Sunday, March 19, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA

WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com





SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA!!
Alipotolewa gundi iliyokuwa imeweka mdomoni, bado Kamishna alikuwa amepigwa na bumbuwazi la mwaka.

"Shemeji wewe ndiyo wa kunifanyia hivi kweli?" Happy aliuliza akiwa haamini kabisa

"Haaa! Kamishna hongera kwa kutumia nguvu zako nyingi na kumteka shemeji yako, ninataka utambue kuwa mimi sipo njiani wala nini. Nipo kitandani nimepumzika kesho naendelea na kazi yangu ya kuwatia matumbo ya kuhara" Sauti ya Norbert iliyokuwa imejaa kejeli ilisikika.



_________________TIRIRIKA NAYO


   Upande wa pili wa maisha yake alikuwa ni mwanaume ambaye alikuwa ni mwenye tamaa sana, fedha alikuwa nazo lakini bado hakuwa akiishiwa na tamaa ya kuztika za ziada. Mke alikuwa anye bado alikuwa haishi kutamani wanwake wengine kila anayekuwa ni mwenye kupendeza macho yake, hilo lilimfanya hadi afikie hatua ya kumtongoza shemeji yake ambaye alikuwa ni mdogo wa mke wake. Kamishna alikuwa akimtamani sana Shemeji yake kwa kipindi cha muda mrefu lakini alikuwa ameishiwa mbinu zote za kumuweka ndani ya umiliki wake, alikuwa hawezi kabisa kutumia jeuri ya fedha kwani huyo Shemeji yake naye alikuwa anazo na hakubabaika kabisa. Kila alipojaribu kuachia chombezo mnaso aweze kumpata aliishia kukataliwa kabisa, alipozidi kumsumbua aliwekewa kitisho cha kusemewa kwa mkewe. Hapo jeuri yoe iliisha na hakuwa na ubavu tena wa kuendelea kumsumbua, umbile la Shemeji yake halikuisha kabisa kumtesa na akatamani kabisa kuwa naye. Alikuwa ameshapuuzia kabisa naye alikuwa ameoa mwanmke mrembo sana ambaye alikuwa na kila kitu ambacho alikuwa akikitamani, sasa tamaa ndiyo ilikuwa ikimuongoza ya kuonja asali ya njiani wakati alikuwa nayo Kibuyu kizima ndani ya nyumba yake. Hadi inafika siku hiyo tayari ilikuwa imepita muda mrefu sana tangu akataliwe na Shemeji yake huyo ambaye alianza kujengea chuki dhidi yake, sasa amemteka bila ya kujua kuwa aliyekuwa akimteka alikuwa ni huyo Shemeji yake ambaye alikuwa amemuonesha  ya kila namna ili aweze kumshawishi kuwa naye lakini aligonga mwamba.


    Happy naye alipoona uso wa Shemeji yake mahala hapo alitambua kabisa kuwa ndiyo alikuwa akihusika na mchezo mzima uliokuwa umetokea, aliamini kabisa kwani alikuwa amewekewa chuki naye baada ya kukataa kuwa na mahusiano naye kutokana na kumuheshimu sana Dada yake. Alibaki akimtazama kwa mshngao sans na muda huo uso wa Kamishna ulikuwa umeingiwa unyonge wa hali ya juu,na moyoni alibaki akimtusi Norbert kwa mchezo aliokuwa amemfanyia.

"Shemeji kisa kukukataa ndiyo unadiriki kuniteka kweli" Happy aliongea akiwa hajui kabisa chanzo cha yeye kuwa hapo, muda huo Kamishna hakujibu kitu chochote aligeuka nyuma na kuwatazama vijana wake. Aliwaashiria kuwaita na wote walisogea karibu yake wakiwa wamekaa kiutiifu sana, uso wake ulikuwa tayari umebadilika kwani aliona vijana hao walikuwa wamefanya uzembe mkubwa sana kwa kumteka yule ambaye hakustahiki kutekwa kabisa.

"Nyinyi ndiyo niliyowatuma hii kazi, mpenzi wa Kaila ni  Shemeji yangu toka lini? Si nawauliza?" Aliongea wa ukali huku akiwatazama wote kwenye nyuso zao.

"Mimi ndiyo mpenzi wa Norbert Kaila kweli tangu nipo chuo" Happy aliongea na kumfanya Kamishna ageuke na kumtazama usoni mwake, jeuri yote ilikuwa imemuisha kwa kusikia jibu hilo na kisha na alimsogelea karibu Shemeji yake kwani roho yote ya ukatili ilikuwa imemtoka.

"Samahani sana Shemeji, sikukujua kama wewe ndiyo mpenzi wa yule Mhalifu. Unaowaona hao ni maaskari wote na Kaila amefanya kosa kubwa ndiyo tukatumia njia kwani ametukimbia" Alidanganya maneno ambayo yalimfanya Shemeji yake amuamini, aliamua kumfungulia hapo alipokuwa amemfunga baada ya uongo wake kumkolea kisawasawa Happy na kisha akaondoka naye.

"Hadi kesho mchana namtaka Norbert Kaila awepo kwenye mikono yenu" Aliongea kwa amri huku akimshikilia Shemeji yake ambaye alikuwa hatembei vizuri kutokana na kufungwa sehemu moja kwa muda mrefu sana.



****


  Ahueni ya ubavu wake alianza kuiona yalipoingia majira ya usiku kwenye nyumba ya kulala wageni aliyokuwa wamejihifadhi, Askofu Valdermar ndipo alipotoka nje ya eneo hilo akiwa amejikaza kisabuni katika kutembea sawasawa ingawa bado alikuwa yu mgonjwa. Pigo alilokuwa amepigwa na Norbert lilikuwa ni zito sana na laiti kama angekuwa hajabana pumzi wakati anapigwa, yanmgekuwa ni mengine kabisa kwani  angekuwa amevunjwa mbavu yake na Komandoo huyo mwenye mchanganyiko wa Ninja. Hakika alikuwa amewezwa sana na hata mawasiliano alikuwa amekata ndani ya siku nzima akiuguza maumivu yake hayo, alikuwa ni mwenye kuletewa vyakula kule chumbani na kuvila tu na hakuwa maetoka nje tangu alipoingia hapo.

  Dawa alizokuwa akizitumia tayari zilikuwa zimempa ahueni ambayo ilimfanya atoke hadi nje kwenda kupunga hewa kidogo, alipokuwa nje huko ndipo alipokumbuka kuwapigia simu watu ambao alikuwa na ushirika nao ili kuwaaambia kila kitu ya kilichotokea kwani aliamini kabisa walikuwa wakimtafuta sana yeye. Hapo alitoa simu yake na kumpigia Meshimiwa Roho kwani alikuwa akitambua kabisa kuwa Mheshimiwa moyo alikuwa hajiwezi na yu kitandani mgonjwa. Simu yake ilipopokelewa tu aliamua kueleza ukweli wa kile ambacho kilikuwa kimetokea hadi akawa yupo kimya namna hiyo, simu yake hiyo aliyokuwa ameitoa taarifa ilikatika  ghafla mawasiliano jabmo mbalo lilimfanya aingiwe na shaka kubwa sana.

"Norbert siku nikikushika nakugeuza supu, umemuua Scrpio na Spider vijana wangu tegemeo. Josephine pia sidhani kama ni mzima" Alijisemea mwenyewe akiwa ameuma meno kwa hasira sana kwani hadi muda huo alikuwa ameshatambua kabisa kuwa vijana wake wote walikuwa wameteketea, hakika hakutegema kabisa kuwa atakuja kuchezewa namna hiyo na kijana mwenye ngozi nyeusi katika nchi ambayo alikuwa akiidharau kila siku kutokana na hali yake ilivyo. Aliona ni kama alikuwa ameanikwa mbele ya hadhira kwa kitendo chake cha kuolewa na mwanaume mwenzie, akiwa amekaa kwenye eneo hilo aliamua kuzitafuta namba za mtu mwingine ambazo alizipiga mara moja na kisha akamueleza juu ya eneo ambalo alikuwepo. Aliahidiwa kuwa angefuatwa mara moja na mtu huyo kwani hakuwa na  mwingine angeweza kumuhifadhi kwa muda huo kwa haraka zaidi baada ya kukatika kwa mawasiliano na Mheshimiwa Roho.


  Haikupita hata  dakika thelathini gari laki fahari ambalo lilikuwa limeagizwa kuja kumfuata liliwasili, Askofu kwakuwa hakuwa na kitu cha muhimu ndani ya Nyumba hiyo ya kulala wageni aliyomua kulala  aliamua kujichukua yeye kama yeye na kuingia ndani ya gari hilo na kuondoka. Safari yake ilikuja kuishia kwenye nyumba ya kisasa kabisa iliyokuwa ipo Tabata Kinyerezi. Hapo gari hilo lilingia ndani ya uzio wa nyumba hiyo baada lango kubwa lililokuwa likiendeshwa kwa mtambo maalum kufunguliwa. Gari hilo lilienda hadi eneo la maegesho ambako alikuta kulikuwa na mwenyeji wake akiwa anamsubiri, Mwenyeji wake hakuwa mwingine ila ni Askofu mkuu wa kanisa katoliki Kardinali Michael Severine ambaye alikuwa yupo ndani ya mavazi ya  kiraia.

  Hapo wote wawili walikumbatiana kwani walikuwa wapo kwenye mnyororo mmoja wa uhaini wa nchi hii, huyu ndiye Askofu ambaye alikuwa yupo pamoja na Askofu Edson kwenye kisa cha WAKALA WA GIZA. Ndiye ambaye alimlaumu Askofu mwenzake kwa kufanya uzembe hadi akauawa kwa uzembe wake, ndiye huyuhuyu aliyeitwa ofisini mwa aliyekuwa Mnadhimu mkuu wa jeshi kupewa kazi maalum akiwa pamoja na Mufti. Walikuwa wapate ujira mkubwa sana kama nchi hii itakuwa imepinduliwa na kisha wao wawafanye raia wakubali mapinduzi haramu waliyokuwa wameyasuka.

  Mambo yalipozidi kombo aliamua kujifanya kinyonga na kisha akalaumu sana kiongozi wa dini ya upande wa pili kwa kushiriki usaliti wa imani yake. Baada ya Rais Zuber kurudi tena kuendela na shughuli zake yeye alimpa baraka zake zote, hii ilisababisha aongezekewe na heshima kwa kitu hicho ambacho haikustahiki apewe heshima hiyo.

  Mpango wa pili  wa kuifuja nchi ya Tanzania baada ya ule wa awali kushindikana yeye alikuwepo yupo ndani yake kama kawada, alikuwa bado yupo nao kwani kazi yake ilikuwa haijafikia kwa yeye kuweza kuifanya. Mambo yalipoharibika na kuelezwa kila kitu alituma gari kwa ajili ya kumleta Akosfu ndani ya nyumba yake hiyo ya siri, muda huo alikuwa naye wakiwa wapo hapo sebuleni kwa pamoja.

"Ndiyo Askofu nipe habari nzima yote" Kardinali Michael aliongea

"Mambo si mazuri kabisa huko Kadrino, Scorpio na Spider wameuawa na Joesphine katiwa nguvuni" Askofu Valdrmar alieleza

"Ni nani huyu anafanya haya au kuna mwingine?"

"Yuleyule kirusi hatari sana ambaye hajazuilika mpaka sasa ndiyo mfanyaji wa yote haya"

"Inamaana pamoja na kuongeza nguvu bado huyu kiumbe anafanya haya kweli"

"Huyo ni hatari sana na nilikuwa sijui kama ni hatari namna hii, hadi nilipopamnana naye. Tazama mwenyewe" Askofu Valderma ra alipoongea hivyo alifungua sehemu ya ubavu wake ambako kulionekana ni penye rangi  nyekundu kutokana na weupe wake"

"Huyu ni Norbert?"

"Ni kiumbe hatari sana na wala sikuwahi kufikiria kuwa kutatokea kiumbe mweusi akanifanya kama hivi, nilikuwa napambana naye kinguvu sana hasa baada ya kujua uhatari wake lakini kutokana na kumuwekea dharau mwanzo haya ndiyo yaliyonikuta"

"Pole sana Askofu, sasa inabidi upumzike hapa nitakuletea mtu akutibu mimi wacha nikimbie nyumbani kwangu kwani sikuiaga famili huko" Kardinali Michael alipoongea maneno hayo alisimama na kisha akatoka ndani ya nyumba hiyo akimuacha kiongozi wa dini wa kigiza mwenzake akiwa amepumzika sebuleni.


****
                          [4]
                   ASUBUHI ILIYOFUATA

  Siku zinayoyoma nazo na hatimaye zimebaki siku nne tu kati ya siku ambazo alikuwa amepewa Norbert kazi hii iwe kamili, asubuhi ya siku hii alitoka kwenye nyumba yake akiwa anatumia usafiri wake ule ule aliokuwa amepatiwa ofisini. Alivuta mafuta akiwa anaelekea katikati ya jiji la Dar es salaam, safari yake ilikuja kuishia kwenye jengo la Tancot 2 lililopo makutano ya barabara ya Sokoine na barabara ya Pamba katikati ya jiji a Dar es salaam. Ilikuwa ni kwenye makao  ya wizara ya uchukuzi nchini, hapo ndipo alipokuwa amepanga kuingia kwa siku  hiyo kuendeleza kazi yake iliyokuwa imeunyima kabisa muda wa kuwa karibu na famili yake. Hapo aliegesha pikipiki yake na kuizima na kisha akaweka ulinzi wa pikipiki yake kama ilivyo kawaida yake, alipiga hatua kuingia ndani ya jengo hilo ambalo lilikuwa lina Mlengwa wake ndani ya siku hiyo.


  Tayari Kirekod sauti kilikuwa kipo ndani ya mfuko wake wa suruali, alifika hadi mapokezi kwenye ofisi ya Katibu mkuu wa wizara hiyo aliyekuwa ana uhakika asilimia zote yupo ofisni kwake.
"Samahani dada habari yako" Alimsabahi Msichana ambaye alimkuta kwenye dawati la Kaitbu Mukhtasi katika ofisi hiyo

"Safi kaka yangu nikusaidie nini?" Aliitikiwa salamu yake na kisha akaulizwa shoda yake ambayo ilikuwa imemfanya kuja eneo hilo.

"Ninahitaji kuonana na Mheshimiwa nina mahojiano naye muhimu sana"

"Nimuambie nani upo hapa?"

"Mwambie Norbert Kaila yupo hapa" Norbeert alipojibu hivyo yule Msichana ambaye tayari alikuwa ameshanyanyua mkonga wa simu aliushusha mara moja akiwa ameingiwa na mshangao baada ya kusikia jina.

"Kumbe ni wewe jinsi ulivyo nilikuwa sijakujua, nice smile kama ulivyo uzuri wako" Aliongea huku akimtazama Norbert usoni, alipopewa tabasamu naye alilisifia tabasamu hilo.

"Uzuri lakini sikuzidi wewe kabisa, ukiongea unabaki kuwa mzuri, ukitabsamu unabaki kuwa mzuri, kila ukifanya unabaki kuwa mzuri. Nahisi ukilia pia unabaki kuwa mzuri vilevile" Maneno hayo yalimfanya atabasmau nusura atake kucheka lakini alijizuia kutokana na simu aliyokuwa ameirudisha sikioni kwa mara ya pili kupokelewa.

"Haloo! Bosi, Mwandishi Norbert Kaila anakusubiri hapa ana maongezi muhimu sana na wewe........Sawa" Aliweka mkonga wa simu mahala pake na kisha akamtazama Norbert akamuambia, "Kasema usubiri kidogo  atakuita uingie."


   Alipoambiwa maneno hayo wala hakuwa na ubishi kabisa yeye alienda kukaa kwenye kiti cha kusubiri, alikaa hapo kwa takribani dakika tano ambapo alimuona Mtu ambaye alikuwa amevaa nguo za Mafundi akisogelea eneo la Katibu Mukhtasi

"Dada Mzee kaniita huko ndani nikatengeneze koki ya sinki la kunawia" Aliongea fundi huyo

"Ok ngoja nimpe taarifa" Katibu Mukhtasi aliongea na kisha akanyanyua simu yake na kupiga kwa mara nyingine tena, alisikiliza simu hiyo kwa dakika kadhaa na kisha alikubali amari aliyokuwa amepewa.

"Unaweze ukaenda.....Norbert pia amekuruhusu uingie ndani anakusubiri huko" Alimuambia pia na Norbert ambaye alijinyanyua kwa taratibu sana,muda huo tayari yule Fundi ambaye alionekana alikuw ni mwenye haraka alikuwa ameshazama ndani ya ofisi ya Katibu wa Wizara hiyo.


  Alijiinua kwenye kiti hicho baada ya kuruhusiwa kuingia humo ndani, alitembea kwa mwendo wa taratibu sana na huku akiwa ameingiza mkono wake mfukoni. Alikiwasha kile kifaa chake alipokuwa ameingiza mkono huo mfukoni na kisha akausogelea mlango wa ofisi ya Mlengwa wake, alipiga hatua kuingia ndani ambapo alitokea kwenye ofisi ya kisasa sana iliyokuwa ina kiyoyozi ndani yake. Ubaridi wa kiyoyozi ndiyo ulimkaribisha kabla hata mwenye ofisi hiyo hajanyanyua mdomo wake kumkaribisha, alikutana na manadhari iliyokuwa imejaa usafi ulipitiliza ambapo mbele yake kulikuwa na Mzee wa makamo aliyekuwa ni mwembamba. Kichwani Mzee huyo alionekana ni mwenye kupungukiwa nywele sehemu ya utosini, alibakiwa na nywele  zilizopo juu ya paji la uso pamoja na nyingine zilizoanzia kwenye sehemu ya nyuma baada ya utosi huo. Alikuwa amevaa miwani ya macho ya bei ghali sana ambayo ilimkaa vyema, alikuwa amefuga sharubu za watani .

  Huyo ndiye alikuwa Katibu Mkuu wa wizara ya uchukuzi ambaye alikuwa akimlenga ndani ya siku hiyo, alipomuona tu alitabasamu na kisha akapiga hatua kusoge zaidi karibu aweze kumtia homa ya kuhara kama alivyowatia wengine aliowapitia kabla yake. Tabasamu la mwenyeji wake lilimfanya azidi kuwa na hari ya kuweza kumtia homa ya kuhara kwani alikuwa ni mmoja kayi ya waliokuweo kwenye orodha ile, alipopiga hatua hata hakufika hatua mbili. Alisikia kitu kizito sana kikitua kwenye eneo la chini kidogo ya kisogo chake.

   Taratibu alianza kujisikia hali ya kupungua uwezo wake wa kuona na huku kizunguzungu kikali kikimkumba, alipomtazama Mwenyeji wake alimuona akiwa na tabasamu lilelile. Norbert aliishiwa nguu kabisa na alianza kwenda chini kwa taratibu huku akisikia kicheko cha kejeli kutoka kwa Mmiliki wa ofisi hiyo.

"Kailaa umepata ulichoki.." Maneno ya mwisho kuyasikia ndani ya masikio yake yalikuwa ni hayo, tena hayakumalizika kabisa kwani fahamu zilikuwa zimeshamtoka tayari. Hakika alikuwa amepatikana kabisa kutokana na kuzidiwa mbinu, sasa hana uwezo kabisa wa kufanya kingine chochote.


  Mwenyeji wake pamoja na yule Fundi ambaye alikuwa yupo ndani ya ofisi hiyo ambaye mwanzo hakumtilia maanani, walipeana ishara ya dole gumba. Kitendo hicho ilikuwa ni mpango kabambe uliokuwa umesukwa na ukasukika, wote walibaki wakitabasamu kwa kuweza kumtia nguvuni kwani tayari sifa zake walikuwa wameshazisikia kama alikuwa ni mjanja sana. Mwenyeji wake alinyanyuka pale kitini alipokuwa amekaa na alijongea hadi eneo ambalo Norbert alikuwa ameangukia, alimpiga teke la kumsukuma na kupelekea ageuke chali kwani alikuwa yupo kifudifudi.

"Simba hachezewi sharubu hata siku moja, sasa kakuparua na kucha"  ALiongea huku akimtazama mateka wake kwa dharau kuu.

*NORBERT KAPATIKANA



ITAENDELEA!!


No comments:

Post a Comment