Thursday, March 16, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com




SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO!!
Kuwafuata wale ambao walikuwa wao mnyororo hatari ilikuwa ni kamari ya kifo lakini alikuwa akijiamini sana, pamoja na hayo alipokuwa kwenye eneo hilo alikumbuka kumshukuru Mungu kwa hatua hiyo aliyokuwa amefikia. Pamoja na kuwa ni mtu ambaye alikuwa  haishi kubadili wasichana bado alikuwa akimkumbuka Mumba kwani imani ilikuwa ipo ndani yake, ndiyo maana alimshukuru ingawa alikuwa akimuasi sana muda mwingine aliokuwa yupo kwenye kazi yake.

  Akiwa yupo kwenye kutoa shukrani hizo kwa aliyemjalia pumzi, simu yake ya mkononi iliita, alipoangalia jina la mpigaji alikuwa ni Kamishna ambaye alikuwa ametoka kumtia homa isiyohitaji  tiba muda mfupi uliopita.





___________________TIRIRIKA NAYO

  Aliamua kuipokea hiyo simu ambayo ilikuwa imeingia kisha akaongea,"Yes Hellow.....nani.....No! No! No! Kafanya nini huyo tena hana kosa ni mimi mwenye makosa....sawa nitakuja"


  Baada ya hao simu ilikatika ambapo ilimfanya Norbert abaki akitabasamu kwani alikisia kile ambacho kilikuwa kimetokea, safari yake ya kuelekea huko alipoelekea ilikuwa ni kutoka na kukisia kitu na ndiyo hicho kimetokea.  Alijua mmojawapo kati ya wale wahalifu atampigia simu na ndiyo huyo kapiga, kikubwa kilichokuwa ndani ya simu hiyo ilikuwa ni kutiwa nguvuni kwa Happy ambapo aliambiwa ajisalimishe ili ampate. Hilo lilikuwa ni jambo ambalo sawa na kitendawili kwa Norbert kwani hakuwa tayari kabisa kujisalimisha kisa Mwanamke, ambaye alikuwa amemfanya makusudi akijua kabisa maadui zake walikuwa wakijiwashia moto wenyewe. Hakutaka kabisa kwenda huko alipokuwa ameambiwa aende ili akampate akiwa na ushahidi wote alikuwa ameukusanya, alimua kubaki hapohapo ndani ya nyumba yake.


****



        ALASIRI

 "Jamani hebu fikirieni vizuri Mheshimiwa Rais akijua tutakuwa vipi?" Bi Kishimba aliuliza

"yaani ni tabu tupu hapa jamani fikireni sura zetu tutaziweka wapi?" Bawana Mushi naye aliongea akionekan kuchanganyikiwa kabisa kwa homa aliyokuwa amepewa na Norbert ambaye alikuja kuvamia ofisi yake mara moja, wote walikuwa wamechangayikiwa ila Kamishna pekee ndiyo alikuwa ana afadhali.

"Jamani huyu mtu kashakuwa mnyonge uoga wa nini sasa?" Kamishna aliuliza


"Mnyonge! Hivi  unafikiri yule kijana ni yupo namna hiyo nakuambia hapa akiliona jua huyu hadi Mheshimiwa Rais anarudi safari yake jua  tumekwisha" Bwana Mushi aliingilia huku akimshangaa Kamishna.

"Hata mimi namshangaa huyu jamani hivi anamjua huyo kijana kweli" Bi Kashimba naye alionesha kumshangaa Kamishna

"Alivyotoka tu ofisini kwangu niliwapa amri vijana wangu wamfuatilie,kaja kuishia Kimara kwenye nyumba ya Hawara wake na vijana wameshuhudia akipigana mabusu na huyo mwanamke. Sasa nimemteka muda mrefu namsubiri ikifika jioni tu ajilete atoe ushahidi wote na kisha nimuue tu akinipa huku hawara wake akiona hamna namna hapa" Kamishna alieleza na kupelekea wote watabsamu kwani ilikuwa ni mbinu nzuri sana.


"Hapo Kamishna nakubaliana na wewe, amani itakuwpo namna hiyo. Umeweza sana kufanya hivyo. Mwanamke ni udhaifu mkubwa sana" Bi Kishimba aliongea huku akishusha pumzi

"Ndiyo mpunguze presha nyinyi mtakufa bure, huyu kijana hiyo JKT aliyoenda inamdanganya  sasa nafikiri nimuambie na Mheshimiwa kuhusu hilo ili aje kumshuhudia" Kamishna alipoongea hivyo alitoa simu na kutafuta namba ya Mheshimiwa wa upande wao, aliipiga kisha akaweka sikioni baada ya simu kupokelewa.


"Haloo  Mheshimiwa......si kwema Norbert Kaila kaja ofisinni kwangu, kwa Mushi  na Bi Kishimba pia katuambia kuhusu mishe zetu na kasema anatoa kwenye gazeti........nimeamua kumshika malaya wake nimuambie aje kujisalimisha maana ni mtu mdogo sana.......nini? Unasem kweli Mheshimiwa basi nitakuwa makini sana naye kuanzia hivi.....sawa" Baada ya hapo alikata simu kisha akawatazama wenzake ambao walikuwa wametulia kimya wote kutokana na yeye kuongea na simu hiyo.

"Jamani kuna jipya limezuka huko nilipompigia simu Mheshimiwa, inabidi tuwe makini sana na huyu kijana kuanzia hivi sasa" Aliongea kwa utulivu mkubwa

"Come on! Nyoosha maelezo wewe mbona hatukuelewi" Bwana Mushi aliongea kwa jazba baada ya kuona anazungushwa sana hasa ilipotolewa hiyo kauli mpya

"Norbert Kaila kwa mujibu wa maelezo ya Mheshimiwa huu uandishi wa habari ni zuga yake tu, ila huyu kijana na Agent hatari wa EASA nafikiri unawajua hawa watu ni bora hata ukavaane na makomandoo" Kamishna alieleza, wote walipigwa na mishtuko kutokana na taarifa hiyo.

"Are you serious?" Bi Kishimba aliuliza akiwa asiyemini kutokana na muonekano wa Norbeet ulivyo

"Toka lini nikawa nipo kwenye utani kwenye masuala kama haya, hapa, huu ndiyo ukweli" Kamishna alilijibu swali la Bi Kishimba ambaye aliingiwa na uog upya baada ya kusikia suala hilo.

"Kwahiyo ndiyo huo mtego kauruka au vipi?" Bwan Msuhi naye aliuliza

"Hajauruka jamani mwanamke ni zaidi ya ukosefu wa kiungo cha mwili atakuja mwenyewe, ila Meshimiwa katuambia tuwe naye makini sana ana akili nyingi sana" Kamishna alieleza

"Yaani mimi sida yngu huyu mtu asipumue tu huenda kashaunasa ushahidi wote uliokuwa ukihitajika na hata ile ripoti ipo mkononi mwake" Bwana Mushi aliongea


"Yaani atatuvurugia kabisa mipango yetu, mkumbuke mimi nataka nigombee Ubunge kwetu uchaguzi ujao sasa yeye ataharibu kila kitu" Bi Kishimba aliongea

"Hilo msihofu jamani hata mimi nina akili vilevile tutakutana huko" Kamishna aliongea kwa kujiamini

"Kamishna tusijiamini hivyo umakini utapungua kwenye kiumbe hatari kama huyu, cha msingi ni kuwa makini tu." Bwana Mushi aliongea na kisha akanyanyuka kwenye kiti na akasema,"jamani wacha niwaache kuna bibie leo ananisubiri mida hii"


"Hay msalimie sana najua ni mtoto wa chuo huyo damu changa kabisa" Bi Kishimba alitia utani na kupelelekea wote wacheke sana.

"Yaani kama ulikuwa vile huyo mwenzetu ni wa mali mpya" Kamishna naye alitia utani

"Maisha yao ya shida wacha tuzitumie shida zao tu kwa tunakivuna wewe" Bi Mushi aliongea  huku akimalizia kutoka nje na kuwafanya wote waliokuwa humo ndani waendelee kucheka.


****



  WIZARA YA NISHATI NA MADINI
     OFISI YA KATIBU MKUU


    Muda huo ambao waki na Kamishna walikuwa wamekaa kikao cha dharura, Norbert alikuwa ameshatia mguu kwenye ofisi ya wizara ya nishati na madini. Huko alipanga kwenda kuonana na Mhusika mwingine ambaye alikuwa yupo kwenye mzunguko wa pili ndani ya orodha hiyo, alikaribishwa kama alivyokaribishwa alipoenda hukoh awali na Katibu mkuu wa wizara hiyo ambaye alikuwa akijiandaa kuondoka. Uzito wake pamoja na kazi zake ndani ya jamii ndiyo vilimfanya Katibu mkuu huyo asitishe kuondoka na abaki akimsikiliza yeye kwanza kabla hajaianza safari ya kuondoka hapo ofisini, Kijana huyu machachari alipoketi kwenye kiti tu aliachia tabasamu pana na kisha akamtazama Mwenyeji wake.

"Ndiyo Bwana Kaila ni adimu wewe sana kuja sehemu kama hizi na ukija basi kuna jambo" Aliambiwa maneno ambayo yalimfanya azidi kutabasamu.

"Na uadimu wangu ukipungua ujue kuna jambo zito sana" Aliongea akiwa ni mwenye tabasamu.

"Ndiyo ndiyo leta habari"


"Mzee wangu nimekuja kukumbusha tu ile kazi uliyoifanya ambayo hukupata malipo sasa ndani ya siku ya Ijumaa utayapata tu"

"Kazi ipi Kaila mbona sikuelewi unachoongelea, hebu funguka Bwana hatupo kwenye vitadawili hapa"

"Ile kazi ya kuwasaliti watanzania na kutumia mapato ya wizara hii vibaya pamoja na kumfanya mkuu wako wa kazi aingie rumande basi malipo yake yamefika usubiri ujira wako akija Mheshimiwa Rais"

"Ndiyo hilo tu Norbert sasa nikuambie hivi wewe bado ni kijana mdogo sana, hayo mambo acha nayo huwezi kufikia malengo yako ya maisha ukijifanya unayafuatilia Kaila. Tutakuzika mapema sana" Katibu mkuu aliongea huku akiminya kitufe kilichopo mezani kwake

"Kufa ni bora kuliko kuishi na viwavi wanaofuja nchi"

"Ok sasa subiri utajua kwanini nilikuambia hivi" Alipoongea hivyo Kaitbu mkuu wa wizara  aliingiza mkono kwenye meza yake na kisha akaibuka na silaha ya moto.

"Sasa Mzee wangu bastola kama hiyo ukinifyatulia hapa si itatoa sauti na wewe uje kushikwa"

"Sijali kuhusu hilo sitofungwa Pesa inaongea" Maneno hayo yalipotoka bastola yake tayari ilikuwa imeelekea kwa Norbert ambaye alikuwa nayo kwa umbali wa mita moja, Katibu mkuu walikuwa amenyoosha mkono wenye bastola kumuelekezea akijua kuwa ndiyo alikuwa amemaliza kazi.

  Kitendo cha kuwekewa bastola namna hiyo akiwa amekaa kwenye kiti aliamua kuchekecha akili kwa haraka sana, alimtazama mwenyeji wake huyo akiwa amefikia hatua hiyo ambayo alikuwa hakuitarajia kabisa. Alitarajia angemuona akichachawa kwa taarifa hiyo na badala yake aliwekewa bastola kuelekea lilipo paji lake la uso, mweyeji wake alikuwa ni mwenye uso usio na mzaha hata kidogo alipokuwa amemuwekea bastola hiyo.

"Kwahiyo pesa  ndiyo itakuweka wewe huru siyo?"  Aliuliza akiwa na lengo la kutafuta nafasi ya kujiokoa kwani  Mwenyeji hakuwa ametambua kama yeye ni kiumbe mmoja hatari sana

"Wewe kajamba nani unaetupekenyua ili upate cha kujaza kwenye jarida lako tuone huo uzalnedo wako utakusaidia nini" Katibu Mkuu aliongea akiwa ni mwenye kuweka jeuri mbele kutokana na cheo alichokuwa nacho.


"Tatizo unajidai una jeuri hata unajisahau kama kuna watu wamekuweka kinasa sauti hapo kwenye mfuko wa shati kinarekodi  yote" Norbert alitamka kauli hiyo ilimfanya mwenyeji wake atazame mahali ulipo mfuko wa shati lake nadhifu, hiyo ilikuwa ni hila kwani alipotazama eneo hilo alisahau kabisa kuwa alikuwa amefanya kosa ambalo lilikuwa likingojewa kwa hamu san. Kitendo cha kuhamisha macho kuelekea ulipo mfuko wa shati ni jambo ambalo halifai kabisa kwa mtu kama huyo aliyekuwa naye ofisini huyo, mtu ambaye alikuwa na kasi zaidi  yake.

  Kitendo cha Katibu mkuu kuhamisha macho hadi kwenye mfuko wa shati lake tayari alikuwa ameweka balaa jingine kabisa, Norbert kwa kasi ya ajabu kabisa aliunyanyua mguu wake mmojwapo akiwa amekaa hapohapo kwenye kiti. Aliupiga mkono wa Mwenyeji wake uliokuwa umeshikilia bastola na kupelekea bastola hiyo ianguke pembeni mbali na hapo. Hakukaa tena kwenye kiti yeye ajifyatua kwa haraka sana na akaruka saraksi moja maridadi sana, baada ya kutua kwenye upande wa pembeni kwa kasi ya ajabu sana alipiga saraksi ya 'roll akaifikia bastola hiyo ambayo aliitwaa na mikono yake.

   Kilikuwa ni kitendo ambacho alikifanya hakikuzidi nusu dakika baada ya mwenyeji wake kufanya kosa la kitoto sana, mwenyeji alipopigwa teke hilo alikuwa akiangalia ilipokuwa ikienda kuangukia bastola yake. Alipokuja kurudisha macho kwenye eneo ambalo alikuwa yupo Norbert hapo, hakumuona kabisa kutokana na wepesi alioufanya. Aliporudisha macho kule ambapo ilikuwa imeanguka bastola yake alimuona akiwa amesimama ameishikilia. Loh! Aliona ni kama alikuwa amefanya uchawi kuweza kutoka pale alipokuwa kusogea pembeni, hakika hakuwahi kumuona kiumbe wa aina hiyo. Alibaki akiingiwa na uoga akiamini kuwa Norbert alikuwa ni mshirikina ndiyo maana alikuwa amefanya  hayo ya ajabu ya kupoteza na kutokea pembeni. Alishindwa kuongea kitu chochhote zaidi ya kubaki na uoga wake, alikutana na uso wenye tabasamu pana sana kutoka kwa huyo aliyekuwa amefanya jambo la ajabu hadi akamuweka kwenye hali ya uoga namna hiyo.


  Norbert hakujishughulisha na kuongea kitu chochote alipoona Mwenyeji wake akiwa amekumbwa na uoga, yeye alitoa Kirekodi sauti kama ilivyo kawaida yake na akasitisha kurekodi. Baada ya hapo kama kawaida aliicheza sehemu aliyokuwa ameirekodi na kisha akatulia, mazungumzo yote yaliyokuwa yakiongelewa ndani yaofisi hiyo yaliweza kusikika. Hapo Mwenyeji wake aliingiwa na kihoro sana kwa jinsi alivyokuwa ameingizwa kwenye mtego , alibaki akiwa ameganda asiongee chochote hadi pale Norbert alipositisha kuicheza sauti hiyo kwenye kifaa chake. Akiwa ameganda hivyohvyo asijue la kufanya, alimtazama Mgeni akitoa kibebea risasi cha bastola yake kisha akazitoa risasi zote. Alirushiwa bastola yake ambayo alikurupuka kuidaka huku akimtazama Norbert kwa uso uliojaa huruma sana, huruma hiyo haikubadilisha kitu chochote kwa mgeni wake huyo aliyekuja kumtia homa ya matumbo. Alimshuhudia akigeuka na kuanza kupiga hatua kuelekea mahali ulipo mlango, alipofika mlangoni alimshuhudia akizitia risasi zake zote kwenye chombo cha kuwekea takataka na kisha alitoka nje. Alibaki akimsindikiza kwa macho na si kuongea chochote kwani hakuwa  hata na ujasiri wa kuongea, pindi alipotoka tu ndipo alipokimbia hadi kwenye chombo kile cha uchafu akachukua risasi zake na kuzirudisha ndani ya bastola na kisha akarudi kitini. Alitambua kabisa hakuwa na uwezo wa kumfanya kitu chochote Norbert ikiwa atauvuka mlango wa ofisi yake, tayari ameuvuka na kaondoka kwa kutumia ujanja wake.


****


         JIONI
  Baada ya kutoka kazini kwake kituo cha kwanza ilikuwa nikwenda hadi eneo ambalo alikuwa ameweka chambo, ni katika eneo ambalo wale vijana wake wote waliokuwa wakimfanyia kazi walikuwa wakikaa na pia kuweka mikakati yao mingine. Kamishna alikuwa akielekea huko akiwa ni mwenye furaha sana kwani alikuwa ameshapata habari nzuri ya kukamatwa kwa mpenzi wa Norbert ambaye alikuwa akijifanya ni jeuri sana. Alipofika kwenye mlango la makao hayo ambayo ilikuwa ni sehemu ya kutengeneza magari iliyojengwa kisasa iliyokuwa haitumiki, aliamua kutoa simu yake mfukoni na kuzitafuta namba za Norbert. Alikuwa yupo jirani na vijana wake ambao walikuwa wakimsubiria kwa hamu sana wakiwa na imani zote kiongozi wao atafurahia kazi waliyokuwa wameifanya, muda si mrefu simu yake ilipokelewa na mtu huyo aliyekuwa anampigia.

"Kaila kijana wangu hivi una jeuri gani wewe? Tukimchinja huyu hawara yako unafikiri utakuwa kwenye hali gani? Hebu fikiria kuhusu hilo siyo kuzidi kutuletea wazimu wako. Sasa ni hivi nakuomba ujisalimishe mwenye kama unampenda huyu mwanamke la si hivyo utakuta maiti yake....siyo nisifanye hivyo nakupa saa moja tu uonekane eneo la Yombo daraja la Tingatinga uletwe huku la si hivyo utaiokota maiti ya huu hawara wako kesho hapohapo....good boy uende na muda" Alipomaliza kuongea na simu alikatana kisha akawatzama vijana wake akawaambia,"Twendeni mkanioneshe huyo malaya wake".

  Kauli hiyo iliwafanya vijana wake hao wageuke na kuelekea huko walipomueka Happy, waliingia ndani ya eneo hilo hadi kwenye sehemu ambayo ilikuwa na magari mabovu mwengi sana. Walitembea hadi mwisho kabisa wa eneo ambapo kulikuwa na mashine ngumu sana  ya gari ambayo ndiyo Happy alikuwa amefungiwa hapo. Muda huo alikuwa akijitikisa sana lakini hakuweza kabisa kutoka, alikuwa amevishwa kofia nzito sana usoni ambayo ilifunika uso wake hadi shingoni. Hakika alimuona ni Mwanamke aliyekuwa na umbo la haja ambalo hata yeye lilimtamanisha sana, kwa umbile hilo aliona kabisa Norbert angejileta mwenyewe.


  Alisubiri kwa muda ambao alikuwa amemwambia Norbert lakini hakutokea kabisa, hilo lilimuudhi na akaamua kumpigia simu kwa mara ya pili tena na muda huo aliweka spika kubwa kabisa. Mlio wa kuita kwa simu ulisikika na muda huo tayari alikuwa amekasirika kwa kutofika kwa Norbert ndani ya eneo hilo, simu ilipopokelewa alikuwa tayari ameshapandwa na jazba kwa kufanyiwa uhuni namna hiyo.

"Kijana hujui kutunza ahadi zako siyo sasa namkata kichwa huyu malaya wako" Aliongea kwa hasira

"No! No! No! Kamishna ninakaribia kufika sasa hivi nipo njiani, muweke kwanza  nimsikie yeye mwenyewe" Sauti ya Norbert ilisikika, hapo Kamishna alisoge hadi karibu ya Mwanamke huyo aliyekuwa na mvuto ingawa alikuwa na mwili mkubwa kisha akaamrisha vijana wamtoe kitambaa kile kilichoficha uso wake.

 Kitendo cha kutolewa kitambaa kwa Happy ilikuwa ni mshangao mkubwa sana kwa Kamishana, hakika hakutarajia kabisa kuwa angekuwa ni huyo mwanamke ambaye alikuwa ni mtu wake wa karibu sana. Alipotolewa gundi iliyokuwa imeweka mdomoni, bado Kamishna alikuwa amepigwa na bumbuwazi la mwaka.

"Shemeji wewe ndiyo wa kunifanyia hivi kweli?" Happy aliuliza akiwa haamini kabisa

"Haaa! Kamishna hongera kwa kutumia nguvu zako nyingi na kumteka shemeji yako, ninataka utambue kuwa mimi sipo njiani wala nini. Nipo kitandani nimepumzika kesho naendelea na kazi yangu ya kuwatia matumbo ya kuhara" Sauti ya Norbert iliyokuwa imejaa kejeli ilisikika.


ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment