WITO WA KUZIMU
NA: HASSAN O MAMBOSASA
MAHALI:TANZANIA
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
+255762 219759
BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com
SEHEMU YA MWISHO!!
Ndani ya chumba hicho alishuhudia wasichana watatu wakiwa wamekaa wanaongea huku wakicheza karata,alisimama mlangoni hapo akiyathaminisha mazingira ya humo. Kabla hata hajamaliza kuyathaminisha alifunguliwa pingu zote alizofungwa na kisha alisukumwa ndani kwa nguvu.
______________TIRIRIKA NAYO
Aligeuka kuwatazama mabinti watatu waliokuwa wamevaa sare kama zake wakiwa wanacheza karata, alibaki akishangaa wasichana hao ambao walimtazama kwa nyodo kila mmoja na kisha waliendelea kucheza karata kama kawaida. Josephine hakuwajali kabisa alienda hadi kwenye eneo ambalo kitanda kimojawapo kilikuwa kitupu kisha akajilaza akiwa anasikilizia maumivu. Alipojilaza tu kwenye kitanda hiko wale wasichna waliweka karata zao chini na kisha wakaenda hadi hapo walipo, bila kuuliza mmojawapo alimvuta mguu kamuangusha chini kisha akampiga teke la ubavu.
NA: HASSAN O MAMBOSASA
MAHALI:TANZANIA
SIMU:+255713776843
+255762219759
WHATSAPP:+255713776843
+255762 219759
BLOG: riwayamaridhawa.blogspot.com
SEHEMU YA MWISHO!!
Ndani ya chumba hicho alishuhudia wasichana watatu wakiwa wamekaa wanaongea huku wakicheza karata,alisimama mlangoni hapo akiyathaminisha mazingira ya humo. Kabla hata hajamaliza kuyathaminisha alifunguliwa pingu zote alizofungwa na kisha alisukumwa ndani kwa nguvu.
______________TIRIRIKA NAYO
Aligeuka kuwatazama mabinti watatu waliokuwa wamevaa sare kama zake wakiwa wanacheza karata, alibaki akishangaa wasichana hao ambao walimtazama kwa nyodo kila mmoja na kisha waliendelea kucheza karata kama kawaida. Josephine hakuwajali kabisa alienda hadi kwenye eneo ambalo kitanda kimojawapo kilikuwa kitupu kisha akajilaza akiwa anasikilizia maumivu. Alipojilaza tu kwenye kitanda hiko wale wasichna waliweka karata zao chini na kisha wakaenda hadi hapo walipo, bila kuuliza mmojawapo alimvuta mguu kamuangusha chini kisha akampiga teke la ubavu.
"Kenge umeingia umetukuta humu ndani hivyo ni wakubwa salimia wewe" Aliongea mmojawapo ambaye alikuwa amenyoa upara huku akiwa amekunja uso kihasira zaidi, mwingine alikuwa akimnyaga na hapo walikuwa wamemkasirisha zaidi sana. Hakuwa akitaka kuonewa zaidi kwani kile kipigo alichokuwa amepewa na maaskari wajeuri kilikuwa kikimtosha hivyo hawa aliona hawana sababu ya kumuonea. Alipowatazama watu wenyewe waliomuonea walikuwa ni wadogo zake kabisa, hivyo aliona hiyo ilikuwa ni dharau kubwa sanakwa hao watu kumuonea. Hakutaka kabisa kuruhusu mwingine ampige teka kwani aliona watakuwa amemdhalilisha sana, wa tatu wake aliponyoosha mguu ampige teke aliudaka na kisha alimrudisha nyuma, alijifyatua akasimama na kisha alimpiga teka zito yule msichana ambaye alikuwa ana sura ya kitoto zaidi akiwa amenyoa kipara. Mwingine alipotaka kuingilia alimrudisha na teke kali sana hadi akaenda kujipigiza kwenye kitanda, yule mwenye upara aliona alikuwa amefanyiwa kitu ambacho hakutakiwa kabisa kufanyiwa na mtu kama huyo ambaye anaingia muda huo gerezani wakati wao walikuwa na miaka wakitumikia kifungo ingawa walikuwa wana muda mfupi ndani ya gereza hilo.
Alimjia kwa kasi sana kumfuata Josephine na akiwa ana lengo la kumzoa aanguke naye chini, kuja huko kwa kasi alipitliza baada ya Josephine kumkwepa na kisha akamuongezea teke la kisigino lililompata kiunoni. Yule msichana mwenye upara alienda moja kwa moja kujigonga kwenye nondo ngumu za gereza na kupelekea kishindo kikubwa kisikike, wafungwa wote wa kike waliokuwa wapo gereza mkabala na hilo walishangilia kwa nguvu sana. Baada ya hapo Josepine alipiga sarakasi moja maridadi a akatua kitanda cha juu akajilaza, wale wafungwa wengine watatu walipoona vitendo alivyokuwa akivifanya walinywea wote wakaona walikuwa wamepata mbabe zaidi yao. Baada ya hapo wote walijikusanya sehemu moja na kisha wakamsogelea karibu, Josephine aliwatazama kwa macho makali lakini alikutana na matabasamu kwenye nyuso zao.
"Getu" Aliongea yule mwenye upara kisha akanyoosha mkono kumpatia akiwa na tabasamu, Josephine naye alionesha tabasamu kisha akampa mkono
"Frida" Mwingine alifuata ambaye alikuwa amesuka mabutu kujitmbulisha na kisha akampa mkono
"Stella" Alimalizia wa mwisho ambaye alikuwa amesuka minyoosho kumpa mkono na kisha wote kwa pamoja wakamtazama kwa tabasamu wakisubiria jina lake.
"Josephine" Alijitambulisha
"Karibu" Walimkaribisha huyo mwenzao mpya ambaye alikuwa ameletwa humo ndani, hao wasichana watatu walikuwa ni wale waliokuwa marafiki zake Marehemu Annie waliokamatwa kwenye kisa cha SHUJAA sasa walikuwa wapo pamoja na humo ndani na walifurahia sana kupata rafiki mpya ambaye aliwapa kipigo muda mfupi walipomchokoza.
****
USIKU
Majira ya usiku huo tayari mtu ambaye alikuwa ametumwa na Norbert kwenda kumfuatilia Kardinali Michael alikuwa amesharudisha majibu, alikuwa ametaja kila kitu juu ya mahali ambapo alikuwa akienda Kardinali katika kipindi ambacho haendi ofisini. Norbert alikuwa amemuagiza huyo kijana ili aweze kupapata hapo kwani aliamini kabisa kuwa kama Askofu Valdremar akiwa yupo hapa nchini basi mtu ambaye alikuwa amemficha alikuwa ni huyohuyo na hakukuwa na mwingine ambaye angemficha yule Askfu kabisa.
Vyeo vya kidini walivyonavyo vilimfanya kabisa aamini kuwa alikuwa amefichwa hapo tu, alikuwa akitambua kabisa kuwa huyo Kardinali hakuwa mtu wa ziara majira ya siku sasa alipopata habari muda mfupi ulipita alikuwa akitoka kwenye nyumba yake ambayo ilikuwa ipo Tabata Kinyerezi ikiwa na ulinzi mkali ambao aliuona baada ya lango kuachwa wazi. Muda huo Norbert alikuwa tayri ameshawasili kwenye eneo la nyumba hiyo baada ya kupokea taarifa hizo. Alikuwa amevaa mavazi ya kininja ambayo yalikuwa na rangi nyeusi kipindi anaufikia ukuta wa nyumba hiyo, akitumia ufundi wake wa kininja aliupanda ukuta huo hadi ndani ambapo ajiachia na kutua chini chini kisha akajibiringita kuepusha asitoe kishindo.
Baada ya hapo alijosogeza hadi eneo la jirani nakwenye maua kisha akajibana kwa muda mfupi akisubiri, muda huohuo alipita mlinzi ambaye alikuwa na silaha. Mlinzi huyo alipofika usawa wake alimrukia shingoni na kisha akamuwekea kitambaa mdomoni, alimshikilia kwa nguvu sana hadi alipotulia ndiyo alimsogeza pembeni na kumuweka kwenye maua ya nyumba hiyo. Alinyata hadi upande mwingine kabisa ambao alimfanyia Mlinzi mwingine namna hiyo kisha akamficha, alifanya namna hiyo akizunguka nyumba nzima akitumia kitambaa ambacho kilikuwa na dawa ya nusu kaputi.
Dakika nne baadaye eneo zima la ndani ya nyumba hiyo lilikuwa ni tupu kabisa, hakukuwa na Mlinzi aliyekuwa anazunguka humo ndani. Baada ya kufanya hivyo Norber alikwea hadi juu ya bati ya nyumba hiyo, alienda hadi sehemu ambayo kulikuwa na tundu kubwa sana ambalo angeweza kupita hata yeye. Tundu hili lilikuwa ni kutokana na kuwepo sehemu ya moto ndani ya sebule hiyo ambayo wazungu hupenda kujenga wakiota moto, nyumba hii ilijengwa kwa mtindo huo ingawa ulikuwa ukijulikana kabisa kuwa mtindo huo ulikuwa ukijengwa kwenye nyumba ambazo zilikuwa zipo maneno ya baridi sana. Norbert aliingia ndani ya tundu hilo na kisha alishuka taratibu hadi chini, alikuja kutokea kwenye uwazi mkubwa sana. Eneo hilo alipochunguliwa tu alikutana na teke kali ambalo lilimfanya aanguke mita moja mbele, alipokuwa yupo hapo chini alimuona Askofu Valdermar akimjia huku akiwa ametanguliza goti mbele kupiga pigo la kummaliza moja kwa moja. Hakutaka kabisa kuona akipigwa pigo hilo kizembe sana aliamua kujibiringisha kwa upesi sana akaenda pembeni kisha akasimama wima kukabiliana na adui yake
"Niliuhisi ujio wako ninja mwenzangu" Askofu Valdermar aliongea na kisha akatoa ishara ya kininja, wote wawili walikaa mkao moja chini ya sakafu ya nyumba hiyo. Walianza kuweka ishara mbalimbali ambazo maninja huweka kabla ya kupambana, baada ya hapo walinyanyuka taratibu na kisha walikaa mkao wa kupambana.
Mpambano ulianza kwa Askofu kurusha mateke mawili akiwa juu mfululizo na yote yalikosa lengo kutokana wepesi aliokuwa nao Norbert katika kukwepa. Naye alikuja ana ngumi mfululizo na kisha akarusha teka, mapigo yake nayo yalionwa na Askofu ambaye aliyapangua kisha akarudha teke la miguu miwili la kifua. Teke hilo lilipita nalo kwani Norbert aliyumba pembeni kiufundi na kisha akamsukuma na mguu wake aangukia kando akiwa bado yupo juu, Askofu alipoanguka chini alijifyatua akasimama na kisha akakunja ngumi kwa namna ya kuvizia akimtazama ninja mwenzake ambaye alikuwa amefunika uso wake. Pigo hilo aliopigwa muda huo alijua kabisa mpigaji alikuwa ni Norbert kwani alishawahi kumuotea hapo awali walipokuwa wakipigana, sasa akaweka akili sawa aweze kukabiliana na Norbert akiwa anakumbuka mitindo yote ya kupigana aliyoitumia.
Hapo alikumbuka kabisa kuwa hizo zilikuwa ni mojawapo ya mbinu ambazo Norbert alizitumia wakati anapambana naye, alijiweka sawa na kisha akaingia tena uwanjani kwenda kupambana naye. muda huo alionekana kuyamudu mapigo yote aliyokuwa akiletewa kutokana na kukumbuka mitindo yote pindi alipokuwa akipigana naye, alifanikiwa kumuotea Norbert pigo la mgongo ambalo lilimpelekea hadi chini. Alitaka kufuata amuongezee lakini Norbert alibinuka kwa saraksi akiwa hapo chini akatua kando, hapo alijipanga upya kumfuata mpinzani akijua atakuwa na mtindo uleule. Alipojaribu kutia ngumi alijikuta yupo chini kwani tayari mpinzani alikuwa amebadili mtindo, sasa likuwa akitumia judo huku akichanganya na mapigo ya Ninjutsu alimaarufu kama ninja. Mapigo hayo yalimfanya Askofu aingie kwenye wakati mgumu kwani alikuwa akiionja sakafu ya nyumba kwa mara nyingi sana kila alipopiga pigo moja, hakukata tamaa aliendelea kumfuata tu Norbert.
Mapigo hayo ya judo yaliyotumika ndiyo ambayo mapigo yalilainisha kila kitu kwa Norbert, ndani ya muda mfupi Akofu alikuja na pigo la kutumia ngumi yake. Mzee wa kazi alikwepa pigo hilo kwa kuyumba pembeni kisha alimrusha kwa mtindo wa judo Askofu akaenda kuangukia ule ubavu ambao alimuumiza, maumivu yalianza upya na hata aliposimama hakusimama sawasawa. Alizidi kujiongezea hatari kwani mpinzani alikuwa ameshajua tayari alikuwa ameumia, alichofanya ni kuja na mtindo mwingine wa kupigana. Huu ulikuwa ni mtindo wa sarakasi kisha anaachia pigo moja, hiyo ilimchangnya sana Askofu na alijikuta akipigwa sehemu ileile aliyokuwa ameumia kwani alikuwa amemuonesha ameumia. Jambo la hatari kuliko yote ni kumuonesha mpinzani kuwa umeumia na Askofu alikuwa tayari amelifanya, haikupita hata dakika za kukadiria ziwe zimefika tano. Askofu alishavunjwa mbavu zake kwa mapigo ya mchanganyiko, hakuwa tena na ujanja na Norbert muda huohuo alimvunja mkono kwa kuzungusha kijudo alijaribu kurusha ngumi. Alipiga makelele kwa kuvunjwa mkono huo lakini hakukubali kushindwa kabisa, alirusha teke ambalo lilikosa lengo baada ya mpinzani kubonyea chini. Akiwa amebonyea huku chini alipiga teke la pembeni maarufu kama 'Yoko geri kekome" ambalo lilitua kwenye maungio na akamvunja kabisa, Askofu alianguka chini akawa hana ujanja tena. Akiwa yupo hapo chini Norbert alimjia na alipomsogelea alichomoa upanga wake ambao alikuwa amueweka nyuma, Askofu alijua kabisa kuwa ulikuwa ni mwisho wake na alikuwa yupo tayari kwa kufa kifo cha kukatwa kichwa. Alijiweka tayari kukatwa kichwa lakini panga hilo lilienda kutua kifuani mwake likaingia kwenye sehemu ambayo moyo upo, alitoa macho nje kwa nguvu sana baada ya kuchomwa eneo hilo kisha akatanu kinywa kinywa. Huo ndiyo ukawa mwisho wake wa kucheza na wanausalama makini sana ndani ya Afrika ya mashariki, sasa si kiumbe hai bali ni aliyeporwa uhai'
"Hustahiki kufa kifo cha kiheshima cha kininja wewe" Alimuambia kisha akaliachia panga na Askofu alidondoka kama gunia, Nobert alipokamilisha kazi hiyo alitoka nje ya nyumba hiyo kwa kupitia njia aliyokuja nayo na kisha aliruka uzio na kutokomea mbali na eneo hilo.
****
[0]
MAPEMA ASUBUHI
IKULU
Muda ule wa kikao ambacho kilikuwa kimeandaliwa ulikuwa ukikaribia, wahusika wote waliokuwa wakitakiwa kwenye kikao hicho walikuwepo hapo. Mawaziri wawii ambao ni Mheshimiwa Liwale nai Mheshimiwa Mahujuraja walikuwepo, upande mwingine walikuwa Katbu wa wizara ya nishati na madini pamoja na Katibu Mkuu wa wizara ya uchukuzi.Humo ndani pia Mhasibu wa bandari Bwana Mushi alikuwepo, Afisa wa juu kabisa wa mamlaka ya mapato Bibi Mushi alikuwepo. Upande wa jeshi la wananchi wa Tanzania Luteni jenerali Belinda ambaye alikuwa ni mnadhimu mkuu wa jeshi alikuwepo, upande wa jeshi la polisi kulikuwa kuna Kamishna fisadi pamoja na IGP Mbwambo ambao walikuwepo wamekaa hapo. Muda hawakuonekana Norbert wala mtu mngine yeyote, kiusalama tu alikuwa ameonekana kwenye meza hiyo Moses Gawaza.
Wote walikuwa wamepambwa na tabasamu kwenye nyuso kwani waliona ulaji ndiyo huo ulikuwa ukijileta, nyuma ya kiti cha kila mmoja alikuwepo yupo mwanajeshi aliyekuwa amesimama kiukakamavu. Hiyo waliambiwa kuwa ilikuwa ni kwa ajili ya ulinzi wa mahala hapo kutokana na unyeti wa jambo walilokuwa wakiongea, waliliamini moja kwa moja kwani kila alikuwa amesima akiwa na mlinzi wa aina hiyo nyuma yake. Ulipotimia muda walimuona Rais Zuber akiingia humo ndani akiwa ameongozana na watu wawili, mmoja alikuwa hajajulikana kwani alikuwa na ndevu nyingi sana na mwngine alikuwa ni Norbert.
Wote humo ndani walisimama na maofisa wale ambao walikuwa na vyeo vya juu kabisa walitoa saluti huku ale waliokuwa wadogo wakikakamaa kiheshima. Rais Zuber pamoja na wote waliokuwa wameingia naye walichukua nafasi wakakaa, hapo kikao kilifunguliwa ulipofikia muda na Rais Zuber.
"Natumai wote ni wazima kabisa wa afya hilo tumshukuru Mungu na pia niwapongeze kwa kuja hapa ndani ya eneo hili, ningependa kuchukua nafasi hii kumtamblisha huyu mmojawapo ambaye mlikuwa hamumjui kabisa hapa. Anaitwa Jama Wa Majama" Rais Zuber alianza utangulizi kisha akatoa utambulisho kwa Jama ambaye alitoa ndevu alizokuwa amezibandika kisha akasimama juu, watu wote waliokuwa kwenye mtandao walipomuona mioyo yao ilipigwa kwa nguvu sana.
"Niliwahi kusema kuwa nitapambana na ufisadi na kila aliyeshikwa na tuhuma hizi alihukumiwa, huu mwendo unaendelea. Sasa naomba kila mtu atulie humu ndani Jama Wa Majama asome ripoti nzima ambayo haikufika kwenye mikono yetu. Hakuna ziara ya Rais wa Marekani bali mliloitiwa ni hili " Muda huohuo ilipotoka amri hiyo taa za humo ndani zilipunguzwa mwanga na kisha Kirusha picha ukutani(projector) iliwashwa na pembeni kulikuwa na ubao mdogo wa kuandika na kalamu ya kuweka alama, Jama alitoa tarakilishi alizokuwa amekuja nazo zote tano akaziweka kwenye meza maalum na kisha aziwasha.
"Hadi siku tunaumaliza uchunguzi huu mimi na wenzangu tulipanga kabisa kuwa ripoti hii ya akiba tuifiche kinamna ya kipekee bila ya mtu kujua. Tulitia password kwenye laptop nne tofauti ambazo ni hizi hapa zenye ukubwa mdogo na kisha hii kubwa tukaweka ripoti hiyo, maneno yaliyokuwa kwenye laptop hizi nne ukiyaunganisha unapata neno 'BARA JANGWA NA USTARABU BARABARA LIWE NA MAHUJAJI ALEKUWA UMRA AU HIJA'" Aliweka kituo kisha akatazama kama alikuwa akisikilizwa.
"Ni neno lisilokuwa na maana kwa mtazamo wa kawaida ila ni neno lenye maana kubwa sana, hili ni neno ambalo ndiyo neno siri la kufungua faili lote lenye ripoti. Lakini lote ni nenosiri bado ulichambue, wazungu wanasema 'transdescribe" ndiyo utapata nno siri ya laptop yenye ripoti kamili. Aliweka kituo kwa mara nyingine, muda huo Mheshimiwa Liwale alinyanyuka kwenye kiti chake.
"Mheshimiwa kumradhi kidogo naenda msalani" Alisema
"Kaa kwenye kiti Liwale mpaka Laptop ifunguliwe ndiyo utarauhusiwa" Rais Zuber alizuia na hakuwa na kupinga alikaa chini.
"BARA JANGWA NA USTARABU NA USTARABU BARABRA tukilichambua tutapata ufupisho BAR JAN NA NSTU BA, sasa tuyabadili hizi silabi na irabu tulizozipata. Kifungu cha kwanza nakiunga na kifungu na tatu na kisha nakiunga tena na kifungu cha tano, ianakuwa BAR-NA-BA na hapa unapata jina la mtu BARNABA. Kifungu cha pili ukikiunganisha na cha nne yaani JAN-STU unapata jina JANSTU" Jama aliweka kituoniten hapo na muda huohuo Mheshimiwa Liwale na Mheshimiwa Mahujuraja walikuwa tumbo joto.
"Tuje kifungu LIWE NA MAHUJALI ALEKUWA UMRA AU HIJA, tunachukua LIW MAHUJ ALE URAJA. Ufupisho tunachukua hicho kifungu cha kwanza na cha tatu tunaunganisha yaani LIW na ALE tunapata jina la mtu LIWALE, tukichukua kifungu cha pili na kuunga na cha nne yaani MAHUJ na URAJA unapata jina la mtu MAHUJURAJA. Sasa hapa password yetu imekamilika tuunganishe vifungu vya kwanza pamoja katika kile upande na vya pili pamoja, BARNABA LIWALE na JANSTU MAHUJURAJA ndiyo unapata sasa tuingize sehemu ya neno siri kwenye faili ya hii laptop kubwa itadai mara mbili na uzingiza maneno kwa wakati tofauti tukianza na la kwanza" Jama alipoonge hivyo alihamia kwenye tarakilishi ambayo picha kubwa ilikuwa ikionekana juu yake, aliingiza maneno yake kama alivyosema na hapo faili hilo likafunguka na kila kitu kikawa wazi.
"Hatua imekamilika sasa kabla hatujaendelea napenda niwambie kuwa wahusika ambayo majina yao ni password ndiyo wahusika wakuu wa uhaini huu wakiwa wanatumia jina Roho kwa Mheshimiwa Liwale na Moyo kwa Mheshimiwa Mahujuraja" Alizidi kuweka mambo wazi na ilipofika hatu hiyo Mheshimiwa Mahujuraja alizidiwa na shinikizo la damu akaanguka chini na kupoteza fahamu
"Askari toa huyo upige pingu huku unampa huduma ya kwanza,weka pingu na Liwale pia" Rais Zuber alitoa amri hiyo na kisha wote walifungwa pingu na wale wanajeshi wakatolewa nje, baada ya hapo Jama alianza kuichambua ripoti nzima hadi ilipofikia mwisho. Alipoifika mwisho alikuwa ametumia saa takribani mbili, muda huo wale wote waliokuwa wapo kwenye mtandaao walikuwa na pingu tayari huku wengine machozi yakiwatoka. Waliobaki humo ndani walikuwa ni Rais Zuber, Jama, L.J Belinda, Norbert, Moses, IGP Mbwambo pamoja na maasakri wote wa jeshi la wananchi.
****
Mwisho wa mafisadi wote ulijulikana na hapo ndiyo ikawa nafasi nzuri kwa Mheshimiwa Kabinuki kuachiwa huru siku iliyofuata tu baada ya kujulikana hakuwa na hatia, ilijulikana wazi wale waliokuwa wakihusika kwa yote hayo walikuwa ndiyo hao waliokuwa wamekamatwa. Agiza lilitolewa kwa Rais Zuber wote walichukuliwa pesa zao benki, wakafilisiwa mali na kisha wakashtakiwa. Walianza kuwa ni wenye kwenda mahakamani kuhudhuria kesi zao kila muda, juma chache zijazo wote walihukumiwa vifungo vya maisha kutokana na mauaji waliyokuwa wameyasuka na walitupwa kwenye shimo la giza kule ambapo walikuwa watu wenye makosa kama yao. Huo ndiyo ukawa mwisho wale wote waliosuka mabomu ya barua wakiyaita wito wa kuzimu ili wapoteze ushahidi wa ufisadi wao.
Ulikuwa ni muda ambao Norbert aliongezewa likizo akawa yupo na familia yake akifurahia, alimkumbuka sana mtoto wake katika muda huo na aliutumia kushinda naye ndani baada ya kumaliza hiyo kazi ambayo ilikatisha raha ya kukaa na mtoto wake. Alifurahia kukaa na mwanamke anayempenda katika muda huo wa likizo aliyokuwa amepewa na ofisi kupumzika, alibaki akiwa yupo Norene pamoja na mwanae katika kipindi chote cha likizo yake.
MWISHO!!
NASHUKURU SANA KWA KUWA NAMI KUANZIA MWANZO WA RIWAYA HII HADI INAFIKIA TAMANI, TUMSHUKURU MUNGU KWA KUIMALIZA RIWAYA HII. NINGEPENDA KUSIKIA MAONI YAO JUU YA KAZI HI KAMA ULIKUWA NAMI PAMOJA KUANZIA MWANZO HADI MWISHO.
TUWE PAMOJA KWENYE RIWAYA ZIJAZO, NORBERT KAILA ATAREJEA TENA.
No comments:
Post a Comment