RIWAYA: SHUJAA
MTUNZI: Hassan O Mambosasa
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
SEHEMU YA THELATHINI!!
Baada ya kutoka katika eneo hilo hakuwa na mahala pengine pa kwenda zaidi ya kwenda kuzunguka katika mtaa mwingine kama mzururaji, alizunguka katika kila mitaa na hatimaye akarudi kule kwenye mtaa aabao alikuwa ameegesha gari lake. Hapo alisaini kitabu kuwa ameshachukua gari na aliamua kuondoka huku akiwa amejipongeza kwa hatua nzuri aliyokuwa amefikia ndani ya siku hiyo tangu aanze kazi yake hiyo