Wednesday, January 11, 2017

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA THELATHINI NA TISA



RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________



SEHEMU YA THELATHINI NA TISA!!



             "Mufti amedondoka kwa mshtuko ofisini kwake na hivi sasa amelazwa Aga Khan"

              "Nilitarajia hilo suala litatokea maana udhaifu wake ndiyo upo mikononi mwetu, sasa mwambie Eva aje nimpe ujumbe aende kule akampe huo ujumbe  ataoukuta akiamka tu"

              "Sawa mkuu"


              "Mwambie aje ofisini sasa hivi leo hii siku ni hakuna kulala"

               " Sawa mkuu"


   
      Norbert alipotoa mari hiyo alikaza mwendo kuelekea ilipo  ofisi ndani ya nyumba hiyo ya kijasusi, Salum alienda moja kwa moja kwenda kumuita Eva kama alivyokuwa ameagizwa na mkuu wake.




______________TIRIRIKA NAYO


         ***KIPANDE CHA MWISHO****

      Taaluma ya  mtu ni kitu kinachomfanya mtu huyo aweze kufanya ufanisi zaidi mambo yanayohusu vitu ambavyo alijifunza kwenye taaluma hiyo, wenye taaluma zao kama vile Daktari hufanya mambo mengi yanayohusu utabibu kwa ufanisi mkubwa kwakuwa ana taaluma nayo kubwa sana. Vivyo hivyo kwa waandishi wa habari hufanya mambo kwa ufanisi na wepesi wa hali ya juu kwa kuwa wana taaluma ya hayo mambo wanayoyafanya, waandishi wa habari huwa na ujuzi wa hali ya juu katika kunyaka habari ambazo zimetoka muda mfupi pasipo kueleweka na watu wa kawaida huwa wanatumia muda gani katika kuzinasa habari hizo na kuzisambaza. Muda ambao Mufti alikuwa akipelekwa hospitalini tangu akutwe amepoteza fahamu katika ofisi yake na mwanamama wa chini yake aliyemtuma amletee nyaraka, habari za kuanguka kwake tayari zilikuwa zimeshafika mikononi mwa wanahabari hata kabla hajfikishwa katika hospitali ya Aga Khan ambako ndiyo alienda kupatiwa matibabu.

   Wanahabari wenye kurasa na tovuti katika mitandao ya kijamii walizinasa habari hizo na kuziweka kwenye kurasa na tovuti zao, hata Mufti akiwa hajaanza kupatiwa huduma katika hospitali ya Aga Khan tangu afikishwe habari hiyo ilikuwa tayari imeshasaambaa mihili ya moto wa nyikani unavyosambaa kwenye nyasi kavu. Wenye tabia ya kusambaza habari mpya kwenye mitandao ya kijamii walikuwa wakisambaziana habari hiyo na hadi muda anaopatiwa matibabu karibu wananchi wote wa Tanzania waliokuwa wakitumia mitandao ya kijamii tayari walikuwa na habari hiyo. Ilikuwa ni habari ya pili iliyochukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari ukiachia ile habari ya hotuba yake aliyoitoa mchana wa siku hiyo, muda huo wa saa tisa alasiri vijiwe mbalimbali vya vjana wanaopenda kukaa pamoja na kupiga soga walikuwa wamekaa wakiizungumzia habari hiyo.

  Moja ya vijiwe vilivyokuwa vikiizungumza habari hiyo kilikuwa ni kijiwe kimoja cha vijana maarufu sana maeneo ya Temeke Mwembeyanga kwenye kiwanja cha mpira kilichopo mita kadhaa kutoka barabara inayoelekea kwenye kona maarufu inayoitwa Davis (Davis Corner) ya Tandika. Vijana hawa muda huo wa alasiri walikuwa wakisubiri jua litulie kidogo na lipunguze ukali wa kuchoma uliokuwa umebakia waweze kucheze mpira kwa muda wa jioni, walikuwa wamekaa kwenye matairi yaliyokuwa yamechimbiwa pembeni ya uwanja huo kila mmoja akiwa ameshika viatu vyake na soksi za kupigia kandanda kwenye mpira huo wa mchangani maarufu kama Ndondo.

     Asilimia kubwa ya vijana walikuwa wamevaa nguo zilizokuwa zikionesha wazi walikuwa wapo hapo kimchezo zaidi, kuwahi kwao katika uwanja huo kulikuwa kumetoa fursa kubwa sana ya kuweza kupiga soga wakisubiri hadi muda wa muadhini wa alasiri na pia swala ya alasiri ipite ndiyo jua liwe limetulia waweze kusakata kabumbu. Walikuwa ni vijana waliokuwa hawajui kile kilichokuwa kikiendelea huko kwenye nyadhifa za juu zaidi ya kuishia kuropoka tu ili kuuepeleka muda mbele, wengi wao walikuwa wakiongea kuhusu  sakata aliloliongea Mufti na pia kuzidiwa kwa Mufti hadi akapoteza fahamu ofisini kwake. Fikra za mawazoni mwao ambazo zilinyakwa barabara na kalamu ya mwandishi ndiyo zilikuwa zikitawala maongezi hayo, wengi wao wlikuwa wakiongea kile kilichokuwa kikiwajia mawazoni mwao ambacho hawakuwa na uhakika nacho hata kidogo.

             "Man umesikia jipu alilolitumbua Mufti na msala uliompata saa moja tu baadaye" Mmoja aliropoka.

             "Dah! Nimeunyaka mwana, huyu Presdaa mafia mwana kamzimisha tayari" Miwngine alidakia

              "Dah! Mama** kumbe kujenga uwanja mpya mkubwa kama wa taifa katika michezo na kutupatia huduma poa kabisa hospital alikuwa anaficha umafia mkubwa sana, jamaa kaumbua tu washamtia janga kalazwa" Miwngine alidakia.

               "Man we acha tu ila mi naona kama kuna uduwanzi fulani pale kwenye hiyo ishu, hatuna uhakika kama ndiyo kamflotisha Mufti hadi yupo kitandani sasa hivi hajitambui" Mwingine alichangia

                "Na wewe acha ukolo kama siyo ukweli unafikiria nini? Au kakupatia mgao nini katika mpango huo na wewe ukaenda kumzima Mufti" Yule kwanza kuchangia alimjia juu huyu aliyekuwa akitetea kuhusu hilo, wengi wao waliokuwa wamelewa maneno ya Mufti alikuwa wakimuunga mkono huyo aliyekuwa akimjia juu mwenzake alipoonesha haungi mkono kauli zao. Ilikuwa kama mzozo baada ya kutoa kauli kila mmoja akimuambia neno lake la kumkashifu.

                 "Nyinyi ndiyo makolo sure, ishu hamuipati fresh mna kazi ya kubwata mam** zenu" Aliyeittetea kauli hiyo aliwajia juu na yeye.

                  "Aaah!  Mwana huyu wa wapi huyu au Prezdaa mjomba wako nini"  Mwingine kabisa alimjia juu.

                  "acheni us****  ma**** kila mkisikia tu ni kweli siasa hizi msiwe mazoba hivyo" Naye hakuwa tayari kushindwa

                   "We kolo unaongea nini wewe" Mmojawapo ambaye alikuwa akionesha zaidi alikuwa ni kijana mwenye shari zaidi alimsukuma huyo jamaa kifuani kumrudisha nyuma baada ya kuona alikuwa wametukanwa wote.

                    "Hazard mvungie huyo hana jipya kama wa haramu vile" Mwingine alikimbilia kumzuia huyo kijana aliyekuwa yupo kishari zaidi huku akimuita jina kutokana na uchezaji wake wa uwanjani, hii huwa ni kawaida sana kwa vijana wa mtaani kupeana  majina ya wachezaji wakubwa wa Ulaya kutokana na uchezaji wa mwenzao ulivyo.

                     "Huniambiaa kitu we boya" Yule aliyekuwa yupo katika kutoamini maneno ya wenzake na pia kutoamini hotuba ya Mufti aliongea huku akimrudishia mwenzake katika kumsukuma kama alivyomfanyia.

                     "Pepe vunga na wewe basi kama unamtetea huyo Cho** Zuber juu yako" Kijana aliyekuwa akiamua ugomvi huo wa kusukumana kwa huyo Pepe na Hazard alimjia juu huyo waliyempachika jina la pepe kutokana na uwezo wake wa uwanjani.

                     "Roja na wewe acha ufala" Pepe alimjia juu huyo aliyekuwa anawaamulia

                     "Oyaa  Pepe tutakutimba ujue tutolee us****  wako" Hazard naye alimjibisha Pepe huku akimsukuma Roja apishe ili waweze kuwekana sawa, Roja alikaza mwili wake akizuia Hazrd asimsogelee Pepe.

                     "Oyaa Pepe na Hazard vungeni basi ama nini wamoja hapa tunasongeza saa tu hapa kupiga stori ishu za kupigana siyo kabisa" Roja aliamua kuwatuliza wote.

                      "haina mbaya mtu wangu" Pepe aliongea huku akimnyooshea ngumi kwa mtindo unaojulikana kama tano Roja ambaye naye alimpa tano, alimfuata pia Hazard akafanya hivyohivyo kisha wakagongesha bega kila mmoja kama ilivyo salamu ya vijana waliopoteana kwa muda mrefu sana.

                      "Pendo moja ama nini" Hazard naye alikuwa amerudi katika hali ya kawaida alipokuwa akiongea maneno hayo wakiwa wanaonesha ishara ya amani ipo katika  urafiki wao na hakuna chochote kilichokuwa kimeharibika kwa kuzozana kwao.

   Haikuwa jambo geni sana kwa vijana wa mtaani kuzozana kuhusu masuala kama hayo au ushabiki wa mpira pamoja na ushabiki wa wasanii wa kizazi kipya, walikuwa wakifikia hata hatua ya kukunjana mashati na hata kuzuka mzozo kama walikuwa ni mahasimu waliokkuwa wakiwindana kwa muda mrefu. Mzozo huo waliokuwa wanawekeana huweza kuisha hata ndani ya dakika tu tangu utokee na hata vijana waliokuwa wakigombana wakawa kama hawakuwa na mzozo, ugomvi wa aina hii ulikuwa ukijulikana kama ugomvi wa kisela kwani wahusika wake hawakuwa na visirani baada ya mzozo huo kuisha. Urafiki baina yao hurejea palepale ugomvi unapoisha, kwa mtu ambaye atawakuta vijana wa aina hii wakiwa wameacha kugombana na wakiongea masuala mengine ya mtaani basi anaweza kusema kuwa hakukuwa na ugomvi baina yao.  Mtu asiyezoea ugomzi wa aina hii wa vijana wa mitaani akiwa wanagombana basi anaweza kusema vijana hao wamerukwa na akili baada ya kupatana, pia anaweza kutokwa na kicheko kabisa akiwaona baada ya kutokea kwa ugomvi huo.

****

   Adhana ya alasiri ilipokuwa ikitolewa kikao cha ghafla kilikuwa kimeitishwa ndani ya kambi ya kina Wilson, wachache waliokuwa wamebakia kabla Norbert hajapitisha fagio la chuma katika kuwafagia ndiyo walikuwa wakihudhuria kikao hicho cha muda mfupi baada ya taarifa ya  kupoteza fahamu kwa Mufti kuwafikia.  Wilson, Mzee Ole,Josephine na L.J Ibrahim ndiyo walikuwa wahudhuriaji wa kikao hicho cha ghafla walichokuwa wamerkiitisha muda huo wa saakumi kasoro alasiri. Ingawa yalikuwa yamebaki masaa machache kuanza kwa mapinduzi bado walikuwa na wasiwasi kwa kutoonekana kwa wenzao ambao walikuwa pamoja kikazi tangu wanaanza harakati hizo, kutokuwepo kwa Kamishna Wilfred na Thomas ni jambo ambalo lilikuwa likiwaumiza kichwa kwa muda mrefu sana wasijue walikuwa eneo gani hadi muda huo.

     Simu zao zote hazikuwa hewani na hata taarifa juu ya eneo walilokuwepo walikuwa hawana, walikuwa wamechanganywa sana na suala hilo ingawa hawakuwa wamekata tamaa kabusa juu ya suala hilo. Hawakuwa wakijua kabisa fagio la chuma lile lililokuwa limefagia utawala mbovu wa Mzee Ole miaka kadhaa iliyopita ndiyo lilikuwa limefagia watu hao waliokuwa wakiwatafuta ambapo moja tu ndiyo alikuwa anapumua kati yao wawili hao waliopitiwa na fagio la chuma, walikuwa wakiumiza kichwa zaidi kwa kutoonekana kwa wenzao muhimu waliohitajika kwa siku hiyo muda wa usiku katika kuhakikisha utawala wa Rais Zuber ulikuwa unaondolewa.

                 "Jamani kuna anayejua Thomas na Kamishna walipo au kuna mwenye taarifa yao  nyingine?" Mzee Ole Aliuliza huku akiwatazama wenzake usoni,  kimya kilipita pasipo swali hilo kujibiwa. Kila mmoja alikuwa akimtazama mwenzake usoni akitegemea anaweza kutoa jibu la swali hilo, hakuna hata mmoja aliyenyanyua mdomo wake kujibu swai hilo kuweza kuwaridhisha aua kuwapa ahueni katika mioyo yao juu ya kutoonekana kwa watu muhimu sana ambao walikuwa ni sehemu ya mpnago wao uweze kutimia.

                 "Kama hamna basi kuna tatizo haiwezekani kabisa watu hawa wasiwepo hap bila kuwepo taarifa yeyote ile, mke wa Kamishna anadai mume wake hajaonekana nyumbani kwake tangu usiku  alipotoka. Asubuhi ya leo nayo Thomas tangu alipotoka hajaonekana, jamani sasa wasipoonekana hawa tutakaa tulitegmee jeshi tu" Mzee Ole aliongea kwa mara nyingine, kimya kilichukua nafasi na hakuna mwingine aliyekuwa akiongea baada ya maelezo hayo.

   Zilipita daika takribani mbili na hakuongea mtu yoyote kutokana na kutokuwa na taarifa ya uhakika juu ya jambo hilo, wakiwa wapo ndani ya kimya hicho simu ya Mzee Ole iliita. Wote kwa pamoja waligeuza macho kwa mzee Ole baada ya kusikia mlio huo wa simu yake na akapokea, wenzake wote walikaa kimya kumpa nafasi nzuri Mzee Ole aongee na simu hiyo.

                 "Ndiyo kijana........Yes  nimepata taarifa za kulipuka kwa hoteli ya Enot.......Oooooh! Shit!....sawa sawa nitumie kwa Whatsapp niione" Mzee Ole alipomaliza kuongea na simu hiyo tayari alikuwa ameshachoka bila kazi ngumu yenye kumchosha kumfanya achoke, aliwatazama wenzake ambao walikuwa wakimtazama kwa shauku sana kujua kile alichokuwa amekipata kutoka kwa mtu aliyekuwa amempigia simu.
                 "Kaka vipi kuna nini?" Wilson aliuliza

                 "Ole vipi kuna tatizo" L.J Ibrahima naye aliuliza.

                 "jamani mambo ni mabaya kabisa" Mzee Ole alianza kuongea kwa taratibu kisha akawatazama wenzake katika nyuso zao na akaendelea "Mlipuko uliotokea katika hoteli ya hapo mbele nadhani mmeusikia kwa siku ya leo, sasa kwa taarifa za kusikitisha ni kwamba  mwili uliokutwa mule ndani umeungua hadi hautambuliki ni wa mwenzetu. Thomas ndiye huyo aliyeungua hadi hatambuliki".

                  "Ohhh! No! Imekuwa vipi hapo?" Wilson aliuliza akisimama wima kutokana na kupagawa na taarifa aliyokuwa amepewa na kaka yake.

                   "Wilson mdogo wangu tulia basi basi sijamaliza, kabla ya tukio kamera za ulinzi za hoteli hiyo zilimuona Thomas akiingia eneo la mapokezi katika hoteli hiyo na alitaja chumba ambacho kulikuwa na mwanamke na mwanaume ambao waliokuwa wameingia. Watu hao waliokuwa wametangulia kabla yake walikuwa wakisubiria ujio wake wake, alipoingia yeye ndiyo kamera hizo zikamnasa kwani hakukuwa na mwingine yoyote aliyeingia ndani ya chumba hicho baada ya watu hao" Mzee Ole alimtuliza mdogo wake kisha akaendelea kuongea  kuwaeleza wenzake kuhusu taarifa ile, maelezo yake hayo yalikuwa ni yenye kuhuzunisha kwa kila mmoja na pia yalikuwa ni yenye kushtua kwa moyo wa Josephine kwani alihisi alikuwa  akikaribia kugundulika kuwa yeye ndiye aliyemkamatisha Thoams na yeye ndiye alikuwa amepita hapo mapokezi na pia ni yeye ndiye alikuwa yupo ndani ya chumba hicho.

    Wakati wakiwa wanaendelea kuumia na habari hiyo simu ya Mzee Ole ilitoa mlio wa kuingia ujumbe mfupi wa maneno, Mzee Ole aliichukua simu yake hiyo kwa haraka  sana na akaufungua ujumbe huo uliouwa umeingia ndani ya simu yake kwa muda huo. Wote walikuiwa wameinamisha vichwa vyao kasoro Josephie ambaye alikuwa akimtazama Mzee Ole kwa macho ya huzuni ingawa moyoni alikuwa na hofu kubwa sana.

    Uso wa mzee Ole ulikuwa amkini sana katika kukitazama kioo cha simu ambapo sauti ya Thomas akiulizia kuhusu chumba ambacho alikuwa ameambiwa aingie ilisikika, wote walipoisikia sauti hiyo walitulia kimya wakimtazama Mze Ole ambaye alikuwa makini akitazama kioo chake. Alikuwa akiangalia video ambayo ilikuwa ipo simu yake hadi ilipoisha ndipo na yeye akmpa simu L.J Ibrahim ambaye aliangalia video hiyo na alipoimaliza akampa simu Wilson. Naye aliiangalia video hiyo hadi ilipoisha akampatia simu Josephine, alipoipokea simu hiyo na kuiangalia video ambayo walikuwa wakiiangalia wenzake moyo wake ulipiga kwa nguvu ingawa alifanikiwa kuuficha huo mshtuko wa moyo wake kwa. Alimuona Thomas akiwa eneo la mapokezi na akijitambulisha kuwa alikuwa na mgeni wake katika chumba cha hoteli hiyo, video hiyo iliishia pale Thomas alipokuwa ameelekezwa mahali chumba hiko kilipo na akawa anapanda ngazi kwa kasi aweze kuwahi huko juu akiwa na hisia kali juu ya Josephine. Video hiyo ilimfanya Josephine awe na mashaka zaidi akihisi kuna jingine linaweza kuzuka kwake kwa muda huio, alirudisha simu mikononi mwa MZee Ole kisha akaenda kuketi kwenye kochi akiwa amenyamza kimya tu.

                  "Damn! Huyu ni Norbeert tu hakuna mwingine na huyuhuyu ndiye aliyefanya Mufti awe hospitali" Wilson aliongea kwa hasira sana.

                  "Wilson cool down brother, ishu ya Mufti labda ni mshtuko tu wa kawaida usimuhisi Norbert. Kikubwa amemaliza kazi yake na mpango unaelekea kufanikiwa" Mzee Ole aliongea kumuambia mdogo wake kisha akawatazama wenzake waliobakia na kusema "jamani tunazidi kuteketea kwa uwepo wa mtu huyu anayeitwa Norbert, Thomas ni tayari na bado anatuwinda sasa inabidi tuwe makini na sisi tumuwinde pia kwa usiku huu wa leo. General muda wako wa kwenda kuhakikisha kikosi kinamuondoa Zuber ndiyo huu, Josephine na Wilson mnatakiwa muende Aga Khan jioni ya leo mkachunguze kipi kilichomfanya Mufti awe na mshtuko hadi akawa vile. Ikiwa ni mpango wa Norbert wa kumfanya atoe siri mummalize upesi kabla hajafungua kinywa chake katika kuyaongea mambo yetu, muda wa kazi sasa hatutakubali kushindwa hadi Zuber atoke Ikulu afungwe".

                   "Sawa kaka, Josephine twende" Wilson aliongea hukua kiwa tayari ameshasimama.

                    "Kanuni moja tu  katika kummaliza  kama ni msaliti, matumizi ya silaha ni marufuku tumeelewana?! Na kama mkitumie muweke viwambo vya kuzuia sauti" Mzee Ole aliwaambia

                    "Tumekuelewa" Wote kwa pmoja waliitikia kisha wakaondoak eneo hilo wakimuacha MZee Ole na L.J Ibrahim wakiwa wamebakia

****

   Majira ya saa kumi na moja jioni Mufti alizinduka tangu alipoanguka kwa mshtuko akiwa ofisini kwake, alijikuta yupo kwenye mazingira tofauti na aliyokuwa hapo awali na wala hakuwa ameelewa alikuwa amefika vipi kwenye mazingira hayo. Kumbukumbu hazikuwa zimekaa sawa alipozinduka na wala hakuwa ametambua kwa haraka kipi kilichokuwa kimempata, kitu  cha kwanza alichokifanya baada ya tu ya kufungua macho ilikuwa kuangaza pande zote. Hapo alijitambua alikuwa yupo ndani ya chumba cha wodi  kutokana na mandhari ya chumba hicho kujionesha wazi, mita kadhaa kutoka hapo alipolazwa alimuona muuguzi wa kiume akiwa ametulia kwenye kiti akimtazama kwa umakini hasa baada ya kubaini kuwa alikuwa tayari ameshaamka. Ilikuwa ni habari njema sana Mufti kuamka na ilimbidi Muuguzi huyo atimue mbio kwenda kwa daktari kutoa taarifa ya kuamka kwa Mufti, Muuguzi huyo alikuwa akisubiria kwa hamu sana kuamka kwake na alipoona alikuwa amefumbua macho alinyanyuka haraka na akatoka ndani ya wodi hiyo aende kutoa taarifa kwa Daktari aliyekuwa akimtibu Mufti tangu alipofika hapo hospitali akiwa hajitambui.

   Muuguzi huyo alipokuwa amemuacha Mufti peke yake ndipo kumbukumbu ya kile kilichokuwa kimemtokea hadi akapoteza fahamu kilimrudia katika kichwa chake, huzuni ndiyo iliyofuata katika kuutawala moyo wake baada ya kukumbuka kitu hicho kilichokuwa kimemfanya apoteze fahamu hadi muda huo anarudiwa nazo. Moyo ulimuuma sana na alitamani hata atafute njia aweze kuiokoa familia yake, njia hiyo hakuwa nayo na waliposhikiliwa hakuwa anapatambua hata kidogo. Akiwa bado anafikira kuhusu hilo suala  mlango wa wodi aliyopo ulifunguliwa taratibu ambao ulimfanya Mufti aelekeze macho yake moja kwa moja mlnaogoni, alimuona Muuguzi wa kike akiingia huku akiwa amebeba ua kubwa sana la plastiki lenye kadi katikati yake. Mhudumu akiwa amejifunmga shungi safi alimsogelea Mufti hadi karibu yake na akamsabahi kisha akampatia kadi hiyo  pamoja na maua.

    Muuguzi huyo hakuongea jambo jingine alitoka wodini humo haraka sana, Mufti alibaki akiyatazama hayo maua aliyopewa. Kadi iliyopo ndani ya maua hayo ilikuwa ni yenye kumtakia afya njema, aliifungua kadi hiyo akiwa na tabasamu hafifu sana katika uso wake akijua alikuwa amejuliwa hali na mmoja wa washirika wake. Ndani ya kadi hiyo alikutana na kikaratasi kilichobandikwa ambacho kilikuwa kimeandikwa kwa mwandiko wa kalamu ya mkono wala si kwa kuchapwa kama yalivyokuwa maandishi mengine yaliyopo kwenye kadi hiyo, kikaratasi hicho kilimfanya Mufti aifunge kadi na akakichukua pekee ambacho kilikuwa na maneno machache sana ambayo yalijionesha dhahiri yalikuwa na maana kubwa sana.

         'Mpango ni uleule Mufti, fuata maelekezo yangu familia yako itakuwa salama. Hivi sasa unatakiwa uite mkutano wa waandishi wa habari kisha ukiri umesambaza uzushi dhidi ya Rias Zuber na uliyoyaongea hayana ukweli wowote. Isifike saa nne usiku leo huo ujumbe uwe tayari umeshafika kwa watanzania wote tena uwataje na washirika wako wote, ukimaliza hayo familia yako itakuwa salama na ukikaidi utajuta
N001'


    Mufti alipomaliza kuusoma ujumbe huo tayari kijasho kilikuwa kikimtoka, hakuwa na ujanja mwingine na alitambua wazi ujumbe ulikuwa unatoka kwa N001. Aliweka mikono kwenye kichwa chake akijifikiria kuhusu suala hilo na alipoitoa alimkumbuka yule binti aliyekuwa amemletea ujumbe huo ambaye tayari alikuwa ameshatoweka, akili za Mufti zilimpa hisia kwamba huyo binti ndiye mbaya wake mwenyewe aliyekuwa akimtafuta na pia ndiye aliyekuwa ameshikilia familia yake.

                "We binti weee!" Mufti alipayuka huku akitoka kitandani na lakini uwepo wa dripu ulimzuia asifike mbali kwani sindano aliyochomwa ilianza kumletea maumivu. mkononi, aliishikilia kwa haraka sindano hiyo ili aweze kuitoa lakini kabla hajaitoa mlango wa wodi hiyo ulifunguliwa. Mufti alipeleka jicho mlangoni akamuona yule Muuguzi wa kiume akirejea akiwa pamoja na Daktari, aliwapuuzia na aliendelea kuitoa ile sindano jambo lililowafanya wamkimbilie hadi pale kitandani na kumshika mikono yote kwa nguvu.

                 "Niacheni mie nikamfuate huyu mshenzi!" Alifoka  kwa nguvu akiwa hafurukuti kwa jinsi alivyoshikiliwa kwa nguvu, Daktari na muuguzi huyo waliendelea kumshikilia Mufti kwa nguvu sana hadi alipotulia mwenyewe na kuacha kufanya fujo. Hapo walimuachia na wakabaki wakimtazama kwani machozi tayari yalikuwa yameshachukua nafasi yake machoni mwake, Mufti alianza kulia kwa muda mrefu kimyakimya na alipoacha kulia alimtazama Daktari aliyekuwa amekuja.

                  "Nahitaji kuongea na waandishi wa habari muda huu huu" Alimuambia Daktari huyo ambaye alikuwa akifahamiana naye sana na alikuwa ni Daktari ambaye ni rafiki yake mkubwa sana, Daktari huyo aliposikia kauli yake hiyo alimkubalia kwa kutikisa kichwa huku akimtazama Mufti kwa tabasamu hafifu.

*USIKOSE IJAYO

TUKUTANE SEHEMU YA AROBAINI KUJUA KILE KINACHOJIRI NDANI YA WAKALA WA GIZA





No comments:

Post a Comment