Monday, February 6, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA NNE

WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com





SEHEMU YA NNE!!
Huo ndiyo ulikuwa ni mwisho wa Mwanamama huyo aliyekuwa na wahka wa kufungua kile kilichokuwa hakimuhusu, mdharau mwiba  mguu huota tende na ndiyo hayo yaliyomkuta hapo mlangoni mwa nyumba yake umbali wa mita kadhaa kutoka mahali nyumba yake ilipo.




___________-TIRIRIKA NAYO

   Asubuhi iliyofuata ndiyo taarifa za vifo vyote vilivyokuwa vimetokea usiku uliopita viliweza kuzagaa na kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi tu, muda huo tayari IGP Mbwambo alikuwa ameshapokea taarifa ya kufariki kwa vijana wake ambao hawakuwa na hata saa ishirini na nne tangu awapatie kazi ya kwenda kuifanya. Tangu aipate taarifa hiyo hakuwa na amani kabisa na kichwa chake kilivurugika. Hakuelewa kabisa kwanini watu wa aina moja walikuwa wakisababisha mauaji hayo ndani ya sehemu tofauti za miji ya nchi ya Tanzania, vifo vya watu wawili waliokuwa sehemu tofauti kwa bomu na pia kifo cha kijana wake aliyekutwa amevunjwa shingo ndani ya nyumba ya Mabina vilimfanya achanganyikiwe kwa  muda alipokuwa ameipokea taarifa akiwa yupo ofisini.

  Tayari kabisa alikuwa ameshapokea simu ya Waziri wa mambo ya ndani pamoja na Rais Zuber Ameir juu yajambo hilo,tishio la kigaidi ndani ya nchi hii ndiyo lilikuwa lipo ndani ya kichwa chake hakuwaza kabisa jingine juu ya kutokea kwa vifo hivyo. Watu kufa vifo vya aina hiyo tena katika muda ambao Tanzania ilikuwa na mahusiano mazuri sana na mataifa mengine na wala haikuwa na ugomvi  na nchi yeyote, wanausalama wa jeshi la polisi waliokuwa wakitumiwa kwa ajili ya kazi nzito kama hizo na hata kufanya utafiti wa matukio ya kigaidi ndiyo  hao walikuwa tayari wameshauawa ndani ya siku hiyohiyo waliyokuwa wamepewa kazi iliyokuwa ikihitajika kukamilishwa haraka iwezekanavyo. IGP Mbwambo alisita kabisa moyoni katika kutoa wanausalama wengine waende kufanya kazi hiyo kwani alikuwa alihofia kuweza kupoteza zaidi vijana wake  aliamini kabisa kuwa suala hilo halikuwa ndani ya uwezo wao kabisa. Alijishauri sana na hatimaye alitaka kupiga simu lakini alisita baada ya kuwahiwa na mlio wa simu yake ya mezani hiyo aliyotaka kuipiga, ilimbidi aipokee simu hiyo kwa haraka sana.

"Ndiyo Mhehimiwa......sawa nakuja sasa hivi" Aliongea baada ya kusikiliza agizo alilopokea kwenye simu hiyo, ilimbidi atoke kwa haraka ndani ya ofisi yake  kuwahi huko alipokuwa ameitwa kwani ilikuwa ni amri ya Mkubwa kuliko wote.





BAADA YA  ROBO SAA
 IKULU 
 MAGOGONI
DAR ES SALAAM


   Ndani ya chumba cha mkutano ndani ya Ikulu Rais Zuber alikuwa ameshaitisha kikao cha haraka sana kutokana na hali iliyokuwa ikitokea ndani ya Tanzania katika sehemu tofauti. Wazri mmoja,wanausalama watatu  pamoja na raia mmoja kufa katika ndani ya siku moja katika vifo vilivyokuwa vikihusiana na ndiyo suala ambalo lilimfanya kwa haraka sana Rais Zuber aitishe kikao hicho cha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini. Mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa Professa Moses Gawaza, Mkuu wa jeshi la polisi IGP Mbwambo, Mkuu wa majeshi nchini Jenerali Marwa, Mnadhimu mkuu wa jeshi nchini Luteni Jenerali Belinda na pamoja na Rais Zuber mwenyewe ndiyo walikuwa wahudhuriaji wa kikao hicho cha dharura ndani ya Ikulu.

"Jamani hii sasa ni too much haiwezekani ndani ya siku moja watu muhimu ndani ya serikali yetu wateketee bila ya sababu. Ni siku nyingi zimepita tangu ubainike wizi wa mabilioni la shilingi katika mamlaka ya mapato, Tanesco, bandarini na katika mapato ya mgodi wa almasi uliogunduliwa Dodoma. Mapato haya yangeweza kuisaidia wanafunzi wa ngazi zote nchi nzima kusoma bure na hata wananchi kupata matibabu bure, lakini kutokana na walafi wa watu wachache waliopo ndani ya serikali yangu mapato hayo yameishia ndani ya matumbo yao. Iliundwa kamati nafikiri baadhi yenu mlikuwa hamjui kuwa kamati hiyo ilikuwa ikiwahusu kina nani zaidi ya kuwajua kuwa ilikuwa ikiwahusu mawaziri wawili pamoja na mbunge mmoja, ilipewa jukumu la kufanya  utafiti wa kila  kitu kwa muda wa mwezi mmoja tu na kisha ripoti hiyo iwasilishwe bungeni na wahusika wachukuliwe hatua. Sasa basi napenda mtambue kuwa kamati hii haikuwa peke yake katika kufanya kazi hii, bali vijana wangu waliopo  chini ya Moses hapa walijumuika nao katika kufanya uchunguzi huo. Vijana hao ndiyo waliaandaa ripoti nzima ya uchunguzi huo na kisha ikawasilishwa kwa kamati iliyoteuliwa kuikamilisha kazi hii,kundi hili liliongozwa na Mabina mkurugenzi wa NSSF na msadizi wake Jama Wa Majama" Rais Zuber aliongea na alipofika hapo aliweka kituo akawatzama wote kama walikuwa wakimsikiliza na kisha akaendelea.

"Kundi hili lilifanikisha kufanya uchunguzi wao na kila  Mhusika tayari alikuwa ameshawekwa kwenye faili na wakawasilisha kwa Bai ambaye ndiyo kiongozi wa kamati maalum iliyoundwa, faili hilo lilipomfikia Bai hakuchukua muda aliuawa kwa bomu. Watafiti wakuu wa hilo suala mmojawapo ambaye ni Mabina nafikiri mnatambua kabisa kuwa hatunaye duniani naye kauawa kwa bomu, siku hiyohiyo mke wa Jama naye kauawa kwa bomu akiwa yupo getini  tu mwa nyumba yake. Hilo suala liliingia pengine baada ya vijana wa CID wa kuaminika kuaawa ndani ya  siku moja katika miji tofauti, hapa inaonekana wazi kuwa kuna mtu anatuzunguka na si vnginevyo. Nimewaita hapa ili niwasikilize na nyinyi juu ya suala hili" Rais Zubber aliongea na kisha akaketi chini, muda huo simu ya Moses iliyokuwa ipo mezani ilitetemeka mara tatu kuashiria kuwa ulioingia ulikuwa ni ujumbe mfupi. Moses aliufungua ujumne huo na kisha akausoma ambapo aliishiwa nguvu kabisa alipoumaliza ujumbe huo, alijikuta akinyoosha mkono juu baada ya kuumizwa alipousoma huo ujumne na kupelekea Rias Zuber amruhusu azungumze.

 Moses alisimama kisha akakamaa kiheshima kumpa heshima yake Rais Zuber na kisha akaongea, "Kwanza napenda niwape taarifa mpya ambayo imenifikia sasa hivi kupitia simu ayngu ya mkononi,waziri aliyesalia wa kamati maalum pamoja na wabunge wote wameuawa kwa bomu ninavyoongea hivi sasa"

  Taarifa hiyo iliwamfanya kila mmoja aliyekuwa humo ndani kushtuka na kuona kuwa nchi ilikuwa ipo kwenye hatari kubwa sana, wote walisikitika kwa kipindi cha muda mfupi na kisha wakanyanyua macho yao kumtazama Moses aliyewapa taarifa hiyo.

"Vijana wote waliokuwa wakifanya utafiti chini ya Mabina nao hawapo duniani wameuawa kwa namna hiyohiyo, aliyesalia ni Jama tu ambaye hajulikani yupo wapi hadi sasa kwani nyumbani kwake ametoweka baada ya kupokea simu iliyokuwa imemuambia angeletewa Wito wa kuzimu hapo nyumbani kwake. Majirani zake wamesema ametekwa na watu wasiojulikana lakini yeye amepiga simu kwa Secretary wangu na kumpa taarifa kuwa yupo salama ila hajataja mahala alipo" Moses aliendelea kueleza na watu wote ndani ya chumba hicho cha mkutano walitulia kumsikiliza.


"Mheshimiwa Rais, na wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini napenda kusema neno lifuatalo. Suala hili limefikia katika ngazi ambayo si ya jeshi la polisi tena bali ni ngazi ya  Usalama wa taifa pamoja na Millitary intelligence maana hivi ndiyo vyombo vynye dhamana ya kuilinda nchi yetu hii dhidi ya mambo kama hayo. Hivyo kazi hii haipaswi kushughulikiwa na  chombo cha kuhakikisha sheria zinafuatwa ndani ya nchi bali ni vya usalama wa nchi, hivyo basi suala hili lipo ndani ya uwezo wetu na naamini kabisa hadi kufikia hivi sasa suala hili litakuwa limeshafika mikononi mwa EASA hivyo napenda jeshi la polisi likae kando na liwe linatoa ushirikiano na si kujiingiza moja kwa moja kwani kufanya hivi nikuendelea kupoteza vijana  wa jehi hilo. Ni hayo tu" Moses alipomaliza kuongea maneno hayo aliketi kwenye kiti chake.


****

"Daddy ona ona nimeweza na mimi kutengeneza kite, ngoja niirushe kama wewe" Mtoto mdogo alimuambia baba yake wakiwa wapo jirani kabisa na bwawa la kuogelea ndani ya nyumba ya kisasa sana.

"Woow! Thats my boy upo very sharp, umenishinda hadi mimi baba yako" Baba mtu ambaye alikuwa ni kijana mtanshati sana aliongea huku akimkumbatia mwanae na kumbeba kiupendo zaidi.

"Daddy nikufundishe na wewe kabla mammy hajaja hapo na kukucheka umeshindwa kutengeneza wakati  mimi nimeweza"

"Enhee! My boy umeongea nifundishe fasta kabla hajarudi yule ameenda kufuata icecream tu, akirudi atanicheka"

"Ok Daddy" Mtoto huyo aliitikia na kisha baba yake akamshusha  chini, kwa haraka mtoto huyo alianza kutengeneza Kishada cha baba  yake lakini hakumaliza kwani sauti ya Mama yake akicheka ilisikika na kumfanya aache na kumuangalia.

"Loh! Yaani wewe Nor huna haya kabisa yaani unampa Jerry ndiyo akutengenezee Kite. Hiloooo! Mtoto anakushinda" Alitokea Mwanake akiwa amevaa mawazi ya kuogelea ambapo alikuwa amejifunga mtandio kiunoni na sehemu ya juu ipo wazi.

"Mummy usimcheke Daddy hawezi kutengeneza namsaidia, I love him" Jerry aliongea


   Mwanaume huyo aliyekuwa akisaidiwa kutengeneza Kishada na mtoto wake hakuwa mwingine ila ni Norbert Kaila akiwa na Norene mpenzi wake wa siku nyingi pamoja na Mtoto wao nyumbani kwao katika bwawa la kuogelea, alikuwa ndiyo ana siku kadhaa tangu arudi kwenye kwenye kazi nyingine ya kijasusi nchini Burundi alipoenda kushirikiana na Jasusi mwenzake Allison Frank ambaye alishirikiana  naye katika kisa cha JINAMIZI pia ndani ya nchi ya Tanzania, muda huo alikuwa yupo mapumzikoni yeye na mpenzi wake ambaye ni jasusi mwenzake aliyekuwa maepewa likizo na yeye. Ulikuwa ni muda wa kufurahia yeye na familia yake na alikuwa yupo ndani ya nyumba hiyo kwa siku tatu mfululizo hakuwa ametoka nje kabisa, alichojali yeye ilikuwa ni kufurahia na familia yake katika muda huo ambao alikuwa amepewa na mkuu wake wa kazi. Ulikuwa ni muda ambao alikuwa akiusibiri kwa hamu sana aweze kupata na sasa ndiyo huo, hakutaka autumie kimakosa kwani alitambua familia yake nayo ilikuwa ikitamani sana muda huo upatikane aweze kukaa nao.

"Haya mtu na baba yake" Norene aliongea

"Na utuache kabisa, Jery mwanangu nitengenezee fasta kubwa kabisa kushinda hiyo Kite ya Mummy wako" Norbert alidakia.

"Ok Daddy" Jerry alijibu huku akiendelea kutengeneza Kishada kwa ajili ya baba yake, kamba ya Kishada hicho alichokuwa akikitengeneza ilipeperuka kwa bahati mbaya na ikapelekea anyanyuke aikimbilie huku wazazi wake wakiwa wanamtazama wakiwa wana furaha sana.

  Muda huo Jerry alivyonyanyuka tu kwenda kufuata kamba ya Kishada alichokuwa akikitengeneza, ndiyo muda ambao simu ya mkononi ya Norbert iliita na kumfanya aitupie jicho lakini kabla hajafikiria hatua ya kuipokea tayari Norene alishaipokea na kuiweka sikioni.

"Mkuu..... ndiyo huyu hapa" Norene aliongea na kisha akampatia simu Norbert na kumpa ishara ya kijasusi zaidi.

"Heshima yako mkuu.....sawa muu nipe dakika kumi na tano tu nitakuwa hapo ofisini" Norbert aliongea na kisha simu ikakatwa, aliiweka simu pembeni na kisha akashusha pumzi kwa maneno aliyoyasikia.

"Vipi Nor mbona hivyo?" Norene aliuliza


"Haki ya Mungu hii kazi ni balaa yaani nimetoka Brundi majuzi tu sasa hivi naitwa kwa ajili ya kazi nyingine, muda wa kukaa na familia hamna kabisa yaani"

"Nor muhimu kufuata majukumu ila naomba uwe makini sana najua unamuona Jerry alivyo mdogo pale bado anahitaji malezi yako"

"Hilo usihofu ngoja niwahi ofisini nikamsikilize"

   Norbert kwa haraka alinyanyuka mahali alipokuwa amekaa kisha akaingia ndani, alitumia muda wa dakika takribani tano akwa amemaliza kujiandaa amako alitoka akamkuta Jeery akiwa ameshamaliza kutengeneza Kishada alimchomuagiza

"Daddy look" Jeery aliongea huku akimuonesha Baba yake, Norbert alipoona kishada alichomuagiza kilikuwa kimekamilika alimnyanyua juu kwa furaha na kisha akawa anakiangalia Kishada alichomtuma amtengenezee.

"Its so nice my boy, mpe Mummy aniwekee ninaenda kukuchukulia zawadi nikirudi tu ninaanza kukichezea" Norbert aliamua kumdanganya mtoto wake na kisha akamshusha na kumuacha akienda kwa Norene.

"Byee daddy" Jerry alimuaga huku akimpungia mkono, muda huo Norbert alikuwa akichangamka sana kuelekea kwenye maegesho ya magari hapo nyumbani.

"Byee" Alijibu huku akikazana kuelekea kwenye moja ya magari yaliyokuwa yapo hapo eneo la maegesho ambalo halikuwa mbali sana kutoka kwenye eneo ambalo lilikuwa na bwala la kuogelea.



****


"Mheshimiwa Rais hata mimi sishauri kabisa vijana wa jeshi la polisi waingie kwenye hii ishu, wao wawe wanatoa msaada tu mdogo ukihitajika" Jenerali Marwa aliongea kisha akaketi kwenye kiti chake, muda huohuo IGP Mbwambo naye alinyoosha mkono.

"Ndiyo Mbwambo" Rais Zuber alimruhusu, IGP Mbwambo alipopokea ruhusa hiyo alisimama na akatoa saluti kwa Rais Zuber.

"Mheshimiwa Rais sipo tofauti na wenzangu kutokana na hali hii ilivyo, vijana waliopotea kwenye kadhia hii ni wa kitengo cha CID na ndiyo kitengo chenye uwezo mkubwa ndani ya jeshi la polisi. Sasa basi haina haja ya kumaliza vijana wengine ikiwa vijana wenye uwezo mkubwa kuliko wao wapo ndani ya nchi hii wapo, mimi nipo tayari kutoq msaada tu ambao ni lazima utoke kwangu na vijana wangu tu. Hili suala nimeliacha kwa wenzangu" IGP Mbwambo aliongea na alipomaliza alikaa chini.

"Vizuri sana je kuna mwenye la ziada?........ Ok sasa basi kuanzia hivi sasa vijana wa Usalama wa taifa na wa Millitary intelligence waingie kazini maana inaonekana hili kundi kubwa sana hivyo kikosi kiongezwe , sina la ziada ni hayo tu" Rais Zuber aliongea akatoka ndani ya chumba hicho cha mkutano akiwaacha wakuu hao wa vyombo vya ulinzi na usalama wakitazamana  usoni mwao kila mmoja kutokana na agizo hilo la muda ambalo lilikuwa la ghafla sana.




****

   Hakuenda tofauti na alivyotoa ahadi yake kwa mkuu wake wa kazi, Norbert ndani ya dakika kumi tu tayari alikuwepo nje ya hoteli ile ambayo ilikuwa ndiyo ina ofisi za EASA  tawi dogo la Dar es salaam maeneo ya Ilala mtaa wa Lindi. Alishuka akapitiliza mapokezi ambako aliwakuta wasichana  ambao aliwazoea kuwakuta. Siku hiyo kutokana na haraka aliyokuwa nayo aliwapungia mkono tu na kisha akaingia kwenye lifti kwa haraka sana, lifti hiyo ilishuka chini hadi kwenye sehemu ambayo ofisi zao zipo ikasimama. Alishuka kwenye lifti hiyo na kisha akaanza kutembea kuufuata ukumbi mwembamba ambao ulimpeleka hadi eneo lenye mlango ambao ulikuwa na sehemu ya kuweka alama ya mkono, hapo aliweka kiganja chake cha mionzi ya kijani ilitokea kwenye eneo hilo na kisha mlango huo ukafunguka huku ukitaja maneno ya kumkaribisha kupitia spika za tarakilishi iliyokuwa imeunganishwa hapo. Norbert aliingia ndani na mlango huo ulijifunga na kisha alianza kutembea akipita vyumba mbalimbali vya ofisi ambako kulikuwa kuna wafanyakazi aliwasalimia kwa uchsngsmfu.

 Norbert alienda hadi kwenye mlango mlango uliokuwa na maandishi yaliyosomeka 'CE', aliufungua mlango huo akaingia ndani kwenye ofisi ambayo alizoea kumuona Norene. Ndani ya ofisi hiyo alimkuta Msichana mwingine ambaye hakuwa mgeni kabisa kwake ambaye alikuwa hapo kutokana na Norene kuwa likizo, Msichana huyo alikuwa akifahamiana naye sana.

"Naona wewe kijogoo umekuja leo,  mke wako umemkosa" Msichana huyo alimuambia

"Kwa akaliaye kiti hicho siku zote ni mke wangu sasa sijamkosa huyo hapo nimemkuta" Norbert aliongea na yeye

"Loh! Lione hivi ukijogoo utaacha lini wewe?"


"Simba akiacha kung'ata na mimi ndiyo nitaacha"



*NORBERT KAILA NDANI YA NYUMBA

*KAZI IMEENDA KWA TISS NA MILLITARY INTELLIGENCE




ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment