Sunday, January 22, 2017

WAKALA WA GIZA SEHEMU YA AROBAINI NA TATU





RIWAYA: WAKALA WA GIZA

MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA


SIMU: +255713776843
          +255762219759


WHATSAPP: +255713776843

SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU MUUMBA WA ULIMWENGU WOTE KWA KUNIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA HII NIKIWA NA AFYA NJEMA




______________+18__________________





***SEHEMU YA AROBAINI NA TATU****


             "ama kweli umdhaniaye siye kumbe ndiye, sikutegemea kabisa kama mtu kama huyu ndiye atakuwa adui wa taifa hili hadi atumike kuja kujaribu kufanya mauaji" IGP Chulanga aliongea.

               "Mkuu unajua bado siamini lakini ule mkanda unaeleza kila kitu" DCP  John aliongea akijifanya kutoamini.

               "John ndiyo hivyo imeshatokea, na hapa hamna uchunguzi wa zaidi hata mchoro hauna haja kwa mtu kama huyu aliyeuawa na mwanausalama anayeijua kazi yake" IGP Chulanga aliongea kisha akawageukia Askari aliokuja nao akawaambia, "hakikisheni mnaangalia huko nyuma hadi muipate kamera yake aliyotumia kufanyia tukio"

          
      "Mkuu" Maaskari hao walitii amri wakapiga saluti na kugeuka nyuma kisha wakawasha kurunzi zao na kuanza kufanya msako.





_______TIRIRIKA NAYO


   KUTI KAVU KUKATIKA
  (MWISHO WA WABEMBEAJI)

     Hali si shwari kabisa tangu taarifa za Mufti kuwa yupo hai zilipofika kwenye meza ya wahusika ambao walikuwa wakitaka kwa udi na uvumba kumuua Mufti, ilikuwa ni kama pigo kwao kusikia jambo hilo ambalo lilikuwa likiwapa wahka sana. Ilikuwa ni ndani ya nyumba moja ya kifahari iliyokuwa ipo Mbezi beach, watu wa ndani ya nyumba hiyo walikuwa wapo tumbo joto baada ya kuvuja kwa siri zao kupitia kwa mwenzao ambaye alikuwa amewekewa mtego na Norbert. Ilikuwa ni nyumba ya waziri mmoja maarufu sana ndani ya serikali ya Rais Zuber ambaye alikuwa akihusika kwa asilimia zote ndani ya mpango huo wa kutaka kuipindua nchi, wziri huyu alikuwa akifanya mambo hayo kwa siri sana na hata kwenye baadhi ya mikutano ya siri hakuwa akitokea kabisa zaidi ya wanamapinduzi wenzake kumfahamu vilivyo.

     Alikuwa aemahidiwa nafasi ya uwaziri mkuu katika serikali itayoundwa na Mzee Ole pmaoja na kitita kikubwa sana cha fedha ikiwa tu atakubali kuunga mkono mapinduzi hayo. Mipango yote iliyokuwa ikipangwa juu ya mpango huo alikuwa akiijua vyema, aliamua kujihusisha katika mapngo huo kwa namna ya siri kwa kuhofia mambo yakiharibika angeweza kupatiwa ushahidi wakuweza kumuweka hatiani. Hivyo hakukaa kwenye vikao vyao hata kama ukipatikana ushahidi wa picha basi hatakuwemo ndani yake, bado alikuwa akijulikana  sana na wenzake ndiyo maana Mufti alifikia hatua ya kutaka kumtaja jina lake lakini Wilson alimuwahi kumnyamazisha kwa kutumia silaha aliyokuwa nayo.  Baada ya kunyamazishwa huko kwa Wilson alipiga simu haraka akamuhitaji Mzee Ole afike ndani ya nyumba yake ambayo ilikuwa haitumiwi na familia yake na ndiyo hapo wakaja kwenye nyumba hiyo wakiwa wawili tu. Muda huo L.J Ibrahim alikuwa akijiandaa kwenye kuongoza vikosi vya majeshi vilivyokuwa vimeizunguka ikulu akiamini kazi ilikuwa imeisha hata kama alitajwa kuwa alikuwa akihusika ndani ya mpango huo.

    Mheshimiwa huyo hali ilikuwa tete sana kwake ilifikia muda huo akaona mambo yalikuwa yamekaa vibaya sana kiupande wake, muda huo walikuwa wamekaa kwenye chumba maalum cha mkutano ndani ya nyumba yake hiyo wakiwa wawili tu waanzishaji wa serikali mpya ijayo ya Tanzania, waanzishaji wa serikali yenye hila ya watanzania ndiyo walikuwa wamekaa humo ndani. Mzee Ole alikuwa yupo kwenye hali ya kawaida sana kwakuwa aliwahi kukumbwa na mazito zaidi ya hayo, Waziri huyu alikuwa yupo kwenye hali tete kwakuwa ni mara yake ya kwanza kukumbwa na balaa kama hilo akiwa anacheza mchezo mchafu wa siasa.

              "Mzee Ole hii ni mbaya  huoni kama akizinduka yule ndiyo heshima yangu imekwisha" Aliongea kwa wqasiwasi mkubwa akiwa amesimama kwenye chumba hicho cha mkutano na Mzee Ole alikuwa ametulia kwenye kiti hana hofu yoyote ile.

               "Relax ndugu ni hali ya kawaida sana katika siasa"

                "Nitaanza vipi kurelax Mzee Ole ikiwa huyu mtu bado anapumua hata Wilson alivyompiga risasi bado tu hakufa"

                 "Nani kakwambia yule Mufti  ataiona siku ya kesho mpaka aje kupata fahamu na kukutaja"

                 "Mzee Ole una uhakika juu ya hilo au unataka kuniletea siasa"

                  "Fikiri mara mbili uwepo wa Leopard Queen kama nurse ndani ya hospitali ile  unafikiri yupo kwa ajili ya kazi gani"

                  "ok kama yupo ndani mwambie ammalize haraka sana kabla huyo N001 hajaja pale"

                   "Hilo ndiyo la muhimu la kusema na si kupanic haraka namna hiyo, hukujua siasa ni mchezo mchafu. Msafi anapakazwa uchafu anaonekana mchafu na mchafu anajisafisha kwa njia haramu anaonekana msafi, hii ndiyo siasa"

                    "Sawa mpigie basi Leopard Queen umuambia amalize kazi Mzee Ole tutachelewa kabisa fikiria IGP yupo tayari ndani ya eneo la hospitali huoni wakiongezeka TISS pia kazi itakuwa ngumu zaidi"

                    "(Mzee Ole aliposikia kauli hiyo alimpatia simu Waziri huyo) Piga hii hapa"
Waziri bila kuchelwa alinyakua simu nna kupiga namba za Jospehine kisha akaweka simu sikioni, aliisubiri kwa muda mrfu sana simu hiyo ilipokuwa inaita hadi ilipokelewa ndiyo alifungua mdomo wake na kuongea.

                     "Leopard Queen maliza kazi nzi watajaa hapo iwe mbaya kwetu......ok ni njema kama upo karibu wewe maliza tu"

   Baada ya kuongea maneno hayo na Josephine alikata simu na aliketi chini kwenye kiti, simu aliiweka mezani na akamsogezea Mzee Ole aliyekuwa amempatia aongeee nayo.
"Vipi kasemaje?"

                      "Yupo karibu na wodi aliyolazwa anaenda kumaliza kazi baada ya IGP na baadhi ya maaskari wake muhimu kutoka walipopata taarifa ambayo haijui ni taarifa ipi?"
"sasa ulikuwa unahofu nini  akiwepo huyo Mufti haponi ujue, hata kama leo akongea ukweli jua mapinduzi yapo palepale hakuna wa kuyazuia"

                        "Lakini bado tutaonekana tumechukua nchi kinguvu kwa maslahi ya watu fulani"

                         "Sasa hofu yako nini kwa ajili ya hilo mimi  nikiwa Rais wewe waziri mkuu, tufanye maajabu mengi kwenye maendeleo ya Tanzania naamini tutawaziba midomo wote hao"

                           "tatizo mataifa ya nje yatatuchukulia vipi?"

                           "Hilo siyo tatizo kabisa future Prime minister, tulete maendeleo ya maana uone kama hatujawafanya waone kama ilikuwa ni haki tosha kumuondoa Zuber aliyekuwa akijifanya ana misimamo hadi akatae dola milioni 600"

                            "Ok nimekupata sasa hivi, nafikiri kazi pekee iliyobakia kutusaidia ni jeshi tu na si nyingineyo"

                              "Ndyio hivyo na Ibrahima kaingia mwenyewe kazini tegemea makubwa zaidi"

                               "Nina imani naye maana jeshi lipo chini ya amri yake, tutegemee makubwa siyo nitegemee"

                               "Kabisaa"

                             "Hivi sasa kidogo nimetulia maana amani haikuwepo"

                              "Utulie kabisa usiwe na hofu hakuna litakaloharibika kabisa"

****

    Askari aliyekuwa amepewa jukumu la kumlinda Mufti alikuwa yupo makini akiendela na kazi yake kwa muda huo, hakuwa akizubaisha hata kidogo macho yake ili asije akafanya uzembe akiwa yupo kazini na kuleta lawama kwa wakubwa zake au hata akaadhibiwa kwa uzembe wake huo alioufanya. Bunduki aina ya SMG T56 ndiyo ilikuwa ipo mikononi kwenye kiti kilichokuwa kimewekwa pembeni ya mlango wa wodi hiyo ambacho ndiyo alikuwa amekikalia, alikuwa akiangaza macho yake katika kila pande zilizokuwa zikimzunguka katika eneo hilo. Ukimya wa eneo hilo ambalo ndiyo ilikuwa ni njia pia ya kupita kuelekea kwenye vyumba vingine haukumfanya kabisa apoteze umakini akiwa yupo kazini, alikuwa yupo makini sana katika kuhakikisha kuwa Mufti anakuwa salama katika muda huo hadi anapatwa na fahamu.

     Akiwa amekaa nje ya wodi akiendelea kuhakikisha usalama wa Mufti unakuwepo, kwenye upande wa kushoto alitokea Muuguzi wa kike mwenye umbo tata ambaye alikuwa amevaa miwani ya macho. Muuguzi huyo alikuwa amebeba baadhi ya vifaa vya kitabibu akiwa anakuja katika njia hiyo aliyokuwa amekaa askari huyo aliyekuwa ana silaha yake. Muuguzi huyo alikuwa akitembea kwa haraka sana akionekana ni mwenye kuwahi katika wodi ambayo ilikuwa ina mgonjwa aliyekuwa akitaka huduma kwa haraka sana.  Kamba za viatu za muuguzi huyo zilikuwa zimelegezwa na kutembea kwa haraka hivyo kulifanya kamba hizo zifunguke kabisa, Muuguzi huyo hakuonesha kujali kwa jinsi kamba hizo  zilivyofunguka yeye alikaza mwendo tu akionekana ni mwenye haraka sana.

     Askari aliyekuwa akilinda kwenye mlango wa wodi aliyokuwa amelazwa Mufti alipomuona jinsi alivyokuwa mrembo na alivyokuwa akitembea kwa hraka hadi mzigo mdogo uliokuwa kifuani ukawa unaleta fujo hafifu, alibaki  akimtazama tu. Askari huyo alianza kumtazama kuanzia kuanzi juu  kisha akashusha macho yake hadi kati,alipoyapeleka macho yake chini alijionea mwenyewe kamba za viatu vya muuguzi huyo tayari zilikuwa zimefunguka na alikuwa akitembea kwa haraka tu.

                  "Oooooh! Si ajali hii ngoja nijionee mwenyewe nijipatie ujiko kumsadia akiisalimia hii sakafu" alijisemea Askari huyo kisha akarudisha macho kama alivyokuwa kawaida.

    Muuguzi alikaza mendo zaidi akionekana yupo katika kuwahi katika sehemu ambayo alikuwa anaenda,hakuonekana kabisa kumtilia maanani Askari ambaye alikuwa yupo katika mlango wa wodi ambayo Mufti alikuwa amelazwa. Alipofika usawa aliokuwepo Askari huyo alikanyaga kamba za  viatu vyake, hapo alijikuta akielekea kusalimiana na sakafu ya eneo hilo hata vifaa alivyobeba vilianza kutangulia kabla yake. Ili kumzuia asianguke na kuumia Askari huyo alinyanyuka kwa haraka sana na akawahi mikono yake kukamata kifua na tumbo kisha akamgeuza na kuwa ameshika kiuno laini cha huyo Muuguzi, alimshikilia barabara asiweze kwenda chini akiona alikuwa amepata ushindi wa  kuweza kuonekana alikuwa anajali sana watu wasije kuumia.

               "Anti yaani unajali usalama wa wengine lakini wako wewe huujali, si ungeumia jamani" Askari huyo alimuambia Muuguzi huyo akionekana ni mwenye kumuonea huruma sana kwa jinsi alivyokuwa akienda kusalimiana na sakafu, pamoja na kumuambia maneno hayo bado hakuwa amemuinua Muuguzi huyo alikuwa bado kamshikilia vilevile.

    Miwani ya muuguzi huyo ilikuwa imemuanguka kwa muda huo na alikuwa amefumba macho baada ya kunusurika kuanguka, Askari huyo aijikuta akimtazama Muuguzi akiwa amefumba macho.

    Hakujua kuwa Muuguzi huyo hakuwa amefumba macho yake kabisa bali alikuwa amefumba kihila, hakujua kabisa hiyo ilikuwa ni hila ya huyo Muuguzi aliyekuwa akimvuta aingie kwenye mtego ambao tayari alikuwa ameshaingia katika mtego wake.
Askari huyo hakujua kabisa huyo aliyekuwa amemshikilia ndiye alikuwa akilinda asiweze kufanya jambo baya kwa Mufti, bunduki nayo tayari alikuwa ameshaisahau kwenye kiti kwa papara tu za kwenda kuushika mwili wa binti mrembo kama huyo.

   Aliona ameushika mwili wa mwanamke huyo mrembo hadi akawa anajisikia faraja sana kwa kuweza kumshika lakini hakutambua kuwa alikuwa ameingia kwenye kichaka cha  chatu, akiwa bado ameendelea kumshika vilevile hakutambua kuwa chatu huyo alikuwa tayari  ameshamuingiza kwenye mawindo yake.

   Ghafla bila kutarajia miguu ya yule Muuguzi ambaye hakuwa mwingine ila ni Josephine, iliidaka shingo ya Askari huyo kwa kasi ya ajabu sana bila yeye mwenyewe kutarajia. Josephina alijitoa kwenye mikono ya huyo Askari kwa haraka sana lakini miguu yake haikuwa imetoka shingoni,kwa kasi ya ajabu alienda chini kisha akamvuta  Askari huyo shingo yake na kumpeleka ukutani kwa mtindo ambao hutumiwa sana na wacheza judo. Askari huyo alijikuta akienda kubinuka na kisha akasambaratika ukutani kwa kupigiza mgongo, bado hata hajafikiria kuhusu pigo lile maumivu yake aweze kujiandaa na pigo jingine Josephine alimshindilia kisigino cha kwenye kifua alipotua chini tu. Pigo hilo lilimfanya askari huyo ajigeuze akiwa hapo sakafuni kutokana na maumivu aliyokuwa ameyapata, Josephin hakutaka hata kumsuburi anyanyuke yeye alimuongeza pigo jingine la nyuma ya kisogo hadi akapoteza fahamu papo hapo.

                "Kwa tamaa zenu mtaangamia kama kuku wanaume nyinyi" Josephine aliongea kwa sauti ya chini kisha akaingia kwenye wodi ambayo alikuwa amelazwa Mufti, alifunga mlango wa wodi hiyo kisha akageuka kule kwenye kitanda mbapo alikuwa amelazwa Mufti akiwa hajitambui. Mlio wa mashine iliyokuwa iikionesha shinikizo la damu la Mufti pamoja na mapigo ya moyo ndiyo ulimkaribihsa humo ndani hadi akaangalia pale kitandani.

    Alimuona Mufti akiwa amelala huku mashine ya kusaidia kupumua ikiwa imefungwa mdomoni, kulikuwa na dripu ya damu pembeni ikiwa inatiririka. Josephine hakutaka kupoteza muda akiwa ndani ya wodi hiyo, alienda moja kwa moja hadi jirani na kitanda alichokuwa amelazwa Mufti.

    Alipofika kwenye kitanda hiko aliangalia kule mlangoni kwa kushuku jambo lakini akaona bado kuo kimya, hapo alirudisha macho alipokuwa amelala Mufti kisha akasonya.

               "Upumzike kwa amani Mufti" Aliongea kisha akachomoa mashine iliyokuwa ikisaidia Mufti kupumua bila hata huruma, mlio wa mashine iliyokuwa ikisaidia kupumua kwa Mufti ndiyo ulifuata lakini Josephine hakutaka  uendelee wakati mtu huyo akiwa anapigania uhai wake kwa muda huo.

    Alichoamua kukifanya kwa muda huo ilikuwa ni kushika shingo ya Mufti na kuizungusha akaivunja kabisa, huo ndiyo ukawa mwisho wa Mufti ndani ya dunia hii kwa kuisaliti dini yake na pia kuisaliti nchi. Alilipwa kwa kile alichokuwa akikifanya akiwa ndani ya dunia bila kujali uwepo wa Mungu, sasa alikuwa akijiandaa kwenda kulipwa zaidi kwa kile alichokuwa amekifanya.

    Josephine alipomaliza kazi iliyomleta humo ndani aliona hakuna umuhimu wa kuendela kubaki humo na ilimlazimu atoke nje ya chumba hicho, alienda haraka hadi akiwa anajiandaa kutoka ndani ya chumba hicho. Alipofungua mlango tuu alikutana na mdomo wa bunduki ambayo ilikuwa imeegemeza kwenye mlango  kizembe na askari wa jeshi la polisi. Kufungua kwake mlango kulisababisha mdomo wa bunduki hiyo uingie ndani zaidi, Josephine aliyumba pembeni mdomo wa bunduki hiyo ulipokuwa ukitaka kumsukuma kutoka na askari aliyekuwa ameishika bunduki hiyo kuwa alikuwa amekandamiza mlango wa wodi hiyo.

     Bila kuchelewa bunduki hiyo ilipomkosa aliidaka bunduki hiyo akaivuta na kupelekea Askari huyo aje mbele bila kutarajia, aliachia goti lake kwa nguvu sana ambalo lilimpata Askari huyo kwenye kifua na akaiachia bunduki ambayo ilibaki katika mkono wake. Askari huyo mwingine alibaki akiumia huku simu yake ya upepo aliyokuwa ameichomeka kwenye kiuno chake ikitoa sauti.

                   "Tunakuja tupo njiani!" Sauti ya kutoka ndani ya simu hiyo ya upepo ilisikika na hapo Josephine akabaini kuwa taairfa kutoka kwa maaskari wengine ilikuwa imeshafika na walikuwa wapo njiani wanakuja, bila kuchelewa aliitoa ile bunduki kibebea risasi kisha akakichukua ili yule Askari asifanye chochote lile ikiwa atakuwa anakimbia.

   Alitoka ndani ya wodi hiyo kwa kasi sana akaeleka katika upande ambao ulikuwa unaelekea mwisho wa ukumbi wa mrefu wa wodi hizo, alipofika mwisho alikutana na ngazi nyingine ambazo zilikuwa zikipanda kuelekea ghorofa ya juu. Josephine  alipofika hapo hakuelekea kwenye ngazi bali alifungua kioo cha dirisha lililokuwa lipo pembeni, alitoka nje ya dirisha hilo kisha akashika mabomba ambayo hupeleka uchafu chini kutoka vyoo vya ghorofani. Alishuka na mabomba hayo kwa utaalamu mkubwa sana hadi chini akatokea kwenye eneo la nyuma ya hospitali hiyo, hapo alipitia njia za panya hadi akatoka nje ya hospitali hiyo bila kujulikana na yeyote.


****


SAA NNE USIKU

    Yakiwa masaa mawili pekee mapinduzi hayo haramu yaliyokuwa yamepangwa kutokea ndani ya nchi ya Tazania, wanajeshi wa majeshi yote ya ulinzi na usalama waliokuwa wapo nje ya Ikulu walikuwa wakijiweka tayari kwa kazi mbili tofauti zilizokuwa zimewaleta katika eneo. Kikosi kimoja che jeshi kilichokkuwa kimetangulia mbele ambacho kilikuwa kikosi cha ardhini kilikuwa kikijiweka sawa kuweza kulinda usalama wa Mheshimiwa Rais pamoja na waliokuweno humo ndani, wengine waliosalia walikuwa wakijiandaa kuhakikisha kuwa Mheshimiwa Rais alikuwa akitoka ndani ya Ikulu hiyo kwa mujibu wa amri waliyokuwa wamepewa.

    Kikosi kimoja kilikuwa kikisikiliza amri ya Rais na kikosi kingine kilikuwa kikisikiliza amri ya Jenerali feki aliyekuwa akijihesabia kuwa yeye ni mkuu wa majeshi rasmi. Kambi zote za vikosi hivyo zilikuwa zikiweka sawa mawasiliano baina ya watu wao waliokuwa wapo kwenye operesheni hiyo,ni operesheni fagio la chuma  dhidi ya opersheni  mapinduzi.

     Operesheni fagio la chuma ilikuwa inataka kuhakikisha kuwa inafagia taka moja iliyokuwa imebaki ambayo ilikuwa ikisababisha hayo,operesheni mapinduzi ilitaka kuhakikisha kuwa inampindua Rais aliyemo madarakani na kuleta  Rais wao mpya waliyekuwa wakimtaka wao. M.J Belinda akiwa ndiyo kamanda wa kikosi cha fagio la chuma kilichokuwa kipo mbele ya ikulu alikuwa akihakikisha kuwa hakuna jambo lolote litakalo hairbika kwenye operesheni hiyo, alikuwa akiwasiliana na makamanda waliopo chini yake kwa kutumia vinasa sauti na si simu za upepo ili asiweze kuingiliana mawasiliano na wanajeshi wa kikosi cha majini ambao walikuwa tayari wapo nyuma yao wakisubiri wao ndiyo waanze kazi. Wanajeshi wa majini wote walikuwa wakifikiria kuwa M.J Belinda na kikosi chake walikuwa wapo upande wao hivyo walikuwa wakiwa tegemea wao sana kuliko kitu kingine chochote ndani ya operesheni hiyo ambayo  walikuwa wakifuata amri za mkubwa wao kijeshi aliyekuwa akiwaamuru kufanya kile alichokuwa akitaka wao wafanye.

   Vifaa vya mawasiliano baina ya kambi hizo za dharura za vikosi viwili tofauti ndiyo zilikuwa zikiendela kwa muda huo, mara chache wao kwa wao walikuwa wakiwasiliana wakihimizana wajiandae kwa ajili ya mapinduzi. Wale waliokuwa wapo mbele walikuwa wakiwaambia wenzao kuwa wapo tayari na walikuwa wakisubiri saa itimie tu jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote ndani yake, ilipotimia saa na nusu L.J Ibrahim alitoka na kwenda kuangalia vikosi vyake kama vipo sawa na alipohakikisha vipo sawa alichukua simu ya upepo ambayo alikuwa akitumia kuwasiliana na M.J Belinda aliyekuwa ni kamanda wa kikosi cha ardhi kilichokuwa kipo mbele yao.

                 "Bado saa moja na nusu hadi hivi sasa tuanze operesheni yetu, msilewe maneno ya kiongozi wa dini aliyewekwa kitimoto kuubatilisha ukweli wake, ikitimia muda kamili ni kuhakikiha mnaanza operesheni tena ikibidi kuingia ndani" Aliongea akiwa ameshika simu ya upepo

                  "Mkuu" Sauti ya M.J Belinda iliitikia

                  "Operesheni ni kumuondoa Zuber tu na si kuharibu mali yoyote ya Ikulu, narudia tena si kuharibu mali yoyote ya Ikulu. Kuua hakuna labda iwabidi. Tunaelewana!"

                  "Mkuu"

                  "Vizuri, silaha ziwe tayari kabisa kwa muda huu"

                  "Sawa mkuu"

   Baada ya kumaliza kuongea na simu alitoa tabasamu la ushindi akiamini kuwa alikuwa amemaliza kila kitu, hakujua kabisa kuwa huyo aliyekuwa akimuonesha kuwa yupo kwa ajili ya kutii  amri zake alikuwa yupo kinyume kabisa na jinsi alivyokuwa akionesha utiifu kwa kwake. Yeye aliona kuwa kazi ilikuwa imeshaisha na sasa muda huo kilichokuwa kimebaki ni kwenda kumtoa Rais Zuber madarakani ili aingie kibaraka mkubwa wa waktu weupe waliokuwa wana nia mbaya na nchi hii, L.J Ibrahim baada ya kutoka hapo alienda kwenye ufukwe wa bahari ya hindi ambapo alikuta boti ndogo ikiwa inamsubiri, alipanda kwenye boti hiyo ambayo ilianza safari muda huohuo kuelekea kwenye Nyambizi ya kijeshi ambayo hadi muda huo bado ilikuwa imeibuka juu ikisubiria operesheni iishe ili vikosi virudi ndani ndiyo izame tena chini.


****


    Ndani ya Ikulu muda huo Moses pamoja na maafisa wengine wa usalama wa taifa walikuwa tayari wameshajiandaa vilivyo, walikuwa wapo tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitkeza humo ndani kwa muda wowote ambao walikuwa wamewekewa ahadi ya kuvamiwa na jeshi. Ikulu nzima ilikuwa imesheheni wanausalama hao ambao walikuwa wana silaha ndogo zenye hatari kubwa, walikuwa wamejipanga vilivyo kwenye maeneo mbalimbali ya Ikulu ambayo yalikuwa yamejificha kwa muda huo wa usiku.

    Rais Zuber hadi muda huo hakuwa amelala kama zilivyo siku nyinge ambazo alikuwa akishinda bila kulala kutokana na hofu aliyokuwa nayo juu ya mapinduzi aliyokuwa ameambiwa, alikuwa yupo ndani ya chumba cha mawasiliano pamoja ulinzi ndani ya ikulu akiangalia kile ambacho kilikuwa kikiendela baina yake na wanausalama wake na hata mawasiliano yaliyokuwa yakiendela.

    Moses alikuwa yupo naye akiwa na silaha yake iliyokuwa imening'inia kwapani na nyingine kiunoni, alikuwa amevaa shati pamoja na suruali ya kitambaa na miguuni alikuwa amevaa viatu vigumu vya ngozi. Yeye ndiye alikuwa akitoa amri kuu baada ya Rais Zuber muda huo ndani ya ikulu  hakukuwa na mwingine yeyote aliyekuwa akipinga amri zao, muda huo walikuwa wakiangalia mazingira ya hapo ndani ya ikulu kwa umakini sana kuhakikisha hakiharibiki kitu.

                 "Mheshimiwa usiwe na shaka kabisa ndani ya usiku huu, ikiwa kama operesheni fagio la chuma ndiyo ilikuleta wewe Rais mzalendo kabla hata haujafanyika uchaguzi mwingine ambao ulikupatia ushindi vilvile. Basi operesheni hii itahakikisha utaendelea kubaki madarakani kwa miaka mitano yako awali na hadi ukigombea tena ukipata ushindi" Moses aliongea huku akimshika Rais Zuber bega.


*JOSEPHINE KASABABISHA KAKIMBIA

"MSHAHARA WA DHAMBI NI UMAUTI MUFTI YAMEMKUTA

"WAPI N0001?

*JE MAPINDUZI YATAFANIKIWA


SEHEMU YA AROBAINI NA NNE HADI MWISHO NDIYO ZENYE MAJIBU USIKOSE
KUFUATILIA RIWAYA HII








No comments:

Post a Comment