Sunday, January 8, 2017

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA THELATHINI NA SITA






MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________



SEHEMU YA THELATHINI NA SITA!!
    Alijikakamua na akajaribu kujiinua sakafuni huku mikono yake ikiwa inamsaidia katika kuinuka huko ikiwa inatetemeka, alijitahidi aweze kufika hatua ya kusimama lakini mikono ilimsaliti na hatimaye akateleza mahali pasipokuwa na utelezi na akaangukia kidevu kwa mara nyingine.
             "Aaaaaaaaargh!" Alitoa ukelele dhaifu kwa viungo yake vya mwili kumsaliti katika kumkabili
Norbert ambaye alikuwa amesimama mita kadhaa  kutoka hapo alipodondoka akimtazama kwa dharau.



_______________TIRIRIKA NAYO
    Damu zilikuwa zikimtoka mdomoni kwa kujing'ata ulimi kwa mara  nyingine alipoanguka na kuzidi kuimletea  maumivu ambayo ni aliyaona yamezidi kiwango, alikaa akiwa amelala kifudifudi kwa sekunde kadhaa huku akihema. Bado hakutaka kuonekana amezidiwa kiwango na Norbert yeye aliamua anyanyuke apambane hivyohivyo, aliweka tena viganja vya mikono huku akimtazama Josephine ambbaye alimbinulia tu mdomo kwa dharau tu. Hapo Thomas alipata ujasiri wa ghafla na akajikakamua viungo vyake vyote na akasimama wima ingawa muhimuli wa kusimama sawasawa hakuwa nao kwa muda huo, alihema kwa hasira sana huku akimtazama Norbert ambaye alikuwa anamsubiri aje vilevile kikondoo alivyokuwa akija hapo awali. Thomas alikuwa akihema kwa nguvu sana kutokana na kushindwa kubana pumzi, kuhema huko kulisababisha aache mdomo wazi kwa hakustahimili kuhema kwa kutumia pua pekee kwa jinsi pumzi zilivyokuwa zimemuishia. Aligeuza tena macho akamtazama Josephine pale kitandani alipokuwa amekaa huku damu ikiwa inamtoka mdomoni kutokana na kujing'ata ulimi alipojigonga kievu sakafuni, kuyumba ndiyo ilikuwa desturi yake kwa muda huo mfupi aliokuwa amepatikana katika mtego wa Norbert.
    Alijaribu tena kumfuata Norbert kwa kupiga ngumi za kizembe mfululizo lakini aliambulia patupu tu kwani Norbeet alimkwepa akaenda kusalimianaa ukuta wa chumba hicho ambao uliigonga mwamba wa pua yake kisawasawa hadi akaenda chini kwa mara nyingine,  kila alipoanguka alikuwa akinyanyua uso wake na kumtazama Josephine  ambapo alizidi kuwa na hasira zaidi kwa dharau alizokuwa akioneshwa na Josephine kwa muda huo.  Damu nazo zilikuwa zikimtoka puani pale alipojigonga mwamba huo wa pua ukutani, maumivu yalizidi ambayo yalimpa kiwewe zaidi.
               "We malaya jua nikitoka mzima hapa ndiyo mwisho wako hutopona kabisa" Aliongea na mawazo yake  huku akimtazama Josephine kwa jicho la chuki halafu akajikaza akasimama tena, safari hakutaka kutumia nguvu zake kabisa katika kurusha ngumi.

    Alimtazama Norbert alipokuwa amesimama kisha akatazama pembeni yake akaona stuli ngumu  ambazo huwekwa kwenye meza za vioo zinazo kaa sebuleni, stuli hiyo ilikuwa imetengenezwa kwa mbao ngumu ya mpingo. Thomas hakutaka kujifikiria mara mbili alipoitazama stuli hiyo yeye aliuma meno kwa hasira  na aliinyanyua juu akiwa ameikamata kwa mikono yake miwili huku akimtazama Norbert, alimtukania Norbert mama yake mzazi kisha akamfuata kwa nguvu akiwa ameishika hiyo stuli akiwa na lengo la kutaka na kumpiga nayo.
    Alipomfikia alimpelekea stuli hiyo usawa wa kifua lakini Norbert alimkwepa, Thomas aliyumba baada ya kumkosa Norbert na hata kabla hajakaa sawa alipokea ngumi nzito  ya kwenye taya kutoka kwa Norbert. Ngumi  hiyo ilimfanya ashindwe kusimama na akawa anaelekea chini akasalimiane na sakafu kwa mara nyingine, akiwa hata hajaifikia sakafu Norbert alimuongeza teke jingine maarufu kama dochi linalopigwa chini ya vidole vya miguu. Dochi hilo la mbavu lilimfanya Thomas aende kusambaratika ukutani, mgongo wa Thomas ndiyo ulipigiza ukutani kwa uzito wa teke hilo hadi akatema damu mdmoni mwake. Thomas alipata maumivu haswa ambayo yalimfanya hata ashindwe kupumua vizuri kwa muda huo, alihisi uti wake  wa mgongo ulikuwa umekosa mawasiliano kwa muda huo uliojipigiza kwenye ukuta
               "Aaaargh!" Ukelele wa maumivu ulimtoka Thomas  baada ya mgongo wake kusambaratika ukutani, alipotua chini alitua kwa upande mwingine wa mbavu  ambao haukupigwa dochi na Norbert. Maumivu ndiyo aliyasikia kwa mara mbili alipotua  kwa ubavu wa pili huo ambao ulikuwa haujaathirika na pigo la Norbert, maumivu hayo yalimfanya hata asiweze hata kuulalia upande alioangukia na akalala kufudifudi huku akitanua mdomo wa shida haswa. Pumzi zilikuwa zikimjia kwa tabu sana baada ya mbavu zake zote kupata maumivu alipoanguka.
                  "Aaargh!" Aliachia ukelele kwa mara nyingine huku akimtazama Norbert na hapo aliamini kabisa alikuwa amekamatika, upande mmoja wa mbavu alihisi ahueni  baada ya pigo lile na upande mwingine alihisi ndiyo kabisa ulikuwa hauna ushirikiano kabisa.

     Alijaribu kujiinua kwa mara nyingine lakini maumivu ya sehemu  ya ubavu aiyopigwa dochi na Norbert yalimfanya ashindwe kabisa kunyanyuka, aliisalimia sakafu tena akabaki akitoa miguno iliyojaa hasira tu. Norbert naye hakutaka kumuacha hata apumzike kwa sekunde kadhaa tangu amuachie pigo hilo la kuuumiza, yeye alimfuata palepale chini akashika ukosi wa fulana aliyokuwa amevaa na akamkunja. Alimuinua juu huku akimtazama kwa macho makali tofauti na ilivyokuwa hapo awali, Thomas alipoinuliwa hivyo akiwa anatazamana uso kwa uso na Norbert alimtemea mate yaliyokuwa yamechanganyika na damu usoni kisha akajaribu kiumpiga kichwa.

   Mate hayo yaliyotua usoni yalimkera sana Norbert na aliwahi kukikwepa kichwa hiko kisimpate, alipokikwepa kichwa hiko alimsukuma Thomas ukutani kisha akampiga ngumi mfululizo kifuani na kummalizia na dochi jingine la pembeni lililopiga sehemu ubavu wake aliyokuwa ameipiga hapo awali hadi mifupa ya ubavu ikatoa sauti ya kugoka. Thomas aliende chini moja kwa moja na hata kuinuka safari hii alishindwa kabisa akabaki akihema kwa tabu, Norbert alimuacha katika eneo hillo kisha akapiga hatua kadhaa hadi ulipo mlango wa choo cha ndani cha hoteli hiyo.

   Alifika kwenye eneo lililokuwa na sinki la kunawia pamoja na kioo lililopo jirani na mlango huo wa choo, alifungua koki za sinki hilo la kunawia na kupelekea maji yaanze kutirirka. Alikunja mikono ya shati lake baada ya kuona maji yanatoka,  alinawa uso wake kuondoa mate ya damu aliyotemewa kisha akafunga koki za maji. Alipomaliza  kunawa alimfuata Thomas hadi pale alipokuwa amelala akamshika mguu mmoja akawa anataka kumvuta, Thomas bado alikuwa na jeuri na hakutaka kujilegeza kwa namna yoyote.  Aliufyatua ule mguu kurusha teke kwa lengo la kukataa kuvutwa na hapo ndipo aliojizidishia majanga mengine kabisa mbele ya mtu makini kama Norbert, alipoufyatua mguu ule kwa kurusha teke Norbert alisogea kando akiwa ameushika ule mguu vilvile. Kitendo cha haraka aliupiga mguu huo teke katika maungio ya goti hadi ukapinda papo hapo kuelekea pembeni.
               "Aaaaaargh!" Thomas alitoa ukelele mwingine wa maumivu baada ya mguu wake huo kuvunjwa huku akifumba macho kwa maumivu aliyoyapata.
    Norbert alimpofanyia kitendo hicho wala hakumjali yeye alianza kumvuta kwa nguvu kuelekea sebuleni, alimvuta hadi sebuleni akamuweka mbele kwa mitaa kadhaa kutoka Josephine alipo.

****

MAKAO MAKUU YA JESHI
    Mlango wa ofisi ya mkuu wa majeshi ulifunguliwa na aliingia mtu mzima anayekaribia kuitwa mzee akiwa amevaa suti nadhifu, mtu alipoingia  tu aliketi kwenye kiti kimoja cha wageni miongoni mwa viti viwili vilivyopo ndani ya ofisi hiyo. Haukupita muda mfupi tena aliingia mtu aliyevaa kanzu, koti la suti pamoja na kofia kichwani mwake, mtu huyo alikuwa na alama nyeusi usoni mwake kuashiria kuwa ni desturi yake katika kugusisha paji la uso katika nyumba ya ibada mara tano kwa siku kila siku. Mtu huyo naye kiumri alikuwa akikaribiana na mtu mwenye suti alienda kuketi kwenye kiti cha pili kilichokuwa kipo jirani na kiti cha mwenye suti.

    Wote wawili walitazama mbele yao kwenye meza yenye makabrasha kadhaa ambayo ilikuwa na kiti kimoja, kikiwa mkabala nao, kwenye kiti hicho alionekana L.J Ibrahim akiwa amevaa mavazi ya jeshi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) yenye rangi ya kijani kibichi pamoja kofia ya rangi hiyohiyo ikiwa na nembo la JWTZ kwa mbele. Walipotazamana na L.J Ibrahim watu hao walitabasamu na yeye pia akatabasamu kama wao, walibaki wakitazamana kwa sekunde kadhaa hadi pale L.J Ibrahim alipovunja ukimya huo kwa kuongea kile kilichokuwa kimemfanya awaite watu hao ofisini hapo.
             "vizuri kwa kwenda na muda Mufti na Askofu, nafikiri kazi yetu inakamilika usiku wa leo kuanzia saa sita usiku. Ikifika asubuhi jueni kwamba Mzee Ole ndiye atakayeingia pale magogoni, hivyo basi tukiwa tunaelekea kumaliza kazi hii kuna wajibu ambao kama viongozi wa dini natakiwa niwape" l.J Ibrahim aliongea kisha akaweka kituo akamtazama kila mmoja usoni.
               "hivi sasa ni saa..." L.J Ibrahim aliongea huku akiitazama saa yake ya mkononi na alipopata uhakika wa majira alisema, "Saa nne asubuhi, zimebaki saa tatu swala ya ijumaa iswaliwe kwa siku ya leo, hivyo basi mufti natambua kuwa katika siku ya leo unatoa hotuba ya ijumaa kule msikitini na vyomba vya habari vitakuwa vikiirusha hotuba hiyo kwa muda husika. Sasa  basi ni wakati wako wa kuhakikisha wananchi wanaamini kuwa Zuber ana hatia na kutoka madarakani ni lazima, propaganda ni sifa ya hotuba na hakikisha katika hotuba hiyo watu hawatotatambua kwamba upo pamoja nami wewe toa msimamo kama kiongozi wa dini".
              "Shaka ondoa kuhusu hilo General, hotuba ipo tayari nafikiri ni muda wake tu uwadie iweze kutoka" Mufti aliitikia huku akitabasamu
               "Vizuri sana Mufti, na kwako askofu.." L.J Ibrahim aliridhishwa na maneno ya Mufti kisha akaongea huku akimegeukia Askofu na akaweka kituo kifupi katika maneno yake. Aliendelea kuongea, "Jumapili ndiyo kazi yako katika kuhakikisha mapinduzi yanapewa baraka na waumini wote wa Katoliki, misa ya jumapili inabidi uitumie katika kuhakikisha wale waumini wote wa dhehebu la upande wako wanaukubali uongozi wa Mzee Ole na kuwa na chuki na Zuber. Wale waliokuwa na upendo na Zuber hakikisha chuki dhidi yake zinashika mizizi katika mioyo yao siyo kuchipua tu, kazi kwako Askofu. Malipo ya kazi kwa wote yatafika siku ya jumamosi baada ya mapinduzi kwenye kila akaunti ya mmoja ila Askofu yataingia nusu kwakuwa kazi yako itakuwa haijakamilika, hotuba yako ya jumapili jua ndiyo kukamilika kwa kazi yako".
              "General hofu ondoa kuhusu hilo kila kitu kipo  ndani ya mpango na siku hii ya leo ni muda wa kuandaliwa tu maneno hayo pamoja na vifungu vya biblia ili walainike mioyo" Askofu aliongea.
               "Yaani hakikisheni waumini wenu wanajuta kumuachia Zuber awe rais wao, nyinyi tu ndiyo mliobaki watu wa kiluteri tayari hawana imani naye kwa kitendo chake cha kukutana na Moses kwa siri. Sina la ziada niwatakie kazi njema, wanamapinduzi wenzangu" L.J Ibrahim aliwaaga wasaliti wenzake huku akinyanyuka kwenye kiti na akapeana mikono na kila mmoja wao, Askofu na Mufti walitoka ofisini humo kwa L.J Ibrahim kwa kutofuatana ambapo kila mmoja alitoka kwa wakati wake kuhofia kuhisiwa vingine.
   Hawakujua kabisa mtandao wa fagio la chuma nao ulikuwa ni mpana sana kuliko hata huo mtandao wao, wakati gari la Askofu likitoka eneo le getini kuna mwanajeshi mwenye cheo cha Sajini mtumishi aliyekuwa karibu na getini alikuwa akilitazama kwa makini sana huku akipiga picha kwa siri sana. Lilipofuata gari la Mufti alifanya hivyohivyo akiwa yupo kwenye kontena  jirani na getini hilo kwenye upande wa kuelekea ilipo Zahanati ya kijeshi, alipomaliza aliziangalia picha zake hizo na kuhakikisha zinaonekana kiufasaha zaidi.

   Alitazama pande zote na akaona yupo peke yake na hakuna aliyemuona, hapo alizituma picha hizo pamoja na picha nyingine alizotumiwa na mwenzake kama yeye aliyekuwa yupo sehemu ya katibu Mukhtasi wa Jenerali. Alitumia mtandao wa Whatsapp katika kuzituma picha hizo na alipohakikisha zimeenda alifuta picha hizo pamoja na rekodi za mtandao huo zikimuonesha alimtuma mhusika mkuu picha hizo. Baada ya hapo alibonyeza vitufe kadhaa vya simu yake kisha akamaliza na kitufe cha kupiga simu, aliitazama simu yake kwenye kioo hadi alipohakikisha imepokelewa ndiyo aliiweka sikioni.
             "Enhee! Madam nimetuma sasa hivi fungua Whatsapp utazipata zote.....nashukuru usijali ni sehemu ya kazi yangu kama mzalendo......fagiaaa" Aliongea kwa sauti ya chini na alipomaliza kuongea na simu hiyo aliikata kisha akafuata uelekeo ilipo zahanati ya kijeshi ndani ya makao makuuu hayo ya kijeshi.

****

    Baada ya kumvuta na kumuweka katika eneo hilo Norbert alimfungulia pingu Josephine na cheni aliyomvalisha, aliwatazama wote wawili  kisha akatabsamu kama ilivyo kawaida yake akiwa yupo kwenye kazi kama hizo aweze kumchanganya adui yake. Bila ya kuwaambia jambo jingine lolote Norbert alifungua ule mkoba alioletewa na vijana wake na akatoa kasha la makaratasi, alilifungua kasha hilo na akatoa bomu la kutega kwa saa maarufu kama C4. Bila ya kuongea neno lolote tena alilibandika bomu hilo ukutani kisha akaliwasha, sauti ya mishale ya saa ya bomu hilo ilianza kusikika ikitembea jambo ambalo lilizidisha hofu sana kwa maadui zake wakaona kabisa mwisho wao ulikuwa umekaribia. Baada ya kumaliza kutega hilo  bomu aliwatazama maadui zake kwa dharau kuu, kisha taratibu akachukua kila kilichokuwa muhimu kwa yeye kukichukua na akasogea hadi mlangoni akaweka dole gumba kwenye bomu lilokuwa lipo mlangoni. Waya wa bomu hilo uliingia ndani ya sehemu moja ya bomu hilo la mlangoni, baada ya kuutoa waya huo Norbert aligeuza  shingo yake akawatazama maadui zake.
             "Mna dakika tano tu za kuweza kutoka humu ndani la si hivyo nyote mtageuka vipandevipande kwa hilo bomu hapo uikutani na hili la mlangoni pia. Nikiubamiza mlango huu waya huu unajirudisha sasa atakayefungua mlango na waya huu ukawamba jua ndiyo kifo chenu wote, buriani nyote" Aliongea maneno hayo kisha akatoka ndani ya chumba hicho na akabamiza mlango, waya uliokuwa upo pale mlangoni ulijirudi na ukatga kama mwanzo.
       Josephine na Thomas wakiwa wamebaki mule chumbani walikuwa wana hofu kubwa sana juu ya bomu hilo, Thomas aljivuta kisha akakaa kwenye kochi akawa anamtazama  Josephine akiamini hakuwa na msaada mwingine zadi ya huyo mwanamke kwenye hatari kama hiyo. Alikuwa amevunjwa mguu na pia alikuwa amevunjwa mbavu na hakuwa na hata uwezo wa kusimama kwa muda huo aweze kujaribu hata  kujiokoa, Josephine alipotazamwa na Thomas yeye alimbinulia mdomo tu na hakumtilia maanani. Aliamua kuvaa gauni lake na akachukua kila kilichokuwa chake, baada ya kumaliza kuchukua vitu vyake alilitazama dirisha la kioo la hoteli hiyo kwa mara moja kisha macho yake akayarudisha kwenye bomu lililokuwa lipo ukutani. Alijikuta akimeza funda moja la mate  baada ya kuona dakika zilikuwa zimebaki mbili tu bomu hilo liweze kulipuka, kwa haraka alifungua dirisha la chumba hicho kisha akasogeza pazia na akavua viatu vyake vyenye kisigino akavishikilia.
                   "Josephine please nisadie usiniache humu" Thomas  aliomba msaada kutoka kwa Josephine ambaye tayari alikuwa ameshaanza kupandisha mguu mmoja adirishani  aweze kutoka nje, kauli hiyo ilimfanya Josephine amuangalie Thomas kwa dharau kisha akamsonya.
                    "Go to hell" Alimuambia huku akiendelea kutoka nje, kauli hiyo ilimfanya Thomas ajirushe kutoka pale kwenye kochi hadi kitandani ambapo pako karibu na eneo la dirisha ambalo Josephine alikuwa akipanda. Bila ya kuchezea muda alijibiringisha kitandani na akasogea hadi dirishani ambapo Josephine alikuwa akimalizia kutoka  mguu wa pili, kwa haraka alimuwahi Josephine shingoni akiwa amepiga magoti kitandani na akamkaba kwa nguvu zote.
                  "Hapa hutoki mpaka utoke na mimi au tufe wote" Thomas aliongea kwa hasira huku akiwa amemkaba akiwa hajali maumivu anayoyapata katika mbavu zake, Josephine alianza kuvutwa kurudi ndani na Thomas akaona ni hatari hiyo kwa yeye kubaki hapo.

    Kujikomboa na balaa hilo aliamua kuutoa mkono wa Thomas lakini hakuweza hata kidogo na  ikabidi ashikilie upande wa dirisha kwa nguvu asiweze kuvutwa kurudi ndani, Thomas naye alizidi kumvuta Josephine ilimradi asiweze kuondoka na bomu liweze kulipuka kwani ilikuwa imebaki dakika moja na sekunde kadhaa baada ya dakika ya pili iliyobakia kukatika hadi muda huo.
    Mlio kengele ya bomu ulianza kusikika kwa taatibu dakika moja hiyo ilipokuwa ikipungua kuelekea kenye sekunde, mlio huo ulimfanya Josephine azidi kuuona umauti ulikuwa ukikaribia kwake kwani muda wowote bomu hilo lingelipuka. Alizidi kukaza mikono yake akitumia nguvu zake za kimazoezi ya kimapigano kuweza kujizuia asiiingie ndani kwani ni hatari zaidi kwake kuingia humo ndani, Thomas alizidi kumvuta kuelekea ndani na akaona alikuwa akifanikiwa baada ya mikono ya Josephine aliyokuwa ameikaza kuanza kuelegea. Naye alilegeza mikono akijua alikuwa akifa pamoja na mbaya wake aliyeweza kumfanya aingie hatarini, aliona Josephine alikuwa akikaribia kuingia ndani na aliamua kutumia nguvu ndogo huku kicheko cha kifedhuli kikimtoka.

   Loh! Salallah! Hakujua kuwa hilo ni kosa kubwa alilokuwa amelifanya kulegeza mikono yake, hakujua kabisa kuwa Josephine naye alifanya hila kulegeza mikono kwa makusudi. Akiwa anaona Josephine alikuwa akikaribia kuingia ndani, ghafla Josephine alishika dirisha kwa nguvu kisha akaachia teke la msamba kwenda juu akiwa hajali kufunuka kwa gauni lake la mpira lenye kuvutika. Teke hilo lilimpata la kwenye paji la uso Thomas hadi akalegeza mikono mwenyewe bila ya kupenda na akamuachia Josephine huku akiyumba, Josephine bila kuchelewa alikaza mikono kwenye pembe la dirisha hilo lisilo na nondo. Alitupa miguu yote miwili kurudi nyuma na ikampata Thomas ya kifuani hadi akaangukia kitandani na akabiringita kwenda chini, baada ya kufanya hivyo alitoka dirishani upesi na akatembea hadi dirisha la chumba cha pili na akashikilia bomba kwa nguvu sana.
                "NOOOOOOO!" Thomas alipiga kelele kwa kukata tamaa alipoangukia humo dani.
      Muda huohuo muda ulikuwa umeshaisha na mlipuko mzito  ulitokea kwenye chumba alichokuwepo hadi dirisha la vioo likapasuka  na moto ukaonekana kwa nje, mayowe ya watu yalisikika baada ya mlipuko huo  na kengele maalum ya moto ikalia kwa ghafla katika hoteli hiyo. Josephine alipoona amesalimika hakutaka kusubiri tena akutwe katika eneo hilo, alipiga kisigino kioo cha dirisha la chumba cha pili hadi likavunjika hadi kikavunjika. Alitazama ndani ya chumba hicho akaona mlango wa kutoka wazi, hapo aliamua kupenyeza mkono kwenye sehemu ya kioo iliyovunjika na kufungua dirisha hilo na akaingia ndani ya chumba hicho. Hakutaka kupoteza muda yeye alikimbia hadi akatoka nje ya chumba ambapo alikuta kundi kubwa la wau likishuka kwenye ngazi za mlango wa nyuma huku wakipiga mayowe ya uoga, naye alijichanganya kwa haraka huku akipiga mayowe ya uoga kama wengine. Alijipenyeza kwenye kundi hilo la watu akishusha ngazi kwa  kasi sana kama ilivyokuwa wengine, hatimaye katika kujipenyeza huko alifanikiwa kufika nje kwa mlango huo wa nyuma na akatoka akijichanganya na watu waliokuwa wakikimbia kutoka huko kwenye mlango wa nyuma kuzunguka kwenye uzio wa hoteli hiyo kwenda kwenye lango kuu la magari na watu na magari.

****

    Muda ambao mlipuko unatokea Norbert hakuwa ameondoka mbali na hoteli hiyo, bado alikuwa yupo ndani ya gari karibu na lango kuu la kuingilia ndani ya hoteli hiyo akiwa na vijana wake wawili aliowatumia katika mpango huo. Baada ya bomu kulipuka vijana wake walionekana kufurahia sana wakijua kuwa kazi ilikuwa imeisha kwa wote waliomo mule chumbani, Norbert hakuwa akifurahia kabisa bali alikuwa akitazama tu kule kwenye lengo la hoteli hiyo.
               "Mkuu nafikiri wote ni marehemu wale" Kijana wa kiume alimuambia.
               "Si wote ila yule binti jua hakufa na katoka mzima, nimemuachia opportunity ya kuweza kujiokoa" Norbert aliwaambia.
               "Kivipi mkuu?" Wa kike aliuliza
               "Wakati natoka mule ndani nilimfungulia pingu na nilimvua ile cheni" nrbert alijibu.
               "He! Bosi huoni ni hatari hiyo si mhalifu yule" Yule wa kike alimuambia
               "Hata kama kwa sasa yule ni sawa na nyoka asiye na sumu kwetu hivyo hatuwezi  kumuhofia, nyoka mwenye sumu tayari amekufa mule kwenye bomu" Norbert aliwaambia
               "Aaaaah! mkuu wanawake siyo watu wa kuwadharau akiwa mzima yule jua ni hatari kwa nchi" Wa kiume alimuambia.
               "Vijana najua nikifanyacho nyinyi acheni  kama ilivyo, si niliwaambia hakufa haya muoneni huyo anatoka nje ya geti akijifanya amechanganyikiwa kama raia wengine" Norbert aliongea kisha akakatisha akawaonesha langoni wakamuona Josephine akiwa anatoka huku viatu kashika mkononi, wote walimtazama na wakajikuta wakicheka kwa jinsi alivyokuwa akiigiza kama kapatwa na kiwewe.
               "Kiwewe cha namna gani kile ukumbuke kuvua viatu uvishike mkononi ukimbie vizuri na si kuvitupa, maigizo ya kibongo haya. Haya tuondokeni" Norbert aliongea huku akicheka na alitoa pia amri ya kuondoka eneo hilo, yule kijana wa kiume ndiye aliyekuwa upo nyuma ya usukani na aliposikia mari hiyo aliliwasha gari na akaweka gia kisha akaliingiza barabarani na kuondoka katika eneo hilo.

*THOMAS HATUNAYE TENA
*JOSEPHINE ATUMIA UJASUSI KUJIKOMBOA, JE HATAKUWA NA MADHARA KAMA ANVYOSEMA NORBERT?
*MUFTI NA ASKOFU WAPEWA AMRI MPYA NA PICHA ZAO ZANASWA, JE NINI HATMA YAO?

TUWE PAMOJA KATIKA SEHEMU YA THELATHINI NA SABA UTAPATA MAJIBU YA MASWALI HAYO USIKOSE!






No comments:

Post a Comment