RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI!!
Dereva teksi huyu aliongeza mwendo na alipokaribia Tegeta alivua kiatu cha mguu wa kushoto makusudi, hali ya hewa ya humo ndani ilibadilika ghafla ikawa ni harufu ya uvundo mzito iliwa imetawala.
"mmh! Gari yako iko nuka harufu baya baya" Scott aliongea kiswahili kibovu cha kuigiza huku akibana pua kutokana na harufu hiyo.
"Usijali bosi ngoja nikuwekee airfresh kuiondoa hiyo" Dereva aliongea huku akifungua mkebe uliokuwa pembeni yake akatoa chupa ya uturi wa kuweka harufu nzuri katika gari, aliupuliza ule uturi sehemu mbalimbali hadi harufu za uvundo wa viatu ikatoka.
"bosi hapo vipi?" Alimuuliza Scott baada ya kupuliza uturi huo.
"hapo safi kabi.." Scott alijibu lakini alidhindwa kumalizia sentensi yake akajikuta amepitiwa na usingizi mzito wa ghafla.
"Scott umekwisha wewe" Dereva wa teksi aliongea huku akizidi kuongeza mwendo wa gari kuitafuta Mbezi akiiacha Tegeta.