Wednesday, February 15, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA KUMI NA TATU



WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com




SEHEMU YA KUMI NA TATU!!
Sehemu hiyo ilifunguka kama mfuniko ambapo ndani yake kulionekana kukiwa na mkoba unaofanana na mikoba ile miwili ambayo muda huo ilikuwa ipo mikononi mwa Norbert, alipouona mkoba huo alitoa tabasamu lake la kizee na kisha akafunika tena ambako hakukuonekana kama kulikuwa na mfuniko. Baada ya kuufunika mfuniko huo alijilaza kwenye kitanda cha kamba kilichokuwa humo ndani, alilala chali akawa anaangalia paa la nyumba hiyo.

"Ipo siku tu" Aliisemea mwenyewe huku macho yakiwa yapo juu




_________________TIRIRIKA NAYO

   Kukamatwa kwa kijana mwingine aliyekuwa chini ya Askofu Valdermar ilikuwa ni pigo jinginye kubwa sana kwao, muda huo watu waliokuwa wakiwafanyia kazi walikuwa wamewaita katika  nyumba ambayo walikuwa wameifanya ndiyo makao yao wa kukutana. Wakubwa wao wawili waikuwa wamechukia sana hasa walipofikiria kuwa walikuwa wakienda kuhadhirika ndani ya siku zijazo ikiwa hawatoithibiti hali hiyo, hilo lilikuwa ni suala ambalo walikuwa hawataki kabisa kuona likitokea. Wote walikuwa tumbo joto kwani walikuwa wakitambua kabisa kuwa huyo alikuwa ni kijana wao, mipango yao sasa ilikuwa imeanza kwenda mrama kwani ilikuwa ni Tarakilishi ya pili hiyo wameikosa kati ya tarakilishi zote tano walizokuwa wakizitafuta. Sasa ilikuwa imebaki moja tu ambayo ilikuwa na nenosiri jingine ambalo lingeweza kupata neno kamili kabla hawajaamua kuitafuta ile ambayo ilikuwa na siri kuliko zote. Tarakilishi ya mwisho kabisa kupatikana na ambayo ingeweza kuwaweka pabaya ilikuwa ni Tarakilishi aliyokuwa nayo Jama, Tarakilishi hiyo ilikuwa ina kila kitu,tayari siri nyingine kutoka kwa wanausalama wasio waminifu ilikuwa imeshafika mbele yao kuhusu tarakilishi zile. Wote walikuwa wameshajua kuwa nenosiri hayo  yaliyopo kwenye tarakilishi nne tofauti yalikuwa yakiunganishwa ndiyo nenosiri kamili ya kuweza kufungua tarakilishi ya Jama ambayo ndiyo ilikuwa na kila kitu kuhusu wao kilikuwepo humo ndani. Watu hawa walikuwa wamezipata taarifa ambazo walivujishiwa kabla hata ripoti yenyewe ikiwa haijakamilika kutoka kwa wanausalama ambao hawakuwa waminifu kabisa, kupitia taarifa hizo ndiyo walibuni mpango mzima wa kuweza kuwafanya wasiwe ndani ya kuti kavu. Hapo waliweza kuleta mpango wenyewe wa kuwamaliza wale wote waliokuwa wamefanya utafiti huo ili kuweza kuchukua siri hizo, hakika mpango huo ulisukwa na ukasukika na ulipangwa ukapangika.


  Mpango huo ulianza ndani ya siku ambayo Mheshimiwwa Bia alifariki kwa bomu la barua, na kisha wakafuata  maofisa wa kitendo cha CID katika jeshi la polisi katika kumalizwa na mpango huo. Walikuwa wameupa jina la wito wa kuzimu. jina la mpango huo lilikuwa na linawakilishwa na barua bomu walizokuwa wakizituma kwa watu ambao walikuwa wameshikilia  siri hizo. Muonekano wa barua hizo ambazo zilikuwa zimekaa kama barua za watu waliokuwa wakiabudu shetani ndiyo waliutumia kuwafanya wahusika wawe na wahka wa ufungua barua. Muonekano huo ulikuwa umeundwa na mhuri ambao waliutumia kupiga juu  ya barua pamoja maneno yaliyokuwa yakiashiria nguvu za giza, stempu ya barua hizo waliunda wenyewe na hawakutaka zijulikane kama walikuwa na stempu ambazo zilikuwa hazihusiki kabisa ndani ya shirika la posta ndiyo maana walivika bahasha nyingine kwa juu. Zilikuwa  ni stempu walizompiga picha mwanamke akiwa hana nguo ya juu akiwa ameonesha mgongo pekee uku chini akiwa na nguo ambayo iliuwa imeegeshwa tu.

   Sasa mpango huo unaanza kuingia doa kwa mara ya pili tena ikiwa bado kazi yenyewe ni mbichi kabisa haijaweza kukamilika hadi waseme kuwa amani ipo, wakuu walikuwa wapo kwenye meza moja ya kulia chakula muda huo na timu nzima waliyokuwa wameiteua kuweza kukamilisha kazi hiyo. Timu nzima ilikuwa ikitambua kuwa wakuu hao walikuwa wamechanganyikiwa sana kutokana na taarifa hiyo iliyokuwa ipo mezani kwa muda huo. Wakuu hao waliokuwa wamepewa jina Roho mmojawapo kutokana na kazi yake ya kufanya hila za kukinga mambo yao yasiharibike na mwingine alikuwa amepewa jina la Moyo kutokana na kuwa ndiyo mtu pekee aliyekuwa akirahisha kabisa mipango yao kama itaingia ugumu wowote. Wote wawili walikuwa  ni watumihi wa umma wa ngazi za juu kabisa ndani ya serikali ambao walikuwa wakipewa  jina la Waheshimiwa lakini waliyokuwa wakiyafanya hayakufaa kabisa wao kupewa jina hilo.

"Jamani bwawa letu linaingia ruba mapema yote hii, nguvu zote tulizotumia na hata maelfu ya watu tuliowapoteza kwa wito wa kuzimu kweli iwe kazi bure" Mheshimiwa Roho aliongea

"Hata mimi nashangaa yaani imekuwaje hamjui kama tunafanya mipango kutufanya tule ugali wote hapa na pia kujitajirisha, sasa iweje kiumbe mmoja aharibu mipango yetu" Mheshimiwa Moyo naye aliingilia kwa ghadhabu

"Jamni tatizo ni kwamba kazi hii imeingiliwa katika muda mbao tulikuwa hatujapewa taarifa kuwa kuna mwanausalama yeyote yuo kazini, hivi ingekuwa tuna taarifa kama ambavyo Bwana Roho ulifanya pale CID walipoingia kazini huyu mtu angepeumua kweli " Askofu Valdermar aliongea

"Jamani si niliwambia mimi kuwa hii kazi waliopo ndani yake ni Milliatary intelligence pamoja na TISS" Mheshimiwa Roho aliwaka


"Kwa mujibu wa taarifa zilizopo mezani kwangu kutoka kwa kibaraka wetu aliyepo jeshini amesema kuwa watu hao wameacha hiyo kazi baada ya mtu mahsusi kuingia kazini sasa siyo hao, hata TISS hivyohivvyo wamepewa agizo la kujitoa na kazi ipo kwa nani sasa?" Askoafu Valdermar aliuliza

"I think ni EASA hawa" Mheshimiwa Moyo alikisia jambo ambalo lilimfanya Josephine ashtuke kabisa.

"Waheshimiwa kama ni hawa EASA wapo kazini basi aliyekuwa yupo nyuma ya haya masuala ni Norert Kaila si mwingine tu" Josephine aliongea

"Are sure Josephine?" Mheshimiwa Moyo aliuliza

"Yes, kwasababu ni yeye ndiye tulimuona jirani na maneno ya garage yetu kule alifuata nini na tulipojaribu kumuua pale Tazara alikwepa kwa kuruka kwenye pikipiki means katujua huyu hakuna jingine tu"

"Hivi huyu mtu ndiyo kweli atusumbue kichwa jamini?" Mheshimiwa Moyo aliuliza

"Mheshimiwa yule siyo kiumbe wa kawaida kabisa, hebu fikiria timu yetu ya awali chini ya  General Ibrahim aliiangamiza yeye mwenyewe" Josephine alifafanua

"Ok kama ni hivyo  nyinyi kuleni naye sahani moja tu, sisi tunatafuta jinsi ya kuweza kuwageuza watu fikra maana umaarufu wetu umepungua kwa jinsi Kabinuki anavyolivalia njuga suala la ripoti hili kila siku Bungeni" Mheshimiwa aRoho aliongea

"Roho huyu ni dawa ndogo tu yaani tumfanyie ili ajue kama mdomo ndiyo ulimponza Ibilisi akalaanika pia, tumuuzie tufani tu nafikiri itakuwa ni zawadi yake kwa kidomo chake" Mheshimiwa Moyo aliongea


"Yaani hii ndiyo njia sasa ili kuwapunguza akili waweke akili kwake tu, nafikiri ni kumuwekea vitendea kazi vyetu pamoja na vidhibiti matata ndani ya eneo lake tu" Askofu Vldermar aliongea

"Hii ni nzuri kabisa, huyu jamaa kila mwisho wa wiki kama yupo ndani ya jiji hili basi safari yake ni huko Kimanzichana naamini huko ndipo kutaweza kuwafanya waamini kuwa anaropokea unafiki tu bungeni" Mheshimiwa Moyo aliongea suala ambalo lilipitishwa kwa watu wote hapo na mipango ilianza mara moja katika kulitekeleza suala hilo kabla jua halijatua jioni ya siku hiyo, mpango ulipokamilika sasa kilichobakia ilikuwa ni utekelezaji wake tu hakukuwa na jingine ndani ya muda huo.


****

 JIONI YA SIKU HIYO
  OYSTERBAY
  DAR ES SALAAM


   Gari ya jeshi la polisi ilionekana ikiingia kwenye nyumba moja ya kifahari sana ambayo ilikuwa na ulinzi mkali sana, muda huo ulikuwa ni muda mbao mwenye nyumba hiyo alikuwa yupo humo ndani. Gari hiyo ilipofika kwenye eneo la maegesho ya Nyumba hiyo watu waliokuwa wamevaa nguo za kiraia walitoka hadi kenye mlango mkubwa wa nyumba hiyo, ujio wao ndani ya nyumba hiyo ulikuwa umeshatambulika dhahiri tangu wapo nje na walipofika tu mlangni milango ilifunguliwa na wakaingia ndani hadi sebuleni ambako walimkuta mzee wa Makamo akiwa amekaa na mke wake.

"Karibuni vijana" Mzee Huyo aliwakaribisha akuiwa ameweka tabsamu usni mwake"

"Asante Mheshimiwa. sisi si wakaaji sana tumekuja kutekeleza agizo la Mheshimiwa" Aliongea mmojwapo.

"Ndiyo nawasikiliza"


"Hichi ni kibali cha kuja kukukamata kimetoka kwa Mheshimiwa mwenyewe, hivi sasa ninavyoongea upo chini ya ulinzi" Yule aliyeitikia ukaribisho aliongea huku akimpatia Mzee huyo karatasi ambayo ilikuwa ni kibali cha kumkamata ikiwa na saini ya Rais Zuber


"Jamani nimefanya nini kwani?"


"Hilo utalijua mbele ya safari kuanzia sasa ongozana na sisi"


  Mke wa Mzee huyo alianza kulia hali kadhalika watoto nao walianza kulia bada ya kusikia mama yao akilia wakaja kushuhdia hicho alichookuwa amekiona mama yao, Mzee huyo ambaye alikuwa ni mtu mzito serikalini alikamatwa na wanausalma hao na kisha akapandishwa kwenye gari ambalo walikuwa wamekuja nao. Aliondolewa eneo hilo akiacha familia yake ikiwa inalia kwa uchungu sana, yeye mwenyewe akiwa yupo ndani ya gari ya jeshi la polisi alionekana ni mwenye huzuni sana kwani hakujua kile ambacho alikuwa amekifanya hadi muda huo aliokuwa amewekwa chini ya Ulinzi.


  SAA MBILI USIKU

  Taarifa ambayo ilikuwa ni kubwa kwenye vyombo vya habari majira hayo ya saa mbii usiku ilikuwa ni kukamatwa kwa Waziri wa nishati na madini Mheshimiwa Kabinuki katika jioni hiyo nyumbani, tuhuma zake kuu ilikuwa ni kuhusika na milipuko yote iliyokuwa imeua maelfu ya watu ndani ya jiji la Dar es salaam. Ilikuwa ni taarifa ambayo iliwashtua wengi kutokana na jinsi Waziri huyo alivyotokea kuwa maarufu ndani ya kipindi kifupi sana cha muda kutokana na kushikiniza sana ripoti iliyokuwa ipo chini ya Mheshimiwa Bai isomwe haraka sana kabla haijaingia dosari. Sasa mabalaa yote hayo yaliyokuwa yamelikumba jiji wanakuja kusikia kuwa yalikuwa yakisababishwa na yeye,, wengi walioishuhudia habari ile walilaani sana juu ya mauaji ambayo alikuwa ameyasababisha.



****


  SAFE HOUSE
 DAR ES SALAAM

   Baada ya kukamatwa ndani ya nyumba yake kituo cha kwazna kuletwa ilikuwa ni ndani ya jengo ambalo lilikuwa likifahamika kama safehouse, ilikuwa ni amri kutoka kwa Rais Zuber ambaye ndiye aliyemarisha kuwa aletwe ndani ya jengo hilo  alikuwa akitaka kumuona huyo msaliti ndani ya serikali yake. Kabinuki aliingizwa ndani kabisa akiwa tayari ameshafungwa pingu na kwenda kuwekwa kwenye sebule ya nyumba hiyo, hapo alikutana na Rais Zuber akiwa amefura kwa hasira kwa jinsi alivyiona sura yake. Kabinuki alikuwa ni mwenye upole mwingi kutokana na kutokana na hali hiyo kwani aliamini kabisa mwenye kuweza kumnusuru alikuwa ni Rasi na hakuna mwingine.

"Mheshimiwa sina hatia mimi naonewa" Alijitetea


"Wee tena funga mdomo wake huna hatia hii ni mali ya nani?" Rais Zuber alifoka kwa hasira sana na alimtupia bahasha ambayo ilikuwa imejaa picha, Kabinuki alipozifungua picha hizo alijikuta haamini kabisa kwani alikuta jengo lilipo shambani kwake kwenye picha moja. Picha nyingine ilikuwa na vitu ambavyo vilikutwa ndani ya jengo hilo ambako aliona bahasha mbalimbali, pamoja na mifuko ya kemikali.

"Yaani sisi tunakaa na kuamini kuwa nchi imekumbwa na ugaidi kumbe ni wewe na kikundi chako mnatengeneza Leter bomb na kusambaza" Alifokewa

"Mheshimiwa sijui chochote kuhusu hili"

"Hiyo ni mali ya nani sasa kama hujui?"

"Ni yangu"

"Kanini hivyo vitendea kazi vya kutengeza hizo silaha viwepo humo ndani, tena orodha ya kuwaua mawaziri wangu. Umemuua Bai wewe kwani kwenye huyo orodha amewekewa X"

"Mheshimiwa hapana sitambui kuhusu hilo"

"Hilo silijui itaenda kuamua mahakama tu"

"Vijana mpelekeni kituo cha Polisi Oysterbay huyu huku mikifanya taratibu za kufungua kesi, kesi ikifunguliwa mahali kwake ni Segerea tu hakuna kwngine" Rais Zuber alitoa amri na vijana hao walitii wakawa wanamtoa humo ndani huyo waziri ambaye alitokea kujijengea heshima kubwa sana nchini Tanzania.


****


           [7]
  Asubuhi iliyofuata ilikuwa ni siku ya Ijumaa siku hii Norert aliamka ndani ya nyumba ya EASA, ilikuwa ni siku ambayo alikuwa akihitajika kwenda kufanya malipo ya gari lake ambalo alilipeleka kwenye matengenezo. Ndani ya siku alivaa kila kitu cha kujihami ndani ya mwili wake kwani alikuwa akitambua wazi kuwa alikuwa akielekea eneo lenye maadui wake. Alitoka akiwa amepanda pikipiki yake ambyo alikuwa amepewa kwa ajili ya kazi, alikuwa amevaa kofia ngumu ambayo ilikuwa kwa ajili ya usalama wake katika kipindi chote alichokuwa akitumia hiyo pikipiki.

  Majira ya saa mbili alikuwa yupo tayari ndani ya Buguruni na alielekea moja kwa moja hadi ndani  ya sehemu ya matengenezo, hapo alielekea hadi ndani kabisa ambako kulikuwa kuna matengenezo ya gari lake. Huko alilikuta likiwa tayari na alipokewa na mpenzi wa hiyari ambaye alimchangamkia sana alipomuona, kwakuwa wote walikuwa wapo eneo la kazi ilibidi wapunguze uchangamfu ilii isije ikaweka maswali kwa wakuu wa kazi wa hapo.

  Akiwa katika eneo hilo alitajiwa gharama halisi na tayari kitabu cha risiti kilikuwa kimeshakuja mbele yake, alipotaka kulipa alitokea msichana mmoja aliyekuwa amevaia nguo za wafanyakazi wa ofisi za ndani ya jengo hilo ambako ni jirani kabisa na ofisi za mkurugenzi wa humo.

"Samahani kaka unatakiwa ukalipie kwa Mhasibu ndani" Msichana huyo aliongea, wafanyakazi wote walishangazwa na agizo hilo lakini hawakuwa na la kupinga kwani haikuwa mara ya kwanza kutokea jambo kama hilo. Ilimbidi Norbert tu aelekee huko alipokuwa akihitajika kulipa, muda huo aliondoka huku akimpungia mkono Cellina ambaye alimuoneshe ishara ya busu


  Norbet alipofika tu ndani ya jengo hilo mfanyakazi huyo alimuongoza hadi eneo ambalo kulikuwa na mlango wa kioo ambao ulikuwa hauoneshi kile ambacho kilikuwa kilichokuwa ndani, hapo alimuonesha ishara kwamba hiyo ndiyo ilikuwa ofisi yenyewe ya Mhasibu aliyokuwa akitakiwa kulipa kisha akaondoka. Alipoondoka Norbert alisimama hapo kwenye kioo na kisha akaanza kufanya utundu kama wafanyao wale wapendao kupendeza kila muda, alijiangalia hapo kwenye mlango wa kioo huku akirekebisha shati lake kama alikuwa akienda kupiga picha ndogo. Baada ya hapo aliingiza mkono kwenye mfuko wake wa suruali na alitoka miwani ambayo ilikuwa ikifanana kila kitu na miwani ya macho , aliivaa miwani hiyo na kisha akawa anajitazama kwenye kioo cha mlango huo pasipo kujali humo ndani walikuwa wakimuona, Baada ya kujiweka sawa akiongezea miwani hiyo ambayo iliongezea kupendeza kwake. Alisukuma mlango huo wa kioo kuingia ndani ya  ofisi hiyo aliyokuwa ameelekezwa kuwa ni ya Mhasibu. Aliingia ndani  akatokea eneo lenye chumba kikubwa sana cha ofisi ambapo mbele yake kulikuwa na kiti kilichokuwa kikiangalia ukutani, kwenye kiti hicho ambacho kilikuwa ni kirefu kwenda juu kilionekana nywele za mwanamke ambaye alikuwa ameangalia ukutani. Norbert alipoona hivyo  kuwa muonekano wa mwanamke huyo ulikuwa ni kama yupo akiendelea na shughuli zingine, ili kumshtua ilimbidi aachie mguno wa nguvu. Alipotoa mguno huo alihisi kunyemelewa, alisogea kando  kwa haraka sana baada ya kuhisi kitu kikija kwa nyuma yake.


ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment