amewaza jingine kabisa.
"Mmmh! Haya hii hapa"
"Ok ile kuna jingine"
"Lipi hilo?"
"Kaa mkao wa kula ninarudi" Norbeet alipoongea hivyo alichukua kinywaji alichoagiza na kisha akalipia kabisa hela ya chupa, alipomaliza alimuaga Msichana huyo huku akimbania jicho moja na kutoka ndani ya eneo hilo. Hakutaka kabisa kuanza mambo ya kuchombeza wakati alikuwa ametoka kufanya tukio muda si mrefu kwenye eneo ambalo hakukuwa karibu kabisa na maficho yake, aliamua kuondoka hadi kwa Mlinzi ambapo hakuongea chochote zaidi ya kumpatia pesa na kisha akachukua kofia yake. Aliiendea pikipiki yake akaitia moto na kutokomea kwenye eneo hilo kwani hakuwa na muda kupoteza kwenye eneo hilo ambalo lilikuwa lipo jirani kabisa na eneo la maadui zake.
Kanuni mojawapo ya kazi yake ilikuwa ni kutoonesha umaridadi ikiwa tayari umeshapata ushindi kwani umairdadi huondoa ufanisi, kukaa kwenye eneo hilo ilikuwa ni kuonesha umaridadi wake kuwa alikuwa ametoka kufanya tukio na sasa anakaa jirani na maadui zake na hawawezi kumfanya chochote. Hilo hakutaka kulifanya kwa maadui hao ambao hawakujua walikuwa idadi gani kwa ukamilifu, aliamua kuondoka kwa haraka eneo hilo.
****
Wakati Norbert akiwa ameshasabaisha tukio na kuondoka ndani ya eneo la Kibada, Moses alikuwa yupo nyumbani kwa Mzee Kabaita kwenye eneo la uani akiwa amekaa naye. Wote wawili walikuwa na bilauri zao mkononi, muda huo alikuwa amekuja kuitikia wito ambao aliyokuwa ameitwa na Mzee huyo ambaye alikuwa akimuheshimu sana kama Baba yake mzazi. Mke wa mzee Kabaita alikuwa yupo ndani ya nyumba kwa muda huo akiwapisha waongee kwani suala hilo alikuwa hatakiwi kabisa kuwepo wakati wakilizungumza.
"Moses hivi hili suala hili la Kabinuki unalichukulia vipi" Mzee Kabaita alimuuliza
"Ni suala ambalo limekaa vibaya sana baba kiupande wake kwani vithibiti vyote vipo" Alijibu
"Kuwa na vithibiti haimaainishi kuwa ndiyo mtuhumiwa mwanangu, wanasiasa wa nchi hii nawajua fika walivyo"
"Tatizo ni kwamba Kondoo kaibiwa na mifupa yake imekutwa kwa Mbwa unafikiri nani hapo atahisiwa ni mwizi? Halafu ukiangalia kabisa Mheshimiwa naye ndiyo katoa kibali cha kukamatwa kwake anasema Mahakama ifanye kazi haraka"
"Unajua tatizo la Zuber ni moja nafikiri hamumuelewi na pia mimi simlaumu kabisa, hataki afelishwe kwenye uongozi kwa sababu ya mmoja tu. Hivyo akisikia kuwa kuna uozo ni moja kwa moja hatua tu kama ushahidi ukifika kwake"
"Ndiyo hivyo sasa kwenye masuala kama haya huwezi kumuambia kitu"
"Sasa sikia mwanangu mimi naomba ufanye kitu hiki kwa ajili yangu kama unaniheshimu, naomba hili suala la Kabinuki ulifuatilie kwa karibu sana na ikiwezekana umuokoe kwenye hii kadhia"
"Baba hulo suala ni gumu sana kwani kesi yake pia ushahidi mwingine upo kwenye ripoti ambayo ipo kwa Jama na hajulikani yupo wapi"
"Nimefanya nao kazi Kabinuki pamoja na wabunge na mwaziri wengi kabla sijastaafu hii siasa, ninachokuomba ni kumsaidia kwani kuna kitendawili kigumu sana hapo hii ni siasa mwanangu. Mwenye usafi hupakwa uchafu ili aonekane mchafu na mwenye uchafu hujiondoa uchafu aonekane msafi"
"Sawa baba nimekuelewa"
"Jama Wa Majama huyu mtu namfahamu fika ni makamo yanayokaribia na wadogo zangu na kuwa mimi kwenye suala la kuweza kukuleta wewe idara hiyo nimepata bahati ya kujuana naye. Huwa hapendi ambaye hana hatia akose haki yake nafikiri ongea naye utaweza kumfanya aje kumuokoa Kabinuki maana siamini kama ana hatia kwenye suala hili"
"Sawa nimekuelewa Baba"
"Sina la ziada kuhusu hili, vipi mkwe wangu na mjukuu hawajmbo?"
"Wajambo na wazima wa afya kabisa"
"waambie waje siku moja wanisalimu naona imepita muda sana hawajaja"
"Hilo tu usihofu kabisa tena inabidi Baba uniandalie silaha maana watamuiba mjukuu wako kazidi urembo"
"Sasa inabidi uwe mkali hapo tu mimi sihusiki"
"Haa! Baba yaani mjukuu wako yue usimlinde"
Maongezi yalitokuwa yametawaliwa na utani ndiyo yalifuata baina yao baada ya kuweza kumaliza suala lao lililokuwa limefanya wakutane hapo, ulikuwa ni utani ambao ulikuwa ukiendela kila wanapokutana kwani walikuwa wakipendana sana kama mtu na mzazi wa damu kweli.
****
MCHANA
Majira ya saa sita mchana gari ambalo maarufu sana kwa wakazi wa jiji la Tanga pamoja wale waliokuwa wakisafiri kuelekea ndani ya jiji hilo, lilionekana likikata kona kuingia kwenye kituo cha mabasi Ubungo baada ya kufika kwenye jiji la Dar es salaam likitokea Tanga. Abiria walishuka mmoja baada ya moja baada ya bsi hilo kufika kwenye eneo lake la maegesho ndani ya kituo hicho,Jama Wa Majama naye alikuwa mmojawapo kati ya watu waliokuwa wameshuka ndani ya basi hilo akiwa na muonekano wake ueule wa kizee, alikuwa ameamua kabisa kuja kumsaidia Kabinuki baada mkinzano wa mawazo yake kuzidi upande huo.
Aliposhuka ndani ya basi hilo akiwa amebeba begi lililokuwa limechoka aliangaza maeneo ya hapo kituoni kama alikuwa ndiyo anaingia kwa mara ya kwanza. Alijifikira sana na kisha akanyanyua begi lake ambalo lilikuwa limechoka sana, muonekano wake ulikuwa hauna tofauti kabisa na Mzee wa kutoka shamba kwa jinsi alivyo. Alipoangaza sana muda huo wale vijana wajanja wa mji walikuwa wameshaanza kumchangamkia ili waweze kummuingiza mjini, Jama hakutaka kuongea na yeyote yeye alianza kupiga hatua kuelekea nje ya kituo hicho kwani alikuwa akipajua vyema eneo hilo kulivyokuwa kukisifika kwa wizi. Akiwa na mfuko wake ambao kimtazamo kabisa ulikuwa umejazwa mizigo ambayo haikuwa imepangwa vizuri kabisa, alifanikiwa kutoka akawa anatembea kwa mwendo wa kujikongoja hadi zilipo Teksi ndani ya eneo hilo la jirani na kituo cha mabasi. Alienda hadi kwenye mojawapo ya teski na kisha akasogea jirani kwa Dereva wake, alikaribishwa kwa kuchangamkiwa sana kisha akasema mahali alipokuwa akienda. Alitajiwa bei akajikuta ameshtuka sana kwani ilikuwa ni bei ya juu sana kwake, aliomba kupungiziwa huku akiweka uso wa huruma hadi Dereva huyo alikubali na kisha alipanda na mzigo wake kwenye gari na safari ikaanza.
"Wauzaji wa kesi safari hii wameuza hivyo wamempa kesi asiye mnunuaji lazima irudi kwao tu" Aljiseme mwenyewe huku akikumbatia mzigo wake akiwa amekaa kiti cha nyuma na si cha mbele, hiyo ilikuwa ni dalli tosha kwa Dereva huyo kuwa alikuwa amempandisha mshamba aliyezidi kiwango kwenye gari lake hadi yeye mwenyewe alijikuta kibanwa na kicheko.
Macho ya dereva huyu katika muda mbao alikuwa akiendehs agri yalikuwa hayaishi kumtazama Mzee huyu kwa umakini sana kwenye mfuko huo ambao alikuwa amebeba, ukumbatiaji wa namna ile wa mfuko huo ulianza kumfanya ahisi kuwa alikuwa amebeba mali hivyo alikuwa akiilinda. Alienda kuendesha gari huku roho ya tamaa ikiwa imemungia akiutzama tu ule mzigo, hakika tamaa ilimzidi kiwango kuliko kitu chochote. Muda aliokuwa akiendesha gari alipokuwa yupo kwenye barabara ya Mandela alitoa simu yake na kupiga mahali na kisha alizungumza kwa lughz ya kikabila na akakata, walipofika jirani na eneo la Tabata relini aliweka gari kando na watu watatu waliingia kwenye gari hiyo. Wawili kati yao walikaa nyuma katika kile upande na kumuweka Jama kati na mmoja alipanda mbele.
ITAENDELEA!!
No comments:
Post a Comment