Wednesday, February 1, 2017

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA MWISHO (KUMALIZIKA)


RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________



SEHEMU YA AROBAINI NA SITA(2)
   
              "Maluteni mimi si mkuu lakini shusheni silaha zenu chini" Alijipa ujasiri na kuongea kuangalia kama wangeweza kutii mari hiyo.

                "Hatukutambui kama mkuu wetu zaidi ya kuwatambua Amiri jeshi mkuu, Meja jenerali Belinda na Meja jenrali Mugiso  basi wewe si mmoja wetu na hapa tupo kwa ajili ya kukumata ufike kule unapostahiki kufika msaliti kama wewe. Afande mkamate huyo" Luteni yule wa kwanza kuongea alimpa amri mwenzake ambaye alinyanyuka na kwenda kumtia nguvuni L.J Ibrahim.
   

                  "Hey! Mnafanya nini mimi ni three star general mkubwa wenu" Alilalalmika wakati akitiwa nguvuni na luteni huyo.



****


    Baada ya kumuona Mzee Ole amesambaratika sakafuni Norbert aliamua kumsogelea Josephine ambaye alikuwa amelala kfudifudi, alimgeuza na kumfanya alale chali kisha akamtazma hali yake. Alimkuta akiwa anakoroma tu akiwa hajitambui kutokana na chuma lile kutua kwenye mgongo wake, alimtazma kwa muda kisha akaachia tabasamu hafifu sana.

               "Ndiyo malipo yako hayo hutopata nguvu mpaka matibabu wakati ukija kutiwa nguvuni na polisi"  Aliongea  akiwa na uhakika kuwa hakuwa na anamsikia, alipoongea mameno hayo alirudisha macho yake kule alipokuwa yupo Mzee Ole akajikuta akitokwa na mguno wa mshangao.

       Mzee Ole hakuwepo kwenye eneo alilokuwa ameanguka hapo awali na hakujua alikuwa ameelekea wapi, alipoangalia vizuri katika eneo ambalo alikuwa ameangukia kwa pembeni aliona kuna mlango ambao haukuwa ukijulikana hapo awali wala hakuuona ukiwa umefunguliwa na kurudishwa tu. Norbert alitoka hadi ulipo  ule mlango na akaufungua taa za mwanga mkubwa ziliwaka humo ndani ambapo aliweza kuona ndani ya mlango huo kulikuwa kuna nini, Kulikuwa na ukumbi mrefu sana uliokuwa umetengenezwa kwa muundo wa duara kama ilikuwa wanapita ndani ya bomba. Norbert aliamini kwa asilimia zote kuwa Mzee Ole atakuwa amepitia njia hiyo kuweza kumkimbia, aliamua kufunga mlango ili aweze kumkimbilia lakini alipoufunga alijikuta akiwa hana namna.

       Kitendo cha mlango ule kufungwa tu taa za mahala hao zote zilizima na kisha mionzi mekundu ikajitokeza kwa mbele ambayo alikuwa akiijua wazi ilikuwa ikiunguza ikiwa ikigusa mwili wa mtu.

                        "Oooh Damn it!" Aliongea kwa hasira na akaufungua tu mlango huo na taa zote zikawaka mionzi hiyo ikapotea, aliamua kukimbia kwa kasi kwani mlango ule ulikuwa ukipitisha muda ulikuwa unajifunga wenyewe.

   
      Hii aliijua kwakuwa aliamini Mzee Ole hakuwa amepita katika mlango huo ukiwa umejifunga  na ulijifunga wenyewe. Kwa kasi yake pamoja na pumzi zote alifanikiwa kulivuka eneo lenye mionzi ile yenye rangi nyekundu akatokea kwnye eneo lenye mfuniko unaoingia chini, Norbert aliungua mfuniko huo tahadhari kisha akachungulia chini.  Aliona kulikuwa na maji mengi  yakiwa yamekusanyika kwenye eneo lililojengewa kama bandari,  eneo  aliokuwa ameliona huko kwa mtazamo kabisa alilijua likuwa limechimbbwa kuelekea baharini ndiyo maana maji hayo ya baharini yalikuwa yakiingia hapo ndani kwenye  bandari hiyo ndogo sana. Alipoangaza vizuri ndani ya eneo hilo alimuona Mzee Ole akihangaika kuwasha boti  iliyokuwa imeegeshwa jirani  na eneo hilo, hapo alitambua kabisa Mzee huyo alikuwa akipanga kutoroka baada ya kuona ngoma aliyokuwa anaicheza ilikuwa imemzidi uwezo. Norbert hakutaka kabisa kupoteza muda yeye aliingia ndani ya mfuniko huo na alishuka chini kwa kutumia ngazi za chuma zilizokuwa zimejengewa kwenye mfuniko huo.

    Alishuka kwa haraka sana lakini alipokuwa yupo katikati ya ngazi hiyo ndiyo boti hiyo aliyokuwa akihangika Mzee Ole kuiwasha iliwaka, alizidi kuongeza kasi ili amuwahi lakini alipofika chini tayari Boti ya Mzee Ole ilikuwa imeanza kuondoka. Norbert aliikimbiza kwa pembeni boti hiyo akiwa na lengo la kurukia lakini Mzee Ole aliongeza mwendo ikamuacha mbali kabisa, ilimbidi asimame na arudi pale kwenye maegesho ya boti hizo akachukua boti nyingine ambayo aliiwasha kisha akaigeuza kuelekea kule alipokuwa ameelekea Mzee Ole. Alimkimbiza kwa nguvu sana akiwa anapita ndani ya njia hiyo iliyo na upana kiasi ikiwa imejengewa mithili ya njia mtaro wa maji mkubwa, aliongeza kasi ya boti hadi akafanikiwa kuiona boti ya Mzee Ole ikiwa ndiyo ipo kwenye mlango wakutokea humo ndani ambao ulijifungua ikatoka nje. Naye aliongeza mwendo hadi akafanikiwa kutoka nje na sasa wakawa wametokea jirani na ufukwe wa Msasani kwenye  eneo lenye mawe sana, ule mlango uliojifungua kwa nje ulikuwa na umbile la jiwe ambapo ni ngumu sana mtu kutambua kuwa huo ni mlango.


****


    Baada ya kuhakikisha kuwa ulinzi wa kuilinda Ikulu M.J Belinda na M.J Mugiso walikutana na wote wakasimamaa sehemu moja wakiwa jirani kabisa na Nyambizi aliyokuwa ameingia L.J Ibrahim, haikuchukua hata muda mrefu I.L Ibrahim alitolewa akiwa ameshikwa vilivyo na wale maluteni wenye jukumu la kuongoza Tarakilishi zilizopo ndani ya Nyambizi hiyo. Aliletwa hadi mbele ya maaskari hao ambao walikuwa wadogo kwake kicheo ambao kwa muda huo tayari walikuwa wakimuona dhalili sana, alipofikishwa mbele yao alishindwa hata kuwatazama kutokana aibu iliyokuwa imemuingia juu ya kile alichokuwa akikifanya na sasa kimemuondolea thamani chote.

                 "Ukiwa mpigaji mzuri wa chenga basi ujue na kukwepa rafu Ibrahim si Luteni jenerali tena, ona sasa hujui kukwepa rafu umepigwa rafu kwa chenga zako haramu. Kwa sasa wewe haikufai kuvaa vyeo kama hii ukiwa unalidhalilisha jeshi tukufu hebu mtoeni" M.J Belinda aliongea na kwa pamoja maluteni wawili walishika vifungo vya mabegani vya kombati alilokuwa amelivaa L.J Ibrahim wakavifungua kisha wakavitoa vyeo alivyokuwa amevishwa Ibrahim, hawakuishia hapo walitoa  hadi pongezi zilizpo juuu ya mifuko kifuani ya kombati lake. Baada ya hapo  maluteni hao walimsukuma hadi alipokuwa yupo M.J Belinda akiwa amesimama na M.J Mugiso.

      Alimpofikia tu M.J Belinda alikutana na teke kali sana la pembeni ambalo lilimpeleka chini moja kwa moja akabiringita hadi katika upande ambao kulikuwa na wanajeshi wakiwa wamesimama ambapo aliangukia miguu wako.

      Akiwa ameangukia hapo chini L.J Ibrahim akili ilimcheza kwa haraka na akaona njia pekee ya kuweza kujiokoa ni kuwatumia hao wanajeshi na si vinginyevyo, hakutaka kupoteza miguu alimchota miguu mmoja wa wanajeshi hao na akachukua silaha ya Mwanajeshi huyo kisha akasimama wima na kuilekeza kule alipo M.L Belinda na M.J Mugiso.

                  "Sasa sifi peke yangu bali nakufa na mmoja wa wakubwa zenu" L.J Ibrahim aliongeaa akiikoki bunduki hiyo ambayo ilikuwa tayari imeshakokiwa na kupelekea risasi moja iruke nje katika sehemu ya kutoa maganda ya risasi.

       Alikuwa kaishika vizuri bunduki aina ya AK47 akiwa amewalekezea wakubwa waliokuwa wapo katika eneo hilo, alipotaka kuifaytua tu alikutana na mvua ya risasi kutoka kwa wanajeshi wengine ambazo zilimpata katika sehemu mbalimbali za mwili wake na huo ndiyo ukawa mwisho wake wa kufanya mabaya yote aliyokuwa ameyafanya akiwa  mkubwa jeshi.

                  "Mshahara wa dhambi ni umauti tu, Mugiso tangaza operesheni fagio la chuma imefanikiwa" M,.J Belinda aliongea na M.J  Mugiso alipiga saluti kisha akaelekea eneo lenye kipaza sauti kwa ajili ya kutangaza.


****

     Baada ya kusikika rai ya fagio la chuma kwa vikosi vyote hadi wanausalama waliokuwa wapo humo ndani ya Ikulu waliitikia, tumaini la kurudi madarakani ndiyo lilirudi katika uso wa Rais Zuber aliposikia operesheni hiyo yenye kuondoa wasalitiwa taifa ikiwa imeungwa mono na wanajeshi wote wa jeshi la wananchi wa Tanzania.

     Furaha ndiyo ilizidi kupita maelezo alipoona kuwa alikitarajia kurudi tena katika imani ya wananchi wake, haikuchukua hata muda mlio wa fataki ulisikika kwa nje huku wanajeshi wakishangilia. Alipochungulia nje aliona neno "fagio la chuma' likiwa limejichora angani. Furaha aliyokuwa nayo ilimzidi kabisa akajikuta akitoka nje kwenda kuangalia, baadhi ya wainzi walifutana naye kwenda kuhakikisha anakuwa salama ndani ya muda huo wote anaokuwa yupo huko.

      Haikuchukua hata muda toka toke nje M.J Mugiso alitangaza juu ya kufanikiwa kumuondoa duniani msaliti wa taifa ambaye alikuwa akijaribu  kuwashambulia alipokuwa chini ya ulinzi. Alitangaza opersheni hiyo ilikuwa imefanikiwa kwa muda huo na sasa Amiri jeshi mkuu atabaki kuwa Rais Zuber tu na si vinginevyo, furaha ilimzidi sana aliposikia kauli hiyo na hakuamini kabisa wanajeshi waliokuwa wamepanga kumtoa madarakani ndiyo hao waliamua kumtetea.

      Mwenyewe aliamua kutoka hadi nje ya ikulu akiwa yupo na walinzi wake, wanajeshi waliokuwa wapo nje ya eneo la Ikulu waliipata taarifa yake ya kuja nje ya Ikulu na walijipnga vizuri kiheshima. Rais Zuber alifika hadi walipo wanajeshi hao ambao wote walipiga saluti kiheshima, alifika hadi pale ulipokuwa upo mwili wa L.J Ibrahim na akautazama kisha akatikisa kichwa kukubali kazi ya vijana wake.

      Baada ya hapo aliomba kipaza sauti ambapo kililetwa cha dharura hadi mbele yake, alikipokea kipaza sauti hicho na kukiweka jirani na mdomo wake.

                    "Najivunia sana kuwa na vijana kama nyinyi ndani ya nchi hii mliokataa kufuata amri za msaliti huyu wa taifa na kufuata amri zangu, ujasiri wenu na uzalendo wenu mlionionesha usiku huu wa leo ni ishara tosha kwa maadui wa taifa hili watambue kuwa ndani ya taifa hili hakuna mchezo na wala wanausalama wake hawafai kuchezewa niwapongeze kwa hilo vijana wangu. Operesheni fagio la chumaaa!" Aliongea na kisha mwishoni akamalizia rai ya operesheni hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya pili.

                     "Fagiaaaa!" Wanajeshi wote waliitikia kwa pamoja.

     Hadi muda huo operesheni inakaribia wale wasiolala wakiona kuna mahala kutawapa ugali wa siku tayari walikuwa wameshafika eneo hilo na walikuwa wakirusha moja kwa moja kila kilichokuwa kikiendela, ni waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbalimbali duniani tayari walikuwa wamefika katika eneo hilo wakiwa na vifaa vyao wakiorusha kile kilichokuwa kikiendelea.


****


    Ndani ya maji ya bahari ya hindi kwa usiku huo ulikuwani mfukuzano mkubwa sana baina ya Mzee Ole na Norbert, Mze Ole akijaribu kukimbia na Norbert akijaribu kumtia nguvini msaliti huyo wa taifa. Hadi mafataki hayo yanalia wao walikuwa wapo ndani ya maji  wakiendelea na mfukuzano huo, Mzee Ole alipoona maandishi ya operesheni fagio la chuma angani tayari alikuwa ameona hali ya kukata tamaa ikiwa ipo mbele yake kwa muda huo na alijua tayari mambo yameharibika. Hakutaka kusimama yeye alizidi kuongeza mwendo wa boti na kuzidi kumkimbia Norbert ambaye alikuwa nyuma kwa mita kadhaa aweze kumfikia, alikuwa akimtazama Norbert kila muda ilia jue alikuwa amefikia wapi muda huo. Walizidi kutokomea katikati ya bahari ya hindi wakiwa wanaelekea mashariki, ndani ya usiku ambapo bahari ilikuwa imetulia wao ndiyo walizidi kuleta fujo na kuzidi kuyatibua maji. Norbert aipoona anazidi kuelekea mbali zadi alitoa simu ya mkononi na mkono mwingine akawa ameshikilia usukani, alipiga namba  zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye simu yake na akaiweka sikioni.

                    "Salum nenda kwenye ile nyumba ya Wilson ukamtie pingu yule Josephine sasa hivi amezorai utamkuta sebuleni" Aliongea baada ya simu kupokelewa kisha akaikata na kuirudisha mfukoni.


     Siku zote kama mtu hakuwa ameangiwa atoroke basi hawezi kutoroka kamwe, Mzee Ole alikuwa akikimbia aweze kutoroka lakini hakuwa anatambua kamwe kilichokuwa kipo mbele yake huko anapoelekea. Laiti kama angelikitambua kilichopo mbele yake basi asingejaribu kukimbia kuelekea huko anapoelekea, akiwa anazidi kutokomea huko katikati ya bahari ya Hindi mbele aliona meli kubwa ikija kwa mwendo wa taratibu sana akiwa ameacha nayo kwa umbali mfupi. Mzee Ole alijaribu kuikwepa meli lakini usukani wa boti hiyo ulipinga amri yake na haukukata kona hata kidogo, alibakia akiukata usukani huo na kuunyoosha huku mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio lakini hakuweza kabisa  kukata kona. Akili ya kuruka pembeni hakuwa nayo kabisa kwa muda huo bali alikuwa ametawaliwa na akili ya kukata kona tu aweze kuikwepa hiyo meli, wala hakujua kabisa kuhangaika huko kukata kona ndiyo alikuwa anazidi kukairibia hiyo meli kubwa.

     Alikuja kupata akili ya kuruka tayari alikuwa yupo karibu na meli hiyo na hakuweza kufanya hivyo, kwani kishindo kikubwa ndiyo kulifuatia baada boti yake kugonga meli hiyo na kisha mlipuko ukachukua nfasi yake.

     Mzee Ole pamoja na udhalimu wake ndiyo akawa ameishia namna hiyo akijaribu kuukimbia umauti ambao hakujua ulikuwa upo huko anapoelekea, alisahau kuwa umauti humzunguka mwanadamu katika kila pande aliyopo hadi yanamtokea hayo.


      Norbert alipoona tukio hilo alipunguza mwendo wa boti yake na kisha akaigeuza kurudi kule alipokuwa ametoka baada ya kazi yake kukamilika, aliongeza mwendo ambapo alitumia muda mfupi tu akawa amefika ufukweni akaiacha boti hiyo na karejea kule ilipo ile nyumba ya Wilson. Alifika akakuta magari ya kampuni ya kipelelezi ya EASA nje na ndani ya nyumba hiyo huku wapelelezi wa idara ya open service wakiendelea na uchunguzi mdogo, aliiingia  ndani kabisa ya nyumba hiyo  akakutana na Salum aliyempa ile kazi ya kumkamata Josephine.

                        "Vipi umemkamata?" Alimuuliza

                       "Sijamkuta nimekuta tu damu zikiwa zipo sakafuni" Salum alijibu.

                       "Shit! Bora ningemmaliza tu huyu mwanamke sasa katoroka"

                       "Inaonekana ni ana mafunzo ya ziada"

                       "Nahisi atakuwa hatari huyu mbele kama akipona kwa kipigo kile, kwa sasa kazi imeisha ngoja nikampumzike endeleeni na kazi"

                        "sawa mkuu"

     Norbert alitoweka ndani ya eneo hilo akiwa amemaliza kazi yake, aliacha watu wengine ambao wakionekana na polisi si shida ila yeye hakutaka kubaki hapo kwakuwa hakutakiwa aonekane na wengine wowote zadi ya majasusi wenzake,


****



  WIKI MOJA BAADAYE
UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA MWALIMU NYERERE
      Eneo la kusubiri wanaowasili na ndege walikuwa wamekaa Norbert, Moses, Norene,Jerry, Dokta Hilary na Irene, wote kwa pmoja walikuwa wamekuja kumpokea mgeni wao ambaye ndiyo kwanza alikuwa hajawasili ila masaa yake ya kuwasili ndiyo yalikuwa yakikaribia.

     Baada ya nusu saa ya kumsubiri mgeni wao hatimaye watu walianza kutoka katike eneo hilo la kuwasili wageni, Moses alipoona watu hao alisimama juu akiwa na hamu kabisa ya kumsubiri huyo mgeni aliyekuwa anawasili. Haikuchukua hata muda mrefu Beatrice alionekana akija huku akiburuza begi, Moses alipomuona alimkimbilia akaenda kumkumbatia mke wake ambaye hakuwa ameonana naye kwa muda mrefu sana. Hakujali watu waliokuwa wapo katika eneo hilo yeye alionesha furaha ya ukweli ya kumuona mke wake akiwa mzima na salama, Beatrice naye alifurahi hadi machozi ya furaha yakawa yanamtoka kwa kumuona Mume wake akiwa ni mzima na salama.

                   "I miss you so much my love(nimekukumbuka sana mpenzi wangu)" Beatrice aliongea

                   "Miss you more my Queen(nimekukumbuuka zaidi malikia wangu)" Moses naye aliongea

                   "We mgeni wenyeji wengine hujawaona hadi umemuona mzee mzima tu" Irene aliropoka na kupelekea wote wacheke

                    "Heee! We bibi nawe" Beatrice aliongea akitazama Irene kwa mshangao huku akimuachia Moses.

                    "nawe nini yaani kama tumekaa hapa magogo vile" Irene aliongea huku akinyanyuka na kukumbatiana na rafiki yake kipenzi tangu wakiwa shule. Alipomaliza hapo alienda kukumbatiana na Dokta Hilary shemeji yake wa toka yupo shule.

                    "Naona alikuwa na sumu mwilini bibie ndiyo akaiwahi dawa kwa jamaa pale kaipata ndiyo anatukumbuka na sisi" Norbert naye alitia neno na kusababisha wote wacheke.

                    "Shem na wewe vituko havikuishi" Beatrice aliongea huku akikumbatiana na Norbert na kicheko ndiyo kilikuwa kimemtawala.

                     "Samaki hawezi nacha kuogelea hata siku moja, vipi salama lakini" Norber aliongea na kumjulia hali.

                      "Salama tu sijui kwako"
 
                      "Mungu ansaidia"

      Baada ya kusalimiana na Norbert alienda hadi kwa Norene akakumbatiana naye huku Jerry mtoto wa Norbert akiwa amewashikilia miguu, walisalimiana kama alivyosalimiana na wengine kisha akambeba Jerry.

                "Toto hujambo wewe" Beatrice alimuambia Jerry

                "Sijambo mam mdogo shikamoo, halafu una tabia mbaya umenikimbia" Jerry aliongea

                "Marihabaa,mmmh! Sijakukimbia toto nilienda kukuchukulia zawadi sasa nimerudi" Beatrice alidanganya na Jrry akamkumbatia kabisa.

                "Nataka zawadi mam mdogo" Aliongea.

                "Tena mwanangu usikubali hapo mdake hiyo shingo kabisa zawadi yako akupe huyo" Norbert alidakia na kupelekea wote wacheke.

    Wote kwa pamoja walitoka eneo hilo la kupokea wageni, waliondoka kurudi walipotokea baada ya kumpokea Beatrice aliyekuwa yupo nje ya nchi kwa siku nyingi sana.



MWISHO!!


ASANTE KWA KUWA NAMI KUANZIA MWANZO HADI MWISHO WA RIWAYA HII NATUMAI UMEJIFUNZWA VYA KUTOSHA TUWE PAMOJA KATIKA SHUGHULI HIZI NA NORBERT KAILA MAHALI HAPA.

MAONI TAFADHALI JUU YA RIWAYA HII




NORBERT KAILA ATAREJEA


No comments:

Post a Comment