WITO WA KUZIMU
NA: HASSAN O MAMBOSASA
MAHALI:TANZANIA
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
+255762 219759
BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com
SEHEMU YA SITA!!
"Haya nyanyuka mwenyewe tena ukiguna maumivu tu kwa sekunde chache wakati nakupa amri hii nakuongeza tena, uongoze njia unipelke ilipo lapatop hiyo"
Hakuwa na ujanja tena wa kuweza kuipinga amri hiyo kutokana na mapigo hayo mawili ya nguvu aliyokuwa amepewa ndani ya dakika zisizozidi mbili tu, mwenyewe aliongoza njia na kumpeleka huko kulipokuwa na kitu hicho alichokuwa akikitafuta Mgeni wake.
NA: HASSAN O MAMBOSASA
MAHALI:TANZANIA
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
+255762 219759
BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com
SEHEMU YA SITA!!
"Haya nyanyuka mwenyewe tena ukiguna maumivu tu kwa sekunde chache wakati nakupa amri hii nakuongeza tena, uongoze njia unipelke ilipo lapatop hiyo"
Hakuwa na ujanja tena wa kuweza kuipinga amri hiyo kutokana na mapigo hayo mawili ya nguvu aliyokuwa amepewa ndani ya dakika zisizozidi mbili tu, mwenyewe aliongoza njia na kumpeleka huko kulipokuwa na kitu hicho alichokuwa akikitafuta Mgeni wake.
_____________TIRIRIKA NAYO
Uchungu wa kipigo hakika aujuaye mpigwaji, maumivu yote ya kipigo haulizwi mpigaji. Majibu yake aliyokuwa akiyajibu aliona wazi ilikuwa ni dharau kubwa sana kwa Msichana huyo aliyeingia hapo ndani ya nyumba yake, ilikuwa ni sawa kunenepa ilihali aliyekuwa anakudai anakonda huku ukidai hali ni ngumu ndiyo mana hujalipa deni. Kipigo hicho kilimtosha wazi kuongoza hadi ndani ya chumba chake ambapo alienda hadi kwenye mtoto wa kitanda wa pembeni, hapo alifungua na kutoa Tarakilishi ya mapakato ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwenye mkoba maalum na alimpatia Msichana huyo huku akiwa bado anaugulia maumivu hayo.
Msichan huyo aliichukua Tarakilishi hiyo ya mapakato na kisha akaifungua na kuitazama muundo wake ilivyo, baada ya hapo alimkazia sana uso Bi Sakina ambaye alikuwa akiugulia maumivu akiwa amesimama wima. Alisonya kwa nguvu sana na kisha aliachia teke la pembeni ambalo lilimpata kwenye goti, mfupa wa goti wa Bibi Sakina ulitoa sauti ya kugoka na yeye mwenyewe akabaki akitoa ukelele wa maumivu. Alianguka chini moja kwa moja akabaki akishikilia goti lake ambalo lilikuwa limepatwa na kadhia hiyo ya kupigwa na miguu ya mrembo ambayo ilikuwa ni imara na yenye nguvu sana.
"Weee! Kelele kabla sijakuongeza pigo jingine" Msichana huyo aliongea na alipoimaliza kauli yake tu alimuongeza teka jingine ambalo lilimfanya aende kujipigiza kitandani akajeruhika zaidi hata alivyojeruhika hapo awali.
Baada ya kumpa pigo hilo mwenye nyumba na Mwenyeji wake aliamua kufungua mkoba wake aliokuwa amekuja nao, alitoa Bahasha na kisha akaiweka chini kwenye miguu yake. Hakutaka kupoteza muda baada ya kuiweka bahasha hiyo, aliamua kugeuka nyuma na kisha akaanza kutoka humo ndani ya cnumba hicho. Alitembea kwa mwendo wa madaha ambao haukuwa ukiendana kabisa na kazi ya ukatili hiyo aliyokuwa akiifanya, alipofika mlangoni alishika kitasa cha mlango huo na kisha akanyonga na kupelekea mlango ufunguke. Alipiga hatua kutoka nje lakini alijikuta akisita na kisha akageuka nyuma na kumtazama Mmiliki wa jengo hilo ambaye alikuwa amemfanyia uonevu mkubwa sana, alionesha sura ya huruma sana alipomtazama Mwenyji wake kama alikuwa akijutia sana kwa kile alichokuwa akikifanya kwake.
"Ubishi wako ndiyo chanzo cha yote haya, chukua malipo yako hayo ambayo laiti ungenipa kwa amani tu hii Laptop ungeyapata na ufaidike. Bakshishi yako hiyo pamoja na wito" Aliamuambia Bi Sakina na kisha akatoka ndani ya chumba hicho na akafunga mlango
Hakutaka kusubiri kitu kingine kabisa yeye alitoka moja hadi lilipo gari lake hapo nje, aliingia ndani ya gari hiyo na kisha akaketi kwenye kiti kwa haraka sana. Akiwa bado ni mwenye haraka aliwasha gari na kuliweka gia na kisha akaondoka katika eneo na kwenda kusimama mita kadha mbele, alipolisimisha gari hilo tu mlipuko mzito ulisikika kutoka nyuma yake na ilimpelekea aangaze macho huko unapotokea mlipuko huo. Aliweza kuishuhudia nyumba ya ambayo alikuwa ametoka kuingia muda mfupi uliopita tu ikiwa inateketea kwa moto, usoni aliachia tabasamu alipoiona nyumba hiyo ilikuwa ikiteketea kwa moto.
Baada ya hapo alichukua simu yake ya mkononi ya kisasa na kisha akatafuta sehemu ya majina na alipopata jina alilokuwa akilitafuta aliweka simu hiyo sikioni, akiwa ameweka simu hiyo sikioni mguu wake wa kulia ambao alikuwa ameutoa sehemu ya mafuta na kuupeleka sehemu ya breki akiurudisha ulipokuwa awali. Aliliondoa gari kwa mwendo mkubwa sana huku mkono mmoja ukiwa upo sikioni, mkono mwingine ulikuwa upo kwenye usukani kuweza kuliweka gari kwenye muelekeo mzuri kabisa.
"Kazi imeshaisha imebaki kwako uende Kiwalani sasa hivi ukachukue Laptop nyingine hadi zote tano zitimie" Aliongea na kisha akakata simu bnada ya mtu aliyekuwa amempa maelekezo kumuambia kuwa alikuwa ameyaelewa maelekezo yake.
****
Akiwa ndani ya pikipiki yake mpya kituo chake cha kwanza kilikuwa ni ndani ya nyumba yake ambayo alikuwa akiishi na mpenzi wake,Norbert alipofikisha pikipiki hiyo eneo la maegesho tu aliizima na kukimbilia kwenye eneo la bwawa la kuogelea ambapo alikuwa ameiacha familia yake ikiwa ipo inacheza kwenye eneo hilo kwa pamoja. Jerry alipomuona tu alimkimbilia kwa haraka na alipofika miguu kwake alimnyanyua na kumuweka mikononi mwake, Norbert alimbeba Jerry na akaelekea hadi kwenye kochi la kupumzika jirani kabisa na bwawa la kuogelea. Aliketi jirani na mpenzi wake huyo na kisha akambusu mdomoni, wote wawili walikumbatiana kwa upendo mkubwa sana wakiwa wamemuweka mtoto wao katikati yao.
"Nipe ripoti ya huko" Norene aliongea baada ya kuachiana
"Aisee hii kazi ni kiboko, nina gunia jipya yaani nikitoka hapa naingia mzigoni" Norbert aliongea
"Yote heri tu ila kwangu la muhimu uende salama na urudi salama sitaki nije kulia mimi na mwanao hapa"
"Hilo usihofu kabisa, nitunzie mwanangua mimi naingia mzigoni" Norbert aliongea na alipomaliza alinyanyuka pale alipokuwa ameketi.
"Jerry acha nikakuchukulie zawadi my boy nitarudi sasa hivi" Alimwambia na kisha akaondoka eneo hilo baada ya kumbusu mpenzi wake na pia kumkumbatia mtoto wake. Alitumia pikipiki aliyokuwa amekuja nayo hapo, aliondoka hapo nyumbani kwake na safari ya kuelekea huko kazini ndiyo ilianza.
Robo saa baadaye alikuwa yupo ndani ya eneo la Yombo Kiwalani ambalo ndiyo alipanga kuanzia kazi, aliingia ndani ya kitongoji hicho ambako alielekea hadi kwenye mtaa ambao ulikuwa na nyumba chache sasa. Mtaa huo ndiyo ulikuwa ni lengo lake la kwanza kabisa kuweza kuianza kazi hiyo aliyokuwa amepewa. Ilikuwa ni miti kadhaa kila baada ya nyumba kuashiria kuwa eneo hilo ndiyo watu walikuwa wakihamia mida hiyo kwa kasi, baada mwendo mfupi ambao ulikuwa umemjaza hamasa ndani yake hatimaye alikuwa akikaribia kufika kwenye nyumba ambayo alikuwa akitarajia kwenda kuanzia kazi.
Kila alipozidi kuikaribia nyumba hiyo ndiyo mapigo yake ya moyo yalivyokuwa yakimuenda mbio sana, akiwa amebakisha mita chache kabisa aifikie alisikia sauti ya honi ya nguvu sana kutoka nyuma yake, alipoangalia kupitia vioo vya pembeni aliiona gari aina ya Subaru impreza ikiwa inakuja kwa kasi sana. Mlio huo wa honi ya gari hiyo ambayo inasifika sana kwa mwendo, alitaka kuongeza mwendo aendane na kasi ya gari hiyo lakini kutokana na ukaribu wa eneo ambalo yupo aliamua kusogeza Pikipiki yake pembeni na gari hiyo ikapita kwa kasi sana. Gari hiyo pamoja na mwendo huo wa kasi ambao ilikuwa imempita nao ilikwenda kusimama palepale kwenye nyumba hiyo aliyokuwa anaelekea, Norbert bado akiwa anaisogelea hiyo nyumba aliweza kushuhudia ndani ya gari hiyo akishuka Kijana mwenye asili ya shombe ambaye mikononi mwake alikuwa ana michoro mingi sana. Kijana huyo aliposhuka tu ndani ya gari hiyo aliangalia katika upande ule ambao alikuwa anakuja Norbert.
Kitendo cha Kijana huyo kumuona mtu kwenye pikipiki kilifanya asite kabisa kuingia ndani ya nyumba hiyo, aliganda akimtazama huyo mwenye pikipiki hiyo ya kisasa. Alijikuta akitoa tabasamu tu alioiona pikipiki hiyo na hadi inafika karibu yake alijikuta akiisimamisha, mwenye lengo kama lake na nyumba hiyo ambaye alikuwa yupo kwenye pikipiki alijifanya alikuwa akitaka kuipita nyumba hiyo. Aliposimamishwa alisimama na kisha akafungua kofia ya aliyokuwa ameivaa kichwani, yule kijana mwenye asili ya Shombe alitoa tabasamu baada ya mwenye pikipiki kusimama.
"Unaendesha chombo cha ndoto yangu, Ha! Ha! Nikupongezae kwa kumiliki chombo kama hicho" Aliongea akionekana kuvutiwa sana na pikipiki hiyo
"Thats my dream" Mwenye pikipki aliongea huku akishika sehemu ya tenki la mafuta la pikipiki hiyo
"Sina kingine mkuu ni kukupa hongera tu, nice Bike" Kijana huyo aliongea na kisha akamuonesha ishra ya ngumi, Norbert aligonga ngumi hiyo kuangana naye na kisha aliiondoa pikipiki kwa mwendo wa kasi sana kuelekea mbele zaidi.
Kijana huyo aliingia ndani ya nyumba hiyo akionekana alikuwa akiifahamu zaidi, alitoa funguo ambazo ndiyo alitumia kuingia nazo ndani ya nyumba hiyo. Aliingia ndani akiwa amehakikisha kuwa nje ya nyumba hiyo kulikuwa kupo salama sana, baada ya kuingia ndni ya nyumba hiyo alifunga lango kuu la nyumba hiyo kama vile kulikuwa hamna mtu ndani ya nyumba na yeye ndiye alikuwa akiingia pekee.
****
Kufunguliwa kwa mlango wa mbele ambao ulikuwa ni mlango mkuu ndani ya nyumba hiyo, kulimshtua sana Mwanamke aliyekuwa amekaa kwenye kochi la kisasa akiangalia filamu. Alishtuka sana alipoona mlango huo ukifunguliwa na kisha kiatu cha kisasa aina ya raba kikitanguliwa, mwanamke huyo aliweza kumshuhudia Kijana ambaye hakuwahi kumtia machoni mwake kabla na hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kuweza kuonana naye.
Aliingia yule kijana ambaye alikuwa ametoka kuongea muda mfupi uliopita na Norbert akiwa ni mewnye mavazi ya kisasa sana, mwanamke huyo alibaki akimkazia macho sana kijana huyo mgeni ndani ya macho yake. Alibaki akijiuliza alikuwa ameingia vipi ndani ya nyumba hiyo hadi afike hapo, milango ilikuwa imefungwa lakini aliweza kuingia ndani ya nyumba hiyo.
"We ni nani na umeingia vipi hapa?" Alijipa ujasiri sana ingawa moyoni alikuwa na hofu sana, ujasiri wake ulimuwezesha kuuliza swali hilo.
"Ni mimi hapa nisiye na jina, nisiyezuiwa hata kwa mlango wa chuma ndiyo nimeingia" Kijana huyo aliongea na kisha akasogea hadi jirani na huyo Mwanamke, alijibwaga kwenye kochi na kisha akaachia tabasamu akimtazama huyo mwanamke.
"Unashangaa kuingia ndani ya nyumba hii ukiwa umefunga milango, Haaaa! Mzimu toka lini ukazuiwa na mlango wewe. Haya hebu kanipe Laptop ya marehemu haraka sana"
"Wee nani?"
"Mzimu kutoka kuzimu nimetumwa kuja kuchukua laptop na Marehemu, sitaki kupoteza muda ongoza njia ilipo unipe"
"Sitoi nakuambia"
"Oooh! Hujui kuwa unaongea na Mzimu wewe, haya ongoza njia mwenyewe" Kijana huyo alipoongea maneno hayo yaliambatana na mkono wake kuingia kinenani, alipoutoa ulikuwa na Bastola jambo ambalo lilimfanya Mwenyeji azidi kuingiwa na hofu zaidi. Alitetemeka akawa anajaribu kujisogeza pembeni ya kochi alilokuwa amekaa pembeni ya kijana huyo, hiyo haikusaidia kitu kabisa kutokana na uwepo wa chombo hicho cha moto kisicho na mzaha kabisa. Chombo ambacho kikikohoa basi ni hatari tupu kwa mkoholewaji wake, mwenyeji wake aliingiwa na ubaridi wa ghafla kwenye moyo wake alipoelekezewa hiyo silaha.
"Ongoza njia ukanipe" Aliamriwa
Mwenyewe bila ya kupenda aliongoza njia na kwenda kutoka hicho kilichokuwa kikihitajiwa, alitembea kwa uoga akiwa anaufuata ukumbi mwembamba ambao ulikuwa upo kwenye njia ya kwenda huko chumbani kwake ambapo kulikuwa na kitu hicho ambacho Mgeni mvamizi wake alikuwa akikihitaji kwa haraka sana. Kutembea huko kulimbidi avuke kizingiti cha hapo sebuleni ndiyo aweze kuingia kwenye ukumbi mwembamba unaotenganisha vyumba, ukumbi huo ambao mwanzoni mwake kulikuwa kuna mlango wa jiko kwa upande wa kushoto.
Mwanamke huyo alitangulia kuongoza njia ambapo ilimbidi avuke vizingiti mbalimbali akianzia hicho cha jiko ndiyo aweze kufika chumbani kwake, alikipita vizuri kizingiti cha hapo jikoni lakini kwa aliyekuwa yupo nyuma yake kuna jingine jipya kabisa liliibuka. Yule Kijana alipotanguliza tu bastola yake kipindi akimuongoza yule mwanamke katika usawa wa mlango wa jiko, alijikuta akitoa yowe la maumivu la kabla hajakaa sawa miguu ya mtu ambaye alikuwa akibembea kwnye dari ya huko jikoni ilijitokeza kwa kasi na kisha yeye mwenyewe akaonekana.
Alionana ana kwa ana na Dereva wa pikipki ambaye alikuwa akimsifia kuwa alikuwa ana pikipiki nzuri, muda huo aliokuwa akionana naye huyo Dereva hakuwa na ujanja tena kwani silaha yake ilikuwa ipo mbali kabisa . Akiwa hata hajafikiria jambo jingine la kufanya alipokea mapigo manne ya karate yaliyokuwa yamejaa siha ya kutosha, alienda chini moja kutokana na mapigo hayo. Akiwa bado yupo hapo chini aliongezewa mapigo mengine ambayo yalimfanya hata siwe na nguvu kabisa ya kuendelea kupambana, alipokea kipigo kikubwa sana na pigo la mwisho kabisa alilokuwa amepokea kutoka kwa Dereva huyo wa pikipiki kwenye kofia lake kichwani ilikuwa ni kichwa cha pua ambacho kilimpata sawia kutokana na Dereva huyo kuvaa kofia ngumu. Alianguka chini kama mzigo akawa hana ujanja tena wa kupigana na adui yake.
Baada ya kutoa kipigo hicho kizito ndipo aliweza kugeuka na kumtazama mwanake yule ambaye alikuwa amekaa chini muda huo akiwa amejikunyata kwa uoga sana, alimsogelea hadi karibu kabisan na kisha akavua kofia yake aliyokuwa amevaa. Norbert ndiyo alionekana mbele ya huyo mwanamke ambapo alimuinua akiwa ni mwenye huruma, baada ya kumuinua huyo mwanamke alimtazama usoni na kisha akamgeukia adui yake ambaye hakuwa na nguvu hata ya kusimama hadi muda huo.
"Sipo hapa kwa ajili ya kukudhuru bali ni kutoa msaada, nafikiri mimi si mgeni kwenye macho yake. Hivyo punguza hofu kabisa na unisikilize kwa umakini sana, nenda katoe kile alichokuwa akikitafuta huyu nakusubiri hapa hii ni kwa usalama wake tu eneo hili halikufai" Alimuambia huyo mwanamke.
Mwanamke huyo kusikia kauli hiyo alitikisa kichwa kwa haraka sana kuitikia na kisha akaelekea chumbani kwake upesi, alimuacha Norbert ambaye alimrudia yule Mpinzani wake na kuanza kumpekua kwenye mifuko yake. Alimkuta akiwa na bahasha kubwa nyeuope pamoja na pochi ndogo,aliichukua hiyo pochi yake na kisha akaifungua na kukuta kukiwa na kadi na vitambulisho mbalimbali. Norbert aliiweka hiyo pochi mfukoni mwake na kisha akachukua bahasha hiyo nyeupe na kuanza kuifungua, alifungua kwa taratibu sana na akakutana na bahasha nyingine ndani ikiwa na stempu yenye picha ya mgongo wa mwanamke aliyejifunika shuka hadi kiunoni. Bahasha hiyo haikuwa tofauti kabisa na bahasha zile ambazo zilikuwa zikiwafikia wale wote ambao hadi muda huo hawakuwa na uhai. Norbert alitaka kuifungua bahasha hiyo lakini alisita bada ya kusikia sauti ya mtu mwenye viatu akija nyuma yake.
Aligeuka kwa kasi ya ajabu na kusimama pembeni akiwa ypo kujihami zaidi, alimuona yule mwanamke akiwa ameshika mkoba wa mabegani akiwa tayari amevaa kwa ajili ya kuondoka. Hapo alishusha pumzi na kisha akaamua kuachana na bahasha hiyo, aliiweka bahasha hiyo chini na kisha akamshika mkono Mwanamke huyo na kutoka naye humo ndani ya nyumba hiyo kwa kutumia mlango wa nyuma wa nyumba ambao ndiyo aliutumia kuingia humo ndani.
ITAENDELEA!!
No comments:
Post a Comment