Friday, February 24, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA ISHIRINI



WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com




SEHEMU YA ISHIRINI!!
Walikuwa wamecheza mchezo mmoja hatari sana ambao haukufahamika hata na Mhudumu mmoja wa ndani ya nyumba hiyo ya kulala wa geni ya kisasa zaidi, mchezo huo ndiyo maana walifanikiwa kutoka bila hata ya kubakisha maswali kwenye vichwa cha Wahudumu hao juu ya yule MZungu ambaye alikuwa ameingia na Eva mahala hapo. Muda huo hesabu ya haraka iliyokuwa imebaki upande wa maadui ulikuwa umebakia na watu wawili tu ambao ndiyo walikuwa na upinzani mkubwa sana, watu hao nao walikuwa wakihitajika kumalizwa ndani ya muda wowote  kwani mzee wa kazi alikuwa amedhamiria kumaliza kazi yake kabla ya muda aliokuwa amepewa.



____________TIRIRIKA NAYO!!

    ILIVYOKUWA
 Norbert kwenda kumalizia kazi yake ilikuwa alikuwa akielekea kwenda kumpunguza nguvu adui yake, tayari alikuwa ameshaujua udhaifu wa mmojawapo ambao alikuwa ameambiwa na msichana ambaye alikuwa amelala  naye. Kitendo cha Cellina kuropoka tu bila ya kujifikiria alijikuta kiwa ameuza ramani ya vita kwa adui, sasa adui huyo alikuwa akiitumia ramani hiyo katika kumshbulia bosi wake.

  Norbert alikuwa amelala naye kwa lengo hilo tu na pia aweze kupata habari nyingine alizokuwa akizitaka, sasa alikuwa amepata hicho na alikuwa anaingia kazini. Ilikuwani hatua moja kubwa sana kuujua udhifu wa adui yako kabla yeye hajujua wa kwako, muda ambao walikuwa wakikaribia kuujua udhaifu wake tayari alikuwa ameshaujua udhaifu wa adui na tayari mbinu dhidi yake ilikuwa imeshagunduliwa.

  Kitendo cha kupenda wasichana ilihali alikuwa akifanya kazi hiyo ilikuwa ni alama nyingine kwa Norbert, kwani alikuwa akitambua kabisa kuwa wazungu wengi hataa wale ambao walikuwa kwenye kazi nzito kama hizi ni watu wasio makini kabisa wakiziona ngozi nyeusi. Dharau waliyokuwa wameijenga juu ya ngozi nyeusi kwamba hawakuwa na uhatari wowote hasa wanawake ilikuwa ikielekea kumgharimu yeye mwenyewe kwani muda huo tayari ilikuwa ikitumika kama silaha, dharau hii ilikuja kutumika kwa kumchukua Eva ambaye alikuwa ni msichana mrembo  sana. Hakuwa na umbile la kimazoezi hivyo uwezekano wa kumuweka matatani ilikuwa ni rahisi kwani alikuwa ana mwili ambao kudhania kama alikuwa ni mwanausalama ni ngumu sana. Siku hiyo walikuwa Salim ambaye walikuwa wameshirikiana naye kwenye kisa cha WAKALA WA GIZA, yeye alikaa ndani ya Klabu kwani ilikuwa ni utaratibu uliozoeleka kwa Scorpio kutia mguu ndani yake.

  Mchezo ulipangwa kwa Eva siku hiyo kuingia na Norbert ndani ya nyumba ya wageni akiwa na mavazi ya heshima sana, alikuwa ameingia wakiwa wamekumbatiana na Norbert hadi eneo la mapokezi ambako walichukua chumba kingine kabisa si kile ambacho walikuwa wamechukua hapo awali. Baada ya hapo waliingia ndani ya chumba hicho wakiwa wamekumbatiana namana hiyo, walikuwa na mkoba mwingine ambao ulikuwa na nguo kama zile alizoingia nazo Eva pamoja na wigi alilokuwa amelivaa kichwani. Kitendo cha kuingia ndani ya chumba hiko walipanga mpango mwingine na kisha walikaa ndani ya chumba hiko kwa muda mrefu sana, muda wa kutoka Scorpio kule kwenye ile ofisi ulipokaribia Eva alitoka kwa  kupita hapo kimaficho  katika muda ambao Mhudumu yule hakuwepo kabisa.

 Alienda hadi kwenye eneo jingine walilokuwa wamelitenga na huko aliingia ndani, alizitoa nguo pamoja na wigi na kisha akavaa nguo zile alizotumia kumnasa Mzungu mwenye uchu. Baada ya hapo alitoka na akarudi hadi kwenye ile nyumba ya wageni, alienda kuchukua chumba kingine kabisa na alipelekwa hadi kwenye chumba hicho na akaachwa mwenyewe. Mhudumu alipoondoka tu kwenye chumba hiko tayari ilikuwa ni nafasi nyingne kwani Norbert aliingia ndani akiwa na mkoba wenye nguo nyingine za msaidizi wake akamkuta Eva akiwa amekaa kwenye kitanda akiwa anamsubiri, mpango uliokuwepo ulikuwa ni Eva kumuacha Norbert ndani ya chumba hiko na kisha kwenda huko lilipokuwa lipo windo lao. Hilo lilifanikiwa na Norbert alienda moja kwa moja kukaa ndani ya maliwato ya chumba hiko na mlango ulifungwa kwa nje na kisha Eva alirudisha funguo mapokezi akitoa ahadi angerejea tena muda mfupi ujao.

  Ulikuwa ni muda ambao Scorpio alikuwa amefika kwenye Klabu ile na kisha akakaa kwenye meza kuu, akiwa anazifakamia pombe ndipo Eva alipojipeleka pale kwenye kiti na akakaa kama vile alikuwa hana habari. Tamaa za mzungu mwenye uchu muda huo ndiyo zilimponza kwani aliingia kwenye mtego, alipoona binti huyo wa kijasusi ambaye alikuwa yupo mbele yake akijifanya ni changudoa aliingia kwenye mtego kweli ndani ya siku hiyo. Walipofikia makubaliano na kisha wote wakatoka, Eva alimpeleka kwenye hoteli bubu ileile na kisha alipofika hapo mapokezi hakuandikisha kwakuwa tayari alikuwa ameshachukua chumba. Alichokifanya ni kuomba tu ufunguo wa chumba chake na kisha akaingia ndani na mzungu huyo baada ya kupewa funguo hiyo, hiyo ilifanya Mzungu mwenye uchu ajenge picha kichwani mwake kuwa alikuwa amebeba kahaba kweli ambaye hadi nyumba hiyo ya kulala wageni walikuwa wamemzoea kiasi cha kumtengea chumba chake cha  kufanyia mambo yake.


  Hivyo ndivyo alivyowekewa mtego na akaingia kichwakichwa bila ya yeye kujua kuwa huo ni mtego, Eva aliposema anaelekea bafuni lengo lilikuwa ni kwenda kumshtua Norbert kuwa mpango ulikuwa umekamilika. Norbert alipokuwa akitoka Eva alikuwa yupo ndani ya bafu hilo akibadili nguo zile alizowekea windo kisha akavaa nuo nyingine zilizokuwa zikifanana na nguo ambazo aliingia nazo akiwa ameshikana na Norbert. Kichwani alivaa wigi pia kama la mwanzo na kisha akatoka, walipofanya tukio na kutokomea ndani ya eneo hilo walimfungia na kutupa funguo chini ya mlango ili akija Mhudumu ajue mlango huo ulikuwa umefungwa kwa ndani. Mapokezi waliweka funguo ya kile chumba ambacho alichukua akiwa na Norbert huku akiwa na mkoba kama alioutumia kuingia ndani hapo ambao ulikuwa na nguo ambazo alizivaa kwa ajili ya mtego.


****


     BAADA YA KUTOKA HAPO
   Norbert akiwa yupo kwenye usukani walielekea moja kwa moja kwenye Klabu ile ambapo walipofika nje tu, walimkuta Salum akiwa yupo nje akiwasubiri. Aliingia ndani ya gari hilo na kisha wote kwa pamoja waliondoka katika eneo hilo wakiwa wameshaacha maafa kwa madui zao, safari yao iliishia Bunju kwenye eneo ambalo kulikuwa na nyumba ya Brian aliyeuawa kwenye kisa cha SHUJAA. Huko Salum na Eva walishuka kwani ndiyo lilikuwa eneo la kazi. Nyumba hiyo kutokana na muundo wake uliojengwa ilikuwa tayari imeshafanywa ofisi za shirika hilo na wafanyakazi walikuwa ni wengi sana wakiendelea na kazi zao, hapo aliwaacha na kisha alirejea katikati ya jiji kuendeleana harakati zingine.





****




 
  Majira hayo Mheshimiwa Roho alikuwa yupo kwenye jengo jingine na vijana wake baada ya kufika kwa taarifa mpya. ilikuwa ni taarifa ya kifo cha Spider aliyekutwa na Askofu nyumbani walipokuwa wakiishi. Hilo lilikuwa ni pigo sana kwa Mheshimiwa huyo kwani hakuwa akidhani kuwa mambo yatakuwa mabaya namna hii katika kipindi kifupi ambacho hata juma moja lilikuwa halijafika, tangu aanze kushirikiana nao kina Askofu na tangu Mzee Ole yupo hai. Hakuwa akiwaza kama mambo yatakuja kuwa mabaya namna hii kiasi cha kuzidi kumuweka mashakani, huyu ndiye alikuwa waziri yule ambaye alitoa agizo Mufti auawe alipotaka kumuweka pabaya. Sasa alikuwa akiendea na ujahili wake katika uchumi wa Tanzania, mambo yalipoharibika ni yeye ambaye alitoa gizo la kufuta ushaidi na pia kuchukua ushahidi mpya ambao ulikuwa umekusanywa. Kuibiwa kwa Tarakilisjhi zile mbili alijikuta akiwa hana amani na mapigo yake ya moyo yakiwa yanamuenda mbio kwani ilikuwa ni pigo kubwa sana kwake na hakuwa akiwaza kama lingekuja kutokea, aliona ushahidi ulikuwa upo mikono salama lakini kuibiwa kwake aliona hakukuwa na usalama kabisa,

 Yaani muda huo alikuwa amekuwa mmoja wa wanasiasa matajiri sana ambaye mali zake alikuwa amewaweka watu wengine ili asizue kitendawili zaidi juu ya alipozipata. Kampuni ya mafuta yote ilikuwa ni ya kwake ingawa alikuwa amemuweka Khemiri kama mmiliki wake. Bado alikuwa na vitega uchumi vingi sana, vyote alivipata kwa namna ya kiharamu. Magari yote ya mafuta yaliyokuwa yapo ndani ya kampuni yake yalikuwa yakisafirisha mafuta na hata mizogo mingine ambayo haikuwa ikitozwa kodi kutokana kuwepo waziri Mwenzake waliyempa jina la Moyo kwani hiyo ndiyo kazi yake. Rekodi za mapato ya TRA mzigo yote ilikuwa imelipiwa kodi lakini haikuwa hivyo, yote ilikuwa ni sehemu ya mchezo mchafu waliokuwa wakiucheza. Yeye ndiye alikuwa akivizima vyombo vya dola ikiwa pakaonekana hakuna sehemu yeyote ile ambayo ilikuwa na usalama, alikuwa akiweka wanausalama wale waliokuwa vibaraka wake katika siku ambayo mizigo yake haramu ilikuwa ikitoka. Pia maafisa wa kodi ambao walikuwa ni haramu alikuwa akiwaweka kwenye siku hizo, yote hiyo ilifnya awe akikwepa ukaguzi wa kila namna kwenye hiyo kampuni yake huku uraiani akisifika  ni mmoja kati ya viongozi waliokuwa wakiaminika sana.

  Kutokana na kazi zake haramu alijikuta akiingiwa na joto katika tumbo lake kwa ghafla sana baada ya kusikia kuwa tarakilishi zile zenye nenosiri zilikuwa zimechukuliwa,muda huo alikuwa amejiinamia akiwa ameshika kifaa cha gesi ambacho hutumiwa na wagonjwa wa pumu. Alikuwa akihema sana  baada ya pumu yake kumpanda kwa ghafla sana, mafeni yaliyokuwa eneo hilo yote yalikuwa yamezimwa kwani ilikuwa nu hatari sana kwake. Alitulia baada ya kipindi cha muda ndipo aliweza kuwa katika hali ya kawaida kidogo, aliinua kichwa chake na kisha akamtazama Askofu ambaye alikuwa ameleta taarifa hiyo akiwa na Josephine aliyetoka kufanya mauaji.

"Hii ni mbaya sana jamani hebu fikirieni mara mbili ikija kujulikana je? Pesa zetu zote zimekombwa na huyu kiumbe na isitoshe amechukua ushahidi uliokuwa ni muhimu sana kwetu. Nimejitahidi kupoteza kushahidi kwa kuwauzia habari juu ya uwepo wanausalama waliotumwa kufatilia kifo cha Bai kule Dodoma ili tu tusiwe pabaya lakini mambo ndiyo haya yanazidi kuwa mabaya zaidi sijui hata tufanyeje" Aliongea kwa sauti ya chini yenye kulalamika

"Mheshimiwa hapa tusiwe namna hiyo ni ishara tosha ya kukubali kushindwa, hapa ni kama tunacheza masumbwi. Jua upande mmoja umetuelemea" Askofu aliongea

"Sasa tufanyeje maana Moyo hajajua chochote kile kuhusu hili tujadilini na kisha tumjulishe kuhusu hili jamani" Aliongea

"Hakuna jambo litakaloharibika Mheshimiwa sisi tuo makini bado na muda huu tunamfuatilia Jama, na imani ipo siku atatoa atarifa idara yake na hapo tutampata vizuri kwani mawasilinao yao yote tunayasikiliza kwa sasa" Josephine aliongea

"Unasema nini wewe Josephine? Hamna lililoharibika na haya yanayotokeni nini?  Khemiri mtu wetu lakini tumemuua kwa mikono yetu kwani yeye ndiye angetuweka pabaya zaidi kwani nyendo zake zilikuwa zipo machoni mwa huyu mtu kutokana na kuharibika mambo ili tujiokoe. Bado mwenzatu ameauwa na pia laptop zote mbili zimeibiwa unasema hakuna lililoharibika hebu chekecha akili yako binti" Alimuambia kisha akaanza kuhema tena kwa nguvu sana na kupelekea aipeleke mashine yake mdomoni kwa mara nyingine na kisha akaiminya na kuvuta hewa iliyokuwa ikitoka ndani yake, baada ya hapo alijiinamia chini.

"Mheshimiwa cool down bado tupo kazini na sasa hivi nitaingia Jack Shaw mwenyewe kazini" Askofu aliongea huku akimshika bega kutokana na hali aliyokuwa nayo hasa akifikiria kuja kujulikana hadharani.

"Siwezi nikawa kwenye hali ya kawaida mpaka haya mambo yawe sawa jamani si kazi ndogo kujenga heshima ambayo ninayo kwa sasa jamani ni kazi nzito sana ina inagharimua hata miaka kumi kwa mtu mwenye kutumia njia za kiuhalali" Aliongea kwa tabu sana

"Mheshimiwa sisi tupo makini na tupo pamoja na wewe usihofu kabisa kuhusu hilo" Josehine alimuambiwa kwa namna ya kupole sana na kupelekea anyanyue kichwa kuashiria kuwa alikuwa amekubali kabisa.

"Ok mpigieni na Scorpio aje hapa na awepo wakati tunapanga mipango mipya" Aliongea pindi aliponyanyua kichwa chake kwa mara ya pili, muda huohuo Josephine alichukua simu na kumpigia Scorpio lakini simu iliita tu bila ya kupokelewa.

"Hapokei simu huyu" Josephine alisema baada ya simu kutopokelewa.

"Pumbavu huyu yupo kwenye umalaya wake, yaani tangu aingie Tanzania hiyo imekuwa kazi yake. Inaonekana wasichana wa kitazania wamemtia wazimu" Askofu aliongea kwa hasira sana

"Yaani mkuu hata mimi nimeshamsema sana kuhusu hilo lakini kila nikimuambia tunakuwa hatupatani kabisa yaani" Josephine aliongea

"Jamani hapa ni kumtafuta tu huyu hatuwezi kuweka mpango akiwa hayupo tutakuwa tunacheza tu kwani yeye ni muhimu pia ndiyo maana tukalipa pesa ya nauli yake kutoka Ujarumani hadi hapa Tanzania" Mheshimiwa naye aliingilia



****


   Muda huo Moses alkuwa akijiandaa kutoka ofisni kwake  kwenye idara ya usalama wa taifa, alikuwa akiweka mizigo yake muhimu kwenye mkoba kwa ajili ya kuondoka nyumbani kwake. Alipomaliza kuweka vitu muhimu kabisa kwenye mkoba wake simu ya mezani ya hapo ofisni iliita, muda huo haukuwa muda ambo alikuwa akipokea simu za kikazi kwani alikuwa umeisha muda ilimbidi ainyanyue simu hiyo na kuipoke an hakuwa  na namna.

"Mkurugenzi hapa ongea........Jama wa Majama ni wewe kweli.....Oooh! Thank god tunakutafuta zaidi hata ya pumzi zetu nakuomba sana tuonane au uje ofisni kwangu....ok nitawasiliana na wewe zaidi" Baada ya hapo alikata simu na kisha alitoka kwenye ofisi hiyo akiwa na tabasamu kwani kazi aliyokua ameambiwa na Mzee Kabaita alianza kuona urahisi wake, kumbe hakujua kabisa kuwa mambo hayo yalikuwa ni magumu sana tofauti na alivyokuwa akifikiria kwani tayari yalikuwa yametupiwa jicho na aliyekuwa yupo upande wa kushoto kwake. Ingawa kulikuwa na mwingine ambaye alikuwa yupo kulia kwake bado  jambo hilo lilikuwa na ugumu sana tofauti na alivyofikiria, hakika hakujua kabisa kuwa walikuwepo waliokuwa wakihaha kuzima hicho alichokuwa akikitafuta.


****

   Muda huohuo simu ya Askofu iliita ikabidi wote wakae kimya ili aweze kupokea, aliipokea simu hiyo na kisha akaongea na huyo mtu ambaye alikuwa amempigia simu muda huo. Ilikuwa ni taarifa ambayo ilikuwa ni njema kabisa kwa upande wao na alipomaliza kuongea na simu alijikuta akitabasamu na kisha akawaangaliz wenzake, wenzake walibaki wanashangaa kwani hawakujua kabisa alikuwa akitabasamu kitu gani hadi muda huo aliokuwa amemaliza kuongea na simu hiyo. Aliwatazama wenzake kwa sekunde kadhaa akiwa yupo kimya kabisa kama vile alikuwa amekumbwa na mshangao wa ghafla sana, baada ya hapo alisimama akiwa bado ni mwenye tabasamu na kisha akaendelea kuwatazama.

"Shaw kuna kitu gani?" Mheshimiwa Roho aliuliza lakini Askofu hakujibu bali alitulia tu huku akiwatazama kwa tabasamu pana usoni mwake

"Mkuu nini kipya?" Josephine naye aliuliza

"Jama Wa Majam hatimaye yupo jijini, amepiga simu kwa bosi wake sasa hivi. Vijan wamenasa location yake tayari" Aliongea na kuwafanya wenzake nao watabasamu.

"Yes! Leo hii tunamfuata hatusubiri  zaidi tukitoka hapa tu jioni hii" Josephine aiongea

"Mfuateni pia msiende kichwakichwa tena inabidi muwe wawili maana yule mtu naye ana akili kama mchawi"  Mheshimiwa aliwambia

"worry out Jack Shaw nipo kazini sasa hivi na tunaenda sasa hivi" Askofu alimtoa hofu

"Yaani tukiipata tu ile paltop yake tutamuachie huyo N001 hayo malaptop yote manne halafu ile tunaiharibu hakuna namna sitaki kwenda Segerea" Mheshimiwa aliongea.

*JAMA WA MAJAMA AJIANIKA BILA KUJIJUA



ITAENDELEA!

No comments:

Post a Comment