Friday, February 10, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA NANE


WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com




 SEHEMU YA NANE!!
  Hadi kurejea kwake kazini alikuwa ameshaacha maafa mengi sana ikiwemo kupoteza maisha kwa Mutonga kule kwenye nyumba ya Mzee Mabina, sasa anaaamua kuungana na Scorpio katika kutafuta ukweli juu ya mwenzao ambaye hakuwa amerejea kabisa tofauti na kazi waliyompa muda iliyokuwa ikitaka ifanyike





_______________________TIRIRIKA NAO

 Josephine Hilarius au maarufu kama Leopard Queen kama alivyokuwa akijiita ndani ya kisa cha WAKALA WAGIZA, ni mmoja kati ya wasichana hatari sana kuendelea kupumua kwa nchi hii ya Tanzania. Uendeleaji wake kupumua ndani ya nchi tayari ulikua umesababisha mambo mengi sana, msichana huyu aliponea chupuchupu katika kisa tajwa hapo  kutokana na Norbert kumuacha akiwa hajiwezi akajua kuwa ndiyo alikuwa hajiwezi baada ya kupigwa chuma la pazia la mgongoni kimakosa na Marehemu Mzee Ole. Sasa amerejea baada ya kutoroka huko kukwepa mkono wa dola usimtie mkononi, umbile lake lile kubwa lililojaa haswa kiasi cha kufikia kumtamanisha mwanakikundi mwenzake lilikuwa limepungua kabisa na muda ingawa halikuwa limepoteza mvuto kabisa tena ndiyo kwanza ulizidi.

  Kifungashio nacho hakikukimbia kabisa pamoja na kupungua kwa mwili bado kilikuwepo kimejaa huku kikijengeka kwa namna tofauti sana, ilikuwa ni mazoezi ya viungo ndiyo yaliyokuwa yameufanya mwili wake uweze kuwa namna hiyo kwa kipindi hiko ambacho alikuwa amepotea kwenye ramani ya macho ya mtu aliyebakia kidogo amuangamize. Nywele ambazo zilikuwa zikificha sehemu kubwa ya jicho lake ndiyo ulikuwa mtindo wake, miwani ya giza kamwe haikumtoka alipokuwa akizunguka katika sehemu mbalimbali majira ya kati. Hadi muda huo hakuwa ametambulika kabisa kuwa mwanamke hatari aikuwa amerudi ndani ya jiji hilo akiwa na jina jingine kabisa.


   Kuja na jina hilo tayari alikuwa ameshafanya maafa makubwa kuliko hata yale ambayo aliyafanya hapo awali, Malkia wa kuzimu ambaye alikuwa akiwapigia watu simu na kuwaonya mambo kabla hawajaletewa wito wa kuzimu ndiye alikuwa huyo hapo  akiwa tayari ameshavipa vyombo vya adola kizunguzungu kwa maafa ambayo alikuwa ameyafanya kwa kipindi tofauti cha muda akiwa yupo nchinI. Alikuwa yupo pamoja na kundi la Jack Shaw au Askofu Achim Valdremar pamoja na yeye mwenyewe ndani ya nchi hii.


   Malikia huyu wa kuzimu akiwa pamoja na Scorpio walitoka hadi sehemu ya ndani kabisa ya ofisi hiyo na wakachukua gari aina ya toyota Altezaa ya rangi nyeusi, wote kwa pamoja waliingia na Scorpio ndiyo alikuwa dereva wa gari hilo. Walitokea katika lango jingine kabisa tofauti na lile lango ambalo alikuwa ameinglia Norbert, walipotokea huko walizunguka upande wa barabarani wakaja kutokea Rozana. Walipokuwa wakiipita stendi ya Rozana Josephine kwa macho yake mawili alimshuhudia Norbert akiwa amechukua usafiri wa pikipiki za kukodisha almaarufu kama 'Bodaboda' na kuingia kwnye barabara hiyo akawa anaelekea yalipo makutano ya  barabara ya     Chama. Alipomuona tu uso wake ulibadilika na ukawa ni uso wenye hasira sana hadi Scorpio aliyekuwa akiendesha gari aligundua hilo.

"Vipi Josephine kuna harufu ya kifo au ugonjwa?" Scorpio aliuliza kwa kimafumbo zaidi, aliposema ugonjwa alikuwa akimaanisha mleta balaa na aliposema harufu ya kifo alikuwa akimaanisha walikuwa wakiwindwa.

"Kuna ugonjwa ambao ulisababisha kazi ya mwanzo mimi na kina Benson ikikwama" Josephine alijibu na kisha akamuashiria  mbele ambako waliona pikipiki ikiitafuna barabarba hiyo kuelekea Buguruni Chama.

"N001 ndiye yule kwenye pikipiki  nafikiri umemuona" Alimpa utambulisho wa mtu huyo ambaye alikuwa amekaa kwenye pikipiki


  Scorpio alipoupokea utambulisho huo uso wake uliweka sura isiyo na mzaha hata kidogo na kwa hasira kabisa, alianza kuongeza gia  kwa nguvu sana. Hakujali kabisa kituo cha polisi kilichokuwa kipo jirani na eneo hilo yeye aliongeza wendo wa gari tu. Kutokana na Toyota Altezaa kuwa ni yenye kuundwa kwa ajili ya mashindano ilishika mwendo mkubwa sana na hadi makelele yake yaliyokuwa yamezoeleka ikinguruma yakazidi. Muda huo  pikipiki aliyokuwa amepanda Norbert ilikuwa ikiwasha taa ya pembeni kuashiria kuwa ilikuwa ikiingia upande wa Kushoto kuelekea yalipo makutano ya barabara ya Tazara, hivyo ilipunguza mwendo pasipo dereva wake kutambua kuwa ilikuwa ikijiwa na gari kwa nyuma ikiwa ipo mwendo mkali sana. Dereva wa pikipiki alipokuwa akijaribu kukata kona Scorpio alikuwa yupo gia namba sita kwenye gari yake na mwendo akiwa yupo kilomita 180 kwa saa, kabla hata pikipiki haijakata kona aliibamiza nyuma kwa nguvu sana majira hayo ya mchana ambako hakukuwa na Askari wa usalama wa barabarani wa aina yeyote yule na kisha Mzungu kichaa aliyekuwa yupo kwenye usukani wa gari hilo alikata kona kuingia upande wa kulia akiwa na mwendo huo akisababisha matairi ya gari hilo kuteleza kama vile gari la mashindano.

  Watu waliokuwa wameshuhudia tukio hilo kama vile walikuwa wakishuhudia tukio la filamu moja ya mbio za magari ya kimarekani lakini ilikuwa ni halisi kabisa, Mzungu Scorpio alipoibamiza pikipiki hiyo kwa nyuma wala hakujihangaisha kabisa kuweza kuijua yeye aliweza kumuangamiza Norbert aliamini kwa mzinga ule aliokuwa amepiga sehemu ya nyuma ya pikipiki hiyo lazima awe ni marehemu hadi muda huo. Alitokomea katika eneo hilo akiwaacha wale watu wasio na umakini katika macho wakiwa wameshindwa kukariri namba za gari hilo, wote waliokuwa wapo ndani ya eneo hilo walishika vichwa kwa jinsi pikipiki hiyo ilivyopatwa na msukosuko.



****



  Muda ambao walikuwa wakikaribia kuigonga pikipiki ile, tayari Norbert alikuwa ameshawaona kwa kutumia kioo cha pembeni cha pikipiki hiyo baada ya kutupa jicho. Walipokaribia kuigusa pikipiki hiyo yeye alijichomoa kwenye kiti cha nyuma na kujitupa pembeni ambako alipiga sarakasi moja matata na kisha akabiringita  kuelekea upande ulipo kituo cha daladala cha chama ambacho kilikuwa kipo karibu na shule ya msingi. Alipokoma kubiringira ndiyo gari ile ilikuwa ikiteleza kueleka barabara ya Mandela njia ya kwenda Tabata kwa ushupavu wa macho yake upeo wake wake mkali aliweza kusiona namba za gari hilo, muda huo tayari ile pikipiki ilikuwa imerushwa hadi barabara ya upande wa pili kati ya barabara hiyo ya njia mbili iliyokuwa ikielekea Ubungo na kuangukia mtaroni pamoja na dereva wake.

    Hakutaka kupoteza muda yeye ajiinua kwa haraka sana na kisha akajifanya ni mtu ambaye alikuwa amechangaywa na ajali hiyo, alikimbia kwa kasi huku akiweka mikono kichwani kama kichaa hadi ilipo sehemu ambako kulikuwa na mashine nyingi za upasuaji mbao jirani kabisa na reli inayoelekea Kurasini pamoja na shimo la Udongo. Alikata kona akaingia ndani kwenye moja  ya mitaa huku akikimbia kwa kasi na kundi la watu lilikuwa likimfukuza likiona kuwa alikuwa amechngayikiwa hivyo alihitaji kuwekwa chini atulizwe, aliongeza mbio zaidi hata wale waliokuwa wakimfukuza aliweza kuwapoteza kwa kona nyingi ambako aliiingia kwenye maeneo ambayo hawakujua kabisa kama kaingia kutokana na mitaa hiyo kuwa imebanana sana. Baada ya kuwapoteza watu hao ndipo alipokumbuka kuangalia vitu vyake akakuta vikiwa vipo salama kabisa kama alivyokuwa ameviacha kwenye mifuko yake ya suruali. Hapo alitoka na kutafuta pikipiki kwa mara nyingine tena na kisha akaingia barabarani akielekea katikati ya eneo la  Bugurunina si kule ambako alikuwa ametokea, aliipita buguruni akaingia hadi Mitaa ya Ilala na hatimaye alienda kutokea Ilala Boma ambako aliunganisha na kuelekea kule ambako alikuwa akihitaji kuelekea kwa muda huo akitoka kule alipokuwa awali.


****


"Kwisha habari yake yule sidhani kama pale atapona ndiyo maana sikujihangaisha kumuangalia" Scorpio aliongea

"Shenzi kabisa mwanaharamu yule akafie mbele huko" Josephine aliongea kwa hasira sana


"Sasa yule alikuwa anawashinda nini nyinyi kazi rahisi kama hivyo"

"Ni mtu ambaye anatumia akili sana kuliko unavyomfikiria, anajua informationa zote kuhusu Don na mkewe"

"Sasa hivi ataenda kutoa information hizo kaburini tu si kwingine shenzi kabisa"

"Yaani kndi letu mwanzo alilimaliza ndani ya siku zisizopungua tano likaisha ni bora tu akafie huko mbele"

"Kweli alikuwa hatari sana huyu kiumbe sasa tuwape hasara hao wananchi wake aliokuwa akihakikisha kuwa wanakuwa salama"


"Hio ndiyo la muhimu kuwapoteza lengo wasijue tunafanya nini ndani ya muda huu shenzi kabisa" Josephine alionge na kisha akatoa simu yake ya mkononi na kubonyeza baadhi ya namba na kisha akaigusa kwenye kioo kwa mara kadhaa na akaiweka sikioni mwake.

"Hakikisha mnaanza kusambaza silaha zetu" Alipoongea maneno hayo alikata simu na kisha akairudisha mahali ilipokuwa awali.

   Muda huo tayari walikuwa wameshapoteza kabisa ushahidi kama walikuwa wanafuatiliwa kutokana na nchi hii kutokuwa na teknolojia ya hali ya juu ya kamera barabarani kwa ajili ya ufuatiliaji magari, waliiingia Tabata ambako walienda hadi ilipo njia ya Kinyerezi na kisha wakaeelekea hadi Ukonga. Kwa kutumia nji za mkato waliweza kufika hadi  Kiwalani ambako walielekea kwenye eneo ambalo mwenzao alikuwa ameenda, hapo walikuta gari ambayo ilikuwa ikitumiwa na mwenzako ikiwa bado ipo palepale kutokana na ulinzi wa gari hiyo. Ilikuwa na ulinzi mkubwa sana na ilihitaji neno la siri kuweza kusogea kwa matairi yake jambo ambalo iliwawia vigumu maafisa wa jeshi la polisi kuivuta gari hiyo, eneo hilo bado maafisa wa jeshi la polisi walikuwa wapo wakiendelea na taratibu ndogondogo  baada ya mwili kuwa imeshaondolewa. Hiyo iliwabidi watulie mahali kuweza kusubiri hadi maofisa hao waondoke kwani waliamini kabisa wasingeweza kukaa kwenye eneo hilo baada ya kukamilisha uchunguzi wao, waliamua kushuka na kuanza kujichanganya na watu ambao walikuwa wapo karibu na eneo hilo ili kuweza kupata umbea kwa kila kitu ambacho walikuwa wameshuhudia kwenye eneo hilo. Muda huo ndipo walipoweza kubaini kuwa aliyeuawa ndani ya nyumba hiyo alikuwa ni mwanaume na si mwanamke kama walivyokuwa wakidhania, hapo walijua kabisa aliyekuwa amepoteza maisha ndani ya nyumba hiyo alikuwa ni mwenzao aliyekuwa yupo kazini katika kuchukua ushahidi ambao ungewaweka mabosi wao matatani.



 Majira ya jioni askari wa jeshi la polisi waliondoka kwenye eneo hilo wakiliacha gari hilo ambalo walikuwa wakienda kutafuta mtaalam wa kuja kusaidia kulitoa eneo hilo kwa kucheza na Tarakilishi, hawakujua kabisa kuondoka katika eneo hilo walikuwa wakiharibu kabisa kwani gari hilo wenyewe hawakuwa mbali nalo na walikuwa wakisubiri tu waweze kutokomea katika eneo hilo wawze kuchukua mali yao na kuondoka nayo katika eneo hilo. Walipoondoka kabisa wote na kuwaacha baadhi ya raia wakiingia kwenye eneo hilo kwa kutoacha ulinzi wakiona kuwa hakukuwa na kingine cha ziada tofauti na nyumba zingine za wanausalama, Josphine ndiyo alikuja kusogea hadi jirani na gari hilo ambalo lilikuwa limefungwa vizuri milango yake.

  Alipolifikia gari hilo alitoa  rimoti mfukoni mwake ambayo alibonyza milango ikatii amri ikafunguka, aliingia ndani ya gari hiyo katika muda ambao watu waliokuwa akiingia kuangalia mabaki ya nyumba hiyo hasa wauza chuma walikuwa hawamtilii maanani kabisa. Watu waliokuwa wapo jirani gari hilo majira hayo ya usiku waliweza kushtushwa na mlio wa kuwaka kwa gari hilo pamoja na taa za mbele kuwashwa. Wakiwa hawajajua ni nani aliyeingia ndani ya gari hiyo walishtukia ikianza kujongea kwenda mbele kuifuata barabara ya mkato iliyokuwa ikielekea barabara kuu, ile Toyote Altezza ilikuwa imetangulia mbele na gari hiyo ikafuata nyuma katika kuliacha eneo hilo.




****



   Kituo cha kwanza kukifikia ilikuwa ni ndani nyumba ya shirika lao, huko Norbert aliingia moja kwa moja hadi wakati namba za gari ambalo lilikuwa likifanya jaribio la kutaka kumuua lilikuwa zilikuwa zipo kwenye kichwa chake. Alienda moja kwa moja hadi kwenye Tarakilishi zenye uwezo mkubwa sana ambazo zilikuwa zipo ndani ya nyumba hiyo na akawasha mojawapo na kisha kuingiza neno la siri kuweza kuzitumia. Norbert alichoamua kukifanya basda ya kufanya hivyo aliamua kuingia kwa njia isiyo rasmi kabisa katika tovuti ya mamlaka ya mapato nchini TRA, ujuzi alionao ambao aliupata kwenye mafunzo ya kiujasusi katika uchambuzi wa Tarakilishi haukumuwia vigumu kabisa kuweza  kufika kwenye eneo ambalo angeweza kuandika namba za gari hilo na kuweza kumpata mmiliki wa gari  iliyokuwa ikidhamiria kupoteza uhai wake muda mfupi uliopita. Aliingiza namba za gari hilo na kisha akasubiri kwa muda na  haikufika hata muda mrefu aliweza kuona gari hilo husika, haikika haikuwa namba ya gari dogo bali ilikuwa ni namba ya lori ambalo ilikuwa halipo barabarani na mmliki wa lori hilo ndiyo ilichnganya zaidi.


 Ilikuwa ni namba ya lori ambalo lipo chini ya Nouther brothers ambayo alikuwa akitambua kabisa wamiliki wake walikuwa tayari wameshaiaga dunia kwa kukatishwa pumzi na yeye mwenyewe. Nouther hiyo brother ilikuwa ikisimama mbadala wa kaka wawili waliokuwa wenyeji wa jiji la Arusha ambako ni kaskazini. Watu hao aliwambua walikuwa ni Filbert Ole maarufu kama Mzee Ole pamoja na mdogo wake Wilson Ole ambao wote ni marehemu hadi muda huo,  alijiuliza kuwa kampuni hiyo ilikuwa ni chini ya nani ikiwa watu hao walikuwa ni marehemu lakini hakupata jibu kabisa Alipotaka kujiaminisha kuwa namba hizo zilikuwa zimebuniwa tu jambo hilo alikataa katakata aliona kulikuwa na uhusiano wa jambo hilo. Aliamua kuangalia kabisa namba ya chesesi ya gari hiyo iliyokuwa imesajiliwa, hapo alibaini kabisa gari hilo ambalo ni Lori kubwa la mizigo lililokuwa na limesajiliwa kwa namba zile zilizokuwepo kwenye ile gari iliyojaribu kuyatoa maisha yake. Zilikuwa zimesajiliwa kwa namba jingine na hata alipoangalia picha za gari hilo aliona kuwa ilikuwa ni lori ikiwa namba za usajili tofauti na awali.

  Hakika ulikuwa ni uozo na uzembe mkubwa sana uliokuwa umefanywa na watu waliokuwa wapo mamlaka ya mapato kwa kuisajili gari moja mara mbili, Norbert aliangalia mmiliki a gari hilo na akaona kuwa lori hilo lilikuwa limehama umiliki na sasa lilikuwa lipo chini ya umiliki wa kampuni ya usafirishaji mafuta kutoka bandarini jijini Dar es salaam na kuelekea nchi za jirani ambazo ziolikuwa zikitumia bandari hiyo.

"Huu ni uzembe mkubwa sana au ni wizi uliofanyika hapa kwa kutumia mgongo wa mtu haiwezekani kabisa suala hilo" Norbert aliongea huku akichukua kijitabu kidogo na kunakili anuani zote za mmiliki mpya wa gari hilo la mizigo ambalo hadi muda huo lilikuwa lipo barabarani likifanya kazi kama kawaida. Baada ya hapo aliamua kuingia kwenye mtandao kwa mara nyingine akaaanza kutazama tovuti ya kampuni ile iliyokuwa ikimiliki gari hilo, aliweza kuichunguza tovuti hiyo kwa umakini mkubwa sana ambako alibaini kabisa kuwa kulikuwa kuna mmiliki mmoja  ambaye alikuwa ni mwenye asili ya bara Hindi na hakukuwa na mwingine. Norbert alinakili anuani za makazi ya mmiliki huyo akiwa amemuweka kwenye orodha ambaye alitakiwa kuipitia kwa ajili ya kazi yake hiyo iliyokuwa ikimkabili.

"Tandu ana miguu mingi sana na kila mguu hutoa mchango wake katika safari yake,nina imani yote nitaifikia" Aliongea mwenyewe huku akimkazia macho mmiliki wa kampuni hiyo ya usafirishaji.

*N001 KATIKA UPEKUZI


ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment