Thursday, February 9, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA SABA

WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com





SEHEMU YA SABA!!

  Aligeuka kwa kasi ya ajabu  na kusimama pembeni akiwa ypo kujihami zaidi, alimuona yule mwanamke akiwa ameshika mkoba wa mabegani akiwa tayari amevaa  kwa ajili ya kuondoka. Hapo alishusha pumzi na kisha akaamua kuachana na bahasha hiyo, aliiweka bahasha hiyo chini na kisha akamshika mkono Mwanamke huyo na kutoka naye humo ndani ya nyumba hiyo kwa kutumia mlango wa nyuma wa nyumba  ambao ndiyo aliutumia kuingia humo ndani.





______________TIRIRIKA NAYO

   Kitendo cha ujio wa Mwanamke huyo akiwa tayari ameshajiandaa na akiwa amebeba mkoba wa mabegani, ulikuwa ni wokovu tosha kwa Norbert na laiti kama angelitambua hilo asingesita kumshukuru huyo mwanamke kwa kuweza kumsogelea akajua ilikuwa ni adui akikaribia kumvamia. Jambo hilo lilifanya aache kabisa kuitazama bahasha hiyo, hakujua kabisa kisanga ambacho kilikuwa kikiwapata wale ambao walikuwa wakifungua bahasha ya namna hiyo. Ujio wa mwanamke huyo ulimfanya apuuzie bahasha hiyo kwa kuona kuwa angemtia wasiwasi zaidi huyo mwanamke kwa kumpekua huyo Kijana ambaye yupo hai muda huo hakuwa  na nguvu. Aliamua kuiacha bahasha hiyo huku akimtazam huyo kijana ambaye alikuwa akiona jinsi Norbert alivyokuwa akitaka kuipekua hiyo bahasha, kijana huyo alipoona Norbert akitaka kufungua hiyo bahasha alijikuta kicheka mwenyewe na alipoiacha alinuna kwani aliona alikuwa amegunduliwa fikra zake.

  Norbert alipoiacha ile bahasha na kutoka ndani ya nyumba hiyo hadi wanafika kenye Pikipiki yake ambayo alikuwa ameigesha kichakani, mlipuko mkubwa sana ulisikika kutoka eneo ambalo nyumba hiyo ilikuwepo. Mlipuko huo uliambatana na milipuko mingine mitatu mfululio kuashiria kuwa ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na vitu viwili ambavyo vilikuwa ni mlipuko mkubwa sana ikiwa vitapata moto au vikisogelewa na moto. Mwanamke yule aliweka mkono kinywani mwake alipoiona nyumba yake ikiwa imetoa mlipuko huo, machozi yalianza kumtoka kila akifikiria jinsi ambavyo alikuwa ametumia ushawishi wa nguvu kutoka kwa mwanaume wake ambaye hadi muda huo ni marehemu. Ushawishi huo ndiyo ulifanya kajengewa nyumba hiyo ambayo kwa muda huo ilikuwa ikiteketea, alipofikiria suala hilo aliona kabisa hakuwa na  wa kumuegemea mwingine ambaye angeweza kufanya hadi ajengewe nyumba kama hiyo pamoja na kuwekewa Samani ndani ya kisasa.

 Kilio chake hicho Norbert hakukijali kabisa yeye aliwasha pikipki yake baada ya kuwa amepanda na kisha akaingiza barabarani akiitoa kule kichakani ambapo alikuwa ameificha, aliondoka eneo hilo kwa kutumia njia nyingine kabisa siyo ambayo alikuwa amekuja nayo hapo awali ambayo ndiyo ilikuwa ni njia kuu ya vyombo vyote vya msaada kuweza kuingia ndani ya mtaa huo. Aliamua kupita upande mwingine ambao ungeweza kumfikisha hadi ilipo barabra kubwa aweze kutoweka ndani ya eneo hilo baada ya kusababisha habari nyingine kabisa.



****



 Kutokea kwa mlipuko ndani ya nyumbe ya mke mdoago kabisa wa mmoja wanausalama wa siri waliohusika na utafiti wa ripoti ya Mheshimiwa Bai, kulishtua sana Idara ya usalama wa tafia kwa mra nyingine kabisa ambao ndiyo walikuwa wapo kazini kuhakikisha wahusika wote wliokuwa wakihusika na milipuko hiyo watiwe nguvuni. Muda huo wanafika hapo eneo hilo la tukio ambapo hata baada ya kuzimika kwa moto ndani ya eneo hilo walitambua kabisa kuwa tarakilishi ambayo ilikuwa na kitu chao muhimu ilikuwa imeshaondolewa na aliyewawahi kabla yao. Hii iliwachanganya sana kwani Tarakilishi hiyo ilikuwa ni Tarakilishi  ambayo ilikuwa na kitu muhimu sana ambacho kingeweza kufanikisha watuhumiwa waliokuwa wakihusika na upotevu wa vitu vya umma wanafikishwa ndani ya vyombo vya sheria. Tarakilishi hiyo ndiyo ilikuwa na nenosiri la kila kitu juu ya wahusika wa kuhujumu nchi hii, ilikuwa ni moja ya kati ya tarakilishi tano ambazo walikuwa nazo wanausalama waliokuwa wamebeba siri hiyo kama kumbukumbu ikiwa faili kuu litapotea.

  Uunguaji wa faili kuu katika mlipuko mmoja na Mheshimiwa Bai uliwafanya wahangaike kuyafuata mafaili hayo ambayo watunzaji wake wengi wao walikuwa wamekufa mmoja baada ya mwingine kwa mlipuko. Taraklishi ambayo ilikuwa imetunza mafaili hayo nayo ilikuwa imeishia ndani ya mikono mibaya. Walichanganyikiwa kutokana na kupotea kwa tarakilishi hiyo, waliona kabisa kuwa kazi yao ilikuwa ikielekea kuwa ngumu zaidi. Walihesabu kuwa tarakilishi hizo zilikuwa zimebaki nne tu huku moja tu ikiwa inajulikana mahali ambako ilikuwepo na nyingine zikiwa hazijulikani mahali zilipokuwepo. Wakiwa ndani ya eneo hilo walipokea taarifa nyingine kabisa ya kuteketea kwa nyumba ya Mwanausalam mwingine ambaye alikuwa ameficha huko Tarakilishi moja inayojulikana ilikuwa na siri kubwa sana. Wanausalama walichanganykiwa kwa taarifa hiyo na wakaona walikuwa na kazi ya ziada, wakiwa ndani ya eneo hilo la tukio huko Bagamoyo waliona kuwa hawakuwa na kingine ambacho kingewafanya wawepo ndani ya eneo hilo ikiwa kile ambacho kilikuwa kimewaleta ndani ya eneo hilo kilikuwa kimechukuliwa na wabaya wao. Wote kwa pamoja waliondoka kwa njia walizokuwa wakizijua wao tu wakiwaacha  Maaskari wa jeshi la polisi wakifanya kazi, hakika waliwahiwa kwa kila walichokuwa wakikiangalia.


****


  Baada ya kumuokoa ndani ya balaa zito Mwanamke yule kituo cha kwanza ailikuwa ni ndani ya nyumba ya Shirika alilokuwa akilianyia kazi, alimuweka mwanamke huyo ndani ya chumba kimoja ambacho kilikuwa na kila kitu alichokuwa akihitajika kupewa mwanadamu. Mkoba wa yule mwanamke ambao ndani yake ndiyo ulikuwa na Tarakilishi ya mapakato ambayo ilikuwa na siri iliyokuwa ikitafutwa. Ulihifadhiwa ndani ya nyumba hiyo ambayo si rahisi kabisa kufikiwa na raia wa kawaida. Baada ya kuuuhifadhi mkoba ule ndipo Norbert alipokumbuka kuwa alikuwa na anahitajika kuichunguza pochi ya mfukoni ya yule Kijana ambaye hadi muda huo alikuwa ni marehemu. Norbert aliitoa ile pochi na kuanza kuifungua na kisha akaanza kutazama kitambulisho baada ya kingine kilichokuwa kipo ndani ya pochi hiyo.

  Alikuja kubaini kuwa mtu yule alikuwa akiitwa Kelvin na alikuwa akifanya kazi katika kampuni kubwa ya utengenezaji magari, kitambulisho hicho kilichoonesha kila kitu juu ya kazi yake hiyo aliyokuwa akiifanya huko. Alibaini mtu huyo alikuwa ni mtaalamu aliyebobea katika uundaji maumbo ya juu ya magari, Norbert alipomaliza kukitazama kitambulisho hicho cha kwanza ambacho kilimwambia hivyo juu ya Kijana yule. Alitazama vitu vingine vingi ambapo aliona kabisa kuwa kulikuwa na kuna kadi nyingi za mawasiliano za kampuni ile ya uundaji magari na uungaji vifaa vya magari. Hii ilimpa ishara tosha kuwa mtu huyo hakuwa na kitambulisho hicho kwa kufoji bali alikuwa ni mfanyakzi halali wa pale, uwepo wa kadi hizo ulimpa uhakika kabisa kuwa alikuwa akizitumia kwa ajili kuwapatia wateja wake pindi watakapohitaji mawasiliano zaidi kwenye kampuni hiyo. Alikutana na kadi mbalimbali za benki ambazo hakuona maana yeyote ile kwake, aliachana na kadi hizo na kisha akatazama kadi nyingine ya kampuni hiyo aliyokuwa akifanyia kazi Kelvin ambayo ilionesha hadi mahali alipokuwa akiishi.


   Baada ya kumaliza kupitia kadi hizo zote aliamua sasa kuingia kazini kwa mara ya pili baada ya kufanikisha kumuokoa mwanamke huyo, aliamua kuiacha pikipiki yake aliyokuwa akiitumia kwa ajili ya kazi na kisha akachukua gari mojawapo ambayo ilikuwa ipo ndani ya uzio wa nyumba hiyo. Alitoka na gari hilo hadi nje kabisa ya uzio baada ya kufunguliwa lango kuu la kuingiza mgari ndani hapo, alianza safari ya kuelekea  huko alipokuwa akitaka kwenda kuanza kazi hiyo iliyokuwa imekatisha vizuri alivyokuwa akivitaka kuwa navyo katika muda huo wa kufurahi na familia yake.



****

 DAKIKA KUMI NA TANO BAADAYE
     BUGURUNI ROZANA
  Gari yenye rangi ilikwanguka katika sehemu kubwa ya bati lake ilionekana ikiwa imeweka kituo kidogo kabisa kwenye lango la kuingilia ambalo lilikuwa limefungwa muda huo, honi ndani ya gari hilo zilisikika zikilia kwa mara moja ambapo muda mfupi aadaye lango hilo la kiksasa la kufunguliwa kwa mashine lilifunguka na kisha gari hiyo ikaingia ndani. Iliingia kwenye eneo ambalo lilikuwa na mitambo mingi sana ambayo ilikuwa imekaliwa na vijana wa kike na wa kiume waliokuwa wamevaa sare za aina moja wakiifanyia kazi.  Kutokana na muonekano wa gari hilo ulivyo ilikuwa ishatambulika kabisa ilikuwa na tatizo gani, hivyo kwa maelekezo ya mmoja wa wafanyakazi wa kike wa ndani ya jengo hilo alielekezwa moja kwa moja hadi mahali ambapo kulikuwa kukifanyika huduma maalum ya kuhusu tatizo la gari hilo. Huko ilikuwa ni ndani kabisa kwenye chumba kilichokuwa kimetengenezwa kwa muundo maalum mithili ya banda la kulazia magari, taa tupu zenye mwanga mkali ndiyo zilikuwa zikimulika ndani ya banda hilo  kutokana kutokuwepo kwa nafasi ya kupitisha mwangaza wowote ndani humo.

   Yule mfanyakazi ambaye alikuwa amemuelekeza dereva wa gari hilo kuegesha humo, aligonga sehemu ya mbele ya gari hilo na kisha akamuashiria Dereva wa gari hilo ashuke, hapo mlango wa gari hilo ulifunguliwa kwa taratibu sana na kisha Norbert akiwaa amevaa kinadhifu kama ilivyo kawaida alionekana mbele ya msichana huyo ambaye alitoa tabsamu murua la kumfanya mteja aone kuwa hakuwa akiliwa hela yake bali ilikuwa ni haki yeye kutoa. Tabasamu hilo lilirudishwa na tabasamu sumu la Mzee wa watoto wazuri na akaangaza ndani ya eneo hilo.  Eneo hilo aliweza kuona kuwa kulikuwa na mabinti zaidi ya wanne ambao wote walikuwa ni warembo sana kama alivyo binti yule aliyekuwa amemuelekeza kuleta gari humo ndani.

"Karibu sana Feather garage, naitwa Cellina mhusika mkuu wa kitengo hichi cha kupiga rangi" Msichana yile ambaye ndiye alimuelekeza kuingia humo ndani alimkaribisha akiwa tayari amesogea mbele yake, alimpatia na mkono huku akiachia tabasamu kwa mzee wa mwenye sumu ya matabasamu.

"Asante sana nimekaribia" Norbert aliitikia.

"Hiki ni kitengo cha upakaji rangi magari je ni style ipi uipendayo katika upigwaji rangi yako?"

"Rangi kama ya uremmbo wako" Norbert aliweka utani kidogo

"Ha! Ha! Ha! Handsome utani tuache, unataka muundo upi ngoja uletewe uchagua" Baada ya kungea hivyo alitoa ishara na binti mmojawapo alikuja na Tarakilishi ya kugusa kioo mithili ya simu akampatia, Norbert aliipokea tarakilishi hiyo na akaanza kupitia mitindo mbalimbali ya rangi. Alipoupata mtindo aliokuwa akiuhitaji alimpa Cellina ambaye alimtazama kwa jicho la  kuhakiki kama ni rangi hiyo pia alikuwa akiihitaji, Jicho hilo lilifanya Norbert amkonyeze na kisha aachie tabasamu.

"Vipi hadi rangi ya jicho lako nalo napaswa kuchagua" Norbert alieka utani baada ya kuona binti huyo alikuwa akimtazama alipompatia tarakilishi hiyo, hiyo ilimfanya huyo binti acheke kwa mara  nyingine na kufanya urembo wake aliotunukiwa uzidi kuonekan dhahiri.


"Boy you are so funny,ok I think uje the day after tomorrow gari itakuwa tayari"


"Ok nilikuwa na kingine kinachohitaji kupendezwa kwa rangi zaidi ya hizi za kutengeneza"

"Sijakuelewa boy"

"Hutanielewa mpaka nikuelewesha na muda huu wa kazi hutakuwa na muda wa kutosha niweze kukuelewsha kuhusu hili"

"Ok be specific"

"Mpiga rangi hupendezesha vingi sana, hivyo nina kingine ambacho ninahitaji ukipendezeshe zaidi ya hiki"

"So ni business outside  ya office"

"Ni more than Business Cellina, nafikiri nikiwa na contact yako" Msichana huyo alipoambiwa hivyo alianza kujifikira huku akizungusha mboni yake ya jicho kwenda pembeni kwa madaha, alikaa kimya kwa sekunde kadhaa na kisha akarudisha mboni yake kumtazama Norbert. Hatimaye alinyoosha kiganja chake cha mkono akihitaji kupata simu ya Norbert aweze kuandika namba zake za mawasiliano, hiyo ilikuwa ni kitendo ambacho alikuwa akikisubiri kwa hamu sana mzee wa kazi na kwa haraka kabisa aliingiza mkono wake kwenye mfuko wa suruali akatoa simu ya gharama sana ambayo ilimuacha mdomo wazi binti huyo.

  Binti huyo aliipokea simu hiyo na kuandika namba zake kwa haraka sana na kisha akairudisha simu hiyo kwa Mhusika, ilipofika mikononi mwa mmiliki aliiminya namba hiyo aliyokuwa amepewa kuhakiki kama ilikuwa ikifanya kazi. Muda huohuo simu ya yule binti ilianza kuita ndani ya mfuko wa suruali yake aliyovaa. Norbert kuusikia mlio huo alitoa tabasamu tu na kisha akambania jicho binti huyo, baada ya hapo aliwapungia mkono wengine  ambao walikuwa wakiendelea na kazi zao na kisha akaondoka mahali hapo. Alikuwa amefanikisha hatua ya awali katika kuingia ndani ya himaya hiyo, hakuwahi kuingia ndani ya jengo hilo hadi sehemu aliyokuwa amefikia na ndani ya siku hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kuingia humo.


****


   Muda huo kwa upande wa ndani kabisa ya kampuni hiyo ya utengenezaji magari, hali ilikuwa si nzuri kabisa kwa bosi wa eneo hilo katika muda ambao alikuwa akitarajia kabisa kuwa mwenzake angekuwa amerudi muda mfupi tu kutokana na kazi aliyokuwa amemkabidhi. Simu zake zilikuwa hazipatikani kabisa tangu waweze kupata taarifa ya kulipuka kwa nyumba waliyomtuma na gari lake kuwepo nje ya nyumba hiyo, taarifa za kuonekana kwa mwili uliokuwa umeharibika ndani ya nyumba hiyo kiasi cha kushindwa kutambulika zilikuwa zimefika hapo. Uchunguzi wa pili a kuhusu mwili huo bado ulikuwa uanaendelea hvyo haikujulikana alikuwa ni jini gani, muda huo ndani ya ofisi hiyo Mkuu wake ambaye alikuwa amemuagiza Kelvin hakuwa mwingine isipokuwa ni yule Msichana ambaye alikuwa amesababisha tukio kule Bagamoyo. Mbele ya meza yake muda huo kulikuwa na kijana wa kizngu maarUfu kama Scorpio, huyu ni kijana mmojawapo kati ya vijanA walioingia na Askofu Valdermar ambao walijaribu kumuua Norbert ndani ya msitu wa Serengeti kwa bomu.

 Haya yalikuwa yametendeka kwenye kisa cha WAKALA WA GIZA ambacho kiliwapa hasara kubwa kwa upande wao, muda huo alikuwa yupo nchini kwa kazi maalum ambayo alikuwa ameagizwa itimie. Alikuwa akimtazama yule Mwanamke ambaye ana mwili wa wastani pamoja na umbo la wastani ambalo lilikuwa limejengeka kimazoezi haswa, Scorpio alionekana kuchangnyikiwa kabisa kwa  taarifa hiyo iliyokuwa hapo.

"Inamaana mpaka sasa hivi hakuna taarifa yake?" Scorpio aliuliza

"Ndiyo hivyo yaani haijulikani na mlipuko ule ni vyombo vyetu vile haiwezekani awe amefungua yeye bahasha" Msichana huyo alijibu.


"Josephine twende wenyewe tukapate taarifa hizo tusisubiri zitangazwe zimfikie Mheshimiwa, tukizipata tutajua ni jinsi gani ya kumtuliza akijua" Scorpio alimuambia msichana huyo ambaye hakuwa mwingine ila ni Josehine ambaye muda huo mwili wake ulikuwa umepungua kidogo, baada ya kusalimika kutoka kuuawa na pia kuwekwa mikononi mwa wanausalama katika kisa cha WAKALA WAGIZA sasa amerejea akiwa na muonekano mwingine kabisa.
.
  Hadi kurejea kwake kazini alikuwa ameshaacha maafa mengi sana ikiwemo kupoteza maisha kwa Mutonga kule kwenye nyumba ya Mzee Mabina, sasa anaaamua kuungana na Scorpio katika kutafuta ukweli juu ya mwenzao ambaye hakuwa amerejea kabisa tofauti na kazi waliyompa muda iliyokuwa ikitaka ifanyike.

*SCORPIO BA JOSEPHINE NDANI YA NYUMBA
*NORBERT AZIDI KUSOGELEA HIMAYA YA MAADUI ZAKE




ITAENDELEA!!


No comments:

Post a Comment