Wednesday, March 15, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE

WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com





SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE!!

"Kwahiyo unanipa hongo siyo"

"Hapana"


"Natoka mama maana ulishaniambia ila ukumbuke kabisa haya niliyokwambia kwani mwenzenu Khemiri ni marehemu sasa mzigo wake mtaubeba nyinyi" Norbert alingea na kisha alitoa Kirekodi sauti kingine ambacho klikuwa tofauti na kile cha awali, alikisitisha kurekodi na kisha akacheza sehemu ile ambayo alikuwa amerokodi . Sauti ya maongezi yao ndani ya ofisi hiyo yalisikika wazi ambapo Mwanamama huyo alizidi kuchanganyikiwa.






________________TIRIRIKA NAYO

   Alipotoka ndani ya ofisi hiyo akiwa amemuachia mlengwa kivumbi cha roho, aliamua kwenda eneo la maegesho na kupanda pikipiki yake. Aliondoka moja na safari ya kwenda kwingine alikuwa imeanza kwani orodha kamili aliyokuwa nayo, ilikuwa bado haijaisha kabisa na ilimbidi akakutane na wahusika wengine waliokuwa kwenye mnyonyoro mmoja. Safari yake iliishia kwenye makao ya jeshi la polisi nchini, hapo aliweka pikipiki kwenye eneo la maegesho na kisha akafungua sehemu maalum ya kuweka mizigo midogo akatoka Kirekodi sauti kingine. Kama kawaida yake aliomba kuonana na mlengwa mwingine kabisa aliyekuwa akimlenga. Kitendo cha kuwa mtu ambaye alikuwa ni mzalendo katika mambo mbalimbali, aliruhusiwa kuingia ndani ya ofisi ya Mlengwa baada ya kutoka ruhusa lwa Mlengwa akijua kuwa ulikuwa ni ujio ambao ulikuwa wa kawaida sana. Mlengwa wa ofisi yake alijua wazi huenda alikuwa akija kuulizwa mambo yanayohusu taratibu za jeshi la polisi kabla ya Mwandishi huyo hajaandaa jarida lake lenye mashiko sana kwa jamii, alikaa ndani ya ofisi yake akiwa amevaa vazi la jeshi la polisi ambalo lilikuwa likionesha ni jinsi gani alivyokuwa na cheo kikubwa sana ndani ya jeshi hilo.

  Aliweza kumshuhudia Norbert akiwa na tabasamu lake lile sliingia humo ofisini, alimkaribisha kwenye kiti akiwa na tabasamu vilevile kutokana na ujio wa mwandishi wa habari huyo. Alimuacha hadi akaketi kisha akamtazama kwa mtazamo uliokuwa ukionesha alikuwa tayari kumsikiliza, mtazamo huo ulimfanya mgeni wake kuamua kuongea kile kilichokuwa kimemleta eneo hilo.


"Kamishna nimekuja kukumbusha tu" Norbert alisema

"Ndiyo Kaila kunikumbusha nini?" Aliuliza akiwa ni mwenye shauku ya kutaka kujua hicho kitu.

"Mzee lile deni lako la kuamrisha vijana wako wahakikishe wanapitisha mizigo yenu haramu kule Bandarini na ile isiyo na kodi, sasa ni muda wa kuilipa kwani waliyokuwa wamekupa nafasi hii wanahitaji ulilipe"

"Kijana sikuelewi"

"Utanielewa tu Mzee wangu,sasa huvi nimetoka Bandari kwa Mr Mushi kisha nikapitia TRA kwa Mrs Kishimba. Wote hao ni wenzako na nafikiri mnajuana, sasa ni hivi napenda ujue kuwa muda wenu wa kulipa lile deni lenu la kupewa  madaraka na kuyatumia vibaya umefika. Ujitahidi kulilipa"

"Kaila! Naona umekuja kunitukana ofisini kwangu sasa naomba utoke kabla sijakutupa ndani ukanyee debe, sishindwi kukupa kesi usionekane kwenye uso wa dunia ukaenda Nyumba ya giza wewe"

"Ohoo! Bado upo kwenye deni la kukitumia cheo chako vibaya na sasa unataka kujiongezea deni jingine siyo, Mzee wangu utaishia pabaya haya yote ninayaandika kwenye jarida"

"Naona hunijui vizuri wewe ngoja nikuonesha mimi ni nani, sasa tuone na hicho unachokiandika utapata faida wakati ni wa kuozea jela wewe" Aliongea huku akinyanyua mkonga wa simu yake  akianza akjiandaa kubonyeza badhi ya tarakimu, kitando hicho kilimfanya Norbert aingize mkono mfukoni mwake na kutoa Kirekodi sauti ambacho kilikuwa ikirekodi, alikisimamisha na kisha akaicheza nafasi ile ambayo aliitumia kwenye mazungumzo. Maneno ambayo yalikuwa yakiwatoka kipindi chote cha mazungumzo yalikuwa yakisikika vyema kwenye Kirekodi sauti hicho, mkonga wa simu aliokuwa ameushika akiwa anajivunia jeuri ya kuwa na cheo kikubwa. Alijikuta akiuachia bila ya kupenda na akabaki akimtazama Norbert kwa jicho la huruma kwani alishajua kuwa alikuwa ameshika makali na mgeni wake ameshika mpini, baada ya kusikika kwa sauti hiyo Norbert alisimama akabaki akitabasamu tu na kisha akakisitisha kile Kirekodi na kukitia mfukoni mwake.


"Kwaheri Mzee wangu tutakutana siku ambayo uso wako utakuwa na aibu kama umefumaniwa na Mama mkwe wako" Norbert alimuaga akiwa anamtazam kwa tabasamu la kejeli Kamishna yule ambaye alikuwa ameingia na unyonge wa ghafla

"Kaila kijana wangu subiri tuzungumze" Alimzuia na kupelekea aliyemvurga kichwa chake ageuke na kumtazama akiwa na macho ya kumsikiliza kile atakachokisema, muda huo hakujua kabisa kuwa kile Kirekodi sauti kilikuwa na uwezo wa kurekodi sauti zaidi ya mara moja. Kitendo cha kumsimamisha tu Mtibuaji huyu wa usalama wake alikibonyeza tena kitufe cha kurekodi, Kamishna aliona ilikuwa ni nafasi nzuri sana ya kuweza  kumshawishi Norbert aweze kuachana na hilo wazo. Aliona kuwa alikuwa ni mwandioshi mwenye kukimbiza pesa, hivyo ilikuwa alidhani ni nafsi nzuri sana ya kuweza kumuhadaa. Aliamini kabisa kuwa hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akikataa pesa kwenye kizazi cha sasa, hivyo aliamua kuitumianafasi hiyo kulimaliza hilo.

"Wanadammu tunasaidiana Kaila ni kawaida, mimi na hao watu tulikuwa tukitegemeana kwenye mambo mbalimbali ndiyo maana tu popamoja kama unavyotuona. Hata wewe unaweza ukawa na msaada kwetu na sisi tukakusaidia"

"Sijakuelewa hapo Kamishna point ni ipi?"

"Utanielewa tu Kaila kwanza nipe namba yako ya benki nikusogeze kiasi kidogo tu, si unajua Mheshimiwa alisema atafuta rushwa serikalini sasa ishafutwa na hii si rushwa bali ni kukusaidia tu kimaisha"

"Ohoo! Unataka kunihadaa na hongo siyo, aibu kubwa mvaaji wa vazi la heshima la jeshila polisi unafanya mambo kinyume cha kiapo chako. Anyway asante kwa kuniongezea ushahidi" Norbert alipoongea maneno hayo alibonyeza kitufe cha kucheza sehemu ya aliyoirekodi kwa mara nyingine, maongezi hayo ya kuomba hongo yalisikika vilivyo kwa Mhusika. Baada ya hapo hakuongea neno jingine lolote lile, alitoka nje ya ofisi hiyo na kisha akauendea usafiri wake na kuondoka upesi akiwa amewaachia hewa chafu walengwa wake ambao muda huo walikuwa hawajatimia kabisa.


****

   Alipotoka nje ya ofisi tu yule Kamishna ambaye alikuwa yupo kwenye mnyororo ule, alichukua simu yake ya mkononi na kuwapigia vijana wake wamfuatilie. Amri hiyo aliyokuwa ameitoa ilichukuliwa hatua mara moja, Norbert alipoingia  barabarani vijan waliokuwa wamepigiwa simu walikuwa wameshafika mara moja, walimuona na walianza kumfuatilia wakiwa kwenye pikipiki kama alivyokuwa yeye. Safari ya kumfuatilia ilikuwa ni ndefu sana lakini hawakukata tamaa waliendelea kumfuatilia, safari hiyo ilienda kuishia Kimara ambapo kwa macho yao walimshuhudia Norbert akisimama kwenye lango la nyumba moja ambalo aligonga hapo. Haukupita muda alikuja mwanamke ambaye alikuwa  ambaye ni binti aliyekuwa na mwili uliojaa, mwanamke huyo alipomuona Norbert alimfuata hadi hapo kwenye pikipiki akamkumbatia akionekana alikuwa na hamu naye sana. Alimbusu Norbert akiwa yupo hapo na kupelekea wale waliokuwa wakimfuatilia waone kila kitu.


   Hiyo ilikuwa ni nafasi adimu sana kwa hao watu kwani walitambua kabisa kuwa huyo alikuwa ni mpenzi wake, hapo walipatwa na na wazo ambalo kabla hawajalifanya iliwabidi wampigie simu Kamishna na kumueleza. Wazo hilo lilikuwa ni lenye kufurahisha sana kwa Kamishna, aliwaruhusu vijana hao walitekeleze upesi sana baada ya Norbert kutoka ndani ya nyuumba hiyo. Muda huo walikuwa wakitazama na kuomuona Nobeet akiingiza pikipiki yake ndani ya nyumba hiyo, walipohakikisha alikuwa ameingiza pikipiki ndani kabisa. Waliamua wawapigie simu wenzao ambao  walikuwa na usafari mwingine waweze kufika eneo hilo, watu hao walikuwa wameshadhamiria kabisa kumteka huyo mwanamke kwani waliona ndiyo utakuwa mwanzo mzuri wa kuweza kumfanya Norbert awe mpole mwenyewe. Waliamini kabisa hakukuwa na mwanaume aliyekuwa na ujanja mbele ya udhaifu wake ukiwa matatani hivyo ilikuwa ni nafasi ya dhahabu, waliendelea kusubiri katika eneo hilo ambalo lilikuwa limejibana kwa muda wote ambao yule waliyekuwa wakimfuatilia alikuwa ameingia ndani ya nyumba hiyo.


****


  Baada ya kutoka kuwatia homa maadui wa taifa  na maendeleo yake, aliamua kwenda moja kwa moja hadi Kimara. Huko kulikuwa na Mpenzi wake ambaye walikuwa wamepotezana kwa muda mrefu sana, mpenzi huyo ambaye alikuwa yupo kwenye mnyororo mrefu wa wapenzi waliokuwa wakimuhusudu ndiyo aliamua kumuona. Ilikuwa ni akili ya ajabu aliyonayo ilikuwa imemjia ndiyo ilipelekea hadi afunge safari kuelekea huko, alifika na alipokewa na mabusu na mwanmke huyo ambaye hakuwa ameolewa ingawa umri wake ulikuwa umeenda sana. Norbert alifunguliwa lango kubwa na aliingiza Pikipiki yake ndani baada  ya lango kufungwa, kilichofuata hapo ilikuwa ni michezo ya kitoto ambayo watu wazima walikuwa wakishriki kwenye eneo hilo ambalo alikuwa ameegsha pikipiki yake. Mwanamke huyo aliyeonesha kuwa alikuwa na hamu naye sana hakujali kuanza kucheza michezo eneo hilo la ndani ya uzio wa nyumba yake,alichojali yeye ilikuwa ni kufanya kile ambacho alikuwa ameshurutishwa na mwili wake. Unene wa mwili wake hakuujali kabisa ,muda huo alikuwa amekaa sehemu ya mbele ya Pikipiki ya Norbert akiwa amemkumbatia huku miguu yake akiwa ameizungusha kiunoni mwa Norbert ambaye alikuwa ameukamata usukuani  barabara na kuweka miguu chini azuie Pikipiki isianguke kwa uzito alionao mwanmke huyo.

  Ulimwengu ule usiojaa viumbe wengi sana ndiyo waliokuwa wapo ndani yake, mandhari yale yaliyokuwa yakileta mchanganyo ndani ya damu zao ndiyo walikuwa nayo kwa muda huo ingawa mmoja bado akili yake ilikuwa ipo kwenye mandhari ya kawaida ikiwa na tahadhari sana. Waliendelea na mchezo ule hadi pale Norbert alipukatisha kwa ghafla sana kitendo hicho bado kilimfanya Mwanamke huyo awe ni mwenye kukazania waendelee kwani alipokuwa amefikia hapakuwa pazuri kiupande wake.

"Nor ndiyo nini hivyo?" Aliuliza baada ya starehe kukatikia katikati.

"Happy nipo kwenye kazi mpenzi wangu, hapa nilipita mara moja nilikuwa naenda mtaa wa pili kwenye mahojiano na mtu muhimu. Naomba uvumilie kidogo nikamalize mahojiano halafu tutakuja kufurahi hadi asubuhi umesikia kipenzi" Alimuambia

"Nor nimekumis ujue, sasa huko utachukua muda gani?" Happy aliuliza

"Yaani ndiyo kwanza hata saa sita bado sasa fikiria nikirudi mchana wote nipo hapa hadi kesho, utaridhka mwenyewe"

"Kweli?"

"Tangu lini kinywa hiki kikatamka uongo kwako jamani"

"Hay basi Mpenzi we nenda ukirudi utanikuta nimejaa tele hapa kama pishi ya mchele

"Na nilivyokuhamu tutakesha hapa"

"Nor nenda basi unazidi kunitia hamu ukiniambia hayo maneno"

"Sawa basi nipe busu la mara ya mwisho nikitoka nikirudi nakupatia langu refu la hadi kunakucha" Hapo Happy aliachia tabasamu na kisha alienda kumbusu kimahaba zaidi Mpenzi wake huyo , baada ya hapo Norbert aliwasha pikipiki yake na kisha alienda kufungua Lango. Pikipiki ilitoka hapo kwake akabaki akiisindikiza hadi ilipoishia ndipo aliporudi ndani ya nyumba yake akafunga lango hilo, alibaki akitabasamu baada ya kufunga lango hilo kutokana na kutembelewa na huyo mwanaume aliyekuwa akimuhusudu sana.


****


  Muda mfupi tangu Norbert aondoke pale kwenye nyumba hiyo ya Happy, gari aina ya Toyota Noah yenye rangi ya zambarau pamoja na vioo vya giza ilifika hapo. Kijana aliyekuwa na mwili uliojaa kimazoezi alishuka ndani ya gari hilo, aliposhuka tu alitazama katika upande ambao walikuwa wamekaa vijana wenzake waliokuwa wamekuja na pikipiki kwenye eneo hilo. Aliwapa ishara mojawapo ya ishara zao na kisha akasogea hadi kwenye lango la nyumba hiyo, aligonga mlango huku akizngalia kulia na kushoto na muda huo wale vijana waliokuwa wapo pamoja naye waliwasili kwenye eneo la langoni hapo wakajibana pembeni.


  Mlango ulifunguliwa na Happy yule ambaye hakuwa akijua chochote kilichokuwa kikiendelea, alipofungua na kukutana mtu huyo ambaye alikuwa amejengeka kimazoezi alibaki akimtazama kwa mshangao. Muoneano mtu yule na jinsi alivyokuwa amekomaa alibaki akiwa ameganda akimtazama sana.

"Habari yako" Yule Mtu alimsabahi

"Safi tu za kwako?" Alijibu na kisha akauliza kuhusu hali yake huyo mgeni.

"Salama... kuna mzigo wako huu" Yule Mtu alijibu  na kisha akaingiza mkono kwenye mfuko wa ndani wa kotilake alilolivaa, alipotoa mkono huo ulikuwa na bastola ambayo ilikuwa imefungwa kiwambo cha kuzuia sauti na alimuelekezea huku akimuwekea kidole cha  shahada mdomoni. Alimuashiria arudi ndani ya nyumba hiyo na yeye alitii huku akitetemeka, wale vijana waliokuwa wamejibana pembeni ya gati nao waliingia ndani kwa haraka sana nakisha wakamshikilia kwa nguvu na kwenda kubana naye kwenye eneo ambalo lilikuwa limejificha hata lango likifunguliwa wasionekne kama wamemshikilia.

  Wachache kati yao walifungua lango kubwa la nyumba hiyo, gari lile ambalo lilikuwa limekuja hapo lilikuwa na mtu ndani yake. Gari hilo liliwashwa na taratibu likaingia ndani ya nyumba hiyo hadi kwenye eneo la maegesho. Lango la nyuma la gari hilo lilifunguliwa, Happy aliingizwa ndani na kisha akafungwa miguu na mikono pamoja na kuwekwa gundi nzito mdomoni.  Baada ya hapo lango hilo lilifunguliwa kwa mara nyingne tena, gari hilo lilitoka na kuondoka kwa mwendo wa kasi eneo hilo huku wale vijana wakifunga lango hilo na kwenda eneo lenye pikipiki zao wakaondoka nao kwani kazi yao ya utekaji nyara ilikuwa imekamilika tayari. Hawakujua kuwa hilo walilokuwa wamefanya lilikuwa ni kosa kubwa ambalo lingeweza kuwagharimu sana, kosa mbalo lingeweza hata kusababisha wakose ulaji wao kwa kazi hiyo waliyokuwa wameifanya. Wote waliona ilikuwa ni haki yao kutimiza wajibu wa mkuu wao aliyekuwa amewatuma, walikuwa na faraja sana kwa kuweza kuikamilisha kazi kirahisi sana.



****


    Walipokuwa wakitekeleza amrikubwa waliyokuwa wamepewana mkubwa, Norbert alikuwa yupo njiani akikata mitaa na muda huo alikuwa ameshafika Ubungo. Alikuwa akijua wazi kitu ambacho kilikuwa kikikaribia kutokea ndiyo maana alielekea eneo lile, aliamini kabisa majuto yatawarudia wale ambao walitekeleza utekaji nyara huo. Muda huo alikuwa akivuta mafuta zaidi kwenye Pikipiki akiimaliza mitaa, alikuwa yupo ndani ya Barabara ya Mandela baada ya kuimaliza Ubungo. Kutokana na mwendo kasi aliokuw akiutumia, baada ya dakika kumi tu alikuwa tayari yupo Buguruni. Aliendela na safari yake hadi akafika Temeke panapo nyumbaye yake ambapo aliingia ndani moja kwa moja, aliegesha Pikipiki hiyo kwenye eneo la maegesho na kisha akazama ndani na aliishia kwenye sebule ya nyumba hiyo aliyokuwa ameikacha kwa siku nyingi akiwa anaishi kule ambapo yupo Mpenzi wake na mtoto wake. Hapo alikaa kwenye kochi mojawapo la sebuleni hapo baada ya kumaliza hatua ya kwanza ya kuwatia wazimu wale waliokuwa maadui wa taifa, alibaki akishusha pumzi kwa hatua hiyo aliyofikia kwani alikuwa akicheza kamari ya kifo. Kuwafuata wale ambao walikuwa wao mnyororo hatari ilikuwa ni kamari ya kifo lakini alikuwa akijiamini sana, pamoja na hayo alipokuwa kwenye eneo hilo alikumbuka kumshukuru Mungu kwa hatua hiyo aliyokuwa amefikia. Pamoja na kuwa ni mtu ambaye alikuwa  haishi kubadili wasichana bado alikuwa akimkumbuka Mumba kwani imani ilikuwa ipo ndani yake, ndiyo maana alimshukuru ingawa alikuwa akimuasi sana muda mwingine aliokuwa yupo kwenye kazi yake.

  Akiwa yupo kwenye kutoa shukrani hizo kwa aliyemjalia pumzi, simu yake ya mkononi iliita, alipoangalia jina la mpigaji alikuwa ni Kamishna ambaye alikuwa ametoka kumtia homa isiyohitaji  tiba muda mfupi uliopita.



   ITAENDELEA!!

No comments:

Post a Comment