Tuesday, February 14, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA KUMI NA MBILI


WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com





SEHEMU YA KUMI NA MBILI!!
"Aaargh! Yaani huyu mlinzi badala apige simu kunipa taarifa anakuja kugonga mlango" Kaboneka alinyanyuka na akiwa anaenda kufungua mlango

"Mr Kaboneka wait" Norbert alimsimisha kisha akaongea kwa sauti ya chini, "Kama mlinzi alikuwa na utaraibu uliomuwekea nakuomba usifunue mlango na unisikilize mimi kwani huyo anayegonga mlango hakika siyo mlinzi"




______________TIRIRIKA NAYO

  Ilikuwa ni kauli ambayo haikuwa ya kawaida kabisa kwa Kaboneka, alimtazama sana Norbert asijue alikuwa amefikiria nini hadi  akaweza kuitoa kauli hiyo kwenye kinywa chake. Kauli hiyo ilifanya hata site kufungua mlango kwa sekunde kadhaa na akabaki akimtazama huyo aliyeitoa. Ilikuwa ni kauli ambayo ilijaa ukweli mtupu hasa alipijifikira, haikuwahi kutokea Mlinzi wake akaja kugonga mlango kama hivyo. Hilo suala lilikuwa lisilopingika kabisa. Alikuwa ameajiri Mlinzi kutoka kampuni ambayo ilikuwa na walinzi wenye utiifu mkubwa na hakuwahi kuvunja masharti ya waajiri wake kabisa, hakika alizidi kumuhusudu sana Norbert alimuona ni kiumbe wa ajabu sana kwa ajinsi akiliyake ailivyokuwa ikifanya kazi.

  Wakati akimtazama hivyo mwenyewe ambaye aliona alikuwa ametoa kauli ya kawaida kabisa alinyanyuka kwenye kochi hilo alilokuwa amekaa na kisha akaenda kukaa kwenye kochi jingine ambalo lilikuwa lipo pembezoni mwa mlango.  Kaboneka alibaki akimtazama sana na muda huo mlango uligongwa tena kwa namna ileile ambayo ilionesha mgongaji alikuwa akigonga mlango wa kitu kigumu sana ikiwa ugongaji huo utasikika kwa mtu mwenye uwezo wa kawaida. Lakini kwa jasusi mkubwa na mwenye uwezo wa hali ya juu kama huyo aliyekuwa ametawala ugeni wa humo ndani ya nyumba hiyo. Huyo alijua kabisa mlango huo ulikuwa ukigongwa na sehemu ya kupigia konzi ambazo zilikuwa zimekomaa sana ndiyo maana sauti ilikuwa ikisikika namna hiyo, ndiyo maana aliamua kuketi eneo hilo kwani alishatambua kabisa kuwa mgongaji hakuwa mtu wa kawaida hata kidogo bali alikuwa ni binadamu wa namna tofauti.

  Alimpa ishara Kaboneka ya kuweza kufungua mlango huo akiwa ameambatanisha na ishara ya kumtaka awe na amani, hapo ndipo mwenyeji wa nyumba hiyo alizungusha sehemu ya kitasa ambacho hufunguliwa kwa ndani tu ikiwa mlango utajifunga. Kitendo cha kuungua mlango tu alikutana na na mdomo wa bastola ambao ulimuelekea kwenye paji la uso, alishtuka sana kwani alikutana na yule kijana ambaye alikuwa ametoka muda si mrefu kumpa usingizi wa dharura mlinzi wake kwenye ofifs ya getini. Alijikuta akitaka hata kupiga kelele lakini alipomtazam huyo aliyemuwekea bastola, alikutana na kidole cha shahada ambacho kilikuwa kipo mdomoni. Hapo alibaki kimya na akawa anamkodolea macho huyo Mvamizi aliyetia mguu kwenye kizngiti kikubwa cha nyumba yake, aliashiriwa arudi nyuma ili Mvamizi wake aweze kuingia. Kaboneka naye alitii kabisa na alianza kurudi nyuma taratibu, Mvamizi naye alipiga hatua moja kuingia ndani akijua wako wawili akiwa ni yeye kiumbe asiye wa kawaida pamoja na kiumbe  wa kawaida. Hakujua kulikuwa kuna kiume asiye wa kawaida pia alikuwa akimngojea yeye, alipopiga hatua ya pili kuingia ndani alitegeshewa mguu na Norbert na kupelekea ayumbe. Ilikuwa ni kitu ambacho hakukitarajia kabisa, akiwa anayumba baada ya kutegeshewa ulimfanya ajikwae. Alituliziwa kitu kizito sana sehemu ya kiunoni ambacho kilimfanya aende  chini  na bastola imtoke mkononi kwani hakuwa ametarajia kabisa kukutana na jambo kama hilo, bastola nayo ilikuwa imeruka mbali kabisa na eneo hilo aliloangukia. Alipotaka kutambaa kwa haraka aifuate ili aweze kuihami, mshushaji wa dhoruba kali iliyomkuta hadi akasalimia na sakafu alifanya mchezo mdogo sana wa kitoto akawa ameifkia bastola hiyo. Alipiga sarakasi ambayo hutumiwa sana na wacheza sarakasi na hata watoto wanaopenda kujifunza sarakasi, mtindo wa hatua za mwanzo kabisa katika kujifunza saraksi ndiyo aliutumia kiumbe mwenzake asiye wa kawaaida ambaye alikuwa akitetea nuru kwenye nchi yake

   Wengi sarakasi hii huifahamu kwa jina la 'Roll' ambalo ni neno la kingereza lenye maana ya 'Biringita' kwa lugha ya kiswahili. Saraksi hii hutumiwa sana na wale ambao wanahitaji kukwepa kitu kinachowajia miguuni au kuruka kizuizi ambacho walikuwa wameshindwa kukiruka kwa namna ya kawaida. Hufanywa kwa kuanza kuruka kama mtu muogeleaji anayejirusha kwenye maji, kisha mrukaji akiifikia sakafu huweka mikono na kujibiringisha. Norbert ndiyo alifanya mtindo huu alipomuona mpinzani wake alikuwa akitaka kuifuata silaha, alitangulia juu yake kwa hiyo sarakasi na kisha akaiwahi yeye silaha na kuishika mkononi halafu akamtazama huku akitabasamu.

   Muda huo Kaboneka alikuwa amekaa kando akiangalia vitu vya ajabu vilikuwa vinafanywa na mgeni wake, alumuona ni kiumbe wa tofauti sana kwa jinsi mambo hayo alivyokuwa akiyafanya. Ilikuwa ni vitendo ambavyo alikuwa akivishuhudia kwenye sinema za mapigano tu na hakuwahi kuvishuhudia moja kwa moja, ila ndani ya siku hii aliweza kuvishuhudia kwa mtu ambaye anahusudu sana kazi zake akikifanya tena kwa wepesi wa hali ya juu. Muda huo Norbert alikuwa akimtazama jinsi Mpinzani wake alivyokuwa amegwaya baada ya kuzidiwa kete katika mchezowa wa kifo, alibaki akimkodolea mcho tu asijue la kufanya kwani alikuwa amezidiwa ujanja na hadi akili ya kufikiria mambo.

"Karibuni ndugu sema utahitaji kinywaji gani?" Norbert alimkaribisha Mvamizi huyo ambaye alikaa kimya tu hakujibu chochote.

"Inaonekana ni muoga wewe basi niambie umekuja kuchukua laptop siyo ili uwafiche mafusadi waliokupa ugali nini?" Alimuuuliza tena lakini hakujibiwa na badala yake alitukanwa.


"Wooow! Ngojera nzuri sana hizo ila hapa umeingia nyumba ya wachonga masanamu si waimba ngonjera"   Alimuambia na kisha alianza kumsogelea kwa taratibu huku akiichezea bastola kwenye mkono wake, alipofika karibu yake yule kijana ndipo akili yake ilifanya kazi na akajifanya amekaa kitako huku akinyoosha miguu mbele. Alipoona Norbert akikaribia jirani alifyatua miguu yake akiwa na lengo la kumpiga chini kidogo ya ugoko ili aanguke.

  Hila hiyo taayri ilikuwa imeshaonwa muda mrefu sana na alipotaka kuifanya tu, miguu ya Norbert ilitanuka kwa upesi mithili haikuwa imepewa amri na mwenye umiliki nayo. Miguu ya  Mvamizi ilipenya katikati ya miguu ya Norbert na kumfanya hata sehemu za mifupa ya kiunoni mwake ishtuke. Alikuwa ametumia nguvu nyingi kuliko kawaida wakati akifyatua miguu hiyo ndiyo maana hata alishtuka mfupa wa kiuno, alibaki akiwa anasikia maunmivu ya kushtuka mfupa huo. Akiwa hata maumivu ya kushtuka mfupa huo hajayazoea alijikuta akipewa teke zito lilimpata kwenye taya hadi akapata hitilafu kwenye meno yake na kutema damu, kichwa chake kilienda chini moja kwa moja na ambapo alibaki akiwa amefumba macho kwa maumivutu.

"Nani aliyekutuma wewe?" Aliulizwa lakini hakujibu chochote aliishia kutema mate yaliyokuwa yamejaa damu ambayo hayakumpta Norbert.

"Anhaa mpole unajifanya jeuri ngoja nikupe zawadi yako" Norbert alipoongea hivyo alimsogelea hadi karibu na kisha alianza kumpa kipigo cha paka mwizi, alipoaacha kumpiga alimtazama jinsi alivyokuwa ameumia sehemu mbalimbali za mwili wake.

"Nasema"  Hatimaye Mvamizi alikiri

"Nimetumwa na.." Hakumalizia kauli yake alitokwa na fahamu kwani kipondo alichokuwa amepewa hakikuwa cha kawaida hata kidogo, Norbert  hapo alitokwa na mguno wa fadhaa na kisha akamtazama mwenyeji wake ambaye alikuwa ametulia kwenye kochi huku akishangaa sana kwa jinsi alivyoona mtu akipewa kipigo.

"Kazi ninayoifanya kufichua maovu lazima niifunze michezo ya kujihami kwani uandishi wa habari wa namna hii ni hatari sana, niishukuru JKT pia kwa kuweza kunifundisha namna za kuzitumia silaha" Aliongea huku akimtazama Mwenyeji wake ambaye alikuwa amekaa kimya tu hakujali alimuambia kwa mara anyingine, "kwa sasa maisha yapo hatarini sana na unawindwa , ninachokuomba ni uchukue ile laptop ya kaka yako na ufuatane na mimi hakuna kukaa humu tena"

  Kilichofuata hapo ilikuwa ni Norbet kuitoa risasi ile bstola hata kama fahamu zikimrudia muda ambao polisi watakuwa wamewasilia hapo, asiweze kabisa kujitetea kwa kuoambana nao. Baada ya hapo alitoa kitambaa mfukoni mwake na kisha akafuta alama zake za mkono na akamshikisha yule mvamizi, alipomaliza hapo aliketi kwenye kochi akiwa anamsubiri mwenyeji wake.

 Kaboneka aliposikia maneno hayo wakati Norbert anaanza kumshikisha bastola mvamizi hakutaka kupinga kabisa yeye aliiingia ndani na akatoka na mkoba wa Tsarakilishi ya mapakato ambao ulifanana kila kitu na ule wa Mwanammke aliyekuwa amemuokoa kule Kiwalani. Walitoka hadi nje na kisha waliingia kwenye gari la Norbert, walipotaka kuondoka Norbert hawakuona dalili za kufunguliwa na kibanda cha mlinzi wa nyumba hiyo. Norbert alipiga honi na hakukuwa na dalili za kuja kwa Mlinzi huyo, aliamua kushuka mwenyewe na kwenda kufungua lango kubwa kwani akili yake tayari ilikuwa imempa hisia kwamba Mlinzi huyo alikuwa tayari amekatishwa pumzi na Mvamizi yule. Alipofungua geti alirudi garini na kisha akalitoa hadi nje, baada ya kulifikisha nje alifunga lango hilo.  Hapo alitoa simu akabonyeza baadhi ya namba na kisha akaongea baada ya simu kuokelea, "Jina lililojitokeza kwenye simu yako si ngeni nafikiri unalitambua wazi, sasa njoo hadi nyumbani kwa mdogo wa Kaboneka mkubwa umchukue mhalifu wako na mwenyeji yupo salma kwenye mikono yangu" Alikata simu na kurejea tena garini ambapo aliliondoa kwa kasi sana.


***


  Muda mfupi baadaye yule Mlinzi aliweza kuzinduka kutoka kwenye usingizi ambao alikuwa amelazwa kwa lazima, kitendo cha kuweza kufungua macho alikutana na bahasha ikiwa ipo mezani kwake ambayo hakuijua ilikuwa imeletwa na nani. Muda huo bado mawazo yake ya kutambua kile ambacho kilikuwa kimepita muda mfupi kabla hajaingizwa usingizi haikuwa imekaa sawa, ilipokuja kukaa sawa ndipo alipokumbuka kuwa kulikuwa na mtu ambae alikuwa amevamia ndani ya nyumba hiyo na kumpiga kofi la ajabu ambalo lilimlaza. Hakuwahi kuona mtu analazwa usingizi wa jabu na kofi na hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza na ilimtokea yeye mwenyewe.


 Akili ya kuzunguka na kutazama usalma wa nyumba hiyo baada ya kuhisi kuwa aliyempiga kofi lile la maajabu hakuwa mtu wa kawaida ilimjia, alipotaka ainuke na kumfuata alijikuta akishindwa kutokana kuwa na shauku ya kuifungua bahasha hiyo. Kwani aliamini kabisa ilikuwa ikimlenga yeye na si mtu mwingine ndiyo maana ilikuwa ipo hapo mezani. Laiti mletaji angetaka kufikisha kwa bosi wake muda ule aliokuwa hana fahamu. Ingekuwa tayari imeshafika kwa bosi wake, aliifungua bahasha hiyo kwa papara akakutana na bahasha nyingine ambayo haikutofautiana na bahasha zile ambazo zilitoa maisha ya watu. Kuona bahasha hiyo iliyokuwa na maneno yaliyokuwa yakiashiria nguvu za giza, akili zake zilimpa wazo jingine kabisa. Aliona kuwa hiyo ilikuwa ni maalum kwa bosi wake kutokana na fedha alizokuwa nazo, alianza kufikiria kuwa bosi wake huyo alikuwa akijihuisha na mambo ya kishirikina. Hapo aliona ni namna gani anaweza kuwa mtu muhimu sana kwa bosi wake ikiwa ataijua siri yake, aliona kupandishiwa mshahara na bosi wake huyo kulikuwa kunafuata na hata kuonwa kama alikuwa ni mmoja wa ndugu zake. Wahka wa kutaka kujua kilichomo ndani ya bahasha hiyo ulimzidi kila idara, hapo akajikuta akiishika bahasha hiyo taratibu na kuanza kuivuta gundi iliyokuwa imewekwa.

 Hakika umbea hauna jinsia kabisa kwani yeyote yule huutekeleza ukimjia ndani ya moyo wake, kitendo cha kuifungua bahasha hiyo aliona Moto wa ghafla ukimvaa naa kisha alirushwa hadi mlangoni ambapo alitokeza hadi nje baada ya mlango wa nyumba hiyo kuvunjika kutoka na mlipuko huo uliotokea. Huo ndiyo ukawa mwisho wake huyo mlinzi  kwa  wahka wa kufungua asichokijua.



****



 Askari wa jeshi la polisi walipowasili ndani ya eneo la nyumba hiyo, walikuta mwili wa Mlinzi ukiwa umeungua na hata ukiwa hautazamiki kutokana na mlipuko ule mkubwa ambao ulimkumba akiwa yupo ndani ya chumba kidogo. Habari za kutokea mlipuko ndani ya nyumba hiyo zilikuwa ni muda mfupi tu tangu zianze kuzagaa ndipo walipowasili, walipoingia ndani ya nyumba hiyo kwakuwa walikuwa wana maelekezo kabisa. Walimkuta yule Mvamizi akiwa hana fahamu na bastola yake ikiwa ipo mkononi mwake, hawakutaka kusubiri kwani walikuwa wameshaelezwa kila kitu juu ya nyumba hiyo kutembelewa na Jasusi hatari ambaye alikuwa amemuokoa mmiliki wake. Walichoamua kukifanya ni kuchukua ile silaha wakiwa wamevaa mipira na kuitia kwenye mfuko wa laioni, kilichofuata hapo ilikuwa ni kumfunga pinfgu yule Mvamizi na kwenda kumtupa kwenye gari lao kwani hawakuona hata haja ya kumkimbiza hospitali ikiwa alikuwa amepoteza fahamu tu na ingemrudia muda wowote ule. Taarifa ya kutokea mlipuko mwingine ndani ya nyumba ya Kaboneka tayari zilikuwa zimeshafika kwa baadhi ya wananchi kupitia wanahabari ambao walikuwa wameshafika ndani ya eneohilo, vyombo  vya habari mbaliimbali viliiripoti taatifa hiyo moja kwa moja.


****


   KIBEWANI
    TANGA

  Majira haya ndani ya kijiji hichi cha udigoni ambacho kipo karibu na Kijiji ch Duga Maforoni, taarifa hii ilikuwa ikisikilizwa na Mzee mmoja ambaye alikuwa amevaa nguo zilizokuwa zimechakaa sana. Mzee huyu alikuwa amekaa kwenye kibaraza cha nyumba yake ya udongo iliyokuwa imeezekwa kwa makuti akisikiliza taarifa hiyo, aliisikiliza hadi taarifa hiyo ilipoisha alibadili  na kuweka kituo kingine cha redio na taarifa ikawa ni ileile tu kwani ndiyo ilikuwa taarifa kubwa iliyokuwa imepamba jiji la Dar es salaam. Ilikuwa ni taarifa ambayo ilikuwa ikiwatisha baadhi ya raia waliopo ndani ya jiji hilo, lakini kwake yeye aliyekuwa yupo mbali kabisa na jiji hilo aliona ahueni kabisa kwani alitambua kabisa kuwa mlipuko huo ulitokea ndani ya nyumba ya mtu aliyetajwa ulikuwa na lengo maalum. Baada ya taarifa hizo kuisha aliamua kuinuka hapo chini kivivu zaidi tena akitumia nguvu nyingi zaidi na kisha akaitwaa redio yake na kuingia nayo ndani ya nyumba yake iliyochoka kabisa. Alifika hadi ndani ya chumba chake ambacho kilikuwa kikipitishwa mwangaza mdogo sana  na akaiweza redio hiyo pembezoni mwa kitandani chake, baaada ya hapo aliketi kitandani kwa uchovu uleule huku akiangalia maeneo ya dirishani kwa tahadhari zaidi, aliketi kitadani alipeleka mikono yake hadi chini kbisa kwenye  sakafu ya udongo na kisha akavuta sehemu moja ya udongo huo uliokuwa umeshindiliwa. Sehemu hiyo ilifunguka kama mfuniko ambapo ndani yake kulionekana kukiwa na mkoba unaofanana na mikoba ile miwili ambayo muda huo ilikuwa ipo mikononi mwa Norbert, alipouona mkoba huo alitoa tabasamu lake la kizee na kisha akafunika tena ambako hakukuonekana kama kulikuwa na mfuniko. Baada ya kuufunika mfuniko huo alijilaza kwenye kitanda cha kamba kilichokuwa humo ndani, alilala chali akawa anaangalia paa la nyumba hiyo.

"Ipo siku tu" Aliisemea mwenyewe huku macho yakiwa yapo juu


ITAENDELEA!!



No comments:

Post a Comment