RIWAYA: WAKALA WA GIZA
MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA
SIMU: +255713776843
+255762219759
WHATSAPP: +255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA
______________+18__________________
SEHEMU YA THELATHINI NA NNE!!
Usoni alikuwa amevaa miwani nyeusi ya jua ambayo ilimfanya azidi kupendeza, M.J Belinda aliposhuka tu alitazama upande ule waliokuwa wapo waandshi wa habari akiwa amesimamamtindo am,bao uliplekea kamera zao zifanye kazi ya kupiga picha tu. Waandishi wa habari wengine walikuwa wakiweka vipaza sauti vyao mbele wakiuliza maswali ambayo hayakujibiwa na M.J Belinda
zaidi ya kuwatzama tu kisha akapiga hatua kuelekea ndani ya hema la kikosi cha ardhi.MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA
SIMU: +255713776843
+255762219759
WHATSAPP: +255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA
______________+18__________________
SEHEMU YA THELATHINI NA NNE!!
Usoni alikuwa amevaa miwani nyeusi ya jua ambayo ilimfanya azidi kupendeza, M.J Belinda aliposhuka tu alitazama upande ule waliokuwa wapo waandshi wa habari akiwa amesimamamtindo am,bao uliplekea kamera zao zifanye kazi ya kupiga picha tu. Waandishi wa habari wengine walikuwa wakiweka vipaza sauti vyao mbele wakiuliza maswali ambayo hayakujibiwa na M.J Belinda
_______
_______________TIRIRIKA NAYO
_________
Kiatu alichovaa na kijeshi na jinsi miondoke yake ya kike aliyokuwa anaitumia, ilimfanya aonekane kivutio kikubwa kwa jinsi anavyotembea kulekea humo ndani ya hema walipo vijana wake. Kizingatio cha umbo matata, mwili uliojaa hasa mapajani bado alionekana ni mlimbwende ingawa alikuwa amevaa nguo hizo ambazo zikionekana na raia wa kawaida huzihofu sana. Balaa alilo nalo katika mapigano ya ana kwa ana halikuonekana kabisa kutokana na urembo wake aliokuwa nao ingawa alikuwa akifanya mazoezi sana. Muonekano wake huo kwa nyuma wakati akikaza mwendo akiwa amewapa mgongo waandishi ulitosha kabisa kufuta mawazo potofu juu ya mwanamke kujiunga na jeshi, wote waandishi wa habari nao walithibitisha juu ya hilo.
Dhana ambayo ambayo ilikuwa imejengeka juu ya wanawake kukomaaa na kuharibika urembo wao wakijiunga na jeshi, M.J Belinda alikuwa ameifuta kabisa kutokana na muonekano huo ambao ulichukuliwa na kamera mbalimbali za waandishi wa habari pindi alipokuwa akielekea ndani ya hema ambalo wamo vijana wake wa kazi wakichakarika. Hadi anafikia kwenye kizngiti cha hema hilo bado waandishi wa habari waliendelea kummulika na kamera zao, kamera hizo M.J Belinda hakuzijali hata kidogo yeye alisogeza kitambaa kigumu chenye asili ya turubai kilichomo katika kizingiti cha hema hilo na kuingia ndani.
Alipoingia tu dani ya hema hilo alikutana saluti ya ukakamavu kutoka kutoka kwa Meja Kibona ambaye alikuwa tayari ameshatambua ujio wake katika eneo hilo pamoja na wanajeshi wote, M.J Belinda naye aliiijibu saluti hiyo kisha akavua miwani ya jua aliyovaa akaanza kuyasanifu mazingira ya humo ndani ya hema. Alitingisha kichwa kuafikiana na hali aliyoikuta humo ndani ya hema kisha akaketi kwenye kiti kilichokuwa kipo nyuma ya wanajeshi ambao walikuwa wakichakarika na tarakilishi zilizokuwa zikchukua mazingira yote ya ikulu.
"Kuna jipya lolote?" Aliuliza akiwa anatazama mazingira ya humo ndani
"jipya lililokuwepo ni taarifa ya kujiandaa na mashambulizi kutoka kwa mkuu Mugiso ambaye amesema nijiandae kutishia amani ya wote wa ikulu ikifika majira saa sita leo" Meja Kibona aliongea.
"Ok sasa nyinyi si mnatambua mpo operesheni tofauti na wao, sasa basi akitoa amri hiyo tu mimi nitatoa amri yangu kazi ianze tunaelewana?!" M.J Belinda aliongea aliongea
"Mkuu!" Meja Kibona aliitika huku akikakamaa kijeshi.
"Vizuri! Nahitaji uongoze njia nikaangalie vijana na silaha zao wamejipanga vipi, hapa muache msaidizi wake atakuwa akikupa taarifa kupitia kinasa sauti maalum juu ya kitakachotokea humu uweze kutoa uamuzi" M.J Belinda aliongea
"Mkuu" Meja Kibona aliitikia
"Tena radio calls zisitumike kwenye mission hii kuanzia hivi sasa tukitoka huko kukagua vikosi hakikisha viongozi wote wa vikosi vilivyopo hapa wapewe vinasa sauti muweze kusikiana, radio call zitasababisha mipngo yetu ikanaswa. Tunaweza tukanda" M.J Belinda alimuonya juu ya utumiaji wa simu za upepo ambazo ni rahisi sana kuingiliana mawasiliano na wanajeshi wa kikosi cha majini na kupelekea mpango wao uvuje kabla haujatimia, baada ya maelezo alimuambia amuongoze hadi alipovipanga vikosi vyote vilivyoingia hapo kwa platoom. Platoom ni sehemu moja kati ya sehemu tatu ya kombania ya kijeshi, sehemu hii ya kijeshi huundwa na section tatu zenye askari ishrini na saba kila moja na kuifanya platoom moja kuwa askari themanini na moja . Section nayo huwa na ashuundwa na unit tatu , unit hizi huwa na askari tisa kila moja na kuifanya section moja kuwa na askari ishirini na saba. Kombania nzima ya kijeshi huwa na askari wapatao mia na themanini na zaidi, huu ndiyo mnpagilio wa vikosi vye jeshi ambavyo hutumiwa wakiwa wapo vitani.
Meja Kibona alitoka nje ya hema hilo akasimama ambapo wanajeshi waliokuwa wapo hapo nje walitoa heshima kwake kutokana na yeye kuwa ndiyo mkubwa pekee baada ya M.J Belinda, kamera za waandishi wa habari nazo hazikuacha kufanya kazi yake baada ya kujitokeza kwake. M.j Belinda alifuatia kutoka na safari hii yale macho yake malegevu yaliyokuwa yamefichwa na miwani ya giza mbele ya kamera za waandishi wa habari yalionekana dhahiri, waandishi wa habari walimpiga picha nyingi zaidi akiwa hawatilii maanani hata kidogo zaidi ya kutilia maanani heshima anazopewa na wanajeshi wake. M.J Belinda alianza kutembea akiwa sambamba na Meja Kibona huku nyuma yao kukiwa na mwanajeshi wa kike mwenye nyota mbili mabegani kwake yaani Luteni, walitembea huku wakifuatwa na waandishi wahabari kwa nyuma ambao hawakuweza kuweza kuwasogelea kutokana na kuonywa vikali sana na wanajeshi.
****
Maji ra hayahaya ambayo M.J Belinda alikuwa akienda kutazama vikosi vyake ambavyo vilikuwa vimeizunguka ikulu, Thomas alikuwa yupo ndani ya mitaa ya Msasani akiwa ametoka kwenye eneo maalum ya kufanya mazoezi(gym). Alikuwa akikimbia mwendo mdogo ndani ya siku hiyo ili aweze kujiandaa vizuri katika kuikabili siku hiyo ngumu sana ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kazi ambayo iliyokuwa imemleta nchini Tanzania. Akiwa anaendelea kukimbia na kurudi kwenye ngome yao njiani alikutana na mtu ambaye alimziba njia kwa ghfla na kupelekea asimame, mtu huyo alikuwa ni kijana muuza magazeti ambaye alimpatia Thomas bahasha pasipo kusema chochote kile kisha akapita na kuendelea na safari yake lakini Thomas alimshika mkono kwa nguvu sana. Mtu huyo alisimama akiwa amepiga hatua mbili tu baada ya kudakwa mkono kwa nguvu na Thomas, mkono wake huo uliminywa kwa nguvu sana na kupelekea ajisikie maumivu hadi akawa anajaribu kujinasua lakini hakuweza. Mikono ya Thomas ilikuwa ni imara sana na yenye nguvu kushinda mikono ya huyo mtu.
"Kakupa nani hii bahasha uje kunipa?" Thomas aliuliza kwa kiswahili fasaha zaidi na kuzidi kumshangaza huyo ambaye ni muuza magazeti.
"Kanipa mdada mmoja yupo pale mbele" Alijibu mtu huyo hukua akifumba macho kwa maumivu baada ya kubwa kwa nguvu mkono wake, alinyooosha kidole upande aliokuwa anatoka lakini hakuwa ameonesha kitu kwani hakukuwa na mtu yoyote upande huo wa aliokuwa akiunyooshea mkono. Mtu huyo alikuwa akiunyooshea mkono upande ambao kulikuwa kuna mgahwa mkubwa sana hapo maeneo ya msasani, Thomas alizidi kumbana zaidi kijana huyo baada ya kutoona mtu mbele yake.
"Mbona hamna mtu pale?" Alimuuliza kwa sauti ya chini huku akimkazia macho.
"Brooo si usifungue kwanza hiyo bahasha uangalie kama nimetuma kitu siyo kuniumiza hivyo" Mtu alilalamika na kupelekea Thomas aifungue bahasha hiyo na kukutana na karatasi ndani ambayo aliitoa kisha akaanza kuisoma.
Ndani ya nyumba ile kuna mitambo maalum ambayo ingeweza kutukuta ikiwa ningekubali kile ulichotaka kukifanya Thomas si kwamba nilikuwa sitaki bali tungeleta matatizo isitoshe wenzetu wamekufa jana tu. Napenda utambue hata mimi nakupenda sana Thomas na hakuna msichana asiyetaka kuwa na mwanaume mzuri kama wewe, nimetoka mapema kwenye ngome si kwamba nilikuwa naenda kununua dawa kwamba kichwa kilikuwa kinaniuma sehemu niliyopigwa na kitako cha bali nilikuwa naenda kutafuta mahala tuweze kuongea na wewe ukitoka huko gym. Hatimaye nimepapata mpenzi nakusubiri kwa hamu sana my dear nipo Enot hotel chumba namba 130. Nakusubiri kwa hamu sana laazizi naomba ufanye haraka sana, nimempa hii karatasi huyo muuza magazeti na mimi nimetangulia chumbani
Akupendaye
Josephine'
Thomas alipomaliza kusoma barua hiyo aijikuta akitabasamu mwenyewe kisha akamuachia mkono yule mtu ambaye aliamini alikuwa ni muuza magazeti, alimtazama huku akitabsamu baada ya kumuachia ilia muondoe hofu yule muuza magazeti kwa kitendo ambacho alikuwa amemfanyia.
"samahani mtu wangu" Thomas alimuambia huku akitabasamu na akili yote ilikuwa ipo kwa Josephine hasa baada ya kumaliza kuisoma barua hiyo.
"usijali broo najua town hatuaminani ndiyo maana ukanikamata hivyo" Mtu huyo aliongea kwa taratibu huku akiishika sehemu aliyokuwa amekamatwa kwa nguvu na Thomas akijichua kwa taratibu.
Thomas baada ya kujiona amefanya kosa kwa huyo mtu aliingiza mkono mfukoni akatoa noti mbili za shilingi elfu kumi ambazo alimpatia kisha akaanza kukimbia kwa taratibu akielekea kwenye eneo ambalo alikuwa ameelekezwa kwa mujibu wa ujumbe huo uliokuwa umekuja kwa njia ya maandishi. Akiwa njiani kumbukumbu za usiku uliyopita masaa machache baada ya Kamishna Wilfred kuondoka na wenzake wote kuingia ndani ya vyumba vyao ndiyo zilimjia, usiku huo alikuwa amepanda juu ya ghorofa akiwa na chupa ya pomba kupitisha saa kadhaa kabla hajaenda kupumzika kwa ajili ya siku hiyo. Baada ya kukaa juu kwa takribani saa moja alirudi chini ili aende chumbani kwake kupumzika na ndiyo hapo alipomshuhudia Josephine akiwa yupo ndani ya kibukta kilaini sana ambacho kilikuwa kimemkaa sawasawa katika mwili wake hadi nguo ya ndani ikiwa inaonekana na kulifanya umbo lake tata lizidi utata. Juu Josephine alikuwa amevaa kiblauzi kidogo sana kilichokuwa kimeacha sehemu kubwa sana ya mgongo wake apmoja na kifua chake, alikuwa ameinama kwenye jokofu refu sana lilokuwa lipo sehemu ya kulia chakula pembeni ya sebule.
Ngazi za kushukia chini kutoka kwenye kibaraza cha juu kabisa ya nyumba hiyo chenye viti ambapo ndiyo Thomas alikuwa amekaa,ilikuwa zipo katika sehemu hiyo ya kulia chakula kwa pembeni ambapo kulikuwa kunatazamana s na friji hilo. Thomas alizidi kukumbuka jinsi maungo yao ya katikati ya miguu yake yalipoumuka na kisha dalili za kuja kwa hisia kali zilipomijia baada ya kumuona Josephine ambaye alikuwa hana habari akiwa ameinama akitafuta vinywaji sehemu ya chini ya friji hilo. Tamaa yake kila alipokuwa akimuona Josephine ndani ya nyumba hiyo zilidi kiwango zaidi hasa baada ya kumuona akiwa akiwa yupo ndani ya mavazi hayo, uzalendo ulimshinda Thomas ndani ya muda huo na akajikuta akimsogelea Josephine akitembea kwa taratibu sana ilia siweze kumsikia. Alinyata zaidi hadi alipofikia meza ya chakula ambayo ilikuwa ipo karibu sana na friji ambapo aliweka chupa ya pombe kwa utaribu sana, Josephine muda huo hukuwa na habari kabisa na uwepo wa Thomas eneo hilo. Thomas akiwa bado yupo akikimbia mchakamchaka alizidi kukumbuka jinsi alivyofanikiwa kufika nyuma ya Josephine na kusikilizia kwa sekunde kadha kisha akaipeleka mikono yake akagusa kiuno kilaini cha Josephine ambacho kilikuwa kinaonekana kipana zaidi kutokana na kuwa ameinama. Josephine aliinuka haraka sana baada ya kushikwa hivyo na kupeleka mkono mmoja wa Thomas uhame kutoka kiunoni na kutua kwenye kifua chake kichanga kilichokuwa kipo ndani ya blauzi hiyo tu, mkono mwingine wa Thomas ulikuwa umeng'ang'qnia kiuno chake huku ukilazimisha kuingia ndani ya blauzi hiyo.
Kila alipofikiria hicho kitu akiwa ndiyo yupo mita kadhaa kuikairibia hoteli hiyo maungo nayo yaliinuka ila kwa msaada wa nguo ya mpira aliyokuwa amevaa iliweza kumsaidia asiweze kuadhirika kwa watu waliokuwa waliopo njiani, bado mawazo ya kile kilichokuwa kikitokea jana usiku ambapo Josephine alichukia kiliendelea kurudi kwenye kichwa chake. Alikumbuka vizuri alivyokuwa akilazimisha kuuupapasa mwili wa Josephine kutokana na papara zilizokuwa zimeuvaa ghfla mwili wake, mkono wake aliokuwa akiulazimisha kuuingiza kwenye blauzi ya Josephine aliuhamishia haraka na kuupeleka chini ambapo mrembo huyo alikuwa amevaa kaptula laini tu pamoja na kifuniko cha mlango wake. Thomas alikumbuka jinsi alivyofanya haraka zaidi kwa kuupitiasha mkono huo kwenye mpira kifuniko hiko, alipokuwa akiyakumbuka hayo tayari alikuwa ameshakaribia lango la kuingia hoteli hiyo aliyokuwa ameelekezewa kwa mujibu wa barua ya Josephine.
Alizidi kuongeza mwendo wake akiwa na hamu kubwa sana ya kumfikia Josephine huku kumbukumbu za kile kilichotokea usiku uliopita zikimrudia, alikumbuka jinsi mkono wake ulivyokuwa na papara sana hasa ulipoingia kwenye kifuniko kilichoziba maungo ya Josephine na kukutana hali ya bustani ndogo sana yenye dalili zote za kufyekwa. Thomas alipokumbuka hapo hisia kali zilipanda zaidi katika mwili wake, alikumbuka tena Josephine alivyoshtuka baada ya mkono wake kufika juu ya malango wake usio na komea zaidi ya pazia la mpira tu ambapo ungeingia ndaye pua hadi akamuachia Josephine ambaye alimsonya na kuondoka hapo kwenye friji kwa kasi hata kinywaji alichokuwa akikitafuta miongoni mwa vinywaji vingi usiku huo akawa hana hamu nacho tena.
Thomas alipokumbuka hilo tayari alikuwa ameshafika kwenye mlango wa kuingia katika hni yangekua mengine. Thomas alipofikia Josephine aliachia kichwa kichwa kikali kilichompata kwenoteli ya Enot ambayo ni maarufu sana hapo Msasani, alijikuta akitabasamu mwenyewe alipokumbuka jinsi alivyopigwa kichwa na Josphine ambacho kilimuachia maumivu pasipo kumletea athari nyingine.
"Wanawake bwana fujo zote zile kumbe yupo katika sight" Thomas alijisemea kwa taratibu muda huo akiwa anafungua mlango wa kuingia mapokezi, aliingia mapokezi ambapo alifika kwenye dawati la wahudumu wa hoteli hiyo na akaulizia juu ya chumba hicho alichokuwa ameelekezwa.
Aliruhusiwa moja kwa moja na kupelekwa kwenye chumba hicho alichokuwa ameelekzwa baada ya wahudumu wa hapo kuwa na taarifa ya ujio wake. Thomas alipotoka tu hapo mapokezi alipanda ngazi moja kwa moja kuelekea juu akiona lifti ilikuwa ikimchelewesdha kufika hicho chumba namba 130, alipanda ngazi hadi ghorofa ya tatu ya hoteli hiyo akatokea kwenye ukumbi mwemba uliokuwa una vyumba vingi sana. Hapo alihesabu mlango wa nne baada eneo ambalo kuna lifti kisha akatembea hadi kwenye mlango huo ulio na namba 130, Thomas alipofika hapo akazidi kukumbuka jinsi mkono wake ulivyokuwa ukitalii kwa lazima umbile lenye ngozi laini la Josephine. Hisia za nwili wake nazo zilimzidi zaidi hadi akaona dalili za wageni kukaribia, hisia hizo zilimpelekea hata asigonge mlango huo na kuufungua kwa papara. Hakujua kama kufanya hivyo lilikuwa ni kosa kubwa sana ambalo hajawahi kulifanya katika kipindi chote alichokuwa akifanya kazi hiyo, alikuwa akiongozwa na tamaa ya mwili kuliko akili zake jambo ambalo ni hatari sana kwa kazi yake hiyo hatari ya kihalifu.
Mllango ulipotii amri ya kufunguka alimuona Josephine akiwa ameketi kitadani tu akiwa amejifunga taulo fupi ambalo lilikuwa limeacha sehemu kubwa ya mapaja yake nje, Thomas alibaki ameduwaa kwa sekunde kadhaa na alipozinduka kutoka kwenye mduwao wake aliingia ndani ya chumba hicho kwa kasi sana pasipo kutambua alikuwa akifanya kosa jingine tena. Akiwa ameongozwa na tamaa zake alipouvuka mlango huo kwa hatua tu alihisi kitu kizito kikitua kwenye shingo yake hadi akakosa muhimili akaanguka chini akiwa hata hajamkaribia Josephine, sauti ya kufungwa kwa mlango ndiyo ilifuata baada ya kupokea ukaribisho huo uliyoifanya hadi shingo yake aione nzito kwa ghafla iliyojaa maumivu sana. Thomas alibaki akiwa haoni vizuri kwa athari ya ukaribisho huo aliokuwa ameupokea.
Kizunguzungu cha ghafla nacho kilimkamata akiwa bado yupo chini hadi nguvu ya kuinuka akaikosa kwa muda huo akisikilizia maumivu, akiwa kwenye hali hiyo ya maumivu alitazama mbele yake kwa sentimita kadhaa akakutana na miguu ya Josephine ambayo alikuwa ameilekeza katika upande ambao unyayo wake ulikuwa umezibwa na kochi ambapo ilikuwa ngumu sana Thomas kuiona wakati anaingia ndani humo. Miguu hiyo ya kirembo ya Josephine ilikuwa ina kitu kingine cha ziada mbacho kilikuwa ni ishara tosha ya kutokuwepo kwa uhuru kwa Josephine, ilikuwa ni pingu ndiyo ishara kutokuwepo kwa uhuru kwa mrembo huyo. Pingu hiyo ambayo ilikuwa ina kamba ngumu sana ambayo ilikuwa imeingia ndani ya uvungu wa kitanda ikiashiria ilikuwa imeenda kufungwa mahall umo uuvunguni, Thomas alijua kabisa alikuwa ameingia katika pango mamba bila kujijua akijua ni shimo la huba ndiyo alikuwa akielekea kuingia.
"Thomas nafurahi kukuona kwa mara ya pili" Alisikia sauti ya kiume ikitokea kule ulipo ule mlango wa kutokea humo ndani ambapo ilimfanya ageuke kwa upesi sana, alipogeuka akiwa bado yupo hapohapo kwenye marumaru alishtuka sana hadi akajivuta nyuma kuelekea upande ambao alikuwa Josephine ili aweze kupata sehemu ya kuegemesha mgongo baada ya kuwa na maumivu sana shingoni mwake.
"Hatimaye tunaonana yena kwa mara ya tatu Thomas vipi utatumia kinyaji gani" Sauti hiyo iliomuuliza kwa mara nyingine ikiwa ina furaha mithili ina mkaribisha mgeni ambaye alikuwa ametarajia kama atakuja kwa ajili ya jambo la furaha zaidi ambalo alitakiwa mgeni huyo awepo.
"Damn! Norbert!" Thomas aliongea huku akimtazama Norbert ambaye ndiye huyo alikuwa akimkaribisha kwa furaha ya kinafiki baada ya kumuachia pigo ambalo limemfanya siwe na nguvu hadi muda huo.
"Yes my best friend (ndiyo rafiki yangu mpendwa) umenikumbuka eeeh! Ni yuleyule tuliyepandwa wote ndege moja kutoka Arusha hadi Dar na ni yuleyule niliyewakaribisha kwenye mchezo wa wenye akili kule nyumbani kwa Ibrahim. Sasa karibu tena na hapa ukiwa pamoja na Josephine msichana mtamu zaidi ya vanilla niliyeuonja utamu wake uliopelekea Benjamin atake kumuua lakini kwa huruma yangu nikamuwahi ingawa alimpiga risasi ya bega kisha nikammaliza mimi" Norbert aliongea huku akimsogelea Thomas akiwa hana silaha yoyote mikononi mwake, maneno hayo aliyoyaongea yalimfanya Thomas amtazame Josephine kwa jicho la chuki akiwa bado yupo pale chini.
Hapo aliotambua kabisa kuwa Josephine alikuwa amewadanganya siku hile alipoeleza juu ya kuuawa kwa Benson, jicho lake la chuki nalo llilipokelewa kwa kutazamwa kwa dharau na Josephine ambaye alikuwa akimchukia sana kwa udhalilishaji wake aliokuwa akitaka kuufanya usiku uliopita kwake. Josephine kila akikumbuka jinsi Thomas alivyokuwa akimshika kama alikuwa akimpapasa kahaba wa bar alizidi kukasirika
"Thomas ulifikiri sheria hiyo ya mashoga itafanikiwa kupita Tanzania muweze kumkomoa Rais Zuber, hilo mmefeli kabisa, mashoga mtabaki kuwa nyinyi tu na nchi zenu na siyo Tanzania." Norbert alimuambia kwa dharau Thomas huku akizidi kumkashifu kwa kumuita shoga na kupelekea Thomas akasirike sana.
"Son of a bitch (mtoto wa mbwa)! Nani shoga?!" Thomas aliongea kwa kwa kali na ajitutumua akasimama ingawa maumivu bado alikuwa nayo na hata nguvu kwenye mwili wake ilikuwa imepungua kabisa, hasira zilezile alizokuwa akimuonya Benson na Santos wasiziendekeze sasa zilimjia yeye na akawa nazo muda huo kutokana na maumivu aliyokuwa nayo. Alisimama kwa kujikaza ingawa bado alikuwa anayumba kwa kukosa nguvu kutokana na teke zito la shingo alilopigwa na Norbert, akiwa kasimama hivyohivyo alikunja ngumi zake kwa nguvu sana hadi mikono ikawa inamtetemeka
*JOSEPHINE AMUWEKA THOMAS MTEGONI
*AINGIA KWENYE ANGA ZA NORBERT KWA MTEGO, JE ATAPONA
*WOTE WANSWA
*JE ALINASWA VIPI HADI AKAMNASISHA MWENZAKE ?
SEHEMU YA THELATHINI NA TANO NDIYO INA MAJIBU YA KILLE UNACHOKIULIZA USIKOSE KUSONGA NAYO TUKIJAALIWA UHAI NNA AFYA
No comments:
Post a Comment