Tuesday, March 21, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA


WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com




SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA!!
Ushahidi ambao ungeweza kumuweka huyo aliyekuwa akimkejeli nyuma ya nondo haukuwepo kabisa ndiyo maana alikuwa akitaabika yeye baada ya kukutwa na vidhibiti vyote vilivyokuwa  ni muhimu san kwa ajili ya kesi hiyo. Hakika alikuwa amepewa kesi ya kuiba Ng'ombe kwa kuwekewa mifupa ndani ya eneo lake, huo ulikuwa ni ushahidi tosha wa tuhuma hiyo ya kuiba Ng'ombe ambayo ilikua ikimkabili hakukuwa na ushahidi mwingine ambao ungeweza kumnusuru.





_________________TIRIRIKA NAYO

****

   Muda ambao alikuwa akiondoka Mheshimiwa Mahujuraja ndiyo muda ambao Norbert alikuwa akiingia kwenye nyumba moja ya kifahari sana iliyopo maeneo ya Mbezi. Alikuta mwanamke mtu mzima aliyekuwa amevaa kiheshima sana, alikuwa ni mwanamke ambaye alikuwa ni mchangamfu sana alidhihirsha uchanganmfu wake. Norbert alikaribishwa hadi ndani ya nyma hiyo kwa uchangamfua mkubwa sana kutokana na heshima aliyokuwa ameionesha kwa mwanamke huyo. Ndiyo matokeo ya uchangamfu huo aliokuwa ameupata hapo nyumbani, alikaribishwa hadi ndani ya nyumba hiyo ambapo alikaa kwenye kochi akiwa yupo sambamba na Mwenyeji wake.

"Karibu san mwanangu" Alizidi kukaribishwa na mama huyo


"Asante sana mama, Baba Askofu nimemkuta?" Norbert aliitikia ukaribihso huo kisha akauliza.

"Kabisa mwanangu umemkuta tena alikuwa akijiandaa kutoka ungechelewa kidogo usingemkuta"

"Sawa mama huu mguu ulikuwa wake"

"Haya ngoja nikamuite sasa hivi"  Mama huyo aliongea na kisha alielekea kwenye upande mwingine wa vyumba hivyo kwenye eneo ambalo lilikuwa na ukumbi mwembamba , zilipopita dakika takribani tano tangu aondoke aliingia Kardinali Michael akiwa ni mwenye usio na furaha kabisa kutokana na ujio huo wa adui yake

  Alibaki akimtazama tu  akiwa hata hajaketi kwenye kiti, Norbert alipomsalimia kwa uchngamfu yeye alikaa kimya tu na wala hakujibu salamu hiyo kutokana na kutofurahia ujio wake. Hilo halikumzuia kabisa Norbert asiendelee kutabsamu kwani alitambua Kardinali Michael hakuwa na ujanja kabisa baada ya kuwa yupo ndani ya nyumba ambayo kulikuwa na familia yake na si nyumba ile ambayo ingekuwa yupo yeye na wenzake.

"Baba Askofu wa nchi hii si nakusalimia jamani" Askofu alimuambia

"Kaila najua hukuja kwa heri hapa nyumbani kwangu naomba useme kilichokuleta na kisha uondoke upesi" Aliongea kwa sauti ya chini iliyojaa ukali

"Baba wewe si mtumishi wa Mungu jamani au biblia inakutuma ndiyo utuambie namna hiyo wanakondoo wako, mgeni kwako ni kiumbe kingine kichopaswa kupokewa kwa namna ya kipekee kabisa jamani si namna hiyo baba yangu" Maneno hayo yalipomalizwa yakiongelewa muda huonuo Kardinali Michael alijibandika tabasamu usoni mwake la ghafla sana, akiwa kwenye tabasamu hilo alionekana mtumishi wa ndani wa nyumba hiyo akileta vinywaji ambavyo aliviweka mezani kwenye eneo ambalo halikuwa mbali sana na alipokuwa Norbert akiwa amevamia ndani ya himaya ya adui yake.

"Karibuni" Mtumishi wa nyumba hiyo aliwakaribisha akiwa na tabasamu pana huku akimtazama bosi wake, ilimbidi Kardinali Michale ajongee hadi kwenye meza hiyo na akatwaa  bilauri mojawapo ya kinywaji hicho. Mtumishi huyo alipomuona bvosi wake amechukua kinywaji, alitoka kwenye eneo hilo kwani alitambua kabisa alikuwa hahusiki na maongezi yaliyokuwa yanaendelea hapo.

"Haya sema kilichokuleta hapa" Kardinali Michael aliongea kwa suati ya chini

"Baba Askofu ndiyo namna ya kumpa ukarimu mgeni hiyo uliyojifunza kupitia sheria za dini, ok tuachane na hayo nimekuja kukupa ujumbe murua sana" Norbert aliongea

"Usizunguke Kaila sitaki mchezo kwenye masuala kama haya hadi familia yangu wajue"

"Ok nimekuja kukuambiwa hivi kesho ni arobaini yenu"

"Unaongea nini wewe?"

"Naongea habari iliyotokana na sentesi, ambayo ilitokana na vichazi ambavyo vilitokana na kuundwa kwa maneno hadi yakaleta maana. Kesho ndiyo mwisho wenu"

"Kama umemaliza toka nje ya nyumba yangu haraka sana"

"Natoka ndiyo ngoja nimalize hii juice maana nimeandaliwa mimi, ni wasifu wafanyakazi wako kwa kujua kutengeneza Juice namna hii Bba Askofu" Alipoongea hivyo alikutana na uso ambao uliojaa chuki sana kutoka kwa Askofu ambaye alikuwa amekerwa sana na ujio wake, hilo hakulijali kabisa yeye aliachia tabasamu pana. Alimuambia kwa mara nyingine, "Hivi umejiandaa vipi kuingia ndani ya gereza lile  lilichongwa katikati ya Mlima kule Iringa maarufu kama Nyumba ya giza, utaiacha vipi familia yako na utaficha wapi uso wako na aibu hii"

"Kaila nakuambia kama huna la maana uondoke"

"Tulia basi hebu fikiri kwanza nikiondoka muda huu utamjibu nini mke wako kwani atahisi kuna namna"

"Sijali hilo mimi"

"Ok kama hujali ila ni hayo nilikuja kukuambia si unajua kama mwenye  kujua kila kitu kuhusu ripoti amepatikana sasa ujiandae. Jama Wa Majama yupo uraiani" Norbert alipoongea maneno hayo alimaliza Shurubati iliyokuwa ipo kwenye bilauri yake na kisha alisimama juu.

"Muite mama nimuage basi huoni itakuwa ni vibaya kuondoka wakati kanikaribisha kwa heshima sana" Aliongea huku akimtazama Kardinali Michael usoni, yeye hakuwa na ujanja kabisa kutokana maneno ahyo aliyokua akiambiwa. Ilibidi tu amuite mke wake ambaye alitoka hadi hapo alipo, aliagana na Norbert akiwa na uchangamfu uleule huku Mumewe naye akivaa tabsamu la bandia kutokana na kutokuwa na furaha muda mchache uliopita tangu alipotembelewa na huyo Adui aliyeigiza kama rafiki mbele ya mke wake.


  Norbert naye alipomaliza kumuaga mke Kardinali Michael hakutaka kabisa kuendelea kubaki kwenye eneo hilo, aliondoka kwa mwendo wa taratibu huku akisindikizwa na wenyeji wake hadi nje alipoegesha Pikipiki yake. Aliipanda  kisha akaiwsha na kuvaa kofia la kichwani, aliwapungia mkono wenyeji wake na kisha aliweka gia kuiruhusu pikipiki hiyo ianze kuondoka.  Alitoka hadi nje ya nyumba hiyo na aliendesha pikipiki hiyo hadi kwenye eneo ambalo lilikuwa na kituo cha kujaza mafuta, hapo aliegesha kando akiwa si mwenye hitaji la kwenda kujaza mafuta kwani Pikipiki ilikuwa mafuta ya kutosha ya kuzunguka hadi anamaliza kazi yake. Hapo alitoa simu yake ya mkononi nyingine kabisa tofauti na aliyokuwa nayo awali ambayo iliishia mikononi mwa maadui zake baada ya kumteka, aligusa mara kadhaa kwenye kioo hicho cha simu yake na kisha akaiweka sikioni baada ya kupata kile ambacho alikuwa anakitafuta

"Nahitaji sasa hivi uje Nyumbani kwa Kardinali, ufuatilie nyendo zake zote uje kunipa taarifa baadaye" Baada ya hapo alikata simu kisha akaiweka mfukoni na aliondoa Pikipiki  kwa kasi kubwa sana, hakuwa na muda wa kupoteza yeye alikuwa ameamua kumaliza kazi kwani alikuwa  amebakiwa  na siku moja tu ambayo ilikuwa ni inayofuata baada ya hapo atakuwa ameenda nje ya maagizo.


****


   GEREZA LA  NYUMBA YA GIZA
       KATIKATI YA MILIMA
         IRINGA


    Helikopta ya kampuni ya EASA ilionekana ikishuka kwa taratibu san katika eneo la ndani ya gereza hilo ambalo lilikuwa limenjenga katikati ya milima iliyokuwa mkonai Iringa ambayo ilikuwa imetobolewa kwa katikati. Helikopta hiyo ilikuwa ikishuka kwa taratibu sana kwenye eneo ambalo ndani yake kulikuwa na gereza jipya ambalo lilikuwa limejengwa kwa waliokuwa wakifanya matukio makubwa ndani ya Tanzania. Ujenzi wa gereza hili ulikuwa umelifanya liwe gereza kubwa nchi nzima na hakukuwa na gereza ambalo lilikuwa kubwa kushinda hili, lilikuwa limejengwa kwa taaluma ya juu wahandisi waliokuwa wameagizwa kutoka China ambao walipasua milima hiyo kati na kupelekea uwazi mkubwa sana ndiyo wakalijenga hilo Gereza. Eneo la katikati  kulikuwa na shimo refu sana ambalo lingegharimu karibia ghorofa tisa kiurefu kuweza kufika juu mtu akitokea chini, hii ilifanya iwe ngumu sana kwa mtu yeyote kutoroka ndani yake kwani hakukuwa na njia ya kutokea nje. Wafungwa waliokuwa wakiletwa ndani ya Gereza hilo walikuwa wakiletwa kwa kutumia Helikopta na hakukuwa na usafiri mwingine wowote wa kuwaleta kwenye neo hilo, ndiyo maana ikaitwa Nyumba ya giza ,asilimia kubwa ya eneo la ndani ya gereza hilo kulikuwa ukiongozwa na mataa maalum kwani mwangaza uliokuwa ukiingizwa ndani ya gereza hilo ulikuwa ni mdogo sana

   Helikopta hiyo ilipofika chini tu tayari maaskari wa jeshi la Magereza walikuwa wameshafika jirani nayo wakiwa na silaha nzito, ilikuwa imetua kwenye eneo maalum lililokuwa limejengewa kwa ajili ya kutua. Maaskari hao walikuwa tayari wameizunguka Helikopta hiyo wakiwa na silaha kwani walikuwa wakijua kabisa walikuwa wanakuja kupokea Mhalifu mwingine mkubwa, wahalifu wa eneo hilo wote walikuwa ni tishio hivyo ulikuwa ni muhimu katika kipindi chote wanaletwa kwani uzembe mmoja tu wangeweza kufanya maafa makubwa sana. Kila Mhalifu aliyekuwa akiletwa humo ndani alikuwa na utukutu wake, hakuna ambaye aliyekuwa humo ndani hakuwahi kabisa kukutwa na tuhuma ya kuua  au kufanya balaa zito. Asilimia kubwa waliokuwa wakiletwa humo walikuwa ni wale Magaidi na waliokuwa na makosa mazito sana.

  Helikopta ilipositisha kuzungusha upanga wake mlango mmoja ulifunguliwa, na kisha mwanamke ambaye alikuwa amevaa mavazi ya kawaida alishushwa akiwa amefungwa pingu kwenye mikono yake yote pamoja na miguuni. Mwanamke huyo alikuwa amefunikwa uso wake na aliposhuwa tu alikuwa ameshikiliwa mikononi na maofisa wawili waliokuwa wamevaa nguo nyeusi zilizo katika mfumo wa gwanda ambazo hutumiwa sana na wanausalama wa EASA wale waliokuwa kitengo kingine ambacho kilikuwa na sare kama jeshi. Maafisa haoo waliposhuka tu heshima za kutoka kwa wanajeshi wa jesi la Magereza ilitoka na kisha wakasogela karibu, walipeana mikono wanausalama hao na yule Mwanamke alichukuliwa na kuwekwa kwenye mikono ya jeshi la Magereza.

"Mzigo wenu huo, huyo ni  hatari sana zaidi ya hao wanawake wote walokuwa wapo ndani ya gereza hili. Mchungeni sana  atakaa humu hadi pale atakapohukumiwa na akihukumiwa atarudi tena humuhumu haya ndiyo maisha yake" Mmoja wa maofisa wa EASA  ambaye alikuwa mkubwa kuliko wengine aliongea.

"Usijali Kamnda amefika huyu hatoweza kutoroka" Afisa mmoja wa jeshi la magereza aliongea na kisha aliitoa kofia iliyokuwa imefunika uso akakutana na sura ya Josephine Msichna mrembo sana. Afisa huyo alimtazama Josephine usoni kisha akasema, "honekani kabisa kuwa ni mahlifu huyu ila hawa ndiyo zaidi ya hatari kabisa"

"Ana kesi ya kuua maelfu ya watu jijini Dar huyu, hivyo ujue nii zaidi ya hatari, chungeni sana huu urembo wake usije ukawahadaa mkautaka huo mwili ulio na umbo lenye kuvutia mtajuta sana  na atatoroka huyu" Aifa wa EASA aliongea

"Ha! Ha! Ha! Ha! Hakuna jambo kama hilo litakalotokea sisi tunajali kazi yetu siyo kuendekeza tamaa"

"Msione nawadhania dhana mbaya natambua kabisa maisha ya humu kukaa muda mrefu wanaume nyinyi mnazidiwa hapo muweke makini sana sisi tumemaliza wajibu wetu. Akitoroka huyo ndani ya gereza hili lililoshindikana  kupatania ya kufanya hivyo mkuu N001 atajua ni nyinyi sasa mjichunge sana nafikiri huyo mkuuwetumnamjua sana"

"Usihofu kabisa halitatokea hilo ndani ya gereza hili"

"Haya sisi hatuna la ziada tunaondoka" Baada ya hapo wote waliagana kwa namna ya kipekee sana, maofisa wa EASA wote walipanda helikopta yao n kuondoka katika eneo hilo. Maofisa wa jeshi la magereza waliokuwa wamempokea Josephine waliingia naye hadi ndani ya gereza hilo ambako kulikuwa na vyumba vyenye taa tupu, walitembea kwa mwendo mrefu sana wakashuka ngazi mbalimbali ambapo walikuwa wakielekea chini zaidi ya gereza hilo ambalo lipo katikati ya Mlima. Walifika kwenye ofisi maalum baada ya kutembea kwa mda mrefu kisha wakamkabidhi kwa Maaskari wa magereza wa kike na wakaondoka, alipokabidhiwa tu aliingizwa moja kwa moja kwenye chumba maalum ambapo alitolewa nguo zote.


  Zoezi la ukaguzi lilianza kwani walikuwa wakihofia huenda akawa ameingia na silaha humo ndani, baada yakuridhika kuwa hakuwa na silaha walimpatia nguo nyingine ambazo ni sare ya wafungwa gereza zenye rangi ya machungwa. Hapo walimpelekea hadi chumba kingine aliandikishwa kisha akatolewa, alikuwa akipelekwa kwa mkukuu sana kuelekea huko kulipokuwa na chumba cha kufungiwa. Mwendo huo aliokuwa akipelekwa ulikuwa ni kukera sana na ambapo alifikia muda akaamua kuwekwa mgomo kwani alikuwa hapendi kuonewa namna hiyo.


  Joephine hakutambua kabisa kuwa humo ndani kulikuwa na wajeuri watupu hata hao maaskari wenyewe walikuwa ni wajeuri pia ingawa walikuwa wamejipamba na kuonakana walikuwa warembo sana. Kugoma huko kwenda akiwa hajakaa sawa bada ya kugoma alichotwa mtama ambao ulipeleka chini mzima kutokana na pingu alizokuwa amefungwa. Akiwa hajaka swaa huko chini alipoanguka alipigwa virungu ambavyo havikuwa na idadi kabisa na hapo alijuta kabisa kugoma, alpokuwa akitoa ukelele wa maumivu wala hakujaliwa kabisa  na Maaskari hao wanawake walio jeuri kupitiliza. Alipozidi kelele aliongezewa mabuti kabisa ya sehemu mbalimbali za mwili wake, alitulia mwenyewe huku akigulia maumivu kwani   hakuona faida yeyote ya kupiga kelele.


  Wale Maaskari wanawake walipoacha kumpiga walimuinua juu kinguvu na kisha wakamtazama jinsi alivyo, Josephine alikuwa na manundu katika sehemu mbalimbali za mwili wake kutokana na kipigo hiko alichokuwa amepewa na watukutu.

"Leta ubishi tena tunakuvunja miguu, ukijifanya umepinda jua sisi tumenyongorota ndiyo maana tukatolewa magereza ya kawaida tukaleta humu" Askari mmoja wa kike aliongea na kisha akampiga kofi la kisogo la nguvu ambalo lilimfanya Josephine aone uchungu wa kupigwa na mkono uliokuwa umekomaa sana

"Ongoza njia kenge wewe" Kofi hilo liliambatana na kuambiwa maneno hayo, hakuwa na ujanja mwenyewe alikuwa mtiifu na aliongoza njia kuelekea huko alipotakiwa kwenda kwani alihofia angeweza kupigwa zaidi. Hadi hapo alikuwa hatamaniki kwa manundu katika sehemu mbalimbali za mwili wake, kuanzia usoni mkononi na sehemu zingine ambazo zilikuwa zikionekana ukiachilia mbali manundu mawili ya asili.

  Alipelekwa hadi ene ambalo lilikuwa na ngazi ambapo alisukumwa akiambiwa ashuke kwa haraka sana, Jopsehine alishuka kwa haraka akiwa anahofia kuongezwa tena kipigo kingine. Walikuja kutokea kwenye eneo ambalo lilikuwa na vymba vingi vya gereza vilivyojengwa kisasa zaidi tofauti na magereza mengine ya ndani ya Tanzania, alipokuwa akitembea kupita kwenye njia ambayo ilikuwa ikitenganisha vyumba hivyo baadhi ya wanawake wengine wataukutu walikuwa wakimnyooshea mikono kutamani sana angewekwa ndani ya chumba chake chao. Wao hawakusimama naye waliongoza naye hivyo  hadi kwenye chumba kimojawapo ambacho watu wake walikuwa wametulia, hapo Askari mmoja wa kike alifungua mlango na kisha akamsukuma  kwenye usawa wa mlango wa chumba hicho kilichokuwa kimejengwa kwa ukubwa wa wastani kikiwa na kila kitu ndani. Kilikuwa ni chumba ambcho kilikuwa na mwangaza kila muda huku ndani yake kukiwa na vitanda vitatu  vya kubebana. Ndani ya chumba hicho alishuhudia wasichana watatu wakiwa wamekaa wanacheza karata,alisimama mlangoni hapo akiyathaminisha mazingira ya humo. Kabla hata hajamaliza kuyathaminisha   alifunguliwa pingu zote alizofungwa na kisha alisukumwa ndani kwa nguvu.


ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment