Wednesday, January 25, 2017

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA AROBAINI NA TANO



RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________




SEHEMU Y AROBAINI NA TANO!!



<<<<SEHEMU YA MWISHO TOLEO LA PILI>>>>>


               "Watakuwa hawanibomoi bali ndiyo kwanza wananijenga na watakuwa wanafanya kazi ya kufuatilia makala zangu online waweze kupata habariza kuuza, wanapata hela kwa maneno yangu huku wananuongezea wafuasi tu" Simon alimaliza kuongea maneno hayo na akafunika tarakilishi yake ya mapakato kisha akajitupa kitandani pamoja na mke wake, alikuwa akitumia akili ya kisiasa ambayo aliona kabisa ilkikuwa ikielekea kumpa mafanikio kwa muda huo huo hadi miaka kadhaa mbele kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania.

    Hakujali kutukanwa wala kukosolewa alichojali yeye ilikuwa kujiongezea wafuasi tu kwenye chama chake kichanga ambacho kimevitingisha vyama vingine tangu akianzishe, alikuwa ana lengo moja tu la kukitingisha chama tawala tu na ndiyo juhudi ameanza.





__________TIRIRIKA NAYO

BAADA YA KUTOKA BARABARA YA SEA VIEW

    Baada ya kufanya tukio la kumungamiza Wilson alitoweika katika eneoo la ufukweni kwa haraka sana, Norbert hakuwa na sehemu nyingine ya kwenda isipokuwa kwa wapinzani wake wakubwa walipokuwa wameweka kambi.

   Akiwa ndani ya usafiri wake alielekea moja kwa moja hadi Msasani mahali alipofikia awali kipindi anakuja kuichunguza nyumba ya Wilson, aliegesha gari kwenye Bar ileile aliyokuwa ameegesha kabla ya kuelekea ndani ya nyumba ya Wilson. Akiwa ndani ya mavazi yaleyale  aliyokuwa amevaa awali pamoja na kofia yake iliyokuwa imeufunika sehemu kubwa ya suso wake, alipitia mlango wa nyuma wa bar hiyo kama alivyokuwa amefanya siku ile wakati anakuja kupeleleza. Njia ileile aliitumia na akaja kutokea jirani kabisa na lango kubwa, alitembea kwenye barabara ileile hadi alipofika usawa wa lilipo geti la nyumba ya Wilson maarufu kama Ngome. Norbert alipofika hapo kwa haraka kabisa alitoa kichupa kidogo sana mfukoni mwake kinachofanana na kichupa cha uturi wa gesi wa mwilini(body spray), alifungua kichupa hucho na alijipuliza sehemu za mdomoni pamoja na pembeni ya mashavu yake. Hakuishia hapo alifungua vifungo vya shati lake halafu akavifunga hovyo, hakika alikuwa akionekana ni kama mlevi aliyekuwa amekosea njia akaingia jirani na geti la nyumba hiyo. kile kichupa alichojipulizia nacho kilitoa harufu kabisa ya pombe hivyo kumfanya aonekane alikuwa amelewa.

   Baada ya kufanya hivyo alikirudisha kichupa hicho ndani ya mfuko wake kisha alijisogeza karibu kabisa na geti hilo, alipokuwa analikaribia geti hilo alianza kuyumba kilevi huku sehemu kubwa ya uso wake ikiwa  imezibwa na kofia aliyokuwa amevaa. Alipofika getini kabisa Norbert alikutana na mwanga mkali sana kutoka kwenye taa maalum zilizopo hapo getini ambao ulimfanya ainamishe uso wake chini, aliweka mikono kabisa kichwani  kujikinga na mwanga huo kama mtu aliyekuwa akijikinga na mvua isiweze kumnyeshea. Kuyumba ndiyo kulikuwa jadi yake kwa muda huo wote aliokuwa  hapo, Norbert aliamua kuinua macho juu huku akihakikisha uso wake wote hauonekani kwenye taa hizo za mwanga mkali zilizokuwa zipo hapo getini alipozitazama taa hizo alirudisha uso chini kwa nguvu sana kisha akatoa mguno wa kukereka baada ya kuzitazama taa hizo. Alipiga hatua moja tena mbele hadi akalifkia kabisa geti hilo na akajigonga nalo, aliyumba baada ya kujigonga nao lakini hakuanguka alijiweza kujizuia.

            "Aaaargh! Ama kweli kuoa mfipa aliyezaliwa na Mpemba ni tabu, ona sasa kashaanza kuniwekea mazingaombwe yake mapema yote hii saa ishirini na moja" Norbert aliongea kilevi sana huku akiitoa simu yake ya mkononi na kutazama saa ambapo alikuta ikiwa inaonesha ni saa tatu usiku ikiwa katika mfumo wa masaa ishirini na nne ndiyo maana alisema saa ishirini na moja. Ilikuwa ni muda ambao bado kabisa hata IGP Chulanga alikuwa hajapata mchoro wa muuaji wa Mufti.

              "Ona sasa anajifanya kawa Mungu na yeye kawasha jua lake linaniwakia hapa utosini mwangu usiku huu, mbele ya mlango kaipoteza nyumba kimazingara kaweka kontena. Pumbafuuu! Anataka majirani wanione mimi chizi siyo yaani nidhanie nipo kwenye eneo la bandari kwenye makontena. Uchawi wake haunipati ng'oo nasema hata kama ni kontena nitaingia ndani  hivyohivyo anione mimi  mchawi zaidi" Norbert alizidi kuongea kilevi muda huo alikuwa akijifanya kuwa haelewi ile iliyokuwa hapo juu ni taa akijifanya anaona ni jua kwa ulevi kumkolea. Alijifanya pia halitambui kuwa hilo hapo mbele yake ni geti yeye aliita kontena lilokuwa amewekewa na mke asione nyumba.

              "We! Mbwa ndiyo umetoa mlango siyo kwa uchawi wako sasa mimi napanda juu naingilia batini" Alizidi kujitoa akili na muda huo alianza kuliparamia  geti akionekana kuelekea juu, vituko vyake havikuchukua muda mlinzi wa hapo getini tayari alikuwa ameshaviona na alifungua mlango wa pembeni wa kupitia watu.

     Alipoufungua tu mlango huo ambao ulitoa sauti hafifu ambayo ilisikika wazi kwenye masikio ya Norbert, alibaki tu akimtazama Norbert ambaye alikuwa akionesha juhudi za wazi kabisa za kuliparamia gati lakini alionekana kutoweza kabisa. Norbert naye alijifanya kutomuona mlinzi huyo na aliendelea kufanya juhudi za kuparamia geti hilo hadi pale mlinzi alipopiga kiatu chake chini kwa nguvu sana kumshtua, mlio wa kiatu hicho ulimfanya Norbert ashtuke kwa nguvu sana hadi akaachia geti alilokuwa amelishikilia wakati akijaribu kupanda. Norbert alianguka hadi chini, yule mlinzi aliyekuwa yupo hapo getini alibaki tu akimtazama Norbert akimuona ni mlevi aliyekuwa amepotea njia.

     Baada ya kuanguka chini alijiinua kivivu sana na akaweza kusimama wima ingawa bado alikuwa akipepesuka kilevi, aligeuza uso wake na akatazama kule alipokuwa yupo yule mlinzi aliyepiga kiatu chini kwa nguvu hadi akashtuka kimaigizo na akajiangusha chini.

                    "Anhaaa! We bwege kumbe ndiye unayeniibia mke wangu yaani bora umejitokeza mwenyewe pumbavu zako, ndiyo ukamwambia huyo malaya augeuza huo mlango wa kuingia ndani upande huo ili mimi nisiingie ndani ule vizuri asali yangu" Norbert aliongea kilevi kumuambiaMlimnzi huyo ambaye hakujibu chochote zadi ya kuishia kumtazama tu.

                     "Muone kwanza dume zima una mahips" Norbert alizidi kuropoka na safari hii akambeza Mlinzi huyo juu ya suruali aliyokuwa amevaa ya sare ya kazi kutokana na kutuna sehemu za mapaja kwenye mfuko ya surusli hiyo, Mlinzi bado alikuwa amekaa kimya huku akiwa amefumbata mikono kifuani mwake.

                      "Kwanza nina wasiwasi na uanaume wako usije ukawa msagaji wewe, mwanaume gani ana manyonyo dume jike wewe umekuja kumsaga mke wangu" Alizidi kumbeza Mlinzi na safari alimtaniaa juu ya kutuna shati la kiulinzi kifuani kutokana na uwepo wa mifuko mikubwa kama iliyopo kwenye suruali yake, maneno hayo yalikuwa ni yenye kuudhi lakini Mlinzi huyo aliamua kuzuia hasira zake.

                      "Haloo wewe! toka hapo ulevi wako usikupeleka pabaya, hapa ni nyumbani kwa watu wazito nitakuharibu sasa hivi!" Mlinzi aliamua kumkoromea Norbet akiamini alikuwa ni mlevi aliyekuwa amepotea njia

                      "Hao wazito wana kilo ngapi  au ndiyo umeniletea wasagaji wenye hela uwasage pamoja na huyo mke wangu ndani, mkaugeuza mlango kichawi ukajua sitauona kwa taarifa yako nimeuona huo hapo tena mmeufanya mdogo kabisa" Norbert aliendela kuropoka kama ilivyo kawaida yake, baada ya kuongea maneno hayo aliutazama mlango  mdogo wa kupitia watu aliopitia yule Mlinzi vizuri.

    Aliutazama kwa sekunde kadhaa mlango wa geti kisha akaropoka, "Wajinhga nyinyi ndiyo mmeamua kuung'a mlango wa mbao ngumu za mkaratusi niliyokuwa nimeuweka kwa hela nyingi mmeuweka huo wa bati mtanieleza leo" Alipoongea maneno alianza kumfuata mlinzi kwa kasi sana akiwa na miondoka ya kilevi, alipomkaribia alirusha ngumi nztio ya kilevi ambayo Mlinzi huyo aliikwepa akaenda chini moja kwa moja akaangukia kifua.

                   "Haaa! Huyu mwanamke ndiyo kakuongeza uchawi ili usiweze kupigwa siyo" Norbert aliongea huku akijinyanyua kwa tabu, alifanikiwa kunyanyuka kilevi na alisimama huku akiyumba sana.

    Eneo alilokuwa amesimama Norbert kwa muda huo kulikuwa na kamera ya ulinzi iliyokuwa imefungwa juu kidogo ya kichwa chake kwenye ukuta, kamera hiyo ndiyo ilikuwa ikichukua matukio yote ya hapo nje. Mlinzi huyo hakujua kama kumkwepa Norbert hadi akaelekea upande huo alikuwa amefanya kosa kubwa sana, ilikuwa ni bora hata angemrudisha kwa pigo la nguvu kulekule alipokuwa awali kuliko alivyomkwepa.
Kamera hiyo ya ulinzi ilipoanza kuzunguka tu Norbert aliiona na aliitazama huku akiyumba, aliweka mkono mdomoni kwa mshangao kama alikuwa amegundua kitu cha ajabu sana.

                 "Alaaaa! Wajinga nyinyi si ndiyo uchawi wenu huu hadi nyumba siioni naona kontena" Norbert aliongea na kwa haraka sana akairuka juu akaishika kamera hiyo ya ulinzi akavuta hadi akaiharibu, tendo hilo lilimuundhi sana mlinzi huyo ambaye alione kabisa huyu aliyekuwa akiamini ni mlevi alikuwa akitaka kumuhairibia kazi yake.

    Uvumilivu wake wa kuvumilia matusi yote aliyokuwa ametukanwa na Norbert ulifika kikomo hadi muda huo, hasira zilianza kumpanda ndani ya kichwa chake na akabaki akimuangalia Norbert aliyekuwa ameanguka chini kilevi baada ya kurukia kamera hiyo na kuiharibu hadi ikazima ikawa haifsnyi. Mlinzi hakutaka kabisa kuendelea kuangalia vituko alivyokuwa akivifanya Norbert, aliona huo ndiyo ulikuwa ni muda wa yeye kumuadhibu ili ashike adabu asiweze kuingia katika eneo kama hilo hata awe mlevi kupita kiasi. Alichomoa rungu lake alilokuwa amechomeka kiunoni na aliamua kumfuata Norbert kwa kasi pale alipokuwa amelala nchini baada ya kuanguka, alijua kuwa alikuwa ameanguka kilevi na hawezi tena kuinuka kumbe ilikuwa ni hila ya Norbert ya kuweza kumvuta ndani ya anga zake aweze kumpa haki yake.

    Mlinzi yule alipomkaribia Norbert alishusha rungu lake kwenye kifua cha Norbert kwa hasira akiamini lingempata, rungu lake hilo lilitua kwenye sakafu ya eneo na halikuweza kabisa kumapata Norbert kwani tayari alikuwa amejibiringisha mbele zaidi. Mlinzi alimposogelea zaidi alikutana na mtama wa haraka sana kutoka kwa Norber ambaye aliuzunguka mguu wake kama feni, alianguka hadi chini na hata kabla hajafikiria kitu kingine cha kufanya alipokuwa ameanguka mguu mzito  wa Norbet ulitua kwenye kifua chake ambaye hakuelewa alikuwa ameinuka muda gani.

    Hakuwa Norbert yule mwenye sauti ya kilevi pamoja na muondoko ya kuyumba bali alikuya yupo imara kabisa, Mlinzi alibaki akiduwaa asiamini kabisa kwa kile alichokuwa amekiona.

    Akili yake akiwa bado yupo chini hapo ilimtuma aupeleke mkono wake kiunoni alipokuwa ameweka silaha yake ili aeze kuichomoa kuweza kumdhibiti Norbert, tayari alikwishatambua kuwa alikuwa amevamiwa na mtu aliyekuwa akijua nini anachokifanya na wala hakuwa mlevi kama  alivyokuwa akidhania hapo awali.Akili ayake hiyo tayari ilikuwa imeshasomwa barabara na akili shupavu na nyepesi aliyokuwa nyo Norbert, kitendo cha yeye kugusa tu sehemu ya kiunoni Norbert aliupiga mkono wake. Bila ya kuchelewa alimuongeza teke jingine la kwenye mbavu hadi Mlinzi huyo akatoa ukelele wa kuuumia ambao  ulimfanya Norbert apepese macho kwa haraka sana katika pande zote. Alipoona pako kimya alizidi kumpa kipigo mlinzi huyo hadi alipohakikisha kuwa alikuwa kalegea kabisa, hapo alimuinua na kumuingiza ndani  kwa kutumia lango mdogo.
Alimburuza hadi yalipo makazi ya mlinzi wa eneo hilo akamuweka chini katika eneo hilo ambalo lulikuwa na mitambo mbalimbali ya ulinzi pamoja na silaha za kujihami.

               "Inamaana huyu mtu nisingemjia kwa njia hii basi kiama changu kilikuwa kinakaribia kabisa, kwa silaha hizi" Norbert alijisemea kisha akamuongeza mlinzi yule teke jingine akiwa yupo naye humo ndani na nyumba ndogo ya ulinzi.

     Mlinzi alizidi kutoa miguno ya maumivu kwa teke hilo alilokuwa amepigwa, Norbert hata hakujali maumivu yake yeye alimuinua akamuweka kwenye kiti cha humo ndani. Alifanya haraka sana akatafuta kamba imara iliyokuwa ipoo  humo ndani ambazo hutumika hasa na wacheza sarakasi, alimfunga ile kamba kwenye kiti hicho  kwa nguvu sana kuhakikisha kuwa hawezi kutoka akiwa yupo katika eneo hilo. Baada ya kumfunga kamba hiyo Norbert ndipo alikaa kwenye kiti kingine kilichokuwa kipo katika eneo hio, mawazoni mwake alikuwa na lengo la kumbana tu Mlinzi yule aweze kusema juu ya kile alichokuwa akikitafuta ambacho kingeweza kumsaidia katika kukamilisha kazi iliyokuwa imemleta katika eneo hilo.

                 "Wakubwa zako wapo wapi?" Alimuuliza lakini hakuambulia jibu lolote zaidi ya Mlinzi huyo kuinamisha uso chini kwa kiburi sana.

                  "Mfumo wa hiii nyumba kiulinzi upoje?"  Aliuliza tena akiwa hatilii maanani swali lile la kwanza ambalo lilikuwa halijajibiwa na Mlinzi huyo, kimya kingine ndiyo kilifutata na si kujibiwa swali kama alivyokuwa akitarajia yeye baada ya kuuliza.

                  "Ohoo! Kiburi sana wewe ngoja nikuoneshe kuwa kuna viburi zaidi yako katika dunia hii" Norbert aliongea kisha akatoka hadi katika eneo lenye silaha ndani ya  chumba hicho, alichukua kikasha kidogo  chenye rangi nyeupe akaja nacho hadi mbele ya  huyo Mlinzi.

    Norbet alikifungua kikasha hicho akatoa bomu dogo sana la kutegesha kwa saa kisha akalitega na kuliweka karibu ya mlinzi huyo chini ya kiti alichokuwa amemfunga huyo.
Mlinzi huyo alianza kuingiwa na hofu alipoliona bomu hilo likiwa limetegwa jirani kabisa na na yeye na huyo aliyekuwa akilitega wala hakuwa ni mwenye kumuonea huruma ndiyo kwanza alikuwa akitabasamu kabisa akiona kile alichokuwa akikifanya kilikuwa ni kitu kizuri sana na kibaya kwa adui yake.

                   "Una dakika mbili tu za kuweza kuishi sali sala zako za mwisho tu ndugu" Alimuambia huku akianza kutembea kutoka nje ya chumba hicho

    Yule Mlinzi alipoona hali ni hiyo hakika uzalendo ulimshinda kabisa na akajuta hata kuwa kiburi kwa mtu kama huyo asiyetaka kuoneshewa kiburi, aljaribu kujiiinua na kujitoa kwenye kiti hicho lakini hakuweza hata kidogo na ndiyo kwanza Norbert alikuwa akitoka nje ya  chumba hicho akiwa anatembea kwa majigambo kabisa baada ya kumaliza kufanya hivyo.

                       "Weee!  Subiri usiniache hapa sitaki kufa mimi" mwenyewe alisalimu mari

                       "Umepewa nafasi unajifanya mbishi haya bishana na bomu hilo lisilipuke kama wewe mbishi kweli" Norbert alimuambia akiwa anafungua malngo.

                        "Nipo tayari kukuambia kila kitu naomba usiniache na bomu hili" Aliongea kwa unyonge sana.

                        "Ok Unaweza kuongea nakusikiliza au niondoke"

                        "Hapana hapana nitakuambia kila kitu, hakuna mtu huko ndani kwa sasa wote wametoka, ulinzi wa nyumba hii asilimia kubwa unaongozwa na mitambo na si walinzi wengi ukitaka kuzuia usionekane adui chukua rimoti ya geti na utembee nayo" Aliongea ukweli mwenyewe ambao ulimfanya Norbert arudi hadi pale alipokuwa amemfungia na akalichukua lile bomu, Norbert alilisimamisha muda wake wakulipuka kisha akamtazam Mlinzi huyo usoni.

                         "Rimoti ya kufungua geti hilo inafanya kazi umbali ule ilipo nyumba?"

                        "Ndiyo inafanya kazi kabisa hata ukiwa mbali zadi ya nje ya nyumba"

                          "Ok asante kwa maelezo yako ngoja nikusafirishe ulimwengu mwingine kwa dharura kidogo" Norbert alipoongea maneno hayo alimuachia pigo la kisogoni Mlinzi huyo hadi akazirai papo hapo.

      Baada ya kumaliza kazi hiyo alichukua rimoti maalum ya kufungulia geti ambayo ilikua ikitumika kulifungulia geti hilo, alitoka ndani ya  ofisi hiyo la mlinzi na kuelekea ilipo nyumba ya Wilson ambayo ndiyo ngome yenyewe iliyokuwa ikitumiwa na kundi zima ambalo kwa sasa limesalia watu watatu tu.



****


DAKIKA ISHIRNI KABLA YA MAPINDUZI

     Kifaa maalum ambacho huwa anakitumia mlinzi wa ngome akiwa yupo mbali na eneo hilo ili kujua magari ya wakubwa zake yamefika, kilipiga mlio ambao ulimjulisha wazi Norbert kuwa kulikuwa na gari mlangoni. Norbert alipokitazama kifaa hicho aliona gari aina ya  toyota hilux ya rangi nyeusi ikiwa ipo getini, gari hiyo ndiyo kwanza ilikuwa imefika na haikuwa hata imepiga honi kuamrisha geti lifunguliwe. Norbert alipokuwa akikitazama kile kifa aliona kabisa sura ya dereva wa gari hilo ambaye alimfanya atabasamu tu kwa kumuona kwake, alikuwa amemuona Josephine akiwa yupo kwenye usukani akiwa hapo getini.

      Bila ya kuchelewa alibonyeza kitufe kimoja kwenye kifaa hiko na geti lilifunguka, gari hilo liliingia ndani na haukuchukua hata muda gari nyingine aina ya Range rover sport ilifika hapo getini. Norbert alikuwa akitazama kifaa hiko kwa umakini sana, alimshuhudia dereva wa gari hio akiwa ni Mzee Ole akiwa ndiyo anarejea Ngomeni akiwa amepishana na Josephine kwa sekunde kadhaa. Alilifungua geti kwa mara nyingine na gari hilo liliingia ndani kisha akalifunga, baada ya kufanya hivyo alitulia kimya akiwa yupo ndani ya nyumba hiyo kwa upande wa sebule wa kulia chakula akiwa amekaa kwenye eneo lenye giza akiwa anatazama kwa umakini sebuleni palipo na mwanga wa taa kubwa.  Bado aliendelea kutulia paleaple kwenye eneo hilo akiwa anawasubiria kwa hamu maadui zake ambao alijua kabisa hawakuwa na silaha yeyote ya kujihami, silaha zote walizokuwa wanazitumia wao alikuwa amezikusanya na muda huo alikuwa ameziweka kwenye meza hiyo ya chakula akiwa anawasubiria kwa hamu sana.

     Kila aina ya silaha ya kujihami alikuwa ameiweka hapo mezani hata zile silaha ambazo wao walikuwa wakizificha sehemu zisiwezekane kwa urahisi kutambulika kuwa kulikuwa kumefichwa sialha.

    Muda ambao wenyeji wa eneo hili walikuwa hawajarejea ambao alikuwa amewahi mapema sana ndiyo alioutumia katika kupekua kila sehemu ya karibu na eneo hilo, maadui zake hawakuwa na hili wala lile juu ya uwepo wa mbaya wao ndani ya nyumba hiyo.

    Norbert naye aliendelea kuvuta subira akiwa yupo ndani ya eneo hilo, macho yake yote yalikuwa yapo mlangoni akiwa na imani kwa asilimia zote lazima maadui zake watumie mlango huo kwani mingurumo ya magari yao ilikuwa imeishia kwenye eneo la kuegesha magari kwa dharura nje ya nyumba hiyo. Mingurumo ya magari hayo hadi inazimika alikuwa tayari ameshatambua kuwa maadui zake walikuwa wameegesha katika eneo la nje ya nyumba hiyo mitaa kadhaa kutoka baraza la nyumba hiyo lilipo. Aliendelea kusubiri akiwa ameuwekea moyo wake subira na si papara yoyote aweze kutimiza kile alichokuwa akitaka kukitimiza katika eneo hilo, milio ya viatu ilianza kusikika ikikaribia eneo la barazani katika nyumba hiyo ambayo nilimfanya akae tayari kwa lolote lile ambalo lingeweza kujitokeza ndani ya eneo hilo.

    Kusikika kwa milio hiyo kuliendelea kusikika hadi kulipoikairibia mlango mkuu wa kuingilia nyumbani hapo, hapo milio hiyo ilitulia kwa muda  ambapo ndiyo kulizdi kumfanya Norbert atege masikkio yake yaliyokuwa yanasikia sawia katika kusikiliza vizuri. Haikupita muda mlio wa kutiwa funguo katika kitasa cha hapo mlango ulisikika, mlio wa kutekenywa kwa funguo ndiyo ulifuatia na kisha kitasa kikanyongwa kwa nguvu sana.

    Mlango ulifunguliwa na Norbert alimshuhudia Mzee Ole akiingia kwa pupa ndani ya nyumba hiyo, Josephine naye alifuatia kuingia ndani ya nyumba hiyo akiwa anatembea kwa taratibu tu akiwa anayatzama mazingira ya hapo ndani kama vile ndiyo kwanza alikuwa anayaona.

                 "Nilikwambia Wilson kasharudi huyu ona hii taa kaiwasha nani sasa wakati tuliizima" Mzee Ole aliongea

                  "Sasa kwanini aaache gari kule kwenye parking hadi muda nalichukua, amerudi na miguu kwahiyo?" Josephine aliuliza

                   "Punguza hofu Leopard Queen huyu kachangayikiwana na kummpiga risasi mtu si  bure yupo huko juu anajinywea pombe" Mzee Ole aliongea kisha akatazama makini kule mezani chupa za pombe zikiwa zipo chini karibu na kingo ya sebule hiyo katika eneo ambalo giza ndiyo lilikuwa linaanza, akiwa hata hajatia neno lolote kuhusu zile chupa simu yake ya mkononi iliita ambayo ilimfanya aache kitazama chuo hizo.

                    "Ndiyo kijana sems....pole ya nini kijana mbona sikuelewi...ndiyo sijui chochte kinachoendelea hebu nijuze basi....unasemaa Wilson amekutwa  na polisi akiwa ni mfu!" Aliongea baada ya kuipokea simu hiyo ambayo ilimfanya ashindwe hata kuendela kuishikilia na aliiachia ikaanguka hadi chini ikavunjika.

      Josephine alikuwa amepigwa na mshngao sana aliposikia taarifa hiyo wala hakuwa amewaza juu ya kuwashwa kwa taa hizo ikiwa Wilson tayari kulikuwa na dalili tosha hakuwa amefika ndani ya nyumba hiyo. Alibaki akimtazama tu Mzee Ole ambaye uchungu ulikuwa umembana tayari ingawa machozi yalikuwa hayamtiririki kabisa, alikuwa ameinamisha kichwa chini. Ujasiri wake aliokuwa nao kipindi akiwa jeshini kabla hajaingia uwanja wa siasa ndiyo ulikuwa upo ndani ya moyo wake kwa muda huo ndiyo maana machozi hayakuwa yakimtoka kabisa, alikuwa asikitika kwa huzuni huku uso wake akiwa ameukunja kwa nguvu sana

                  "Aaaargh! Sasa naona ameamua kuikata furaha yangu, Aaaaargh!Norbert!" Mzee Ole aliongea kwa nguvu sana akiwa hajui kuwa huyo anayemuiita yupo hapo kwa umbali mita chache tu.

                 "My name(jina langu)" Norbert aliitika kidharaua na kusaabishwa wote kwa pamoja watazame kule kwenye sebule ya chakula kwa mshngao.



*NGOMA HIYO IPO KWENYEWE

*MZEE OLE NA JOSPEHINE USO KWA USO NA NORBERT KWA MARA NYINGINE

*JE WATATOKA SALAMA AU NORBEET ATATOKA SALAMA?



NI IJUMAA TU PANAPO MAJALIWA NDIYO UTAJUA HAYA KATIKA SIKU AMBAYO TUNAIMALIZA WAKALA WA GIZA USIKOSE KABISA HICHO KITU




No comments:

Post a Comment