Saturday, February 25, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA


WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com



SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

"Yes! Leo hii tunamfuata hatusubiri  zaidi tukitoka hapa tu jioni hii" Josephine aiongea

"Mfuateni pia msiende kichwakichwa tena inabidi muwe wawili maana yule mtu naye ana akili kama mchawi"  Mheshimiwa aliwambia

"worry out Jack Shaw nipo kazini sasa hivi na tunaenda sasa hivi" Askofu alimtoa hofu

"Yaani tukiipata tu ile paltop yake tutamuachie huyo N001 hayo malaptop yote manne halafu ile tunaiharibu hakuna namna sitaki kwenda Segerea" Mheshimiwa aliongea.



___________________TIRIRIKA NAYO


              USIKU
 Majira  hayo Jama Wa Majama alikuwa ameketi kwenye kiti ndani ya moja ya chumba ndani ya nyumba yake, akili iikuwa ipo katika kutafakari kitukile ambacho kilikuwa kimemfanya hadi akatoa mguu kutoka kijijini hadi akafika mjini hapo. Akili ilikuwa ipo makini tu katika kupanga mkakakti wake maalum wa kuweza kufanya kile akilichokuwa kimemleta hapo, huruma aliyokuwa nayo kwa mtu asiye na hatia kupewa kesi ndiyo ilimfanya hadi awe hapo. Alikuwa amekuja kwa siri sana na alijua kuwa uwepo wake ndani ya eneo hilo utaendelea kuwa siri, hakujua kabisa kuwa alikuwa ameshauza siri yake ya kuwepo ndani ya eneo hilo kwa watu  waliokuwa wakimsaka kwa udi na uvumba.

      Alichojua kuchikicha  ubongo wake ambao ulikuwa umegeuka chekecheo la mawazo, ilikuwa ni jinsi ya kuweza kumfanya Mheshimiwa Kabinuki atoke nje ya nondo na heshima yake irudi kama ilivyokuwa hapo awali. Uzalendo aliokuwa nao Mheshimiwa yule, aliona haikufaa kabisa kuweza kuwekwa nyuma ya nondo kwani ilikuwa ni sawa na kumkosea heshiam sana na kumtusi. Muonekano wake wa kuvaa nguo ambazo zilikuwa zikiunadi umasikini asiokuwa nao, alikuwa ameshauodoa na muda huo alikuwa amevaa suruali nyeusi ya kitambaa pamoja na shati jeusi ambalo lilikuwa limempendeza sana. Bado hakuwa ameutoa ule muonekano wake wa kizee aliendelea kuwa nao kama kawaida, hakutaka kuutoa katika muda huo aliokuwa akitafutwa kwa udi na uvumba. Hata msiba wa mke we kipenzi hakuwa amehudhuria kutokana na kuwa na kitu kile ambacho kilikuwa na manufaa kwa taifa lake, aliona ni bora aonekne ni nuksi kwa familia na ndugu wa mke wake kuliko kupoteza kitu muhimu sana kwa taifa zima.

  Muda akiwa anachekecha mawazo kwenye ubongo wake alianza kusikia sauti ya mbwa waliokuwa wakifanya ulinzi nje ya nyumba hiyo wakibweka kwa nguvu sana, kubweka huko kuliashiria kuwa kulikuwa na ugeni ambao haukuwa wa kawaida kabisa. Aliposikia sauti hizo  alinyanyuka kwenye kiti alichokuwa amekiwekea kalisho lake, alisogea hadi dirishani na kisha akachungulia nje. Aliwaona mbwa wake wakiwa wanabweka kwenye eneo ambalo taa za nyumba hiyo zilikuwa zimefika kikomo, ilikuwa ni ndani ya eneo lenye giza ndiyo Mbwa hao walikuwa wakibweka kwa nguvu sana jambo ambalo lilimfanya asiwe hata na hamu ya kuendelea kukaa ndani ya chumba hiko. Alichoamua kukifanya ilikuwa ni kuinua silaha yake na kisha kuipachika kunoni na  akatoka nje ya nyumba hiyo, akiwa ni mwenye hadhari kwa akili na hata mwili. Alitembea hadi kunako mlango wa kutokea nje, alipokuwa yupo njiani katika kutembea huko ghafla mbwa wote walinyamaza kimya ghafla na hwakuendelea kubweka. Hilo lilimfanya asikubali kabisa kuwa hao mbwa alikuwa wakibweka tu kwakuwa nje ya eneo hilo amepita mpita njia nje ya uzio, alitoka nje kwa mlango mwingine kabisa na akasogea hadi eneo ambalo walikuwa wapo mbwa wake akiwa ni mwenye kuhadhari mazingira hayo yaliyokuwa yapo karibu.

 Aliwakuta mbwa wake wakiwa wamelala chini kama vile walikuwa na usingizi, alipoona hali hiyo alijua kabisa kuwa kwenye himaya yake hiyo kulikuwa na ugeni ambao haukuwa rasmi wala taarifa. Hilo lilimfanya aaangalie eneo lote kwa tahadhari na kisha asogee jirani kabisa na eneo hilo, alipowagusa mbwa wake hao kuwatazama hali zao aliona hawakuwa wameondokwa na uhai zaidi ya kuingiwa na usingizi usio na ratiba. Jama Ma Majama vinyweleo vyote vya mwilini mwake vilimsisimka alipogundua hilo, alikuwa ni kama alikuwa amekumbwa na msisimkoo wa ghafla kutokana na kufanyiwa kile ambacho husisimua mwili. Hali kama hiyo alikuwa akijua kabisa kuwa utokeaji wake ulikuwa ukiambatanishwa na kuwepo kwa hali isiyo ya kawaida, akiwa kwenye msisimko huo hata haikupita dakika alihisi kitu kikitua kwenye kiuno chake kwa  nyuma na kumfanya aende chini. Akiwa anaanguka kwenda huko chini alijiwahi kwa kupiga sarakasi maridadi sana, alibiringika mtindo wa 'roll' ili asije akaumia. Alipokaa sawa aligeuka nyuma kwa namna ya kipekee kwani alikuwa ameshatambuwa kuwa ndani ya nyumba hiyo alikuwa amevamiwa, alikutana na mwanadada aliyekuwa amevaa nguo ya mazoezi akija  kwa teke la kasi sana. Jama  hapo alidunda kamz mcheza masumbwi na kisha akasoge kando kwa kasi ya ajabu, yule Mwanadada alipitiliza na teke lake na kisha aliongezewa na teke jingine ambalo lilimyumbisha nusura limuangushe.

   Mwanadada huyo alipokaa sawaa kugeuka nyuma kupambana ma Mamba aliyekuwa kitetea himaya yake, alimkuta akiwa tayari ameshajiweka sawa. Alichokifanya baada ya hapo ni kukunja mikono ya shati lake alilokuwa ameliva kwani alishatambua kabisa huyo Mwanadada hakuwa kiumbe cha kawaida , teke ambalo ilitua kiunoni uzito wake tayari ulikuwa umeshatangaza kuwa alikuwa amevamiwa na kiumbe ambaye alikuwa na uwezo naye sawa. Baada ya kukunja shati hilo alianza kunesa huku akimsogelea huyo Mwanadada, naye hakuwa nyuma alipoona anasogelewa na mtu ambaye alikuwa na muonekano wa kizee aliona ulikuwa si muda wa yeye kumtuliza kwani aliamini kabisa hakuwa huyo waliyekuwa wakimtafuta. Aliingia kwa ngumi ya kikarate akilenga sehemu mbalimbali za mwili wa Jama, ngumi hizo zilitoka nje ya lengo kabisa kwani alikutana na mpanguaji mzuri sana wa mapigo kama hayo ambayo yote yaliishia nje. Aliletewa mapigo naye aliyapangua kwa ustadi hapo na hapo ndipo na yeye akatambua kuwa alikuwa akipambana na kiumbe kama yeye, aliongeza mashambaulizi hayo kwa kiumbe huyo lakini hayakufikia lengo. Alipobadili mtindo wa upiganaji alikutana na kiumbe huyo alikuwa akiujua mtindo huo, alipigana kwa muda na hatimaye Mwanadada huyo alianza kuishiwa pumzi na hapo ndiyo ikawa nafasi nzuri kwa Jama.


  Hakuwataka kuipoteza nafasi hiyo kabisa yeye alianza kushambulisha kwa nguvu zake zote huku akiwa karibu  ya mwanadada  huyo, kuishiwa na pumzi pamoja na kuwa karibu na adui yake ambaye alikuwa amemzidi ghafla mwendo wa upiganaji. Lilikuwa ni suala ambalo lilimchnganya sana Mwanadada huyo aliyekuwa akimudu mwanzo kusimama na  mpinzani wake katika pambano hilo, alijaribu kuzuia lakini alijikuta akipatwa na baadhi ya mapigo ambayo yalizidi kumpunguza nguvu kabisa. Alipozidi kupungua zaidi Jama Wa Majama alifanya kitu cha haraka ambacho kilikuwa ni kama kumlevya huyo Mwanadada asizidi kuleta upingamizi, aliachia ngumi mfululizo ambazo chache zilikosa lengo kutokana na kubahatishwa kukwepa. Hakusubiri zaidi alijirusha juu akijiandaa kutoa teke la kuzunguka maarufu kama 'round kick', akiwa yupo juu kabla hajatoa teka hilo alijikuta akisukumwa na kitu kigumu sana kwenye bega na alienda kusalimiana na ardhi ya eneo hilo. Lilikuwa ni teke ambalo  lilitoka kwa haraka kwa Kiumbe mwingine aliyekuwa amevamia eneo hilo kuja kupambana nao, teke hilo lilikuwa ni zito kuliko lile la kwanza. Alipoanguka chini alibiringita hakutaka kukaa sehemu moja hiyo aliyoangukia kwa hofu ya kuongezewa pigo jingine la kushushwa, alipobiringita na kukaa katika ambalo ulimuwezesha kujiinua. Aliweza kumuona Mwanaume wa kizungu ambaye uso wake ulikuwa hauonekani vizuri, hakutaka kujiuliza mara mbili kuwa huyo mtu alikuwa ni kiumbe wa hatari kiasi gani. Alijifyatua kutoka hapo chini na akasimama wima na kisha alibadili mtindo wa upiganaji Wa kumfuata Mzungu huyo, kitendo cha uvamizi wa mzungu huyo alijua kabisa kuwa alikuwa akitazama mtindo wa upiganaji aliokuwa akiutumia. Hivyo kutumia mtindo ule ilikuwa ni hatari nyingine kabisa kwake, kwani angepigwa vibaya.


   Alikuja na mtindo wa kombati  katika kupigana na huyo Mzungu lakini hakufua dafu kwani mapigo yote yalizuiwa na Mzungu huyo alionekana alikuwa ni kiumbe mwenye kazi zaidi kuliko kawaida. Alianza kupewa mapigo ya ajabu kutoka kwa yule Mzungu ambaye yalimrudisha chini tena katika upande ule aliokuwa ameangukia, hapo alijua alikuwa akipambana na Jinamizi na si kiumbe kama yule aliyekuwa akipambana naye mwanzo. Jinamizi hili hakuwa na uwezo wa kupambana nalo kwani lilikuwa limemzidi ujuzi, pamoja na kukiri hayo bado alisimama tena wima kupambana.

"Komando" Aljisemea moyoni  hukua akiwa amekunja ngumi kumuagalia Mzungu yule ambaye alikuwa amekaa kwenye mkao wa kimadharau kabisa. Alimfuata kwa mtindo wa aina nyingine wa kupigana kwani alitambua kabisa alikuwa akipigana na mtu ambaye alikuwa  na uwezo sawa na idadi ya wanajeshi mia moja wa kawaida, yeye hakuwa amefikia ngazi hiyo.

 Alipigwa sana kutokana na Mzungu huyo kubadili mapigo na kutumia yaliyokuwa yakimchosha zaidi, alipigwa hadi kaanguka chini na kushindwa kuinuka. Muda huo Yule Mzungu alimsogelea karibu yake akiwa amenyoosha mkono wake akitaka kumaliza pigo la mwisho, kabla hajapiga pigo hilo alisikia upepo ukivuma kwa nguvu sana kuelekea kichwani mwake. Mzungu huyu alitambua kabisa huo upepo haukuwa upepo wa kawaida kabisa bali lilikuwa ni pigo la nguvu sana, alipiga saraksi moja matata kulikwepa pigo hilo na kisha akaosogea ambali na eneo hilo.

"Norbert" Mzungu huyo aliita huku akimtazama huyo aliyemletea pigo hilo.


"Askofu Valdermar hatimaye tunaonana tena, sasa hivi ni kimakabiliano zaidi" Norbert aliongea huku akimsogelea Askofu kwenye eneo ambalo alikuwa amesogea baada ya kukwepa pigo lake.


  Majinamizi mawili yaliyokuwa yakikaribiana kiuwezo kwa mara ya kwanza yalikuwa yamekutana ndani ya mpambano, wale waliokuwa wamjeruhiwa walikuwa wamekaa kando huku wakiangalia mpambano huo uliokuwa ukiwahusu wale waliokuwa na maajabu kuliko wao. Mpambano ulianza kwa kila mtu kuonesha ujuzi wake katika kupigana, wote walipigana kwa uwezo wao  na ikafika muda hakuna aliyekuwa amefanikiwa kutia pigo kwa mwenzake. Hiyo ilisababisha wote kwa pamoja watie mbinu za kininja kwenye mpambano huo, hapo ndipo aliyekuwa na ujuzi kushinda mwenzake aliweza kujulikana walipotia mbinu hizo. Haikufika hata muda wa dakika tano tayari Askofu alikuwa amesharuhusu mapigo matano tofauti kuingia kwenye mwili wake kutokana na kuzidiwa uwezo, mtindo wa sarakasi pamoja kukwepa vitu kwa ufundi wa hali ya juu ndiyo vilifuata kwa muda huo waliokuwa wakipambana.  Norbert alidhihirisha wepesi wake na Askofu vilevile alidhihirisha ingawa alikuwa akipatwa na baadhi ya mapigo, ujuzi wa kininja wa hali ya hai ya juu alionao Mzee wa kazi ulisababisha aweze kumtawala Askofu ndani ya pambano hilo. Muda mfupi baadaye aliachia pigo ambalo lilimpata Askofu kwenye mbavu hadi akaenda chini, pigo hilo halikuleta athari kubwaa nyingine kwenye mbavu zake zaidi ya kuzijeruhi. Askofu hapo aliona alikuwa amezidiwa hatua kubwa sana na laiti kama angeendelea kupambana angekuwa ameshajiweka kwenye hali mbaya sana kutokana na kujeruhiwa huko, ingawa alikuwa amejua hilo alijaribu kupambana kwa mara ya mwisho na alipoona alikuwa amezidiwa aliamua  kuuruka uzio wa nyumba hiyo na hakujali kabisa Josephine aliyekuwa amenguka chini akiwa hajiwezi. Aliona alikuwa na mzigo tayari kwa kujaeruhiwa na laiti kama angemchukua Josephinea angekuwa amejiongezea mzigo, alimuacha hapo kwenye mikono isiyo salama kabisa ndani ya nyumba ya adui waliyewakuwa wamemvamia.


 Hilo lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa Josephine na muda huo ndipo alipijuta kuingia kwenye kundi hilo, alimlaani sana Askofu kwa kukimbia na kumuacha eneo hilo wakati walikuwa wapo apmoja. Umoja waliokuwa nao katia mambo mbalimbali hasa wakiwa mtuna Bosi wake aliuona ulikuwa wa kinafiki ikiwa ameshindwa kumsaidia akiwa yupo kwenye eneo hilo, akiwa amelala chini alimshuhudia Norbert akimuinua Jama wa Majama na kisha akajongea naye kwa taratibu hadi eneo ambalo alikuwepo muda huo alikuwa amekaa kitako.

"Nafikiri ushaiona faida ya kuwa Mhalifu ukiwa kwenye shida  hukumbukwi" Alimuambia na kisha alimuongeza teka la mdomo hadi akatema damu mdomoni kutokana na uzito wa teka hilo.

"Hii ni trela tu,ulinikimbia na kisha unakuja kuua Watanzani leo utaniambia mwenyewe anayewatuma" Norbert alimuambia na kisha alimuachia Jama mara moja ambaye alijiegemeza kwenye ukuta, alimpiga teka la tumbo Josephine na wala hakujali kabisa jinsi alivyokuwa akitoa miguno ya maumivu.

"Ni bora ningemsikiliza Eva nikakuua na bomu pamoja na Thomas kumbe kukudharau ndiyo ukaota mapembe na kurudi tena" Aliongea huku akisitisha kumpiga na kisha akamnyanyua na kuingia ndani ya nyumba ya mwenyeji wake, mwenyeji wake alifuatia kwa nyuma akiwa anajikongoja akiushikilia ukuta wa nyumba hiyo.


****


   Taarifa iliyokuwa imepamba vyombo vya habari kwa muda huo ilikuwa ni kuzidiwa ghafla kwa waziri wa fedha Mheshimiwa Janstu Mahujuraja, ilikuwani shinikizo la damu ambalo lilikuwa limemkamata Mheshimiwa huyu aliyekuwa akiheshimiwa sana  ndani ya nchi kutokana na sifa zake alizokuwa amejijengea akiwa yupo chini ya Rais Zuber. Kuzidiwa kwake na hadi kukimbizwa kwenye hospitali ya Regency maeneo ya Upanga, ilikuwa ni jambo la kusikitisha sana kwa watanzania. Ilikuwa ni shinikizo la damu la kupanda ndiyo lilikuwa limemkumba kwa ghafla sana akiwa yu ndani ya nyumba yake, kuanguka huko kwa shinikizo hilo kulipelekea hata simu yake ya kisasa aliyokuwa akiitumia nayo isalimiane na sakafu ya nyumbani kwake. Alikuwa amepokea taarifa ambayo ilimfanya aanguke huko hadi apoteze fahamu kutokana na shinikizo la damu, pamoja na kuanguka huko hadi akafikia hatuz ya kupoteza fahamu bado jambo hilo lililosababisha hadi akaanguka halikujulikana kabisa na familia yake haikuwa imefungua mdomo kuzungumza kwa kile kilichokuwa kimemfanya aanguke.

  Uzushi wa vyombo vya habari ndiyo suala ambalo walikuwa wakilihofia sana famiia hiyo, hakutaka kabisa kusema kuwa chanzo ilikuwa ni simu. Waandishi wa habari wapekuzi walikuwa wamefika kwenye neo hilo la hospitali ambako kulikuwa kumewekwa ungalizi mkubwa kwenye chumba alichokuwa amelazwa. Walianza kufanya mahojiano na wanafamilia hao lakini hawakuambulia kitu chochote, walipozidisha maswali yenyee kuudhi na kukera walijikuta wakafukuzwa kama Mbwa aliyekuwa ameingia nyumba ambayo haikuwa ya kwao. Bado waandishi hawa hawakukoma kabisa waliendela kubaki nje ya hospitali hiyo kwani walijikua kabisa kulikuwa na ulaji ndani ya eneo hilo, tabia ya mamba akikosa windo kubaki kwenye eneo ambalo kulikuwa na nafasi ya kupata windo ndiyo walikuwa nayo. Hata imani za kuwa windo hilo litaurdi tena ilikuwa imejengeka kwenye vichwa vyao, hawakuwa tayari kunyanyuka eneo hilo hasa waandishi wa habari wa magazeti.

   Waliendelea kukaa kwenye eneo ilo hata walipoanza kuingia mawaziri wengine waliokuja kumuona mwenzao, wao walijaribu hata kuwahoji hao kutokana na kuisaka habari kwa nmna yeyote ile huku wakiwapiga picha mbalimbali walipokuwa wakiingia eneo hilo. Waandishi wa hxbari hao walibaki midomo wazi baada ndani ya eneo hilo kuingia waziri mbaye alikuwa ni chui na paka na Mheshimiwa Mahujuraja, huyu hakuwa mwingine ila ni Mheshimiwa Barnaba Liwale aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani. Yeye alikutana na  maswali ya waandishi wa habari kuhusu ugomvi wao waliokuwa nao ingawa walikuwa ni wanachama wa chama kimoja, maswali hayo yalikuwa ni yenye kuudhi lakini Meshimiwa Liwale aliweka uvumilivu.


*JOSEPHINE MIKONONI MWA NORBERT
*ASKOFU AINGIE MITINI BAADA YA MAJI KUZIDI UNGA


ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment