Tuesday, March 14, 2017

WITO WA KUZIMU SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU




WITO WA KUZIMU

NA: HASSAN O MAMBOSASA

MAHALI:TANZANIA


SIMU:+255713776843
      +255762219759

WHATSAPP:+255713776843
         +255762 219759

BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com




SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU!!
Aliipekua ndani ambako alitoka akiwa na kifa kidogo klichokuwa kikiwa taa ya rangi ya bluu na akamuonesha Norbert ambaye alisikitika tu.


"Huyu ndiye mchawi ndani ya ofisi hii ananasa mawasiliano na pia simu zinazoingia na eneo zinapotoka"  Norbert aliongea na kisha alimpa ishara Moses jun ya cha kufanya kwani walikuwa wametambua wazi kuwa walikuwa wakisilikizwa na msaliti huyo ambaye yupo humo ofisini.





__________________TIRIRIKA NAYO

   Hawakutaka kuongea suala jingine lolote la siri baada ya kujua kuwa walikuwa wakifuatiliwa na mtu mwingine, ambaye alikuwa yupo upande wa maadui zao akwa anavujisha taarifa Mtu ambaye alikuwa amevunja kiapo cha utii alichokiwek kipindi anajiunga na ofisi hiyo, Moses aliipokea tu ishara hiyo kisha akamuonesha Norbeert alama ya dole gumba kuashiri amemuelewa. Kilichofuata hapo ilikuwa ni Norbert kuaga kuwa anaondoka humo ofisini, alifuatiwa na Jama ambaye naye aliaga vilevile kuwa alikuwa akiondoka baada ya kuweza kufika kuonana na mkuu wake wa kazi.

 Wawili hawa walioingia pamoja ndani ya ofisi hiyo walitoka kwa pamoja wakiwa ni wenye macho ya tahadhari katika kila eneo walilokuwa wakipita ndani ya ofisi hizo zilizokuwa zimesheheni vitengo tofauti vilivyokuwa vimejitosheleza. Walifika hadi nje kabisa ya jengo la ofisi hizo na kisha wote kwa pamoja walipanda pikipiki aliyokuwa akiitumia Norbert kwani hawakuwa mwaekuja mahala hapo na  gari.


  Waliondoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi sana na walizunguka kwenye mitaa mbalimbali ya jiji la Dar, hawakutka kunyooka moja kwa moja kuelekea walipokuwa wakitaka kuelekea kwa hofu ya kufuatiliwa baada ya kubainika kuwa walikuwa wametoka ofisini kwa mtu ambaye alikuwa nao kwenye harakati moja za kuwaumbua wale waliokuwa wanaifuja Tanzania kwa manufaa yao binafsi. Baada ya kuzunguka mitaa mbalimbali huku wakipita njia ambazo hazikuwa na umuhimu wowote hatimaye walifika Kurasini na si Pugu tena, Norbert aliingiza Pikipiki ndani ambako alipokewa na mmoja wa vijana wa EASA ambaye yupo humo ndani ya hiyo nyumba kama sehemu muhimu ya kufanyia kazi. Muda huo walipofika tu Tarakilishi ile ambayo ilikuwa na siri zote pamoja na majina wahusika kuanzia ngazi za chini hadi za ju, ilifunguliwa kwa mara nyingine ambapo Norbert aliyakariri majina yote yaliyokuwa yapo kwenye tarakilishi hiyo ya watumishi wote wa serikali wa ngazi za chini  kisha alimuaga Jama Wa Majama na kuingia kazini kwa mara nyingine.


****


   Baada ya wenzake waliokuwa naye kwenye mbio moja kutoka ofisini kwake, aliona huo ndiyo ulikuwa muda muafaka wa yeye kuchunguza kile ambacho kilikuwa kimetokea. Moses aliamua kutoka ofisini kwake akiwa amekitoa kile kifaa kwenye simu yake na sasa alikuwa nacho mkononi, alitokea kwenye eneo ambalo lilikuwa na dawati la Katibu Mukhtasi na kisha kukifuatiwa na madawati mengi sana ya wafanyazi waliokuwa wapo chini yake kwenye idara hiyo wakiwa wanaendelea na kazi zao kama kawaida.

  Alianza kuwatazama mmoja baada ya mmoja huku akiwa ni mwenye jicho la umakini sana, akili yake ile iliyofanya aajiriwe kwenye idara nyeti kama hiyo ndiyo iliamka katika kuwatazama wafanyakazi hao. Hakuwa akimmini kabisa kuwa msaliti ndani ya idara hiyo alikuwa akitoka mbali na ofisi yake kutokana na mfumo wa kifaa  kilichowekwa, alitambua kabisa  mtu huyo alikuwa yupo karibu kabisa na ofisi yake kwani kile kifaa kilikuwa kikiendesha nao kuwa kina mionzi ambacho kilikuwa kikichukua taarifa kwenye kifaa kile kilichokuwa kipo ndani kilikuwa hapohapo  alitambua kingine kilichokuwa kikichukua mionzi kwenye kifaa kile. Hakutaka kukubali kabisa kuwa kifaa kile kilikuwa  kipo umbali hata wa mita kumi kutoka mahali ilipo ofisi yake


  Macho yake yalipokuwa yapo eneo hilo kila mmoja alikuwa akizidisha umakini wake wa kazi, hilo suala halikumuhadaa kabisa hadi apunguze kuwatazama kwani alishajua kabisa kuwa mbaya wake yupo ndani ya eneo hilo. Baada ya kuwatazama kwa umakini mkubwa sana hatimaye macho yake yoe yalikuwa yametua mahali ambapo alikuwa amekaa Mfanyakazi mmoja mabye alikuwa amevaa spika za masikioni, mfanyakazi huyu alikuwa akihusika na kunasa njia zote za mawasiliano ndani ya ofisi  hiyo ambazo hazikuwa salama hata kugundua wale wote waliokuwa wakifanya mchezo wa kufuatili mawasiliano na kuwaharibia. Moses hakutaka kupoteza muda kabisa aliamua kupiga hatua na kumsogelea karibu zaidi na kisha akabaki akimtazama yule Mfanyakazi ambaye alikuwa yupo makini sana katika kufuatili kitu kwenye tarakilishi akiwa hajatilia maanani uwepo wa mkuu wake mahala hapo. Aliweka mikono kwenye meza yake akawa anamtazam kwa umakini sana kisha akageuka kwenye dawati ambalo lilikuwa lipo pembeni ya huyo mfanyakazi, Hapo alikutana na Mfanyakzi mwngine akiwa anaendelea na kazikama kawaida akionekana naye yupo makini katika kufanya kazi.

  Macho yake yalivutika kabisa na Mfanyakazi huyo na akapelekea azidi kumwangalia zaidi, alijikuta akitabasamu kila akimuangalia Mfanyakazi huyo ambaye alikuwa akionekana yupo makini sana kwenye ofisi hiyo kila siku akiingia hata kama alikuwa ameingia kw ghfla. Macho yake yaliaanza kumuangalia mfanyakazi huyo kisha yakashuka kwenye kioo bapa ambacho kilikuwa kimeungwa na sehemu ya mfumo wa tarakilishi, mashine nzima ya kicho hicho ilikuwa ikijulikna zaidi ilikuwa ipo chini ya meza yake iliyokuwa imewekewa juu kwani ndiyo ilikuwa utaribu wa kila siku. Moses alijikuta akifuatilia waya uliokuwa ukitoka kwenye mashine hiyo  ambayo ulikuwa ukiunganisha na mashine ya chini maarufu kama 'VGA(Video graphic arrays) cable'.


  Waya huo aliukuta ukiwa haujaelekea katika eneo ambalo mashine ipo bali ulikuwa umeelekea kwenye uwazi uliokuwa upo meza yake iliyokuwa na mitoto mingi sana, kuuona huo waya alijikuta akiingwa na wasiwasi kkwani haikuwa utaritibu wa ofisi hapo kwa nyaya kuwa namna hiyo.  Hapo Moses alijiua moja kwa moja kuwa huyo ndiye alikuwa msaliti wake haiwezekani kabisa kuwa waya huo uliochukua taarifa kwnye mashine usiende kwenye mashine na  badala yake uingie kwenye upenyo uliokuwa ukielekea eneo lenye mitoto mingi sana, alijua wazi kuwa kulikuwa na mashine nyingine iliyokuwa imefichwa huko ulipoelekea huo waya. Mashine nyingine ya Tarakilishi iliyokuwa haijaunganishwa na mashine  na mfumo wa mawasiliano wa humo kama ilivyo mashine zote za kuweka chini zilizopo humo ofisini. Hakutaka kujiuliza swali mara mbaioli alipiga hatua kwenye hadi kwenye dawati hilo huku akiweka kifaa kile mfukoni, alipofika alianza kutazama kama alivyokuwa akiwatazama wengine na kisha alitoa bastola yake kwa ghafla sana na kumuwekea kichwani.

"Inuka hapo kama ulivyo" Alimuambia huyo Mfanyakazi ambaye alishtuka sana, wafanyakzi wote waligeuza macho kumtazama huyo mwenzao ambaye alikuwa amewekewa bastola kichwani.

"Wewe mfunge pingu huyu na umshikilie" Alimpa amri mfanyakazi mwingine kabisa ambaye alitoa pingu kwani hazikuwa mbali nao, alimfunga yule mfanyakazi na kisha akamshikilia barabara.


 Moses alipopata uhakika kuwa Mfanyakazi huyo hawezi kutoroka aliingia hadi kwenye eneo lake la kufanyia kazi kisha mkono wake akaupeleka chini ya meza hiyo, alikuta na kitu ambacho kilimpa uhakika kabisa wa jinsi mawazo yake yalivyokuwa. Huko alipeleka mkono hadi kagusa sehemu ambayo waya wa kioo cha tarakilishi ile ulikuwa umeingia, alifungua nati za  waya huo. Baada ya hapo aliingia chini ya meza ile vizuri ambapoa aliweza kuona waya mwingine uliokuwa ukitoka kwenye mashine ya awali na kuingia kwenye mashine kwenye mashine hiyo isiyo rasmi ambayo ilikuwa ikitumika kwa kazi haramu hapo ofisini kwake. Moses alipoona hicho hicho kitu aliamua kuichukua ile mashine  haramu ha kuiweka juu ya mashine ya ofisini na kisha vyote akavisukuma kuelekea nje ya meza hiyo kwa upande wa mbele, wafanyazi wote walishuhudia mashine hizo mbili zikitolewa ambapo moja ilikuwa ikitegmea nyingine ili iweze kupata umeme wake  wa kuongoza mfumo mzima uliokuwa upo ndani. Ilikuwa ni mashine ndogo sana kuliko hata zile ambazo huwekwa nyuma ya kioo cha Tarakilishi, wote waliipoona mfumo wa nyaya za mashine hiyo ndogo ikiingia kwenye mashine kubwa. Walijua kabisa kuwa mwenzao alikuwa akifanya jambo la haramu humo ofisini, walijua pia ndiyo ulikuwa mwisho wake wa kuendelea kubaki humo na badala yake kifo au gereza lilikuwa likimuita.

"Unaweza kuniambia hii Kompyuta ya pili inafanya nini humu?" Alimuuliza kwa ukali, lakini hakupata jibu. Alipoona amekaa kimya alienda hadi kwenye Tarakilishi ile haramu ambayo ilikuwa ni ndogo akaifungua mfuniko wa juu na kuanza kuangalia vifaa vya ndani, alikuta kifaa kama kile kilichokuwa kimewekwa kwenye simu yake ambacho alikichomoa na kisha akamuonesha yule msaliti.


"Sound detecter plus phone track and locator(Kinasa sauti jumlisha kinasaji na kionesha uelekeo wa simu) Vinafanya nini humu? Kwanini usitumie tarakilishi ya ofisi kama ulikuwa ukitumia kazi za humu mpaka ulete nyingine ya haramu na uifunge kienyeji."Alipoongea kwa mara nyingine alitumbukiza mkono kwenye mfuko wake wa suruali akatoa kile kifaa kilichokuwa kipo kwenye simu yake ya ofisini.

"Si ndiyo ukaniweka hiki ili uweze kunasa simu zangu na kuwauzia taarifa maadui wa taifa, hebu pelekeni chumba cha adhabu huyo akapate malipo ya usaliti wake mjinga sana" Aliongea akiwa mwenye hasira na mwisho wake alitoa amri juu ya huyo msaliti wake na kisha aliingia ofisini kwake.



****


      BANDARINI
  
    Alipoondoka kwenye nyumba ya shirika lake kituo cha kwanza ilikuwa ni ndani ya ofisi za Bandari jijini Dar es salaam, alikuwa amepanga kabisa  kuonana na  Mhasibu mkuu wa bandarini hapo kwani kutoa mguu kutoka kule muda huo wa asubuhi majira ya saa tano. Ilikuwa ni kuja kuonana na huyo Mhasibu mkuu wa bandari, alikuta Mlengwa wake akiwa ni mwenye wageni wengi sana jambo lililomfanya asubirie kwenye viti vilivyopo jirani na  mapokezi. Zamu yake ilipofika tu aliingia ndani ya ofisi hiyo, alimkuta Mzee wa makamo aliyekuwa hana nywele hata moja kichwani akiwa amevaa suti nadhifu sana. Alipomtupia jicho Mzee huyo aliona kabisa alikuwa akitangaza ukwasi aliokuwa nao kwa jinsi ambavyo muonekano wake ulivyo, alienda kukaa kwenye kiti kilichopo mkabala na yeye na kisha akatoa salamu ambayo iliitikiwa kwani huyo Mhasibu mkuu alikuwa akimjua vyema Norbert kuwa ni mwandishi wa habari hivyo hakupata tabu ya kuhoji sana ujio wake.

"Ndiyo Bwana Kaila nikusaidie nini?" Alimuuliza

"NImekuja kukumbusha unatakiwa ulipedeni ulilokuwa ukidaiwa haraka iwezekanavyo" Norbert alimuambia na kupelekea atokwe na mshangao sana.

"Kijana ujue sikuelewi kabisa"

"Utanielewa tu Mzee tulia nikueleweshe, ni hivi mwenzako Khemiri ambaye mlikuwa mkishirikiana naye katika kupitisha bidhaa bila kodi na hata kuingiza Magendo kinyelemela yasikaguliwe amefariki nafikiri hili unalijua. Sasa ukwepaji kodi wote ni deni kwako unatakiwa ukalipe sasa hivi ninavyokuambia, watazania wanakudai wewe uliyewaweka kwenye shida ukakaa hapo ukitumbua jasho lao"

"Kijana usiniletee mchezo toka nje ya ofisi yangu kabla sijakuitia polisi"

"Sasa sitoki ita hao polisi  ukanyee debe vizuri, Ushahidi wote ninao na nitautoa kwenye gazeti hivi punde tu" Maneno ahyo yalimfanya Mhasibu huyo aanza kutokwa na jasho ingawa kulikuwa na kiyoyozi kilichokuwa kikifanya kazi humo.

"Vipi Mzee nikuwashie feni naona hali ya hewa ya Dar inakusumbua sana hadi kiyoyozi hakina nafasi" Norbert aliongea kwa kejeli


"Norbeet tafadhali sana naomba hili suala lisifike huko, tuongee kiutuzima na mimi mzee wako"

"Kwani hapa tunaongee kitoto, au maneno yetu ya awali yalikuwa yakinuka maziwa"

"Nooo! Najua na wewe unataka kusogeza life yako, sema unataka kiasi gani nikupe ili usilitoe kwenye magazine yako hili"

"Khaa! Kwahiyo unataka kunipa rushwa siyo" Norbeet aliongea aliongea huku akichomoa kanda ya kurekodi iliyokuwa ipo mfukoni na akaisitisha kurekodi, baada ya hapo aliicheza na maongezi yote yaliyokuwa yakiongelewa hapo yakisikika vyema na aliamua kuisitisha tena na akaitia mfukoni.

"Norbert usiniadhirishe kumbuka mimi ni sawa na Mzee wake please tulimaliza hili suala"

"Sina la ziada ndugu kizito kwaheri" Alimuaga na kisha akatoka nje ya ofisi hiyo akimuacha Mhasibu huyo akiwa amesimama wima asijue cha kufanya kwa jinsi alivyokuwa amezidiwa ujanja.


  Norbert alipotoka hapo alienda hadi kwenye makao makuu ya mapato(TRA) kwenye ofisi ya mtu mwingine ambaye alikuwa yupo kwenye orodha ile, huko aliomba kuonana na Mhusika mwingine aliyekuwa amemkusudia kuendana na orodha ile ilivyo. Kutokana na kuwa mwandishi wa habari na kuhofiwa kuweza kuipa sifa mbaya ofisi hiyo, aliambiwa subiri hadi pale atakapotoka mtu aliyekuwa yupo ndani ya ofisi  hiyo ndiyo aingie. Aliporuhusiwa muda wa kuingia kutokana na zamu yake kufika, hakutaka kupoteza muda hadi yule Kizito wa bandari  aje kukawa na akili sawa ampe taarifa huyu. Aliingia ndani moja kwa moja akakutana na Mwanamke wa makamo ambaye alikuwa ni umri wa kuweza kumzaa yeye, Norbert alipomuona tu huyo mwanamke alitoa tabasamu usoni mwake na kisha na kisha akaketi kwenye kiti kilichokuwa kikitazamna naye. Alipokewa na tabasamu kutoka kwa Mwenyeji wake ambaye  alikuwa mtu mzima ingawa si haba sana, kwani pesa ilikuwa haizeeshi sana kaisi cha kumfanya aonekane amechoka. Tabasamu lake la usoni lilimfanya mwanamke huyo aonekane na mvuto wa sura aliokuwa nao mgeni wake huyo aliyekuwa ni kijana matanashati, alijua ulikuwa ni ugeni uliokuwa hauna shari ndani yake kupitia tabasamu hilo ambalo lilikuwa likimpa matumaini hayo kabisa.

"Ndiyo Kaila nikusaidie nini?" Alimuuliza

"Mama yangu ujio huu ni wako na nimekuja kukumbusha tu kuwa unatakiwa ulipe madeni unayodaiwa na  watanzania" Norbert aliongea na kupelekea huyo Mwanamke amtazame kwa jicho akionesha kutomuelewa.

"Sijakuelewa kabisa Norbert go straight to the point" Aliongea Mwanamke huyo

"Ok ni hivi zile pesa ulizokuwa ukila kwa kufanya uhaini ndani ya mamlaka hii ikiwemo kuonesha rekodi feki za kuwa kodi yote iliyokuwa ikidaiwa kampuni ya Khemiri imelipa, sasa ni hilo ni deni kubwa sana kwa Watanzania wanaolia njaa kwasababu yako"

"Eeeeh!"

"Sijakuita nimekukumbusha tu huo ni wajibu wako kwani ulikuwa ukijaza tumbo lako kwa kuwa mmoja aliyekuwa akifanya mizgo haramu iingie. Mama ulipe deni la watu kabla serikali haijakulipisha"


"Norbert out of my office"

"Kabla sijatoka mama napenda ujue kuwa haya yanatoka kwenye jarida langu la mwezi huu"

"Nooo please isiwe usitoke kwanza tulimalize hilo kumbuka mimi ni sawa na mama yako, sema kiasi gani nikupe si rushwa hii bali nasogeza maisha yako mbele kidogo tu"

"Kwahiyo unanipa hongo siyo"

"Hapana"


"Natoka mama maana ulishaniambia ila ukumbuke kabisa haya niliyokwambia kwani mwenzenu Khemiri ni marehemu sasa mzigo wake mtaubeba nyinyi" Norbert alingea na kisha alitoa Kirekodi sauti kingine ambacho klikuwa tofauti na kile cha awali, alikisitisha kurekodi na kisha akacheza sehemu ile ambayo alikuwa amerokodi . Sauti ya maongezi yao ndani ya ofisi hiyo yalisikika wazi ambapo Mwanamama huyo alizidi kuchanganyikiwa.


*WIZI MUUJUE KUINGIA JELA MUOGOPE

"NORBERT KATIKA UBORA WAKE





ITAENDELEA!!
 

No comments:

Post a Comment