Wednesday, February 1, 2017

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA MWISHO (KIPANDE CHA KWANZA)




RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________





SEHEMU YA AROBAINI NA SITA!!


>>>>>>SEHEMU YA MWISHO<<<<<<


    Josephine alikuwa amepigwa na mshngao sana aliposikia taarifa hiyo wala hakuwa amewaza juu ya kuwashwa kwa taa hizo ikiwa Wilson tayari kulikuwa na dalili tosha hakuwa amefika ndani ya nyumba hiyo. Alibaki akimtazama tu Mzee Ole ambaye uchungu ulikuwa umembana tayari ingawa machozi yalikuwa hayamtiririki kabisa, alikuwa ameinamisha kichwa chini. Ujasiri wake aliokuwa nao kipindi akiwa jeshini kabla hajaingia uwanja wa siasa ndiyo ulikuwa upo ndani ya moyo wake kwa muda huo ndiyo maana machozi hayakuwa yakimtoka kabisa, alikuwa asikitika kwa huzuni huku uso wake akiwa ameukunja kwa nguvu sana

                    "Aaaargh! Sasa naona ameamua kuikata furaha yangu, Aaaaargh!Norbert!" Mzee Ole aliongea kwa nguvu sana akiwa hajui kuwa huyo anayemuiita yupo hapo kwa umbali mita chache tu.

                    "My name(jina langu)" Norbert aliitika kidharaua na kusaabishwa wote kwa pamoja
watazame kule kwenye sebule ya chakula kwa mshngao.





______TIRIRIKA NAYO

    Mshtuko ndiyo uliyokuwa imeipata mioyo ya kina Josephine na Mzee Ole kwa kumuona Norbert akiwa mahala hapo katika muda ambao hawakutarajia kabisa atakuwepo, macho yalikuwa yapo upande ule wa meza ya kulia chakula wakionekana kutoamini kabisa kwa kile walichokuwa wamekiskiaa katika muda huo.

    Hawakuweza kuona chochote katika upande ule wa meza ya kulia chakula kutokana na giza nene lililokuwa lipo upande ule kwa muda huo wa usiku, mapigo ya moyo ndiyo yalikuwa yakienda mbio zadi kuliko hata akili zao za kufikiri jinsi ya kukabili mtu hatari kama huyo aliyekuwa yupo ndani ya himaya yao katika muda ambao hawakutarajia kabisa kama angeweza kufika ndani ya himaya hiyo. Hakika wasiwasi huondoa kabisa uwezo wa kufikiri wa mwanadamu akiwa nao ndani ya moyo wake, hiyo ndiyo ilikuwa kwa Mzee Ole na Josephine baada ya kusikia sauti ya Norbert kaika eneo hilo tena ikionekana alikuwa akiwangojea kwa hamu sana kwa kipindi cha muda mrefu walichokuwa wametoka ndani ya Ngome yao.

     Josephine aliyekuwa amevaa nguo ya mazoezi chini(trck suit) pamoja na fulana yenye ukosi mnene alikuwa ameingiwa na wasiwasi haswa alipofikiria kuwa ndani ya siku hiyo hawakuwa  wamebeba silaha yao zaidi ya ile ambayo alikuwa nayo Wilson walipokuwa wanaenda kummaliza Mufti. Alijilaumu kabisa kwa kosa hilo alilokuwa amelifanya la kutobeba silaha akiwa anatoka ndani ya nyumba hiyo na laiti kama angelikuwa ameebeba angeweza kuitumia kwa muda huo akiwa ndani ya ngome yao penye uvamizi.

    Hiyo haikuwa kwake tu bali hata kwa Mzee Ole aliyekuwa na lawama hizo ndani ya nafsi  yake kwa kuacha silaha zikiwa zote zipo ndani ya maficho katika nyumba hiyo, Mzee Ole pia aliulaumu uamuzi wake wa kuwaambia kina Wilson na Josephine wasibebe silaha walipokuwa wanaenda tukioni ili wafanye tukio kimyakimya. Aliona muda huo laiti kama angekuwa amewaruhusu kubeba silaha basi angeweza kabisa kuwa na mtu ambaye  angemmaliza  Norbert ndani ya muda mfupi tu, hapo ndiyo aliona umuhimu wa kutembea na siaha hata akiwa anaenda kwa rafiki yake ili iweze kumsadia kwani laiti kama ndani ya muda huo angekuwa anayo basi wangekuwa ni wao wakijiamini na ingekuwa ni zamu ya Norbert kuwa na wasiwasi nao lakini siku hiyo walikuwa wamewahiwa wao na sasa hawakuwa na ujanja wowote ule ndani ya muda ambao hawakuwa wamemuona adui yao alikuwa yupo namna gani. Akili  ya Mzee Ole tayai ilikuwa imefikia mwisho kabisa katika kubuni mbinu huku akili ya Josephine ikiwa imejiwa na mbinu mpaya kabisa ndani ya kichwa chake akiwa hata hajui kuwa kama angeweza kupata mbinu kama hiyo katika muda huo.

     Josephine alikuwa amekumbuka uwepo wa silaha za dharurra ambazo huwa wanazichomeka hapo sebuleni, alikukmbuka kabisa kuwa silaha hizo ndiyo zingeweza kumkomboa ndani ya muda huo. Alizungusha mboni yake ya jicho kwa wepesi zaidi akaona kochi lililokuwa lipo karibu yake ambalo ni kochi la kukaa watu watatu, kitendo cha haraka alichokifanya baada ya kuona kochi hilo hilo ilikuwa ni kujibirisha kwa nguvu sana hadi jirani na kochi hilo. Alifanya ushupavu wa hali ya juu kwa kupiga teke sehemu ya kwenye kochi hilo aina ya sofa ambayo ni chini ya sehemu ya kukalia katika eneo ambalo mtu akikaa basi nyama za nyuma ya ugoko ndiyo hugusa. Alipofanya hivyo sehemu ya kukalia ya kwenye kochi ilifunguka kama mlango wa jokofu la  kugandisha mabarafu,kwa haraka zadi alitia mkono ndani ya eneo ambalo mto wa kulaia wa kochi hilo ulifunguka akatoka na bastola aina ya IMD Desert eagle ambazo ndiyo silaha zao wanazozitegema katika kazi hizo.

      Kitendo kingine cha haraka alichokifanya ni kupiga sarakasi kwa nguvu sana kwenda pembeni kutoka katika eneo ambalo lilikuwa mkabala na eneo alilokuwepo Norbert, eneo hilo alibakia Mzee Ole ambaye muda huo tayari alikuwa ameshaanza kutabasamu huku akimtazama Norbert.

                   "Sawasawa Norbert najua ndiyo jina lako na umajileta mwenyewe bila ya kukutafuta, karibu kwenye mdomo wa mamba kijana" Mzee Ole alianza kuongea kwa kejeli, huku akigeuza jicho akimtazama Josephine aliyekuwa yupo pembeni katika eneo kulikuwa na kitufe ambacho alikibonyeza.

     Taa zilizokuwa zipo ndani ya sebule ya chakula ambazo hazikuwa zikiwashwa kwa umeme wa kawaida ziliwaka ndani ya muda huo na kumfanya Norbert aonekane akiwa amekaa kwenye kiti na wala hakuwa na wasiwasi wowote.

                 "Ulipozima taa hiyo kwa kutumia  siwchi iliyopo hukohuko ulidhani ndiyo umezuia usionekane, hapana hujafnikiwa kuzuia usionekane Norbert kuna taa za sola ambazo haziwashwi na siwchi hiyo" Mzee Ole alizidi kuongea kwa dharau kisha akacheka  kama vile siye yeye aliyekuwa akisikitika kwa kuambiwa taarifa ya kifo cha mdogo wake.

     Josephine alisogea  hadi pale alipokuwa amesimama Mze Ole na mkono wake mmoja ukiwa umeshika silaha ambayo alimuelekezea Norbert, uso wake ulikuwa na hasira sana hasa akikumbuka mtu huyo ndiyo alikuwa Muuaji mkubwa  aliyeua wenzao na hata mpenzi wake. Alikuwa akimtazama Norbert kwa macho ya chuki sana akiamini kuwa siku hiyo ndiyo ilikuwa ni arobaini yake na hakuwa na uwezo wa kutoka kwa shabaha alizokuwa nazo akiwa ameshika silaha mkononi mwake, shabaha hadi muda huo ilikuwa ipo katika kichwa cha Norbert tu ili aweze kumuangamiza na si kuendelea kusikiliza ngonjera zake ambazo huzileta akiwa amewekewa silaha ili aweze kumpoteza adua yake lengo.

    Mbinu hiyo tayari alikwisha itambua tangu siku ile alipoitumi kumuua Benjamin na sasa hakuwa tayari kuiruhusu imuhadae naye, alidhamiria kwa lengo moja tu ni kumuangamiza Norbert bila hata kuanza kusikiliza maneno yake ambazo huwa na maudhi pamoja na kukasirisha mtu ili amtoe nje ya lengo alilokuwa ameweka juu yake. Kukutana na  Norbert katika sehemu tofauti kulimfanya amuelewe vizuri juu ya mbinu yake hiyo na hakuwa tayari kumruhusu aitumie ndani ya muda huo amuue yeye kama alivyowaua Thomas na Benjamin.

                    "Norbert jua leo ndiyo siku yangu ya kulipiza kisasi jihesabie umekwisha" Aliongea akiwa na hasira sana kwa mwanaume huyo aliyelala naye zaidi ya mara moja.

                     "Ohoo unataka ulipe kisasi kwa mimi kumuaa mpenzi wako siyo nadhani ushachelewa kabisa Josephine a.k.a Leopard Queen, Mungu hakupenda kabisa nife na bastola hiyo uliyoishika hivyo huwezi kuniua wewe" Norbert aliongea kwa kujiamini.

                     "Anhaa! Nidyo uanvyojidanganya hivyo sasa jihesabie umeenda wewe na sikupi nafasi utoe ngonjera zako zenye maudhi kama ulivyofanya kwa mpenzi wangu ukampoteza lengo na kumuua. Kwaheri Norbert" Aliongea kisha akakiminya kitufe cha kufyatua riasi mara moja shabaha ikiwa kwenye kichwa cha Norbert.



DAKIKA TANO KABLA KUTIMIA SAA SITA KAMILI USIKU

    Muda huo  tu ulipofikia tu M,J Belinda alichukua simu yake ya mkononi na kuanza kutuma ujumbe uliojaa kielelezo katika sehemu mbili tofauti, baada ya kuhakikisha kuwa kila kitu kip sawa alikiweka vizuri kinasa sauti kisha akawa anatzama mbele kwenye mitambo ya Tarakilishi ambayo ilikuwa ikionesha wazi ramani ya eneo walilokuwepo hapo.

                      "Kaeni tayari masection kamanda wote kwa ajili ya kazi, Platoom sajenti wote anza kupanga watu wako vizuri mmenipata?!" Aliongea kwenye kinasa sauti chake kisha akamgeukia kijana aliyekuwa akichakarika na tarakilishi kuangalia maeneo yote yaliyokuwa yamezunguka wenzao.

                       "Hakikisha unakava wenzako vizuri hawa wapizani wenu hawako nyuma yenu tu bali wapo hata pande zingine, usiweke macho kenye upande huo weka macho hata huko nyuma ya Ikulu vijana wakigeuka kwani kwani adui anaweza kutokea  mahali popote pale ndani ya muda wowote. Tunaelwana" Alimpa maelekezo huku akitazama muda ulivyokuwa unayoyoma na ulikuwa umebaki ni dakika tatu yaani saa sita kasoro dakika tatu usiku kuweza kutimia siku ya mapinduzi yaliyokuwa ymeendaliwa na kina L.J Ibrahim na washirika wake

***

    Upande wa wanajeshi wa maji L.J Ibrahim alikuwa yupo ndani ya moja ya Nyambizi akiwa anaangalia kila kitu jinsi kilivyokuwa kikiendelea ndani ya muda huo. Hali iliyokuwepo ndani ya muda huo ilikuwa ni ya kuridhisha sana kwa asilimia kwa mia moja kiupande wake, alikuwa akifanya kila aina ya mwasilianao na vijana wake waliokuwa wapo nchi kavu na hao waliokuwa wapo majini waliokuwa wamebakishwa kama kikosi cha akiba ikiwa makomandoo waliopo ndani ya Ikulu wataweza kuwazidi  vijana wake kutokana na opersheni haikutakiwa kutumia siala nzito ya aina yoyote ile ambayo ingesababisha uharibifu ndani ya ikulu iliyokuwa na mpango pakipambazuka ili Mzee Ole ndiyo awe mtumiaji wa Ikulu hiyo kwa miaka yote iliyobakia na ataendelea kutawala. Akiwa amekaa hapo  akiwa tazama vijana wake waliyokuwa wapo kwenye mitambo ya tarakilishi aliona kila kijana wake akitoa simu ya mkononi ndani ya muda huo, vijana hao waliangalia simu zao hizo kisha wakazirudisha kwenye suruali zao.

                      "Hey nyinyi nani kawaruhusu kuingia na simu kwenye operesheni kama hii, haya kaziwekeni chumba chenu cha kubadili nguo kwenye makabati na mziffungie mrudi hapa" L.J Ibrahim aliwakoromea, aliona kama alikuwa anawawajibisha lakini hakujua kama alikuwa amefanya kosa kubwa sana kuwaruhusu hao vijana waende kwenye cumba chao hicho.

     Vijana hao walitii na kunyanyuka kwenye viti vyao na muda huo wakimuacha akiwa ameshika  simu ya upepo, walipotea katika upeo wa macho yake kwenda huko kuziweka simu alipokuwa amewaamuru.

                       "Eeeeeh! Mugiso hakikisha vijana wanakava pande zote hawa wa huku nimewaondoa mara moja wameingia na simu eneo la kazi" Aliongea kwa kutimia simu ya upepo.

                      "Mkuu" Sauti ya Mugiso ilisikika ikitii amri ya L.J Ibrahima liyokuwa amempa ndani ya muda huo




         SAA SITA KAMILI USIKU

    Sauti ya vyuma vikilia baada ya kubonyezwa kifyatulio cha bastola ndiyo ilisikika ndani ya muda huo ambao Josephine aliifyatua bastola yake ili alipe kisasi cha kuuawa kwa mpenzi wake, ulikuwa  ni mlio ambao uliokuwa ukiashiria kuwa bastola hiyo haikuwa na risasi ndani yake. Josephine alibaki akiwa amepagwa sana kutoka na hali hiyo aliyokuwa ameiona ndani ya muda  ambao alikuwa akitarajia kumundoa Norbert ndani ya dunia hii kulipa kisasi chake.

                      "Nilikwambia Mungu hakunipangia niuliwe na bastola hiyo uliyokuwa umeishika nadhani hukunielewa nafikiri sasa maana ya maneno hayo niliyokwambia umeipata" Norbert alimwambia huku akimtazama akiwa anatabsamu tu.

                       "Wakati naingia ndani ya nyumba hii nilipekua kila sehemu na nikaziona silaha zenu zote na ndiyo hizi ninazo hapa mezani muda huu, nilikuachia moja tu ambayo ndiyo hiyo niliyoitoa risasi nikijua mtajifanya wajanja sana mkijiona ni wenyeji ndani ya nyumba hii. Komandoo na ninja kama mimi huwa sina ugeni na nyumba yoyote iliyopangwa silah kijeshi. Mbinu zote mnazozitumia ni mbinu ambazo si ngeni kwangu first class wa EASA" Norert aliwaambia.

                       "Hata kama Norbert leo ufe wewe au tufe sisi ila hutatoka ndani ya nyumba hii kukosa silaha haimaanishi ndiyo hatuwezi kupambana" Mzee Ole alioongea huku akikunja mikono ya shati lake. Josephine naye aliitupa bastola chini

                      "Ohooo kumbe ngoja sasa niondoe hizi zana" Norbert aliwaambia kisha akachukua silaha zote alizokuwa amezichukua akafungua dirisha na kuzituoa nje, alipomaliza hivyo alitembea  mwendo wa taratibu sana akawa anawafuata maadui zake waliokuwa wamekaa tayari kwa ajili ya kupambana naye.

         Kitendo cha yeye kutia mguu kwenye ardhi ya sebuleni ilikuwa ni kukaribishwa kwa mateke mawili ya kwa pamoja kutoka kwa Josephine aliyoyaachia kwa kasi kubwa sana, aliyapangua yote yakawa yamekosa lengo. Hajakaa sawa Mzee Ole alileta masumbwi imara kabisa tofauti na Norbert alivyotarajia kutoka kwa Mzee huyo ambaye hakuwahi kumuona hata mara moja akipambana, Maumbwi hayo aliyumba kushoto la mkono wa kulia likapita na aliyumba kulia la mkono wa kushoto likapita. Hata kabla hajatahayari alisikia teke la kifua likimpiga kutoka kwa Josephine hadi akaanguka chini papo hapo lakini aliwahi kujibiringisha kiufundi akakaa sawaa tena kuweza kupambana na nao. Norbert alijitazama sehemu ya kifuani akaona alama ya kiatu cha Josephine kwenye shati ambayo aliipangusa kwa mikono yake kisha akalegeza vifungo vya shati lake na akafungua mikono ya shati na akaikunja vizuri.

      Aliwafuata wote kwa pamoja ambapo kwa Josephine alikutana na ngumi ambayo aliipangua kisha akamuachia konde zito la kwenye komwe lililompeleka hadi chini, Mzee Ole alimlenga na teke la kwenye kisogo ambalo lilimkosa baada ya kuinama kisha akauchota mguu wake ambaye alienda kupigiza mgongo wake kwenye sakafu.

      Hakutaka hata kuwapa nafasi alimfuata Josephine ambaye ndiye alikuwa akijiinua hapo chini alipokuwa, alimshambulia kwa ngumi mfululizo kisha akampiga teke la nguvu la bega ambalo lilisababisha ayumbe hadi akajigonga kwenye ukuta akaanguka chini tena. Alipohakikisha Josephine yupo chini alitaka kugeuka kumfuata Mzee Ole lakini aijikuta akisukumwa na teke la mgongo, alipogeuka alikutana na Mzee Ole  akija huku katanguliza miguu mbele kwa mateke ya kumaliza mchezo. Norbert alihama pembeni kwa haraka sana kisha akamuachia Mzee Ole teke la mbavu akiwa bado yupo kulekule juu hadi akaruka kwenye meza ya kulia chakula iliyokuwa ipo upande huo alipomsukumia. Meza hiyo ilivunjika papo hapo kutokana na uzito aliokuwa nao Mzee Ole.

     Hakutaka hata kusubiri kwa nusu dakika alimfuata Josephine ambaye alikuwa akijizoa chini kwa muda huo aweze kusimama, alimpa teke la chini ya kidevu ambalo hupigiwa sehemu chini ya vidole vya miguu hadi damu zake zikaruka. Josephine aliyumba kutokana na pigo hilo na hata kabla hajaugulia maumivu ya pigo hilo Norbert alimpiga mateke mawili ya sehemu zote za mbavu kushoto na kulia kisha akamshindilia na teke la miguu miwili kifuani. Josephine alienda kujipigiza kwenye mlango wa kuingilia ndani sehemu ya mgongoni na kisha akawa anasambaratika sakafuni, hata kabla hajafika chini alikutana na teke jingine la uso kutoka kwa Norbert ambalo lilimfanya arushwe pembeni akaenda kujigonga kwenye ukingo wa kochi ambao huwa na mbao ngumu tu pasipo kuwepo kwa godoro laini.

                      "Sikuwahi kuwaza kuwa nitakuja kupigwa teke na mtoto wa kike kijinga namna hiyo" Norbert aliongea kisha akamnyanyua Josephine akiwa hatamaniki kwa jinsi alivyokuwa akivuja damu usoni mwake, alimpiga ngumi mbili za nguvu sana kwenye taya kisha akamuongeza teke jingine la kifuani ambalo lilimfanya adondokee kwenye kochi.
Hakutaka kumuachia apumzike hata kidogo akiwa kwenye kochi alimvuta nguo yake akaanguka hadi chini na akamuongeza  teke jingine la mbavu hadi Josephine akaachia mguno wa maumivu ambao haukushawishi Norbert amuonee huruma zadi ya kumsonya tu.

    Alimshika ukosi wa fulana yake aliyokuwa ameivaa akamuinua juu lakini hata kabla hata hajampa pigo jingine alisikia ukelele wa Mzee Ole ukitoka nyuma yake, ukelele huo ulimjulisha wazi  kuwa alikuwa amebeba kitu ambacho alikuwa akija kumpiga nacho kutokana na jinsi alivyokuwa akiutoa. Ulikuwa ni ukelele ambao ulishiria alikuwa akiachia pigo la kutumia zana ya mkono, Norbert aliupousikia hakutaka kufanya kitu kingine kingine chochote aliuachia ukosi wa fualna ya Josephine kisha akaruka pembeni kwa haraka sana.

      Kitendo cha kusogea pembeni tu alipishana na upepo mzito wa kuletwa kwa chuma cha kuchomekea pazia ambalo lilimkosa na likatua kwenye mgongo wa Josephine ambaye alitokwa na damu mdomoni kisha akatoa ukelele akaenda sakafuni.

       Mzee Ole alipoona amekosa lengo lake na akampata mtu mwigne hakutaka kabisa kuwa na muda wa kujilaumu yeye alinyanyua chuma kupeleka upande ule kule aliokuwa Norbert yupo lakini hata kabla hajalifikisha alikutana na teke la mbavu la pembeni kutoka kwa Norbert hadi chuma likamtoka mkononi akiwa hajakaa hata sawa alikutana na mvua ya ngumi kutoka kwaa Norbert ambazo zilimrudisha kwa nyuma katika upande ambao kulikuwa na mlango wa kioo. Ngumi hizo zilimfanya aegmee kioo lakini kabla hajafanya jambo jingine lolote, teke zito kutoka kwa Norbert lilimpata pale alipojaribu kusogea mbele kumkabili hadi akarudi nyuma akavunja kioo akaingia ndani ya mlango huo. Alienda kupigiza mgongo wake katika sehemu yenye mtungi wa gesi wa kuzimia moto hadi akaanguka chini na akatulia papo hapo.


****


     Ilipotimia saa sita kamili usiku L.J Ibrahim alitoa amri kwa kikosi cha M.J Belinda kuanza kazi, pia aliamrisha kikosi cha vijana wake kiichoppo chini ya M.J Mugiso kuanza vilevile.

      Amri hiyo ilipofiika kwa M.J Belinda alikipa amri kikosi chake tofauti na amri aliyokuwa ameitoa mkuu wake kicheo, M.J Belinda yeye alikiammrisha kikosi chake waipe mgongo ikulu na kuelekeza silaha zote upande ambao kipo kikosi cha majini kikiwa kimeleekezza silaha zao.

                    "Viongozi wa kombania zote kaeni tayari kwa lolote, iwe kufa au kupona lengo letu ni kumlinda Amiri jeshi mkuu tu, fagio la chumaaa" M.J Belinda aliongea

                     "Fagiaaaaa" Sauti ya wanajeshi wake ilisikika huko nje ambayo ilimfanya atoe tabsamua tu. Baada ya kutoa amri hiyo sauti ya kukoroma kwa simu yake upepo ilisikika ndani ya muda huo ambayo ilimfanya aiweke jirani na mdomo wake.

                     "Wee! Belinda kwanini unaenda kinyume na amri zangu unamtetea msaliti na unapinga amri za mkuu wako" Sauti ya L.J Ibrahim ilisikika.

                      "Siwezi kupinga amri za senior kuliko wote ambaye akiwepo wewe na yeye huwa nalazimika kumpigia saluti  yeye tu na siyo wewe msaliti uliyemuua General kwa tamaa ya pesa. Pia umeua  wengine wengi kisa tu Ole arudi madarakani, mkuu wangu ni Amiri jeshi mkuu tu na si wewe" M.J Belinda aliamua kumwambia ukweli L. Ibrahima ambao ulizidi kumchanganya sana.


     Baada ya kutoka kwa amri hiyo L.J Ibrahim akiwa anajishughulisha kukuna kichwa chake aangalie mbinu nyingine ya kufanya ghafla kikosi chote cha majini kilichokuwa kipo chini ya amri yake nacho kiligeuka nyuma kikawa kimekaa kama walivyokuwa wamekaaa kikosi cha rdhini kuilinda Ikulu.

               "Fagio la chumaaa!" Ilisikika sauti ya M,J Mugiso ikiongea kwenye kipaza sauti kilichopo ndani ya hema na sauti ikasambaa nje

                 "Fagiaaaaa!" Sauti ya wanajeshi la maji pamoja na nchi kavu wote kwa pamoja zilisikika zikiitikia, muda huo huo ndege za kivita za jeshi la anga zilianza kurandaranda kuizunguka ikulu hiyo kuongeza ulinzi kwa Rais Zuber



KIFO CHA NYANI MITI HUTELEZA

      L.J Ibrahim hakuamini macho yake kwa kile alichokuwa akikiona ndani ya  muda huo akiwa yupo nyuma ya vijana wa kikosi cha maji waliokuwa wapo ndani ya Nyambizi, ajabu ilipotolewa tamko la pili la fagio la chuma na M.J Mugiso hadi vijana hao waliokuwa wapo nyuma ya tarakilishi walinyoosha ngumi zao na kusema neno 'fagia'.

                 "Hey! Nyinyi ndiyo nilichowaamrisha hiko!" Aliwakaripia wote kwa pamoja na kupelekea vijana wote waliokuwa wamempa mgongo wageuze viti vyao vya kuzunguka na kumtazama L.J Ibrahima ambaye alikuwa mpole mwenyewe kwa kile alichokionea. Vijana wote walikuwa wameshika bastola na walimuelekezea kwa pamoja akawa hana ujanja wowote, alibaki akiwa haamini kile kile kilichokuwa kimetokea.

                  "Mnafanya nini nyinyi?" Aliwauliza akiwa na taharuki kuu moyoni mwake

                  "Tunatimiza wajibu wetu wa kulilinda taifa hili dhidi ya wavamizi na wasaliti kama wewe, umeshiriki kumuua General hata Mufti alitangaza ila mkamuua tena halafu unataka kumpindua Rais aliyeboresha jeshi na maslahi yote ya wanajeshi" Mmoja wa wale maaskari wataalamu wa tarakilishi alimuambia.

                   "Tena simu zetu zilipoingia ujumbe mfupi kutoka kwa Madam Belinda ulikuwa ni video na picha ya kile unachokifanya kwa maslahi binafsi angalia mwenyewe" Askari  mwingine alimrushia simu ya mkononi ambayo aliifungua akakuta kila kitu ambacho kilimfanya azidi kunyongea akiona hana ujanja mwingine tena.

                    "Maluteni mimi si mkuu lakini shusheni silaha zenu chini" Alijipa ujasiri na kuongea kuangalia kama wangeweza kutii mari hiyo.

                     "Hatukutambui kama mkuu wetu zaidi ya kuwatambua Amiri jeshi mkuu, Meja jenerali Belinda na Meja jenrali Mugiso  basi wewe si mmoja wetu na hapa tupo kwa ajili ya kukumata ufike kule unapostahiki kufika msaliti kama wewe. Afande mkamate huyo" Luteni yule wa kwanza kuongea alimpa amri mwenzake ambaye alinyanyuka na kwenda kumtia nguvuni L.J Ibrahim.

                       "Hey! Mnafanya nini mimi ni three star general mkubwa wenu" Alilalalmika wakati akitiwa nguvuni na luteni huyo.


USITOKE TAFADHALI NGOMA INAMALIZIKA LEO HII


*USIKOSE KINDUMBWENDUMBWE HIKI JIONI YA LEO PANAPO MAJALIWA TUMALIZE WAKALA WA GIZA







No comments:

Post a Comment